Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Form 4 Opener Term 1 Exams 2022

Share via Whatsapp

KISWAHILI
Karatasi ya 2

MAAGIZO

  • Jibu maswali yote


Maswali

  1. UFAHAMU (ALAMA 15)
    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali:

    Mwanamke wa kisasa anazaliwa na kukulia katika mazingira yaliyobadilika mno. Matazamio yake maishani ni tofauti na yale ya wanawake waliosihi mapote mawili yaliyopita; wanawake makamu ya nyanyake na mamake –kuu.

    Yeye hatarajii kuzaliwa, kukua, kuolewa, kuwa mke wa bwana, kumzalia watoto, na daima dawamu kuwa “mwandani wa jikoni” akawapikia watoto na bwanake chakula; na akitoka jikoni aelekee shambani kulima, kichakani, kuchanja kuni,, mtoni kufua nguo na kuteka maji ya kutumia nyumbani. Mwanamke wa kisasa huandamana na mwanamume. Akanyagapo mume naye papo huutia wayo wake.

    Mwanamke wa kisasa huenda shule na kujifunza yote yafunzwayo huko. Hushindana na wanawake kwa wanaume na kuibuka mshindi si mara haba. Huibuka mshindi katika masomo yake ya lugha, historia, jiografia, hesabu, sayansi na mengineyo, sawa na mwanamume.

    Mwanamke wa kisasa hutaka kufanya kazi za kibega, akazifanya. Akitaka kuwa mwalimu, akawa. Akataka kuwa daktari, akafanikiwa. Almuradi, siku hizi mwanamke hufanya kazi yoyote ile afanyayo mwanamume. Kuna wanawake marubani wa ndege, masonara, waashi wahandishi, madereva wa magari, mawakili, mahakimu, mawaziri wakuu na hata marais wananchi. Hakuna kazi isiyofanywa na mwanamke siku hizi.

    Mwanamke wa kisasa hateswi akafyata ulimi. Anapohiniwa yeye hupigania haki kwa dhati na hamasa. Katu hakubali’mahali pake’ katika jamii alipotengwa na wanaume wenye mawazo ya kihaidhina yaliyopitwa na wakati.

    Siku hizi mwanamke huolewa tu wakati amepata kazi ya kumwezesha kujikimu maishani au pale anapokuwa na hakika kwamba biashara yake, iwapo ni mfanyi biashara, imepiga hatua ya kutomrudisha ukutani.

    Mwanamke wa kisasa haamuliwi katika jambo lolote, bali hufanya maamuzi yake mwenyewe. Kwa upande mwingine, mwanaume wa ‘kisasa’, ambaye bado amefungwa pingu na taasubi za kiume, hapendezwi na mwanamke huyu. Huuma kidole akatamani yale ya akale, lakini wapi! Analazimika kukubali mwanamke huyu kama mshirika sawa maishani, na kuishi naye, apende asipende. Shingo upande analazimika kukubali kwamba mabadiliko haya sio mithili ya kiwingu kipitacho, bali ni ya aushi.

    MASWALI
    1. Msemo ‘mwendani wa vijungu jiko’ unadhihirisha hali gani ya mwanamke katika jamii? (al.2)
    2. Jamii imefanya mwanamke kuwa hayawani wa mizigo. Fafanua. (al.2)
    3. Eleza maana ya ‘akanyagapo mume papo huutia wayo wake’ (al.2)
    4. Mlinganishe mwanamke wa kiasili na wa kisasa katika maswala ya ndoa na elimu. (al.4)
    5. Mwanamume wa kisasa anamwonaje mwanamke wa kisasa? (al.2)
    6. Eleza maana ya:
      1. Akafyata ulimi (al.1) 
      2. Ukatani (al.1)
      3. Taasubi za kiume (al.1)
  2. UFUPISHO
    Soma kifungu kisha ujibu maswali.

    Imesemekana na kurudiwa tena na tena kwamba, iwapo tuna maono ya kujiondoa katika umaskini wa kupindukia, ni lazima tukipe kilimo umuhimu. Zaidi ya Wakenya milioni kumi wamo katika hatari ya kufa katika maeneo mbali mbali kwa sasa kufuatia uhaba wa chakula nchini.

    Kiini kikubwa cha njaa hiyo ni mapuuza ya muda mrefu katika sekta ya kilimo.Imesahaulika kuwa karibu asilimia sabini na tano ya Wakenya wanategemea kilimo kwa chakula na mapato ya kifedha kila siku. Kilimo hutoa karibu robo tatu ya nafasi za kazi kwa wananchi na pia kuletea serikali karibu robo ya mapato yake kutokana na mauzo ya mazao katika mataifa ya nje.
    Wataalamu wa maswala ya zaraa wanaeleza kuwa pato la nchi linatokana na kilimo huangamiza njaa mara nne zaidi ya mapato yanayotokana na shughuli nyinginezo za kiuchumi. Hiyo ni kwa sababu shughuli za kilimo hulenga kuzalisha vyakula moja kwa moja.

    Imebainika kuwa, katika mataifa mengi yanayostawi, asilimia sabini na tano ya wananchi huishi katika maeneo ya mashambani na idadi hii hutegemea kilimo kujimudu kimaisha ilhali hapa Kenya ni asilimia nne pekee ya bajeti inayowekezwa katika kilimo.Kwa wakati huo, ushuru unaotozwa bidhaa za kilimo katika maeneo haya umebainika kuwa mkubwa. Hii imepelekea uwekezaji katika kilimo kupungua na hivyo kuchangia kukithiri kwa baa la njaa.

    Wakati umewadia kwa serikali za Afrika na wapangaji wa masuala ya uchumi kuweka juhudi maradufu katika kushabikia ili kumaliza njaa na umaskini. Kuna haja ya kuwajulisha, kuwahimiza na kuwaelimisha wakulima wa mashamba madogo madogo kuhusu mihimili ya zaharaa kama vile uzalishaji wa matunda na mboga, ufugaji wa ndege, samaki na ng’ombe mbali na kuweka mikakati ya kuanzisha nafasi za kazi katika sekta ya kilimo.

    Serikali itafikia lengo hili iwapo itaanza kufadhili kilimo, kupunguza gharama za pembejeo za kilimo, kuweka sera zinazodhibiti uuzaji na ununuzi wa vyakula hasa baina ya mataifa na kuongeza sehemu ya bajeti inayotengewa kilimo. Bila hilo hatutakuwa na linguine bali kukimbilia mataifa yalistawi kuomba misaada ili kuwanusuru raia wetu kutokana na ghadhabu na njaa.
    1. Fupisha aya mbili za mwanzo (maneno 50 – 55) (al.6, 1 ½ ya mtiririko)
      Matayarisho
      Nakala safi
    2. Bila kubadili maana,fupisha aya mbili za mwisho. (maneno 55 – 60) (al.6, 1 ½ utiririko)
      Matayarisho
      Nakala safi

SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA ( ALAMA 40)

  1. Taja irabu zozote mbili za Kiswahili. (alama 2)
  2. Tofautisha kati ya shadda na kiimbo. (alama 2)
  3. Kwa kuzingatia muundo, taja aina tatu za sentensi. (alama 3)
  4. Weka maneno haya kwenye ngeli zake.
    1. Kiwete (alama 1) _______________________________________
    2. Ua (alama 1) __________________________________________
  5. Bainisha aina za maneno kwenye sentensi hii. (alama 3)
    Mtoto wa mwalimu alikuwa akicheza uwanjani.
  6. Kwa kutolea mifano , eleza matumizi mawili ya kistari kifupi. (alama 2)
  7.          
    1. Eleza maana ya mofimu. (alama 1)
    2. Taja aina mbili za mofimu. ( alama 2)
  8. Tunga sentensi zenye vivumishi vinavyoleta dhana hizi.
    1. kumiliki (alama 1)
    2. kutobagua (alama 1)
  9. Tambua aina za vielezi katika sentensi hii. ( alama 2)
    Kamau alilia kitoto alipoanguka sakafuni pu!
  10. Changanua sentensi hii kwa kutumia majedwali. ( alama 4)
    Omolo analia kwa sauti ilhali Akinyi anapika Samaki.
  11. Nyambua vitenzi hivi kwenye kauli zilizowekwa mabanoni. ( alama 3)
    1. la ( tendeka) ________________________________________
    2. nywa (tendea) ______________________________________
    3. fa(tendewa) ______________________________________
  12. Bainisha viambishi kwenye kitenzi hawakukupikia. ( alama 3)
  13. Eleza maana ya kitenzi cha asili ya kigeni. (alama 1)
  14. Tambua shamirisho katika sentensi hii. (alama 3)
    Wafula alimpikia dadake sima kwa sufuria.
  15. Kwa kutolea mifano, onyesha matumizi matatu ya -ki-
  16. Tofautisha sentensi hizi. ( alama 2)
    1. Ningelisoma kwa bidii ningelipita mtihani.
    2. Ningalisoma kwa bidii ningalipita mtihani.

ISIMUJAMII: (alama 10)
Nipe chai, andazi mbili na egg moja………….

  1. Taja sajili inayorejelewa na maneno haya (alama 2)
  2. Fafanua sifa nane zinazohusishwa na sajili hiyo. (alama 8)


Mwongozo wa Kusahihisha

  1.      
    1. Mahali pa mwanamke. kazi yake ni kutumikia jamii (1x2)
    2. Anafanyishwa kazi nyingi. (1x2)
    3. Afanyayo mwanaume mwanamke pia hulifanya. (1x2)
    4. Ndoa
      • Kiasili
        • Ndoa ya lazima 
        • Alilazimika kumzaia mume watoto
        • Anazaa watoto kwa hiari
        • Alitumishwa
        • Alifanya kazi jikoni
        • Aliamuliwa kwa kila jambo
        • Alimtegemea mume
        • Alinyamaza alipoteswa
        • Hujitetea akiteswa/ hupigania haki
      • Kisasa
        • Ndoa si lazima     
        • Ana uhuru wa kufanya atakalo
        • Si lazima aende jikoni
        • Anajiamulia mwenyewe
        • Anajiteegemea/ hujikumu (zozote 2x1 = 2)
          ELIMU
          Hakuenda shuleni - Anaenda shuleni
          Alikuwa na Elimu ya kiasili - Hana elimu ya kiasili (1x2 = 2)
    5. Hapendwi naye. Ni mkaidi, mshindani, mzushi. (1x2=2)
    6.      
      1. Akafyata ulimi – akanyamaza
      2. Ukatani – umaskini
      3. Taasubi za kiume – fikra/ wazo la kibaguzi/ uchoyo mwanaume kuona bora kuliko mke. (1x 3=3)
  2.       
    1.         
      1.  Ili kujiondoa kutoka umaskini ni lazima tuthamini kilimo/ tukipe kilimo umuhimu.
      2. Mamlioni ya Wakenya / Zaidi ya / kwa sababu ana njaa.
      3. Sababu ya njaa ni kupuuzwa kwa kilimo.
      4. Wakenya asilimia sabini na tano hutegemea kilimo kwa chakula na fedha.
      5. Kilimo hutoa nafasi za kazi.
      6. Huletea serikali robo ya mapato yake. (al.6)
    2.     
      1. Serikali za Afrika na wanaopanga masuala ya uchumi kujitahidi ili kumaliza njaa na umaskini.
      2. Wafunze wakulima wa mashamba madogo kukuza na kuzalisha matunda na mboga na kufuga Wanyama na ndege.
      3. Kuanzisha nafasi za kazi
      4. Serikali kufadhili kilimo
      5. Kupunguza gharama za pembejo
      6. Kuweka sera zinazodhibiti ya kilimo
      7. Tusipofanya hivyo tu tazidi kuomba mataifa (al.6)
        Makosa ya sarufi : ½ alama hadi makosa 6 x ½ = alama 3.
        Mtahini waakipata 0 mkosa ya sarufi hayaadhibiwi. Makosa ya hijai/ tahajiahuondolewa hadi makosa 6 x ½ = 03
  3. SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA ( ALAMA 40)
    1. Taja irabu zozote mbili za Kiswahili. (alama 2) /a/ /e/ /i/ /o/ /u/
    2. Tofautisha kati ya shadda na kiimbo. (alama 2)
      • Shadda ni hali ya kuweka mkazo kwenye vitamkwa ilhali kiimbo ni hali ya kupandisha au kushusha sauti wakati wa matamshi.
    3. Kwa kuzingatia muundo, taja aina tatu za sentensi. (alama 3)
      • Sentensi sahili
      • Sentensi ambatano
      • Sentensi changamano
    4. Weka maneno haya kwenye ngeli zake.
      • Kiwete (alama 1) A-WA
      • Ua (alama 1) U - ZI
    5. Bainisha aina za maneno kwenye sentensi hii. (alama 3)
      Mtoto wa mwalimu alikuwa akicheza uwanjani.
      • mtoto - nomino
      • wa – kihusishi/ kivumishi cha a unganifu
      • mwalimu - nomino
      • alikuwa – kitenzi kisaidizi
      • akicheza - kitenzi kikuu
      • uwanjani. - kielezi
    6. Kwa kutolea mifano , eleza matumizi mawili ya kistari kifupi. (alama 2)
      • Kuandika tarehe 14- Juni- 2021
      • Kutenga silabi ba – ba
      • Kutenga neno na maana paa- mnyama wa pori.
    7.        
      1. Eleza maana ya mofimu. (alama 1) kipashio kidogo sana chenye maana na hakigawiki zaidi.
      2. Taja aina mbili za mofimu. ( alama 2) mofimu huru na mofimu tegemezi
    8. Tunga sentensi zenye vivumishi vinavyoleta dhana hizi.
      1. .kumiliki (alama 1)
        • Mtoto wangu amelala.
        • Mtoto mwenye kikaragosi ni huyu.
      2. kutobagua (alama 1)
        • mwalimu alimsaidia mwanafunzi yeyote.
    9. Tambua aina za vielezi katika sentensi hii. ( alama 2)
      • Kamau alilia kitoto alipoanguka sakafuni pu!
      • Kitoto- E namna kimfanano alipoanguka – po ya wakati ( E wakati) pu! E namna kiigizi
    10. Changanua sentensi hii kwa kutumia majedwali. ( alama 4)
      • Omolo analia kwa sauti ilhali Akinyi anapika Samaki.
            S(ambatano)   
           S1  U    S2
        KN  KT   


        ilhali  
         KN  KT

        Omolo  
         T  E  N
         Analia  kwa sauti Akinyi  anapika  samaki.
    11. Nyambua vitenzi hivi kwenye kauli zilizowekwa mabanoni. ( alama 3)
      • la ( tendeka) - lika
      • nywa (tendea) - nywea
      • fa(tendewa) – fiwa
    12. Bainisha viambishi kwenye kitenzi hawakukupikia. ( alama 3)
      • ha – kikanushi cha nafsi ya tatu wingi
      • wa – nafsi ya tatu wingi
      • ku – ukanusho wa wakati uliopita
      • ku – mtendwa/yambwa
      • pik - mzizi
      • i - kauli ya kutendea
      • a - kiishio
    13. Eleza maana ya kitenzi cha asili ya kigeni. (alama 1)
      • Hiki ni kitenzi ambacho huwa na kiishio cha irabu /e/ , /i/ au /u/ .
    14. Tambua shamirisho katika sentensi hii. (alama 3)
      • Wafula alimpikia dadake sima kwa sufuria.
      • Dadake- kitondo
      • Sima- kipozi
      • Sufuria – ala/ chombo/ kifaa/ kitumizi
    15. Kwa kutolea mifano, onyesha matumizi matatu ya -ki-
      • Kielezi cha namna – mwalimu Metobo hufunza kistadi.
      • Kiambishi ngeli – kiatu kiko kwa fundi.
      • Kitenzi kishirikishi kipungufu – kikombe ki mezani.
    16. Tofautisha sentensi hizi. ( alama 2)
      • Ningelisoma kwa bidi ningelipita mtihani. kuna uwezekano.
      • Ningalisoma kwa bidi ningalipita mtihani. Hakuna uwezekano.
  4. ISIMU JAMII (ALAMA 10)
    1. Hotelini/mkahawani
    2.      
      • Lugha si sanifu
      • Kuchanganya ndimi
      • Utohozi
      • Sentensi fupi
      • Lugha ya heshima
      • Lugha ya biashara
      • Lugha ya ucheshi
      • Matumizi ya jazanda
      • Msamiati maalum k.m. menu n.k.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Form 4 Opener Term 1 Exams 2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest