Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Form 4 Opener Term 1 Exams 2022

Share via Whatsapp

KISWAHILI 
Karatasi ya 3
FASIHI

MAAGIZO

  • Jibu maswali manne pekee.
  • Swali la kwanza ni la lazima
  • Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki yaani; Tamthilia, Hadithi Fupi, Ushairi na Fasihi Simulizi
  • Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
  • Majibu yote yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili


Maswali

SEHEMU A: RIWAYA
 Matei: Chozi La Heri

  1. Lazima
    Mara moyo unaanza kumwenda mbio na vipapasio vya akili yake kusimama wima. Anajihisi kama anayetarajia kuanza kinyang’anyiro kikali cha upiganaji masumbwi. Kwa mbali anaskia mbisho hafifu … anatoka nje kwenda kuitikia mbisho huu … mara anaskia moyo wake ukimwambia. “Yako ya arobaini imefika, “ …
    1. Eleza muktadha wa dondoo. (alama 4)
    2. Jadili aina mbili za taswira kwenye dondoo hili. (alama 2)
    3. Bainisha mbinu nne za lugha katika dondoo. (alama 4)
    4. Kwa kurejea riwaya nzima, jadili suala la ukatili. (alama 10)

SEHEMU B: TAMTHILIA
P. Kea: Kigogo

  1.        
    1. Jimbo la sagamoyo limepitia changamoto sawa na zile zilizoko barani Afrika. Tetea ukweli wa kauli hii. (alama 10)
    2. Majoka ni joka. Jadili ukweli wa kauli hii kwa kutolea mifano kumi. (alama 10)

  2. “ Nilijua ninawaponza, nilijua ninawapunja, nilijua ninawadhuru… lakini nilimezwa na tamaa.”
    1. Eleza muktadha wa dondoo. ( alama 4)
    2. Jadili sifa nne za mnenaji. ( alama 4)
    3. Tambua mtindo katika dondoo. ( alama 3)
    4. Taja umuhimu wa mzungumziwa. ( alama 5)
    5. Kwa kurejelea tamthilia nzima, onyesha athari za tamaa. ( alama 4)

SEHEMU C: HADITHI FUPI
D. Kayanda Na A. Chokocho: Tumbo Lisiloshiba Na Hadithi Nyingine

  1.            
    1. Mtunzi wa hadithi ya Tumbo Lisiloshiba amefanikisha matumzi ya jazanda. Jadili. ( alama 7)
    2. Kwa kujikita kwenye hadithi ya Tumbo Lisiloshiba jadili maudhui yafuatayo:
      1. Tamaa na Ubinafsi ( alama 7)
      2. Umaskini ( alama 3)
      3. Unyanyasaji ( alama 3)
  2. “Wanafunzi wa chuo kikuu si kama Watoto wakembe wa shule za chekechea…”
    1. Eleza muktadha wa dondoo. ( alama 4)
    2. Binadamu amegeuka kuwa kupe mlaza damu. Jadili ukweli wa kauli hii kwa kuonyesha jinsi binadamu hutegemea wenzake kwa kiasi kikubwa. ( alama 6)
    3.  Onyesha namna mtunzi wa hadithi Mapenzi ya Kifaurongo alivyoshughulikia maudhui yafuatayo:
      1. Elimu ( alama 5)
      2. Utabaka ( alama 5)

SEHEMU D : USHAIRI

  1. Niokoa muokozi, uniondolee mashaka
    Kuyatukua siwezi, mjayo nimedhikika
    Nimekitiri simanzi,ni katika kuudhika
    Mja wako nasumbuka,nipate niyatakayo

    Mja wako nasumbuka,nataka kwao afua
    Nirehemu kwa haraka,nami nipate pumua
    Naomba hisikitika,na mikono hiinua
    Mtenda ndiwe moliwa,nipate niyatakayo

    Mtenda ndiwe moliwa,we ndiwe Mola wa anga
    Mazito kuyaondoa,pamoja na kuyatenga
    Ukauepusha ukiwa,ya pingu zilonifunya
    Nikundulia muwanga,nipate niyatakayo

    Nikundulia muwanga,nipate toka kizani
    Na huzuni n’ondolea,itoke kwangu moyoni
    Mambo mema niegheshea,maovu nisitamani
    Nitendea wa manani,nipate niyatakayo

    Igeuze yangu nia,dhaifu unipe mema
    Nili katika dunia,kwa afia na uzima
    Moliwa nitimizia,yatimize yawe mema
    Nifurahike mtima,nipate niyatakayo.

    Maswali
    1. Eleza bahari zozote mbili za shairi hili (alama 4)
    2. Eleza muundo wa shairi hili (Alama 4)
    3. Mshairi ametumia uhuru wake wa utunzi. Eleza mifano minne huku ukitoa mifano (alama 4)
    4. Andika ubeti wa pili katika lugha nathari (alama 4)
    5. Fafanua dhamira ya mtunzi wa shairi hili (alama.2)
    6. Eleza maana ya misamiati ifuatayo kama ilivyotumika katika shairi (alama 2)
      1. Nimedhihika
      2. Nifurahike mtima

SEHEMU E : FASIHI SIMULIZI

  1. Hapo zamani za kale paliishi sungura na ndovu. Wanyama hawa waliishi baharini.Maulana alikuwa amewatunukia mapenzi si haba.Makazi yao yalikuwa yamepambwa yakapambika.Walitegemea matunda mbalimbali yaliyokuwa baharini kama mapera, matomoko matikitimaji na kadhalika.

    Siku moja usiku wa manane, maji yakaanza kupwa.Ndovu aliathirika zaidi. Alijaribu kuinama majini lakini hakuweza . Alimwita sungura amsaidie lakini sungura alikuwa ametoweka. Ndovu aliamua kwenda kumtafuta sungura. Alimtafuta hadi msituni lakini hakumpata. Alihofia kurudi baharini na hadi wa leo yumo msituni.

    MASWALI
    1. Tambua utanzu na kijipera chake. (al.2)
    2. Taja fomyula zingine mbili za kutanguliza kifungu hiki. (al.2)
    3. Eleza umuhimu wa kijipera hiki. (al.5)
    4. Eleza sifa za kifungu hiki. (al.5)
    5. Eleza umuhimu wa fomyula:
      1. Kutanguliza (al.3)
      2. Kuhitimisha (al.3)


Mwongozo wa Kusahihisha

  1. Lazima
    Mara moyo unaanza kumwenda mbio na vipapasio vya akili yake kusimama wima. Anajihisi kama anayetarajia kuanza kinyang’anyiro kikali cha upiganaji masumbwi. Kwa mbali anaskia mbisho hafifu … anatoka nje kwenda kuitikia mbisho huu … mara anaskia moyo wake ukimwambia. “Yako ya arobaini imefika, “ …
    1. Eleza muktadha wa dondoo. (alama 4)
      • Haya ni maneno ya msimulizi akimrejelea Sauna. Sauna yuko kwenye mtaa wa ghushi kwa Bi. Kangara . kwa sasa Sauna ndio wanatiwa mbaroni na polisi kwa kuwateka nyara Watoto.

    2. Jadili aina mbili za taswira kwenye dondoo hili. (alama 2)
      • Taswira muono/oni - msomaji anauona moyo wa Sauna ukimwenda mbio.
      • Taswira Sikivu – msomaji anausikia mbisho hafifu.

    3. Bainisha mbinu nne za lugha katika dondoo. (alama 4)
      • Uhuishi – moyo kumwenda mbio
      • Methali – siku za mwizi ni arobaini.
      • Mdokezo/ dukuduku - … anatoka nje kwenda kuitikia mbisho huu …
      • Taswira - taswira ya vipapasio kusimama wima.
      • Tashibihi – anajihisi kama anayetarajia kuanza kinyang’anyiro

    4. Kwa kurejea riwaya nzima, jadili suala la ukatili. (alama 10)
      • Ukatili ni ukosefu wa utu. Kwa mfano :
      • Wanafunzi kutenga Ridhaa.
      • Mzee Kedi kuiteketeza familia ya Ridhaa.
      • Vijana watano kuwabaka Lime na Mwanaheri.
      • Rehema kumwacha Chandachema na nyanyake.
      • Mamake Riziki Imaculata kumtupa kwenye biwi la taka.
      • Mzee Maya kumbaka Sauna.
      • Mamake Sauna kuuficha uozo wa mumewe.
      • Naomi kumwacha Lunga na wanawe.
      • Mavyaa wa Subira kumsingizia wizi wa mayai.
      • Sally kumwacha Billy.
      • Annete kumwacha Kiriri.
  2.              
    1. Jimbo la sagamoyo limepitia changamoto sawa na zile zilizoko barani Afrika. Tetea ukweli wa kauli hii. (alama 10)
      • Majoka kuruhusu ukataji miti.
      • Majoka kupatiana kibali cha uuzaji wa pombe haramu.
      • Soko la chapakazi kufungwa.
      • Waandamanaji kupigwa bila kuleta ghasia (ni haki yao.
      • Kuamuru mkuu wa polisi (Kingi) awapige watu risasi.
      • Ashua kufungiwa seli bila hatia.
      • Majoka kumfuta kingi kazi/chopi kutishwa atamwaga unga.
      • Jabali kuuawa/ngurumo
      • Tunu kuvamiwa/kuumizwa
      • Kutishiwa kuuawa km Chopi alipangiwa kuuawa.
      • Sudi kushinikizwa achonge kinyago.
      • Babake tunu kuuawa katika kiwanda cha majoka.
      • Vijana watano kuuawa wakati wa maandamano.
      • Kuongeza bei ya vyakula maradufu
      • Kubomoa vioski katika soko la chapakazi.
      • Majoka kumtaka ashua kimapenzi
      • Wanafunzi shuleni kuadhibiwa watumie dawa za kulevya.
      • Uwanja wa soko kunyakuliwa.
      • Kutozwa kodi zaidi
      • Kutosafisha soko ilhali watu wanalipa kodi
      • Kufungwa kwa vituo vya habari
      • Ngurumo kuzikwa juu ya maiti wengine.
        (zozote 10 x 1 = alama 10)

    2. Majoka ni joka. Jadili ukweli wa kauli hii kwa kutolea mifano kumi. (alama 10)
      • Unyakuzi wa ardhi: Majoka na mshauri wake walijitwalia eneo la soko la chapakazi ili ajenge hoteli ya kitalii.jambo hili linasababisha madhara makubwa kwa wananchi waliokuwa wakitegemea soko hili kukimu familia zao
      • Mauaji ya watu: vijana watano wanauwawa wakati maadamanona wengine wanaumia.
      • Kutumia vitisho:wanaharakati wanaopinga utawala wa majoka wanatishwa.kuna vikaratasi vinavyo rushwa katika makazi yao ili wahame
      • Kuangamiza wapizani wake:jabali aiuwawa kwa jama za Majoka na chama chake kikasambaratika. Tunu,kiongozi wa wanaharakati wa kudai haki nusura auawe yule aliyetumwa kutekeleza mauaji yake hakutimiza lengo lake.
      • Ukosefu wa utu:majoka hadhamini utu/uhaiwa mtu.majoka anaamlisha watu wapigwe risasi bila kujali kuwa wana haki ya kuchagua viongozi wanaowataka.
      • Tengatawala: katika jimbo la sangamoyo kuna sumu ya nyoka ; yaani uhasama unaopendwa na viongozi ili kuwagawa wanainchi.kwa mfano Sudi ana uhasama na Boza ambaye ni mchonga vinyango mwenzake. Sababu ya uhasama wao ni kwa kuwawako katika milengo tofauti ya kisiasa. Aidha,Ngurumo na kundi lake la walevi tayari wameshatiwa sumu na utawala wa majoka , hivyo wanawahasimu wanaharakati Tunu na Sudi.
      • Kuzorota kwa maendeleo : jimbo la sagamoyo limetimiza miaka sitini ya uhuru lakini bado liko nyuma kimaendeleo.
      • Rushwa: mamapima anatoa hongo ya uronda kwa ngurumo ilia pate mladi wa kuoka keki ya uhuru.vilevile , Boza na kombe wanapokea kipande cha keki kutoka kwa kenga ili wawe wafusi wa utawala wa majoka.vivyo hivyo kwa Ngurumo. ukataji wa miti.

  3. “ Nilijua ninawaponza, nilijua ninawapunja, nilijua ninawadhuru… lakini nilimezwa na tamaa.”
    1. Eleza muktadha wa dondoo. ( alama 4)
      • Msemaji – mama Pima ( Asiya)
      • Msemewa – Tunu
      • Mahali – Lango la soko la Chapakazi
      • Sababu – baada ya kugueukwa na serikali ya Majoka kwa kumwagiwa pombe na kunyang’anywa leseni.
    2. Jadili sifa nne za mnenaji. ( alama 4)
      • Mkware- anashiriki ngono na Ngurumo.
      • Fisadi – anapewa kibali cha kuuza pombe haramu.
      • Mwenye tamaa- anatamaa ya kupata mali kwa haramu.
      • Mpyaro – anawakejeli kina Tun una Sudi huko Mangweni.
    3. Tambua mtindo katika dondoo. ( alama 3)
      • Takriri – nilijua
      • Mdokezo
      • Uhuishi – nilimezwa na tamaa.
    4. Taja umuhimu wa mzungumziwa. ( alama 5)
      • Kielelezo cha watu wasomi.
      • Kielelezo cha watetezi haki.
      • Kielelezo cha watu jasiri.
      • Anaashiria watu wenye msimamo thabiti.
      • Anawakilisha mashujaa wa jamii.
    5. Kwa kurejelea tamthilia nzima, onyesha athari za tamaa. ( alama 4)
      • Tamaa huleta kifo. Km Tamaa ya sumu ya nyoka ilimuua Ngao Junior.
      • Tamaa huleta uhasidi. k.m Majoka alimtamani Ashua na kumfanya Sudi adui.
      • Tamaa huleta ufisadi. Kenga alipewa kiwanja cha umma na Majoka.
      • Tamaa huharibu mazingira. Majoka anakata miti.
  4.         
    1. Mtunzi wa hadithi ya Tumbo Lisiloshiba amefanikisha matumzi ya jazanda. Jadili. ( alama 7)
      • kiti kulalamika – malalamishi ya maskini kuhusu dhuluma
      • jitu la miraba minne – utajiri/ uwezo mkubwa wa kifedha.
      • Tumbo lisiloshiba – tamaa kubwa ya matajiri
      • Tumbo lisiloshiba – pia ni jiji la kifahari lisilotosheka na maendeleo.
      • Jitu kukalia sehemu ya watu wanne- Tajiri mmoja kunyakua mali za maskini wengi.
      • Mstari mkali wa radi na umweso – uelewa wa wanamadongoporomoka.
      • Meza kuonekana ndogo – matajiri kuwadhulumu maskini kwa kiasi kikubwa.
      • Vyakula mkahawani– mali za watu wa madongoporoka.
    2. Kwa kujikita kwenye hadithi ya Tumbo Lisiloshiba jadili maudhui yafuatayo:
      1. Tamaa na Ubinafsi ( alama 7)
        • Jitu kula chakula chote bila kuwajali wengine.
        • Jitu kukalia sehemu ya watu wanne.
        • Jitu kula ardhi ya wanamadongoporomoka.
        • Jiji lina tamaa ya kupanuka na kustawi.
        • Wakuu wa jiji kupanga kuwapa visenti maskini badala ya kuwafidia ipasavyo.
      2. Umaskini ( alama 3)
        • kuwepo kwa vibanda uchwara.
        • Kuwepo kwa mkahawa mshenzi.
        • Kuwepo kwa mashonde na vinyesi.
        • Kuwepo kwa vibwagizo vya maji machafu.
      3. Unyanyasaji ( alama 3)
        • jitu kula chakula cha wanamadongoporomoka.
        • Jitu kutaka kula ardhi ya wanamadongoporomoka.
        • Wakuu wa jiji kutotaka kuwafidia watu.
  5. “Wanafunzi wa chuo kikuu si kama Watoto wakembe wa shule za chekechea…”
    1. Eleza muktadha wa dondoo. ( alama 4)
      1. Msemaji- Dkt. Mabonga
      2. Msemewa- wanafunzi
      3. Mahali – Ukumbi kwenye Chuo Kikuu Cha Kivukoni
      4. Sababu – baada ya msichana kuuliza swali la kitoto.
    2. Binadamu amegeuka kuwa kupe mlaza damu. Jadili ukweli wa kauli hii kwa kuonyesha jinsi binadamu hutegemea wenzake kwa kiasi kikubwa. ( alama 6)
      1. Penina kumtegemea babake ampe shilingi elfu tano kila wiki.
      2. Penina kumtegemea Dennis apate ajira.
      3. Penina na Dennis kuwategemea wazazi wa Penina walipe kodi na chakula.
      4. Wazazi wa Dennis kumtegemea Dennis kuwaondolea umaskini.
      5. Shakila kumtegemea mamake ampe// amtaftie kazi.
      6. Wanafunzi kutegemea mali za wazazi wao.
    3. Onyesha namna mtunzi wa hadithi Mapenzi ya Kifaurongo alivyoshughulikia maudhui yafuatayo:
      1. Elimu ( alama 5)
        • Dennis ni mwanafunzi wa Chuo kikuu.
        • Penina ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu.
        • Shakila ni mwanafunzi pia.
        • Dkt. Mabonga amehitimu kama Mhadhiri.
        • Bw. Kitime, babake Penina ana elimu kwani ni Katibu wa kudumu wa wizara ya fedha.
        • Mamake shakila ni msomi kwani ni mkurugenzi wa shirika la uchapishaji magazeti.
      2. Utabaka ( alama 5)
        • Kuna tabaka la juu na la chini. Wahusika wa tabaka la juu ni:
          • Wazazi wa Penina. Babake ana cheo serikalini.
          • Wanafunzi wenye Ipad na vipatakalishi.
          • Mamake shakila kwa kuwa yeye ni mkurugenzi.
          • Wanafunzi ambao wazazi wao wanamiliki magari ya umma na maghorofa.
        • Tabaka la chini :
          • Dennis na wazazi wake. Wazazi hawa ni vibarua kwenye mashamba ya matajiri. Dennis naye hana chakula chuoni na mandhari ya chumba chake pia ni duni.
  6.                        
    1.                           
      • Mathnawi - pande mbili
      • Ukaraguni - vina hubadilika badilika
      • Pindu - sehemu ya mshororo wa mwisho unaanza mshororo unaofuatia
    2.          
      • beti tano
      • Mishororo mine kila ubeti
      • Kila mshororo pande mbili
      • Kila upande mizani mine
      • Hamna kibwagizo
    3.         
      • Inkisari-nondolea-niondolee
      • Zilonifunga-zilizonifunga
      • Mazida-muokozi-mwokozi
      • Kuboronga sarufi-iseuze yangu nia
      • Tabdila-afia-afya
    4.          
      • Kiumbe wako nimeteseka mno
      • Naoma unip afueni na unipe afueni na unirehemu
      • Niwaomba nikikusulia wewe diwe
      • Unayeweza kunipa ninayohitaji
    5.         
      • Kuonyesha njia hana nguvu
      • Mungu ampe maisha mema
      • Anataka Mungu anitoe gizani
      • Amekumbwa na majaribu
    6.         
      1. Nimeteseka
      2. Nichangamke/nistarehe
  7.                
    1.                
      1. Utanzu – Hadithi (1x1)
      2. Kipera – Ngano za usuli (1x1)
    2.        
      1.       
        • Fanani : paukwa
        • Hadhira : pakawa
      2.           
        • Fanani : Hadithi! Hadithi
        • Hadhira : Hadithi njoo
    3.         
      • Huburudisha wanajamii husika
      • Huelekeza wanajamii husika
      • Huelimisha wanajamii husika
      • Huhifadhira huziona ya jamii husika
      • Huonya wanajamii wa jamii husika
      • Hujenga ushirikiano wa jamii husika
      • Hujenga kumbukumbu ya wanajamii zozote (5x1)
    4.           
      • Huhusisha wahusika wanyama
      • Wanyama hupewa tabia za binadamu
      • Huwa na ucheshi mwingi
      • Hutoa matumaini kwa wanyonge kwamba mwishowe watakuwa washindi
      • Hutoa maadili na kuonya kwa njia ya kuchekesha isiyoumiza. Zozote 5x1

    5. Umuhimu wa fomyula ya kutanguliza
      • Humtambulisha mtambaji
      • Huvuta makini ya hadhira
      • Hutoa hadhira kutoka ulimwengu halisi hadi wa ubunifu
      • Hutofautisha kipera cha hadithi na vipera vingine
      • Huashiria mwanzo wa hadithi
      • Hushirikisha mtambaji na hadhira. zozote 3x1

FOMYULA YA KUHITIMISHA

  • Hupisha shughuli nyinginezo
  • Huashiria mwisho wa hadithi
  • Hutoa funzo kwa hadithi
  • Humpisha mtambaji mwingine
  • Hupumzisha hadhira
  • Hutoa hadhira kutoka ulimwengu wa hadithi hadi ulimwengu halisi Zozote 3x1
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Form 4 Opener Term 1 Exams 2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest