Displaying items by tag: kiswahili
Sarufi na Matumizi ya Lugha - Class 8 Kiswahili Revision Notes
- Vihisishi
- Vivumishi
- Viunganishi
- Viulizi
- Vielezi
- Ngeli pamoja Na Kirejeshi Amba
- Kirejeshi-amba
- Matumizi ya -ndi
- Matumizi ya -si
- Matumizi ya Na
- Matumizi ya katika, Ni, kwenye
- Usemi Halisi na Taarifa
- Mnyambuliko wa vitenzi
- Ukubwa na Udogo
Vihisishi
Kuelezea maana ya vihisishi
Hutumiwa kuonyesha hisi au hisia ya msemaji kidhihirisha
- Furaha
- Mshangao
- Mshtuko
- Hasira
- Uchungu
- Maumivu
- Uchovu
- Huruma
- Dharau
- Wito
- Laana
Kutunga sentensi akitumia vihisishi alivyopatiwa
Vivumishi
Vivumishi ni maneno yanayotumiwa kuelezea zaidi kuhusu nomino
Aina za Vivumishi
- A -Unganifu
- Sifa
- Pekee
- Viulizi
- Idadi
- Vimilikishi
- Viashiria
Viunganishi
Neno linalotumiwa kuunganisha neno na neno, sentensi na sentensi, wazo na wazo
Kutoa mifano tofauti ya viunganishi
- Kasoro-lakini, bali
- Kusalia kitu kimoja-ila, isipokuwa
- Kinyume na matarajio-ingawa, ijapo, ilhali
- Kulinganisha kuonyesha tofauti
- Kuongezea-aidha, mbali na, licha ya
- Kuwaongoza kutunga sentensi
A - Unganifu
Kijineno kinachotokana na kuambatanisha A na herufi tofauti kwa kutegemea ngeli
Jedwali
Ngeli A-unganifu
A – WA wa - wa
KI – VI cha - vya
LI – YA la - ya
U – I wa - ya
U – ZI wa- za
I – I ya - ya
U – U wa - wa
U – YA wa - ya
YA – YA ya - ya
I – ZI ya - zi
KU kwa - kwa
PAKUMU pa – pa , kwa – kwa, mwa - mwa
Mkato wa Maneno
Huhusu nomino pamoja na vimilikishi vyote vitatu
Mifano
Baba + yake = babake
Dada + yake =n dadake
Nyanya + yenu = nyanyenu
Shangazi + yake = shangaziye
Kaka + yako = kakako
Mjomba + yake = mjombake
Viulizi
Maneno yanayotumiwa kuuliza maswali
Mifano
- Nani: hutumika katika ngeli ya A – WA kujua cheo, jina , ukoo wa watu
- Nini: kujua ni kitu cha aina gani
Hutumika katika ngeli zote isipokuwa ya A - WA - Gani:kujua aina , jamii, hali au tabia
- Lini: kiulizi cha siku au wakati
Hutumiwa kutaka kujua kipindi, siku au wakati wa tukio - Wapi:ni kiulizi cha mahali
- Vipi:kiulizi cha namna gani
Je ni neno la kuanzisha swali - Ngapi:kuuliza idadi kamili ya vitu , vyombo katika jumla
- Pi: kubainisha kati ya nyingi ili kupata kihusika au mhusika Fulani mahususi
Vielezi
Neno linaloeleza jinsi kitendo kilivyotendeka au kufafanua zaidi kuhusu kitendo
Aina za vielezi
- Wakati
- Namna
- Jinsi
- Mahali
- Idadi
- Vuhusishi
- Tanakali
- Takriri
- Tashbihi
Hutumika kwa - Lini- wakati
- Wapi – mahali
- Vipi – jinsi au namna
- Kiasi gani- idadi
Mifano
Wakati mahali namna
Leo nyumbani taratibu
Kesho darasani harakaharaka
Juma ijayo Nairobi ghafla
Mtondogoo machoni kivivu
Vielezi vya Mkazo
Takriri au shadda ni maneno yanayotumiwa kutilia mkazo au kusisitiza jambo
mifano ya takriri
- salama salimini
- bure bilashi
- raha na buraha
- kufa kupona
- liwalo liwe
- haambiliki hasemezeki
- fanya juu chini
- si wa uji si wa maji
- daima dawamu
- buheri wa afya
- hakubali hakatai
- hawashi hazimi
Ngeli pamoja Na Kirejeshi Amba
amba ni kitenzi kisaidizi kinachorejelea mtendwa au mtendaji kwa kutambulisha ama kueleza zaidi ya jambo fulani
kirejeshi –o hutumika badala ya AMBA
o-rejeshi na AMBA havitumiki pamoja
mfano
Kuku ambaye alitaga ni mkubwa
Nomino | Ngeli | Amba- | o-rejeshi |
Kuku |
A-WA |
Ambaye-ambao |
Ye-o Cho-vyo Lo-yo O-yo Yo-zo O-zo Yo-yo O-oO -yo Yo -yo Ko Po Ko MO |
Kirejeshi –amba
Kirejeshi –o cha awali na kirejessho o- cha tamati
Kufafanua jinsi ya kuambisha o rejeshi tamati na awali
o-rejeshi awali hutokea kabla ya mzizi wa kitenzi –o- rejeshi tamati hutokea mwishoni mwa sentensi
Kitenzi | o-rejeshi awali | o- rejeshi tamati |
Kimbia Kula Kuwa Kua |
Anayekimbia Anayekula Anayekuwa Anayekua |
Akimbiaye Alaye Awaye Akuwaye |
Matumizi ya –ndi
Kiainishi –ndi ni kishirikishi cha kukubali kwa msisitizo
Huambatanishwa na viwakilishi nafsi au virejeshi ili kutilia mkazo
Hutumia o-rejeshi kwenye vitenzi
Nafsi
Ndi + mimi = ndimi
Ndi + wewe = ndiwe
Ndi + yeye = ndiye
Ndi + si = ndisi
Ndi + nyinyi = ndinyi
Ndi + wao = ndio
o- rejeshi
ndi + ye = ndiye
ndi + o = ndio
Matumizi ya –si
Ni kiainishi cha kutilia mkazo
Huambatanishwa na viwakilishi nafsi au virejeshi ili kuleta msisitizo wa kukanusha
Nafsi
Si + mimi = simi
Si + wewe = siwe
Si + yeye = siye
Si + sisi = sisie
Si + wao = sio
o- Rejeshi
A –WA si + yeye = siye si + o = sio
KI – VI si + cho = sicho si+ vyo = sivyo
Matumizi ‘na’
Kiunganishi NA huambatanishwa na kiwakilishi nafsi kuonyesha PIA NA PAMOJA NA
Hutumiwa pamoja na 0-rejeshi
Nafsi
Ngeli Na + o- rejeshi
A – WA na+ye = naye nao
KI –VI na + cho = nacho navyo
LI –YA na + lo = nalo nayo
U – I na + o = nao nayo
U – ZI na + o = nao nazo
I – I na+ yo = nayo nayo
U – U na + o = nao nao
U – YA na + o= nao nayo
YA – YA na +yo = nayo nayo
I – ZI na + yo = nayo nazo
KU na + ko = nako
PAKUMU na+po na+ko na+mo
Matumizi ya ‘katika’, ‘ni’ , ‘kwenye’
Hivi ni vihusishi vya mahali
Hutumiwa kuonyesha kuwapo kwa kitu kilichotajwa mahali Fulani
Ngeli hubadilika hadi PA KU MU
Kuhimiza kuwa ni kosa kutumia hivi vihusishi pamoja
Kuambatanisha nomino na vivumishi
Vivumishi | Darasa | darasani |
Viashiria Vimilikishi Ote Oote Enyewe Enye Ingine Sifa |
Hili, hilo, lile Langu, lako,lake Lote Lolote Lenyewe Lenye Jingine Zuri, jema, baya Eupe, eusi Halina |
Hapa, hapo, pale |
Usemi Halisi na Taarifa
Usemi halisi ni maneno yalivyotarajiwa na msemaji mwenyewe
Usemi taarifa ni ripoti au maelezo yakitolewa na mtu mwengine kutoka kwa msemaji halisi
Kueleza jinsi ya kubadilisha usemi
Usemi halisi usemi taarifa
leo siku hiyo
Jana siku iliyopita/tangulia
Kesho siku ijayo
Viashiria hapa hapo au pale
Vimilikishi vya karibu ake
Mbali kidogo ako
Nafsi ya kwanza ni nafsi ya tatu
Wakati ta, ki nge
Mnyambuliko wa vitenzi
Kunyambua ni kurefusha mwisho wa vitenzi katika hali tofauti
- Tendeka
- Tendesha
- Tendeshwa
Katika kauli ya kutendeka vitenzi humalizika kwa ‘ka’
Kitenzi kauli ya kutendeka
Vuka vukika
Sahau sahaulika
Maliza malizika
Bomoa bomoka
Kula kulika
Lala lalika
Lima limika
Pika pikika
Soma someka
Fagia fagilika
Kitenzi tendesha kauli ya kutendeshwa
Lala laza lazwa
Pika pikisha pikishwa
Kimbia kimbiza kimbizwa
Rudi rudisha rudishwa
Toa toza tozwa
Ota otesha oteshwa
Oa oza ozwa
Soma somesha someshwa
Ukubwa na Udogo
Maneno katika hali ya ukubwa huwa ni kukipa kitu ukubwa usio wa kawaida na pia maneno katika hali ya udogo ni kukidunisha kitu kuliko hali ya kawaida
Ngeli pia hubadilika katika hali ya ukubwa na kuwa LI- YA ,na katika hali ya udogo huwa KI – VI
Njia tofauti za kubadili maneno katika ukubwa na udogo
Kudodosha – mw, ny na kutia j
Mfano
- ng’ombe – gombe
- Mkono – kono
- Ndama – dama
Kudodosha herufi moja na kutia ji
Mfano
- Mji – jiji
Kudodosha ki na kutia ji
Mfano
- Kisu – jisu
Kuongeza ji bila kudodoa chochote
Mfano
- Jicho – jijicho
Kutia j kwa nomino zinazoanza kwa irabu
Mfano
- uso – juso
- Uta – juta
Kiswahili - Class 8 End Term 1 Exam 2021 Set 2
DARASA LA 8, MWISHO WA MUHULA WA 1
KISWAHILI
JINA....................................................SHULE...............................
Soma vifungu vifuatavyo vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu munne hapo. Jaza pengo kwa kuchagua jawabu lifaulo zaidi.
1 marafiki wote 2 kuwa nao, siwezi kumsahau Tito asilani. Yeye 3 kuainisha aina mbalimbali 4 maneno. 5 alinifahamisha kwamba maneno kama vile 6 huitwa vielezi. Isitoshe, 7 ya kushirikiana na wengine katika shughuli za kimasomo kwani 8 , 9 nilifaidika sana kutokana na urafiki wetu.
- A. Baadhi ya B Miongoni mwa C. Fauka ya D. Licha ya
- A. niliyewahi B. aliowahi C. niliyowahi D. niliowahi
- A. ndiye aliyenifunza B. ndio alionifunza C. ndivyo alivyonifunza D. ndiye alionifunza
- A. ya B. na C. za D. wa
- A. Mathalan B. Ihali C. Kwani D. Kumbe
- A. mbali, ila. njema B. tamu, nzuri, bora C. hizo, vile, tena D. taratibu sana, vizuri
- A. alinivunja moyo B. alinitia shime C. alinipiga kumbo D. alinionea gere
- A. Mchumia juani hulia kivulini
B. Jirani ni akiba
C. Kofi hazilii ila kwa viganja viwili
D. Jua vimeundwa - A. Yakini B. Katu C. Kamwe D. Asilani
Elimu ina manufaa 10 Mtu 11 elimu ya kumfaa, maisha yake hugubikwa na giza 12 . Kwa mfano, kupitia elimu ya mazingira, tunajifunza jinsi 13 kuongeza 14 katika mazingira yetu. Vijana nao hufunzwa kutumia vipawa 15 kujikimu kimaisha
- A. anuwai B. nyingi C. mingi D. kiasi
- A. asiopata B. asingepata C. asipopata D. asikopata
- A. tiriri B. totoro C. kochokocho D. furifuri
- A. tunaoweza B. tunayoweza C. tunaweza D. tunavyoweza
- A. thamani B. dhamani C. ridhaa D. riba
- A. zao В yao C. vyao D. chao
Kuanzia nambari 16 mpaka 30, chagmujawahu lifaalo zaidi kwa kila swali
- Bainisha matumizi ya kiambishi-ka kwenye sentensi.
Mwalimu alituita akatushauri- Kuonyesha masharti
- Kuonyesha hali ya kuendelea
- Kuonyesha kutegemeana kwa vitendo
- Kuonyesha kufuatana kwa matukio
- Chagua maelezo ambayo ni sahihi.
- Kikuku ni pambo la shingoni.
- Kipuli huvaliwa upande wa kushoto wa pua
- Kishaufu ni pambo la puani.
- Bangili ni pambo la mviringo la shingoni.
- Tunasema jua, juza na nawa
- navya
- nawia
- nawishwa
- nawika
- Andika katika wingi. Jirani ameniazima uteo wake.
- Jirani wamelazima uteo wao.
- Jirani wametuazima teo zao.
- Majirani wametuazima teo yao.
- Majirani wametuazima teo zao.
- Kamilisha: Mgonjwa alibebwa na wauguzi kwa _____ hadi kwenye wodi.
- ambulensi
- machela
- toroli
- nyoka
- Kanusha: Mtoto alipoangukaaliumia.
- Mtoto alipoanguka hakuumia.
- Mtoto hajaanguka wala hakuumia
- Mioto asipoanguka hataumia.
- Mtoto hakuanguka na kuumia.
- Kutokana na kitenzi tii tunapata sifa gani?
- Utiifu
- Katii
- Mtiifu
- Tiliwa
- Geuza sentensi ifuatayo katika hali ya udogo.
Mtoto alifurahi aliponunuliwa mkoba- Kitoto alifurahi aliponunuliwa kikoba
- Toto lilifurahi liliponunuliwa koba.
- Vitoto vilifurahi viliponunuliwa vikoba.
- Kitoto kilifurahi kiliponunuliwa kikoba
- Tegua kitendawili kifuatacho.
Mlima wa Kwale hupandwa kwa kucha.- Kula sima.
- Kusuka nywele
- Muwa
- Jiwe
- Sentensi gani kati ya hizi ni tashbihi?
- Sikio la kufa halisikii dawa.
- Jina jema ni hazina maishani.
- Mikono yake ni baridi kama barafu
- Wezi wale walikimbia mkiki mkiki.
- Fahali ni kwa mtamba kama ilivyo kipora kwa
- jogoo
- tembe
- beberu
- kuku
- Andika katika usemi halisi.
Kaka aliniambia kuwa tungeenda shambani siku ambayo ingefuata.- "Utaenda shambani kesho" Kaka aliniambia.
- "Kesho wanaenda shambani" Kaka aliniambia
- "Tungeenda shambani kesho", Kaka aliniambia.
- "Mtaenda shambuni kesho," Kaka aliniambia.
- Msemo 'kuwa na kichwa kizito' una maana ya,
- kuwa na usingizi
- kutosikia
- kuwa na kichwa kikubwa
- kuwa mwerevu
- Kamilisha: Angalijua huko kulikuwa na wezi _______mlango.
- angefunga
- asingefunga
- hangalifunga
- angalifinga
- Chagua methali nyingine yenye maana sawa na hii.
Akutanguliaye chanoni hukuzidi tonge.- Mwenda mbio subiri achoke.
- Ukiona vyaelca jua vimcundwa.
- Atanguliaye kisimani hunywa maji mengi.
- Mchimba kisima huingia mwenyewe.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali kuanzia 31 mpaka 40.
Hakuna kitu muhimu maishani kuliko afya ya akili. Kwa hakika afya hii ya akili ndiyo humwezesha mtu kutenda mambo jinsi anavyotakikana. Mtu mwenye afya ya akili huweza kutangamana vyema na wenzake bila kuwabughudhi kwa lolote. Aghalabu mtu huyu huwa mfurufu wakati wote, jambo ambalo humsaidia kudumisha hata afya ya mwili.
Matendo ya watu wengi katika siku za hivi karibuni yanadhihirisha kuwa afya ya akili inazidi kudorora. Imekuwa kawaida kama sheria kusikia kuwa mtu fulani amechukua silaha na kumwumiza mwenzake vibaya. Wengine wanatumia silaha za maangamizi ya halaiki pasi na kisa wala sababu. Baadaye watu hawa wakipelekwa mbele ya sheria huonekana kuchanganyikiwa; yaani hawajijui hawajitambui.
Je, ni nini hasa kinachochangia kuvurugika kwa afya ya akili? Kwanza, binandamu anapokabiliwa na hali ngumu ya maisha kila uchao, hujipata akihangaika kimawazo. Hali hii ikiendelea kwa muda mrefu pasipo kushughulika ipasavyo, akili ya mhusika huweza kuenda tenge. Watu wengi, wakubwa kwa wadogo wanaendelea kuhangaika kwa sababu mbalimbali.
Matumizi mabaya ya vileo yamewafanya baadhi ya watu kuwa punguani. Kwa mfano, uvutaji wa bangi ni sababu kuu ya vijana wengi kurukwa na akili. Ni vyema tujitenge na waraibu wa mihadarati kwani niazi mbovu ni harabu ya nzima.Kwa hakika dawa hizi hazina manufaa yoyote.
Ili kudumisha afya ya akili, ni lazima ushauri nasaha uimarishwe katika sekta zote za kijamii. Kupitia ushauri walmarika shuleni kwa mfano, vijana watashauriwa kuhusu madhara ya kuandama sana starehe vilevile, watajifunza kuratibu muda wao na kuutumia kwa njia ya manufaa. Vilevile, wataelekezana kutambua mbinu mwafaka zaidi za kuepuka vishawishi vinavyoambatana na ujana.
Serikali haina budi kukabiliana na ulanguzi wa dawa za kulevya. Hili halitafanyika kwa kuwatia nguvuni waraibu tu. Huku ni kama kupogoa matawi ya mti na kuutarajia ukauke. Biashara hii sharti ikomeshwe kuanzia kwa wauzaji wa humu nchini na hata magenge ya kimataifa.
Mtu anapokabiliwa na tatizo, ni vyema kuwaendea washauri ili aongozwe kwa njia ifaayo. Wale walioathirika nao wajikubali na kutafuta matibabu kabla hali zao hazijazorota zaidi. Taifa halitaweza kupiga hatua bila raia wake kuwa razini.
- Chagua maelezo yanayolingana na aya ya kwanza.
- Afya ya akili ndicho kitu muhimu pekee maishani.
- Mtu akiwa na matatizo ya akili huoneakana waziwazi.
- Mtu asiye na afya ya akili ni mwendawazimu.
- Utendaji wa mtu huweza kuathiriwa na afya ya akili.
- Wanajamii wakiwa na afya ya akili,
- hudumisha uhusiano mwema baina yao.
- huvuruga maingiliano miongoni mwao.
- hawakabiliwi na shida zozote maishani.
- hukabiliwa na changamoto nyingi maishani.
- Kulingana na aya ya pili,
- malezi mabaya ya watoto yamewafanya wengi kupotoka.
- maovu yameongezeka kutokana na kuzorota kwa afya ya akili.
- matumizi ya silaha yanavuruga afya ya akili.
- si kawaida kwa watu siku hizi kuumizana kwa silaha.
- Maneno hawajijui hawajitambui yametumia tamathali gani ya usemi?
- Sitiari
- Tanakali za sauti
- Vielezi ya kutilia mkazo.
- Tashbihi
- Chagua jibu lililo sahihi.
- Wote wanaohangaika hupata shida za kiakili.
- Kukosa kusaidiwa husababisha matatizo ya akili.
- Kuhangaika kwa muda mrefu huathiri afya ya akili.
- Hali ngumu ya maisha ni mfano wa shida za kiakili.
- Hali anayopinga mwandishi hasa katika aya ya nne ni,
- hali ya vijana kurukwa na akili.
- madhara ya mihadarati hasa katika familia.
- watu wanaotumia pesa kununua mihadarati.
- matumizi mabaya ya vileo.
- Methali 'Nazi mbovu harabu ya nzima' ina maana kuwa,
- Ukifuatana na watu wabaya watakupotosha.
- Ukitumia mihadarati vibaya utahasirika.
- Vijana wakitumia mihadarati watakuwa punguani.
- Watu wazima wakiingilia ulevi vijana watawaiga.
- Yapi ni manufaa ya ushauri wa marika?
- Vijana huonyeshwa jinsi ya kuandama starehe.
- Vijana walioshauriwa hawapatani na vishawishi vyovyote.
- Vijana hujifunza kutumia muda wao ipasavyo.
- Vijana hushauriwa kuhusu dawa zifaazo.
- Kupogoa matawi ya mti kumelinganishwa na
- kuwanasa walanguzi wa mihadarati.
- kuwashika wanaotumia mihadarati.
- kukabiliana na magenge ya kimataifa.
- kumaliza kabisa biashara ya mihadarati.
- Kichwa kifaacho zaidi kwa makala haya ni
- Madhara ya mihadarati.
- Umuhimu wa ushauri nasaha.
- Umuhimu wa afya ya akili.
- Serikali kupunguza shida za maisha.
Soma makala yanayofuata kisha ujibu maswali kuanzia 41 - 50.
Msenangu alifahamika katika kijiji chao na takriban kila mtu. Watoto walimfahamu kutokana na mtindo wake wa kutembea. Alitembea wima kama askarijeshi na kila alipokwenda kupiga chupa zake, alikuwa na mazoca ya kupiga kwata kama mwanajeshi gwarideni. Sababu nyingine iliyomfanya Msenangu afahamike ni ucheshi wake. Aliwasimulia vijana hadithi za kila aina na kuwavunja mbavu kwa umahiri wake wa kuzitamba hadithi zenyewe.
Ingawa Msenangu alikuwa na umri mpevu sana, alikuwa mmoja kati ya wazee wachache wa kwao waliojua kusoma. Idadi ya waliojua kusoma wakati huo ilikuwa akali sana na mzee huyo aliona fahari kuwa miongoni mwa hao wachache. Habari za kuandikwa kwa katiba mpya zilipofika kijijini, Msenangu alifurahi na kuchanua uso. Hii ni nafasi ya kuhakikisha kuwa nimewaeleza yote yanayohitajika kufanywa : alijitapa Msenangu. Wanakijiji walitaka kuteua vijana wawawakilishe ambapo tume ya kuandika katiba ampya ingefika pale kijijini. Hata hivyo, Msenangu alikazania kuwa ni lazima angekuwa mmoja wao. Licha ya uwezo wake wa kusoma, wanakijiji wengi hawakuamini kuwa alijua lolote kuhusiana na katiba.
Siku yenyewe, vijana walioteuliwa walitumia lugha ya kisheria ambayo ni dhahiri wanakijiji wengi hawakuielewa. Muda is muda, watu walianza kuondoka ukumbini mmoja mmoja. Ndipo bila kungoja aalikwe, mzee Msenangu alisimama. Watu waliokuwa nje ya ukumbi waliambiana, "Haya Msenangu huyo!' Alianza kuongea," Ndugu wanakamati, nimcisubiri fursa hii kwa hamu kubwa. Maneno yangu mimi si mengi kwani sikusoma mambo hayo ya "yesi" "yesi". Lakini ningependa kusema machache niliyo nayo moyoni. Nataka iandikwe katiba itakayoiendesha nchi yetu, kwa njia nzuri, kwa miaka mingi ijayo.Katiba hiyo ni lazima iwalinde raia wote, walemavu na wasio walemavu waonao na wasioona, waumini na walevi' alianza Msenangu. Watu walimtazama kwa mshangao mkubwa.
"Tulieni tumsikilize!” Wengine walisema. Wale waliokuwa wakiondoka ukumbini walirudi haraka kuketi. iangu akaendelea, “Katiba inayoifaa nchi ni ile isiyozingatia matakwa ya kundi moja la jamii tu... zima ziwepo njia za kuwadhibiti viongozi hawa kuhakikisha kuwa wanapotwaa madaraka hawatugeuzi sisi wanyonge kuwa wanase sere wao wa kuchezea, "alisema Msenangu na kutua. Ukumbi mzima sasa ukawa umemtegea sikio ndi!
Wanakumati walikuwa wakiandika huku wakiitikia kwa vichwa vyao. "Sisi wanyonge tunaoishi huku mashambani tuna shida. Wahenga walisema "Sheria ni msumeno hukata mbele na nyuma" Lakini kwetu huku haikati, inakala nyuma tu. Wenye vyeo wanapotamani vikataa vyetu wanavitwaa tu kwa njia rahisi wakitumia vyeo vyao. Tunaposhindwa kulipa pesa za michango ambazo hatuna, machifu wanaamuru mifugo yetu isombwe. Pawepo na sheria za kuwadhibiti watu kama hao. Kwa kifupi, iwe sheria inayotetea tajiri na maskini, mr yonge na mwenye nguvu, aliye nacho na asiye nacho.
Wanakamati wapendwa, usalama umeadimika kama mito jangwani. Sisi wenyewe tumegeuka walinda usalama. Lakini jambo la kushangaza ni kwamba tuwatiapo wahuni hao mikononi mwa walinda usalama wanazunguka mbuyu na kuwa huru.
Katika nchi inayothamini raia wake, bei za bidhaa haziongezeki shaghalabaghala tu. Ningetaka katiba iangalie jambo hili."
Baada ya kusema haya Msenangu akachukua mkongojo wake na polepole akatoka ukumbini na kuuacha umati umeduwaa. Kisha ukumbi ukalipuka pu kwa makofi na vigelegele ukimshangilia Msenangu ambaye alikuwa tayari ameshaondoka.
- Chagua jibu lisilo sahihi
- Watu wote walimfahamu Msenangu.
- Msenangu alikuwa na tabia ya ulevi,
- Msenangu alizoca kuwafurahisha watu.
- Watoto walimfahamu Msenangu kwa kutembea kijeshi.
- Maana ya kuwavunja mbavu ni
- kuwaumiza mbavuni
- kucheka kisirisiri
- kuwachekesha sana
- kuwashangaza watu
- Ni jambo lipi alilojivunia Msenangu?
- Kupendwa na watu wengi.
- Elimu aliyokuwa nayo.
- Kuwashinda vijana kiclimu.
- Kuwa na wasomi kijijini.
- Msenangu alifurahishwa na habari za kuandikwa kwa katiba mpya kwa sababu,
- angeonyesha ubingwa wake kwa wale wasiomjua.
- angeshindana na vijana katika maarifa yao.
- aliwachukia viongozi waliokuwa mamlaka
- angependekeza njia za kuboresha utawala.
- Kwanini wanakijiji walianza kutoka ukumbini?
- Muda ulikuwa umeyoyoma.
- Hawakuzielewa hotuba ya wazungumzaji.
- Walikerwa na maneno ya Msenangu.
- Walipuuzwa na waandishi wa katibampya.
- Watu walishangazwa zaidi na Msenangu kutokana na,
- umaarufu wake wa kusema
- kupinga maovu ambayo hawakuyajua.
- kupigana na serikali iliyokuwa mamlakani.
- kuchangia hoja nzito zenye umuhimu.
- Sheria ni msumeno hukata mbele na nyuma kwani,
- haipendelei wala kumbagua yeyote.
- sheria haina manufaa kwa mtu yeyote.
- sheria wakati wote huwabagua wanyonge.
- huwaumiza watu wote katika jamii.
- Kulingana na maneno aliyoyasema Msenangu
- usawa ulikuwa ukizingatiwa huko zaidi.
- katiba ya zamani ilikuwa bora zaidi.
- wanyonge walikuwa wakidhulumiwa katika jamii.
- viongozi wa jamii walionyesha uzalendo.
- Nini kilichangia zaidi kudorora kwa usalama?
- Wananchi kukosa kushirikiana.
- Uhaba wa kazi katika jamii.
- Kukosa sheria za kuwahukumu wahalifu.
- Ufisadi uliowafanya wahalifu kuachwa huru.
- Kilingana na aya ya mwisho
- Hotuba ya Msenangu ilikatizwa kwa makofi.
- Msenangu hakuwepo aliposhangiliwa.
- Bei za bidhaa zilikuwa juu sana.
- Msenangu alituzwa kwa mkongojo.
INSHA
Wewe ni mmojawapo wa wanafunzi wa darasa la nane shuleni mwako. Andika hotuba utakayowatolea wanafunzi wengine shuleni kuhusu jinsi ya kuimarisha matokeo yao katika mitihani.
MAAKIZO
- B
- D
- A
- C
- A
- D
- B
- C
- A
- A
- C
- B
- D
- A
- C
- D
- C
- A
- D
- B
- A
- C
- D
- A
- C
- B
- D
- A
- D
- C
- D
- A
- B
- C
- C
- D
- A
- C
- B
- C
- A
- C
- B
- D
- B
- D
- A
- C
- D
- B
Kiswahili - Class 7 End Term 1 Exam 2021 SET 2
Tumia msamiati ulio mwafaka zaidi ujaze kwenye vihasho 1 hadi 15.
Ni kweli kwamba jinsi tunavyoendelea kukua ndivyo __1__ kujifunza mambo mengi aushini. __2__ya hayo ni kazi. Kazi ndiyo _3_ wa maisha ya binadamu. Kazi ni kazi, iwe ya_4_au rahisi; usichagve. Kwani kazi_5_hutusaidia_6_ riziki yetu. Tujizoeshe, tupende na__7__ kazi mapema. Wajibu_8_nyumbani ni kuwasaidia wazazi katika kazi zote. Ubwete haufai_9_ hauwezi kutulisha. Tuchape kazi kwanza_10__tupumzike.
-
- tunazidi
- tunavyozidi
- tunakozidi
- tunakozidi
-
- Mmojawapo
- Mojawapo
- Kimojawapo
- Umojawapo
-
- uti wa mgongo
- uti wa mkono
- uti wa kichwa
- uti wa mguu
-
- suluhu
- sulu
- zulu
- sulubu
-
- ndicho
- ndiyo
- ndilo
- ndio
-
- kusunbua
- kuzubua
- kuzumbua
- kusafirisha
-
- kuendeleza
- kuendelesha
- kuendelea
- kuendeleshwa
-
- yetu
- zetu
- letu
- wetu
-
- na
- wala
- ingawa
- lakini
-
- ndiyo
- ndio
- ndipo
- ndiko
Je_ 11_ wajua kuwa ni haki ya kila mtoto kupata elimu? Ni kwa kutambua jambo hili _12_serikali ya Kenya ilitangaza kuwa itatoa elimu bila malipo kwa watoto wote ili kila _13__ apate nafasi ya kujipatia elimu ya msingi. Hali kadhalika watoto wa_14_wa kwenda shule hawapaswi kuajiriwa mahali_15 .
-
- ,
- ?
- !
- .
-
- ambako
- ambao
- ambaye
- ambapo
-
- moja
- mmoja
- mamoja
- mojawapo
-
- rika
- wakati
- umri
- muda
-
- pote
- kokote
- popote
- kote
Kutoka swali la 16 mpaka 30, jibu kulingana na maagizo.
- Sentensi;
Nilipigiwa mpira ina maana zifuatazo isipokuwa- mpira ulipigwa ukielekezwa kwangu
- nilisaidiwa kupiga mpira
- nilipigwa kwa sababu ya mpira
- mpira ulitumiwa kunipiga
- Umbo hili ni
- mstatili
- mche
- duara dufu
- pia
- Neno "maji" liko katika ngeli gani?
- I-I
- YA-YA
- I-ZI
- LI-YA
- Kamilisha methali: Mchumia juani
- hulia kivulini
- hali wali mkavu
- huumiza mkonowe
- marejeo ni ngamani
- Chagua umoja wa sentensi hii:
Watajiwakilisha wao wenyewe- Nitajiwakilisha sisi wenyewe
- Atajikilisha wewe mwenyewe
- Nitajiwakilisha mimi mwenyewe
- Atajiwakilisha yeye mwenyewe
- Petro alitia ________ masomoni na akuibuka mwanafunzi _______ zaidi.
- chumvi, mzuri
- bidii, upya
- fora, bora
- kauri, kauli
- Msichana alitumia __________ kulia vibanzi.
- umma
- uma
- kijiko
- mwiko19.
- Ni sentensi ipi iliyoakifishwa vizuri?
- Nilinunua sukari, chumvi, mayai, biskuti
- Baba wa Wambui ni karimu
- Lo! Ameshindwa kufunga bao!
- Mji wa Mombasa unapendeza
- Ni vazi gani lisilovaliwa na wanaume?
- Chupi
- Kizibao
- Fulana
- Kanchiri
- Andika kwa wingi
Mama yake alipoteza ufunguo- Mama zao walipoteza funguo
- Wamama wao walipoteza funguo
- Kina mame zao walipoteza funguo
- Mama zetu walipoteza funguo
- Chagua kiunganishi katika sentensi hii.
Nilifika sokoni ijapokuwa nilichelewa.- sokoni
- nilifika
- ijapokuwa
- nilichelewa
- Tambua kimilikishi katika sentensi ifuatayo:
Tulimkuta mlevi akiwa amelala nyumbani kwake.- mlevi
- kwake
- nyumbani
- amelala
- Mnyama wa porini anayefanana na ng'ombe
- swara
- twiga
- pundamilia
- mbogo
- Kalamu yangu ______ jana
- iliibiwa
- iliiba
- iliibwa
- uliibwa
- Kifaa cha ufundi kinachotumiwa kukerezea mbao ni
- msumeno
- patasi
- nyundo
- timazi
Soma kisa kifuatacho kisha ujibu swali 31 hadi 40.
Siku ya kurudi shuleni iliwadia wazazi wa Pendo waliandamana naye kurudi shuleni. Ulikuwa mwisho wa mwezi na magari ya abiria yalijaa pomoni. Hata hivyo, walifika shuleni salama salimini. Pendo alikuwa amejawa na soni usoni. Hakutaka kumwona yeyote pale shule hasa wanafunzi. Hata hivyo alijikaza kwani alimaizi kuwa lisilobudi hutendwa.
Walimu walimweleza mzazi wa Pendo vile mwanao alivyopotoka zaidi ya kuwa na vipawa adinu. Waliwaeleza pia kuhusu Maria. "Huyu mtoto wa kitajiri ndiye anayempotosha Pendo. Ni lazima aachane naye kabisa ili afaulu katika maisha ya baada "Mwalimu mkuu alisema.
Babake Pendo aliposikia jina Maria likitajwa alianza kutafakari. “Mbona jina hili si geni kwangu?" Alijisaili moyoni. Jina lilo lilifanana n a mtoto wa mwajiri wake hata ingawa majina hufanana. Hakuona uwezekano wa mtoto wa mwajiri wake kuwa ndiye aliyemharibu mwanawe. Vilevile, hakuona kama kuna uwezekano kuwa mtoto wa tajiri angesomea hapo. .
Musa, babake Pendo, hakujua alikosomea mtoto wa kiwajiri wake. Hata hivyo, fikra na jina hilo zilimtatiza kwa muda baba mtu. Baada ya muda mapi kupita, Musa alimuuliza mwalimu jinsi ya kumsaidia Pendo. Mwalimu mkuu alieleza kwamba jambo lilo lingesuluhishwa vizuri kwa kuwahusisha wazazi wa Maria.
Mwalimu alielezea kwamba wazazi wa Maria walikuwa mabwanyenye katika mitaa ya kifahari Dhahiri shahiri kuwa haingekosa kuwa yule alikuwa mwajiri wake. Hakutaka mwalimu ajue hivyo licha ya kuwa hisia zake zilidhihisha mengi.
Mwishowe waliagana kwamba Pendo alipaswa kusauriwa na mwalimu na angeripoti katika ofisi ya mwalimu kila alasiri. Pia alipaswa kuadhibiwa kwa kosa lake la kutoroka na ashauriwe barabara na mwalimu kabla ya kwenda kulala.
- Magari yalijaa pomoni kwa nini?
- Ilikuwa siku ya kurudi shuleni
- Ilikuwa asubuhi
- Ni kawaida ya magari kujaa
- Ulikuwa mwisho wa mwezi
- Pendo alirudi shuleni
- kwa hiari yake
- siku ya kufungua shule
- kwa furaha mpwitompwito
- shingo upande
- Pendo alikuwa nyumbani kwa sababu
- ulikuwa mwisho wa mwezi
- ulikuwa wakati alikizo
- alitumwa nyumbani kwa utovu wa nidhamu
- alitaka kuja shuleni ma mzazi wake
- Maisha ya baadaye ni maisha gani?
- Maisha ya kisogoni
- Maisha ya masomo
- Maisha yajayo
- Maisha ya furaha
- Pendo alisomea shule ya aina gani?
- Ya malazi
- Ya wavulana na wasichana
- Ya wasichana pekee
- Yakutwa
- Kwa nini Musa hakutaka wazazi wote wahusike kutafuta suluhisho?
- Wazazi wa Maria hakujulikana
- Walikuwa ndio waajiri wake
- Wangetumia wakati mwingi
- Wazazi wa Maria walikuwa bwanyenye
- Neno bwanyenye lina maana gani?
- maskini hohehahe
- mti anayeajiri wengine
- mtu mkubwa serikalini
- Mtu mwenye mali mengi
- Pendo alikuwa amefanya kosa gani?
- Hatujaambiwa
- Kupigana
- Kutoroka shuleni
- Kupendana ma Maria
- Ni jambo gani Pendo alipaswa kutenda?
- Kusauriwa kila siku
- Kuadhibiwa
- Kutumwa nyumbani
- Kuachana ma marafiki wote
- Hisia za Bwana Musa zilidhihirisha nini?
- Kwamba mtoto alikuwa na shida
- Kwamba alimjua mzazi wa Maria
- Kwamba Pendo alikuwa hajafanya kosa
- Kwamba mtoto angeadhibiwa
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41 had 50.
Ni wazi kama jua la mtikati kuwa demokrasia katika nchi yetu ya Kenya imekua kwa kiwango kikubwa. Bila shaka hili ni suala la kujivunia kwani inamaanisha kuwa tunaenda na wakati. Demokrasia ni mfumo wa kuendesha serikali iliyochaguliwa na watu kwa manufaa ya watu wenyewe. Tangu tulipojinyakulia uhuru yapata miongo mitano iliyopita, nchi yetu imepiga hatua kubwa katika ulingo wa kisiasa.
Rais wa kwanza wa taifa letu tukufu hayati Mzee Jomo Kenyatta aliposhika hatamu za uongozi, alihakikisha kuwa amewaunganish wananchi wote wa taifa hili na kuwapa sababu tosha ya kuionea fahari nchi yao. Aliasisi falsafa ya Harambee ambao ulikuwa mwito wa kuwahamasisha wananchi kushirikiana na kuchangia maendeleo yao kwa kuvuta pamoja. Mwito huo ulileta ari na mshawasha kwa wananchi wa Kenya na kuwahimiza wafanye kazi kwa bidii ili kuinua uchumi wa nchi yao.
Aliposafiri kwa njia ya marahaba mnamo mwaka wa elfu moja mia tisa sabini na nane, hayati rais Daniel Toroitich Arap Moi alishikilia uzi huo huo na kuanzisha mwito wa Nyayo ambao ilimaanisha ya kuwa angefuata nyayo za mtangulizi wake na kuhimiza Wakenya kuishi kwa amani, upendo na umoja.
Hayati Rais Moi alikaa kwenye kiti cha enzi liwa miaka ishirini na minne. Ijapokuwa hakuna kapa isiyokosa usubi, alifanya mengi ya kujivunia pia. Hatimaye Rais Mwai Kibaki ambapo Kenya ilijipatia Katiba mpya ambayo hadi sasa imebadilisha sura ya uongozi katika nchi yetu. Kuna mabadiliko mengi ambayo yamejidhihirisha waziwazi hususan katika ulingo wa kisiasa, siyo jinsi mambo yalivyokuwa katika miaka ya awali.
Kwa mujibu wa katiba ya sasa, wakati wa uchaguzi mpiga kura atahitajika kuwachagua viongozi zaidi ya watano. Atahitajika kumchagua rais, gavana wa jimbo lake, seneta, mbunge, mwakilishi wa wanawake bungeni na mwakilishi wa baraza la jimbo. Kwa ujumla, inatazamiwa kuwa katiba hii itaibua viwango vya hali ya juu vya uwajibikaji miongoni mwa wanasiasa na wale wote walio katika nafasi za uongozi.
- Kidemokrasia, viongozi wa serikali hupigiwa kura na kuchaguliwa na ________ wa nchi husika.
- wabunge
- watu
- wazalendo
- raia
- Kiongozi mkuu kabisa wa nchi ambayo ni jamhuri na huchaguliwa kidemokrasia
- Gavana
- Waziri mkuu
- Rais
- Mfalme
- Ni kauli ipi si sahihi kwa mujibu wa kifungu?
- Kenya imekuwa nchi huru kwa zaidi ya miaka hamsini
- Kenya ilijinyakulia uhuru wake mwaka wa hamsini
- Rais wa kwanza na wa pili kwa sasa hivi ni hayati
- Kenya tulibadilisha katiba wakati wa Rais Mwai Kibaki
- Katika aya ya pili, mwandishi hatudokezei kuwa
- Hayati Mzee Jomo Kenyatta aliwapa wananchi wa Kenya sababu tosha ya kuionea fahari nchi yao .
- Hayati Daniel Toroitich Arap Moi aliaga mwa wa elfu moja mia tisa sabini na nane
- Rais Moi alianzisha kauli mbiu ya kufuata nyayo za Mzee Kenyatta
- Mwito wa Harambee ulianzishwa
- Msemo"................ Aliposafiri njia ya marahaba ........." haumaanishi?
- alipoaga
- aliposafiri jongomeo
- alipofariki
- alipoenda na kucheza ngoma
- Kulingana na kifungu
- Hayati rais Moi aliongoza nchi ya Kenya kwa zaidi ya miongo miwili
- Kauli mbiu ya Harambee ilihimiza Wakenya kutoishi kwa amani, upendo na umoja
- Rais Kibaki alibadilisha sura ya uongozi
- Katiba mpya imeibua maswala mengi mazito
- Methali nyingine yenye maana sawa na
"Hakuna kapa isiyokosa usubi" ni- hakuna kovu la masimango
- hakuna masika yasiyokuwa na mbu
- kila shetani na mbuyu wake
- haba na haba hujaza kibaba
- Nchi ya Kenya ilipatia uhuru mwaka wa
- 1973
- 1964
- 1963
- 1978
- Katika aya ya mwisho tunadokezewa ya kwamba
- mpiga kura atapiga kura kuwachagua viongozi watano
- katiba mpya itaibua viwango vya ajabu
- bunge litakuwa na wawakilishi wa wanawake
- rais, makamu wake, spika na seneta ni baadhi ya viongozi wa serikali ambao watachaguliwa wakati wa uchaguzi
- Neno miongoni mwa limepigwa mstari katika ufamu liko katika kitengo kipi cha sarufi?
- Kihisishi
- Kihusishi
- Kiunganisho
- Kivumishi
KISWAHILI INSHA
- Soma kichwa cha insha kwa makini na uandike insha
Andika insha ya kusisimua sana ukimalizia maneno yafuatayo
....................................................................................................... Kwa kweli niligundua ya kuwa, Mungu akifunga nafasi moja, hufungua nyingine.
MARKING SCHEME
- C
- B
- A
- D
- B
- C
- A
- D
- B
- C
- A
- D
- B
- C
- C
- D
- D
- B
- A
- D
- C
- B
- C
- D
- A
- C
- B
- D
- C
- A
- D
- D
- C
- C
- A
- B
- D
- C
- A
- B
- D
- C
- B
- B
- D
- A
- B
- C
- C
- B
Kiswahili - Class 6 End Term 1 Exam 2021 Set 2
DARASA LA 6, MWISHO WA MUHULA 1
KISWAHILI
JINA....................................................SHULE.............................
Soma vifungu vifuatavyo. Kina nafasi 1 hadi 15. Kwa kila nafasi, umepewa maneno manne hapo. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa
Mtoto 1 aliacha mchezo 2 aliokuwa nao na akafuata maneno 3 akiambiwa afuate na baba yake. Alitokea 4 mtoto 5 6 wote 7 darasani 8 , kwa hivyo mtihani 9 yeye ndiye 10 wa kwanza.
- A. ule B. yule C. wale D. vile
- A. yake B. zake C. wake D. lake
- A. aliyokuwa B. aliokuwa C. alizokuwa D. alilokuwa
- A. kua B. kuka C. kuwa D. kukuwa
- A. mhodari B. hodari C. mbora D. mshujaa
- A. kumliko B. kuwaliko C. kuliko D. kukiliko
- A. huo B. hilo C. hiyo D. humo
- A. mwao B. lao C. yao D. nao
- A. ulikuja B. ulipokuja C. uliyekuja D. ilipokuja
- A. atakayekuwa B. aliyekuwa C. angekuwa D. angalikuwa
Ama kweli, elimu ni bahari 11 haina mwisho. Kila siku, mja 12 jambo 13 ambalo hakulijua. Nayo elimu humfaa mmiliko wake kwa 14 na marefu. Mtu aliyesoma, kwa mfano, hupata kazi nzuri na hujua 15 na watu.
- A. ambalo B. ambao C. ambaye D. ambayo
- A. amejifunza B. anajifunza C. hujifunza D. atajifunza
- A. mpya B. jipya C. mapya D. lipya
- A. mapana B. mengi C. machache D. mageni
- A. Kutengana B. kutengemana C. kutangamana D. kutegana
Kutoka swali la 16 mpaka 30, chagua jibu lililo sahihi
- Kitenzi 'choka katika kauli ya kutendesha ni
- chokesha
- choza
- chosha
- chokea
- Tumia kiunganishi mufti kujaza pengo
Niliweza kumwua ndovu ______ swara- laiti
- ilhali
- sembuse
- lakini
- Udogo wa neno 'mwana' ni
- jijana
- jana
- Kimwana
- kijana
- Chagua kinyume cha neno lililopigiwa mstari katika sentensi ifuatayo
Baada ya kutabasamu, alianza kuhutubia hadhira- kucheka
- kununa
- kughafilika
- kulia
- Kamilisha methali ifuatayo
Dua la kuku halimpati- mjinga
- ndege
- mbwa
- mwewe
- Sehemu ya chini ya sikio huitwa
- ndewe
- masharubu
- paji
- mashavu
- Andika wingi wa sentensi ifuatayo.
Mti uzaao embe unaitwa mwembe.- Miti zizaazo miembe zinaitwa maembe.
- Miti izaayo miembe inaitwa maembe.
- Miti izaayo maembe huitwa myembe.
- Miti izaayo maembe inaitwa miembe.
- Jaza pengo kwa kivurishi kilaache
Mtoto _____ alianguka vibaya sana- mwenye
- wenyewe
- mwenyewe
- enyewe
- Mtu anayefanya kazi ya kujenga kwa mawe huitwa
- sonara
- mwashi
- hamali
- nokoa
- Tegua kitendawili hiki
Njoo umwone umpendaye.- Kioo
- Picha
- Runinga
- Filamu
- Malipo ya kuolewa huitwa
- nauli
- koto
- mahali
- mahari
- Kanchiri, shimizi, kaptura na kocho kwa jina moja ni
- nguo
- mavazi
- mapambo
- maumbo
- Bainisha akisami inayoonyesha subui
- 1/7
- 1/3
- 1/8
- 1/9
- . Tumia '-ingine kwa usahihi:
Mama amenunua nguo _______ nyingi- zingine
- ingine
- nyingine
- mengine
- Tumia 'amba' kwa usahihi
Mwalimu aliyeingia na vitabu ni Bwana Mirobi.- Mwalimu ambaye anayeingia na vitabu ni Bwana Mirobi
- Mwalimu ambaye aliyeingia na vitabu ni Bwana Mirobi
- Mwalimu ambaye aingiaye na vitabu ni Bwana Mirobi
- Mwalimu ambaye aliingia na vitabu ni Bwana Mirobi.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31-40
Adili alijiandaa kwa safari ya kuitikia wito wa mfalme.
Farasi watatu walitandikwa matandiko mazuri. Yeye alipanda farasi mmoja, na mmoja kwa kila nyani. Ikibali alipanda farasi wake mwenyewe. Farasi wa Adili na yule wa Ikibali walikwenda sambamba njiani. Nyuma yao waliandamana nyani juu ya farasi. Kila mtu aliyeona nyani wamepanda farasi alistaajabu. Mnyama kupandwa na mnyama! Ulikuwa mpeo wa miujiza kwa watu.
Vinywa vya umati wa watu vilikuwa wazi kwa kivumo cha lo salala! Wakati umefika wa mawe kusema, miti kujibu na wanyama kuwa watu! Ikibali aligeuza uso wake kwa Adili akasema kwa ucheshi, "Mbwa wanatubwekea kama walionusa kundi la wanyama wanaowindwa." Adili alikubali kwa kuinamisha kichwa akitabasamu. Walisafiri hivi mpaka nchiya mfalme. Baada ya kutua, Adili alipelekwa mbele ya mfalme na manyani wake.
- Adili alijizatiti kwenda
- kumsalimia mfalme
- kuonana na mfalme
- kumwua falme
- kuwatandika farasi
- Farasi watatu waliandikwa matandiko walikuwa ni wa kuwabeba
- Mfalme, Adili na Ikibali
- Adili, Ikibali na mfalme
- Ikibali, Adili na nduguze
- Adili na nyani wawili
- Farasi wa Ikibali na wa Adili walikwenda sambamba. Maana yake ni kuwa walikwenda
- mmoja mblele mwingine nyuma
- karibu karibu
- unyounyo mwendo wa asteaste
- sawasawa ubavu kwa ubavu
- Manyani waliandamana nyuma ya Ikibali na Adili. Ndiko kusema Adili na Ikibali waliandamana na nyani
- sambamba
- unyounyo
- mkabala
- chapuchapu
- Kilichowashangaza watu zaidi katika habari hii ni
- Adili kuongozana na ikibali
- Adili kupanda farasi.
- Nyani kupanda farasi
- Mawe kusema, miti kujibu na wanyama kuwa watu
- kibali aliposema kwa ucheshi, bila shaka
- alinuna
- alighadhabika
- alinong'ona
- alitabasamu
- Mbwa alibweka. Je, wangekuwa fahali wangefanyaje?
- Wengeroroma
- Wangenguruma
- Wangekoroma
- Wangetetea
- Ikibali alipogeuza uso wake kwa Adili, bila shaka
- alimtazama Adili
- alimpa Adili kisogo
- alimkabidhi Adili
- hakumwangalia ana kwa ana
- Walipofika na kuwasili ughaibuni
- mfalme waliwalaki
- nyani walichoka
- Adili na Ikibali waliagana
- Adili alifikishwa maskanini pa mfalme
- Kauli ipi si sahihi kulingana na makara haya?
- Watu walishangazwa na nyani waliopanda farasi
- Watu walishangilia ili nyani wapande farasi
- Mbwa nao waliobweka walipowaona Ikibali na Adili
- Adili na nyani waliitwa na mfalme
Soma barua ifuatayo kisha ujibu maswali 41 hadi 50
Zera Ahmed.
S.L.P 27001,
MOMBASA
27-01-2001
Meneja wa Benki Kuu,
S.L.P 20101
NAIROBI.
KUH: OMBI LA KAZI
Mimi nina umri wa miaka thelathini, nimesomea kazi hii ya kufanya kazi kwenye benki kama mhasibu. Niliupata waraka mliokuwa mmetuma mkitafuta mhasibu. Mimi ni mmoja wa wahasibu wale bora na maarufu zaidi nchini.
Nimeisomea kazi hii katika mojawapo wa vyuo vikuu nchini. Nilikuwa katika chuo kikuu kisha nikajaribu kufanya kazi kwa miaka miwili kwani nilikuwa nikijua kuwa, haba na haba hujaza kibaba.
Mimi ni stadi katika hisabati na lugha nyingine nyingi kama vile Kiswahili, King'eng'e, Kifaransa, Kijerumani pamoja na lugha nyingine nyingi.
Sipendi mapendeleo labda katika kabila, aila au hata rangi ya sura.
Huu ndio mwanya peke yake ninao wa kupata kazi hii ya uhasibu. Tafadhali ninakusihi unipe kazi hii.
Wako mwaminifu,
Zena Ahmed.
- Barua ya aina hii huitwa
- barua ya kindugu
- barua ya kirafiki
- barua rasmi
- barua kuu
- Anwani ya pili katika barua hii ni ya
- mwandishi
- mwandikiwa
- Zena
- mhasibu
- Barua hii iliandikwa mwezi gani?
- Februari
- Machi
- Juni
- Januari
- Nia ya mwandishi huyu kuandika barua hii ni
- Kuwa meneja
- kuenda chuo kikuu
- kuwa tarishi wa benki
- ombi la kazi katika benki
- Mwandishi amesomea kasi ya
- utabibu
- uhasibu
- ualimu
- ukadamu
- Kazi ya uhasibu ni ipi?
- Kazi ya kuhesabu pes
- Amali ya kuchunga pesa
- Riziki ya upelelezi
- Kazi ya ufundi
- Baadhi ya mapendeleo ambayo mwandishi hayapendi na yametajwa ni kama vile
- ukabila
- jinsia
- lugha
- elimu
- Mwandishi wa habari hii amesoma hadi
- shule ya msingi
- chuo kikuu
- shule ya upili
- chekechea
- Zena Ahmed alisomea kazi hii ya uhasibu wapi?
- Chuo kikuu
- Shule ya upili
- Shule ya msingi
- Chuo cha ufundi
- Mwandishi wa habari aliandika barua akiwa wapi?
- Makerere
- Mombasa
- Benki
- Nairobi
INSHA
Andika insha kuhusu: SHEREHE YA SIKU YA KUZALIWA KWANGU
MARKING SCHEME
- A
- C
- A
- C
- B
- C
- D
- A
- B
- B
- D
- C
- B
- A
- C
- C
- C
- D
- B
- D
- A
- D
- C
- B
- A
- D
- B
- A
- C
- D
- B
- D
- D
- B
- C
- D
- A
- A
- D
- B
- C
- B
- D
- D
- B
- A
- A
- B
- A
- B
Kiswahili Activities - Grade 5 End Term 1 Exam 2021 SET 2
COMPETENCY BASED CURICULUM
GREDI YA 5, MWISHO WA MUHULA WA 1
SHUGHULI ZA KISWAHILI
JINA....................................................SHULE............................................
ZOEZI 1: KUSOMA KWA UFAHAMU
Soma kifungu kifuatacho kisha uyjibu swali la 1 hadi la 7
Mipango yote ya sherehe ya kuzaliwa kwa baba yangu ilikuwa imepangwa ikapangika.Ilikuwa siku ya tatu ya juma. Baba alikuwa akikamilisha miaka thelathini na tisa. Yeye hakuwa amekula chumvi nyingi kama alivyokuwa babaye Meishisana.
Mapochopocho ya vyakula mbalimbali yalikuwa yakinukia mezani na hata mekoni. Vyakula kama vile pilau, biriani , maandazi na vibanzi vilivutia sana machoni pa wageni watano waalikwa. Nilishangaa nilipomwona Bwana Kauleni akidondokwa na mate kwa sababu ya kuitamani keki yenyewe. Watu wengine ambao sikuwatambua kwa majina yao, walikuwa wameketi kitako sebuleni huku wamejipamba kweli kweli. Bila shaka wote walijawa na tabasamu nyusoni pao. Keki yenyewe ilikuwa tamu kama halua. Mimi mwenyewe nilihusika kwa kuwakaribisha marafiki zangu kwenye viti baada ya kuvipanga.
Maswali
- Je, kisa hiki kinahusu sherehe ya nani?
________________________________ - Sherehe yenyewe ilikuwa siku gani ya juma?
________________________________ - Mwandishi alitumia maneno, "hakuwa amekula chumvi nyingi." Je, hii inamaanisha nini ?
________________________________________________________________ - Wageni walikuwa wameketi kitako. Pigia mstari kielezi katika sentensi hii.
________________________________ - Je, sherehe hii ilihudhuriwa na wageni wangapi waalikwa?
________________________________ - Taja jina la babuye mwandishi.
________________________________ - Kifungu ulichokisoma kinahusu nini?
________________________________
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 8 hadi la 14.
Mwaka huu ulipoanza, sote tulifurahi kurudi katika shule yetu. Shule hiyo inajulikana kama Mematele. Ina wanafunzi elfu moja na mia mbili na mabasi sita. Mabasi yote ya shule hiyo yamepakwa rangi ya manjano.
Tulipowasili shuleni, tuliingia madarasani na kuketi kwenye viti vyetu. Mwalimu mmoja ambaye tulimpenda sana alingia darasani na kutuamkua, " Hamjambo wanafunzi " Nasi tukajibu, "Hatujambo
mwalimu Matunda. Shikamoo"
Kengele ilipopigwa tulielekea gwarideni Tulisimama wima tulipokuwa tukiimba wimbo wa taifa. Baadaye mwalimu alitukagua endapo kucha zetu zilikuwa safi. Mwalimu wetu alitushauri tuwe tukinywa maji mengi kila siku ili tuwe na afya njema.
MASWALI - Malizia sentensi hii
Mwaka huu ulipoanza sote tulifurahi
________________________________ - Mwandishi husomea katika skuli gani?
________________________________ - Shule ya mwandishi ina wanafunzi wangapi?
________________________________ - Mabasi ya shule katika nchi hii ya msimulizi yamepakwa rangl gani?
________________________________________________________________ - Salamu hamjambo hujibiwa hatujambo je, masalheri hujibiwa aje?
________________________________ - Ni nani aliwashauri wanagenzi kunywa maji mengi?
________________________________ - Kwa nini wanafunzi walishauriwa kunywa maji mengi?
________________________________
ZOEZI II:SARUFI
- Teua salamu ambayo haijaambatanishwa ipasavyo.
Habari ya jioni.... njema
Kwa heri..... ya kuonana
Alamsiki.... aleikum salaam
Makiwa .... unayo - Je, kati ya maneno haya katika kamusi, ni neno gani litakuwa la pili?
Muhubiri, Muhutasari, Muhula, Mtihani, Mshtakiwa ________________________________ - Mstatili huu una maneno matano ya nomino za vitenzi-jina. Je, ni neno lipi halifai kuwa hapa?
[Kulala, Kukimbia, Kalia, Kusoma, kutibiwa]
________________________________
Andika kwa wingi. - Mtoto aliacha dawati lake shuleni.
________________________________ - Mwalimu wangu huja mapema shuleni
________________________________
Chagua neno lifaalo kujaza nafasi. - Matata ___________nyanya samaki. (alibeba, alimbebea, alimbeba)
- Tulienda sokoni ___________tununue matunda. (ili, kwa sababu).
- Kamilisha methali hii. Asiyekujua ___________{akuthanini, hakuthamini, hakudhamini}
- Ni sentensi gani haijakanushwa vyema?
Tunaenda sokoni Hatuendi sokoni Mama yangu amechelewa Mama yangu hachelewi Walionana mwaka jana Hawakuonana mwaka jana. Juma ni mwanafunzi hodari Juma si mwanafunzi hodari - Nomino,"jua, lepe, jasho, joto na giza," hupatikana katika ngeli ya ___________
- Andika sentensi hii katika hali ya ukubwa
Mtoto wake anasoma _________________________________ - Je, sentensi hii iko katika wakati gani?______________________
Mlinzi mwenyewe analilinda rinda la mama. - ______________________(Karamu ,Ghulamu, Kalamu) ya arusi ilikuwa ya kupendeza sana.
- Siku hiyo ___________(pipi,vivi, bibi) arusi alivaa gauni jeupe pe pe pe.
Jaza mianya iliyoachwa kwa maneno yafaayo kutoka kwenye mabano (Shule, mwiko, vitunguuu,, sabuni) - Mama alipokuwa akisonga ugali alitumia______________________
- Idadi ya wanafunzi katika ___________yetu ni elfu mbili.
INSHA
Andika insha kuhusu: MWALIMU NIMPENDAYE
MAAKIZO
- Sherehe ya kuzaliwa ya baba( ya mwandishi)
- siku ya tatu
- Hakuwa mzee sana
- kitako
- watano
- Meishisana
- sherehe ya siku ya kuzaliwa
- kurudi katika shule yetu
- Mematele
- elfu moja mia mbili
- manjano
- aheri
- mwalimu
- wawe na afya njema
- alamsiki
- mtihani
- kalia
- watoto waliacha madawati yao shuleni
- walimu wetu huja mapema shuleni
- alimbebea
- ili
- hakudhamini
- mama yangu amechelewa
- LI-YA
- jitoto lake linasoma
- wakati uliopo
- karamu
- bibi
- mwiko
- shule
Kiswahili - Class 8 End Term 1 Exam 2021 Set 1
Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 hadi 15, Kwa kila nafasi umepewa majibu manne, Chagua jibu lifaalo kati ya ale uliyopewa.
Wahenga ______1_______ waliposema kuwa ______2______. Watahiniwa wengi huandika insha ______3______ mithili ya vipofu pasi na kutambua _______4______uandishi wa insha. Kama yalivyo maswali mengine katika mitihani ______5______ uandishi wa insha vilevile ni ______6______ kujibiwa kwa kuzingatia ______7______ yanayotolewa kabla ya swali lenyewe. Jambo la ajabu ni kwamba, wengi wa wanafunzi huanza tu kuandika ______8______ ya kuisoma sehemu hii muhimu. Amri ya mtahini ni muhimu sana na ni sharti ifuatwe kikamilifu.
-
- hawakukosea
- walikosea
- hawakutuandaa
- walituandaa
-
- asiyekujua hakuthamini
- kuyumbayumba sio kuanguka
- mla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe
- jambo usilolijua ni usiku wa kiza
-
- kitamaduni
- kilevi
- kipopo
- kijuzi
-
- sintofahamu inayoikumba
- suitafahamu inayoukumba
- suitafahamu inayoikumba
- sintofahamu inayoukumba
-
- ;
- ,
- :
- ?
-
- maswali ambalo yanafaa
- swali ambalo halifai
- maswali ambayo hayafai
- swali ambalo linafaa
-
- mashauri
- maonyo
- maagizo
- ushauri
-
- minghairi ya
- sembuse
- maadamu
- mintarafu
Fisi alikuwa amezoea _______9________ kwa muda mrefu sana. Maisha yake ya kuiparamia _______10______ na wanyama wengine yalikuwa yamemshinda. Hii ni ______11______ wanyama kama simba na chui waliyateketeza mabaki ya mawindo yao. Aliamua kuanza kufanya ______12______. Alitengeneza silaha kama mishale ili kuwawinda wanyama wengine,jambo ambalo lilikuwa limepingwa vikali na mfalme wao. Tendo hilo lilikuwa ______13______. Juhudi zake ______14______ kwani mishale yake ilikuwa ______15______ na haingemudu kumfuma mnyama yeyote.
-
- kuvuna mahali ambapo hakupanda
- kupanda mahali ambapo alivuna
- kupanda kabla ya kwenda kuvuna
- kuvuna mahali ambapo alipanda
-
- vyakula vilivyoliwa
- mizoga iliyosazwa
- wanyama waliouwawa
- nyama zilizoliwa
-
- kwasababu
- kwa kuwa
- kwa sababu
- kwa minajili
-
- jambazi
- ujambazi
- ujangili
- jangili
-
- halali
- lilikataliwa
- likiharamia
- haramu
-
- hazikufua dafu
- zilizaa matunda
- hazikuambulia patupu
- zilifua dafu
-
- si butu
- butu
- kali
- bora
Kutoka swali la 16 mpaka 30, chagua jibu sahihi.
- Chagua sentensi isiyoakifishwa vizuri
- Mwanafunzi bora-aliyeongoza katika mtihani-alituzwa.
- Mtu anayeipenda nchi yake (kwa dhati) huitetea zaidi.
- Sokoni mlikuwa na matunda mengi: mapera, maparachichi na karakara.
- Usilijibu swali lolote," mtahini alielekeza.
- Tambua sentensi yenye vivumishi vya pekee
- Mwanariadha hodari alizawadiwa.
- Wageni wenyewe waliula mkate wote.
- Mtu mzuri ni anayevifanya vitendo vizuri kwa kuradidi.
- Shuleni palikuwa na bawabu mwenye maarifa tele.
- Ni kitenzi gani kilichoradidiwa katika sentensi zifuatazo?
- Anayetembea upesiupesi hufika kwa haraka
- Ukiwasemasema watu utakuwa mfitini.
- Machungwa yale yale ndiyo yaliyoliwa.
- Tulitembea asteaste kuelekea madhabahuni.
- Bainisha usemi wa taarifa wa:
"Wanafunzi wawa hawa ndio waliotia fora mtihanini, "mwalimu mkuu alisema.- Wanafunzi wale wale ndio waliotia fora mihanini mwalimu mkuu alisema.
- Mwalimu mkuu alisema kuwa wanafunzi wale wale ndio waliotia fora mtihanini
- "Mwalimu mkuu alisema" wanafunzi wawa hawa ndio waliotia fora mtihanini.
- Mwalimu mkuu atasema kuwa wanafunzi wale wale ndio watakaotia fora mtihanini. B.C. mgawa
- Neno mwanasesere ina silabi ngapi?
- 9
- 5
- 7
- 4
- Neni karibu limetumikaje katika sentensi ifuatayo?
Wastaafu wote walilipwa zaidi ya karibu milioni moja.- Kuonyesha nusura
- Kuonyesha maagano
- Kuonyesha umbali
- Kuonyesha makisio
- Tumia kiunganishi kifaacho.
Ni kwa nini umenmpa funguo za nyumba yako ________________ unajua kuwa yeye ni mwizi?- maadamu
- ilhali
- ingawa
- isitoshe
- Andika sentensi ifuatayo bila kirejeshi -amba
Mfanyakazi ambaye atafanya bidii atapandishwa madaraka.- Mfanyakazi afanyaye bidii atapandishwa madaraka
- Atakayefanya kazi kwa bidii atapandishwa madaraka.
- Mfanyakazi ambaye atakayefanya kazi kwa bidii atapandishwa madaraka.
- Mfanyakazi anayefanya kazi kwa bidii atapandishwa madaraka.
- Ni upi wingi wa sentensi hii?
Ubavu wa mnyama wangu umevunjwa na jirani mwenye wivu.- Ubavu wa wanyama wangu umevunjwa na majirani wenye wivu.
- Mbavu za wanyama wetu zimevunjwa na majirani wenye wivu.
- Ubavu za wanyama zangu zimevunjwa na jirani wenye wivu.
- Mabavu ya wanyama wetu yamevunjwa na jirani wenye wivu.
- Kama juzi ilikuwa Jumatano tarehe kumi na nane, mtondo itakuwa siku gani tarehe ngapi?
- Jumatatu tarehe ishirini na tatu
- Alhamisi tarehe ishirini na tisa
- Jumapili tarehe ishirini na mbili
- Ijumaa tarehe ishirini.
- Ni sentensi ipi yenye maana sawa na
Sio nadra wao hutembeleana.- Wao hutembeleana mara chache
- Wao hutembeleana mara nyingi
- Si mara kwa mara wao hutembeleana
- Kutembeleana kwao ni adimu
- Ni methali gani yenye maana sawa na:
Ngoja ngoja huumiza mtu matumbo?- Asiyesikia la mkuu huvunjika glu bidii atapandishwa madaraka.
- Pole pole ndio mwendo D.
- Chelewa chelewa utakuta mwana si wako
- Haraka haraka haina baraka
- Chagua sentensi iliyotumia sitiari.
- Maua ni sungura siku hizi.
- Moyo wake ulimshauri asikate tamaa.
- Alice alijifungua salama salimini.
- Ondigo ni mweusi mithili ya masizi.
- Andika sentensi ifuatayo katika kauli ya majirani wenye wivu kutendewa
Kaguai alienda uwanjani akaucheza mpira.- Mpira ulichezwa na Kaguai uwanjani.
- Kaguai aliuchezea mpira uwanjani.
- Mpira ulichezwa na Kaguai
- Uwanjani ulichezwa mpira na Kaguai.
- Makao ya mchwa si
- kingulima
- kinyago
- lishirazi
- kichuguu
Soma taarifa ifuatayo kisha uiibu maswali 31- 40
Akiba ni nini? Kwa kifupi, akiba ni kitu kilichotengwa kwa ajili ya manufaa ya baadaye. Watu wanaoamini akiba huwa wanafahamu kuwa maisha yana nyuso mara mbili: wakati wa mavuno mema na wakati wa mavuno hafifu. Wanazaraa hawa wanafahamu fika kuwa kuna uwezekano wa kupata mavuno kama hayo mbeleni. Taifa linalowajali wazalendo wake huhakikisha kuwa maghala yamejaa vyakula nomi. Akiba maarufu zaidi ni ya kuhifadhi pesa benkini.
Watu wengi duniani wamebakia kuwa walalahoi kwa kutojua wala kutambua namna ya kuweka akiba. Utawasikia wengi wakisema kuwa hakiba huwekwa na waja wenye vipato vikubwa. Kabla ya kufikiria hivyo ni vyema ujue kuwa waliokuwa au walionavyo, mwanzoni hawakuwa navyo. Mtu anaweza kuweka akiba hata kama kipato chake ni cha chini kabisa. Kumbuka kuwa hakiba haiozi na kidogo kidogo hujazaa kibaba.
Wengine hulalamika eti hawawezi kuweka akiba kwani mapato yao huishia tu wanapokidhi matakwa
yao ya lazima. Hawajui kwamba iwapo wanataka kuwa na uchumi thabiti katika siku za usoni ni sharti kujinyima. Kukosa kuweka akiba eti kwa kusingizia mshahara mdogo ni kujipumbaza tu. Kuna baadhi ya watu vilevile wanaodhani kuwa wao ni wachanga zaidi kuanza kuweka hifadhi. Kuna wanaofanya mipango mizuri zaidi ya kuzitumia pesa zao lakini tamaa na uchu huwafanya tena kupotoka kabisa. Kupanga kufanya jambo na kisha ukakosa kulitekeleza ni kupoteza muda. Utawaona watu wanalipwa mshahara, wanatumia kila kitu na kuendelea kufanya kazi kungojea mshahara mwingine. Huku ni kuzungukia sehemu moja kama tiara bila kupiga hatua.
Ni jambo la busara sana kuanza kuweka akiba kutoka utotoni. Akiba hizi zinaweza kufanywa kwa njia ayami. Mwanzo mtu anaweza kuwa na mkebe mdogo uliotengenezwa kwa njia ya kipekee. Mkebe huo huwa na kishimo kidogo kinachomwezesha mtu kuweka pesa bila kutoa. Njia nyingine ni kuwa wazazi au walezi wao kuwawekea. Wazazi na walezi wanaweza kuwafungulia watoto wao akaunti kwenye benki. Kuweka pesa benkini ni bora zaidi kuliko akiba nyingine zozote. Hii ni kwa sababu ya ulinzi wa pesa pale benkini. Isitoshe, pesa zinazowekwa kwenye benki huzaa riba. Vilevile pesa hizo zinaweza kuwekezwa kwa njia ambazo faida zitaonekana na mtoto mwenyewe. Mtoto anaweza kununuliwa mifugo kama vile; kuku, sungura, mabata ambao watazaana na kumletea mtoto faida zaidi.
Mtoto anapoona kuwa pesa zake zinaweza kuendelea kuzaa huwa na motisha wa kuendelea kuweka
akiba. Mwana akilelewa kwa tamaduni hizi za kuwekeza, kamwe hataacha hata akiwa mtu mzima. Atakuwa na mshawasha wa kuendelea kuzalisha milele. Kuweka akiba kutoka utotoni humfanya mtoto kuwa na pesa za kutosha hata kuyaendeleza masomo yake bila kutegemea wafadhili. Huku ndiko kujitegemea. Mtu anayejitegemea huishi maisha ya amani na raha mstarehe.
Je, wewe tayari una akiba au utaanza kuweka leo? Kumbuka kuwa kuweka akiba ni ishara kubwa zaidi ya kuwa na nidhamu.
- Kwa mujibu wa aya ya kwanza,
- akiba muhimu zaidi ni za vyakula vya wakulima
- akiba huwekwa baada ya kupata mapato mengi
- mtu anafaa kuweka akiba hata kama mapato yake ni finyu
- maisha kamwe hayana nyuso mbili
- Ni kwa nini watu wengi wameishia kuwa maskini kulingana na taarifa uliyoisoma?
- Mapato yao ni machache
- Wanafahamu fika maana ya kuweka akiba
- Wanachelea kuweka akiba wakidhani hawana vya kutosha
- Walalahai wameyachukua mapato makubwa wakawamalizia
- Chagua methali iliyo kinyume na methali iliyotumiwa katika sentensi ya mwisho wa aya ya pili
- Chururu si ndo! ndo! ndo!
- Papo kwa papo kamba hukata jiwe
- Haba na haba hujaza kibaba
- Mchumia juani hulia kivulini
- Serikali inawezaje kuwahakikishia watu wake uthabiti wa kiuchumi kulingana na ufahamu?
- Kuwashauri watu wake kuweka akiba
- Kuwalazimisha wananchi wake kuweka akiba
- Kuwapa wananchi wake mapato makubwa ili waweke akiba
- Kuwawekea wananchi wake vyakula vya kutosha kwenye maghala
- Watu wengi hawapendi kuweka akiba kwa sababu zote hizi ila
- wanadhani kuwa mapato yao hayatoshi
- wanaona kuwa umri wao ni mdogo mno
- wanafanya mipango mizuri lakini hawaitekelezi
- mapato yao yanawaruhusu kuweka akiba ndogo mno
- Huku ni kuzungukia sehemu moja kama tiara... Ni tamathali gani ya lugha iliyotumiwa hapa?
- Tashbihi
- Methali
- Istiara
- Semi
- Ni ijambo lipi linalowazuia watu wenye mipango mizuri kuweka akiba?
- Mipango yao huwa na kasoro fulani.
- Wanayapangia mapato bila kufahau kuwa hayatoshi
- Mshahara wao mdogo kukosa kuwaruhusu kuitekeleza mipango yao
- Hulka zao za kuvitamani sana vitu vingine
- Kati ya mbinu zifuatazo, ni mbinu gani si bora
- Kuweka pesa kwenye mkebe maalum
- Kuwapa wazazi wao pesa wawawekee
- Kuzitumia pesa ili kukirimia matakwa yao
- Kuweka pesa kwenye akaunti za benki
- Ni kwa nini mtu anafaa kuanza kuweka akiba akiwa na umri mdogo?
- Atakuwa tajiri kwa haraka mno
- Atakuwa na utamaduni huo maishani
- Pesa zake zitakuwa maradufu
- Mtu hahitaji kujipanga akiwa ameweka akiba
- Mtu anayepoteza kazi yake ilhali ameweka akiba;
- atakuwa mtegemeaji wa wengine
- anaweza kuanzisha biashara
- ataanza kuweka akiba kidogo kidogo
- ataweza kwenda ziarani kujivinjari na familia
Soma ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali 41-50
Nyanya Matinda alikuwa ametualika twende kumsalimia. Mwanzo aliwauliza wazazi wetu iwapo sote tungepatikana wakati wa sikukuu ya Krismasi. Wengi waliitikia ualishi huo isipokuwa shangazi ambaye aljitetea kuwa binamu yetu Juma angekuwa na shughuli muhimu chuoni. Baada ya majadiliano ya kina na watu wote wa ukoo, uamuzi ulitolewa kuwa twende kumtembelea wakati wa kiburunzi.
Mimi sikuwa nimemwona bibi huyu kwa zaidi ya nusu mwongo. Nilikuwa na mchanganyiko wa furaha na maswali. Furaha kwa kuwa ningepata nafasi ya kuzuru watu wa nyumbani na maswali ya kujua tuliloitiwa. "Je, nyanya anataka kuishia ahera ama vipi? Niliwaza na kuwazua. Nilitaka kuingojea siku hiyo ili nijue dhahiri shahiri. Bibi alikuwa ametayarisha kuchinja ndume wake kuwa kitoweo chetu.
Kufikia saa tisa alasiri tarehe thelathini na moja Desemba, kila mmoja alikuwa amewasili. Mimi ndimi niliyefika karibu wa mwisho. Nilipofika kwa nyanya nilishangazwa na wingi wa watu. Ukweli ni kwamba, singewajua wala kuwatambua wote. Wengi walikuwa ajinabi machoni pangu. Kulikuwa na harufu nzuri ya vyakula hewani. Nilianza kudondokwa na mate bila kujua. Punde si punde, tuliombwa na ami mkuu tuingie ndani sote. Nyumba ya nyanya ilikuwa na bahari ya sebule. Tulimezwa sote na hakukuwa aliyetapikwa hata mmoja. Ilikuwani nyumba ya kisasa iliyojengwa kwa teknolojia mpya.
Pale sebuleni. kila mmoja alionekana akishughulika na simu za mkononi. Wengine walikuwa kwenye mtandao, wengine wakicheza michezo, wengine wakiandika jumbe na wengine wakipiga picha almaarufu 'selfie". Mara nyanya Matinda alinyerereka asteaste na kuingia ndani. Cha ajabu ni kwamba, hakuna aliyemwona isipokuwa mimi. Wote walikuwa na shughuli. Nyanya alionekana kukasirika. Alitoka shoti na kuingia katika chumba chake cha kulala. Aliporudi alikuwa amebeba gunia. Alikohoa. Kila mmoja aliinua kichwa na kumwangalia. "Hata hamna muda wa kuzungumza mjuane? Simu..simu.simu tu! Kila mmoja aiweke simu yake kwenye gunia hili." Nyanya alifoka kwa ukali. Tulitii amri ingawa kwa shingo upande.
Sote hatukufurahia lakini tukajibu, "Pole nyanya Matinda kwa kukuudhi'"kwa kauli moja. "Ni kwa nini mmechangamkia elimu ya ulimwengu na huku elimu ya ukoo mmeipoteza? Ni kwa nini hamuwezi kuzungumza mkajuane? Hamjui kwamba dunia imeharibika siku hizi? Hamjawaona ndugu wa damu wakioana kwa kutojua? Ni kwa nini dunia hii inawapotosha wajukuu wangu? Ama nyote mnajuana?" Hapana nyanya," tulijibu kwa pamoja. "Haya hebu sasa mwangalie mwenzako," alitoa kauli nyingine.
"Ah! Wajukuu wangu, mmedanganyika na kupotoka kabisa. Hebu tazameni humu mwangu, ni kitu
gani cha kisasa ambacho hakiko? Angalieni runinga yangu na simu yangu. Hivi vyote si vya kisasa? Sasa
hebu mniambie iwapo vimenikatiza kujua watu wa ukoo wangu?" Nyanya alisimulia kwa masikitiko.
"Vyombo hivi vyote vya teknolojia ni vyema. Nyinyi ndinyi mnavitumia isivyofaa. Mimi nilipozaliwa
nilipata kuwa kulikuwa na magazeti na televisheni. Baba yangu alikuwa na kijiredio cha mbao ambacho
hakuna hata mmoja aliyeruhusiwa kukigusa." Tuliangua kicheko. "Acheni kucheka. Hata tulikuwa na
televisheni ya "Sanyo' ambayo ilionyesha rangi nyeusi na nyeupe."tulicheka tena. "Isitoshe, kijiji kizima
kilifika kwetu wakati wa Magharibi kutazama taarifa ya habari!"
Wakati huo wote tulishindwa kuzuia vicheko. Nyanya pia aliongezea kuwa baba yake alikuwa na saa kubwa sana. Saa hiyo iliyotajwa kuwa ya "Majira' iikuwa kubwa zaidi kiasi kwamba iliwekwa sakafuni.
Alidokeza kuwa saa hiyo haikutumia betri. Kila mara ungesikia ikitoa sauti kwaa krabu zake, ch! ch! ch!
Saa ishirini na nne.
Wajukuu wangu, nimemaliza mizungu. Sasa karibuni tule na tufurahie kuwa watu wa ukoo mmoja." Sinia za minofu zilianza kuletwa mezani.
- Familia ya nyanya Matinda ilimtembelea lini kulingana na aya ya kwanza?
- Wakati wa Krismasi
- Mkesha wa mwaka mpya
- Mkesha wa Krismasi
- Siku yake ya kuzaliwa
- Ni nani aliyetoa sababu ya mwanawe kutopata nafasi tarehe kamili za awali za ualishi?
- Binamu yake shangazi
- Mtoto wa kiume wa shangazi
- Ndugu wa kiume wa mama
- Ndugu wa kike wa baba
- Msimulizi hakuwa amemtembelea nyanya yake kwa muda wa
- zaidi ya miaka mitano
- takribani miaka kumi na miwili
- zaidi ya miaka kumi
- zaidi ya nusu ya mwaka
- Unafikiri ni kwa nini mwandishi wa makala haya alifurahia baada ya kupata ualishi?
- Alikuwa anajiuliza sababu kuu ya nyanya kuwaita
- Alidhani kuwa siku za nyanya zilikuwa zimeyoyoma
- Binamu yake alikuwa na shughuli na kwa hivyo hawangeenda
- Angepata nafasi ya kutembea nyumbani na kuwaona watu wao
- Kifungu, bahari ya sebule, kimepigiwa mstari. Kinamaanisha kuwa
- nyumba ya nyanya ilikuwa na bahari ndani
- sebuleni palikuwa na kidimbwi kikubwa
- sebule ilikuwa kubwa zaidi
- bahari iliyokuwapo ilitumeza sote tukapotea
- Kulingana na aya ya nne
- nyanya Matinda anaonyeshwa kutoipenda mitambo yoyote ya teknolojia
- nyanya Matinda anashangaa ni kwa nini wajukuu wamekuwa watumwa wa simu badala ya kujuana
- nyanya Matinda anadhani kuwa simutamba huhifadhiwa kwenye gunia
- wajukuu wale waliziweka simu zao kwenye gunia kwa hiari
- Ni jambo gani linaloonyesha kuwa wajukuu wale walikuwa na heshima?
- Hawakuwa wanazungumziana kwa hivyo waliheshimiana
- Walimwambia nyanya Matinda pole baada ya kumkasirisha
- Walikubali kuziweka simu zao kwenye magunia kwa furaha
- Wajukuu wote walikuwa wamemiliki simu ya mkononi.
- Kifungu ulichokisoma kimebainisha kwamba elimu ya ukoo
- hutuwezesha kufahamu jamaa na koo zetu
- hutuwezesha kufahamu ulimwengu wa tovuti
- huturahisishia kujua elimu ya dunia
- haijapuuzwa na vijana hata kidogo
- Kauli zifuatazo zinazotolewa na nyanya zinaonyesha ucheshi isipokuwa masimulizi kuhusu
- kuwepo kwa magazeti yaliyosomwa na wakongwe
- saa kubwa ajabu ambayo haikutumia betri
- runinga iliyotazamwa na karibu kijiji kizima
- kuwepo kwa kijiredio cha mbao ambacho hakikuguzwa na yeyote
- Ni kauli gani iliyo sawa kulingana na makala uliyoyasoma?
- Elimu ya ukoo hufunzwa pamoja na elimu za dunia
- Hapakuwa na vyombo vya teknolojia hapo zamani
- Vyombo vya kiteknolojia ni vyema lakini vinatumiwa visivyo
- Vyombo vya teknolojia vililetwa ili kupoteza ukoo wa watu
MARKING SCHEME
- A
- D
- C
- B
- B
- D
- C
- A
- A
- B
- C
- C
- D
- A
- B
- B
- B
- C
- B
- B
- D
- B
- A
- B
- A
- B
- C
- A
- B
- B
- B
- C
- A
- A
- D
- A
- D
- C
- B
- A
- B
- D
- A
- D
- C
- B
- B
- A
- A
- C
Kiswahili - Class 7 End Term 1 Exam 2021 SET 1
DARASA LA 7, MWISHO WA MUHULA WA 1, 2021
KISWAHILI
JINA....................................................SHULE..........................................
Tumia msamiati ulio mwafaka zaidi ujaze kwenye vihasho 1 hadi 15.
Ni kweli kwamba jinsi tunavyoendelea kukua ndivyo 1 kujifunza mambo mengi aushini. 2 ya hayo ni kazi. Kazi ndiyo 3 wa maisha ya binadamu. Kazi ni kazi, iwe ya 4 au rahisi; usichague. Kwani kazi 5 hutusaidia6 riziki yetu. Tujizoeshe, tupende na 7 kazi mapema. Wajibu 8 nyumbani ni kuwasaidia wazazi katika kazi zote. Ubwete haufai 9 hauwezi kutulisha. Tuchape kazi kwanza 10 tupumzike.
- A. tunazidi B. tunapozidi C. tunavyozidi D. tunakozidi
- A Mmojawapo B. Mojawapo C. Kimojawapo D. Umojawapo
- A. uti wa mgongo B. uti wa mkono C. uti wa kichwa D. uti wa mguu
- A. suluhu B. sulu C. zulu D. sulubu
- A. ndicho B. ndiyo C. ndilo D. ndio
- A. kusumbua B. kuzubua C. kuzumbua D. kusafirisha
- A. kuendeleza B. kuendelesha C. kuendelea D.kuendeleshwa
- A yetu B. zetu. C. letu D. wetu
- A. na B. wala C. ingawa D. lakini
- A. Ndiyo B. ndio C.ndipo D. ndiko
Je 11 wajua kuwa ni haki ya kila mtoto kupata elimu? Ni kwa kutambua jambo hili 12 serikali ya Kenya ilitangaza kuwa itatoa elimu bila malipo kwa watoto wote ili kila 13 apate nafasi ya kujipatia elimu ya msingi. Hali kadhalika watoto wa 14 wa kwenda shule hawapaswi kuajiriwa mahali 15 .
- A., B.? C. ! D..
- A. ambako B. ambao C. ambaye D. ambapo
- A. moja B. mmoja C. mamoja D. mojawapo
- A. rika B. wakati C. umri D. muda
- A. pote B. kokote C. popote D. kote
Kutoka swali la 16 mpaka 30. jibu kulingana na maagizo.
- Sentensi;
Nilipigiwa mpira ina maana zifuatazo isipokuwa________- mpira ulipigwa ukielekezwa kwangu
- nilisaidiwa kupiga mpira
- nilipigwa kwa sababu ya mpira
- mpira ulitumiwa kunipiga
- Umbo hili ni
- mstatili
- mche
- duara dufu
- pia
- Neno "maji” liko katika ngeli gani?
- I-I
- YA-YA
- I-ZI
- LI-YA
- Kamilisha methali:
Mchumia juani- hulia kivulini
- hali wali mkavu
- huumiza mkonowe
- marejeo ni ngamani
- Chagua umoja wa sentensi hii:
Watajiwakilisha wao wenyewe- Nitajiwakilisha sisi wenyewe
- Atajwakilisha wewe mwenyewe
- Nitajiwakilisha mimi mwenyewe
- Atajiwakilisha yeye mwenyewe
- Petro alitia masomoni na akuibuka mwanafunzi_____zaidi.
- chumvi, mzuri
- bidii, upya
- fora, bora
- kauri, kauli
- Msichana alitumia__kulia vibanzi.
- umma
- uma
- kijiko
- mwiko
- Ni sentensi ipi iliyoakifishwa vizuri?
- Nilinunua sukari, chumvi, mayai, biskuti
- Baba wa Wambui ni karimu
- Lo! Ameshindwa kufunga bao!
- Mji wa Mombasa unapendeza
- Ni vazi gani lisilovaliwa na wanaume?
- Chupi
- Kizibao
- Fulana
- Kanchiri
- Andika kwa wingi
Mama yake alipoteza ufunguo.- Mama zao walipoteza funguo
- Wamama wao walipoteza fungu
- Kina mama zao walipoteza funguo
- Mama zetu walipoteza funguo
- Chagua kiunganishi katika sentensi hii.
Nilifika sokoni ijapokuwa nilichelewa.- sokoni
- nilifika
- ijapokuwa
- nilichelewa
- Tambua kimilikishi katika sentensi ifuatayo:
Tulimkuta mlevi akiwa amelala nyumbani kwake.- mlevi
- kwake
- nyumbani
- amelala
- Mnyama wa porini anayefanana na ng'ombe ni
- swara
- twiga
- pundamilia
- mbogo
- Kalamu yangu ______jana.
- iliibiwa
- iliiba
- iliibwa
- uliibwa
- Kifaa cha ufundi kinachotumiwa kukerezea mbao ni
- msumeno
- patasi
- nyundo
- timazi
Soma kisa kifuatacho kisha ujibu swali 31 hadi 40.
Siku ya kurudi shuleni iliwadia wazazi wa Pendo waliandamana naye kurudi shuleni. Ulikuwa mwisho wa mwezi na magari ya abiria yalijaa pomoni. Hata hivyo, walifika shuleni salama salimini. Pendo alikuwa amejawa na soni usoni. Hakutaka kumwona yeyote pale shule hasa wanafunzi. Hata hivyo alijikaza kwani alimaizi kuwa lisilobudi hutendwa.
Walimu walimweleza mzazi wa Pendo vile mwanao alivyopotoka zaidi ya kuwa na vipawa adimu. Waliwaeleza pia kuhusu Maria. "Huyu mtoto wa kitajiri ndiye anayempotosha Pendo. Ni lazima aachane naye kabisa ili afaulu katika maisha ya baada "Mwalimu mkuu alisema.
Babake Pendo aliposikia jina Maria likitajwa alianza kutafakari. "Mbona jina hili si geni kwangu?" Alijisaili moyoni. Jina lilo lilifanana na mtoto wa mwajiri wake hata ingawa majina hufanana. Hakuona uwezekano wa mtoto wa mwajiri wake kuwa ndiye aliyemharibu mwanawe. Vilevile, hakuona kama kuna uwezekano kuwa mtoto wa tajiri ungesomea hapo.
Musa, babake Pendo, hakujua alikosomea mtoto wa mwajiri wake. Hata hivyo, fikra na jina hilo zilimtatiza kwa muda baba mtu. Baada ya anuda m pi kupita, Musa alimuuliza mwalimu jinsi ya
LON kumsaidia Pendo. Mwalimu mkuu alieleza kwan ha jandbo Jílo lingesuluhishwa vizuri kwa kuwahusisha wazazi wa Maria
Mwalimu alielezea kwamba wazazi wa Maria walikuwa mabwanyenye katika mitaa ya kifahari. Dhahiri shahiri kuwa haingekosa kuwa yule alikuwa mwajiri wake. Hakutaka mwalimu ajue hivyo licha ya kuwa hisia zake zilidhihisha mengi.
Mwishowe waliagana kwamba Pendo alipaswa kusauriwa na mwalimu na angeripoti katika ofisi ya mwalimu kila alasiri. Pia alipaswa kuadhibiwa kwa kosa lake la kutoroka na ashauriwe barabara na mwalimu kabla ya kwenda kulala.
- Magari yalijaa pomoni kwa nini?
- Ilikuwa siku ya kurudi shuleni
- Ilikuwa asubuhi
- Ni kawaida ya magari kujaa
- Ulikuwa mwisho wa mwezi
- Pendo alirudi shuleni
- kwa hiari yake
- siku ya kufungua shule
- kwa furaha mpwitompwito
- shingo upande
- Pendo alikuwa nyumbani kwa sababu
- ulikuwa mwisho wa mwezi
- ulikuwa wakati alikizo
- alitumwa nyumbani kwa utovnidhamu
- alitaka kuja shuleni ma mzazi wake
- Maisha ya baadaye ni maisha gani?
- Maisha ya kisogoni
- Maisha ya masomo
- Maisha yajayo
- Maisha ya furaha
- Pendo alisomea shule ya aina gani?
- Ya malazi
- Ya wavulana na wasichana
- Ya wasichana pekee
- Yakutwa
- Kwa nini Musa hakutaka wazazi wote wahusike kutafuta suluhisho?
- Wazazi wa Maria hakujulikana
- Walikuwa ndio waajiri wake
- Wangetumia wakati mwingi
- Wazazi wa Maria walikuwa bwanyenye
- Neno bwanyenye lina maana gani?
- maskini hohehahe
- mti anayeajiri wengine
- mtu mkubwa serikalini
- Mtu mwenye mali mengi
- Pendo alikuwa amefanya kosa gani?
- Hatujaambiwa
- Kupigana
- Kutoroka shuleni
- Kupendana ma Maria
- Ni jambo gani Pendo alipaswa kutenda?
- Kusauriwa kila siku
- Kuadhibiwa
- Kutumwa nyumbani
- Kuachana ma marariki wote
- Hisia za Bwana Musa zilidhihirisha nini?
- Kwamba mtoto alikuwa na shida
- Kwamba alimjua mzazi wa Maria
- Kwamba Pendo alikuwa hajafanya kosa
- Kwamba mtoto angeadhibiwa
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41 bad 50.
Ni wazi kama jua la mtikati kuwa demokrasia katika nchi yetu ya Kenya imekua kwa kiwango kikubwa. Bila shaka hili ni suala la kujivunia kwani inamaanisha kuwa tunaenda na wakati Demokrasia ni mfumo wa kuendesha serikali iliyochaguliwa na watu kwa manufaa ya watu wenyewe. Tangu tulipojinyakulia uhuru yapata miongo mitano iliyopita, nchi yetu imepiga hatua kubwa katika ulingo wa kisiasa.
Rais wa kwanza wa taifa letu tukufu hayati Mzee Jomo Kenyatta aliposhika hatamu za uongozi, alihakikisha kuwa amewaunganish vananchi wote wa taifa hili na kuwapa sababu tosha ya kuionea fahari nchi yao. Aliasisi falsafa ya Harambee ambao ulikuwa mwito wa kuwahamasisha wananchi kushirikiana na kuchangia maendeleo yao kwa kuvuta pamoja. Mwito huo ulileta ari na mshawasha kwa wananchi wa Kenya na kuwahimiza wafanye kazi kwa bidii ili kuinua uchumi wa nchi yao.
Aliposafiri kwa njia ya marahaba ninalo mwaka wa elfu moja mia tisa sabini na nane, hayati rais Daniel Toroitich Arap Moi alishikilia uplíuo huo na kuanzisha mwito wa Nyayo ambao ilimaanisha ya kuwa angefuata nyayo za mladgulizi wake na kuhimiza Wakenya kuishi kwa amani, upendo na umoja.
Hayati Rais Moi alikaa kwenye kiti cha enzi kwa miaka shirini na minne. Ijapokuwa hakuna kapa isiyokosa usubi, alifanya mengi ya kujivunia pia. Hatimaye Rais Mwai Kibaki ambapo Kenya ilijipatia Katiba mpya ambayo hadi sasa imebadilisha sura ya uongozi katika nchi yetu. Kuna mabadiliko mengi ambayo yamejidhihirisha waziwazi hususan katika ulingo wa kisiasa, siyo jinsi mambo yalivyokuwa katika miaka ya awali.
Kwa mujibu wa katiba ya sasa, wakati wa uchaguzi mpiga kura atahitajika kuwachagua viongozi zaidi ya watano. Atahitajika kumchagua rais, gavana wa jimbo lake, seneta, mbunge, mwakilishi wa wanawake bungeni na mwakilishi wa baraza la jimbo. Kwa ujumla, inatazamiwa kuwa katiba hii itaibua viwango vya hali ya juu vya uwajibikaji miongoni mwa wanasiasa na wale wote walio katika nafasi za uongozi.
- Kidemokrasia, viongozi wa serikali hupigiwa kura na kuchaguliwa na______ wa nchi husika.
- wabunge
- watu
- wazalendo
- raia
- Kiongozi mkuu kabisa wa nchi ambayo ni jamhuri na huchaguliwa kidemokrasia ni
- Gavana
- Waziri mkuu
- Rais
- Mfalme
- Ni kauli ipi si sahihi kwa mujibu wa kifungu?
- Kenya imekuwa nchi huru kwa zaidi ya miaka hamsini
- Kenya ilijinyakulia uhuru wake mwaka wa hamsini
- Rais wa kwanza na wa pili kwa sasa hivi ni hayati
- Kenya tuliadilisha katiba waskati wa Rais Mwai Kibaki
- Katika aya ya pili, mwandishi hatudokezei kuwa
- Hayati Mzee Jomo Kenyata aliwapa wananchi wa Kenya sababu tosha ya kuionea fahari nchi yao
- Hayati Daniel Toroitich Arap Moi aliaga mwa wa elfu moja mia tisa sabini na nane
- Rais Moi alianzisha kauli mbiu ya kufuata nyayo za Mzee Kenyatta
- Mwito wa Harambee ulianzishwa
- Msemo ".... Aliposafiri njia ya marahaba ...." haumaanishi?
- alipoaga
- aliposafiri jongomeo
- alipofariki
- alipoenda na kucheza ngoma
- Kulingana ma kifungu
- Hayati rais Moi aliongoza nchi ya Kenya kwa zaidi ya miongo miwili
- Kauli mbiu ya Harambee ilihimiza Wakenya kutoishi kwa amani, upendona umoja
- Rais Kibaki alibadilisha sura ya uongozi
- Katiba mpya imeibua maswala mengi mazito
- Methali nyingine yenye maana sawa na "Hakuna kapa isiyokosa usubi" ni
- hakuna kovu la masimango
- hakuna masika yasiyokuwa na mbu
- kila shetani na mbuyu wake
- haba na haba hujaza kibaba
- Nchi ya Kenya ilipatia uhuru mwaka wa
- 1973
- 1964
- 1963
- 1978
- Katika aya ya mwisho tunadokezewa ya kwamba
- mpiga kura atapiga kura kuwachagua viongozi watano
- katiba mpya itaibua viwango vya ajabu
- bunge litakuwa na wawakilishi wa wanawake
- rais, makamu wake, spika na seneta ni baadhi ya viongozi wa serikali ambao watachaguliwa wakati wa uchaguzi
- Neno miongoni mwa limepigwa mstari katika ufamu liko katika kitengo kipi cha sarufi?
- Kihisishi
- Kihusishi
- Kiunganisho
- Kivumishi
MAAKIZO
- C
- B
- A
- D
- B
- C
- A
- D
- B
- C
- A
- D
- B
- C
- C
- D
- D
- B
- A
- D
- C
- B
- C
- D
- A
- C
- B
- D
- C
- A
- D
- D
- C
- C
- A
- B
- D
- C
- A
- B
- D
- C
- B
- B
- D
- A
- B
- C
- C
- B
Kiswahili - Class 6 End Term 1 Exam 2021 Set 1
Soma kifungu kifuatacho. Kina nafasi 1 hadi 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne. Chagua lifaalo zaidi.
Ni _____1_____kadhaa _____2______ na mwalimu huyo. Alikuwa mwalimu _____3______ sana katika lugha ya Kiswahili. _____4______mwalimu huyo alikuwa na _____5_____moja. Alikuwa na hasira za _____6______. Jambo ______7______ tu ______8______ akasirike vilivyo. Sisi ______9______ tulimpenda na kumtamania lakini ______10______ alipopandwa na ______11______ tulikuwa ______12______ kwa woga. Katika hali kama hiyo, macho yake ya ______13______ yangebadilika rangi na kuwa ______14______. Daima dawamu sitamsahau mwalimu huyo aushini _______15______.
-
- vitu
- mambo
- masaibu
- malalamiko
-
- tulichofunzwa
- tulizofunzwa
- tuliofunzwa
- tuliyofunzwa
-
- mstadi
- hatari
- mhodari
- stadi
-
- Hata hivyo
- Na
- Kwa
- Ndiposa
-
- jambo
- ila
- tatizo
- wahaka
-
- fisi
- simba
- kihongwe
- mkizi
-
- ndogo
- dogo
- lidogo
- mdogo
-
- lingetume
- ingesababisha
- lingesababisha
- zingesababisha
-
- sote
- zote
- wote
- nyote
-
- nyakati
- wakati
- pindi
- saa
-
- damu
- nyusi
- mori
- raha
-
- tukifyata ulimi
- tukilia
- tukicheka
- tukicheza
-
- paa
- kikombe
- mamba
- ustadi
-
- mekundu
- miekundu
- nyekundu
- kwekundu
-
- kwangu
- zangu
- mwangu
- pangu
Kutoka swali la 16 hadi 30, jibu kulingana na maagizo
- Jibu maamkizi haya:
Salaam aleikum ___________________________- salaam aleikum
- binuru
- marahaba
- aleikum salaam
- Shairi lenye mishororo minne katika kila ubeti huitwa:
- Tarbia
- Tathlitha
- Uwili
- Takhmisa
- Mtoto mdogo ameanguka vibaya. Kielezi katika sentensi hii ni:
- mtoto
- mdogo
- vibaya
- anguka
- Silabi za kati na za mwisho katika mishororo ya shairi huitwa,
- ubeti
- kibwagizo
- vina
- mizani
- Neno lipi haliko katika ngeli moja na mengine?
- Mwalimu
- Mlima
- Ndovu
- Daktari
- Mkoba wa kisu huitwa;
- podo
- upote
- ala
- ngao
- Kanusha sentensi ifuatayo:
Muthungu amekuja shule leo.- Muthungu hajaja shule leo
- Muthungu hajakuja shule leo
- Muthungu haji shule leo
- Muthungu hakuja shule leo
- Andika sudusi mbili kwa tarakimu:
- 3/5
- 3/6
- 2/5
- 2/6
- Malipo ya mtu aliyeshinda ni;
- faini
- karo
- mahari
- zawadi
- Tumia 'o-ote' katika sentensi hii;
Maskani haya hayana manufaa ________________________- zozote
- yoyote
- yeyote
- wowote
- Watu walipiga _____________ kumchagua mbunge wao.
- kura
- kula
- kalamu
- karo
- Anayetibu wagonjwa hospitalini huitwa:
- bawabu
- mhunzi
- tabibu
- mwalimu
- Dada ya baba yako huitwa:
- shangazi
- halati
- mjomba
- shemeji
- Jaza jina la makundi.
________________ cha barua.- Kikoa
- Doti
- Kipeto
- Kitosi
- Tegua Kitendawili
"Nikitolewa majini hufa." Jibu ni:- moyo
- yai
- chura
- samaki
Soma ufahamu huu kisha ujibu maswali 31-40
Dawa ya kulevya ni chochote kinachoathiri hali ya kawaida ya mwili wa binadamu. Kuna aina mbalimbali za dawa za kulevya kama vile bangi, kokeini, heroini, madraksi na za nusu kaputi. Aidha, sigara pombe na gundi ni dawa za kulevya zinazouzwa na watu pasipo kufikiria madhara yake.
Pia kuna dawa zinazopendekezwa na daktari ili kupunguza maumivu au uchungu mwilini. Zinapotumiwa vibaya huleta uraibu unaoweza kuadhiri afya ya mtumiaji.
Watu tofauti hutumia dawa za kulevya kwa sababu zinazohitilafiana. Kuna wale wanaotaka kudadisi dawa hizi kwa kuiga mienendo ya marafiki zao na kukinaishwa na maisha. Wengine huzitumia kwa kuwa hawana shughuli za kufanya. Wameadhiriwa na vyombo vya mawasiliano hasa runinga na uozo wajamii.
Matumizi ya dawa hizi kwa muda mrefu husababisha uzoefu ambao ni vigumu kuukatiza. Hivyo basi huleta madhara mengi yasiyo na kifani. Miongoni mwa hayo ni kukosa makini kazini na masomoni. Aidha kichaa, saratani ya mapafu hasa kwa wavutao sigara, uhalifu ili kugharamia dawa hizi ghali na kudhoofisha uamuzi wa kiakili unaosababisha hasara kubwa.
Wakiwa katika hali hii ya kutojijua wala kujitambua, wengi huweza kujidunga kwa sindano chafu zinazoweza kusababisha maradhi mengi yakiwemo ukimwi. Hatima yao huwa ni kifo kwa wote wanaofuata njia hiyo.
Madhara haya yaweza kuepukika endapo sote tutawajibika kwa kukataa kuandamana na marafiki wabaya, wapotovu, kukataa kutumiwa na walanguzi wa dawa hizi na kutafuta uraibu unaofaa na kuheshimu miili yetu.
Mwito basi ni kushirikiana bega kwa bega ili kujaribu kuangamiza dawa za kulevya na biashara yake.
- Dawa za kulevya ni nini?
- Chochote kinachopendekezwa na daktari
- Chochote kinachoathiri hali ya binadamu
- Chochote kinachoathiri mwili wa binadamu
- Chochote kinachoathiri kawaida ya mwili.
- Mifano ya dawa za kulevya zinazouzwa na watu wengi ni:
- bangi, madraksi na chai
- kokeini, madraksi, na kahawa
- madraksi, chai ya mkandaa na bangi
- sigara, heroini, pombe na kokeini
- Ni kweli kusema, uzoefu wa mihadarati ni:
- vigumu kuukatiza
- vibaya kuukatiza
- rahisi kuukatiza
- vigumu kuupunguza
- Hatima ya wanaotumia dawa za kulevya ni ipi?
- Madhara
- Mauti
- Unusu kaputi
- Uhalisi
- Kisawe cha zinazohitilafiana ni:
- Zinazosikilizana
- Zinazolingana
- Zinazotofautiana
- Zinazoshahibiana
- Neno kukinaisha lina maana sawa na:
- kuwa na matumaini ya maisha
- kutosheka na maisha
- kufurahishwa na maisha
- kuchoshwa na maisha
- Matumizi ya mihadarati huleta uraibu unaoweza:
- kupunguza afya ya binadamu
- kudumisha afya ya binadamu
- kuboresha afya ya bianadamu
- kudunisha afya ya binadamu
- Ni maradhi yapi ambayo huwezi kupata kutokana na utumiaji wa mihadarati?
- Pumu
- Kichaa
- Saratani ya mapafiu
- Uraibu
- Ipi kati ya hizi si jinsi ya kuepukana na athari hizi?
- Kukataa kuandamana na marafiki wabaya
- Kukataa kutumwa na walanguzi wa dawa hizi
- Kutafuta uraibu unaofaa na kuheshimu miili yetu
- Kutumia na kulangua mihadarati
- Neno dawa liko katika ngeli gani?
- LI-YA
- U-ZI
- I-ZI
- KU-KU
Soma ufahamu huu kisha ujibu maswali 41-50.
Sote tulikuwa tumeketi chumbani ndugu alipojitoma ndani ghafla bin vuu, huku akihema kama aliyenusurika kumezwa na chatu. "Kulikoni? Mbona unahema kama mgonjwa wa pumu?" Nilisaili.
Alitueleza kuwa alipigwa kabari na wanyang'anyi wakamwibia kila kitu. Aliwaendea polisi kuwaambia yaliyojiri lakini badala ya kumsaidia walipora kichache kilichobaki. Tukashindwa kutofautisha wezi na polisi.
Yale maneno ya ndugu yangu yalinichochea kuwaza wajibu wa walinda usalama ni upi? Askari ndio wanaofaa kulinda raia na kuhifadhi haki za wananchi. Hata hivyo wao wamebadilika na kukiuka sheria zenyewe. Wanahujumu raia. Endapo yule aliyetunukiwa jukumu la kukulinda ndiye anayekuhasiri. je usalama wetu uko wapi?
Sio askari wote wanaodhulumu raia. Kuna kikosi cha askari kanzu au wapelelezi ambao wamejaribu kwa mapana na marefu kulinda jina la idara yao. Kuna visa vichache sana vya makachero wanaofanya uhalifu dhidi ya umma. Wapokee pongezi zetu kama wananchi.
Na wale askani wanaovaa mavazi rasmi tunawarai kuwa wasipokee rushwa barabarani, wasiwaibie raia, wasiwasaidie wezi wala wasitumie bunduki zao vibaya.
- Nani aliyeingia chumbani kwa kasi?
- Askari polisi
- Rafikiye mwandishi
- Kakake mwandishi
- Nduguye askari
- Alipigwa kabari na wezi ina maana:
- walimkimbiza mbio mbio
- walimsindikiza hadi nyumbani
- walimkaba koo wakamwibia
- waliomzomea mhusika
- Polisi walipopata habari za wizi huo:
- walimwibia mhusika
- walianza kusaka wezi
- walimfukuza aliyeiba
- walifungua kesi kituoni
- Askari hawana jukumu la kulinda:
- wananchi
- waporaji
- umma
- raia
- Ina maana gani kuwa askari wamebadilika?
- wanachunga sheria
- hawakiuki sheria
- wanalinda sheria
- wanavunja sheria
- Ukihasiriwa na anayefaa kukulinda:
- huna matatizo
- huna usalama
- huna la kuogopa
- huna wasiwasi
- Kikosi gani kimetajwa kufanya kazi vizuri?
- Askari kanzu
- Askari polisi
- Askari jela
- Askari jeshi
- Hii ni fani gani ya lugha?
Hema kama mgonjwa wa pumu?- Takriri
- Methali
- Nahau
- Tashbihi
- Askari wanashauriwa:
- wapokee hongo barabarani
- wadhulumu raia
- wasitumie silaha zao ovyo ovyo
- wawasaidie wahalifu katika njama
- Kichwa kifaacho habari hii ni?
- Kudumisha usalama nchini
- Uhalifu wa askari wote
- Ndugu aliyevamiwa na kukabwa
- Usalama wa askari
INSHA
- Umepewa dakika 40 kuandika Insha yako.
- Andika insha ya kusisimua kuhusu;
ASIYESIKIA LA MKUU HUVUNJIKA GUU
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
_____________________________________________________________________________________
Marking Scheme
- B
- D
- D
- A
- B
- D
- B
- C
- A
- C
- C
- A
- B
- A
- C
- D
- A
- C
- C
- B
- C
- A
- D
- D
- B
- A
- C
- A
- C
- D
- C
- D
- A
- A
- C
- B
- D
- D
- D
- C
- C
- C
- A
- B
- D
- B
- A
- D
- C
- A
Kiswahili Activities - Grade 5 End Term 1 Exam 2021 SET 1
COMPETENCY BASED CURICULUM
GREDI YA 5, MWISHO WA MUHULA WA 1
SHUGHULI ZA KISWAHILI
JINA....................................................SHULE............................................
SEHEMU 1
KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA
Mwalimu amsomee mwanafunzi kifungu hiki kisha amwulize mawasli yafuatayo
Paka yuko jikoni. Amebeba panya mdomoni. Panya huyo ni mweusi. Paka anajificha mvunguni mwa meza. mama anamwona paka.
- Paka yuko wapi?
(mwananfunzi ajibu) - Paka amebeba nini mdomoni?
(mwananfunzi ajibu) - Panya huyo ni wa rangi gani?
(mwananfunzi ajibu) - Paka anajificha wapi?
(mwananfunzi ajibu) - Nani anamwona paka?
(mwananfunzi ajibu)
SEHEMU 2
KUSOMA KWA SAUTI
Mwanafunzi asome kifungu hiki kwa sauti
Ilikuwa siku ya Ijumaa tulipokuwa sebuleni tukitazama runinga. Baba alianza kutusimulia jinsi ambavyo mwalimu wao alikuwa akiwaeleza kuhusu umuhimu wa miti. Hata ingawa alikuwa shuleni miaka sitini iliyopita, alikuwa anayakumbuka vizuri.
Alianza kwa kusema kuwa mwalimu wao alisema kuwa miti huwa maskani ya wanyama mbalimbali sanasana nyuni ambao hutengeneza viota vyao na kutagia mayai humo. Aliendelea kutuambia kuwa wanyama wengine wanaotegemea miti kama makazi ni wanyamapori vile samba , chui, pundamilia na wengine.
SEHEMU 3:
UFAHAMU
Mwalimu asome kifungu hiki na kujibu maswali
- NDOTO YA AMINA
Babu alimnunuluia Amina godoro na foronya. Usiku alipolala, aliota ndoto. Aliota kuwa alikuwa msichana mkubwa. Alikuwa akifanya kazi ya ualimu. Baada ya miaka miwili aliacha ualimu akawa mkulima. Aliuza mazao akapata shilingi laki tatu. Alipokuwa akipeleka pesa zake benkini, aliamka kutoka usingizini.- Nani alimnunulia Amina godoro?
- Aliota ndoto wakati gani?
- Mara ya kwanza alikuwa akifanya kazi gani?
- Baada ya miaka miwili alianza kufanya kazi gani?
- Alikuwa akipeleka pesa zake wapi?
- MWALIMU BIDII
Mwalimu Bidii ni mwalimu wa Kiswahili. Anafundisha katika shule ya msingi ya Hekima. Kila siku yeye hutukumbusha kuwa tuwe watoto safi. Kuna siku alituletea ndizi. Tulifurahia mno. Alituahidi kuwa atatupeleka jijini Mombasa.- Mwalimu Bidii hufundisha somo gani?
- Mwalimu Bidii hufundisha katika shule gani?
- Mwalimu Bidii huwahimiza wanafunzi kuwa watoto__________________
- Mwalimu aliwaletea nini?
- Mwalimu aliwaahidi kuwa atawapeleka wapi?
SEHEMU 4: SARUFI
- Tunga sentensi ukitumia maneno haya
- Jiwe
- Embe
- Mwiko
- Soko
- Fimbo
- Andika sentensi kwa wingi
- Kiatu chake kimeraruka
_______________________________________________________________ - Mtoto yule anakula tunda
_______________________________________________________________ - Goti lake limeumia.
_______________________________________________________________ - Kioo hiki kilivunjika jana.
_______________________________________________________________ - Meza hii ni ya mwanafunzi.
_______________________________________________________________
- Kiatu chake kimeraruka
- Andika akisami kwa maneno
- 1/6
- 1/4
- 1/2
- 1/3
- 1/5
- Geuza maneno yafuatayo katika hali ya ukubwa
- Mto
- Mtu
- Mke
- Mti
- Mji
INSHA
Andika insha kuhusu
NYUMBANI KWETU
MAAKIZO
SEHEMU 1
Mwanafunzi anafai kujibu kulingana na swali aliloulizwa
SEHEMU 2
Mwanafunzi anafai kusoma kwa sauti kifungo chote
SEHEMU 3
- NDOTO YA AMINA
- Babu
- Usiku alipolala
- Ualimu
- ukulima
- benkini
- MWALIMU BIDII
- Kiswahili
- Shule ya msingi ya Hekima
- watoto safi
- Ndizi
- (jijini) Mombasa
SEHEMU 4: SARUFI
- Kutunga sentensi:
Mwanafunzi anafai kutunga sentensi kulingana na maana sahihi ya maneno aliyopewa - Wingi
- Viatu vyao vimeraruka
- Watoto wale wanakula matunda
- Magoti yao yameumia
- Vioo hivi vilivunjika jana
- Meza hizi ni za wanafunzi
- Akisami
- Sudusi
- robo
- nusu
- thuluthi
- humusi
- Ukubwa
- Jito
- jitu
- jike
- jiti
- jiji