Displaying items by tag: kiswahili
Kiswahili Questions and Answers - Class 8 End of Term 1 Exams 2022
MASWALI
Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo. Jaza kila pengo kwa jawabu lifaalo zaidi.
Bahili hakujua__ 1___ ya ukarimu __ 2 _siku _ 3 _ na ya kumfika. Yeye alikuwa_ 4 watu wanaosadiki kuwa kwa lolote ambalo __5 _mtu yeyote, hawana budi 6. malipo. Watu hawa hujitetea kwa methali isemayo, _ 7__'. Siku hiyo alipoteza nauli yake alipokuwa akirejea nyumbani. Juhudi zake za kuomba msaada hazikufua dafu. Basi __ 8hadi chengoni huku amechoka tiki.
-
- thamani
- dhamani
- umuhimu
- sababu
-
- tangu
- hata
- wala
- hadi
-
- aliofikwa
- aliyefikwa
- alipofikwa
- alivyofikwa
-
- baadhi ya
- mithili ya
- kati ya
- miongoni ya
-
- wanalomtendea
- wanamtendea
- wamtendealo
- wakimtendea
-
- kumtoza
- kumtolesha
- kumtoesha
- kutozwa
-
- Jaza ya hisani ni hisani
- Lisilo budi hubidi
- Tenda wema nenda zako
- Mkono mtupu haurambwi
-
- akaenda joshi
- akapiga milundi
- akatia mrija
- akapiga vijembe
Ni jambo la kusikitisha kuwaona vijana wakiingilia starehe 9 .Jambo hili limechangia _ 10_ kwa maadili katika jamii. __11___vijana hata wanaoingilia uhalifu__12__starehe hizi. Wengine nao huzurura mithili ya 14 wakitafuta wenzao watakaowanunulia vileo.__15___ na hali hii huenda tukakipoteza kizazi cha kesho.
-
- wasiozimudu
- wasioimudu
- wasizozimudu
- wasivyozimudu
-
- kuzorota
- kufilisika
- kuimarika
- kutekelezwa
-
- kuko
- iko
- раро
- wapo
-
- japo
- ili
- bali
- ila
-
- kugharimia
- kugharimu
- kugharamia
- kugharamisha
-
- dira
- mwewe
- mbwakoko
- pakashume
-
- Tukienda
- Mkiendelea
- Wakiendeleza
- Tukiendelea
Kuanzia swali la 16 mpaka 30, jibu kila swali kulingana na maagizo uliyopewa.
- Chagua sentensi iliyotumia kielezi cha kutilia mkazo kwa usahihi.
- Wao ni marafiki wa kufa kupona.
- Kamau ni rafiki yangu wa toka nitoke.
- Tumeuenzi utamaduni wetu tangu asili na jadi.
- Waombolezaji walilia kwa shangwe na hoihoi.
- Nyuzi ni wingi wa uzi aidha ni
- kasi ya mawimbi baharini.
- vipimo vya joto.
- viwango vya mvua iliyonyesha.
- Makadirio ya masafa ardhini.
- Tambua sentensi iliyotumia ji ya hali.
- Mtoto alijichafua akicheza.
- Mwimbaji yule ni maarufu sana.
- Utunzaji wa mazingira ni wajibu wetu sote.
- Jigari hilo ni la mjoba wake.
- Ukitaka kupima usawa wa ukuta utatumia kifaa kipi?
- Timanzi
- Patasi.
- Jiriwa.
- Pimamaji.
- ______ ni zao zima la mmea uzaao ndizi.
- Chane
- Mgomba
- Kipeto
- Mkungu
- Andika wingi wa sentensi ifuatayo:
Hukujua kuwa angeniuliza swali kama hilo.- Hawakujua kuwa mngewauliza maswali kama hayo.
- Hamkujua kuwa wangeniuliza maswali kama hiyo.
- Hamkujua kuwa wangetuuliza maswali kama hayo.
- Hawakujua kuwa mngetuuliza maswali kama hayo.
- Akifisha sentensi ifuatayo.
Mwalimu aliwauliza mnafanya nini hapa.- Mwalimu alitaka kujua walichokuwa wakifanya hapo?
- Mwalimu aliwauliza, "Mnafanya nini hapa?"
- Mwalimu aliwauliza, "mnafanya nini hapa?"
- Mwalimu aliwauliza, "Mnafanya nini hapo?
- Ainisha maneno yaliyoangaziwa katika sentensi ifuatayo. Timu hii ni hodari kuliko ile.
- Kivumishi, kielezi, kiwakilishi.
- Kivumishi, kihusishi, kivumishi.
- Kivumishi, kiunganishi, kielezi.
- Kiwakilishi, kihusishi, kivumishi.
- Kinyume cha methali:
Mtoto akililia wembe mpe ni- Mpanda ngazi hushuka.
- Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
- Mchagua jembe si mkulima.
- Pilipili usiyoila yakuwashiani?
- Kati ya vyombo hivi vya muziki, kipi cha asili?
- Gitaa.
- Fidla.
- Tarumbeta.
- Siwa.
- Mimi ni mvulana. Jina langu ni Tito. Nina dada mmoja anayeitwa Asha. Kila tunapoonana sisi huitana
- kaka.
- mpwa.
- umbu.
- mnuna.
- Mzigo huu ni nanga ukiubeba kidogo tu unalowa jasho chapachapa. Sentensi hii imetumia tamathali gani za uscmi?
- nahau, tashbihi.
- Sitiari, tanakali za sauti.
- Chuku, milio.
- Sitiari, nahau.
- Zawadi anayopewa mtu kwa kupata kitu kilichopotea huitwaje?
- Fichuo.
- Arbuni.
- Koto.
- Kiangazamacho.
- Mkutano ulimalizika wakati wa jua la utosi.Je huu ni wakati gani?
- Adhuhuri.
- Macheo.
- Machweo.
- Asubuhi.
- Chagua kikundi cha sifa zisizochukua viambishingeli.
- imara, halali, dhaifu, laini.
- bora, safi, chafu, gani.
- tele, refu, embamba, kali.
- tajiri, tano, gumu, kadhaa.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31 – 40
Hivi karibuni, nchi ya Kenya iliingia katika hesabu ya zile nchi ambazo zimewahi kudungwa na mwiba wa vita vya wenyewe kwa wenyewe. Japo vita hivi vilisababishwa na uchaguzi wa mwaka Elfu mbili na saba, vilituonyesha namna tulivyogawanyika katika misingi ya kikabila. Kuna mengi ambayo tunaweza kufanya ili kuuziba ufa huu ambao umetugawanya.
Kwanza tunaweza kuhimiza matumizi ya lugha ya taifa katika nyanja zote za maisha badala ya watu kutumia lugha zao za mama. Vilevile, viongozi waache ukabila na wawe na mtazamo wa kitaifa. Wamechangia sana kuchochea hisia za kikabila badala ya kuwaunganisha Wakenya. Maeneobunge mengine yamegawika katika misingi ya kikabila na hata kupewa majina ya kikabila. Pia inafaa kila Mkenya ahubiri umoja wa kitaifa.
Shule zetu za upili zimekuwa vyungu vya kuchemshia ukabila. Isipokuwa shule za kitaifa ambazo huchukua wanafunzi kutoka maeneo yote nchini, shule za magatuzi almaarufu kaunti na zile za wilaya huchukua asilimia sabini ya wanafunzi kutoka maeneo ya karibu. Hivyo basi utapata mwanafunzi amesomea eneo hilo kutoka shule ya msingi mpaka kidato cha nne. Wanafunzi kama hawa hutumia lugha za mama na kwa hivyo hawachangii katika utaifa. Itafaa vilevile iwapo kutakuwa na ugavi sawa na rasilimali. Ilivyo sasa ni kuwa maeneo mengine yana maendeleo ya hali ya juu na mengine hayana hata chakula. Jambo hili linaleta uhasama wa kimaeneo.
Tunaweza vilevile kuwa na siku ya utamaduni ambapo tuna maonyesho ya kitamaduni. Kwa kuonyesha utamaduni wa kila kabila nchini, tutafurahia tamaduni anuwai tulizo nazo na kuzichukulia kuwa kitegauchumi kuliko kuwa sababu ya vita.
Makundi haramu pia yanaleta ukabila. Wakati wa vita vilivyozuka hapa nchini, kila kabila lilikuwa na kundi lake la kulipigania. Kulikuwa na uhalifu mkubwa uliosababishwa na makundi haya yafaa kupigwa marufuku.
Nafasi za kazi nazo ziwaendee wale waliohitimu na wala si kutolewa kwa misingi ya kikabila. Vilevile, iwapo viongozi watakuwa mifano mizuri watasaidia sana viongozi waache matamshi kama vile, “kabila letu linaonewa," au "Ndugu zangu tunamalizwa.” Iwapo watakuwa na mitazamo ya kitaifa, basi watasaidia sana kuleta mtagusano katika nchi hii.
Wananchi wenyewe waelewe kitu kimoja, kuwa makabila nchini Kenya ni mawili - matajiri na maskini. Kwa mfano, hata baada ya kuwachonganisha Wakenya viongozi wetu huonekana wakila na kucheka pamoja. Sisi wananchi tumebaki na kinyongo lakini wao ni marafiki baada ya kututumia na kupata walichotaka, madaraka.
Vyombo vya habari vinapaswa kuarifa, kuelimisha, kuburudisha na kuyafichua maovu. Hata hivyo, kuzuka kwa idhaa za kikabila kimechangia kuvuruga umoja. Viongozi hutumia vyombo hivi kuhubiri chuki kwa watu wa makabila yao. Mambo ya aina hii hudhoofisha juhudi za kulinganisha taifa.
Hakika, ni vyema tufikirie kuhusu wajibu wetu katika maendeleo yetu binafsi na ya taifa letu. Chombo hakiendi ila kwa kafi. Tukijijenga, taifa zima tutapiga hatua kubwa pia. Badala ya kutumia juhudi zetu kuzozana kwa misingi ya kikabila, ni vyema tushikane mikono ili tusonge mbele pamoja.
- Ni sahihi kusema kuwa,
- Kenya ilijiunga kupigana na mataifa yenye vurugu.
- Kenya imehusika tena katika machafuko ya kisiasa.
- Kenya imekuwa mojawapo ya nchi zilizoshuhudia machafuko.
- Kenya ilikuwa nchi ya kwanza kushuhudia vita vya kikabila.
- Vita hivi vinavyozungumziwa,
- vilitokea kabla ya uchaguzi mkuu nchini.
- vilitokana na tofauti za kikabila zilizojitokeza kisiasa.
- vilisababishwa na viongozi wenye maono ya kitaifa.
- vilikuwa baina ya makabila makuu na yale madogo.
- Umuhimu wa lugha ya kitaifa kulingana na kifungu hiki ni,
- kuyaangamiza makabila.
- kutambulisha taifa.
- kukuza utamaduni.
- kuliunganisha taifa.
- Shule za upili nazo zimelaumiwa kwa
- kutohimiza utangamano wa jamii mbalimbali.
- kutoa mafunzo kwa kutumia lugha ya marna.
- kupokea wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali.
- kuwanyima nafasi wanafunzi wa jamii za karibu.
- Kuendelea kwa baadhi ya maeneobunge kuliko mengine ni ishara kuwa,
- ubaguzi unajitokeza katika ugavi wa rasilimali.
- mipaka ya kimaeneo imewekwa kwa misingi va kikabila.
- watu wa maeneo haya wana bidii kuliko wenzao.
- serikali inazingatia usawa katika ugavi wa rasilimali
- Kulingana na aya ya nne,
- kuwepo kwa tamaduni mbalimbali kunahujumu umoja wetu.
- Maonyesho ya kitamaduni yamechangia ukabila nchini.
- tofauti zetu zinaweza kutufaidi badala ya kutugawanya.
- kila kabila lina siku ya utamaduni ya kitaifa.
- Makundi haramu nchini,
- yanasaidia kutetea makabila yao yasinyanyaswe.
- mara nyingi hutetea haki za makabila yote.
- hayana uhusiano wowote na makundi ya kikabila.
- hutekeleza uhalifu kwa visingizio vya kutetea jamii.
- Makala haya yameonyesha wazi kuwa,
- Viongozi wa kisiasa ni maadui wakubwa.
- Viongozi wa kisiasa huwatumia wanyonge kujifaidi.
- Nchi hii haina makabila mengi jinsi tunavyofikiria.
- Idhaa za kikabila huanzishwa na Wanasiasa nchini.
- Methali 'chombo hakiendi ila kwa kafi' ina maana kuwa,
- maendeleo hayatapatikana bila watu kuwa na ubinafsi.
- juhudi za kuliunganisha taifa nila serikali na viongozi.
- taifa haliwezi kuendelea bila mchango wa wananchi.
- wananchi hawawezi kuungana bila viongozi wa kisiasa..
- Neno mtagusano jinsi lilivyotumika lina maana sawa na,
- utangamano.
- utengano.
- mvurugano.
- utamaduni.
Payuka alikuwa kilimilimi hivi kwamba lolote alilonasa kwa yeyote awaye yule, sharti angeliwasilisha na kumtaarifu mwingine. Hakujali lilisemwa na nani au kwa nini. Hata mambo ya faragha ya baraza la wazee angeingilia tu, sijui akiwa mgeni wa nani, kisha angeyasambaza hata kwa vibaka na vigoti. Udukizi wa namna hii ulimpelekea kuwa na rabsha baina yake na wote waliomzunguka. Kila aliyemwona akikaribia alijaribu kuyafunika maneno yake hadi apite. Msemo, “funika kombe mwanaharamu apite," ukawa wamlenga yeye.
Waaidha, alikuwa na ulimi wa upanga. Kungalikuwa na mashindano ya kukaripiana, neno la kwanza la payuka lingalimpiga dafrao mpinzani wake hata ajiuzulu mara moja. Alifikiri maisha ni jukwaa la mashindano na kwake yeye aliyekuwa na upyaro wa msimu ndiye angeshinda. Maneno yake yote yalikuwa mfano wa sumu ya joka kali. Naye kwake, hili lilikuwa na hasara pia. Aliuvaa uso usiofurahi, kila wakati umekunja mapeto, midomo imekunjana na uso umejaa makanyanza kama mzee mwenye umri wa miaka mia moja. Mgeni yeyote aliyemwona na kusikia kuwa alikuwa mtoto ambaye hata ubwabwa haujamtoka shingoni alimaka.
Payuka pia alikuwa mcheza shere. Ukweli ukawa neno lisilo na maana kwake. Hakuiona ahadi kuwa deni kazini angeahidi jambo fulani wala asingelitimiza asilani. Mkutanapo angekupiga chenga kukudanganya. Angekupaka mafuta kwa mgongo wa chupa na uridhikapo na kuenda, angeahirisha utekelezaji wa ahadi yenu hadi mtakapokutana tena. Kwa mtendwa, hii ilikuwa dhihaka iliyokithiri.
Uchokochoko wake ulimfanya awe ndumakuwili. Akimwona yeyote akinawiri angejitokeza kama anayeteremea mno na mwenye kusherehekea pamoja na apataye. Hili lingefanya anayelengwa kumfunulia moyo wake wote na kuuacha wazi kwake amchunguze atakavyo. Maadui wangevutwa kwa ulimi. Kuna walioibwa kutapeliwa, kuhujumiwa kwa mioto au kwa namna yoyote ile, wengine waliuawa kutokana na hila zake kumbe alitafuta jinsi ya kufaidika yeye!
Naye avumaye baharini papa kumbe wengine wapo? Ukiua kwa upanga, kwa upanga pia utakufa. Chokochoko za payuka zikawabughudhi vijana wengi kwa muda mrefu, nao wakampangia njama. Wakaitumia njia ile ile aliyotumia kulipizia kisasi - ulimi mtamu. Walijua kuwa yeye alipenda kuutumia ulimi wake kupata sifa. Wakati huo makachero walikuwa wakichunguza kwa kina vyanzo vya visa mbalimbali vya uhalifu kitongojini humo. Wakajua kumsifu kwa kiasi kidogo tu kungemfanya kujisahau na kuelezea siri zake zote
Licha ya kuutumia kuropoka, ulimi wa Payuka pia ulitumiwa kuchapa maji. Siku ya mtego, vijana hao walijifanya karimu kwelikweli, wakamnunulia kileo. Alipokwishauchapa ugimbi, vijana wakaanza kumsifu Payuka kwa ujanja huku wakiwakashifu watu mbalimbali waliojua kuwa walikwishahasiriwa na afriti huyu. Kusikia sifa zake zainuka, alianza kutokwa na maneno shelabela. Alieleza alivyowashusha wote hao kwajinzi mbalimbali - kuna aliowapangia kuuawa, kuibiwa, kuchomewa nyumba na kadhalika.
Wakati huu wote, kachero mmoja alikwishakaribia akiwa na kiredio cha kunasia sauti. Akishaboboka bobobo, makachero wawili wakajitokeza, wakajitambulisha na kumfahamisha Payuka shughuli zao pale. Alipojaribu kujitetea kiredio kikafunguliwa, akayasikia yote aliyosimulia. Akalevuka palepale, akawaangalia vijana wale majirani ambao sasa walikuwa wakitabasamu. “Twende kituoni!” Makachero wakamwamuru. Waliokuwepo wakajisemea nyoyoni, “Kweli heri kujikwaa dole kuliko kujikwaa ulimi”.
- Chagua jibu lililo sahihi.
- Payuka aliyachunguza mambo vizuri kabla ya kuyasambaza.
- Wengi walipenda kuzisikiliza chokochoko za Payuka.
- Baraza la wazee lilimtumia Payuka kutangaza mambo yake.
- Payuka alipenda kuchunguza maneno ili ayasambaze.
- Kutokana na hulka ya Payuka,
- mara nyingi alivurugana na watu.
- alijizolea umaarufu kila mahali.
- alipendwa sana na vibaka na vigoli.
- alijipata akizungukwa na watu mara nyingi.
- 'Neno la kwanza la Payuka lingalimpiga dafrao mpinzani wake hata ajiuzulu mara moja'. Kauli hii imetumia tamathali gani za usemise
- sitiari, nahau.
- nahau, chuku.
- tashihisi, chuku.
- tashbihi, kinaya.
- Payuka alionekana kuwa mzee kwa sababu ya,
- upyoro wake
- kununa mara nyingi.
- kuchukiwa na watu.
- maneno mengi aliyojua.
- Sifa nyingine ya Payuka iliyojitokeza ni,
- kutotimiza ahadi.
- kuingiliana na wageni.
- kupenda vita.
- kuhepa watu wasikutane.
- Msemo mwingine wenye maana sawa na, angekupaka mafuta kwa mgongo wa chupa'ni
- angekupiga vijembe.
- angekuvika kilemba cha ukoka.
- angekuonea gere.
- angekutia kiwi.
- Payuka alijenga uhusiano na wale waliofanikiwa ili,
- azijue siri zao na kuwatangazia wengine.
- aige nyendo zao na kufanikiwa kama wao.
- atangaze siri zao waweze kutiwa mbaroni.
- awavute karibu na kupata nafasi ya kuwadhulumu.
- Madhara ya ulevi yanayojitokeza katika i kifungu ni,
- mtu kushindwa kudhibiti maneno yake.
- kunaswa na makachero bila kujitetea ipasavyo.
- kutoa siri za wenzetu kwa maadui zao.
- kuwafuata hata maadui ili kufaidika.
- Payuka hakuweza kujitetea kwa kuwa,
- alikuwa mlevi kupindukia.
- ushahidi dhidi yake ulikuwa dhahiri.
- wenzake walitoa ushahidi dhidi yake.
- alishtakiwa kwa mambo ambayo hakuyajua.
- Kulingana na kifungu, ni wazo kuwa,
- askari walipofika pale walikuja kumchunguza Payuka.
- vijana waliomnunulia Payuka pombe walikuwa makachero.
- Payuka alikuwa mhusika mkuu kwenye maovu kijijini.
- vijana waliomsaliti Payuka walikuwa washirika wake maovuni.
MARKING SCHEME
- A
- D
- C
- C
- B
- A
- B
- B
- C
- A
- D
- B
- A
- C
- D
- C
- B
- C
- A
- D
- C
- B
- A
- B
- D
- C
- B
- D
- A
- A
- C
- B
- D
- A
- A
- C
- D
- B
- C
- A
- D
- A
- C
- B
- A
- D
- D
- A
- B
- C
Kiswahili Questions and Answers - Class 8 End of Term 1 Exams 2022 Set 1
QUESTIONS
Soma vifungu vifitatavyo vina nufasi 1 mpaku 15. Kwa kila nafasi umepewa majihu munne hapo. Juze pengo kwa kuchagua jawabu lifualo zaidi.
Umuhimu wa teknolojia ya kisasa _1_ maisha ya binadamu _2_ kupuuzwa _3_, _ 4__ sekta zilizonufaika pakubwa_5_ na uvumbuzi huu ni ile ya mawasiliano. Ilapo zamani mawasiliano _6_ katika matumizi ya mbinu kama vile_7_ upigaji wa magoma, kuwasha moto _8_ moshi angani _9_ kuwatuma wajumbe mbalimbali.
-
- ya
- wa
- katika
- kwa
-
- hauwezi
- huwezi
- haiwezi
- hayawezi
-
- kabisa
- tena
- vile
- kamwe
-
- Baadhi ya
- kati ya
- miongoni ya
- mithili ya
-
- kutokana na
- kilingana na
- mintaarafu ya
- zaidi ya
-
- yalikuwa
yamejikita - yangekuwa
yalijikita - yamekuwa
yakajikita - yanakuwa
yamejikita
- yalikuwa
-
- ;
- _
- :
- ---
-
- uliovusha
- iliyovusha
- uliyofusha
- uliofusha
-
- japo
- halikadhalika
- angaa
- wala
Shama _10_ wazo la kujiunga na chuo cha kiufundi kuwa _11_ kujiendeleza maishani. Hata hivyo, aliolewa dhahiri shahiri kuwa _13_ usingepatikana vivi hivi tu bali bidii na uwajibikaji _15_ ulihitajika.
-
- aliiona
- aliuona
- alijiona
- aliliona
-
- nzuri
- njema
- lema
- zuri
-
- lingempa
- linampa
- litampa
- limempa
-
- jogoo la shamba haliwiki mjini
- mtaka cha mvunguni sharti ainame
- mchuma janga hula na wa kwao
- juhudi si pato
-
- wake
- wako
- wenu
- wao
-
- wenye
- hiyo
- wenyewe
- ambao
Kuanzia nambari 16 mpaka 30. jibu kila swali kulinganu na maagizo uliyopewa.
- Kiambishi ki-kimctumika vipi katika sentensi ifuatayo.
Wanafunzi wale walikuwa wakizingatia nidhamu.- Kuonyesha masharti.
- Kuonyesha hali ya kuendelca.
- Kuonyesha jinsi ya kutenda.
- Kuonyesha vitendo vinavyofanyika pamoja.
- Kutokana na kitenzi vumilia tunapata sifa gani?
- Uvumilivu
- Kuvumilia
- Vuma
- Vumilivu
- Andika wingi wa sentensi ifuatayo.
Sonara alinifulia mkufu huu.- Sonara walitufulia mikufu hii.
- Masonara walinifulia mikufu hii.
- Sonura walitufulia mikufu hizi.
- Masonara walitufulia mikufu hii.
- Ipi ni sauti ghuna?
- b
- th
- sh
- f
- Chagua ukanushaji wa sentensi ifuatayo.
Bakari ameuchukua mkoba wake.- Bakari hakuuchukua mkoba wake.
- Bakari hajauchukua mkoba wake.
- Bakari hauchukui mkoba wake.
- Bakari hatauchukua mkoba wake.
- ....................................ni mtu ambaye huwabobca watu mizigo kwa malipo.
- Dalali
- Megazega
- Mjumu
- Hannali
- Ainisha maneno yaliyoangaziwa katika sentensi ifuatayo.
Nyumba yenu imejengwa vizuri lakini ile si thabiti.- kivumishi kivumishi, kielczi
- kiwakilishi, kiunganishi, kiashiria
- kivumishi kiunganishi, kiwakilishi
- kielczi, kiunganishi. kiwakilishi
- Mtu unapotaka kupishwa njia husemaje?
- Simile
- Ashakum
- Samahani
- Hebu
- Akisami 5/7 kwa maneno ni
- subui tano
- humusi saba
- thumni tano
- saba kwa tano
- Chagua jozi ambayo hailingani.
- simba, shibli
- nzige, kimatu
- papa, kincngwe
- sungura, kinyempre
- Andika kauli ya kutendewa ya sentensi ifuatayo.
Fundi alimshonea Shama kiatu kibandani.- Kiatu cha Shama kilishonwa na fundi kibandani.
- Shama alishonewa kiatu kibandani na fundi.
- Kiatu kilishonewa kibandani kwa Shama na fundi.
- Fundi alimshoneshea Shama kiatu kibandani.
- Tegua kitendawili kifuatacho;
Hausimiki hausimami.- Moto
- Mkoba
- Moshi
- Mkulu
- Chagua sentensi iliyoakifishwa ipasavyo.
- Kibe ni kijana mpole: Yeye ni mwerevu darasani
- "Uwanja huu," akasema mwalimu una nyasi ndefu.
- Wakazi wengi wa mtaa huu ni wafanyabiashara
- Selina (yule wa runingani) ana sifa kochokocho.
- Kanda ni utepe wa kunasia sauti au picha.
Kanda pia ni- mfuko wa ngozi wa kuhifadhia vitu.
- namna ya chombo cha usafiri baharini.
- mtu mwenye tabia ya udanganyifu.
- kuivisha vitu kama mikate kwenye joko.
- Andika methali yenye maana sawa na hii
Kikulacho ki nguoni mwako.- ibilisi wa mtu ni mtu.
- Mla nawe hafinawe ila nizaliwa nawe.
- Zimwi likujualo halikuli likakumaliza.
- Dawa ya moto ni moto.
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali kuanzia 31 mpaka 40
Mwili wa mwanadamu hawezi kufanya kazi kama inayotarajiwa iwapo hauna afya. Watu wengine hudhani kuwa afya ni jambo la nasibu tu. Hawa huachilia miili yao kufanya kazi kama punda bila kujali maslahi yao. Mtu asiyejali rai yake huchakaa haraka na kuwa dhaifu.
Njia mojawapo ya kuhakikisha kuwa mwilfuna nguvu na siha inayostahili ni kupitia kwa vyakula. Uzingatiaji wa lishe bora ni muhimu kwa afya ya mwanadamu. Lishe bora huurutubisha mwili na kuacha ukiwa katika hali nzuri. Maandalizi bora ya vyakula ni kuhakikisha kuwa vimeiva kabisa ili kuepuka maumivu ya tumbo na kasoro nyinginezo. Aidha, vyakula visivyoandaliwa vizuri humfedhesha mwenyeji mbele ya wageni wake.
Ulaji wa chakula haumaanishi kula bila breki. La, unamaanisha kula vyakula ambavyo vina manufaa kwa mwili yetu. Baadhi ya watu hula vyakula vyenye wingi wa mafuta, Mafuta mengi hatimaye huleta madhara hasa kwa mtu asiyefanya mazoezi ya viungo vya mwili Ulaji wa mayai kwa wingi pamoja na nyama ya kuchoma huweza kumletea mlaji matatizo ya kiafya. Vyakula hivi na vingine huhitaji kuliwa kwa vipimo.
Mikono haina budi kuwa safi kabla ya kuanza kula kwa wengine, kumwanikaida tu, hawatumii sabuni kamwe. Kukipakia chakula bila kuzingatia usafi huweza kusababisha uele wa waba. Isitoshe, maji yasipochemshwa huweza kusababisha maradhi haya. Ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha kuwa viwango vya usafi vimezingatiwa kila wanapotaka kula
Yapo maradhi mengine ambayo husababishwa na wadudu, Mfano wa haya ni malaria na malale, Ni vyema kuzingatia usafi wa mazingira yetu ili kuyaepuka magonjwa haya. Vitu vinavyovunda navyo visiachwe kuzagaa kila mahali ili kuwaondoa nzi wanaoweza kucheza magonjwa. Aidha, nyasi na vichaka vinufaa kufyekwa bila kusahau kuondoa mikobe na vidimbwi vya maji takat.
Uvutaji wa sigara na ulevi ni baadhi ya tabia ambazo huwaletea waja matatizo ya kiafya. Moshi unaovutwa una madhara mengi sio tu kwa afya ya mvutaji bali pia kwa walio karibu naye. Pombe humdhuru mnywaji kwa namna nyingi; kuna wale ambao hukumbwa na tatizo la ini. Miili ya hawa hushindwa kufanya kazi na hivyo wakaishia kutangulia mbele ya haki.
Mwili vilevile huhitaji mazoezi ya viungo ili kuweza kubaki katika hali nzuri ye afya na utendakazi. Baadiri ya watu hufanya mazoezi ya kukimbia asubuhi na jioni jioni. Wengine hutembea masafa fulani ili kama wanavyosema wenyewe kunyosha miguu. Wengi hununua baiskeli ili watumie nguvu kuziendesha; kusudi darnu ipate kuranda vizuri kote mwilini na viungo kunyooka. Baadhi hujinunulia vifaa vya kufanyia mazoezi nyumbani au kulipa ada ya kutumia sehemu zenye vifaa hivyo.
Rai zetu ni ngao zetu. Bila siha, sisi silolote si chochote. Mtu huwa kama gogo tu. Ni wajibu wetu kuzingatia na kufanya yote tunayoweza ili kuhakikisha kuwa siha zetu hazituponyoki.
- Chagua maelezo sahihi kulingana na aya ya kwanza.
- Mwili wa mwanadamu haufanyi kazi yoyote bila afya.
- Afya ya mwanadamu ni jambo la nasibu.
- Afya huusaidia mwili kuendesha shughuli ipasavyo.
- Mwili wa mwanadamu unapochakaa madhara ya afya nzuri hujulikana.
- Kwa nini vyakula visipoivishwa vizuri huleta hasara?
- Vyakula hivyo hukosa virutubishi.
- Vyakula hivi haviwezi kutafunika.
- Mwili hushindwa kuondoa vyakula hivi.
- Husababisha shida za afya na kuleta aibu.
- Ulaji mzuri ni ule wa
- kutumia vipimo vidogo vya chakula.
- kutumia kipimo kikubwa cha vyakula.
- kutumia kipimo kifaacho cha chakula.
- kutumia kipimo chochote cha chakula.
- Kuhusu vyakula vya mafuta, mwandishi wa makala haya anapendekeza kuwa,
- wanaotumia mafuta mengi wafanye mazoezi.
- watu wasitumie mafuta katika vyakula.
- vyakula vyenye mafuta vitumiwe na watu wenye miili midogo.
- viliwe kwa wingi ili kuimarisha afya ipasavyo.
- Kwa baadhi, kunawa in kaida tu'kauli hii ina maana gani?
- Watu wote hunawa vizuri kabla ya kula.
- Wengine hunawa kimazoca tu bila kuwa makini.
- Wengine hunawa kwa kulazimishwa tu.
- Wao hunawa kwa njia ifaayo wakati wote.
- Mdudu anayeambukiza ucle wa malale huitwaje?
- Mbungo
- Mbu
- Parare
- Funza
- Sigara huwa na madhara yapi?
- Kuwaathiri hata walio mbali sana na mvutaji.
- Humwathiri mvutaji peke yake.
- Huwaathiri wengine badala ya mvutaji.
- Humwathiri mvutaji na walio karibu naye.
- Watu hununua baiskeli kwa sababu.
- kuimarisha afya zao.
- kufika kazini haraka.
- kuwabebea jamaa zao.
- kumaliza nguvu yao.
- Kulingana na aya ya mwisho.
- mtu asipokuwa na afya hugeuka kuwa gogo.
- afya ni silaha ya kujikinga na maadui.
- ni vyema kuzingatia njia mbalimbali za kuboresha afya.
- ni vizuri watu wanene watembee kuimarisha afya.
- Maana ya neno "huurutubisha' jinsi lilivyotumika ni
- huunenenpesha
- huustawisha
- huudhalilisha
- huutia mbolea
Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali kuanzia 41 mpaku 50
Juma alipiga goti huku machozi yakimdondoka njia nne nne. Mbele yake palikuwa na makaburi mawili. Waliokuwa wamelala mle hawakuwa na habari juu ya kihoro na simanzi ya aliyepiga magoti pule. Iala kwanza lilikuwa kongwe kiasi na lilikuwa limemca vichuka na magugu. La pili likionyesha upya kwani mashadu ya maua yaliyowekwa na wuombolezaji yalikuwa bado mabichi. Babake na mamake Juma walikuwa wamelazwa makaburini humu mtawalia.
Kwa Juma, maisha hayakuwa na maana tena. Alikuwa mwanafunzi wa miaka kumi na miwili na alikuwa katika darasa la saba. Hakuwa amchitimu kujitegemea na kukimu mahitaji yake. Aliokuwa akiwategemea sasa wamemwacha akiwa yatima. Hakuna yeyote ambaye ungelijaza pengo lililo achwu mu wavyelo wake. Zaidi ya haya alisononeka kuwapoteza wazazi wote wawili kwa kipindi cha miaka miwili tu. Ilaya yalikuwa kwake kama dondandugu lisilopona.
Kwa sasa Juma anayakumbuka mengi. Anakumbuka maisha ya babake. Alikuwajibaba zito na lenye sura jamala na siha nzuri. Baba mtu alikuwa na chake na alijiweza kiuchumi. Wengi pale mjini walimheshimu na kumstahi kutokana na uwezo wake huo. Aidha, alitunza familia yake vilivyo. Juma bakumbuki hata siku moja aliyokosu chochote alichohitaji kutoka kwa babake. Alikuwa mwenye bidii kazini mwake pia.
Walakini kama mja asiyckamilika, baba mtu alikuwa na taksiri moja. Aliyapenda maisha ya anusa na kufukuzia wasichana wadogo mlc mjini. Mamake Juma aliyajua fika haya. Alijaribu kuzozana ntuye ili aache tabia hii potovu. Lakini kila alipothubutu, mama mtu alifokewa na kukemewa kuwa anche upuuri wa wanawako. Akafika kufyata ulimi na kumwachia Molu uyaongoze maisha ya mumewe.
Hata hivyo, hakuna marcfu yasiyo na kikomo. Baada ya kuponda raha na vimanda si haba alianza kuugua. Maradhi yake yakawa na msururu. Mara alipata mafua yasiyopona, mara kucndesha mara maradhi ya ngozi. Haya yalimtia wasiwasi. Baada ya kukaguliwa na matabibu kadhaa alipatikana kuwa "ameumwa na mdudu" Hakuyaamini haya. Baba aliyekuwa na bushasha na mcheshi aliingiwa na upweke! na kutotaka kutangamana na yeyote hata jamaa yake.
Waliosema kuwa hakuna msiba usiokuwa na mwenzake hawakutupaka mafuta kwa mgongo wa chupa. Maradhi haya yaliifilisi jamaa huku aing ang'aniwa kupata tiba. Wakaenda kwa waganga na waganguri, Waganga nao wakafidi tamu.
Muda si muda, mama naye akaanza kuugua. Baada ya uchunguzi akapatikana na ugonjwa sawa na wa bwanake. Ikawa ni kama mji umcrogwa. Baadaye babaye akaaga dunia na mamaye hakukawia sana. Akasalimu amri na kumfuta mumewe. Juma, kijana mdogo akaachwa na upweke.
Kama kawaida, mja hakosi neno. Wengi walisikika wakisema hili na lile kuhusu vifo hivi. Wengine walionera minong'ono lakini Juma alijua ukweli wa vifo vya wazazi wake
- Juma alipiga goti kwa sababu ya.
- makaburi yaliyokuwa yamemea vichaka.
- wazazi wale walikuwa makaburini,
- huzuni ya kufiwa na wazazi wote.
- kuweko kwa makaburi mawili,
- Ni kweli kuwa,
- mama alitangulia kufariki.
- baba alitangulia kufariki.
- wazazi walifariki wakati mmoja.
- baba na mama walifariki baada ya mwaka.
- "Babake Juma aliheshimiwa kwa kuwa,
- alikuwa mwenye sura ya kuvutia.
- aliturva familia yake vilivyo.
- alikuwa tajiri wa kutajika.
- alikuwa mwenye bidii kazini.
- Neno jingine lenye maana sawa na taksiri
- dosari
- huzuni
- raha
- fujo
- Chagua sifa za babake Juma kulingana na kifungu
- mpenda raha, asiyejali familia yake.
- mwenye mali, anayejali maslahi ya wote.
- mwenye sura nzuri, asiyewajibika kazini.
- mpenda anasa, anayelunza aila yake.
- Baba Juma alimfokea mkewe kwa kuwa,
- mke alikuwa akifuata uvumi.
- mke alikuwa ukimwambia ukweli.
- mke alikuwa akimfuatafuata mjini.
- mke alitaka ushauri kutoka kwake.
- Maana ya kifungu ameumwa na dudu ni
- Aliambukizwa maradhi ya UKIMWI,
- Aliambukizwa maradhi ya kuendesha.
- Alifikiwa na wadudu ambao walimwuma.
- Alichokoza wadudu akapata maradhi
- Methali "Hakuna msiba usiokuwa na mwenzake inamaanisha,
- kumliwaza mgonjwa kulileta huzuni
- familia ya mhusika iliambukizwa maradhi ya baba.
- kuugua kwa mama kulimletea baba huzuni.
- ugonjwa wa mzazi ulifuatwa na matatizo mengine
- Maelezo yapi si sahihi kulingana na kifungu?
- Juma hakuelewa chanzo cha vifo vya wazazi.
- Majirani walijua chanzo cha vifo vya wazazi
- Mgonjwa alipotibiwa hakupata nafuu.
- Baba alipofariki mama hakuishi muda mrefu.
- Funzo la kifungu hiki ni kutva.
- Kufuata starehe sana hakuna mwisho mwema.
- Mara nyingi UKIMWI huambukizwa wale wanaojitunza vyema.
- Kubaki yatima kulimfanya Juma awajali wazazi
- Kuambukizwa maradhi huileta familia pamoja.
INSHA
Umepewa dakika 40 kuandika insha yako. Andika insha ya maelezo kuhusu.
MADHARA YA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA
....................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................
MARKING SCHEME
Kiswahili Activities Questions and Answers - Grade 4 Opener Exam Term 1 2022
KISWAHILI ACTIVITIES
Maswali
SEHEMU YA 1:
- Kusikiliza na kuzungumza
Sema umuhimu wa vifa hivi - Taja miezi mitatu ya mwaka,
- Eleza umuhimu wa mazingira
SEHEMU YA 2:
- Kusoma
Halima ni mwanafunzi mzuri. Nyumbani kwao wana duka kubwa sana. Humo dukani wao huuza sukari, mikate, unga na mafuta. Jana kaka alinunua kilo tano za sukari na mikate mitatu. Alimpea muuzaji pesa kisha akaenda.
Alipofika nyumabni, mama alimuuliza, "mbona hukununua mafuta?" Kaka alisema mafuta yaliuzwa kwa bei ghali sana. Halima alitwambia kuwa duka lao huwapatia faida nyingi sana. - Kusoma ufahamu
Twiga hupatikana katika maeneo ya kusini mwa Afrika, pamoja na Afrika mashariki-Kenya, Uganda na Tanzania. Ndiye mnyama mrefu zaidi duniani. Urefu wake ni kati ya mita nne nukta tatu na mita tano nukta nane. Uzito wa twiga na kilo mia nane na elfu moja, mia mbili na hamsini. Aliye na uzito wa juu ni wa kiume.
Twiga ana maisha ya takribani miaka ishirini na mitano. Chakula chake ni nyasi na majani ambayo huyafikia kwa shingo lake ndefu sana. Ulimi wa twiga unafikia urefu wa centimita arobaini na tano.
Mtoto wa twiga azaliwapo ni mrefu kuliko mwanadamu aliyekomaa. Mtoto huyo anaweza kusimama baada ya dakika kumi. Baada ya saa kumi anaweza kukimbia kando ya wazazi wake.
twiga ndiye alalaye kwa muda mfupi zaidi, kati ya dakika kumi na saa mbili kwa usiku. Twiga ana uwezo wa kulala huku akisimama. Yeye ni kivutio kwa watalii.- Taarifa hii inahusu mnyama gani?
- Taja eneo moja ambayo twiga hupatikana
- Kati ya twiga wa kiume na wa kike, nani ana uzito wa juu?
- Ulimi wa twiga unafikia urefu wa centimita ngapi?
Andika kweli au la - Twiga ana uwezo wa kulala huku akiwa amesimama
SEHEMU YA 3
Sarufi
Jaza "juu ya" au "chini ya"
-
Paka ako _____________ meza. -
Mpira uko _____________ kiti.
Mtoto amelala _____________ kitanda
Jaza 'Huyu' au 'Hawa'- _____________ ni wanaume
- _____________ walimu wananipenda
SEHEMU YA 4
KUANDIKA
Andika insha juu ya:
MNYAMA NIMPENDAYE
Mwongozo wa Kusahihisha
SEHEMU YA 1
- Mwanafunzi anapaswa kutaja umuhimu wa kila kifaa kilichoonyeshwa
- Mwanafunzi anapaswa kutaja miezi yoyote tatu
- Mwanafunzi anapswa kutaja umuhimu wa mazingira
SEHEMU YA 2
- Kusoma ufahamu- Mwanafunzi anapaswa kusoma hadithi vyema
- Kusoma ufahamu
- twiga
- kusini mwa afrika na afrika mashariki
- twiga wa kiume
- centimita arobaini na tano
- Kweli
SEHEMU YA 3
- chini
- juu
- juu
- Hawa
- Hawa
SEHEMU YA 4
Mwanafunzi anapaswa kuandika insha juu ya mada aliyopewa.
Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Opener Exams Term 1 2022
Maswali
Chagua jibu sahihi ujazie nafasi wazi
Baada ya siku 1 kupita, wakaona kisiwa 2 mbali, wakakusudia kwenda 3 . Walipokaribia , wakaona 4 moja zuri lakini hakukuwa na 5 yoyote ya watu,wanyama 6 ndege. Miti na majani yalikuwa kama yamelala. 7 nanga, wakashuka kisiwani na wakaingia 8 . Kila 9 , waliona watu wamelala bila 10 yoyote;walistaajabu mno. Wakapanda juu ya 11 jumba , wakaingia 12 chumba , wakaona mambo ni 13 tu. Wakaja hata 14 chumba cha yule mlezi 15 wakazidi kustaajabu.
A | B | C | D | |
1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 |
mingi na kuitazama jumba dalali au wakatua jumba walipopita ufahamu kile na ile ile katika nayo |
nyingi ya kutazama chumba dalili ila wakatoa jumbani waliopita kufahamu ule wa yale yale kwa naye |
mengi kwa kukitazama nyumba dhalili wala wakaweka kwa jumba walipita fahamu Ile cha hiyo hiyo na nao |
wengi kuwa Kupatazama vyumba adili na wakatia katika jumbani waliyepita hamu lile kwa yaya haya wa nacho |
Chagua jibu sahihi kutoka swali la 16-30
- Ni ipi sio maana ya kitawe shinda
- faulu
- kukaa kutwa
- isiyojaa
- tabu
- Magurudumu nikwa motokaa ilhali ________ ni kwa kitanda.
- matendeguu
- miguu
- matendegu
- maguu
- Kule mahakamani ,shahidi alitakikana atoe __________
- shada
- shahada
- ushuhuda
- ushahidi
- Mtoto ___________ alianguka vibaya sana.
- mwenye
- yeye
- mwenyewe
- enyewe
- Andika ukubwa wa
Mtoto wa ngo’mbe anaitwa ndama.- Jitoto la ngo’mbe linaitwa dama
- Toto la gombe linaitwa dama.
- Jitoto la gombe linaitwa ndama.
- Toto la ngo’mbe anaitwa ndama.
- Nyoka ______ ana meno ______
- yule , ndefu
- ile , marefu
- yule , marefu
- ule , refu
- Nini maana ya ‘Tulipeana’
- alinipea nami nikampea
- tulimpa akachukua
- nilimpa naye akanipea
- tuliwapa nao wakatupa
- Chagua sentensi sahihi
- Mtoto ambaye aliyefaulu amezawadiwa.
- Mtoto ambao alifaulu amezawadiwa.
- Mtoto aliyefaulu ametuzwa zawadi.
- Mtoto ambaye aliyefaulu amepewa zawadi.
- Watu wanapofiwa huwa wanaambiwa?
- alamsiki - binuru
- mpo - tupo
- poleni - asante
- makiwa - tunayo
- Kamilisha kwa usahihi
Msimwache mgonjwa _______- akufe
- afe
- aafe
- akakufe
- Mwindaji haramu wa wanyama pori huitwa _______
- jasusi
- jambazi
- jangili
- msasi
- Kama juzi ilikuwa ijumaa tarehe sita, mtondo itakuwa siku gani na tarehe ngapi?
- Jumatano tarehe kumi na moja
- Jumapili tarehe nane
- Ijumaa tarehe kumi na tatu
- Jumatano tarehe kumi
- Tumia –a unganifu kwa usahihi
Pua _______ mtoto inauma- la
- wa
- ya
- za
- Chagua sentensi iliyo katika wakati timilifu.
- aende shuleni
- hajaenda shuleni
- ataenda shuleni
- huenda shuleni
- Jaliza mwanya
Mahali hapa ______ uchafu mwingi.- nayo ina
- nako kuna
- napo kuna
- napo pana
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31 mpaka 40.
Naikumbuka siku hiyo vizuri. Niliamka alfajiri mbichi tayari kuanza safari kutoka kijijini mwetu hadi mji mkuu. Hii ndiyo iliyokuwa mara yangu ya kwanza kuuzuru mji huu. Moyoni nilikuwa na bashasha isiyokuwa ya kawaida kwa sababu siku hiyo ningeuona mji ambao sifa zake nilikuwa nikizisikia tu kutoka kwa wenzangu waliobahatika kuutembelea. Hamu ya kuona majengo marefu, barabara zilizosakifiwa, magari mengi, watu wa asili mbalimbali na mabustani ya starehe ilinigubika ikawa sijifai kwa matumaini.
Nilitembea hatua chache hadi kituo cha mabasi, nikapata daladala moja iliyotoza nauli nafuu, nikaiabiria mpaka mji uliokuwa pua na mdomo kutoka kitongojini mwetu. Hapo nilitumainia kupata matwana ya kusafiria hadi mji mkuu. Kwenye stesheni kulikuwa na msongarnano wa matwana na harakati za utingo waliokuwa waking’ang‘ania abiria. Nikaingia katika matwana moja iliyoitwa Upepo. Nilikuwa abiria wa kumi na wawili kuingia. Baada ya dakika tano hivi, gari lilijaa abiria,wote kumi na wanne. Tukang’oa nanga. Mandhari ya kupendeza yalijikunjua mbele yangu. Upepo mwanana kupitia dirishani,mpito wa kasi wa miti, mazigazi ....vyote vilishirikiana kunipumbaza kiasi cha kunisahaulisha kufunga mkanda wa usalama.
Baada ya robo saa utingo alidai nauli. Nikapeleka mkono kwa tahadhari kwenye kibindo changu ambamo nilikuwa nimezifutika hela za usafiri na masurufu. Nikatoa noti ya shilingi mia mbili na kumkabidhi utingo huku nikitarajia baki. Utingo alinikazia macho, akanyoosha mkono na kusema, “Mia mzaidi!“ Nikarudi tena kwenye kibindo, nikatoa noti mbili za shilingi hamsini na kumpa. Safari ikaendelea.
Tulipofika mji mdogo wa Pilia, matwana ilisimama. Utingo aliinama chini ya viti, akatoa vibao na kuviweka baina ya viti vya kawaida. Kisha akaanza kutangaza. “Wa Jiji na mia; mia hamsini”. Abiria walioonekana kuwa wachovu kwa kungojea na kupigwa na mzizimo wa kipupwe walipigana vikumbo kuingia huku utingo akiwaelekeza kwenye vile vibao. Viti vilivyotengenezewa abiria watatu vikaishia kubeba abiria watano. Matwana nayo ikawa haina budi kustahimili uzito wa abiria ishirini na watatu. Tukawa tunabanana kweli kweli. Utingo naye alining’inia mlangoni huku shati lake likipeperushwa na upepo. Nilipojaribu kulalamikia hali hii nilinyamazishwa hata na abiria wenzangu.
Gari Iikaanza mwendo tena huku likiendeshwa kwa kasi ya umeme. Abiria waliokuwa wakizungumza sasa walinyamaza kila mmoja roho i mkononi. Kimya cha kaburi kikatawala hadi pale utingo alipomwambia dereva. “Weka ngoma.“ Muziki ukahanikiza hewani kwa fujo. Baadhi ya abiria wakaanza kuyumbisha vichwa kwa kufuata mdundo wa muziki ambao ulitishia kuvipasua viwambo vya masikio yangu.
Njiani tulikutana na walinda usalama ambao walitusimamisha. Utingo alishuka na kwenda chemba na mmojawapo wa hao maafisa kisha akarudi huku kipaji chake kimenawiri kwa tabasamu. Akasema, “Nimempaka mafuta viganjani.” Baadhi ya abiria walitikisa vichwa, wengine wakacheka kama kwamba wameona kinyago. Mimi nilibaki kuduwaa tu. Gari liliongeza mwendo na baada ya muda mfupi tukafika kwenye mji mmoja ambao ulikuwa na majengo makubwa makubwa. Nikadhani tumefika mji mkuu. Nilipomuuliza abiria jirani aliniambia kuwa huu ulikuwa tu mji mkuu wa Jimbo la Buraha. Tukazidi kuyakunja rnasafa ya safari hii kwa kasi ya kuogofya huku dereva akitafuna majani aliyokuwa akiyatoa mfukoni mwa shati lake. Kadiri alivyoyatafima ndivyo alivyozidisha kasi. Nikahisi kama gari linapaa juu angani. Nikataka kumwambia dereva jambo, lakini nikajiambia, “Ikiwa wengine wamenyamaza sembuse mimi?“
Baada ya kitambo kidogo mvua ilianza kunyesha. Kukawa na ukungu na utelezi barabarani. Abiria mmoja alimsihi dereva kupunguza mwendo. Hayo hayakumgusa dereva mshipa. Aliongeza kasi kana kwamba hajasikia lolote. Gari Iilifika kwenye kuruba,dereva akawa haoni vizuri. Ghafla nikasikia, “Kirrr..!“ Kisha_“Mungu wangu!" Halafu, ‘ngu!'Kiza cha kaniki kikatanda.
Maswali:
- Kulingana na kifungu;
- Wenzake msimulizi waliwahi kupata fursa ya kuishi katika Mji Mkuu.
- Barabara za Mji Mkuu hazina mashimo.
- Mji Mkuu una majumba mengi marefu.
- Msimulizi ana mwao na hali ilivyo katika Mji Mkuu.
- Chagua jibu sahihi kuhusu vituo vya magari kwa mujibu wa aya ya pili:
- Wasafiri wengi kushindania nafasi
- Magari mengi kushindania wasafiri
- Misongamano mingi ya kungangania wasafari
- Shughuli nyingi za kungangania nafasi.
- Mazingira ya kuvutia yalimwathiri Msimulizi kwani:
- Aliduwaa na kujisahau.
- Alifurahia upepo na kujisahau.
- Alizubaa na kupuuza sheria za usafiri.
- Alipumbaa na kupinga sheria za usafiri.
- Msimulizi alikuwa amehifadhi pesa katika:
- Mfuko mdogo ndani ya suruali.
- Mfuko mdogo mbele ya suruali.
- Mfuko wa nguo iliyoshonwa kiunoni.
- Mkunjo wa nguo uliofingwa kiunoni.
- Katika mji wa Pitia abiria walipigana vikumbo kuingia garini kwa sababu:
- Kulikuwa na uhaba wa magari.
- Kulikuwa na uhaba wa viti.
- Walikuwa wamechoka kungojea matwana
- Walikuwa wamepigwa na baridi na mvua.
- Kulingana na kifungu ajali barabarani husababishwa na:
- ukosefu wa magari, kubeba abiria wengi.
- kiburi cha madereva. kutozingatia maelekezo barabarani.
- ukosefu wa mikanda ya usalarna, madereva kutowajibika.
- muziki wa kupasua viwambo madereva kutoona vizuri.
- Msimulizi ni mkakamavu kwa vile:
- Alishutumu hali ya gari kubeba abiria kuliko kiasi.
- Alishutumu hali ya shati na utingo kuning‘inia nje.
- Alinyarnaza alipoona dereva akikaribia kuruba kwa kasi.
- Alinyamaza alipoona utingo akienda chemba na afisa.
- Chagua jibu lisilo sahihi kulingana na kifungu:
- Abiria wengine waliufurahia muziki garini.
- Ufisadi unaweza kusababisha ajali barabarani.
- Abiria wanaweza kuzuia ajali barabarani.
- Kuruba ndiyo iliyosababisha ajali garini.
- Ni mfuatano upi wa matukio ufaao kwa mujibu wa kifungu?
- Kucheza muziki, kukutana na polisi, kufikia kuruba, mvua kunyesha, kupata ajali
- Kukutana na polisi, kuhonga, kucheza muziki, kufikia kuruba, kupata ajali
- Kucheza muziki, kukutana na polisi, kuhonga, kufikia kuruba, kupata ajali.
- Kukutana na polisi, gari kupaa juu, mvua kunyesha, kufikia kuruba, kupata ajali.
- 'Kiza cha kaniki kilitanda’ kulingana na kifungu ina maana:
- Msimulizi akapoteza fahamu.
- Msimuiizi akapoteza uwezo wa kuona.
- Kukawa na weusi mkubwa.
- Kukawa na giza totoro.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41 mpaka 50.
Tenga alilelewa katika mazingira yaliyojaa neema, furaha na uchangamfu. Wazazi wake Bwana Mtanga na Bi. Zuhura waiikuwa wakwasi wa kutajika katika janibu hizo, si kwa mali tu bali kwa nyoyo zao zilizokuwa tayari kila mara kuwakirimu wanakijiji kwa lolote.
Bwana Mtanga na Bi. Zuhura hawakuiala maskini wakaamka matajiri. Mtanga alianza kazi kama tarishi katika Makavazi ya Umma. lngawa hii ilikuwa kazi ya kijungu jiko . Mtanga hakwenda nguu: alijitahidi kwa vyovyote vile kujinyanyua. Akajisajili kwa kozi mbalimbali za usimamizi wa makavazi na kuhilimu vyeti tofautitofauti vikiwemo stashahada na shahada katika masuala ya usimamizi wa mashirika ya umma. Jitihada zake zikazaa matunda. Akapandishwa cheo mwaka baada ya mwingine hadi akawa msimamizi wa Makavazi ya Umma. Baadaye akaajiriwa na shirika la Msalaba Mwekundu kama Mkrurugenzi wa Huduma za Kijamii.
Bi. Zuhura naye baada ya kuhitimu masomo ya shule ya upili,alisomea taaluma ya ukutubi na baadaye kuajiriwa katika maktaba ya chuo kikuu cha Tungama. Hapa Zuhura alitambua kuwa amepata nafusi adimu ya kutia makali ubongo wake. Akajisajili kwa kozi ya ukutubi na kuhitimu shahada ya daraja la kwanza katika taaluma hii. Wakuu wake kazini wakavutiwa na juhudi zake na kumpandisha cheo akawa Mkutubi Mkuu.
Wakati Bwana Mtanga na Bi. Zuhura walipokuwa wakijiendeleza kitaaluma na kiuchumi,Tenga naye alikuwa anajikalia tu kama uyoga bila mpalilizi. Nyadhifa za wazazi wake zilimpokonya Tenga ushirika wa wazazi wake. Ile michezo yake na wazazi wake kabla ya chajio, yale matembezi ya kila Jumapili yote yakatoweka. Baba na mama wakawa wanarudi nyumbani baada ya saa nne usiku wakiwa wametoka kwenye masomo ya kuupigia msasa ujuzi wao; Jumamosi na Jumapili wana majadiliano na wanafunzi wenzao. Nyakati nyingine wazazi wote wawili walikuwa kwenye safari za kikazi. Nyakati kama hizi Tenga angepelekwa kwa shangazi ambako angekaa na kijakazi wake kwa wiki tatu; anaenda shuleni na kurudi huko huko kwa shangazi.
Wahenga walisema kwamba, akosaye la mama hata la mbwa huamwa. Pengo la malezi lililoachwa na wazazi wa Tenga Iilijazwa na walezi wengine wakiwemo vijakazi , shangazi, marika,walimu,majirani na hata vibonzo. Tenga alijifunza mengi kutokana na walezi hawa. Alifunzwa namna ya kupigana miereka kutumia ujanja kujitoa katika matatizo,kutumia maneno makali,kujihami alipochokozwa na wenzake, pamoja na mitindo mbalimbali ya kujinadhifisha. Mafunzo ambayo Tenga aliyapata hasa kutoka kwa marika yaliutia ila mwenendo na uhusiano wake na walimu. Darasani akawa anaishi kuvuruga masomo kwani kila mara angetenda kituko ili mwalimu na wanafumi waubaini uwepo wake. Vituko hivi vilisababisha kudorora kwa alama zake. Walimu wakajaribu kuurekebisha utundu wake lakini zikawa kama juhudi za mfa-maji. Tabia ya Tenga haikuwa ufa tena bali ukuta ambao ulihitaji kujengwa upya. Mkuu wa Idara ya Ushauri na Uelekezaji shuleni ilibidi ahusishwe. Akamhoji Tenga na kupambaukiwa kuwa vitendo vya Tenga vilikuwa na asili ambayo ilihitaji kuchunguzwa. Akampendekezea mwalimu wa darasa kuwashirikisha wazazi kalika kutafuta mbinu za kumwelekeza Tenga zaidi.
Bwana Mtanga na mkewe Zuhura walipoambiwa kuhusu hali ya Tenga walipigwa nu bumbuazi. Hawakuwa wameyawazia madhara ya kutoshiriki kikamilifu katika malezi ya mtoto wao. Mwalimu aliwaambia ya kwamba nusura Tenga ajiingize na wenzake katika matumizi ya dawa za kulevya Iakini akakataa na kusema kuwa hata babake hakujaribu kutumia kitu chochote. Wazazi waliona haya na kujilaumu. Hata hivyo walishukuru ya kwamba walimu waliyagundua matatizo haya kabla hayajaiangziniiza familia yao.
Chagua jibu sahihi kwa mujibu wa kifungu.
- Bwana Mtanga na Bi. Zuhura:
- walimlea Tenga kwa kushauriana, walikuwa mashuhuri;
- walimlea Tenga kwa kuchangamkiana, walikuwa maarufu
- waliingiliana vyema na majirani, walipenda kusaidia
- waliingiliana vyema na walimu, walipenda kutoa.
- Utajiri wa wazazi wa Tenga ulitokana na:
- uwajibikaji wao katika shughuli zao
- kupata vyeo katika madaraja tofautitofauti
- kupata shahada na stashahada mbalimbali
- uwajibikaji wao katika taaluma zao
- Wazo kuu linalojitokeza katika aya ya nne ni kwamba:
- Jambo Iolote likifanywa bila ushirikiano huleta madhara
- Jambo lolote likifanywa bila kipimo huweza kuleta madhara
- Jambo lolole likifanywa bila utulivu huweza kuleta madhara
- Jambo lolote likifanywa bila mtazamo huweza kuleta madhara
- Kifungu kinaonyesha kuwa ukosefu wa malezi bora husababisha:
- kupigana miereka daima ili kupata maslahi
- kudhoofika kwa maadili
- kuharibu masomo darasani ili kuonekana kote
- kuharibika kwa urafiki
- "Tabia ya tenga haikuwa ufa bali ukuta abao ulihitaji kujengwa upya" ina maana;
- Tabia ya tenga ilikuwa imeharibika kabisa kiasi cha kuhitaji kurekebishwa kikamilifu
- Tabia ya tenga ilikuwa imeharibika kabisa kiasi cha kuhitaji kushauriwa kikamilifu
- tabia ya Tenga ilihitaji kushughulikiwa kikamilifu
- tabia ya Tenga ilihitaji kutambuliwa kikamilifu
- Kwa mujibu wa kifungu. Idara ya Ushauri ya Uelekezaji inasaidia katika malezi kw
- kuwahoji vijana na kuwaita wazazi wao
- kutambua matatizo ya vijana na kuonyesha mbinu za kuwashirikisha
- kutambua matatizo ya vijana na kuangazia mbinu za kuyasuluhisha
- kuwahoji vijana na kuwaambia matatizo yao
- Kulingana na aya ya mwisho, wazazi wa Tenga
- hawakujua umuhumi wa kukaa karibu na watoto wao
- walipuuza umuhimu wa ushirika wa karibu wa walezi wao
- walipuuza umuhimu wa ushirika wa karibu na mtoto wao
- hawakujua umuhimu wa kukaa karibu na walezi wao
- Chagua jibu lipi linaloonyesha sifa za Tenga.
- mcheshi, mwenye kupenda wazazi
- mwenye mapenzi ya dhati anayelafuta kushirikishwa
- mchangamfu mwenye kupenda unadhifu
- mwenye msimamo imara, anayetafuta kutambuliwa
- Kisawe cha, ‘hakwenda nguu.’ ni:
- hakujitia kapuni
- hakujitia hamnazo
- hakufa moyo
- hakufa kikondoo
- Maana ya, ‘kujihami' kwa mujibu wa kifungu ni:
- kujitetea
- kujinasua
- kujihadhari
- kujizatiti
Majibu
- B
- C
- C
- A
- B
- A
- D
- B
- A
- C
- D
- D
- B
- A
- C
- D
- C
- D
- C
- B
- C
- D
- C
- D
- B
- C
- A
- C
- B
- D
- D
- B
- C
- D
- A
- B
- A
- D
- C
- A
- C
- D
- B
- B
- A
- C
- C
- D
- C
- A
Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 End of Term 3 Exams Set 2
MASWALI
- KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA (Alama 5)
- Tunga sentensi ukitumia vitanzandimi vifuatavyo.(alama 2)
- Kasa _______________________________________________________________
- Kaza _______________________________________________________________
- Saa ________________________________________________________________
- Zaa _________________________________________________________________
- Tegua kitendawili kifuatacho (alama 1)
Bak bandika bak bandua ________________________________________________________ - Kamilisha methali zifuatazo (alama 2)
- Mtaka cha mvunguni ______________________________________________
- Chanda chema __________________________________________________
- Tunga sentensi ukitumia vitanzandimi vifuatavyo.(alama 2)
- UFAHAMU (Alama 10)
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Mlolongo wa magari matano ulikuwa ukipita kwa utaratibu ambapo kando ya barabara, watu waliyatazama magari hayo kwa makini mno kutokana na jinsi yalivyopambwa kwa maua kochokocho.
Miongoni mwa wale waliojipanga barabarani kuyashuhudia hayo, alikuwa kijana Abdala. Ilikuwa ni siku ya Jumamosi alasiri. Gari la kwanza ambalo lilikuwa limepambwa zaidi, liliwabeba bwana na bi arusi.- Ni magari mangapi yaliyotajwa katika kifungu hiki? _____________________________________(alama 1)
- Watu walitazama magari wakiwa wapi?____________________________________________ (alama 1)
- Ni nini kilichovutia macho ya watazamaji? ___________________________________________(alama 1)
- Taja mhusika mmoja kati ya walioshuhudia magari hayo __________________________________________(alama 1)
- Eleza maana ya neno alasiri ____________________________________________ (alama 1)
- Tukio hili lilifanyika siku gani?__________________________________________________(alama 1)
- Gari la kwanza lilibeba akina nani? _______________________________________(alama 1)
- Eleza aina ya nomino zifuatazo kama zilivyotumika katika kifungu hiki (alama 3)
- Mlolongo wa magari
- Jumamosi
- Gari
- SARUFI (Alama 20).
Jibu kulingana na maagizo- Andika wingi wa sentensi hizi. (alama 2)
- Mji ulio karibu na kwetu ni huu
_____________________________________________________________ - Duka langu lina bidhaa nyingi
_____________________________________________________________
- Mji ulio karibu na kwetu ni huu
- Majira ya baridi kali huitwaje? __________________________________________________(alama 1)
- Jibu la lala salama ni ___________________________________________(alama 1)
- Taja mapambo mawili yanayovaliwa kichwani (alama 2)
- ___________________________________________________
- ___________________________________________________
- Tambua nomino za makundi katika sentensi zifuatazo (alama 2)
- Dobi aliosha tita la nguo chafu ______________________________________
- Genge la wezi lilivamia mzee Busara ___________________________________________
- Neno 'meza' liko katika ngeli gani? ________________________________________ (alama 1)
- Tumia viambishi sahihi (alama 3)
- Waraka huo _____________ likuwa mrefu
- Ukurasa wa kitabu ________________ na picha.
- Unywele _________________ mekatwa.
- Taja visawe vya maneno yafuatayo. (alama 3)
- barabara _________________________________
- hongo _______________________________________
- mgonjwa _____________________________________
- Nyambua vitenzi hivi katika kauli ya kutendewa na kutendeka (alama 5)
Kitenzi Kutendewa Kutendeka (i) Jenga
(ii) Tega
(ii) Imba
(iv) Shika
(v) Ita
- Andika wingi wa sentensi hizi. (alama 2)
- Kuandika
Andika insha ya kusisismua kuhusu kichwa kifuatacho ( Alama 10)
SOMO NILIPENDALO
__________________________________________________________________________________________________
__________________________________________________________________________________________________
__________________________________________________________________________________________________
__________________________________________________________________________________________________
__________________________________________________________________________________________________
__________________________________________________________________________________________________
__________________________________________________________________________________________________
__________________________________________________________________________________________________
__________________________________________________________________________________________________
__________________________________________________________________________________________________
__________________________________________________________________________________________________
__________________________________________________________________________________________________
__________________________________________________________________________________________________
__________________________________________________________________________________________________
__________________________________________________________________________________________________
__________________________________________________________________________________________________
__________________________________________________________________________________________________
__________________________________________________________________________________________________
__________________________________________________________________________________________________
__________________________________________________________________________________________________
_________________________________________________________________________________________________
__________________________________________________________________________________________________
__________________________________________________________________________________________________
__________________________________________________________________________________________________
MARKING SCHEME
-
- Kusikiliza na kuzungumza
Sahihisha kulingana na majibu ya mwanafunzi - nyayo
-
- sharti ainame
- huvikwa pete
- Kusikiliza na kuzungumza
- Ufahamu
- matano
- kando ya barabara
- jinsi yalivyopambwa kwa maua kochokocho
- Abdala
- wakati kati ya saa tisa mchana na jua linapotua.
- Jumamosi
- Bi an Bwana arusi
-
- nomino ya makundi
- nomino ya kipekee
- nomino ya kawaida
- Sarufi
-
- miji iliyo karibu na kwetu ni hii
- maduka yetu yana bidhaa nyingi
- kipupwe
- pia nawe
-
- Taji
- Shela
-
- Tita la nguo
- Genge la wezi
- I - Zi
-
- u
- u
- u
-
- baraste
- kadhongo
- mwele
-
Kitenzi Kutendewa Kutendeka (i) Jenga
(ii) Tega
(ii) Imba
(iv) Shika
(v) Itajengewa
tegewa
imbiwa
shikiwa
itiwajengeka
tegeka
imbika
shikika
itika
-
- Kuandika
Kiswahili Questions and Answers - Class 7 End Term 3 Exam 2022 Set 2
MASWALI
Soma kifungu hiki na ujalize nafasi 1-15
Nilikaa __1__ na __2__ maswali __3__ sana. Pamoja na maswali __4__, nilishangaa ni kwa nini mara __5__ watu __6__ kukitumia Kiswahili shaghalabaghala __7__ ya kutumia Kiswahili aula? Ukweli __8__ jambo __9__ ni __10__ wanadamu wengi hawako tayari kujishughulisha katika kufanya utafiti na __11__ hawana __12__ kwamba utafiti __13__msingi wa kupata ukweli na uhakika wa kitu au jambo __14__. Kiswahili bora hakipatikani __15__ bila kujifunza kwa makini na kwa dhati.
-
- Chali
- kufudifudi
- kingalingali
- kitako
-
- Kujiuliza
- kuuliza
- kumwuliza
- kuliuliza
-
- nyingi
- mengi
- mingi
- vingi
-
- hayo
- hiyo
- hizo
- hivyo
-
- mingi
- nyingi
- mengi
- vingi
-
- wanaitakia
- wanakubali
- wanakubalishwa
- wanaitishwa
-
- badala
- wala
- vile
- baada
-
- ya
- wa
- la
- za
-
- hili
- huu
- hii
- hiki
-
- kua
- kuua
- kwa
- kuwa
-
- ila
- wala
- wale
- bila
-
- habari
- bahari
- bohari
- heri
-
- ndiye
- ndiko
- ndio
- ndivyo
-
- yoyote
- zozote
- lolote
- wowote
-
- hivi vivi
- vivi hivi
- vivyo hivyo
- hivyo hivyo
kutoka swali la 16 mpaka 30, chagua jibu sahihi kulingana na maagizo.
- Udogo wa neno njia ni ___
- Kinjia
- jia
- kijia
- kijijia
- Tambua kihusishi katika sentensi ifuatayo
Nyoka hatari alimuuma mbuzi aliyelala chini ya miti.- chini ya
- mbuzi
- hatari
- alimuuma
- Taja ngeli ya neno ‘uongozi’
- U-U
- A-WA
- U-YA
- U-ZI
- Tumia kauli ya kutendesha kukamilisha sentensi ifuatayo.
Halima alim___ mgeni wake kabla ya kula.- nawisha
- navya
- nawa
- nawiza
- konokono no kwa kombe kama vile buibui ni kwa ___
- kizimba
- utando
- sega
- kifukofuko
- Chagua wingi wa sentensi hii
Moyo wangu ulidunda nilipokuona- Mioyo yetu ilidunda nilipomwona
- Mioyo yetu ilidunda tulipomwona
- Nyoyo zetu zilidunda nilipomwona
- Nyoyo zetu zilidunda tulipowaona
- Neno ‘chuku’ lina sauti ngapi.
- 2
- 5
- 4
- 3
- Ni tamathali gani yam semi hutumia ulinganisho wa moja kwa moja bila kutumia sifa?
- Istiara
- tashbihi
- nahau
- methali
- Tegua kitendawili kifuatacho.
Kisima changu hakitindiki maji.- Kinywa
- shimo
- moto
- mamba
- Asilimia Ishirini na tano ni saw na:
- Sudusi
- Robo
- humusi
- ushuri
- Chagua sentensi yenye kiambishi –po- cha wakati.
- Uwele ulipomshika alitibiwa kwa haraka
- Painamapo ndipo painukapo
- Anapofanyia kazi ni pazuri
- Walipohamia pana usalama wa kutosha
- Baini sha usemi taarifa.
“Kesho uje na mzazi,”mwalimu mkuu alimwambia rukia.- Rukia aliambiwa na mwalimu mkuu aende kesho
- Mwalimu mkuu alitaka Rukia aende na mzazi siku hiyo
- Mwalimu mkuu alimwambia rukia uje na mzazi kesho.
- Mwalimu mkuu alimwambia Rukia aende na mzazi siku iliyofuata
- Kanusha
Mtoto ambaye Analia amepigwa- Mtoto ambaye Analia hajapigwa
- Mtoto ambaye halii hajapigwa
- Mtoto ambaye Analia hakupigwa
- Mtoto ambaye halii hakupigwa
- Chagua neno baki
- Muhibu
- Saibu
- Masena
- Mwandani
- Tambua methali isiyowiana na uliyopewa “Haba nah aba hujaza kibaba”
- Tembe na Tembe huwa mkate .
- Tone na tone huwa mchirizi
- Chovya chovya humaliza buyu la asali
- Hayajai hayajai kumbe yanajaa
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali 31-40.
Dawa za kulevya ni kitu chochote kinachoathiri hali ya kawaida ya mwili wa binadamu. Dawa hizi pia hutimiwa kwa njia tofauti sawa na madhara yake yalivyo. Dawa hizi ni kama vile: bangi, madraksi, heroini na pombe. Sigara, gundi na chang’aa ni vileo vinavyoouzwa na watu wengi na kupatikana kwa urahizi.
Sababu za kutumia mihadarati ni tofauti kulingana na watu walivyo tofauti. Wengine hutaka kudadisi dawa hizi au kuiga tabia za wengine. Wengine hutumia kwa kuathiriwa na vyombo vya mawasiliano kama runinga na upotovu wa jamii.
Dawa hizi zikitumiwa kwa muda mrefu husababisha uzoefu ambao ni mgumu kuacha. Vilevile zina madhara maridhawa kama vile kukosa makini masomoni, kukosa utaratibu wa kufanya mambo na kuwa kichaa. Uvutaji wa wa sigara na bangi husababisha saratani ya mapafu. Baadhi ya dawa hizi ni ghali mno na husababisha umasikini.
Wengine nao hujipata katika matukio ya kutisha. Kutokana na uzoefu na gharama yake wengi hutumia sirinji moja kujidunga. Katika harakati hizo wengine huambukizwa uwelehatari wa ukimwi. Hatima ya waja hawa ni kuifuata njia ya marahaba. Akina mama wajawazito hujipalia makaa katika vichwa vyao wanapohusika katika uraibu huu. Dawa hizo huathiri watoto ambao hawajazaliwa. Yafaa sote tuupinge ulanguzi kwa vyovyote vile.
- Dawa za kulevya ni ________
- Vitu vyovyote vya aina mbalimbali
- Chochote kinachoathiri binadamu
- Chochote kisichopendekezwa na daktari
- Chochote kinachotumiwa na kuathiri hali ya mwili wa binadamu.
- Madhara ya dawa za kulevya ni ___
- Sawa
- Tofauti na watu
- Tofauti kulingana na dawa
- Sawa kwa wote.
- Dawa zinazotumiwa sana na wengi ni ___
- Madraksi, sigareti na kokeini
- Madra, chang’aa na sigareti
- Chang’aa, sigara na gundi
- Gundi, chang’aa na kokeini.
- Taja kisawe cha dawa za kulevya.
- Madraksi
- Mihadarati
- Hadharani
- Dawa
- Kufuata njia ya marahaba ni ___
- Kufaulu katika maisha
- Kujibu salamu za ‘shikamoo’
- Kuwa maskini
- Kuaga dunia
- Ni ipi kati ya sababu hizi haiwafanyi watu kutumia mihadarati?
- Kuathiriwa na vyombo vya habari
- Kufanya udadisi
- Upotovu wa jamii
- Uchumi wa nchi
- Saratani ya mapafu husababishwa na ___
- Sigara
- Madraksi
- Kokeini
- Chang’aa
- Kutokana na taarifa hii ni kweli kusema __
- Kuna dawa ambazo hudungwa mwilini
- Dawa zote huvutwa
- Sigara huvutwa na kila mmoja
- Dawa za kulevya hupatikana kwa urahisi na kwa bei ya chini.
- Dawa za kulevya zikitumiwa na wajawazito____
- Huathiri udhaifu mwilini
- Huathiri watoto ambao hawajazaliwa
- Huwa wenda wazimu
- Huwama haraka.
- Kichwa kifaacho habari hii ni ___
- Faida za dawa za kulevya
- Chang’aa, pombe na kokeini
- Dawa za kulevya
- Tabia mbaya.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41-50
Baada ya mateso ya muda mrefu kwenye mikono ya mwajiri katili, subira alinyanyuliwa na maafisa wa serikali waliosimamia haki za watoto. Mwajiri wake alijikuta mashakani alipopatikana akimtesa. Siku hiyo kweli ilikuwa ya afua kwa subira Mwajiri wake alitiwa mbaroni.
Subira alipelekwa shuleni aendelee na masomo yake. Kweli liandikwalo na Mungu lazima liwe, naye subira alisoma hadi kilele cha masomo hata ingawa alikuwa maskini hohehahe. Kutokana na misaada ya watu mbalimbali, alihitimu masomo yake ya shule ya upili na kupita vilivyo. Alikwenda chuoni kusomea ukandawala na baada ya kukamilisha kozi hiyo akaajiriwa. Hapo aliweza kupata pesa nzuri hiyo akaajiriwa. Hapo aliweza kupata pesa nzuri kwa mahitaji yake.
Huko nymbani, wavyele wake walizidi kudhoofika kimisha. Waliposikia kuwa mtoto wao wa pekee kupata kazi, wingu la tamaa liliwajia. Ajabu ni kuwa wingu hilo halikuwa mvua ya mafanikio kwao. Subira aliponda mali na kutia kutia masikio nta. Hakukumbuka alikotoka. Maharawa walimzingira kama nzi kidondani. Ama kwa hakika mirija yao ilivukuta uhondo wa kutosha kutoka kwa mwenzao. Waliogelea katika mavuno ambayo hawakuyapalilia wala kunyunyuzia maji.
Kwa bahati mbaya, kutokana na makossa madogo subira alipigwa kalamu. Hapo ndipo lisani , ‘mla naw e hafi nawe ila mzaliwa nawe’ ilisibu.wavyele wake waliposikia hivyo walikwenda kumtafuta wakaisha naye hadi akapata kazi nyingine.
- Ni nani aliyekuwa akimtesa Subira?
- Mwajiri wake.
- Katili wake.
- Maafisa wa serikali
- Wavyele wake
- Methali liandikwalo na Mungu lazima liwe ina maana gani?
- Barua kutoka kwa Mungu haisemi uongo.
- Subira alipita vizuri alivyoambiwa na Mungu
- Jambo lolote alipopenda Mungu litokee lazima litokee.
- Subira alisomeshwa kwa sababu Mungu aliamrisha.
- Subira alisomea kazi gani?
- Kuendesha pikipiki
- Kuendesha garimoshi
- Kuendesha matwana
- Kuendesndege
- Chagua jibu ambalo si sahihi kulingana na habari.
- Subira alishughulikia wazazi wake vizuri
- Wazazi wa subira hawakumbeza alipofutwa kazi
- Subira alikuwa na mashoga wengi
- Subira alipopata kazi baada ya chuo aliwasahau wazazi wake.
- Kauli “Waliongelea kwenye mavuno ambayo hawakuyapalilia wala kuyanyunyuzia maji” inatumika kurejelea nani?
- Wavyele
- Subira
- Marafiki
- Waajiri wake.
- Kazi ambayo subira alikuwa akiifanya ilikuwa ya aina gani?
- Kazi ya sulubu
- Kazi ya kijungujiko
- Taaluma
- Masaragambo
- Kwa nini wavyele wa Subira walimtafuta baada ya kufutwa kazi
- Walikuwa wamemtafutia kazi nyingine
- Marafiki walikuwa wamemtoroka
- Subira hakuwa amewatimizia mahitaji yao.
- Damu ni nzito kuliko maji .
- Tamathali gani ya usumi haiijatumika katika fungu.
- Tashbihi
- Methali
- Nahau
- Tanakali za sauti
- Kutia masikio nta ina maana gani?
- Kupaka nta kuyaziba
- Kujifanya husikii lolote
- Kusikia kila jambo
- Kuwa kiziwi kabisa
- Je, jambo gani lilisababisha kufutwa kwa Subira?
- Anasa
- Chudi kazini
- Shirika kufilisika
- Alipata kazi kwa njia ya mkato.
MWONGOZO
INSHA
Umepewa dakika 40 kuandika Insha yako.
Andika insha isiyopungua ukurasa mmoja na nusu ukifuata maagizo uliyopewa.
Mwandikie rafiki yako barua ukimueleza kuhusu umuhimu wa kutia bidi masomoni.
Kiswahili Questions and Answers - Class 6 End of Term 3 Exams Set 2 2022
Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya vale uliyopewa.
Sisi _ 1_ na mama_ 2__mkali sana. Mama_3_ hakuturuhusu_4_ sheria zozote kiamboni petu. Kila alipohisi kuwa 5_kuoga, alitulazimisha kuoga maji baridi lakini 6 kutumia sabuni mbayo 7__ vizuri sana. Au kila alipogundua ___8utovu kinidhamu, tulikaripiwa na kukumbushwa kuwa ulikuwa wajibu 9 _kuwalinda wavyele wetu kwa tabia.
-
- tulilelewa
- tulielewa
- tulilelea
- tulilea
-
- aliyokuwa
- aliyekuwa
- aliyekua
- aliokuwa
-
- huo
- hio
- huyo
- hilo
-
- kuvuja
- kufunja
- ufuja
- kuvunja
-
- tuliogopa
- tumeogopa
- tutaogopa
- wanaogopa
-
- ingawa
- na
- kwa
- kuwa
-
- ilinukwa
- ilinukia
- inanukia
- ilinuka
-
- tuna
- mna
- wana
- lima
-
- wangu
- wetu
- wao
- yetu
Mawasiliano ni kitendo cha_10_ujumbe. Hii ni _ 11_. binadamu sanasana. Kuna njia 12 za mawasiliano. Kunazo zile za jadi kama vile kuwasha moto, kupiga uyoma au kutuma watu maalum_ 13 ujumbe mahali ulipohitajika, siku hizi, watu 14_ simu, magazeti, majarida na vifaa__15_ kuwasiliana.
-
- kupishana
- kupashia
- kupashika
- kupashana
-
- licha ya
- katikati ya
- baina ya
- mithili ya
-
- ' mingi
- nyingi
- jingi
- mingi
-
- kuupeleka
- kuzipeleka
- kulipeleka
- kukupeleka
-
- walitumia
- hutumia
- wametumia
- wangetumia
-
- nyinginezo
- zinginezo
- mengineyo
- vinginevyo
Kuanzia swali la 16-30. jibu kila swali kulingana na maagizo.
- Chagua orodha ambayo ni ya vielezi
- hivi, nyingi, yoyote, chake
- nyinyi, wewe, mimi, sisi
- sana, upesi, hakika, kabisa
- lini, gani, vipi mbona
- Chagua kiashiria takriri kilicho sahihi kujaza pengo:
Vikombe vilianguka hapa.- Vivi hivyo
- hivyo hivi
- hivi vivi
- vivi hivi
- Jaza pengo kwa neno sahihi:
Mama alienda shambani na alishinda kuko huko mchana -- kutua
- kutwa
- kutwaa
- kucha
- Ni yupi mpangilio uletao mfululizo ufaao wa wakati?
- Alfajiri, asubuhi, adhuhuri, alasiri magharibi
- Alasiri, asubuhi, alfajiri, magharibiadhuhuri
- Asubuhi, alfajiri, alasiri, adhuhuri,magharibi.
- Alfajiri, asubuhi, alasiri, adhuhuri,magharibi
- Umbo hili ni
- duara
- mche
- mpira
- duara dufu
- Mnyama ana manyoya mwilini, naye binadamu ana
- nywele
- malaika
- ndewe
- mashamba
- Tegua kitendawili hiki:
Mava hapo mava pale- kifo
- kioo
- kumetamcta
- kivuli
- Kutangaza kwa sauti kubwa ni
- kupiga maji
- kupiga mayowe
- kupiga mbiu
- kipiga domo
- Chagua kinyume cha sentensi ifuatayo:
Kitindamimba alifurahi sana.- Kifunguamimba alifurahi sana.
- Kitindamimba alikasirika sana,
- Mwanambee alifurahi sana.
- Mwanambee alikasirika sana.
- Kanusha: Nimekula nikashiba
- Sijala nikashiba.
- Sijakula nikashiba.
- Sijala wala kushiba.
- Sikula wala kushiba.
- Jaza pengo kwa usahihi:
Nyinyi mli tualika karamuni.- ndinyi/o
- ndiwo/ wo
- ndio/o
- ndio/ ye
- Tunasema shungi la nywele la kuni pia la mchanga.
- chane/ tita
- tita/ fungu
- shado/koja
- kicha/ bumba
- 3, 7, 17, 31 na 43 ni baadhi ya nambari
- tasa
- shufwa
- chanya
- witiri
- Kamilisha sentensi kwa usahihi:
Mahali hapa palifyekwa- pakafyekana
- pakafyekeshwa
- pakafyekela
- pakafyekewa
- Katika milioni sita kuna laki ngapi?
- Sita
- Sitini
- Elfu sita
- Mia sita
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31 mpaka 40.
Mlango ulibishwa. Bakari akachungulia kwenye tundu la mlangoni. Akaona mwanamke na mwanamume wamesimama wamebeba matunda. “Baba na mama wako?" waliuliza watu wale wawili. "La, hawapo, wameenda sokoni," Bakari alijibu,
“Basi watakapokuja wasalimie na uwape matunda haya na kuku huyu," wakamaliza. "Ngojeni niwapokee, insiende tafadhali." Bakari alisema huku akifungua mlango. Kufumba na kufumbua, Bakari alijikuta amewekewa bastola kichwani. “Funga mdono wako ukitaka usalama wako, ng'ombe wewe. Nyinyi mnashiba na watu wafa njaa!" Alisema mwanamume yule kwa ghadhabu. "Pesa, dhahabu na vyombo vya mama yako viko wapi?" Mwanamke aliuliza huku akizaba Bakari makofi mawili mazito. Bakari akamwonyesha kila kitu kwani roho yake ilikuwa mikononi, alikuwa hajijui hajitambui!
Wezi wale wawili wakaisafisha nyumba na kuifanya msikiti. Wakampulizia Bakari dawa ya usingizi. Papo hapo akaanguka na kulala fofofo!
- Bakari alikuwa na nani nyumbani?
- Pekee
- Bibiye
- Rafiki yake
- Mama na baba
- Watu wale wawili waliuliza akina nani?
- Baba
- Wazee
- Baba na mama
- Mama
- Ni nini kilichomfanya Bakari afungue mlango?
- Alishurutishwa kufanya hivyo.
- Zawadi alizoambiwa ni za wazazi wake.
- Alitaka kuwaona wageni wale vizuri.
- Aliwaona mwanamume na mwanamke.
- Bakari alipigwa makofi na nani?
- Mamake
- Rafikiye
- Mwanamume yule
- Mwanamke yule
- "Kufumba na kufumbua' ina maana gani?
- Hapo hapo
- Mara kwa mara
- Baadaye
- Kwa haraka kabisa
- Kumpokea mtu ni kufanya nini?
- Kumchukia
- Kumkaribisha
- Kumwongelesha
- Kumfungulia mlango
- Kuwa roho mkononi ni sawa na kusema
- kuwa karibu kufa.
- kuwa na woga zaidi.
- kwenda na roho kwenye mkono.
- kubeba roho kwenye mkono.
- Wezi walilalamikia nini?
- Kutofunguliwa mlango.
- Wao kushiba na watu kufa kwa njaa.
- Kutokuweko na wazazi.
- Kutopata dhahabu, vy'ombo na pesa.
- Wezi hawa wangeshikwa wakiiba tungewaambia methali gani?
- Siku za mwizi ni arubaini.
- Mtaka yote hukosa yote.
- Bendera hufuata upepo.
- Mtegemea cha nduguye hufa masikini.
- Neno ghadhabu lina maana gani kuligana na ufahamu?
- Elekeza
- Haraka kabisa
- Hofu kubwa
- Kukasirika
Soma kifingu kifuatacho kisha ujibu maswali 41 mpaka 50.
Simu ni chombo cha watu cha kuwasiliana. Simu hutumia mawimbi ili kupokea sauti au picha. Kuna aina mbili za simu. Rununu na simu ya ofisi.
Stepford Press and Publishers, 2021
Simu ya ofisi au simu ya nyumbani mara nyingi hutumiwa ofisini ama nyumbani. Simu hii huwekwa mahali fulani maalum katika ofisi. Simu hii huwekwa katika mapokezi. Inapopigwa, huwezi kuona nambari ya anayepiga.
Rununu pia huitwa simu tamba, selula au rokono. Rununu ni simu ndogo ambayo unaweza kuibeba mahali popote unapoenda. Rumunu hutuinia simu kadi. Pia hutumia kadihela ili kupata muda wa maongezi. Manufaa ya rununu ni tumbi tumbi. Hata kama ni ndogo wahenga walisema usione wembamba wa reli, gari moshi hupita.
Manufaa ya rununu ni kuwa huweza kutuma arafa. Arafa ni ujumbe mfupi unaotumwa kwa njia ya kuandika. Pia, hutumika katika biashara kwa kutuma pesa za kununua bidhaa.
Simu pia hutumika kuwapa watu ajira kwa kuajiriwa katika duka la M-pesa, kuuza rununu na vifaa vyake. Watu wengine huzitengeneza simu zilizoharibika kwa malipo na wao hupata ajira.
Hakuna kizuri kisichokuwa na hila. Rununu ina hasara pia. Inaweza kutumiwa na waovu kuwaibia watu pesa. Aidha kutuma ujumbe wa chuki, matusi na picha chafu zisizofaa.
Daima, tutumie rununu kwa uangalifu mkubwa tusije tukajuta majuto ya mjukuu ambayo huja baadaye.
- Simu ndogo ambayo mtu anaweza akatembea nayo mahali popote inaitwa
- simu tamba
- simu ya nyumbani
- simu ya ofisi
- arafa
- Rununu ni kifaa cha
- maliasili
- ajira
- teknolojia
- madini
- Rununu pia haiitwi
- ofisi
- selula
- rukono
- simu tamba
- Kadi ambayo hununuliwa yenye nambari fulani za rununu ambazo mtu hutumia kwa kitambulisho chake pekee huitwa
- ajira
- kadi
- simu kadi
- simu hela
- Ipi si manufaa ya rununu?
- Kutuma arafa.
- Kuwapa watu ajira.
- Kuwaibia watu pesa.
- Kupata pesa kwa kutengeneza rununu zilizoharibika.
- Manufaa ya rununu ni tumbi tumbi.
Maana ya tumbi tumbi ni- si tele
- chache
- nyingi
- haba
- Maana ya neno ‘ajira' ni
- Kazi
- pesa
- malipo
- hela
- Ni methali gani inalingana na maelezo haya: Rununu, hata kama ni kifaa kidogo, kina faida nyingi?
- Enga kabla ya kujenga.
- Hakuna kizuri kisichokuwa na ila.
- Majuto ni mjukuu huja kinyume.
- Usione wembamba wa reli gari moshi hupita.
- Mojawapo ya hasara za rununu ni
- kuuza rununu na vifaa vyake kwa malipo kwenye duka la simu kama mfanyi kazi.
- kuwasiliana na marafiki.
- kutuma ujumbe wa chuki na matusi.
- kuajiriwa katika duka la M-pesa.
- Kichwa mwafaka cha kifungu hiki ni
- Kadihela
- Rununu
- Mawasiliano
- Arafa
INSHA
Umepewa dakika 40 kuandika insha yako.
HASARA ZA MMOMONYOKO WA UDONGO
MARKING SCHEME
- A
- B
- C
- D
- A
- C
- B
- A
- B
- D
- C
- B
- A
- B
- D
- C
- D
- B
- A
- B
- A
- D
- C
- D
- C
- C
- B
- A
- C
- B
- A
- C
- B
- D
- B
- B
- A
- B
- A
- D
- A
- C
- A
- C
- C
- C
- A
- D
- C
- B
Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 End of Term 3 Exams 2022 Set 1
KISWAHILI
GREDI YA 5
MWISHO WA MUHULA WA 3
MAAGIZO.
- Hii karatasi ina sehemu sita kuu.
- Jibu maswali yote ku lingana na maagizo.
Maswali
SEHEMU 1: Mazungumzo ya ana kwa ana (Alama 5)
Ni asubuhi na mapema unaelekea shuleni, kisha unamkuta mzee mgongwe barabarani akid edema.
- Ni kitu kipi utakachokifanya unapokutana na mzee huyu?
- Eleza salamu utakazomuamkua mzee?
- Mzee atajibu vipi?
- Utamsaidiaje mzee ili afike alipokuwa akienda?
- Taja watu katika jamii wanaohitaji msaada wetu
SEHEMU 2: Ufahamu wa kusikiliza( Alama 4)
Msikilize walimu akisoma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.
Siku moja Mwanasiti alipokuwa akichanja kuni alijikata kisigino chake na shoka. Damu ilianza kububujika kwa kasi. Mamake alichukua gari lao na kumpeleka hospitalini.Alipofika hospitalini alibebwa na kupelekwa kwa daktari. Daktari alimdunga sindano ya kuzima kutoka kwa damu, kisha akashona kile kidonda na kutia bendeji. Mwanasiti alipomaliziwa alionywa na daktari kuwa awe makini anapotumia shoka au vitu vyenye makali.
- Unadhani mwanasiti alipofika hospitalini alibebwa kwa
- Jina jingine la daktari ni
- Taja vifaa vingine viwili ambavyo daktari alitumia kumtibu Mwanasiti?
- Ni onyo lipi alilopewa Mwanasiti?
SEHEMU 3: Kusoma kwa sauti (Alama 15)
Soma kifungu kifuatacho kwa sauti.
Sikukuu ya Madaraka nchini Kenya huwa tarehe moja, Juni. Siku hii ni ya muhimu sana katika nchi yetu. Wananchi hujumuika katika maeneo mbalimbali kusherehekea ukombozi wetu kutoka kwa wakoloni. Nchi yetu ilikuwa imetawaliwa na wakoloni na mabeberu miaka hamsini na minane iliyopita.
Wengi wa wale waliopigania uhuru katika nchi yetu hukumbukwa siku hii. Wengine hutajwa na kupewa zawadi na raisi wa jamhuri ya Kenya. Wengine hupewa makao. Wale waliopoteza maisha wakati wa ukombozi mabango hujengwa ili kuwakumbuka.
Sisi kama wananchi wazalendo ni lazima tutimize amani. Tuhakikishe kila mmoja wetu ana uhuru wake. Kila jimbo limepewa siku yake ya kuadhimisha sherehe hizi eneo lao. Lengo kuu ni kuwaleta Wakenya pamoja.
SEHEMU 4: Ufahamu wa kusoma
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Chausiku ni msichana mrembo na mwenye umbo la kuvutia. Ni kitinda mimba katika familia ya Mzee Sonu na Bibi Washuka. Msichana huyu ana tabia ya kupendeza. Huwaheshimu wakubwa na wadogo. Akitumwa na mamake yeye huenda bila kupinga. Katika familia yake yeye ndiye mtoto ndiye amesoma hadi darasa la tano. Wengine wote walikwamilia madarasa ya chini na wengine ya chekechea.
Wazazi wake wanampenda sana. Kila mara wanamhimiza awe mwenye hekima na kufanya bidii masomoni. Shuleni, Chausiku anabobea katika masomo na michezo mbalimbali. Mwalimu wake wa darasa anajivunia kuwa na mwanafunzi ambaye hulka yake inatamaniwa na wengine shuleni. Chausiku alichaguliwa kuwa kiranja wa darasa la tano. Kila Ijumaa hukutana na wenzake na kupanga mikakati ya kufaulu masomoni. Kwa kweli mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Chausiku anapendwa na wanafunzi si wa darasa lake tu bali shule nzima na hata walimu wanampenda.
Maswali
- Taja sifa mbili za Chausiku?
- Ndugu zake Chausiku walifika madarasa gani?
- Ni kitu gani wazazi wake Chausiku walikuwa wakimhimiza kila mara?
- Chausiku alichaguliwa kama?
- Andika methali ingine yenye maana sawa na mtoto umleavyo ndivyo akuavyo?
- Ipe hadithi mada inayoifaa?
SEHEMU 5: Sarufi (Alama 20)
Andika wingi wa nomino hizi.
- upishi
- uwele
- uzi
Kamilisha methali hizi. - Mchumia juani
- Mvumilivu hula
- Subira huvuta
Tunga sentensi ukitumia maneno haya. - Barabara
- sketi
- kofia
Andika katika umoja. - Vyandarua vimereruka
- Vyakula vimeiva
- Vyungu vimepasuka
Akifisha sentensi zifuatazo. - mama alijipamba kwa herini mkufu na bangili
- je mtafungua shule siku gani
- nampenda paka wangu niliyemnunua nchini burundi
Pigilia msitari nomino za dhania. - mwalimu, bidii, kimbia, safi, mlango, uhodari
Tazama picha kisha utaje nomino ya kundi hilo. -
-
-
SEHEMU 6: Kuandika(Alama 10)
Tazama picha hii kisha uandike insha fupi kuihusu.
Mwongozo wa kusahihisha
SEHEMU A
Sehemu 1: Tathmini
Sehemu 2: Ufahamu wa kusikiliza tathmini
Sehemu 3: Tathmini
Sehemu 4: Ufahamu wa kusoma
- Mrembo na mwenye umbo la kupendeza mwenye heshima
- Ya chini na chekechea
- Awe mwenye hekima na kutia bidii
- Kiranja wa darasa la tano
- Mti ukunje ungali mbichi
- Chausiku
SEHEMU 5: Sarufi
- mapishi
- mawele
- nyuzi
- hulia kivulini
- mbivu
- heri
- sentesi iwe kamilifu
- sentesi iwe kamilifu
- sentesi iwe kamilifu
- Chandarua kimeraruka
- Chakula kimeiva
- Chungu kimepasuka
- Mama alijipamba kwa herini, mkufu na bangili
- Je, ni siku gani mtafungua shule?
- Nampenda paka wangu niliyemnunua nchini Burundi
- Bidii, safi, uhodari
- Kundi la magari
- Tita la kuni
- Kundi la magari
SEHEMU 6: Kuandika
Mtungo ni alama kumi. angazia kanuni za usahihishaji wa mtungo kama hati, mtiririko, uasilia na ubunifu.
Kiswahili Questions and Answers - Class 6 End of Term 3 Exams Set 1 2022
Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo. Jaza kila pengo kwa kuchagua lifaalo zaidi
Kuna njia 1 za kuhakikisha kuwa tuna afya bora. Kwa 2 , tunashauriwa kula chakula 3 , kufanya mazoezi, kujiepusha na 4 na kutafuta matibabu tukiwa wagonjvva. Mtu akiwa mgonjwa, 5 kufanya kazi wale kusoma kwa njia inayofaa. Kipindupindu, kichocho na kuendesha ni baadhi ya 6 ambazo husababishwa na 7 usafi wa mwili na mazingira. Kila 8 ana jukumu la kuhakikisha kuwa mwili wake ni safi, anakula chakula safi na kuishi mahali safi. Wadudu hatari kama vile 9 nao hushambulia vidole vya mtu anayeishi mahali penye uchafu. Sote tujiepushe na uchafu.
-
- ambazo
- mengi
- mingi
- nyingi
-
- vile
- kuwa
- sababu
- mfano
-
- inayofaa
- kinachofaa
- linalofaa
- vinavyofaa
-
- madawa ya kulevya
- dawa ya kulevya
- dawa za kulevya
- madawa za kulevya
-
- anaweza
- hawezwi
- hawezi
- hawawozi
-
- magonjwa
- ndwele
- ugonjwa
- maradhi
-
- kutozingatia
- kuzingatia
- kujua
- kutojua
-
- moja
- kimoja
- umoja
- mmoja
-
- tekenya
- mende
- kunguni
- chawa
Asubuhi 10 , wazazi wa Kajua 11 kuelekea shuleni iii wajue kwa nini mtoto wao alirudishwa nyumbani. Walianza safari hata biia kunywa 12 yao kama ilivyokuwa kawaida. Walipofika 13 waliarifiwa kuwa Kajua alipatikana akicheza na simu wakati wa masomo. Wazazi walishangaa na 14 sana. Walimpa 15 kali na kumpokonya simu hiyo Nadi akamiIishe masomo yake. Kajua aliomba msamaha na kubadilika kabisa.
-
- hiyo
- hio
- huo
- huwo
-
- walikata shauri
- walikata kauli
- walikata kamba
- walikata kiu
-
- kiamshakinywa
- staftahi
- chamcha
- uji
-
- ndani mwa shule
- katika shuleni
- kwa shule
- shuleni
-
- kulia
- kushangilia
- kuhuzunika
- kusherehekea
-
- adabu
- viboko
- adhabu
- heshima
- Kivumishi gani ambacho ni tofauti na vingine?
- zote
- wengi
- yeyote
- chenye
- Chagua maelezo ambayo si sahihi.
- Figo ni kiungo ambacho husafisha damu mwilini.
- Kiwiko ni sehemu ya mkono ambapo saa hufungwa.
- Mfupa ambao hufunika meno huitwa
- Mapafu huingiza hewa safi mwilini na kutoa hewa chafu.
- Chagua ukanusho wa;
Unga umeletwa na mama.- Unga hujaletwa na mama.
- Unga haujaletwa na mama.
- Unga umepelekwa na baba.
- Unga haukuletwa na mama.
- Tambua sentensi iliyotumia "ki" kuonyesha udogo.
- Ukimwona mwalimu shuleni uniambie.
- Magari yote yalikuwa yakioshwa na wafanyakazi.
- Kijibwa cha nyanya kimelala.
- Wacheni kucheza kijinga mtaumia.
- Neno eshukuru' lina herufi ngapi?
- 3
- 7
- 6
- 5
- Tambua usemi wa taarifa wa sentensi ifuatayo.
"Kesho tutaenda Mombasa," mwalimu alisema.- Mwalimu alisema kuwa wangeenda Mombasa siku iliyofuata.
- Mwalimu alisema kuwa tungeenda Mombasa kesho.
- Mwalimu alisema kuwa wataenda Mombasa siku iliyofuata.
- Mwalimu alisema kuwa tutaenda Mombasa kesho.
- Sentensi ifuatayo itaandikwaje katika wingi?
Kuli ameweka chupa karibu na ukuta.- Makuli wameweka chupa karibu na nyuta.
- Makuli wameweka vyupa karibu na kuta.
- Kuli wameweka chupa karibu na kuta.
- Makuli wameweka chupa karibu na kuta
- Rangi ya chini kabisa kwenye upinde wa mvua huwa ipi?
- nyekundu
- urujuani
- nili
- machungwa
- Tambua aina za maneno yaliyopigiwa mistari.
Tulitembea polepole na kusimama chini ya mti.- nomino, kihusishi
- kivumishi, kielezi .
- kielezi, kihusishi
- livumishi, kitenzi
- Sentensi gani iliyotumia kiashiria kisisitizi?
- Mkeka ule radio ulionunuliwa_
- Kinywaji hiki hiki kitapewa mtoto.
- Nguo yenyewe ndiyo iliyopigwa pasi.
- Baiskeli iyo hiyo itapelekwa kwa fundi
- Orodha ipi iliyo ria msamiati wa aina moja?
- funza, nzi, mbuni
- randa, msumeno, tarumbeta
- sabmarini, purutangi, machela
- dania, mdalasini, tangawizi
- Chagua sentensi ambayo ni
- Chaff ambacho kimeiva ni kitamu.
- Nyumba yenye imejengwa ni ya babu.
- Usinywe maji chafu, kunywa maji safe.
- Kutembea kunakopendeza ni kwa mtoto.
- 'Lima' ni kwa `mkulirria' kama vile ni kwa 'msomaji.'
- soma
- andika
- fundisha
- masomo
- Mpira wa kandanda huwa na umbo gani?
- tufe
- duara
- duaradufu
- tao
- Kiambishi kimetumikaje katika sentensi ifuatayo?
Mtoto huyo amejiangusha chini.- kirejeshi
- hall
- mtendaji
- ukubwa
Soma kifungu kifuatacho kisha ulibu maswali 31- 40.
Vita ni hall ya kukosa amani na utulivu. Hall hiyo husababisha kutoelewana na kupigana. Mara nyingi, vita husababishwa na ugpmvi. Vita huweza kutokea kila mahali na kwa kila umri. Pengine hata mahali unaposomea, shuleni au darasani, umewahi kuona wanafunzi wenzako wakipigana. Pengine hata wewe mwenyewe umewahi kuhusika katika vita. Je, umewahi kuona watu wakipigana njiani ukielekea nyurnbani kutoka shuleni? Kuna nyakati ambapo vita hutokea kati ya watu wazima kama vile wazazi au makabila mawili ambayo ni tofauti. Kiwango cha juu cha vita huwa ni vita katika nchi. Vita kama hivi huweza kutokana na kutoelewana katika jambo la kitaifa kama vile matokeo ya uchaguzi. Vita vina madhara gani?
Ifahamike kuwa vita husababisha kuumia kwa watu na mifugo. Watu walioumizwa wakati wa vita hulia kwikwikwi kutokana na maumivu. Wengine huishia kuaga dunia kutokana na majeraha katika vita. Mali nayo huharibiwa mno. Utapata kuwa maduka ya watu na nyumba zao huchomwa bila sababu maalum. Magari hupigwa na kuvunjwa vioo au kuchomwa. Uharibifu huu wa niali hurudisha nyuma uchumi wa taifa letu. Masomo, biashara na kazi haziwezi zikafanyika kwa kuwa ni vigumu kusafiri katika mazingira yaliyo na vita. Wanafunzi na walimu hubakia katika nyumba zao wakihofia kuangamizwa na wapiganaji. Hakuna awezaye kuuza wala kununua chochote kwa kuwa maduka yote hufungwa. Upendo na umoja katika nchi nao hurudi chini. Hilo ni tatizo kubwa kwa kuwa umoja na ushirikiano ni muhimu sana.
Kunapotokea kutoelewana, njia ya pekee huwa ni kupigana ama kuna njia nyingine? Mwenzako anapokukasea shuleni ama nyumbani, unafaa kufanya nini? Jinsi tunavyojua, kupigana hakufai hata kidogo. Mazungumzo yanafaa kuwapo kati ya watu wawili waliokosana ama makundi mawili ambayo yamekosana. Kama hakuna kuelewana, husisheni mtu au watu wengine iii wasaidie kuleta utulivu. Aliyekosea hushauriwa kuomba msamaha na aliyekosewa amsamehe mwenzake. Tukumbuke kuwa kiln mtu hukosea. Hakuna mkamilifu ila Mungu pekee.
- Ufahamu unaeleza kuwa vita husababisha
- amani na utulivu.
- kutoelewana na amani.
- kutoelewana na kupigana.
- kupigana na utulivu.
- Ni kweli kuwa vita huweza kutokea wapi?
- Shuleni na njiani
- Sokoni na darasani
- Njiani na sokoni
- Kila mahali
- Kiwango cha juu cha vita kinahusu nini?
- Vita vinavyotumia bunduki
- Vita katika nchi
- Vita vinavyoleta kifo
- Vita kati ya watu wakubwa
- Ufahamu unaonyesha kuwa vita huongeza yafuatayo isipokuwu
- uchumi.
- vifo.
- umaskini.
- chuki.
- Maneno 'hulia kwikwikwi' ni mfano wa
- nahau.
- sitiari.
- tashbihi.
- tanakali ya sauti.
- Msimulizi anaeleza kuwa hall ya kukosana ikitokea watu wafanye nini?
- Wasigombane wala wasipigane sana.
- Wazungumze na kusameheana.
- Wapigane to ikiwa msamaha haupatikani.
- Aliyekosea anafaa kuombwa msamaha.
- Msimulizi ametumia maneno kuwa umoja na ushirikiano ni muhimu sana'.
Methali gani inayokubaliana na maneno hayo- Polepole radio mwendo.
- Mkono mmoja hauchinji ng'ombe.
- Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
- Akufaaye kwa ndiye rafiki.
- Kulingana na ufahamu, hakuna mtu ambaye
- hana makosa.
- hukosea.
- huomba msamaha.
- husamehewa
- Nini ambacho huwa hakichomwi wakati wa vita kulingana na ufahamu?
- Nyumba
- Magari
- Maduka
- Vioo
- Ufahamu huu unahusu umuhimu wa nini?
- Vita
- Amani
- Mazungumzo
- Kutoetewana
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41- 50.
Katika cha Jikaze, paliishi kijana mmoja aliyeitwa Musa. Aiikuwa kijana wa miaka kumi na
mitano. Musa alipenda kufanya rnzaha na kuchezea wenzake. Wakati mwingine alipokuwa shuleni, alianguka chini na kuanza kulia. Walimu na wanafunzi waliingiwa na wasiwasi sana. Baada ya kuulizwa kwa mucla mrefur Musa alisema kwa sauti ya unyonge, "Mimi ni rngonjwa, ninaumwa na tumbo." Walimu walitafuta njia ya kumrudisha nyumbani kwao. Kula nyumbani alilala kidogo kisha akasimama na kusema kuwa amepona. Aliifanya hii kuwa tabia yake hasa alipojua kuwa hakuwa amefanya kazi yoyote ya mwalimu. Alijifanya mgonjwa kiasi cha kushindwa kutembea. Wanafunzi wengine walimsikia siku moja akimwambia mwenzake kuwa hiyo ilikuwa njia rahisi ya kutonaswa vvameiti tura' Wakati akiwa katika likizo ya Disemba, alikuwa akitumwa na wazazi wake kuwapeleka mifugo msituni wale nyasi. Kwa kuwa hakutaka kuifanya kazi hiyo, alitafuta njia ya kuwafanya wazazi waache kumtuma msituni. Baada ya muda mfupi wa kuwafikisha ng'ocr be malishoni, angeanza kupiga kelele, "Uuuuwi! Wooi! Weziii!" Wanakijiji walifika pale kwa kasi sana. Ajabu ni kuwa mifugo wote walikuwa wametulia tuti wakila nyasi. Musa naye alikuwa juu ya kitima fufani akiruka na kupiga kelele. Wanakijiji hao walikasirika na kuondoka. Wiki moja ilipopita, wanakijiji tena walizinduliwa kutoka katika shughuli zao na kamsa. "Jameeeni! Mungu wanguuu! Woooi! Mayoo!" Wanakijiji walifika pale kwa kasi ya umeme wakidhani kuwa amevamiwa na wezi au mnyama hatari. Waliondoka wakiwa wameudhika kwelikweli.
Siku moja, Jumamosi, Musa aliwasili malishoni wakati wa adhuhuri. Alijilaza chini ya mti na kutulia. Ghafia kama ajali, aliwaona wezi wakiondoka na mifugo wao. "Woooi! Mayoo! Woooi! Weziii!" Alipiga kelele na kuomba msaada. Hakuna aliyeonekana iii kumsaidia. Mwizi mmoja alimshika na kumfunga kwenye mti. Mifugo kumi walichukuliwa, watano wakauawa na wengine watano wakaachwa kwa sababu walikuwa wachanga. Mtoto wa watu akabaki akiwa amefungwa kwenye mti.
- Kulingana na ufahamu, ni kweli kuwa
- Musa alikuwa mgonjwa mara mbili.
- Musa hakuwa mgonjwa wakati wowote.
- Musa alikuwa akiumwa na tumbo.
- Musa alipenda sana masomo.
- Kwa nini Musa alikuwa akisema kuwa yeye ni mgonjwa?
- Ndipo apelekwe hospitalini.
- Ndipo awasaidie wazazi kuwalisha mifugo.
- Ili asiadhibiwe kwa kutofanya kazi.
- Ili apate nafasi ya kucheza na wenzake.
- Mara ya pill Musa alipopiga kelele;
- alisema kuwa ameshambuliwa na wezi.
- alisema kuwa ameumwa na nyoka.
- alisema kuwa ameshambuliwa na mnyama hatari.
- hapakuwa na hatari yoyote iliyomkumba.
- Mara ya tatu, Musa aliwasili malishoni saa ngapi kulingana na ufahamu?
- saa na nane
- saa tano
- saa kumi
- haijulikani
- Ufahamu unaonyesha kuwa Musa alikuwa na tabia gani?
- mwerevu na mtiffu
- mjanja na mzembe
- mwoga na mchafu
- mzuri na mwenye heshima
- Unadhani kwa nini wanakijiji hawakwenda kurnwona Musa alipopiga kelele mara ya tatu?
- Hawakusikia akipiga kelele.
- Walitaka wezi hao wa mfanye abadilishe tabia.
- Walifikiri kuwa Musa alikuwa akifanya mchezo kama kawaida.
- Walijua kuwa wezi hao hawakutaka kumwua Musa.
- Mifugo wa akina Musa waliibwa siku gani?
- Jumamosi
- Ijumaa
- Jumapili
- Alhamisi
- Kifungu hiki kinatushauri tuache tabia gani?
- Ya kufanya mzaha na kuwachezea wengine.
- Ya kusema kuwa sisi ni wagonjwa.
- Ya kupiga kelele tukiwa na mifugo msituni.
- Ya kuwaita watu kwa sababu ya wezi.
- Musa alikuwa na mifugo wangapi msituni?
- Ishirini
- Kumi
- Watano
- Kumi na watano
- Kichwa gani kinachofaa kwa makala haya?
- Musa na wezi.
- Vituko vya Musa.
- Musa shuleni.
- Musa na marafiki take.
INSHA
Andika insha ya kusisimua inayoanza kwa maneno yafuatayo
Hayawi hayawi huwa. Siku tuliyokuwa tumeingojea kwa hamu kuu baadaye ilifika. Wanasoka wa shule yetu walikuwa wamejiandaa vya kutosha
MARKING SCHEME
- D
- D
- B
- C
- C
- B
- A
- D
- A
- A
- B
- B
- D
- C
- C
- B
- C
- B
- C
- B
- A
- D
- B
- C
- D
- D
- D
- A
- A
- C
- C
- D
- B
- A
- D
- B
- B
- A
- D
- C
- B
- C
- D
- A
- B
- C
- A
- A
- A
- B
Kiswahili Questions and Answers - Class 7 End Term 3 Exam 2022 Set 1
MASWALI
Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo. Jaza kila pengo kwa kuchagua jawabu lifaalo zaidi.
Sherehe za kuukamilisha mwaka na kuanza mwaka____1__huwa na shamrashamra chungu nzima. Siku ya mwisho ya mwaka_ 2_huonyesha mwanzo wa sherehe hizo. Watu hukesha 3 wakiwa makanisani, katika vyumba vya burudani au maeneo mengine ya 4 Usiku, wakati wa saa sita kamili, watu__5_mwaka mpya kwa shangwe, hoihoi na vigelegele. Wengi huadhimisha mwaka mpya kwa njia tofauti. Wengine huvaa nguo mpya__6__ kupendeza huku wengine wakichinja kulingana na uwezo _7_ . Watu 8 , huamkuana kwa kutakiana heri njema na mwaka mpya wenye mafanikio _9_ .
-
- mingine
- ingine
- mwingine
- nyingine
-
- unayokamilisha
- unaokamilika
- unaokamilisha
- unayokamilika
-
- mchana kucha
- mchana kutwa
- usiku kucha
- usiku kutwa
-
- kujifurahisha
- kukufurahisha
- kumfurahisha
- kutufurahisha
-
- huyapokea
- hulipokea
- huipokea
- huupokea
-
- za
- ya
- la
- mwa
-
- wake
- wangu
- wako
- wao
-
- wamepokutana
- walipokutana
- wanapokutana
- wangepokutana
-
- mingi
- tele
- haba
- nadra
Kila mzazi au mlezi__10_jukumu__11__ kumkuza mtoto kwa njia inayofaa. Ni lazima ahakikishe kuwa mtoto huyo anapata mahitaji ya 12 katika maisha. Mahitaji hayo ni kama vile___13_ .___14__, mzazi au mlezi anafaa kuwa kielelezo bora kwa mtoto. Ajue kuwa mtoto huiga tabia zake. Hii ndiyo sababu wahenga wakasema kuwa____15___.
-
- ana
- hana
- hawana
- wana
-
- la
- ya
- wa
- kwa
-
- kijumla
- kitaifa
- kimsingi
- kijuujuu
-
- masomo, makao na malazi
- chakula, makao na mavazi
- malezi, elimu na
- usafiri matibabu, chakula na malezi
-
- Na
- Hata hivyo
- Mathalani
- Aidha
-
- asiyesikia la mkuu huvunjika guu
- mwana hutazama kisogo cha nina
- fimbo ya mbali haiui nyoka
- uchungu wa mwana aujuaye ni mzazi
- Chagua udogo wa sentensi ifuatayo.
Mtoto aliumiza uso wa mbwa.- Toto liliumiza juso la jibwa.
- Kitoto kiliumiza kijuso cha kijibwa.
- Kijitoto aliumiza kijuso wa kijibwa.
- Kimtoto kiliumiza kiuso cha kimbwa.
- Maelezo gani ambayo ni sahihi?
- Watu wakiagana bila matumaini ya kuonana tena huambiana binuru.
- Ukitaka kupewa nafasi ya kupita utaomba kwa kusema simile.
- Shikamoo ni salamu za mtu mkubwa kwa mdogo.
- Sabalheri na masalheri ni mifano ya salamu za asubuhi.
- Sentensi gani iliyotumia 'po' kuonyesha mahali?
- Wote walipowasili tulipiga makofi.
- Mlipoegesha magari yenu pana kivuli.
- Usiposoma kwa bidii hutapita mtihani.
- Nilipomwona nilijificha ndani ya nyumba.
- Tambua sentensi iliyoakifishwa kwa kutumia alama za mtajo.
- . Watapikiwa vyakula vingi: Wali, chapatti, nyama, samaki na kadhalika.
- Nimeamini kuwa asiyesikia la mkuu...
- Mbung'o wanafonza damu ya ng'ombe.
- Nyote leteni madaftari yenu," mwalimu akasema.
- Wakati wa machweo jua huwa upande gani wa dira?
- Kusini
- Kaskazini
- Magharibi
- Mashariki
- Sentensi gani ambayo ni sahihi kisarufi?
- unga ambao uliomwagika ni huu.
- Gari lile jeusi lina abiria wengi.
- Angejua njia ya kwenda nyumbani hangepotea.
- Hapo nyumbani kwao kutakuwa na sherehe.
- Orodha ipi yenye vivumishi vimilikishi?
- wangu, zao, chake
- lote, mwingine, yenyewe
- safi, mzuri, kitamu
- gani, yupi, wangapi
- Jibu gani halijaunganisha sentensi zifuatazo kwa usahihi?
Dhahabu alipewa zawadi. Dhahabu hakufurahi.- Licha ya Dhahabu kupewa zawadi hakufurahi.
- Dhahabu alipewa zawadi bali hakufurahi.
- Ingawa Dhahabu alipewa zawadi hakufurahi.
- Dhahabu hakufurahi maadamu alipewa zawadi.
- Jaza nafasi kwa jibu linalofaa.
Kitanda ........................kilivunjika kitatengenezwa.- chenye
- kile
- chenyewe
- ambacho
- Ulinganisho upi ulio na kitenzi
kilichoundwa kutokana na nomino?- mwandiko - uandishi
- kilio -- mlio
- ulinzi - linda
- mwalimu - elimu
- Petero alikuwa na nusu ya mkate, akawagawia watoto wake wanne vipande sawa. Kila mtoto alipata akisami gani ya mkate?
- ½
- ¾
- 1/6
- 1/8
- Chagua neno baki kwenye orodha ifuatayo.
- Jogoo
- Koo
- Jimbi
- Kikwara
- Tambua nomino ambayo
haijalinganishwa kwa usahihi na ngeli yake.- Kipepeo KI-VI
- Moyo U-ZI
- Bustani PAKUMU
- Ukuti U-ZI
- 'Ungewasili mapema usingeadhibiwa' ndiko kusema kuwa
- uliadhibiwa kwa kuwa hukuwasili mapema.
- kuwasili mapema kulifanya hukuadhibiwa.
- kutowasili mapema kulifanya hukuadhibiwa.
- kuadhibiwa kwako kulitokana na kuwasili kwako mapema.
- Fundi wa kujenga nyumba kwa mawe huitwaje?
- Seremala
- Mwashi
- Mhunzi
- Malenga
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31-40.
Kama kuna kitu ambacho kila mtu hupata kwa kiwango sawa, ni wakati. Kila mtu hupata saa ishirini na nne kwa siku. Haijalishi kama yeye ni tajiri au maskini, wa kiume au wa kike, kijana au mzee. Tofauti kubwa hutokana na namna tunavyoutumia wakati wetu. Je, wewe mwanafunzi unafaa kuutumiaje wakati wako hasa wa likizo? Awali ya yote, utumie wakati wako kuujenga uhusiano wako na Mungu. Hakikisha kuwa unasoma mafundisho kuhusu Mungu na kupiga dua kila wakati ili Jalali akujaalie fanaka kochokocho katika maisha yako. Hakikisha kuwa unaenda maabadini na kushirikiana na wenzako kumpa Mola sifa na kumshukuru. Aisee, mwomba Mungu si mtovu. Mungu ndiye atakayekusaidia kufaulu maishani.
Vilevile, ni jambo la busara kuwasaidia wazazi wako katika shughuli zao. Ni vyema sana kumwaviza mama yako katika shughuli mathalani kuosha vyombo, kufua nguo na kuzipiga pasi, kucheza na wanuna wako na kadhalika. Ikiwa baba yako ana duka pale sokoni, enda dukani pale ili umpige jeki katika shughuli za uuzaji. Unaweza kumsaidia kuwapa wateja bidhaa na kupiga hesabu. Huko kuwasaidia kutakuimarisha katika njia anuwai. Hewaa! Utaelewa kuyafanya mambo mengi ambayo pengine hukuyajua. Usisahau kuwa masomo bado yanaendelea. Hata kama umekamilisha masomo ya shule ya msingi, kumbuka kuwa elimu ni bahari. Naam, elimu haina mwisho. Endelea kusoma vitabu, magazeti na majarida ili upate maarifa chungu nzima kama mchanga wa bahari. Ukipata vitabu vya kidato cha kwanza, viinamie kama mwanasheria atafutaye neno la ushindi katika daawa. Ni nani asiyefahamu kuwa mizizi ya elimu ni michungu lakini matunda yake ni matamu?
Licha ya hayo, shirikiana na watoto wenzako katika michezo kadhaa kijijini penu. Kila unapokamilisha shughuli zako, shirikianeni kama kiko na digali katika michezo kama vile kibe, kurusha tiara, kucheza kandanda na mingineyo. Michezo hii ina faida kochokocho katika maisha. Michezo haichangii kuimarisha tu afya bali pia hukuza maadili. Mnaposhiriki katika michezo, viungo vya mwili huimarika na afya kuwa thabiti. Kumbuka kuwa afya ni bora kuliko mali? Pia, ushirikiano na umoja ujengwao wakati wa michezo ni muhimu kama dhahabu katika maisha ya kila mja. Wahenga hawakutuchezea waliposema kuwa umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.
Aidha, jitolee mhanga na kujikaza kisabuni kuhakikisha kuwa uhifadhi wa mazingira unaendelezwa. Kuhifadhi mazingira kuna manufaa sio kwako tu bali pia kwa jamii nzima. Ukiwa na ndugu na marafiki zako, fanyeni juhudi za mchwa ili kupanda miti na kuitunza Pandeni mbegu za miti mbalimbali kisha msubiri ziote. Pandeni miche hiyo katika sehemu zinazofaa na kunyunyizia maji. Usafi wa mwili na mazingira nao una umuhimu usiopuuzika. Bidii zenu ni muhimu katika kuhakikisha kuwa mnaishi katika mazingira yaliyo safi kama msahafu. Vilevile ninakushauri uwaepuke marafiki wenye tabia mbaya. Marafiki kama hao wanaweza kukuingiza katika mtego wa utovu wa maadili. Kutangamana na watu wenye maadili ni njia mojawapo ya kuhakikisha kuwa tabia zako zinakuwa za kuigwa. Hewaa! Mtu ni utu, asiye na utu ana kutu.
Yote tisa, kumi ni kuwa jiepushe na matumizi mabaya ya mtandao. Usiwe mwenye mazoea ya kutazama runinga usiku na mchana. Filamu, picha na video chafu nazo uziepuke kama ugonjwa wa korona. Kumbuka kuwa vitu uvitazamavyo na kuvisikiliza mara kwa mara huathiri tabia zako. Mihadarati nayo ni sumu kali mno. Usijaribu hata kuionja mihadarati hiyo. Wapo wengi walioanza kutumia mihadarati kimzaha tu. Sasa hivi wanajiuma kidole na kulia kilio cha mbwa mdomo juu. Kifo nacho kimewatanulia kinywa cha mamba na kuwakodolea macho ya bundi. Ukitaka kuishi kwa miaka na mikaka, epuka matumizi ya mihadarati.
- Kulingana na ufahamu, ni kweli kuwa kila mtu;
- hutumia wakati wake kwa njia sawa na wengine.
- hufanya mambo yanayofanana na ya wengine katika wakati wake.
- hupata muda unaotoshana na wa wengine.
- hupewa wakati kulingana na bidii yake.
- Aya ya kwanza inashauri kuwa mhusika;
- aende kanisani kila wakati na kumwomba Mungu.
- atumie wakati wake kujenga uhusiano.
- ahakikishe kuwa anasoma vitabu vya kutosha.
- ampe Mungu nafasi ya kwanza katika maisha yake.
- Kupiga dua' ina maana gani jinsi ilivyotumika katika kifungu?
- kusali
- kufanya bidii
- kusoma
- kuendelea
- Jambo gani ambalo anayeshauriwa hawezi akafanya akiwa nyumbani kwao?
- Kucheza na ndugu zake
- Kusoma
- Kuuza dukani
- Kufua nguo na kuzipiga pasi
- ...mizizi ya elimu ni michungu lakini matunda yake ni matamu...' ni maneno yenye maana gani?
- Masomo yenyewe ni kama mizizi ikiwa pamoja na matunda.
- Faida za masomo hutokea baada ya kuvumilia hali ngumu tunaposoma
- Matatizo ya masomo huwa mengi na yenye uchungu hadi mwisho.
- Mazao ya mimea hayawezi yakawa matamu iwapo mizizi si michungu.
- Ufahamu unaeleza kuwa michezo huimarisha
- maadili na uchumi.
- umoja na viungo.
- afya na uhusiano.
- afya na tabia.
- Kulingana na aya ya nne, anayetaka kuwa na tabia nzuri anashauriwa kufanya nini?
- Kufuata ushauri wa walimu na wazazi
- Kuandamana na marafiki watovu wa nidhamu
- Kutembea na marafiki wenye tabia nzuri
- Kuepuka matumizi ya dawa za kulevya na tabia mbaya
- Aya ya mwisho inashauri kuwa;
- mhusika asitumie mtandao ili asiwe na tabia mbaya.
- mhusika asitazame runinga usiku wala mchana.
- mhusika aepuke ugonjwa wa Korona.
- mhusika awe mwangalifu anapotumia mtandao.
- Nini kinacholinganishwa na sumu katika ufahamu?
- mtandao
- dawa za kulevya
- uvivu
- tabia mbaya
- Kulingana na aya ya mwisho, mtu asiyetumia mihadarati
- huishi bila magonjwa yoyote.
- huwa na marafiki wengi.
- huishi kwa muda mrefu.
- hufaulu maishani.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31-40.
Mathayo alikuwa mwanafunzi wa darasa la saba katika shule ya Eshikalame. Alikuwa mtoto mwerevu sana. Mungu alimjalia akili za sumaku. Alinasa kila kilichofundishwa na mwalimu yeyote. Alifaulu katika masomo mengi. Wanafunzi wengi walitamani sana kuwa kama yeye. Wengi walimwendea kwa ushauri na msaada wa kimasomo. Hata hivyo, Mathayo mwenyewe hakuishi maisha ya furaha. Umaskini wao kule nyumbani ulimuudhi. Alikuwa na mzazi mmoja pekee aliyefanya kazi za kijungujiko pale kijijini ili kukidhi mahitaji ya mwanawe wa pekee. Zaidi ya umaskini huo, kilichomkasirisha zaidi ni hali ya mama yake kimaumbile. Mama yake alikuwa na jicho moja tu, alikuwa chongo. Mathayo hakutaka kabisa kujihusisha na mama yake. Alidhani kuwa wenzake walimcheka kutokana na ulemavu wa mama yake.
Katika shule ya upili, Mathayo hakuwahi kumwita mama yake katika mkutano wowote wa wazazi shuleni. Wakati wa likizo, alienda tu nyumbani kwa kukosa mahali pengine pa kuelekea. Mama alipomuuliza kwa nini wazazi hawakwenda shuleni kwa mkutano wowote, alisema kuwa walimu walitaka kuutumia muda wao katika masomo ya wanafunzi badala ya kupoteza muda wakifanya mikutano na wazazi. Mathayo aliendelea kuwa mchwa katika masomo. Alitia fora katika kidato cha kwanza hadi cha nne. Kama hakuwa nambari ya kwanza, alikuwa ya pili au ya tatu. Katika mtihani wa kidato cha nne, alipata alama za kumezewa mate. Alijiunga na chuo kikuu katika jiji moja katika nchi hiyo. Katika chuo hicho hakulegeza kamba. Alipokamilisha masomo yake, alipata kazi iliyokuwa na mshahara mzuri. Matatizo aliyopitia kitambo aliyasau kabisa.
Ajabu ni kwamba Mathayo hakutaka kabisa kurudi kijijini kule ambako mama yake aliishi. Wanakijiji walishangaa walipomwona mama yule akiendelea kuteseka katika maisha ya umaskini. Ilipotokea kuwa Mathayo ameenda kijijini, japo kwa nadra sana, hakukaa kwa zaidi ya saa nne. Alimbagia mzigo wa bidhaa na kung'oa nanga kurudi kule mjini. Mkewe alipomwuliza kuhusu wazazi wake, alisema kuwa alikuwa yatima. Alimweleza kwamba alikuzwa na kusomea katika makao ya watoto wasiokuwa na wazazi.
Siku moja Mathayo alipata ujumbe kuwa mama yake alikuwa mgonjwa, hali mahututi kule nyumbani. Aliingia ndani ya shangingi lake na kutua kijijini. Mama alikuwa hajiwezi kutokana na ugonjwa. Hakujua aingiaye wala atokaye. Kwenye meza palikuwa na barua, "Kwa mwanangu Mathayo. Mimi ninaona ni kama nitaaga dunia kutokana na ugonjwa huu. Hata kama sijakuachia chochote cha maana, ninakuachia jicho langu. Ulipokuwa mdogo, uligongwa na kijiti mkicheza na wenzako. Jicho lako liliumia kiasi cha kutoweza kuona tena. Nilijitolea kulipeana jicho langu moja ili wewe mwanangu usiwe chongo bali uyaone maisha vizuri. Hii ndiyo sababu huwa sina jicho moja mwanangu. Kwaheri ya kuonana."
Mathayo alipigwa na butwaa nusura azimie. Kwa kasi ya umeme, mama yake aliingizwa katika gari na kukimbizwa hospitalini. Mathayo aliagiza afanyiwe matibabu ya hali ya juu zaidi hadi apate nafuu. Pale kwenye pambajio, Mathayo alilia kwa kite huku akimfafanulia mkewe kisa cha maisha yake tangu mwanzo hadi mwisho.
- Aya ya kwanza inaeleza kuwa;
- Mathayo alifaulu katika masomo yote shuleni.
- Mathayo alikuwa na mzazi mmoja baada ya kifo cha baba yake.
- Mathayo alichekwa na wenzake kutokana na ulemavu wa mama yake
- Mathayo hakupendezwa na umaskini wao na ulemavu wa mama yake.
- Kulingana na ufahamu, 'kazi za kijungujiko' ni kazi zenye;
- kutumia nguvu nyingi
- kufanywa kwa kulazimishwa
- kufanywa kwa ushirikiano
- malipo ambayo ni kidogo
- Katika shule ya upili,
- Mathayo aliongoza katika mitihani iliyofanywa
- Walimu hawakutaka kupote wakifanya mikutano na wazazi.
- Mathayo alifanya vizuri katika mitihani yote.
- Mathayo aliwaambia wenzake kuwa alikuwa yatima.
- Maneno 'aliendelea kuwa mchwa' ni mfano wa fani gani ya lugha?
- Tashbihi
- Sitiari
- Nahau
- Tanakali
- Kifuungu hiki kinaonyesha kuwa Mathayo alikuwa na tabia gani?
- mwongo na mwenye bidii
- mjanja na mzembe
- mjanja na karimu
- mwenye bidii na mwaminifu
- Methali gani isiyoweza kurejelea ujumbe ulio mwishoni mwa aya ya pili?
- Achanikaye kwenye mpini hafi njaa.
- Dau la mnyonge huendeshwa na
Mungu. - Baada ya dhiki ni faraja.
- Damla mnyonge haliandi inshi
- Mathayo alikamilishia masomo yake katika kiwango gani?
- Shule ya msingi
- Chuo kikuu
- Shule ya chekechea
- Shule ya upili
- Mama wa Mathayo alikuwa mzazi bora kwa kuwa
- alimuuliza mwanawe kwa nini wazazi hawakuitwa shuleni.
- alimwandikia mwanawe barua kabla ya kuaga dunia.
- alijinyima na kujikosesha ili mwanawe aishi vizuri.
- alimlipia mwanawe karo katika shule nzuri zaidi nchini.
- Unadhani kwa nini Mathayo alikuwa akilia katika aya ya mwisho?
- Hakutamani kulitumia jicho alilopewa na mama yake.
- Aliona aibu kumweleza mkewe kuwa huyo ndiye aliyekuwa mama yake.
- Alihuzunishwa na habari za kifo cha mama yake.
- Aliaibikia maovu aliyomtendea mama yake.
- Funzo kuu linalopatikana katika kifungu hiki ni lipi?
- Tunafaa kuvithamini vilivyo vyetu hata vikiwa havipendezi.
- Hatufai kuwasaidia watoto ambao baadaye watatudharau.
- Mtoto asiishi mjini baada ya kukamilisha masomo yake.
- Tunafaa kuoa mke wa kutoka katika kijiji chetu ili tusiwadharau wazazi.
MWONGOZO WA KUSAHISHA
INSHA
Andika insha itakayokamilika kwa maneno yafuatayo.
.....................................................Hakika, siku hiyo ilikuwa ya furaha sana. Tuliwasili nyumbani tukiwa tumechoka huku tukicheka kwa furaha na kumshukuru Mungu.