Displaying items by tag: kiswahili
Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 End of Term 3 November 2022 Exams Set 2
MASWALI
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1-5.
(Mwamba na Baruti ni wakulima katika kaunti ya Jashotamu. Yafuatayo ni mazungumzo yao walipokutana kijijini.)
Baruti:Salaam aleikum bwana Mwamba! Sikudhani kuwa tungekutana hapa wakati kama huu. Niliarifiwa kuwa ulisafiri hadi Mchangabaridi kwa maonyesho ya kilimo. (Wanakumbatiana kwa furaha)
Mwamba:Aleikum salaam yakhe. Sikupata uwezo wa kufika huko bwana. Mazao niliyoyapeleka sokoni hayakupata wateja kutokana na kuwa hayakuwa bora kama msimu uliopita. (akionyesha uso wa majonzi)
Baruti:Inawezekana kuwa ulitumia mbinu zisizofaa za ukulima. Mbolea uliyokuwa ukitumia haikuwa salama kwa udongo na hata mazao. Nilikushauri kutumia samadi zaidi badala ya mbolea nyingi za madukani.
Mwamba:Ni kweli ndugu Baruti. Tatizo ni kuwa tayari nilikuwa nimekwishayamimina makopo kadhaa ardhini. Matokeo yake ni kuwa maboga na matikiti niliyoyavuna hayakuwa lolote wala chochote... madogo na yenye rangi isiyopendeza.
Baruti:(Huku akimliwaza kwa kumpapasa bega) Usihofu bwana mkubwa. Naelekea mkutanoni sasa. Nitakaporudi, nitakupigia simu ili tukutane pale Makutano mkahawani nikupe ushauri zaidi kuhusu mbinu bora za kilimo.
Mwamba:Inshallah bwana! Tupatane wakati huo.
- Bwana Baruti hakutarajia kukutana na bwana Mwamba kwa kuwa
- kulikuwa na giza nene.
- bwana Mwamba alipaswa kuhudhuria maonyesho.
- bwana Mwamba hakupenda kutembea kijijini.
- kazi zilikuwa nyingi mashambani.
- Bwana Mwamba hakuweza kuhudhuria maonyesho ya kilimo kwa sababu
- yaliandaliwa mbali mno na kijiji chao.
- hakutaka kuhudhuria maonyesho hayo
- hakuwa na pesa za kumfikisha huko.
- maonyesho hayo hayakuwa na maana kwake.
- Mazao ya bwana Mwamba hayakuweza kununuliwa kwa sababu
- hakujua mbinu bora za kuvuna.
- yalikuwa bora zaidi.
- haukuwa msimu mzuri.
- hayakuvutia.
- Mazao yaliyotajwa katika mazungumzo haya ni
- matikiti na maboga.
- mboga na matikiti.
- maharagwe na maboga.
- matikiti na mahindi.
- Bwana Baruti alikuwa amemshauri bwana Mwamba
- kutumia samadi zaidi.
- kuhudhuria maonyesho ya kilimo.
- kukutana naye huko Makutano.
- kuhudhuria mkutano.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 6 hadi 9.
Kijiji cha Twangapepeta kilikuwa kimekumbwa na janga la maporomoko ya ardhi. Japo hakuna aliyeaga dunia, nyumba nyingi zilifunikwa na udongo. Kwa kuwa wakazi waliishi kwa upendo, waliamua kuungana pamoja ili kuzisaidia familia zilizoathirika. Waliamua pamoja kuwajengea wenzao makao mapya katika maeneo salama. Ingawa mwanzoni ujenzi huo ulionekana kuwa kazi ngumu na nzito, kufanya kazi pamoja kuliifanya iwe rahisi ajabu.
Vilevile, kila mmoja alifanya kazi kwa zamu ili kuimaliza kazi hiyo haraka. Serikali nayo haikuachwa nyuma. Iliwasaidia wanakijiji walioathirika kwa kuwapa mahitaji muhimu kama vyakula, dawa, mavazi na maji. Kufanya kazi bega kwa bega na serikali kuliwapa moyo waathiriwa.
- Ni kwa nini wanakijiji waliamua kuwajengea wenzao makao mapya?
- Walikuwa na upendo.
- Walitaka kujionyesha.
- Walikuwa na pesa nyingi.
- Kujenga kulikuwa rahisi.
- Nijanga gani lilikikumba kijiji cha Twangapepeta?
- Mafuriko ya kutisha.
- Ukame wa hali ya juu.
- Maporomoko ya ardhi.
- Magonjwa ya kila aina.
- Mahitaji muhimu yaliyotajwa si pamoja na
- vyakula.
- dawa.
- mavazi.
- elimu.
- Serikali iliposhirikiana na wanakijiji, ilionyesha kuwa
- haraka haraka haina baraka.
- kidole kimoja hakivunji chawa.
- serikali ina mkono mrefu.
- heshima si utumwa.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 10 hadi 12.
Maisha ya mwanadamu yana changamoto. Pia yana mazuri na mabaya. Mtu akitaka kuishi vizuri hapa duniani, ni muhimu amtegemee Mungu. Wahenga walisema kuwa mwomba Mungu si mtevu. Ni lazima mwanadamu awaheshimu wanadamu wenzake kwa sababu heshima si utumwa. Mwanadamu anafaa kuwa mwadilifu na asiyejiingiza katika mambo mabaya kama vile ulevi, wizi, chuki, vita na uvivu. Awaepuke marafiki wabaya ambapo hawana faida yoyote kwake. Hawa matokeo yao huwa ni hasara tu. Ni vizuri mwanadamu aipende elimu kwa sababu elimu ni ufunguo wa maisha mazuri. Mtu anafaa aitumie elimu kujiendeleza na kuwaendeleza wengine. Ni jambo muhimu mwanadamu kuitunza afya yake na ya wengine. Kila mtu anafaa kujiepusha na mambo ambayo yanaweza kuhatarisha maisha yake na ya wenzake. Vyema pia ni kuyatunza na kuyalinda mazingira. Tukumbuke kwamba tukiyatunza mazingira, nayo yatatutunza. Tukiyaharibu nayo yatatuharibu.
- Mwandishi anasema kuwa maisha ya mwanadamu yana
- changamoto.
- mazuri.
- mabaya.
- mabaya, changamoto na mazuri.
- Ni gani orodha ya mambo mabaya yaliyotajwa katika kifungu ulichokisoma?
- Ulevi, uadilifu na chuki.
- Bidii, vita na uvivu.
- Wizi, chuki na uvivu.
- Chuki, vita na lawama.
- Kwa maoni yako, tunawezaje kuyatunza na kuyalinda mazingira? Kwa
- kutumin kuni zaidi katika upishi.
- kuchoma makaa kwa wingi.
- kupanda miche ili kukuza miti.
- kuoga na kufua mitoni.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswall 13 hadi 15.
Siku iliyofuata, tulirauka tayari kuianza safari yetu ya kurejea jijini Bisenta. Ingawa tulianza safari mapema, tulikwama katika eneo la ukaguzi la Soweto. Magari mengi yaliyotutangulia yalikuwa pale pale, nayo yakatuzuia kupita. Ilibidi nasi tusubiri ukaguzi ukamilike. Kilichofurahisha mno ni mbinu ya usafiri ya wale wasio na magari ya kibinafsi. Kwa kuwa eneo hili halina huduma ya mabasi wala matatu, abiria hulazimika kusafiri juu ya malori. Wakati mwingine, malori mengine huwa yamewabeba wanyama kama ng'ombe mbuzi na kondoo hivyo huwabidi wasafiri kuwa makini ili wasiwaangukie wanyama hawa. Safari kama hii huchukua muda wa hadi siku tatu kufika Bisenta na huwabidi wasafiri kuvumilia miale ya jua, upepo, vumbi na hata mvua. Wanaobahatika kusafiri kingwana hukaa kando ya madereva ingawa huwa ghali mno.
Hatimaye magari yalianza kuondoka moja moja huku yakiacha mawingu ya vumbi yaliyomtatiza dereva wetu, Rungu, kuendesha vizuri.
- Ni kwa nini kina mwandishi walikwama walipofika Soweto?
- Kulikuwa na vumbi jingi barabarani.
- Kulikuwa na shughuli ya ukaguzi.
- Hakukuwa na namna ya usafiri.
- Watu walikuwa wengi barabarani.
- Kulingana na habari hii, ni nini kilichofurahisha?
- Jinsi wasafiri walivyowaangukia wanyama
- Namna Rungu alivyoshindwa kuendesha gari.
- Mbinu ya usafiri ya wale wasio na magari yao.
- Wasafiri walivyovumilia jua, upepo, vumbi na mvus.
- Ni nini kilimzuia Rungu kuendesha vizuri?
- Jua.
- Mvua.
- Upepo.
- Vumbi.
Soma kifungu kifuatacho. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa
Chakula _16_ ni ugali. Chakula hiki hupikwa kwa kutumia_17_. Chakula hiki huupa mwili wangu nguvu ya _18_ na pia kufanya kazi. Ugali huweza kuliwa pamoja na nyama, samaki, maziwa au mboga. Mimi hufurahia ugali kwa kabeji. Kabeji ni _19_nazo mboga huipa miili yetu vitamini ambayo hutukinga tusipate _20_
-
- nikipendacho
- ninakula
- nitakayo
- nipendacho
-
- nyanya
- unga
- vijiko
- mikono
-
- kusinzia
- kulala
- kunguruma
- kucheza
-
- mboga
- boga
- mtamu.
- zuri
-
- shida
- kuungua
- magonjwa
- dawa
Katika swall la 21-30. Jibu swall kulingana na magsize uliyopewa.
- Kitenzi piga katika kauli ya kutendana huwa
- pigwa.
- pigana
- pigiwa.
- pigika.
- Ni neno lipi halijaambatanishwa na kisawe chake?
- Shule--darasa.
- Haraka--upesi.
- Tarakilishi--kompyuta.
- Runinga--televisheni.
- Tambua nomino iliyo katika ngeli ya KU-KU
- Kuni.
- Kuku.
- Kuona.
- Kumi.
- Chagua wingi wa sentensi ifuatayo: Upishi umekamilika.
- Upishi umekamilika.
- Wapishi wamekamilika.
- Pishi zimekamilika.
- Mapishi yamekamilika.
- Chagua nahau inayohusiana na usafi.
- Piga pasi
- Angua kicheko
- Piga hatua
- Kata kamba
- Ni methali gani kati ya hizi inahusu bidii?
- Tamaa mbele mauti nyuma.
- Mtaka cha mvunguni sharti ainame.
- Kawia ufike.
- Haraka haraka haina baraka
- Ni ipi orodha ya nomino za makundi pekee?
- Umati, upepo, utajiri.
- Sukariguru, batamzinga,kombamwiko.
- Kusoma, kupika, kucheza.
- Kicha, mlolongo, safu.
- Ni ukifishi upi ulio sahihi?
- Darasa la kina Roda limepakwa rangi.
- Kwa nini hamjawaletea wageni sharubati.
- Uchaguzi wa mwaka huu ulikuwa wa amani furaha na upendo.
- Tutaandika insha alhamisi ijayo.
- Bangili ni pambo ambalo huvaliwa wapi?
- Shingoni.
- Mguuni
- Mkononi.
- Kiunoni.
- Chagua orodha ya wanyamapori pekee.
- Farasi, paa, tembo.
- Punda, twiga, pundamilia.
- Kondoo, ng'ombe, mbuzi.
- Ndovu, kifaru, nyati
MWONGOZO WA KUSAHIHISHA
|
|
|
Kiswahili Questions and Answers - CBC Grade 6 KPSEA End Term 3 2022 Set 2
Maswali
Soma mzungumzo yafuatayo kishu ujibu maswali 1-4
Jona: Shikamoo dada? Umetulia sana hapa jikoni. Unafanya nini?
Hadija: Marahaba ndugu yangu. Nataka nimalize kuosha vyombo. Ningependa kumrahisishia mama kazi atakapokuja kuandaa chajio.
Jona: Huo ni uamuzi wa busara. Hebu nikusaidie ili tumalize kazi hiyo nawe ukafanye kazi ulizopewa shuleni.
Hadija: (Akitabasamu) Asante. Naona unaelewa kuwa kinga na kinga ndipo moto liwakapo.
Jona: (Huku ukizichukia suhuni azioshe kwenye kuro) Wajua ni jukumu letu kuwasaidia wazazi hapa nyumbani. Huu ndio mchango wetu katika kupunguza matumizi. Au wasemaje dada?
Hadija: Kweli kabisa. Hapo umegonga ndipo. Hakuna haja ya wazazi kuwaajiri vijakazi na vitwana wafanye kazi za nyumbani ilhali mzazi ana watoto wakubwa kama sisi.
Jona: Maadamu tumeimaliza shughuli ya usafi naomba uje unielekeze kufanya hesabu mbili zinazonitatiza.
Hadija: Hlewala, nitakusaidia.
Jona: Asante dada. Tahika ndugu ni kufaana, si kufanana.
- Mazungumzo haya yanaonyesha kuwa
- Jona ni mkubwa kuliko Hladija.
- Tadija ni mkubwa kuliko Jona.
- Hadija ni mkubwa kuliko Jona.
- Jona ni mwerevu kuliko Hadija.
- Watoto hawa ni wenye busara kwa sababu,
- wanajua umuhimu wa kuwasaidia wazazi.
- wanafanya kazi za nyumbani badala ya kusoma.
- wanafahamu ubaya wa vijakazi na . vitwana.
- wanaogopa kugombezwa na wazazi wao.
- Usemi hapo umegonga ndipo' una maana. kwamba
- aliyosema Jona si kweli.
- aliyosema Jona hayawezekani.
- aliyosema Jona yanashangaza.
- aliyosema Jona ni ukweli.
- Umuhimu wa ndugu kulingana na mazungumzo ni
- kuishi pamoja.
- kupeana msaada.
- kufanana sana.
- kufanya hesabu.
Soma kifungu kifuatacho kishú ujibu muswali 5 - 8
Kobe alikuwa akitoka cheteni kuuza mboga zake. Siku hiyo, mboga zilinunuliwa zote hata akahitajika kupeleka zaidi. Wateja wake walifurahishwa na mboga zake maadamu hakutumia kemikali zenya madhara. Hakutaka wale waliotumia mboga hizo wadhurike.
Njiani, alikutana na Pundamilia na Ngiri. Aliwasaili kuhusu walikokuwa wakitoka wakati ule. Pundamilia alimjibu, "Tumetoka kupanda miti upande wa mashariki wa msitu huu. Tumegundua kuwa binadamu ameikata miti mingi sana. Hali hii akiendelea kutatokea kiangazi.” Kobe aliwashukuru na kuwapongeza wenzake kwa uamuzi wao wa busara. Kisha akasema, “Hakika mtego wa panya huingia waliokuwemo na wasiokuwemo. Ni muhimu tuzuje hatari ya ukosefu wa mvua kwa kupanda miti. Nitaenda huko kesho nitimize wajibu wangu."
Baada ya hapo, wanyama wale walipungiana mikono, Kobe akajiendea zake. Akilini aliwaza, "kwa nini binadamu hatumii akili yake razini? Tamaa hii ya kukata miti kwa kutaka utajiri wa haraka, si itamwangamiza? Isitoshe, juzi nilipopita karibu na kijiji chao, niliona wamerundika taka kila mahali. Hakika wasipoubadili mkondo huo watajuta baada ya kuathirika.”
- Neno jingine lenye maana sawa na cheteni ni
- sokoni
- nyumbani
- shambani
- mjini
- Kwa nini wateja walizipenda mboga za Kobe? Kobe
- alikuwa rafiki wa kila mtu.
- alikuwa mkulima hodari.
- alijali afya ya wateja wake.
- aliziuza kwa bei nafuu.
- Ahadi aliyotoa Kobe ni kuwa,
- A. angezuia uharibifu wa msitu wao.
- angeenda kupanda miti siku iliyofuata.
- angemshauri binadamu aache kuharibu mazingira.
- angeenda kupeleka mboga upande wa mashariki.
- Tabia za binadamu zinazokashifiwa na Kobe ni
- uchoyo na uharibifu.
- ukatili na uvivu.
- mapuuza na kujitenga.
- tamaa na uharibifu.
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 9 - 12.
(Sunkuli na Malaika wamekutana njiani)
Sunkuli: Habari rafiki yangu?
Malaika: Nzuri mwenzangu sunkuli. Je, safari ya wapi jioni hii?
Sunkuli: Naenda kwa Mama Fatuma kumpekelekea chakula. Amekuwa akiugua tangu juzi. Mama amenituma nikamjulie hali na kumpa maziwa haya
Malaika: Ooh! Bi Fatuma yuaugua. Kumbe ndiposa sijamwona akipita karibu na kwetu hivi karibuni. Wajua hawezi kupita bila kutoa salamu.
Sunkuli: Kwa hakika Bi Fatuma ni mtu wa watu. Watu wote wangemwiga yeye, taifa lingekuwa na mshikamano mzuri sana. Maovu mengi yangeisha kwani kila mtu angemchukulia mwenzake kama ndugu.
Malaika: Haya ukifika kwa Bi Fatuma umpe salamu zangu. Nitaenda kumjulisha mama kuhusu maradhi yake. Nikipata kibali nitaenda kuzuru kesho mwendo wa adhuhuri.
Sunkuli: Sawa Malaika. Nina uhakika kuwa utapewa idhini hiyo. Wema hauozi. Hakuna mtu anayeweza kumnyima Bi. Fatuma msaada.
Malaika: Haya, hebu nenda usije kuchelewa. Kwaheri.
Sunkuli: Kwaheri na uwe na jioni njema,
- Sunkuli alipokutana na Malaika alikuwa,
- akitoka kumsaidia Bi Fatuma.:
- ameenda kuona kama Bi Fatuma aliugua.
- ameenda kumjulia hali Bi Fatuma.
- ametoka kuchukua maziwa kwa Bi Fatuma.
- Neno ooh! ni aina ya
- kielekezi
- kiingizi
- kihusishi
- kiwakilishi.
- Bi Fatuma ni mtu wa watu ndiko kusema,
- anajulikana na watu wengi.
- anasaidiwa na watu wengi.
- amewasaidia watu wote.
- anahusiana vyema na watu.
- Malaika anaahidi kuenda kumsaidia Bi fatuma. Msaada huu utatolewa ikiwa
- atapewa ruhusa.
- atapata wakati
- hatakuwa amepona.
- hatakuwa na kazi nyingine.
Soma kifungu kifuatacho kisha uyajibu maswali 13 - 15
Shawe alikuwa na mazoea ya kuenda msalani mara kwa mara kwa haja ndogo. Mwalimu wake aligundua jambo hilo. Alimwita mlezi wake ofisini mwake. “Asante kwa kuitikia mwito wangu, Naomba umpeleke mwana wako kwenye hospitali achunguzwe," Mwalimu akasema.
Shawe alipelekwa hospitalini kwanza alipimwa uzani wake. Baada ya kadi yao ya matibabu kukaguliwa, walitumwa maabarani. Damu yake ilifanyiwa vipimo. Daktari alimwuliza maswali kadhaa. “Daktari, kibofu changu hujaa haraka nami hushindwa kustahimili,” Shawe alimwambia tabibu. Shawe alipigwa picha ya eksirei. Picha hiyo ilionyesha kuwa mafigo yake yalikuwa na tatizo. Kwa bahati nzuri tatizo liligunduliwa mapema. Alipendekezwa kulazwa hospitalini ili atibiwe himahima. Ndugu zake, majirani na wanafunzi wenzake walimwombea apate afueni.
- Jambo linaloonyesha kuwa Shawe alikuwa na shida ni kwamba
- mwalimu alimwita mlezi wake shuleni.
- alikuwa akienda msalani mara mojamoja.
- alienda kujisaidia mara kwa mara.
- mwalimu alimwona amejikunyata darasani.
- Shawe alikuwa na bahati kwani,
- shida yake haikuwa hatari.
- hakuwa na shida yoyote.
- shida yake iligunduliwa mapema.
- watu wote walimwombea.
- Viungo vya mwili vilivyotajwa hulahta kazi gani?
- Kusukuma damu mwilini.
- Kusafisha damu.
- Kuyeyusha chakula.
- Kuhifadhi mkojo.
Soma kifungu kifuatacho. Kina nafasi 16 mpaka 20. Kwa kila swali umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.
Watu 16 wanashiriki, michezo huwa na afya 17 . Jambo hili huwasaidia 18 magonjwa 19 kuhatarisha maisha yao. Hata hivyo, mtu 20 mazoezi, huathirika kiafya.
16. | A. ambaye | B. ambapo | C. ambao | D. ambayo |
17. | A. mzuri | B. njema | C. jema | D. mwema |
18. | A. kuepuka | B. kuepusha | C. kuepukana | D. kuepukia |
19. | A. zinazoweza | B. inayoweza | C. yanaweza | D. yanayoweza. |
20. | A. akishiriki | B. alishiriki | C. anashiriki | D. asiposhiriki. |
Kutoka swali la 21 hadi la 30 chagua jibu lifaalo zaidi kulingana na maagizo uliyopewa.
- Tumia kiulizi kifaacho zaidi Kimaru aliwauza sungura
- ngapi
- mangapi
- wagani
- wangapi
- Lifuatalo ni jedwali la maneno. Kundi lipi lina vielezi pekee?.
A kali tamu safi bora B pole pole kwa kasi sana haraka C sahani kikombe maua uteo D juu ya kando ya katikati ya ndani ya - Bakari ni kaka' wa mama yangu. Kwa hivyo nitamwita
- mwamu
- mpwa
- ami
- mjomba
- Andika wingi wa:
Birika hilo lina chai nyingi.- Birika hizo zina chai nyingi.
- Mabirika hizo zina chai nyingi
- Mabirika hayo yana chai nyingi.
- Birika hayo yana chai nyingi.
- Tegua kitendawili kifuatacho: .
Chauma bila meno, chaumiza bila silaha.- Siafu.
- Moto.
- Chungu.
- Kiraka
- Nomino maziwa na mazingira huorodheshwa katika ngeli moja. Itambuc. ngcli hiyo.
- YA - YA
- I-ZI
- U - YA
- U-ZI
- Methali zifuatazo zinaonyesha ushirikiano.
Ni ipi iliyo tofauti?- Mgaagaa na upwa hali wali mkavu.
- Umoja ni nguvu.
- Wawili si mmoja.
- Kidole kimoja hakivunji chawa.
- . Shairi ambalo huwa na mishororo mitatu katika kila ubcri ni
- tarbia
- tathnia
- tathlitha
- kibwagizo.
- Mtu mwenye sifa ya upole hufananishwa na kiumbe yupi?
- Fisi
- Punda
- Paka
- Njiwa.
- Kufanya kazi kwa ushirikiano ni :
- kujifunga nira
- kupinda mgongo
- kufanya kikoa
- kupiga deki.
Majibu
|
|
|
Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 End of Term 3 November 2022 Exams Set 1
MASWALI
SEHEMU 3: Ufahamu
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali
Siku takapoamka, ujipate na maskini,
Usije ndugu kumaka, ukakosa tumaini,
Jua kuna kuikuka, aka unajithamini.
Ufukara haudumu, unahitaji juhudi
Mosi ukienda shuleni, masomo makinikia,
Elimu kuithamini, hadi kuimalizia,
Utapata tumaini, uje kujitegemea,
Ufukara haudumu, unahitaji juhudi.
Kazi itakapokuja, pesa uanze kuigiza,
Jua kesho inakuja, sifanye kwangamiza,
Usije ukazifuja, maisha kuangamiza,
Ufukara haudumu, unahitaji juhudi.
Pesa zinapokwezesha, kununua yako mali,
Ni muhimu kuboresha, kwa hali pia kwa mali,
Hekima kuzalisha, kimoja kiwe kiwili,
Ufukara haudumu, unahitaji bidii.
Chunga gharama nyumbani, vifaa napotumia,
Si mojawapo bafuni, si umeme kuonea,
Lishe kibaki mezani, yafaa kuhifadhia,
Ufukara haudumu, unahitaji juhudi.
- Taja vina vya kati vya ubeti wa pili;
- -a
- -ni
- -na
- -ka
- Shairi hili lina beti ngapi?
- Nne
- Tano
- Nane
- Kumi na sita
- Taja kibwagizo cha shairi bili.
- mosi ukienda shuleni masomo makinikia
- siku yanapoamka ujipate maskini
- Ufukara haudumu unahitaji juhudi
- chunga gharama, nyumbani vifaa napotumia
- Ubeti wa kwanza una mizani ngapi?
- 16
- 64
- 8
- 17
- Shairi hili ni la aina gani?
- Tathnia
- Tathlitha
- Tasdisa
- Tarbia
- Ubeti wa tatu unatuhimiza kuwa;
- tumia pesa au mali vizuri
- tuwe na hekima
- tufanye bidii
- tuthamini elimu
- Neno 'gharama' lina silabi ngapi?
- Saba
- Tano
- Tatu
- Nane
- Mtu anayetunga shairi huitwa;
- Manju
- Sogora
- Malenga
- Mghani
- Kulingana na shairi hili kumaliza ufukara tunafaa kufanya nini?
- Kuamka mapema
- Kufanya bidii
- Kununua mali
- Kula lishe bora
- Kibwagizo cha shairi hili kina mizani ngapi A.
- 16
- 8
- 64
- 32
Soma ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali yafuatayo
Nyani na binamu walikuwa marafiki wa kufa kuzikana. Waliishi pamoja wakisaidiana kazi za bani. Wote walikuwa na ngozi laini na nyororo. Siku moja nyani na binamu walitayarisha maharagwe kuvaweka kwenye sufuria. Waliwasha jiko la seredani na kuweka sufuria ya maharagwe juu ya yake.
Kama ilivyokuwa kawaida yao, nyani na binamu walienda kuoga mtoni, nyani alijisugua kichwa na mwili wote. Binamu pia alifanya vivyo hivyo huku maharagwe yakiendelea kuiva.
Hatimaye nyani na binamu yake walienda nyumbani. Walijipakulia maharagwe yaliyoiva. Kila mmin akapata kiwango sawa na mwengine. Nyani alikula sehemu vake, naye binamu ale sehemu yake hin ani hushiba. Nyani alitamani kujiongeza mlo. Hivyo basi alitafuta nama va kuiongezea chakula
Maswali
- Nyani na binadamu walikuwa marfiki wa kufa kuzikana. Hii ina maana gani?
- Wote walikufa
- Walipendana sana
- Walisaidiana
- Walifahamiana
- Nyani na binadamu walipika chakula gani?
- Madondo
- Pure
- Ndovi
- Wali
- Nyani na binadamu walikuwa na mazoea ya kufanya nini?
- Kupika maharagwe
- Kuoga mtoni
- Kuwasha jiko
- Kula sima
- Nyani na binadamu walitumia jiko la seredani je, jiko hili linatumia nini?
- Kuni
- Mafuta
- Makaa
- Gesi
- Mbona nyani alipanga njama ya kujiongeza chakula?
- Alikuwa mlafi
- Alitaka kuwapelekea wanawe
- Kilikuwa kitamu sana
- Hakushiba
- Taja methali moja ambayo inaonyesha ushirikiano kati ya nyani na binadamu?
- ajizi ni nyumba ya njaa
- umoja ni nguvu utengano ni udhaifu
- bidii hulipa
- mwana hutazama kisogo cha ninaye
- Nyani na binadamu walipenda kuoga mtoni. Neno mto liko katika ngeli gani?
- PA-KU-MU
- U-I
- LI-YA
- I - ZI
Jaza nafasi zilizoachwa kwa majibu yanayofaa
Safari_18_ nilikuwa _19_ dhidi ya _20_ kinywani chochote_21_ kuepukana na kutiliwa dawa za kulevya ambazo zingedhuru afya yangu.
-
- kilifika
- itakapofika
- imefika
- ilipofika
-
- nimeruhusiwa
- nimeonywa
- nimepewa
- nimekabiliwa
-
- kunyweshwa
- kunywewa
- kukunywa
- kunywa
-
- ndani ya njia
- njia
- karibu na njia
- njiani
- Ni lipi jibu mwafaka kwa maamkizi makiwa?
- yamepita
- jaala
- nawe pia
- asante
- Ni lipi si pambo la mwili katika kundi lifuatalo?
- Aproni
- Mkufu
- Herini
- kidani
- Chagua nomino ya dhahania katika orodha inayofuata.
- kiamshakinywa
- maisha
- Jumamosi
- tita-la kuni
Andika wingi wa sentensi hii
Chupa yake imevunjika.
- Chupa zao zimevunjika
- Chupa zake zimevunjika
- Vyupa vya vimevunjika
- Machupa yao yamevunjika
- Chagua methali yenye maana sawa na Mgaagaa na upwa hali wali mkavu.
- asiyesikia la mkuu huvunjika guu
- mtaka cha mvunguni sharti ainame
- majuto ni mjukuu
- heshima si utumwa
- Ni neno lipi kati ya maneno haya halina maana sawa na ugonjwa?
- Maradhi
- Uele
- Uwele
- Ukongo
- Chagua kundi la maneno ya ngeli ya U-ZI
- upishi, ulezi uovu
- ukuta, nguo, nywele
- mkoba, miti, mkono
- nyasi, nywele, uta
- Ni neno lipi limeambatanishwa vizuri na kinyume chake?
- Rafiki - mwandani
- Simama - usisimame
- Tabasamu - cheka
- Nuna - tabasamu
- Chagua kiunganishi katika sentensi ifuatayo Alinunua koti kubwa lakini halipendezi.
- alinunua
- lakini
- kubwa
- halipendezi
INSHA
Andika insha ya kusisimua ukizingatia mada ifuatayo;
CHAKULA NIKIPENDACHO
MWONGOZO WA KUSAHIHISHA
|
|
|
Kiswahili Questions and Answers - CBC Grade 6 KPSEA End Term 3 Exam 2022 Set 1
Maswali
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1-5.
(Mchezaji wa kabumbu amekutana na mkufunzi wake. Wanajadiliana kuhusu hali ya mchezaji.)
Kocha : Vipi kaka? Habari za asubuhi? Waonekana kuchechemea. Kulikoni? (akionyesha mshangao mkuu)
Mchezaji: Habari nzuri ila si sana. Ni kweli, nachechemea kutokana na maumivu ya goti langu la kushoto. Nadhani unakumbuka kilichotokea katika uwanja wa Mwagajasho tulipocheza dhidi ya timu ya Majimoto.
Kocha : Naam, nakumbuka ulichezewa visivyo ikakubidi kuuaga mchezo. Nilidhani ulipata nafuu. Je, umepokea matibabu yoyote hadi sasa?(alimgusa na kumpapasa gotini)
Mchezaji: Naam, bata sasa nimetoka kupokea huduma pale hospitalini Dawatamu. Daktari Siha amenishauri kuufanyisha mazoezi mguu huu ili goti lipone upesi. (akiukunja na kuunyosha mguu wake wa kushoto)
Kocha : Nakutakia afueni ya haraka bwana Kadenge. Kumbuka kuwa tutakuwa na mechi kali dhidi ya timu ya Wazee Hukumbuka wiki ijayo. Mchezaji: Aa! Nitakuwa nimepona kocha. Asante sana kwa kunikumbusha.
Kocha : Hewallah bwanamogo. Tutaonana wakati mwingine majaliwa
- Hali ya mchezaji ilikuwa shwari ila
- viungo vyake.
- miguu yake
- magoti yake.
- goti lake
- Je, ni nini kinatueleza kuwa mkufunzi alimjali mchezaji wake?
- Alimkumbusha mchezaji kuhusu mechi iliyokaribia.
- Alimshughulikia mchezaji wake vilivyo kimatibabu.
- Alitaka kufahamu sababu ya mchezaji kuchechemea.
- Alimsaidia mchezaji kunufanyisha mgw mazoezi.
- Kulingana na bwana Siba, mazoezi ya Kadenge ni nani?
- Yule mchezaji aliyeumia wakati wa mechi.
- Mkufunzi wa mchezaji yule.
- Mwuguzi katika hospitali ya Dawatamu.
- Daktari katika hospitali ya Dawatamu.
- Je, kocha alipokutana na mchezaji huyo alikuwa ametoka wapi?
- Hospitalini Dawatamu.
- Hatujaelezwa.
- Kwa daktari. '
- Uwanjani.
- Kulingana na mazungumzo haya, mara kwa mara yalikuwa na umuhimu gani?
- Yangemwongeza mchezaji nguvu
- Ili mchezaji awe imara.
- Yangeiponya miguu ya mchezaji .
- Yangeharakisha kupona kwa goti la mchezaji.
Soma kifungu kifuatacho kisha wilbu maswali 6 hadi 8.
Katika enzi za kale, watu hawakuwa wakivaa nguo zozote. Wacheshi husema kuwa walivalia suti ya Mungu! Miaka ilivyozidi kubingirika, watu wakaona umuhimu wa kujisitiri . Hapo, wakaanza kujifunika kwa ngozi za wanyama. Baadaye, walianza kutumia mablanketi na mashuka.
Leo hii tunapozungumza, kuna aina nyingi sana za mavazi kiasi kuwa ni vigumu kuchagua ya kununua. Kama ilivyo kawaida, watu hutofautiana katika chaguzi za aina na rangi za mavazi. Yapo mavazi ambayo ni ya wanaume pekee. Vilevile, kunayo yale ambayo ni ya wanawake tu. Baadhi ya haya ya kike ni kanchiri au sidiria, marinda, sketi, blauzi na mengineyo. Watoto nao hawajaachwa nyuma Yapo mavazi ambayo ni ya watoto tu. Je, wafahamu kuwa kuna mavazi yanayoweza kuvaliwa na wanawake na pia wanaume?
- Kulingana na taarifa,
- zamani watu walivalia mavazi ya bei rahisi.
- hakukuwa na nguo zozote kitambo.
- kitambo, watu walikuwa na tatizo la kuchagua nguo za kununua.
- watu walijisitiri kwa majani mapana
- Ni jibu gani laonyesha hatua alizopitia binadamu hadi kuufunika mwili wake?
- Mablanketi na mashuka, mavazi, ngozi za wanyama.
- Mavazi, mablanketi na mashuka, ngozi za wanyama.
- Ngozi za wanyama, mablanketi na mashuka, mavazi.
- Mablanketi na mashuka, mavazi, ngozi za wanyama.
- Kulingana na ufahamu huu, watu wa sasa tatizo gani kuhusiana na nguo?
- Nguo zilizopo hazimtoshelezi kila mmoja.
- Wingi wa aina za mavazi hufanya kuchagua kuwe kungumu.
- Mavazi mengi ya kisasa ni ya wanawake na wanaume.
- Kunayo mavazi ya wanaume, wanawake na watoto.
- Baadhi ya mavazi ya wanawake katika kifungu ni ana
- marinda, sidiria na blauzi.
- sketi, chupi na kanchiri.
- suruali, marinda na sidiria.
- kanchiri, tai na sketi.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 10 hadi 12.
"Wageni wetu waheshimiwa, wazazi, walimu, wakufunzi wa michezo, wachezaji na wanafunzi wenzangu, habari za wakati huu? Hakika, bila kubahatisha maneno, leo ni siku muhimu sana katika tukio ya humu shuleni ya mwaka huu. Naam, ni siku ya kutiwa katika rekodi ya kumbukumbu ili isisahaulike na yeyote. Kama tujuavyo sote, michezo ni njia mojawapo ya kuonyesha uwezo na talanta alizotujalia Mwenyezi Mungu. Naomba nigusie faida kadhaa za michezo. Michezo huipa miili yetu na kutufanya tuwe na afya bora. Kupitia michezo, uwezo wetu wa kushiriki vyema katika timu huonekana. Viungo vyetu hufanya kazi vizuri, uhusiano wetu na wenzetu hujengeka na mawasiliano miongoni mwetu huwa bora. Kujihusisha na michezo baada ya kazi za darasani na nyumbani hupumzisha akili. Tunapojiandaa kushiriki mchuano wa leo, nawatakia kila la heri. Asanteni kwa kunisikiliza."
- Unadhani aliyetoa maelezo haya alikuwa yupi?
- Mzazi.
- Mwalimu
- Mwanafunzi.
- Mchezaji.
- Ni gani hapa si umuhimu wa michezo
- kulingana na kifungu hiki?
- Miili yetu hupata nguvu na kutufanya tuwe na afya bora.
- Baadhi ya magonjwa hutuondoka miilini tukishiriki michezo.
- Uhusiano baina yetu na wenzetu huimarika.
- Michezo huleta pumziko la akili baada ya shughuli fulani ngumu.
- Kuna uwezakano kuwa siku hiyo ilikuwa ya
- kuwatakia wachezaji kila la kheri.
- kufungwa rasmi kwa shule.
- kuzawidiwa kwa wachezaji bora
- michezo shuleni humo.
Soma kifungu kifuatacho kisha vilbu maswali 13 hadi 15.
Kila Jumamosi, mama huenda katika soko la Marikiti ili kuuza bidhaa zake. Yeye huruza matunda ya aina nyingi kama mapapai, maparachichi, maembe, mananasi, machungwa na makarakara. Vile vile, huuza mboga kama kabeji, mchicha na sukumawiki. Aliacha kuuza nyanya na vitunguu baada ya bidhaa hizo kuwa ghali zaidi katika soko kuu.
Mimi ndimi mwanambee katika familia yetu, hivyo, mama huniachia majukumu kila aondokapo. Kaka zangu wawili na dada zangu watatu hunisaidia kufanya kazi pale nyumbani.
Jumamosi iliyopita, mama aliondoka kwenda sokoni kama ilivyokuwa kawaida. Tuliamua kugawana kazi pale nyumbani ili tuzimalize kabla hajarejea kutoka sokoni. Niliwaambia dada zangu wafue, wasafishe nyumba na kupika kishuka. Kaka zangu walitakiwa kufyeka nyasi, kuulengata ua na kuchoma taka. Ghafla, niliskia mlio wa mbuzi wetu. “Ni nani atakayewapeleka mbuzi malishoni?" Nikajiuliza.
- Familia ya kina mwandishi ina jumla ya watu wangapi?
- Saba
- Sita.
- Wanane.
- Watano.
- Ni kwa nini mama wa mwandishi hauzi nyanya na vitunguu?
- Bidhaa hizo hazipatikani katika soko kuu.
- Bei ya bidhaa hizo imepanda mno katika soko la Marikiti.
- Bidhaa hizo zimekuwa ghali mno katika soko kuu.
- Nyanya na vitunguu hazipatikani katika soko la Marikiti.
- Chagua orodha ya bidhaa ambazo mama wa mwandishi huuza.
- Karoti, mboga na nyanya.
- Kabeji, matunda na vitunguu.
- Mayai, matunda na mboga.
- Kabeji, makarakara na maembe.
Soma kifungu kifuatacho. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa
Uchaguzi uliokamilika hivi majuzi ulidhihirisha kuwa, kwa sasa, wananchi ni wapenda amani. Wengi walidhani kuwa, baada ya mshindi wa 16 urais kutangazwa, wakenya wangetafuta silaha za kutoana 17 na kuharibiana mali. Kinyume na hivyo, amani 18 kote. Huu ndio moyo wa uzalendo. Tukubali matokeo na tuendelee kufanya kazi ili kuboresha 19 Ni kweli bayana asiyekubali kushindwa 20 .
16 | A. meza ya | B. dawati la | C. kiti cha | D. kabati la |
17 | A. mamlakani | B. roho | C. ofisini | D. mikono |
18 | A. imetamalaki | B. imepungua | C. imezorota | D. imepotea |
19 | A. uhuru | B. umaskini | C. utawala | D. uchumi |
20 | A. ni mshindi | B. si mshindani | C. si mshindaji | D. ni mshindani |
Katika swali la 21 - 30, jibu swall kulingana na maagizo uliyopewa.
- Ni sentensi gani haijatumia amba kwa usahihi?
- Maua ambayo walichuma yananukia.
- Wageni ambao walingojewa walifika.
- Majina ambao walitajiwa hayakuwa yao.
- Masomo ambayo tulisomeshwa yalitufaa.
- Chagua neno lililo katika ngeli tofauti.
- Mezani.
- Mfukoni.
- Sahani.
- Chumbani.
- Chagua sentensi iliyo katika kauli ya kutendesha..
- Tiko na kosa huandikiana barua.
- Rama ameufunga mlango.
- Mzee Tomoko amepanda miche.
- Mvua kubwa ilikatiza safari
- Ni mnyama yupi hapa baishi majini?
- Samaki.
- Kuchakulo.
- Mamba
- Kiboko
- Tumia kiámbishingeli sahihi kukamilishia sentensi ifuatayo:
Hatuku la uyoga wenye sumu.- U
- ya
- i
- zi
- Chagua wingi wa sentensi ifuatayo: Maji yaliyotekwa yamemwagika.
Maji- zilizotekwa zimemwagika.
- yaliyotekwa yamemwagika.
- iliyotekwa imemwagika.
- waliyoteka yamemwagika.
- Kamilisha methali ifuatayo: Kidole kimoja
- hujaza kibaba
- walaji ni wengi.
- huvikwa pete.
- hakivunji chawa.
- Ni sentensi ipi haijatumia kivumishi kimilikishi kwa usahihi?
- Jirani yangu anaitwa Tindi.
- Madarasa yao yameoshwa vizuri.
- Kina mama yao wana mioyo safi.
- Mjomba wetu hapendi kununa.
- Chagua majina yaliyo katika ngeli ya A-WA.
- Uzi,
- Kuta, nyuzi, ufizi.
- Nzi, kipepeo, kiroboto.
- Utepe, uteo, uchafu.
- Chagua sentensi iliyoakifishwa kwa usahihi.
- Wanyama wafugwao ni pamoja na: ngo'mbe, mbuzi na kondoo.
- Ukienda, ng'ambo uniletec haya: vikoi, saa na mkufu.
- Ala, kumbe unajua kuendesha baiskeli.
- Mwalimu alisema tulete nini kesho.
Majibu
|
|
|
|
|
|
Kiswahili Questions and Answers - Class 7 End Term 2 2022 Set 2
Maswali
Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 hadi 15.Kwa kila pengo, umepewa majibu manne. Chagua jawabu lifaalo zaidi.
Wavyele na washikadau wengine katika 1 ya elimu 2 na wazazi kuhusu 3 la kudumisha nidhamu 4 watoto wa shule. Walimu wanawanyoshea kidole cha 5 wavyele hasa baada ya 6 ya kiboko 7 nchini. Kwa upande wao, wazazi wanajitetea kuwa walimu ndio kushutumiwa maadamu wanashinda 8 watoto hawa 9 . Hata hivyo, suala la nidhamu linahusisha kila mmoja katika jamii.
A | B | C | D | |
1 | shirika | taasisi | sekta | kazi |
2 | wamehitilafiana | wameelewana | wameulizana | wamekubaliana |
3 | dhima | wadhifa | juhudi | jukumu |
4 | dhidi ya | miongoni mwa | mbali na | zaidi ya |
5 | lawama | laana | baraka | ushindi |
6 | vita | adabu | adhabu | mapigano |
7 | kupigwa vijembe | kupigwa dafrau | kupigwa kalamu | kupigwa marufuku |
8 | kwa | na | ya | pa |
9 | mchana kutwa | usiku kucha | usiku kutwa | mchana kucha |
Wakazi wengi wa mjini 10 na tatizo la uhaba 11 maji 12 . Jambo hili hufanya 13 yao kushindwa kuyatunza mazingira yao. 14 serikali ichukue hatua ya kusambaza maji kote ili kuepuka kuzuka kwa maradhi kama vile 15 .
A | B | C | D | |
10 | wamekutwa | wanakabidhiwa | wanakabiliwa | wamejuzwa |
11 | la | ya | za | wa |
12 | masafi | safi | yasafi | msafi |
13 | baadhi | wengi | wengine | baina |
14 | Bora tu | Yamkini | Kama | Ni bora |
15 | pepopunda | kifaduro | waba | surua |
Kutoka swali la 16 hadi 30. jibu kila swali kulingana na maagizo uliyopewa.
- Tambua sentensi yenye tashbihi,
- Kaka yake ni msini kama usiku.
- Maneno yake yalikuwa msumari moto.
- Ukitaka kumla nguruwe chagua aliyenona.
- Unywaji pombe husababisha balaa na belua
- Mfinyanzi ni kwa finyanga kama vile msasi ni kwa;
- msako
- saka
- uasa
- uasi
- Tunasema Mkungu wa ndizi na ________ cha ufunguo
- kicha
- kifurushi
- kitita
- chane
- Andika tarakimu 100,001 kwa maneno.
- Laki moja elfu na moja
- Laki moja na moja elfu
- Laki mia moja na moja
- Laki moja na moja
- Alikiona kilichomtoa kanga manyoya.
Kiambishi 'ki' kimetumikaje katika sentensi hii?- Kuonyesha masharti
- Kuonyesha hali ya kuendelea
- Kuonyesha kiwakilishi
- Kuonyesha udogo
- Ni sentensi gani yenye kihisishi?
- Mchezaji yule ni hodari sana
- Kitoto kimezaliwa chini ya mti
- maneno yake yaliniumiza sana.
- Sote tulikimbia mkikimkiki.
- Majira baina ya saa tisa mchana na magharibi
- alasiri
- adhuhuri
- mawio
- macheo
- Tegua kitendawili kifuatacho;
Dhahabu yangu haishuki bei.- Macho
- Almasi
- Shamba
- Jiwe mtoni
- Chagua maelezo sahihi ya viungo vya mwili.
- Taya ni nyama zinazoshikilia meno
- Kwapa huwa chini ya bega
- Nyonga huwa juu ya kiuno
- Kisugudi ni scheinu baina ya muundi na wave
- Kanusha sentensi ifuatayo kwa usahihi.
Mtoto akila sana hunenepa.- Mtoto asipokula sana hunenepa
- Mtoto akila sana hanenepi.
- Mtoto akila sana huwa hanenepi.
- Mtoto asipokula sana huwa hanenepi
- Sentensi gani imetumia 'kwa' ya umilikaji?
- Wageni walikuja kwangu jana.
- Sherehe iliandaliwa kwa Maria. cha funguo
- Bi. arusi alikaribishwa kwa vishindo.
- Tulienda moja kwa moja hadi mjini.
- Farasi ni mnyama wa jamii ya punda. Farasi pia
- elimu ya mienendo ya nyota
- chombo cha kufumia nyuzi
- anayefuga wanyama wa kupandwa
- fremu ya baiskeli
- Shughuli yoyote ikitendwa kupita kiasi huharibika.
Chagua methali inayolingana na maelezo haya.- Ngoja ngoja huumiza matumbo
- Ngoma ikilia sana hupasuka kiwambo
- Tamaa mbele mauti nyuma
- Chombo cha kuzama hakina usukani
- Kikembe cha papa huitwaje?
- Kinengwe
- Kitekli
- Kiwavi
- Kipura
- Andika katika usemi wa taarifa;
“Tafadhali niletee miwani yangu nisome gazeti," babu akaniambia.- Babu alimwambia ampelekee miwani yake asome gazeti.
- Babu aliniagiza nimpe miwani yake asome gazeti.
- Babu aliniomba nimpelekee miwani yake asome gazeti
- Babu alimwamuru ampelekee miwani yake asome gazeti
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31 - 40.
Waziri wa Afya nchini. Bwana Bora, amesema kuwa huduma za afya nchini zimeimarika kwa kiasi kikubwa katika miaka iliyopita. Akiwahutubia wananchi waliokuwa wamejumuika katika, zahanati mpya ya Pona Bw.Bora alisema kuwa wizara yake imeongezea zahanati takriban mia tatu katika kipindi kifupi, hasa katika sehemu ambazo wananchi walikuwa wakitembea kwa mwendo mrefu kusaka huduma. Alisema kuwa zahanati nyingi zilizojengwa majuzi zina vifaa vya kutosha kutoa huduma za kimsingi na kukabiliana na magonjwa yanayowataabisha wananchi kama vile malaria na homa ya matumbo. Aliongeza kuwa wizara yake imejenga maabara na kutoa mitambo ya kisasa katika zahanati hizo itakayoweza uhakika wa magonjwa yanayowasumbua wagonjwa. Alisema kuwa zahanati dawa za kutosha.
Aliongeza kuwa wizara yake imeongezea vituo vingi vya afya ili kuwahudumia wananchi. Vituo hivi vina mitambo iliyo na uwezo wa kupiga picha viungo vya ndani ili kuweza kutambua magonjwa ya ndani kwa ndani yanayowasumbua wananchi. Aliongezea kuwa kila kituo kina wodi ndogo zenye uwezo wa kuwalaza wagonjwa takribani thelathini. Hii ni hatua nzuri ikikumbukwa kuwa awali hata kupata dawa ilikuwa shida jambo lililowapelekea watu wengi kufariki.
Bw. Bora alitoa wito kwa wananchi wajitahidi kuyatunza mazingira. Hali hii itaweza kuwaepusha na magonjwa yanayoweza kuzuilika kama vile malaria na homa ya matumbo. Akitoa vyandarua vilivyotiwa dawa, Bw. Bora alisema kuwa sasa idadi ya watu wanaoambukizwa ugonjwa huu imepungua sana katika maeneo megni humu nchini. Alitoa mwito wa watu hasa kina mama wajawazito na watoto walale chini ya vyandarua. Waliougua walihimizwa kutafuta matibabu haraka iwezekanavyo. Aliwakumbusha kuwa matibabu ya malaria sawa na yale ya ugonjwa wa kifua kikuu na UKIMWI hutolewa bure kote nchini. Aliwahimiza wananchi kujua vianzo vya magonjwa mbalimbali ili waweze kujiepusha nayo.
- Kulingana na waziri wa Afya Bw. Bora;
- afya imeweza kuimarishwa kote nchini
- watu wengi nchini watakuwa wenye afya
- matatizo ya kiafya yanashughulikiwa vizuri
- serikali itaanza kutoa huduma bora za afya
- Maana ya neno ‘wamejumuika' kwa mujibu wa kifungu ni;
- wamefumukana
- wamefungamana
- wametandazika
- wametengamana
- Kwa sasa, zahanati zilizopo ni;
- zaidi ya mia tatu
- mia tatu kamili
- chini ya mia tatu
- kama mia tatu hivi
- Ugonjwa wa malaria husababishwa na nini?
- Mbung'o
- Maji yaliyotuama
- Mbu
- Viroboto
- Malaria na homa ya matumbo;
- ndiyo maradhi pekee yanayohangaisha wananchi
- ni baadhi tu ya shida za wananchi hawa
- ni maradhi yanayowashika watoto
- ni magonjwa yasiyotibika kwa urahisi
- 'Mitambo iliyo na uwezo wa kupiga picha viungo vya ndani.' Hii ni mitambo ipi?
- Kamera
- Uyoka
- Hadubini
- Machela
- Watu wengi walifariki kutokana na;
- uhaba wa hospitali
- ukosefu wa wodi
- uhaba wa matibabu
- ukosefu wa matibabu
- Kutunza mazingira ni muhimu kwa kuwa;
- husaidia kuponya magonjwa yawezayo kuzuilika
- huzuia kuenea kwa ugonjwa wowote ule
- hudhibiti kuenea kwa maradhi yawezayo kuzuilika
- ndio njia pekee ya kutunza afya zetu
- Ni magonjwa mangapi yanayotibiwa bila malipo kwa mujibu wa makala haya?
- Mawili
- Matatu
- Yote
- Manne
- Kichwa mwafaka kwa makala haya ni;
- Huduma za afya
- Hotuba ya Rais
- Afya bora
- Ugonjwa wa malaria
Yasome makala yafuatayo kisha ujibu maswali 41 - 50.
Hamasa hakuwa mwenda guu. Aliamua kufanya lolote ambalo lingempa posho ya siku. Akaona bora asibague kazi. Nguo zake zilizochakaa sana na viatu vyake vilivyokuwa vimepasuka soli vingefaa sana katika kazi nyingine. Akamwendea mwenye mikokoteni mjini kuomba afaliwe, awabebee watu mizigo kisha amlipe jioni. jioni. Akaambiwa kuwa katika dunia hii ya nipe nikupe malipo huwa ya asubuhi. Maskini Hamasa hakuwa na senti zozote. Ilimbidi kuwabebea watu mizigo katika maduka makuu kwa mikono kwa muda akiwapelekea katika vituo vya magari ili apate chochote. Hatimaye aliweza kukusanya pesa za kutosha kukodi rukwama. Msomi mwenzetu akawa hamali.
Alifanya kazi hii kwa moyo wake wote, akawa akirauka alfajiri kuenda kuwapelekea wachuuzi mizigo yao sokoni. Hakusahau kumshukuru Mungu kila uchao kwa hali yake na kumwomba siku njema baadaye.
Baada ya siku nyingi za kazi hii ya sulubu, mwenzetu aliweza kujinunulia suti moja na jozi la viatu akajiwekea nyumbani. Alikuwa na matumaini kuwa siku moja jua la baraka lingemwangaza. Akaendelea kuvaa magwanda ya kazi ya mkokoteni.
Siku moja kilitokea kisa ambacho kilikuwa mchanganyiko wa simanzi na baraka - wakati mwingine baraka hujia motoni. Alikuwa ameiburura rukwama yake nzito kwa msaada wa kijana mmoja aliyekuwa akishirikiana naye wakati ambapo mizigo ingekuwa mizito zaidi. Walikuwa wamechoka niki. Mara likatokeza gari moja la kifahari, likakosa mwelekeo likaugonga mkokoteni na kuwaumiza vibaya. Mwenzetu hakujua lililofuata.
Alipozinduka, alijikuta hospitalini baada ya siku kadhaa. Alikuwa kavunjika mguu wa kulia na mkono wa kushoto. Juu ya dawati lake aliziona nakala za vyeti vyake vya chuo ambavyo daima alivibeba mfukoni
Vilikuwa vimechakazwa na wingi wa damu iliyommwagikia wakati wa ajali ile. Alimwona msukuma rukwama mwenzake katika kitanda kingine upembeni. Karibu naye pia walikuwa mahamali wenzake waliomzuru kumjulia hali. Pia alikuwepo mtu mmoja aliyeonyesha wazi kuwa ukwasi ulikuwa umemwota si haba.
Mtu yule alimpa pole na kujitambulisha kwake kuwa yeye ndiye aliyemgonga Hamasa. Ni jambo lililomhuzunisha sana. Ila alikuwa na jingine. Alinhakikishia kuwa angelipwa fidia na shinika lililomkatia bima. Pia alimweleza kuwa yeye alikuwa mkurugenzi wa shirika kubwa zaidi nchini lisilo la kiserikali. Alivichukua vyeti vya Hamasa na kuvikagua. Akamwomba akavidurusu. Alipovirejesha, akajiendea zake na kuahidi kurudi baadae. Japo alikuwa akishetasheta, mkurungezi yule alikuwa pale na hakikisho. Alitabasamu, akamkabidhi barua iliyomwatua moyo kijana yule - yaliyoandikwa yalikuwa ya kuacha kinywa wazi. Alikuwa ameajiriwa tayari kama meneja mkuu wa shirika lile. Hii ndiyo kazi aliyokuwa arneisomea chuoni. Alikuwa aripoti kazini baada ya miezi miwili, muda uliotosha kupona kwake.
- 'Hamasa hakuwa mwenda guu' ndiko kusema;
- alikata tamaa
- hakufa moyo
- hakutembea kwa miguu
- alikuwa na masomo ya juu
- Hamasa alimwendea mwenye mikokoteni kwa lengo la;
- kuomba kazi ya uhamali
- kukopeshwa mkokoteni
- kumweleza matatizo yake aliyopitia
- kupewa mkokoteni ili alipie kodi baadaye
- Anayebeba mizigo kwa rukwama ni hamali ilhali muuzaji maji ni;
- mzegazega
- mchuuzi
- mwanamaji
- dalali
- Jambo alilozingatia sana Hamaşa maishani ni;
- kurauka mapema na kujihurumia maishani
- kuwafaa wengine na kuomba maishani
- kushukuru kwa hali yake na kuomba neema
- kuomba asubuhi na kuwashukuru wateja
- Hamasa alinunua suti na viatu kwa kuwa;
- alivihitaji wakati asipokuwa kazini
- alitarajia kuvitumia baada ya kuneemeka
- alitaka kuwa tofauti na mahamali wengine
- angevihitaji atakapowatembelea wazazi
- 'Wakati mwingine baraka hujia motoni'
Kifungu hiki kinaeleza kuwa;- baraka huja matumaini yakiwa hafifu
- baraka huwaendea waonekanao duni
- baraka huwafuata wenye imani kubwa
- baraka huja kwa njia inayodhaniwa kuwa ya taabu
- Gari lililomgonga Hamasa lilikuwa;
- shangingi
- kachara
- karandinga
- rukwama
- Mzee mkwasi alionyesha kuhuzunishwa na;
- hali mbaya ya Hamasa
- ajai aliyoisababisha
- damu kwenye vyeti
- kutomakinika barabarani
- Mafanikio ya Hamasa yanaweza kuelezwa na methali kuwa;
- mgaagaa na upwa hali wali mkavu
- dawa ya moto ni moto
- Mungu akiziba hapa huzibua pale
- dau la mnyonge haliendi joshi
- Maana ya neno 'a kishetasheta' kulingana na muktadha ni;
- alitetemeka sana
- akienda kwa mkongojo kwapani
- akichechemea
- akijikokota
INSHA
Andika insha ya kusisimua inayohusu methali hii;
MCHUMIA JUANI HULIA KIVULINI.
Majibu
- C
- A
- D
- B
- A
- C
- D
- B
- A
- C
- D
- B
- A
- D
- C
- A
- B
- A
- D
- C
- B
- A
- C
- B
- D
- A
- D
- B
- A
- C
- C
- B
- D
- C
- B
- B
- D
- C
- B
- A
- B
- D
- A
- C
- B
- D
- A
- B
- C
- B
Kiswahili Questions and Answers - Class 7 End Term 2 2022 Set 1
Maswali
Soma vifungu vifuatavyo. Viina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo.. Chagua lifaalo zaidi kati ya uliyopewa
1 siku hiyo, Karanga 2 umuhimu wa ujirani 3 . Makuu 4 yalikuwa funzo kwake. Aliufahamu ukweli kuwa 5 . 6 mtaa wa kifahari 7 aliwabeza majirani 8 Aligaagaa pale kitandani kwa maumivu ya 9 . Alipoteza fahamu. 10 macho yake, alikuwa amezingirwa na madaktari!
A | B | C | D | |
1 | Tangu | Kweli | Hadi | Madhali |
2 | alidharau | aliukumbatia | aliudharau | aliubeba |
3 | nzuri | duni | mwema | mbaya |
4 | yaliyompiga | yaliyomsumbua | yaliyomgonga | yaliyomfika |
5 | mtegemea cha nduguye hufa maskini | fimbo ya mbali haiui nyoka | damu ni nzito kuliko maji | ndugu mui heri kuwa naye |
6 | Katika | Humo | Kule | Pale |
7 | aliishi | aliishia | alikoishi | alikuwa |
8 | wake | yake | wao | zake |
9 | ghafla | sasa | kali | taratibu |
10 | Alipovumba | Alipovumbua | Alipofumbua | Alipofunba |
Migomo 11 taifa letu sana. Ule wa madaktari 12 Disemba mwaka elfu mbili na kumi na sita 13 ndio mbaya zaidi. 14 wa ajali waliohitaji matibabu ya dharura waliachwa hoi 15 wa kuwajali.
A | B | C | D | |
11 | imeathiri | imeliathiri | imeliadhiri | imeadhiri |
12 | kwanzia | kuanzia | mnamo | tangu |
13 | labda | bora | ilhali | Kweli |
14 | Majeraha | Manusura | Majeruhi | Matapeli |
15 | bali | kweli | na | bila |
Kutoka swali la 16 hadi 30. jibu swali kulingana na maagizo.
- Nomino kombamwiko yaweza kuorodheshwa katika ngeli ipi?
- U-I
- A-WA
- I-I
- I-ZI
- Ni ala gani kati ya hizi hutumiwa pamoja na mkwiro?
- Firimbi.
- Marimba.
- Zeze.
- Parapanda.
- Ni sentensi gani iliyo na karibu ya nusura?
- Kombo ameketi karibu na baba yake.
- Karibu anisukume aliponipita mlangoni.
- Kina Yohana ni karibu arobaini darasani mwao.
- Mtihani u karibu kuanza.
- Kitenzi shona katika kauli ya kutendua ni
- shonwa.
- shonua.
- shonesha.
- shonewa.
- Kamilisha methali:
Ajidhaniaye kasimama- miti yote huteleza.
- hafikilii mbinguni.
- aangalie asianguke.
- huja kinyume...
- Chagua kauli yenye kiashiria radidi
- Nguo zizo ndizo za kina Rita.
- Mto huo huo ndio wenye mamba hatari.
- Tutawapelekea zawadi zizi hizi.
- Udongo huo nao ni wa nani?
- Fagio 10 001 kwa maneno ni fagio
- kumi elfu na mmoja.
- elfu kumi na moja.
- laki moja na mmoja.
- laki moja na moja.
- Chagua kinyume cha; Ajuza alianika nguo jioni.
- Shaibu alianua nguo asubuhi.
- Ajuza hakuanua nguo asubuhi.
- Shaibu hakuanua nguo jioni.
- Ajuza alianika nguo jioni.
- Ni nomino gani inayoweza kuundwa kutokana na sifa -ema?
- Sema.
- Jema.
- Wema.
- Mema.
- Chagua sentensi yenye kivumishi cha pekee.
- Watu wengine hupenda kula kwa vijiko.
- Mtoto huyu naye ni mdogo.
- Abiria walioumia ajalini walikuwawanne tu.
- Mwanamke wa tatu kuwasilialikuwa Bi. Leo
- Mama alimwambia bintiye kuwa angefaulu angempa tuzo katika usemi halisi ni
- "Ukifaulu utanipa tuzo," mama alimwambia bintiye..
- “Ukifaulu nitakupa tuzo," Mama alimwambia bintiye.
- "Mama alimwambia bintiye," ukifaulu nitakuyla tuzo.
- “Nikifaulu utanipa tuzo," mana alimwambia bintiye.
- Tambua matumizi ya ki.
Tasha amekibeba kitoto chake.- Masharti.
- Ngeli. .
- Udogo.
- kiwakilishi.
- Mama ameenda sokoni kwa wingi ni
- kina mama wameenda masokoni.
- mama wameenda sokoni.
- kina mama wameenda sokoni.
- mama wameenda masokoni.
- Kanusha:
Ningepita ningetezwa.- ningepita nisingetuzwa..
- nisingepita nisingetuzwa.
- nisingalipita nisingelituzwa.
- nisingelipita nisingalituzwa.
- Ni chombo gani cha usafiri kilicho tofauti?
- Teksi.
- Daladala.
- Lori,
- Meli.
Soma taarifa ifuatave kisha wilbu maswali 31 hadi 46.
Ajira ya watoto ni kazi ambazo zinawatumia na kuwaathiri vibaya watoto kati ya miaka mitano na kumi na saba kwa namna fulani kama vile kiakili, kimwili hata kimakazi. Madhila yanayowakumba watoto katika ulimwengu wa ajira ya w duniani ni mengi.
Sababu moja ya ajira ya watoto ni itikadi fulani katika jamii. Itikadi ni imani. fulani katika jambo fulani. Katika baadhi ya jamii, wazazi huzaa watoto wengi kwa minajili ya kuwatumia kuchuma. Wao huwalazimisha watoto hao kuajiriwa kuteka maji, kutema kuni, kufua nguo, shughuli za shambani miongoni mwa kazi nyingine nyingi. Waajiri huwapokea kwa mikono miwili kwa kuwa masharti ya kuwaajiri huwa nafinu..
Sekta inayowaajiri watoto wengi ni ile ya nyumbani. Jambo la kusikitisha ni kuwa zaidi ya asilimia tisini ni wasichana. Hawa nao mara kwa mara hutendewa unyama na ukatili na waajiri wao. Wakati mwingine, hawalipwi mishahara.
Duniani kuna visa vingi vya watoto kuingizwa katika shughuli za ukahaba na zile za kuchukuliwa video za ngono kwa malipo duni. Jambo hili limekithiri katika maeneo yenye shughuli za kitalii. Majiji tajika duniani nayo pia yana shughuli hizi. Isitoshe, watoto huhusishwa katika uchuuzi wa mihadarati.
Hatari ni kuwa wasipoangamizwa na ulevi wanaouchưuza, hupoteza uhai, katika vita vya magenge. Uwezekano wa watoto hao kuambukizwa UKIMWI na magonjwa mengine ya zinaa huwa jw sana,
Ni wazi kuwa njia moja na madhubuti ya kuangamiza jamii ni kuwaajiri watoto, Ustawi wa kiuchumi wa baadhi ya nchi za bara Asia unatokana na ukweli kuwa nchi hizi zinawatunza watoto wao, kizazi cha kesho, kizazi ambacho kimerithishwa elimu na maarifa ya kuendeleza na kukuza uchumi.
Mataifa hayana budi kuungana kuzua mikakati ya kutokomeza ajira ya watoto., Hatua ya kwanza ni uongozi. Lazima serikali za nchi ziwajibike.
- Kwa mujibu wa aya ya kwanza, ni kweli kuwa
- watoto wanaoajiriwa huwa wamepita umri wa kuwa shuleni.
- huenda watoto wanaoajiriwa hawapotezi makao.
- baadhi ya watoto wanaoajiriwa hupata majeraha mwilini.
- ajira ya watoto huwadumisha.
- Madhila ni
- shida.
- maono.
- mawazo.
- maoni.
- Kifungu hiki hakidhihirishi kuwa
- imani huchangia ajira ya watoto. kuangamizwa na
- ajira ya watoto ni chanzo cha mateso yao.
- ajira ya watoto hueneza uovu.
- uchumi wa nchi hukua kwa minajili ya ajira ya watoto. -
- Baadhi ya wazazi huwazaa watoto kwa kuwa wanawachukulia kama
- mtaji.
- kitegauchumi.
- riba.
- fola.
- Huenda waajiri wanapenda kuwaajiri watoto kwa kuwa
- wanataka kutumia pesa kidogo.
- kazi zao ni nyepesi.
- watoto hawana nafasi katika jamii.
- ni rahisi kuwalazimisha kufanya kazi.
- Jinsia kubwa ya waajiriwa katika kifungu hiki ni ile ya
- kiume.
- wasichana
- wavulana.
- kike.
- Video za ngono huendeleza
- maadili.
- uozo jamiini.
- vizazi.
- uadilifu.
- Watoto wanaochınıza dawa za kulevya wanakodolewa macho na hatari ya
- UKIMWI.
- magonjwa mengine.
- wahalifu.
- vita.
- Kuwaajiri watoto
- ni kuendeleza ukuaji wa uchumi.
- hukosesha jamii wakuzauchumi.
- hurithisha jamii uchumi ulionawiri.
- ni kurithisha jamii maarifa.
- Methali murua kujumlishia aya ya mwisho ni
- baada ya dhiki faraja.
- mchumia juani hulia kivulini.
- mchuma janga hula na wa kwao.
- kidole kimoja hakivunji chawa.
Soma tagrifa ifuatayo kisha ujibu maswali 41 hadi 50.
Raha na Tele walikuwa marafiki wa chanda na pete. Urafiki wao ulishinda hata udugu. Uchungu wa mmoja aliyeuhisi ni mwenzake. Waliishi katika mtaa wa Timayo na kusoma katika shule ya Matokeobora.
Shuleni, walifanya bidii za mchwa. Mungu aliwajalia vichwa vyepesi. Raha alikuwa hodari katika somo la Kiswahili naye Tele alikuwa mweledi katika Sayansi na Kiingereza. Katika masomo haya, hakuna aliyeweza kuwapiku. Hata hivyo, katika mtihani wa mwisho wa muhula, Raha hakufanya vizuri katika somo la Kiswahili. Mwalimu alishindwa kusoma hati yake, jambo ambalo lilimpotezea alama kumi. Mawazo yake katika insha alikuwa ameyapanga vizuri lakini tatizo lilikuwa ni kukosa kuandika kila wazo katika aya yake. Tele naye alikuwa ameanguka katika Kiingereza kutokana na makosa yayo hayo. Mwalimu alishindwa kusoma mwandiko wake mbaya.
Bwana Busara, mwalimu wao wa darasa, aliwaita afisini mwake ili kufahamu sababu zao za kuanguka. Walikiri kuwa wangeutilia maanani mwandiko wao. Waliahidi kufanya kila wawezalo kuirekebisha hati yao. Tele aliwashangaza walimu katika chumba chao cha shughuli rasmi aliposema bayana kuwa yeye hunakili somo la Hisabati kutoka kwa wenzake. Hilo lilikuwa jambo ambalo mwalimu hakuwa amelishuku.
Mwalimu aliwaarabia kuwa ni kosa kunakili kazi za wengine. Hatimaye, mwalimu aliwashauri wasaidiane katika masomo yote kwa kuwa kila mmoja amejaliwa kipawa tofauti.
Wanafunzi wale walifuata ushauri wa mwalimu kwa makini. Mwisho wa muhula uliofuata, Raha na Tele walifua dafu: Waliibuka washindi na kuwa na raha tele. Hati yao ikawa ya kupigiwa mfano kote shuleni.
- Kulingana na aya ya kwanza, ni kweli kuwa Raha na Tele
- hawakuwa wakiishi katika mtaa mmoja.
- walikuwa ndugu.
- walisomea shule tofauti.
- walikuwa marafiki wakubwa.
- Aliyekuwa stadi katika somo la Kiswahili alikuwa
- Tele.
- Tele na Raha.
- Raha
- Mwalimu.
- Mwandishi wa kifungu anasema kuwa
- ingawa Tele na Raha walifanya vibaya, waliongoza katika darasa lao.
- Tele na Raha walishindana katika darasa lao.
- Tele na Raha walikuwa watukutu
- mwalimu aliwapenda sana Tele na Raha.
- Kwa nini mwalimu alishindwa kusoma insha ya Raha?
- Hati hiyo ilikuwa ndogo.
- Mwandiko ulikuwa mbaya.
- Mwalimu hakujua kusoma.
- Herufi zilikuwa kubwa.
- Ni kwa nini mwalimu Busara aliwaita Raha na Tele afisini?
- Alitaka kuwaadhibu.
- Ili ajue sababu za kuanguka kwao.
- Alitaka kuwafunza kuandika kwa hati nadhifu.
- Ili kuwatuma nyumbani.
- Ni jambo gani ambalo mwalimu hakuwa amelishuku?
- Tele kunakili Hisabati.
- Raha kunakili Kiswahili.
- Tele kufanya vizuri katika Sayansi.
- Raha kuanguka katika Kiswahili.
- Chumba kinachorejelewa katika aya ya tatu ni
- msala.
- sebule.
- majilisi.
- ghala.
- Tele alikuwa
- mzembe.
- mwaminifu.
- mjanja.
- mkora. .
- Kushinda kwa Raha na Tele katika mtihanini kulionyesha wazi
- walipuuza ushauri wa mwalimu.
- walidharau ushauri wa mwalimu.
- walikuwa werevu zaidi.
- walitilia maanani ushauri wa mwalimu;
- Walifua dafu ni sawa na
- waliendelea vizuri.
- walifanya bidit zaidi.
- walifanya uamuzi
- walifanikiwa.
INSHA
Andika insha inayomalizika kwa naneno yafuatayo:
Zamani kidogo katika msitu wa Patapotea wanyama waliishi kwa amani na upendo. Walisaidiana katika mambo mengi. Siku moja ...........
Majibu
- A
- B
- C
- D
- B
- A
- C
- D
- A
- C
- B
- C
- A
- C
- D
- B
- B
- B
- A
- C
- B
- A
- A
- C
- A
- B
- C
- A
- B
- D
- C
- A
- D
- B
- A
- D
- B
- A
- B
- D
- D
- C
- A
- B
- B
- A
- C
- B
- D
- D
Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 End of Term 2 CBC Exams 2022 Set 2
Swali la 1 hadi 5: Soma mazungumzo haya kisha ujibu maswall 1 hadi 5
Rehema: (Huku akiutoa mkoba wako mabegani) Mama umeshindaje leo?
Mama: Nimeshinda vyema sana, labda wewe mwanane.
Rehema: Nami pia.
Mama: Nenda basi ukafue sare. Nami naenda jikoni kuandaa chajio.
Rehema. Sawa mama. Nataka pia nifanye kazi ya ziada tuliyopewa na mwalimu.
- Mazungumzo haya yalifanyika wakati gani?
- Asubuhi
- Mchana
- Jioni
- Usiku
- Neno 'sare' kama lilivyotumika kwenye mazungumzo lina maana ya
- Nguo za sherehe
- Kaptura na shati
- Rinda na sweta
- Mavazi yanayovaliwa shuleni
- Mamake Rehema alikuwa na shughuli gani?
- Kuandaa chujio
- Kufanya kazi ya ziada
- Kuandaa chamcha
- Kuenda shambani
- Ni nani aliyempa Rehema kazi ya ziada?
- Mama yake
- Mwalimu wake
- Baba yake
- Rafiki yake
- Kitendo cha Rehema kukubali kufanya kazi ya ziada aliyopewa kinaonyesha kuwa yeye ni
- mtukutu
- mtundu
- mtiifu
- mvivu
Swali la 6 hadi 10, Soma hadithi ifuatayo kisha ujibu maswali.
Ilikuwa likizo ya mwezi wa Aprili. Mimi na dada yangu Pendo tulihudhuria harusi ya shangazi yetu, Zainabu. Tulikuwa tumealikwa ili kubeba pete za bibi na bwana harusi, Watu wengi walihudhuria harusi hiyo ambayo ilikuwa ya kufana na kila mtu alitaka kuona shangazi yetu akifunga pingu za maisha na mpenzi wake Jabali.
Watu walifurahia kula keki na vyakula vya aina mbalimbali. Kulikuwa pia na vinywaji. Baada ya kufunga pingu za maisha shangazi yangu na mume wake Jabali walibebwa na ndege kuelekea Uarabuni.
- Ni nani na nani walifunga pingu za maisha?
- Mimi na dadangu
- Pendo na dadake
- Zainabu na jabali
- Shangazi na Pendo
- Kila mtu alitaka kuona nani akifunga pingu za maisha?
- Shangazi
- Mjomba
- Mama
- Dada
- Bwana harusi alikuwa anaitwa nani?
- Mpenzi
- Zainabu
- Mume
- Jabali
- Baada ya harusi, mume na mke walienda wapi?
- Uaribuni
- Kwa ndege .
- Nyumbani
- Pwani
- 'Kufunga pingu za maisha' ni aina gani ya tamathali?
- Nahau
- Tashbihi
- Methali
- Kitendawili
Swali la 11 hadi 15, Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali
Wanyama wanaofugwa huitwa mifugo. Wanyama hawa ni kama mbuzi, kondoo, ng'ombe, ngamia na punda. Wanyama hawa wana faida nyingi sana. Mfugaji huwakamua ng'ombe, ambao humpa maziwa ambayo humpa pesa nyingi akiyauza.
Maziwa pia hutumiwa kutengeneza siagi. Maziwa ni tamu sana, Kondoo hutupa sufi ambazo hutumiwa kutengeneza fulana. Maziwa ya mbuzi ni mazuri sana. Ngamia hutumiwa kutubebea mizigo. Maziwa yake pia hunywewa na watu wengine huamini kuwa ni dawa. Wanyama wote wanahitaji kutunzwa, Sharti waishi mahali safi na wapewe chakula cha kutosha ili wawe na afya nzuri.
- Wanyama wanaofugwa nyumbani huitwa
- mifugo
- Ng'ombe'
- Jibini
- Sufi
- Ni mnyama yupi kati ya hawa hafugwi nyumbani?
- Ng'ombe
- Mbuzi
- Kondoo
- Simba
- Ni ipi si faida ya maziwa
- Hutupa pesa
- Kutengeneza siagi
- Kunywewa
- Kutengeneza sufi
- Ni mnyama yupi hutumika kubebea mizigo
- Ng'ombe'.
- Kondoo
- Mbuzi
- Ngamia
- Anayewafuga wanyama huitwa _________________
- Mtu
- Mfugaji
- Mfungaji
- Wavulana
Soma kifungu hiki kisha ujaze nafasi 16 - 20 kwa jibu sahihi.
Elimu ni kitu chenye umuhimu ____16____ kwetu. Kwanza elimu hutufanya tujue kusoma na ___17___ . Bila elimu hatuwezi___18___ wa wenzetu kwa njia ya kuandika au kusoma. Watu ___19___ hawajasoma hukumbwa na changamoto ___20___. Sharti sote tuipende elimu.
-
- Kubwa
- mkumbwa
- kikubwa
- mkubwa
-
- kulia
- kuandika
- kuketi
- kucheka
-
- kuwasiliana
- kuwasilisha
- kuwasiliwa
- kuwasilika
-
- ambayo
- ambaye
- ambamo
- ambao
-
- mingi
- nyingi
- jingi
- wengi
Swali la 21 hadi 30. Chagua jibu sahihi.
- Kanusha sentensi hizi: Alisoma hadithi.
- Hangesoma hadithi
- Hakusoma hadithi
- Hajasoma hadithi
- Hatasoma hadithi
- Andika kwa wingi: Ndoo hii imejaa maji..
- Ndoo hizi zimejaa maji
- Ndoo haya yamejaa maji
- Mandoo hizi zimějaa maji
- Mandoo hizi zimejaa maji
- Kisawe cha barabara ni ___________
- chete
- lami
- njia
- soko
- Tegua vitendawili hivi: Nyama nje ngozi ndani
- Firigisi
- Muwa
- Mkate
- Ndizi
- Kamilisha methali hizi: Kidole kimoja hakivunji ______________________
- kidole
- chawa
- dawa
- mto
- Tumia kimilikishi '-ake' ipasavyo:Mtoto analilia kalamu
- yake
- lake
- chake
- vyao
- Jibu la 'Alamsiki" ni
- alamsiki
- vyema
- aheri
- binuru
- Kikundi cha matunda huitwa
- pakacha
- mtumba
- bumba
- numbi
- Andika kwa tarakimu
Elfu kumi na moja- 11000
- 10001
- 1001
- 1100
- Kitendo cha kupasha chakula moto
- kukanza
- kupika
- kuinjika
- kuoka
INSHA
Andika insha kuhusu;
LIKIZO YA KUPENDEZA
MARKING SCHEME
- C
- D
- A
- B
- C
- C
- A
- D
- A
- A
- A
- D
- D
- D
- B
- D
- B
- A
- D
- B
- B
- A
- C
- A
- B
- A
- D
- A
- A
- A
Kiswahili Questions and Answers - Class 8 End term 2 2022 Set 2
Maswali
Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo. Jaza kila pengo kwa kuchagua jawabu lifaalo zaidi.
Amani ni uwepo wa hali 1 utulivu katika eneo fulani. Nchi 2 na amani 3 kichumi 4 raia wake huishi 5 . Ni jukumu la kila kutetea hali ya amani kwa vyovyote vile. 7 hatuwezi kuwaachia viongozi wa kidini na vyombo vya usalama pekee 8 wajibu huu muhimu.
A | B | C | D | |
1 | na | wa | ya | kwa |
2 | isiokuwa | kuskokuwa | lisilokuwa | isipokuwa |
3 | haiathiriki tu | huathirika tu | ikiathirika tu | itaathirika tu |
4 | mbali na | bali pia | ilhali | angaa |
5 | roho mkononi | shingo upande | mkono kinywani | moyo kifuani |
6 | mlowezi | mhaini | mdhamini | mzalendo |
7 | Papo kwa papo kamba hukata jiwe | chelewa chelewa utapata mwana si wako | Kingana kinga ndipo moto | Hiari yashinda utumwa |
8 | kuutekeleza | kuutelekeza | kuuteketeza | kuuelekeza |
Sherehe zilihudhuriwa na 9 watu. Nyimbo za kitamaduni zilitamalaki kote 10 11 ngoma kwa ustadi mkubwa. Vijana wa shule 12 mashairi yenye mishororo mitatu, yaani 13 . Sherehe zilifana sana. Hata baada ya 14 niliondoka nikijivunia utamaduni wa jamii zetu. Ilikuwa sherehe ya 15
A | B | C | D | |
9 | kigaro kikubwa cha | umayamaya mkubwa wa | genge kubwa la | msoa mkubwa wa |
10 | Masogora | Malenga | Wajumu | Wazegazegà |
11 | wakicheza | wamecheza | walicheza | wangecheza |
12 | walilonga | walitamba | walisimulia | walighani |
13 | tathnia | thuluthi | tathlitha | tarbia |
14 | kujumuika | kufumukana | kutangamana | kufungamana |
15 | ndovu kumla mwanawe | nyani kuvaa miwani | mbwa apige mswaki | lila na fila kutangamana |
Kuanzia swali la 16 puku 30, jibu kila swali kulingana na maagizo uliyopewa
- Chagua sentensi isiyoonyesha hali ya masharti
- Ungefika mjini ungejionea mambo mengi
- Mtoto akielekezwa vyema atakuwa mwadilifu
- Kikulacho ki nguoni mwako.
- Mimea ingalinyunyiziwa maji ingalinawiri
- Ainisha maneno yaliyoanagziwakatika sentensi ifuatayo:
Wengi wamekuwa wakiharibu misitu kiholela.- kiwakilishi, kivumishi
- kivumishi,kielezi
- kivumishi, kiwakilishi
- kiwakilishi, kielezi
- Andika wingi wa sentensi ifuatayo:
Uwele uliovunwa utahifadhiwa katika ghala.- Ndwele zilizovunwa zitahifadhiwa katika maghala.
- Uwele uliovunwa utahifadhiwa katika ghala.
- Mawele yaliyovunwa yatahifadhiwa katika ghala.
- Mawele yaliyovunwa yatahifadhiwa katika maghala.
- Chagua maelezo yaliyo sahihi.
- Bambo ni fimbo ya kutembelea lakini pambo ni kitu kinachoongeza uzuri.
- Tanga ni mkutano wa kupanga mazishi lakini danga ni maziwa ya kwanza ya myama aliyezaa.
- Kombo ni kukosa kunyooka lakini gombo ni sura moja ya kitabu.
- Zihi ni nguvu ya kufanya kazi lakini sihi ni hali ya kuwa na afya.
- Orodha gani ina msamiati wa aina moja.
- buli, uteo, kumbwewe
- zuhura, mirihi, almasi
- kekee, bisibisi. pimamaji
- kiwanja, kuli, plau
- Tegua kitendawili kifuatacho:
Ana mikono lakini hawezi kushika kitu.- Konokono
- nyuni
- maji
- upepo
- Buda ni kwa ajuza ilhali beberu ni kwa
- kikwara
- mbarika
- mtelea
- mtamba
- Chagua kitenzi chenye kiwakilishi tu cha mtenda
- Tutawatembelea
- Alitujulisha
- Walituona
- Ulitutambulisha
- Ni sentensi gani iliyo katika wakati uliopita hali ya kuendelea?
- Mjomba alikuwa amebeba kikapu chenye matunda.
- Mwanahamisi atakuwa akiliwakilisha eneo lake.
- Juma alikiona kigari hicho kilipopita.
- Shemeji alikuwa akifua nguo zake nilipofika
- Ni sentensi ipi iliyoakitishwa ipasavyo?
- Shughuli zote, zile ulizotuachia, vimekarnilika.
- Mwalimu alituita ofisini mwake: alitaka kutushauri.
- "Kesi hii." alisema mlalamishi. "Imechukua muda mrefu."
- Wageni - wote wale - walioalikwa wamewasili.
- Kanusha: Mtoto akilelewa vyema atakuwa mwadilifu.
- Mtoto akilelewa vyema hatakuwa mwadilifu.
- Mtoto asiolelewa vyema hatakuwa mwadilifu.
- Mtoto asipolelewa vyema hatakuwa mwadilifu.
- Moto asipolelewa vyema atakuwa mwadilifu.
- Ni sentensi gani iliyotumia karibu ya nusura?
- Maguri yaliegeshwa karibu na maktaba.
- Karibu Orenge aibuke mshindi wa mbio hizo.
- Mkutano ulikuwa wa karibu watu hamsini?
- Siku ya michezo iko karibu kufika.
- Akisami 3/8 kwa maneno ni
- thuluthi nane
- khumusi tatu
- thumni tatu
- thuluthi tatu
- Nahuu gani imeambatanishwa ipasavyo na maana yake.
- Kula debe - aibika kwa kukosa kitu.
- Kula kisogo-kujifanya humwoni mlu.
- Piga shoti- pata hasara katika jambo.
- Piga taswira - eleza mtu ukweli.
- Sentensi ifuatayo imetumia tamathali gani za usemi?
Timu hiyo ni jogoo, hufunga mabao kumi kila dakika.- tashbihi, kinaya
- taswira.chuku
- sitiari, kinuya
- sitiari chuku
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali kuanzia nambari 31 mpaka 40
Pasi alipojiunga na shule yetu, wengi tulimchukulia kama kijana wa kawaida tu aliyeletwa shuleni na kiu ya masomo. Sikuliona lolote la ajabu kwake kwani kimo, umri na hata sura yake illifanana na zetu kama shilingi kwa ya pili. Uwezo wake masomoni ulikuwa wa wastani kwa hivyo sikumchukulia tishio lolote kwa nafasi yangu ambapo nilikuwa na kifuambele wakati wote. Sio kwamba nilikuwa na kinyongo naye ila uhusiano wetu ulikuwa vuguvugu tu.
Kwa baadhi ya wanafunzi, Pasi alikuwa muujiza wa kame hii. Madhali alitoka mjini, wengi waliajabia waledi wake wa lugha ya kimombo na lugha ya vijana ambayo ni mseto wa Kiswahili. KIngereza si lugha ya mama. Hata mimi binafsi nilijiona kama limbukeni mbele yake hususan kwa kuwa nilisitasita wakati wa kunena nilipojaribu kutema msamiati mwafaka wa kutumia. Wengi tulijitahidi kutumia Kingereza kwa ufasaha ilimradi tumridhishe Pasi. Nililobaki kujivunia zaidi ni ugwiji wangu wa Kiswahili ambuo niliuonea fahari siku zote.
Si hayo tu yaliyowapumbaza wengi kumhusu Pasi. Maarifa yake kuhusu filamu mbalimbali, vifaa vya kidijitali na vipindi vya runingani hayakuwa na mshindani. Wakati wa buraha na hata katika haadhi ya vipindi vya masomo, wanafunzi wengi walimzingira jinsi siafu wamzungukavyo mdudu mfu kwani hawakusema wasemao mtegemea nundu haachi kunona? Jitihada za kiranja wa darasa za kuwatuliza ziliambulia kidole gutu. Hapo ilibidi niingilie kati nikawakumbusha kuwa mwangata mbili moja humponyoka. Wengine wakanitupia jicho upembe lakini walipoona nimesimama kidete wakarudi kwenye madawati yao.
Haukupita muda mrefu tulipoanya mtihani wetu wa kaatikati ya muhula. Wanafunzi wengi hawakuweza kutimiza malengo yao. Kuna wale waliojiasa wakaanza kuinamia cha mvunguni. Hata hivyo, asilimia kubwa ilijitia hamnazo kucheza ngoma watakazo. Hawa walikuwa chombo cha kuzama ambacho hakina rubani.
Pasi aliwapa siri mpya ya kukabiliana na hali yao. Idadi ya wafuasi wake sasa iliongezeka maradufu. Kila mara alipokuwa nje ya darasa, aliandamwa kama imamu na maamuma wake. Hapo alijiona kama jemedari mwenye jeshi kubwa. Wafuasi hawa walishaanza kuigiza ile lugha ya kiongozi wao. Matokeo yao nayo yaliendelea kudidimia dididi japo hakuna kati yao aliyeonekana kujali togo wala jando.
Mambo yalipomfikia mwalimu wa darasa kooni, alikata shauri kupeleleza kiini cha hali hii. Uchunguzi wake ulibaini kwamba Pasi na genge lake lilikuwa likibugia dawa haramu. Alimfikishia kinara wa shule taarifa hiyo naye hakusita kuwaita wavyele wa vijana hawa. Kwa kuelewa kuwa mbiu ya mgambo ikilia kuna jambo, wazazi walirauka na kufika hata kabla ya wakati waliopangiwa. Vijana waliitwa kadamnasi wakasomewa mashtaka ambayo walikiri kwa fedheha. Ungaliwaona walivyoshusha nyuso kwa tua usingalikosa kuwaonea shufaka.
Kikao kilipomalizika ilipitishwa kwamba idara ya ushauri nasaha iwashughulikie vijana hawa. Hapo ndipo liliponijia wazo la kuanzisha kilabu cha ushauri wa marika shuleni. Amini usiamini! Pasi na wafuasi wake ndio waliokuwa wafuasi wa kwanza wa kilabu kile waliamua kutupa jongoo na mti wake. Hata ninapovuta taswira na kuona hatua zilizopigwa hadi kulikweza jina la shule yetu kileleni, fahari hunivaa hata nikajipata nikishusha pumzi kwa bashasha.
- Chagua jibu sahihi kulingana na aya ya kwanza
- Uwepo wa Pasi katika shule ya msimulizi uliwashangaza wengi
- Sare na umri wa Pasi ulimfanya msimulizi kumpuuza Pasi
- Pasi hakuweza kufanya vyema katika masomo yake shuleni.
- Kuja kwa Pasi hakukuathiri utendaji wa msimulizi darasani.
- Uhusiano wetu ulikuwa vuguvugu tu ndiko kusema.
- Msimulizi nu Pasi hawakuweza kupatana.
- Uhusiano wa Pasi na msimulizi ulikuwa wa kawaida
- Msimulizi alihofia nafsi yake kunyakuliwa na Pasi.
- Uhusiano wa Pasi na msimulizi ulikuwa motomoto.
- Maelezo yapi ni kweli kuhusu Pasi kwa mujibu wa kifungu hiki?
- Alikuwa na welewa mzuri ya Kiingereza, Kiswahili na lugha ya mama.
- alikuwa bingwa wa Kiswahili na teknolojia ya kisasa.
- Alikuwa na ujuzi wa kidijitali licha ya udhaifu katika lugha ya Kiswahili.
- Alikuwa mwenye bidii licha ya kutofanya vyema masomoni.
- Si kweli kusema kuwa,
- msimulizi alikuwa kielezo darasani kwa mambo yote.
- zipo nyakati ambapo msimulizi alijiona duni mbele ya Pasi.
- wale waliompuuza Pasi hawakuathirika masomoni.
- msimulizi alikuwa mweledi wa lugha ya Kiswahili.
- Methali mtegemea nundu haachi kunona ina maana kuwa
- waliomfuata Pasi waliishia kufanya vibaya darasani
- waliomfuata Pasi walijifunza mengi kuhusiana na teknolojia.
- waliompuuza Pasi walipoteza nafasi ya kuuona ukakamavu wake.
- waliompuuza Pasi walijikosesha nafasi ya kujiimarisha kwa vifaa vya kidijitali.
- Msimulizi
- hana marafiki darasani mwake.
- anaogopwa na wanafunzi kwa ukali wake.
- alikuwa kiranja wa darasa lake.
- ni mwenye kipawa cha uongozi.
- Baada ya mtihani wa katikati ya muhula.
- Msimulizi na wenzake hawakutimiza malengo yao.
- Pasi na baadhi ya wanafunzi walibadili hulka zao.
- Wanafunzi waliotambua kosa lao walianza kujibidiisha..
- Waliotia masikio nta walianza kujiimarisha
- Wazazi wa vijana waliohusika
- walijua umuhimu wa kuziba ufa.
- ni wachelea wana kulia.
- wanakataa mwito bali si waitiwalo.
- wamepuuza malezi bora ya wana.
- Jambo linalomtia fahari mwandishi wa kifungu hiki ni
- kujiona akiwa kidede katika darasa lake.
- mchango wake katika kuinua hadhi ya shule.
- idadi ya vijana waliojiunga na kilabu chake.
- hatua alizochukua za kuripoti maovu.
- Neno kiini jinsi lilivyotumika lina maana ya,
- moyo wa kitu.
- undani wa jambo.
- chembechembe za kitu.
- matokeo ya hali.
Yasome makala hawa wanaofuata kishu wiibu maswali kuanzia namba 41 mpaka 50
Zaraa ni uti wa mgongo wa mataifa mengi ikiwemo Kenya. Viwanda vingi nchini hutegemea kilimo kupata malighafi yake. Aidha, taifa haliwezi kujilisha ikiwa shughuli za kilimo zitapewa mgong. Licha ya umuhimu wa sekta hii, mkulima, ambaye ndiye nguzo muhimu, anaendelea kukabiliwa na matatizo atinati yanayokwamisha juhudi zake.
Mojawapo ya matatizo yanayomzonga mwanazaraa ni ukosefu wa ushauri unaohitajika. Wataalamu wanaotarajiwa kumshauri mkulima kuhusu nija bora za kuzalisha na kuongeza pato lake ni haba akilinganishwa na idadi ya wale wanaohitaji nasaha yake. Walioko nao wanakwamishwa na mambo tofauti. Mathalani, utawapata hawaendi nyanjani ili kukutana na wakulima kwa kuwa hawana usafiri. Iwapo usafiri upo, huenda petroli ikawa ni kizungumkuti.
Halikadhalika baadhi ya wataalamu huwa ni walaza damu na mafisadi. Kuna wale wanaofika ofisini na kushinda kutwa nzima wakisoma magazeti huku wakijaza mirabu, wakicheza bao au karata. Kuna wale ambao huangika koti au sweta kitini ili waonekane kuwa bado wapo na kisha kutokomea kuenda kushughulika masuala yao ya kibinafsi yanayohusu ndewe wala sikio kazi waliyoajiriwa kufanya.
Ukosefu wa sera mwafaka kuhusa ardhi nao ni suala jingine linalotatiza kilimo nchini. Serikali haijaweka sera mahsusi kuhusu matomizi ya ardhi. Waja wengi huongozwa na ta jamaa zao. Taratibu hizi kupendekeza ugawaji wa ardhi kwa minajili ya urithi kulingana na warithi waliopo. Si ajabu kuwa kote nchini ardhi inayofaa kwa kilimo imekatwakatwa vipande vidogovidogo ambavyo haviwezi kuwa na faida kwa zaraa.
Kushindwa kwa mkulima kuongeza virutubishi ardhini ni changamoto nyingi inayokabili kilimo nchini. Ulimaji wa kile kipande miaka nenda miaka rudi minghairi ya kukipa nafasi ya kupumzika huufanya udongo kupoteza virutubishi muhimu vinavyohitajika na mimea. Ili kutatua tatizo hili, wakulima wengi hukimbilia mbolea za kisasa ambazo badala ya kuwasaidia huwaongezea madhila. Mbolea hizi zinatumbulika kuchangia uchafuzi wa mchanga na ardhi.
Mabadiliko ya hali ya anga yamemfanya mkulima kushindwa kupanga wakati anaotakiwa kutayarisha shamba, kupanda, kupalilia, kunyunyizia dawa na kadhalika. Mvua imekuwa adimu. Badala yake panakuwa na vipindi virefu vya kiangazi ambavyo huathiri bidii za mkulima. Maji nayo yanaendelea kupungua na mkulima hawezi kukimu mahitaji ya unyunyiziaji wa maji shambani.
Maradhi pamoja na wadudu waharibifu kama vile viwavi, kupe, na mbung'o ni changamoto nyingine inayotatiza juhudi za mkulima nchini. Haya hupunguza uzalishaji katika kilimo au wakati mwingine kupunguza mimea au mifugo wao.
Mbali ya haya ukosefu wa chete, matatizo ya uchukuzi, gharama ya juu ya uzalishaji na mashindano tobana na bidhaa za nje ni changamoto kubwa. Mkulima wa Kenya anahitaji msaada wa dharura ili aweze kunyanyua kilimo. Lau haya hayatafanyika, uchumi wetu utaendelea kudidimia
- Maneno, zaraa ni uti wa mgongo wa taifa yana maana kuwa
- kilimo kimepewa kipaumbele nchini.
- umuhimu wa kilimo unajulikana kote nchini.
- kilimo kinategemewa sana nchini.
- manufaa ya kilimo yanaendelea vyema nchini.
- Viwanda vinahusianaje na kilimo nchini?
- Mazao ya shambani huishia kupelekwa viwandani.
- Mali ya kuundia bidhaa mbalimbali hukuzwa mashambani.
- Viwanda vya kuundia bidhaa aghalabu hujengwa mashambani.
- Mbegu zinazokuzwa mashambani huhifadhiwa viwandani.
- Chagua kauli sahihi kulingana na hii nakala
- Njia mbovu za usafiri zina madhara kwa kilimo.
- Kuwepo kwa vipindi vya kiangazi ni balaa kwa mkulima.
- Maafisa wote wa nyanjani hawana uwajibikaji.
- Ufisadi ukikomeshwa matatizo yote yataisha.
- Mwandishi anapendekeza sera ya ugavi wa ardhi iwe;
- waja wote wagawiwe viwango sawa vya ardhi.
- ardhi igawanywe vipande vidogovidogo ili viendeleze upesi.
- watu wakiuke tamaduni zao ili wagawiwe ardhi.
- vipande vikubwa vya ardhi vitengwe ka minajili ya kilimo.
- Yote haya hupunguza rotuba ardhini isipokuwa
- kulima shamba moja kwa bidii mwaka baada ya mwaka.
- matumizi ya mbolea vinazotoka viwandani kwa wingi.
- kuzingatia njia za utaalamu wa kilimo
- kumomonyoka wa udongo katika sehemu husika.
- Uhaba wa mvua kwa kawaida huchangia
- mafuriko
- kiangazi
- vuli
- ukame.
- Upi ni utaratibu mwafaka wa matayarisho shambani?
- Kupanda, kulima, kupalilia, kuvuna.
- Kuvuna, kulima, kupanda, kupalilia
- Kulima, kupanda, kupalilia, kuvuna.
- Kapalilia, kupanda, kulima, kuvuna.
- Lipi halijatajwa kama tatizo mojawapo la mkulima?
- Ukosefu wa soko la mazao.
- Kutatizwa na wadudu waharibifu.
- Kubadilika kwa utaratibu wa majira.
- Uhaba wa bidhaa za masoko ya nje.
- Kulingana na aya ya mwisho, mwandishi anasema kuwa,
- sharti wakulima waungane kuimarisha kilimo.
- wakulima wakipigwa jeki uchumi utaimarika.
- kilimo kimechangia kudorora kwa taifa letu.
- wakulima watafute njia mbadala za kusaka riziki.
- Neno kukimu lina maaya ya
- kutosheleza
- kupata
- kununua
- kuhifadhi
INSHA
Umepewa dakika 40 kuandika insha yako. Malizia insha kwa maneno yafuatayo huku ukiifanya iwe ya kusisimua zaidi.
..................... Ama kweli sherehe hiyo ilifana sana; kila mmoja aliondoka akisimulia matukio ya siku hiyo.
Majibu
- C
- D
- A
- B
- A
- D
- C
- A
- B
- A
- C
- D
- C
- B
- A
- C
- D
- D
- A
- C
- B
- B
- A
- D
- A
- B
- C
- C
- A
- D
- D
- B
- C
- A
- B
- D
- C
- A
- B
- B
- C
- B
- A
- D
- C
- D
- C
- D
- B
- A
Kiswahili Questions and Answers - Class 8 End term 2 2022 Set 1
Maswali
Soma vifungu vifuatavyo kisha ujibu maswali 1 - 15 ukitumia jibu sahihi
Mtoto 1 mvulana 2 umri wa miaka kumi na mitano 3 na simba katika 4 cha Gakoigo karibu na mji wa Nairobi mnano Jumamosi wiki 5 kulingana na kituo cha polisi cha Wema. Mkasa huo ulitokea nyumbani kwa Bwana na Bi. Stano. 6 mtoto huyu 7 mkasa huo alisema kuwa 8 ya kula pamoja 9 , aliondoka kwenda katika chumba cha kulala hatua hamsini kutoka nyumbani kwa wazaziwe.
A | B | C | D | |
1 | moja | mmoja | umonja | monja |
2 | chenye | wenye | yenye | mwenye |
3 | alishambulia | alishambuliwa | alimshambulia | alishambua |
4 | kitongoji | mji | kitongojini | kijijini |
5 | kesho | leo | jana | ijao |
6 | Mamake | Mamaze | Mamaye | Mamao |
7 | akasimulia | akisimulia | akipeana | akitowa |
8 | badala | baada | baadhi | baadaye |
9 | staftahi | kishuka | chajio | msosi |
Ama kweli, zaraa 10 uti wa mgongo wa taifa 11 Kamwe hatuwezi kuishi bila kutia chakula 12 tumboni. Chakula hiki 13 hutokana na kilimo. Yafaa vijana 14 kuhusu umuhimu wa kilimo ili 15 kwa hamu kuu.
A | B | C | D | |
10 | ndio | ndicho | ndiyo | ndilo |
11 | yetu | letu | zetu | mwetu |
12 | yeyote | chochote | lolote | yeyote |
13 | naye | nalo | nacho | nayo |
14 | washurutishe | wakatiliwe | wahukumiwe | wahamasishwe |
15 | wakikumbatie | walikumbatie | wamkumbatie | wazikumbatie |
Kutoka swali la 16 hadi 30. jibu kila swali
- Mtu akisema kisu hiki ni wembe, maana yake
- kidogo
- butu
- kizee
- kikali
- Jaza pengo kwa usahihi;
Mkutano ulihudhuriwa na watu wengi sana.
Yaani wake _______ wanaume,- na
- pamoja
- kwa
- pa
- “Nilikuona jana.' Sentensi hii inaonyesha kuwa kulingana na maagizo. aliyeonwa ni nani?
- Yeye
- Wewe
- Mimi
- Nyinyi
- Maji yaliyoganda na kuwa magumu kama jiwe huitwa;
- mvuke
- mangati
- theluji
- barafu
- Kitenzi 'choka' katika kauli ya kutendesha kitakuwa;
- chokwa
- chosha
- chokesha
- chokea
- Kanusha sentensi.
Wewe umekuja.- Wewe hujakuja.
- Wewe haujaja.
- Wewe hujaja.
- Wewe haujakuja
- Milioni tatu, mia tatu na thelathini elfu, mia sita na tisa kwa tarakimu itakuwa;
- 3330609
- 3300906
- 3030609
- 3303699
- Mtaalamu aliye na ujuzi mkubwa wa utengenezaji wa barabara anaitwa;
- mhasibu
- mhandisi
- mhazili
- mhazigi
- Kipini huvaliwa kwenye;
- uti wa pua
- sikio
- shingo
- pua
- Chagua sentensi ambayo imetumia kivumishi kisisitizi kwa usahihi.
- Viti vivi hivi ni vya wageni
- Watu hawa hawa nawajua
- Matunda haya yaya yameiva
- Vyungu zizi hizi ni ghali
- Kamilisha methali;
Usitukane wakunga;- kabla ya kuvuka mto
- na kizazi kingalipo
- usije ukafa mzigana
- kabla ya kukata mbeleko
- Mke wa mjomba huitwa; .
- mbiomba
- mkwarima
- mkemwenza
- mkaza mjomba
- Kanusha sentensi hii;
Ningemsaidia angefurahi.- Singemsaidia asingefurahi
- Singemsaidia asingefurahi
- Ningamsaidia asingefurahi
- Nisingemsaidia asingefurahi
- Jaza pengo kwa usahihi;
Wanafunzi ______ walifanya mtihani vizuri.- kumi
- wasaba
- tano
- wakumi
- Andika sentensi kwa udogo;
Mtoto yule mdogo analia.- Kitoto yule mdogo analia.
- Kitoto kile kidogo analia.
- Kitoto kile kidogo kinalia
- Katoto kale kadogo kanalia
Soma kifungu hiki kisa wjibu maswali 31 - 40.
Ni jambo la kusikitisha mno tunapoona jinsi vijana wanavyojitumbukiza katika janga la kutumia au kuuza mihadarati kwani vijana ndio nguzo na matarajio ya taifa lolote.
Ni matarajio ya umma wowote kuwakuta vijana wakitumia nguvu zao katika kuimarisha na kulijenga taifa badala ya kuzama katika shughuli za dawa za kulevya.
Wimbi hili la kutumia mihadarati limeingia kwa kasi kubwa na yote ni kwa sababu ya uhaba wa kazi, ukosefu wa mwelekeo na wa maongozi kwa vijana hawa. Zaidi ya hayo, wale matajiri walafi ndio wanaowapotosha vijana kwa kuwaingiza katika janga la kuuza mihadarati. Vijana hawa wanakubali kuwa
makala wa matajiri wenye uroho. Hii ni kwa vile wanavutiwa na malipo ya juu wanayolipwa hasa wakilinganisha wepesi wa kazi hizo na pato lake.
Bila shaka muuza mafuta mazuri lazima ajipake ili kuwavutia wanunuzi. Vivyo hivyo, muuza mchuzi inambidi kuonja kukolea kwa chumvi ili kuhakikisha kuwa mapishi ni ya hali ya juu. Lazima atumie angalau kwa kiasi kidogo mwanzoni kabla ya kitendo hicho kuwa ni uraibu na ada asiyoweza kuiepuka kwa hali yoyote ilivyo.
Vijana ni rasilimali kuu kwa nchi na jamii yoyote kuwaacha kupotea katika uraibu huu mikononi mwa mabepari walafi na waroho ni kama kuwakubalia kuwa mshumaa.
Visa vya vijana waliojiangamiza wenyewe, kama afanyavyo pweza anapokaangwa, ni vingi na vya kuhuzunisha. Wamemalizika wakiwa hohehahe na mwishowe tutakuwa na taifa la mbumbumbu na maamuna lisilokuwa na mawazo wala msimamo.
- Mwandishi anasikitika kwa sababu;
- ya matumizi na uuzaji wa mihadarati
- mihadarati ni ghali
- vijana wanapotea
- ya ugonjwa unaoenea
- Mihadarati ni;
- dawa za kulevya
- sigara b
- angi
- ulevi
- Matarajio ya taifa lolote kwa vijana ni;
- kujenga taifa
- kusambaza mihadarati
- kuhujumu taifa
- kutumbukia katika mihadarati
- Vijana wanaingizwa katika shughuli za kuuza mihadarati na;
- polisi
- wazazi
- viongozi
- matajiri
- Ipi si sababu kuu ya vijana kutumia mihadarati?
- Ukosefu wa maongozi
- Ukosefu wa elimu
- Marafiki wabaya
- Uhaba wa kazi
- Vijana wanakubali kuuza mihadarati kwa sababu ya;
- kuipenda kazi hiyo
- kulazimishwa
- kutoroka kazi
- malipo mazuri
- Ni kina nani kati ya hawa wanaowaingiza vijana katika ulanguzi wa mihadarati?
- Wakwasi wenye mate ya fisi
- Marafiki ambao ni kielelezo bora
- Fakiri wasiokuwa na mbele wala nyuma
- Watu wa hirimu yao
- Maana ya 'uraibuni' ni;
- kuharibu jambo
- kupendelea jambo au kitu
- kujaribu mara kwa mara
- kupendelea kitu kizuri
- Kukubali kuwa mshumaa inamaanisha;
- kujisaidia binafsi
- kupambana na wengine
- kupoza wengine
- kutumiwa kufaidi wengine
- Methali inayomhusu pweza makala haya katika inasema 'umekuwa pweza ......'
- huogopi mtu
- huwezi kukosa ulipendalo
- waishi baharini tu
- wajipalilia makaa
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali 41 hadi 50.
Nilizaliwa na kulelewa katika familia iliyotajika. Baba yangu Mlajasho alikuwa tajiri wa mali na moyo. Mimi na ndugu yangu mdogo hatukujua maana ya uhitaji kwani baba alitukidhia mahitaji yetu yote. Nyumbani mwetu kila siku mlishiba na kutapika watu wa kila sampuli waliokuja kulilia hali kwa baba. Baba aliwasabilia kwa mengi. Kuna waliopewa ruzuku mbalimbali za vyakula, kuna waliopewa vibarua mashambani na waliofanya kazi pale nyumbani.
Almuradi kila mwanakijiji alifaidika kutokana na mkono wazi wa baba. Ndugu yangu mdogo hakuisha kuwabughudhi waja hawa na kuwaita waegemea nundu.
Siku zilisonga na kupita kama maji ya mto, hata nikajipata katika shule ya msingi. Niliyakumbatia masomo yangu kwa hamu kubwa. Sikuwa na wakati wa kufanya ajizi, kwani baba pamoja na pato lake nono hakuwahi kudekeza hisia za ugoigoi. Nasi ilibidi tufuate nyayo zake, kwani mwana akibebwa hutazama kisogo cha nina. Nilifanya mtihani wangu wa darasa la nane na kuvuna nilichopanda. Asubuhi baada ya kutangazwa kwa matokeo ya mtihani huo niliamshwa na sauti ya “pongezi mwanangu,” kutoka kwa baba. Baba alikuwa amebeba gazeti la siku hiyo, usoni amevaa tabasamu kubwa. Sikuamini maneno yake. Nilimnyang'anya gazeti na ikawa kweli mwenye macho haambiwi tazama. Nilikuwa mwanafunzi bora nchini. Nilijiunga na shule mojawapo ya kitaifa.
Siku nilipokuwa kizingitini cha lango la shule ya kitaifa ya Tindi ndipo maisha yangu yalipoanza kuingia ufa.Nilikutana na Tamasha, mwanafunzi mchangamfu na mcheshi. Alijitambulisha kuwa alisomea shule iliyokuwa jirani na ile yangu ya msingi. Urafiki shakiki ukazaliwa kati yake nami. Tukawa daima tunaandamana. Hayo hayakunitia shaka, kwani Tamasha, alinihimiza kila mara nitie bidii masomoni. Hata hivyo, jinsi siku zilivyosongea ndivyo tabia yake halisi ilivyonibainikia.
Jioni moja Tamasha alikuja chumbani mwangu akiwa amebeba unga aliouita dawa ya homa, Aliniambia ibu kutibu homa ambayo ilikuwa imenikaba kwa siku ayami. Nami kwa kutotaka kumvunja rafiki yangu, nikachukia unga huo na kuutia kinywani; ingawa kwa kweli mwalimu wetu alikuwa ametuonya dhidi ya kutumia dawa zozote bila maelekezo ya daktari. Unga huo haukuitibu homa yangu, ila ulinipa utulivu mkubwa wa akili, utulivu ambao sikuwa nimewahi kuushuhudia maishani.
Tamasha alifika chumbani mwangu usiku kunijulia hali. Alinipata nimejituliza juu ya kitanda changu, Alinisalimu na kukenua kama aliyetarajia jawabu fulani kutoka kwangu. Nilimweleza hali yangu naye akaniambia kuwa hivyo ndivyo dawa hiyo ifanyavyo kazi; kwamba amekuwa akiitumia kwa muda, hata nyakati za mtihani, naye hupata nguvu za kukabiliana na majabali yote. Alinielekeza kwa Mzee Kamaliza ambaye ndiye alimuuzia unga huo. Kuanzia siku hiyo, nikawa mteja mwaminifu wa Mzee Kamaliza. Nilitumia unga huo bila fikira nikidhani kuwa ilikuwa dawa ya homa tu! Sukujua ilikuwa dawa ya kulevya na alikuwa mraibu sugu wa dawa hiyo na nyingine nyingi!
"Uzuri wake huu ni wa mkakasi tu?” Nilijiuliza. “Laiti ningalijua.” Hata hivyo, maswali yote haya hatakuwa na faida tena. Nilikuwa tayari nimazama katika tatizo sugu la matumizi ya dawa za kulevya,
Nilijisuta moyoni kwa matumizi ya dawa za kulevya ambayo yalinielekeza kuytagongesha mwamba maisha yangu shuleni. Hata hivyo, haikuwa rahisi kuacha kwani nilichelea kuitwa kimbukeni na wenzangu. Matokeo ya haya yote yakawa kuzorota kwa masomo yangu. Walimu hawakuchelewa kuona mabadiliko yaliyonikumba. Walijaribu kunishauri na kutaka kujua kilichokuwa kikinisumbua. Walipoona kwamba hali yangu haibadiliki na kwamba nimeshindwa kuwaambia tatizo langu, walimjulisha mwalimu mkuu ambaye hakukawia kumwita baba. Mazungumzo kati ya baba na mwalimu mkuu yalinitia fadhaa kubwa kwani sikutaka kuwaambia nilitumia dawa za kulevya, ingawa kwa kweli mwalimu mkuu alishuku. Walijaribu kunishika sikio kuhusiana na tabia hii yangu lakini tangu lini sikio la kufa likasikia dawa? Niliendelea na uraibu wangu hadi siku nilipofunzwa na ulimwengu baada ya kufumaniwa na naibu wa mwalimu mkuu wa shule mjini nikipiga maji. Nilipewa adhabu niliyotarajia. Nilijipata nyumbani kwa muda wa mwezi mzima, nikiuguza vidonda vya moyo na akili. Kijiji kizima kilijua nimefukuzwa shule kwa sababu ya matumizi ya dawa za kulevya. Sikuwa na pa kuutia uso wangu. Hata hivyo, hili lilikuwa funzo kubwa kwangu.
Mama yangu aliweza kunipa nasaha na kunishauri niache kutumia dawa hizo. Mara hii, maneno aliyoniambia yalikuwa na maana. Niliyasikiliza kwa makini hata baba alipopata barua kumwarifu anirejeshe shule. Nilikuwa nimeamua kujiunga na chama cha vijana wanaopigana na matumizi mabaya ya dawa shuleni.
- Mambo yanayoonyesha kuwa Mlajasho alikuwa tajiri wa mali na moyo ni;
- kukidhi mahitaji ya wana, watu kufurika kwake
- kukidhi mahitaji ya wana, kumkana mwanawe
- kukidhi mahitaji ya wana, kuwapa watu riziki
- kukidhi mahitaji ya wana, watu kumlilia hali
- “Ndugu yangu mdogo hakuisha kuwabughudhi waja hawa na kuwaita waegemea nundu" inaonyesha kuwa ndugu mdogo alikuwa;
- mwenye uchoyo
- mwenye mapuuza
- mwenye kujisifu
- mwenye uzushi
- Msimulizi alisoma kwa hamu kwa kuwa;
- alipenda masomo yake
- baba yake alikuwa mwenye bidii
- baba yake alikuwa mkali
- alitaka kufuata nyayo za ndugu yake
- Kifungu 'ndipo maisha yangu yalipoanza kuingia ufa' kinamaanisha;
- maisha ya msimulizi yalianza kupata matatizo
- maisha ya msimulizi yaliporomoka
- maisha ya msimulizi yalianza kubadilika
- maisha ya msimulizi yaliharibika mara moja
- Msimulizi hakutaka kuacha 'unga' kwa sababu;
- alichelea kudunishwa na wenzake
- alichelea kuondolewa kundini na wenzake
- hakutaka kumuudhi Tamasha
- alikuwa amezoea uraibu kwa Kamaliza
- Mambo yanayoonyesha kuwa kifungu hiki kinapinga matumizi ya dawa za kulevya ni;
- msimulizi kufukuzwa shuleni, msimulizi kujiunga na vijana wanaopinga matumizi mabaya ya dawa shuleni
- walimu kumshauri msimulizi, mama pamoja na mwalimu mkuu kumwonya msimulizi shuleni
- Kamaliza kuacha kuuza dawa, mama kumshauri msimulizi
- mwalimu kugundua tatizo la msimulizi, msimulizi kurudi shuleni
- Kulingana na kifungu hiki, jamii inakabiliana na tatizo la matumizi mabaya ya dawa kwa;
- wazazi kwenda shuleni wanapoitwa, kuwajibika kwa vijana
- ushirikiano kati ya wazazi na walimu, kuwajibika kwa vijana
- ushirikiano kati ya wazazi na walimu, kuaibika kwa vijana .
- kuwapeleka watoto shuleni, matajiri kuwasaidia watu
- Methali ambayo haifai kujumlisha ujumbe wa taarifa hii ni;
- mchovya asali hachovyi mara moja
- mtegemea nundu haachi kunona
- mchezea tope humrukia
- nazi mbovu harabu ya nzima
- “Uzuri wake huu ni wa mkakasi tu' ina maana kuwa;
- hakuweza kutegemewa
- hakuweza kuaminika
- alikuwa mnafiki
- alikuwa mcheshi
- Msimulizi alikuwa 'sikio la kufa' kwa sababu;
- alipata adabu aliyotarajia baada ya kupiga maji
- alifumaniwa na naibu wa mwalimu mkuu akipiga maji
- hakuacha uraibu wake baada ya kuonywa na baba na mwalimu
- hakupona homa baada ya kutumia unga
INSHA
Andika insha ya kusisimua itakayomalizika kwa maneno haya
...nilipowaona marafiki wangu, ni8lifurahi si haba. Tuliungana na kurudi nyumambani kwa furaha.
Majibu
- B
- D
- B
- A
- B
- C
- B
- D
- B
- C
- B
- B
- C
- D
- A
- D
- C
- B
- C
- B
- C
- A
- B
- B
- A
- B
- D
- D
- A
- C
- A
- A
- A
- D
- B
- D
- A
- B
- D
- D
- A
- A
- C
- A
- C
- A
- B
- B
- A
- C
Kiswahili Questions with Answers - CBC Grade 4 End of Term 2 Exams 2022 SET 2
MASWALI
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1-5
(Ni wakati wa likizo fupi.Hamisi na Zainabu wanakutana)
Hamisi: U hali gani Zainabu? Kumbe nawe waishi huku Tushauriane kama mimi!
Zainabu: Hali yangu ni njema. Naam. Tulihamia huku Tushauriane kwa kuwa mwenye nyumba alitaka kuipaka rangi nyumba yote.
Hamisi: Kabla ya kufunga shule hukuwa umeniambia kuwa umekuwa jirani yangu(wote wanacheka) Yaani tunasoma katika darasa moja na huwezi kuni...
Zainabu: Aaah! Nawe! Samahani basi. Huenda nilisahau. Hata hivyo, tutarudi Mnarani ufundi ukikamilika.
Hamisi: Sawa kabisa. (akikohoa kidogo)Nilikuwa nikielekea kwa kina Fauzia anieleze namna ya kutumia viunganishi katika
Zainabu: Usihofu Hamisi. Tukakae pale kivulini nikusaidie. (wakielekea chini ya mti) Je, unajua mifano gani ya viunganishi?
Hamisi: Lakini, kwa sababu, ingawa, ila na vingine vichache. Tatizo langu ni kuvitumia katika sentensi
Zainabu: Haya tukae nikuonyeshe. (wanaketi huku Hamisi akitoa daftari, kitabu na kalamu mkobani.)
- Kulingana na mazungumzo haya,kina Zainabu walikuwa wakiishi wapi kitambo?
- Tushauriane.
- Mnarani.
- Kivulini.
- Hatujaelezwa.
- Je, ni kwa nini familia ya Zainabu ilihama?
- Wazazi walitaka waishi karibu na shule
- Zainabu alitakiwa kuwa karibu na Hamisi ili amsaidie kimasomo.
- Nyumba ya kina Zainabu ya kitambo ilikuwa ikipakwa rangi.
- Waliupenda mtaa wa Tushauriane.
- Unadhani Hamisi alifika kwa kina Fauzia?
- La.
- Naam.
- Haiwezekani.
- Yawezekana.
- Tatizo la Hamisi lilikuwa gani?
- Kujua mifano ya viunganishi.
- Alitaka Zainabu amwambie kuwa walikuwa wamehama. shule.
- Kutaka kuhamia Mnarani.
- Hakujua kutumia viunganishi katika sentensi.
- Inawezekana kuwa Fauzia ni
- mwalimu.
- mzazi.
- mwanafunzi.
- Zainabu.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 6 hadi 8.
Ni wajibu wa kila mkenya, awe kijana au mzee, kushiriki katika uhifadhi na ulinzi wa misitu yetu. Kila mmoja ana nafasi yake ya kutekeleza kulingana na umri na uwezo wake. Upanzi wa miti unafaa kuongozwa vijana kwa sababu wana nguvu ya kutosha. Msimu mzuri wa kupanda miche ni msimu wa mvua nyingi.
Ili kuipanda miti mingi nchini, serikali imetenga siku moja kwa mwaka iwe ya upanzi wa miche, yaani miti michanga. Wengi hivi karibuni wamekosa kuitilia maanani siku hii muhimu. Hapo awali, shughuli hii ilikuwa ikichangamkiwa na kila mmoja katika jamii.
- Kulingana na ufahamu, uhifadhi wa misitu ni wajibu wa
- vijana.
- watu wazima.
- watu wote.
- wanafunzi.
- Je, ni kwa nini vijana ndio wanaofaa kuongoza katika upanzi wa miti?
- Wana nguvu ya kutosha.
- Wanajua kupanda miche zaidi.
- Wao ndio wengi nchini.
- Hiyo ni sheria ya nchi yetu.
- Katika mwaka mzima, ni siku ngapi zimetengewa upanzi wa miche?
- Tatu.
- Mbili.
- Nne.
- Moja.
- Kulingana na ufahamu,
- hata sasa, wanajamii wanachangamkia upanzi wa miche.
- mti mchanga sana huitwa mche
- hapo awali watu hawakupenda kupanda miche. .
- miti ina faida kwa vijana pekee.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 10 hadi 12.
Kuna umuhimu mkuu wa kudumisha afya bora. Binadamu akiwa na afya bora, huweza kufanya shughuli zote vizuri na kwa wakati unaofaa. Ili kuwa na afya bora, ni vizuri kuzingatia lishe bora. Chakula tunachokila lazima kiwe na kabohaidreti, protini na vitamini kwa viwango vinavyofaa mwilini. Vile vile, ni vizuri kunywa maji safi na salama kila siku. Je, wajua kuwa matunda hutukinga tusiwe wagonjwa? Wapishi na watu wote wanaoandaa chakula ni lazima wawe safi ili tusipatwe na magonjwa
- Taarifa hii inasema kuwa kuna umuhimu wa kudumisha
- lishe bora.
- chakula bora.
- afya bora.
- usafi.
- Tumeambiwa kuwa chakula chetu lazima kiwe na
- kabohaidreti na protini.
- vitamini na kabohaidreti.
- kabohaidreti na protini.
- vitamini, kabobaidreti na protini.
- Kulingana na taarifa, matunda
- hutuletea magonjwa.
- hutukinga tusiwe wagonjwa.
- huwa na ladha nzuri.
- yanafaa kuwa safi na salama.
Sonia kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 13 hadi 15.
Mayowe alikuwa ameketi kando ya ghala lake tupu. Tumbo lilimnguruma kwa njaa. Aliishi hivyo kwa siku tatu. Mtama aliokuwa ameuweka katika ghala uliibwa na manyani na tumbili waliotoka katika msitu wa Marura. Mahindi nayo yaliyokuwa tele humo ghalani yaliliwa yote na kuchakulo. Kando yake kulikuwa na kibuyu. Kibuyu hicho kil'isoma akili yake haraka na kumwambia kwa sauti, “Fanya chaguo!" Mayowe, kwa sauti alisema, "Nataka chakula!” Ghafla bin vuu, ghala likajaa mihogo na viazi. Mayowe alifurahi kuliko siku zote za maisha yake.
- Mwanzoni mwa ufahamu, ghala la Mayowe lilikuwa na nini?
- Mihogo na viazi.
- Lilikuwa tupu.
- Mahindi na mtama.
- Mtama na viazi.
- Tumeambiwa kuwa Mayowe alihisi njaa kwa muda wa
- wiki tatu.
- miaka mitatu
- saa tatu.
- siku tatu.
- Manyani na tumbili wale walitoka wapi?
- Katika kijiji jirani.
- Mlimani.
- Hatujaelezwa.
- Msituni Marura.
Soma kifungu kifuatacho. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.
Jana_16_ , kipindi cha kwanza kilikuwa cha Kiswahili. Kila mmoja wetu alifurahi . kwa sababu _17_ wetu alituambia kuwa siku hiyo angetufundisha mengi kuhusu pande kuu za _18_ Alianza kwa kutueleza kuwa jua huchomoza_19_ na kutua au kuzama_20_ Jioni hiyo, tulitakiwa kulichora jua na kulipaka rangi.
-
- asubuhi
- jioni
- usiku
- mchana
-
- mzazi
- walimu
- mwalimu
- mjomba
-
- uwanja
- darasa
- shule
- dira
-
- magharibi
- mashariki
- kusini
- kaskazi
-
- kaskazini
- kusini
- magharibi
- mashariki
Katika swali la 21-30. jibu swali kulingana na maagizo uliyopewa.
- Ni rangi gani hapa haipo katika bendera ya Kenya?
- Nyekundu.
- Manjano.
- Nyeupe.
- Kijani.
- Chagua wingi wa sentensi hii:
Mwaka umeisha bila vita.- Miaka imeisha bila vita.
- Mwaka imeisha bila vita.
- Miaka umeisha bila vita.
- Miaka zimeisha bila vita.
- Kamilisha methali ifuatayo:
Mtoto umleavyo- hutazama kisogo cha nina.
- ni nyoka.
- ndivyo akuavyo.
- mkanye angali mdogo.
- Chagua umoja wa
Madirisha mekundu yamefungwa.- Madirisha nyekundu limefunguliwa.
- Dirisha jekundu limefunguliwa.
- Dirisha nyekundu limefungwa.
- Dirisha jekundu limefungwa.
- Mwembe hutupa maembe, nao mgomba hutupa
- ndizi.
- kahawa.
- mchele
- matunda.
- Chagua neno lililo katika ngeli tofauti na yale mengine.
- Jua.
- Joto.
- Jani
- Jasho
- Nahau taka idbini ina maana ya
- toa tangazo
- omba ruhusa
- omba msamaha
- pata habari
- Baba amenunua televisheni mpya. Chagua kisawe cha neno lililopigiwa mstari.
- Baiskeli
- Redio
- Simu
- Runinga
- Kati ya hawa, ni yupi mnyama wa porini?
- Swara.
- Farasi.
- Mbuzi.
- Punda
- Kitenzi soma katika kauli ya kutendwa huwa
- someka.
- somea.
- somwa.
- somesha.
MWONGOZO WA KUSAHIHISHA
|
|
|