Displaying items by tag: kiswahili

Soma kifungu hiki kisha ujibu swali la 1-5.
GRD4KISW1

Siku moja tulienda shambani na mwalimu wetu Bi. Zawadi. Ilifaa darasa letu la 4B watoe magugu shambani, wanafunzi wa darasa la 4A. Walifyeka nyasi ndefu zilizokuwa karibu na vyoo vya wasichana, nao wanafunzi wa darasa la 4D walipalilia miharagwe. Tulifanya kazi kwa bidii sana. Tulilima hadi jioni wakati tulipowaona viboko wawili wakija upande wetu. Tulijawa na woga mwingi sana. Kila mmoja wetu alikimbia huku na kule akipiga nduru. Wanafunzi wawili wa darasa la 4D walianguka chini na kuumia vibaya. Mmoja wa darasa letu alitegwa na kuchomwa na mwiba. Alipelekwa hospitalini kwa haraka. Walimu walikuja na kuwafukuza viboko hao. Ilikuwa siku mbaya sana kwetu!

Maswali

  1. Mwanafunzi anayezungumza ni wa darasa gani?
    1. 4C
    2. 4D
    3. 4A
    4. 4B
  2. Wanafunzi wa Gredi ya 4D walifanya nini?
    1. Kupalilia mahindi.
    2. Kulima.
    3. Kupalilia miharagwe.
    4. Kufyeka nyasi.
  3. Ni nini kilichomfanyikia mwanafunzi aliyepelekwa hospitalini?
    1. Alidungwa na mwiba.
    2. Alitegwa na mkulima.
    3. Alichomwa na mkuki.
    4. Alikanyagwa na viboko.
  4. Wanafunzi wangapi wa darasa la 4D walioumia vibaya?
    1. Wanne
    2. Wawili
    3. Watatu
    4. Wote.
  5. Ni shughuli ipi haikufanyika shambani?
    1. Kufyeka
    2. Kuvuna
    3. Kupalilia
    4. Kulima.

Soma makala haya kisha ujibu swali 6-10.

Juma ni mwanafunzi mwenye bidii sana. Yeye huja shuleni kila siku. Mara nyingi humaliza kazi yake upesi sana. Kazi yenyewe huwa bila makosa yoyote. Walimu, wanafunzi na wazazi wake wanampenda sana. Juma huwasaidia wanafunzi wenzake wanaoshindwa na kazi walizopewa darasani. Siku moja ya Ijumaa, Juma alitoka kwenda kwa rafiki yake Joni. Alikuwa amekamilisha kazi zake zote za siku hiyo. Alitoka nje ya lango lao na kulifunga. Kabla ya kulifunga lango, mtu mmoja alimshika mkono. Moyo wake ulimpiga kwa kasi kwa sababu hakumjua mtu huyo. Alijaribu kutoroka lakini hakuweza Mtu yule alimwamuru Juma warudi nyumbani kwao amfungulie mlango. Juma alipiga mayowe. Majirani walikuja kumsaidia kumkamata yule mwizi. Polisi walipigiwa simu wakaja na kumtia pingu kisha kumpeleka jela.

Maswali

  1. Juma hufanya kazi yake
    1. polepole.
    2. kiholela
    3. kwa haraka
    4. bila kujali.
  2. Watu wafuatao wametajwa kwenye kifungu kama wanampenda Juma isipokuwa
    1. wazazi
    2. wafanyakazi
    3. walimu
    4. wanafunzi.
  3. Juma alitaka kwenda kwa rafiki yake lini?
    1. Ijuma.
    2. Alhamisi
    3. Ijumaa.
    4. Jumamosi
  4. Ni nani aliyemshika Juma mkono?
    1. Rafiki yake.
    2. Mama yake.
    3. Mwizi.
    4. Polisi.
  5. Polisi walipokuja walifanya nini?
    1. Walimtia pingu mwizi.
    2. Walimfungulia mlango Juma.
    3. Walijaribu kumtoroka.
    4. Walimpiga mwizi.

Soma ufahamu kisha ujibu swali 11-15.

GRD4KISW2

Sokoni ni pahali panapouzwa bidhaa mbalimbali kama vile mboga, matunda, nafaka, nguo, mifugo na vitu vinginevyo. Soko pia huitwa cheto. Mimi hupenda soko safilisilo na wadudu hatari wanaosambaza magonjwa. Soko chafu huwavutia wadudu hatari kama vile nzi ambao wanaweza eneza ugonjwa wa kipindupindu. Soko letu linaitwa Sufi. Soko hili hupendeza sana kwa sababu huwa safi na lina vitu vingi ajabu! Hupata wateja wengi sana hata kutoka kaunti nyingine. Siku ya Ijumaa ndiyo siku maalum ya biashara ya matunda na mboga Watu hufurika sana sokoni kwetu siku hiyo ili wanunue matunda kama vile matufaha, machungwa, mapapai, mifenesi, limau na maparachichi. Mifugo huuzwa na kununuliwa siku ya Jumanne. Fahali haswa ndio wauzwao siku hiyo. Naipenda soko Sufi sana!

Maswali

  1. Kipi kisichouzwa sokoni kulingana na kifungu?
    1. Vitanda
    2. Nafaka.
    3. Matunda
    4. Mavazi.
  2. Wadudu wanaoletwa na uchafu husambaza ugonjwa gani?
    1. Malaria
    2. Tumbo
    3. Kipindupindu
    4. Kansa.
  3. Mbona soko Sufi hupata wateja wengi?
    1. Lina bidhaa nyingi.
    2. Kuna watu wengi huko.
    3. Ni kubwa.
    4. Vitu ni bei rahisi.
  4. Wanyama huuzwa siku gani?
    1. Ijumaa.
    2. Jumamosi.
    3. Jumanne.
    4. Jumatano.
  5. Fahali ni mnyama yupi? Ng'ombe
    1. jike
    2. dume
    3. mdogo
    4. mnono.

Soma mtungo ufuatao kisha ujaze mapengo kwa kutumia maneno uliyopewa

Kenya ni                  ya kupendeza sana. Watalii wengi hufurahia kuzuru taifa                    .Kuna mbuga                       sana Kenya. Mojawapo ya mbuga hizo ni Maasai Mara. Mbuga hii ina wanyama wengi kama vile                       ambao huiletea Kenya pesa za kigeni. Nalipenda taifa langu sana. Mimi ni                  .

16. A. inchi    B. nchi   C.mahali    D. nji  
 17. A. hilo   B. lile    C.hili    D. hii 
  18. A. nyingi    B. mingi   C. mengi   D. wengi 
 19. A. suala    B. swali    C.suara   D. swara 
 20. A. jambazi   B. mzalendo    C. mwafrika    D. mbunge  
  1. Kanusha sentensi hii; Vikapu vinauzwa.
    1. Vikapu haviuzwi.
    2. Vikapu havitauzwa.
    3. Kikapu kinauzwa.
    4. Vikapu havikuuzwa.
  2. Tegua kitendawili: Fatuma mchafu
    1. Nyumba.
    2. Ufagio
    3. Nguruwe
    4. Nzi
  3. Chagua alama ifaayo ya uakifishi.
    Je, ulimtembelea shangazi
    1. .
    2. ,
    3. ?
    4. !
  4. Tarakimu '82' kwa maneno ni
    1. thelathini
    2. themanini na mbili
    3. thelathini na mbili
    4. nane mbili.
  5. Chagua sentensi iliyo kwenye nafsi ya tatu wakati ujao.
    1. Mimi nitachora.
    2. Yeye anasoma.
    3. Wewe ulicheka.
    4. Wao watacheza.
  6. Jaza pengo: Februari, Machi, Aprili,                    
    1. Juni
    2. Julai
    3. Mei
    4. Agosti
  7. Chagua neno lenye sauti mbili zinazotamkwa pamoja.
    1. maji 
    2. bidii
    3. fyeka
    4. kazi.
  8. Anayewatibu wagonjwa huitwa
    1. nesi 
    2. tabibu
    3. rubani
    4. muuguzi.
  9. Tumia -angu' kujaza pengo katika sentensi hii.
    Mkate                   
    1. zangu
    2. yangu
    3. wangu
    4. langu.
  10. Paka ameketi wapi?
    GRD4KISwqn30
                    ya meza.
    1. Chini 
    2. Kando
    3. Ndani
    4. Nje.

Andika insha fupi kuhusu picha hii.
GRD4KISWinsha

MWONGOZA ;

  1. D
  2. C
  3. A
  4. B
  5. B
  6. C
  7. B
  8. C
  9. B
  10. A
  11. A
  12. C
  13. A
  14. C
  15. B
  16. B
  17. C
  18. A
  19. D
  20. B
  21. A
  22. B
  23. C
  24. B
  25. D
  26. C
  27. C
  28. B
  29. C
  30. A

Soma kifungu hiki kisha ujibu swali la 1-5.   

G5SwaT1SE23P1
Mzee Siri ni seremala shupavu sana. Katika karakana yake hutengeneza meza, makochi, vitanda na vifaa vingine. Yeye hupenda kuvaa bwelasuti afanyapo kazi ili nguo zake zisichafuke. Pia huvaa chepeo kujikinga dhidi ya ukali wa jua. Nyumba yake imejengwa kusini mwa shule ya Bora. "Nyumba hiyo ina vyumba sita.

Kila jioni yeye pamoja na familia yake; yeye, mkewe na wanawe wawili huketi sebuleni kupata chajio. Chakula hicho huwa kitamu kama asali. Watoto huwasubiri wazazi wao wanawe kisha wao hufuata. Kila mtu hula kwa heshima. Baada ya mlo wao hunawa mikono na kuviondoa vyombo mezani. Baada ya kula, watoto humsaidia mama yao kuviosha vyombo kisha wanaenda vyumbani mwao kulala fofofo!

Maswali

  1. Karakana ya mzee Siri hutengeneza vitu vifuatavyo isipokuwa
    1. meza
    2. ndoo
    3. makochi
    4. vitanda.
  2. Ili kujikinga na miale ya jua, Bw. Siri huvaa vazi gani kichwani?
    1. Chepeo
    2. Bwelasuti
    3. Chupi
    4. Kabuti.
  3. Nyumba ya Bw.Siri ina vyumba vingapi?
    1. 5
    2. 6
    3. 4
  4. 'Chakula kitamu kama asali' ni mfano
    1. methali
    2. tashbihi
    3. nahau
    4. kitendawili.
  5. Familia ya Bw. Siri ina ya watu wangapi?
    1. 2
    2. 3
    3. 5
    4. 4

Soma shairi hili kisha ujibu swali la 6-10.

Nakushukuru mzazi, haja kunitimizia,
Vyakula nayo mavazi, yote waniangalia,
Japoni huna hata kazi, bado wanifikiria,
Pongezi mzazi wangu, kazi nzuri waifanya.

Shuleni kanipeleka, sare yote ukanipa, 
Ukabaki na mkeka, vitu vyote ukanipa,
Huku mimi nikicheka, kipenzi watapatapa,
Pongezi mzazi wangu, kazi nzuri waifanya.

  1. Shairi hili lina beti ngapi?
    1. Mbili
    2. Nne
    3. Nane
    4. Tano.
  2. Kila ubeti una mishororo mingapi?
    1. Mitatu
    2. Miwili
    3. Minne
    4. Minane.
  3. Mshairi anampongeza nani?
    1. Nyanya yake
    2. Rafiki yake
    3. Mzazi wake
    4. Mwalimu wake.
  4. Kisawe cha neno pongezi ni kipi?
    1. Pole
    2. Hongera
    3. Tafadhali
    4. Karibu.
  5. Mshororo wa mwisho una silabi ngapi?
    1. 2
    2. 4
    3. 16
    4. 8

Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali 11-15   

Mfalme wa wanyama, Simba, alikuwa akiwatesa sana wanyamapori. Baadhi ya wanyama kama vile Sungura, Fisi, Ndovu na Mwewe waliamua kumfunza adabu. Ijumaa moja, walikusanyika nje ya nyumba yake kwa hasira. Walikuwa wameapa kuikomesha tabia yake ya kuwatesa wanyama wanyonge.

Sungura alienda kuubisha mlango wa pango la Simba. Simba alinguruma kwa mshtuko wa sauti kubwa ya kuogofya. Wanyama wote walitimua mbio kama Swara isipokuwa Fisi. Walishangaa ikiwa siku hiyo ingewaishia vyema. Walipouona ujasiri wa Fisi,walirudi na kuungana naye. Wal'zungumza kwa sauti ndogo kisha wakaelewana kufanya maongezi kwa amani bila kuzua fujo. Hatimaye walielewana na Simba akaahidi kutokula chakula cha wenzake tena ila angekuwa anaenda kuwinda chakula chake mwenyewe.

  1. Mfalme wa wanyama alikuwa nani?
    1. Fisi
    2. Ndovu
    3. Simba
    4. Mwewe.
  2. Wanyama walimtembelea Simba siku gani?
    1. Alhamisi
    2. Ijumaa
    3. Jumatano
    4. Jumamosi.
  3. Ni mnyama yupi hakuenda kwa Simba?
    1. Tembo
    2. Fisi
    3. Sungura
    4. Swara.
  4. Simba aliwatesaje wanyama wengine
    1. Aliwachapa.
    2. Aliwanyima maji.
    3. Aliwanyang'anya mlo.
    4. Aliwatesa waliokuwa wanyonge.
  5. Kati ya wanyama waliomtembelea Simba, ni yupi aliye tofauti?
    1. Mwewe
    2. Sungura
    3. Fisi
    4. Ndovu.

Soma kifungu hiki kisha ujaze mapengo katika swali 16-20 kwa jibu mwafaka.

Sote ___16___ katika lango la mbuga ya wanyama la Nairobi saa ___17___ kamili. Lilionekana kuwa ___18___ kuliko mlango wa kawaida. Mtu ___19___  alitukaribisha. Tulienda sehemu mbalimbali na kuwaona wanyama ___20___.

   A   B   C   D 
 16.   walifika   tulifika   mlifika   nilifika 
 17.  pili   wawili  miwili  mbili
 18.  kikubwa   mkubwa   kubwa  mikubwa 
 19.  mmoja  moja  kimoja  wamoja
 20.  nyingi  chache  wengi  mingi

 

Kutoka swali la 21 hadi 30, chagua jibu sahihi.

  1. Ni neno lipi litapatikana kwanza katika kamusi?
    1. Beba
    2. Babu
    3. Bata
    4. Benki.
  2. Neno mkono katika ukubwa ni _______________
    1. kono
    2. likono
    3. jikono
    4. mikono.
  3. Ni neno gani linapatikana katika ngeli ya LI-YA?
    1. Jua
    2. Joto
    3. Ua
    4. Giza.
  4. Andika sentensi ifuatayo katika wingi.
    Mti umekatwa.
    1. Miti imekatwa.
    2. Miti zimekatwa.
    3. Miti yamekatwa.
    4. Miti zitakatwa.
  5. Kinyume cha shangazi ni
    1. mbiomba
    2. amu
    3. mjomba
    4. nyanya.
  6. Kamilisha methali hii.
    Mtoto akibebwa hutazama _________________________ cha nina.
    1. kichwa
    2. nywele
    3. uso
    4. kisogo
  7. Ala! Hujapata chakula?
    Neno 'Ala!' ni _____________________
    1. kihusishi
    2. kihisishi
    3. kielezi
    4. kivumishi
  8. Jozi ipi iliyo na visawe?
    1. Papa - baba
    2. Toa - doa
    3. Simu - rununu
    4. mama - baba
  9. Jibu la hujambo ni?
    1. Hatujambo
    2. Njema
    3. Sijambo
    4. Nzuri.
  10. Kamilisha tashbihi ifuatayo.
    Nyeupe kama ________________________
    1. theluji
    2. unga
    3. neti
    4. malaika.

INSHA

KUANDIKA

Andika insha kuhusu: 'NCHI YANGU'

MARKING SCHEME

  1. B
  2. A
  3. C
  4. B
  5. D
  6. A
  7. C
  8. C
  9. B
  10. C
  11. C
  12. B
  13. D
  14. D
  15. A
  16. B
  17. D
  18. C
  19. A
  20. C
  21. B
  22. A
  23. B
  24. A
  25. C
  26. D
  27. B
  28. C
  29. C
  30. A

MASWALI

Soma kifungu kifuatacho na ujaze nafasi zilizoachwa 

___1___ Siku ya Jumamosi. ___2___ ilikuwa siku aliyopanga baba kutupeleka  matembezi. Tulipanga kuzuru bustani ___3___Uhuru. Mimi na mnuna wangu Maria tulijawa ___4___ furaha. Tuliingia kwenye gari. ___5___ baba. Kabla ya kung'oa nanga sote tulijifunga mikanda.

   A   B   C   D 
 1.   palikuwa   mlikuwa   ilikuwa   kulikuwa 
 2.  Hili  Hii   hio   hicho 
 3.  la  wa   ya   na 
 4.  ya  la   wa    na 
 5.  cha  kwa   la   za 

 

Kati ya nomino hizi ni gani ambayo ni nomino ya pekee

  1.  
    1. Kisumu
    2. Mti
    3. Dada
    4. Gari
  2.  
    1. Msichana
    2. Darasa
    3. Mto Athi
    4. Kikombe
  3.  
    1. Kitabu
    2. Naivasha
    3. Ng'ombe
    4. Chakula

Chagua neno ambalo liko na sauti tofauti

  1.  
    1. Theluji
    2. themanini
    3. dhamana
    4. thelathini
  2.  
    1. Nyanya
    2. nyuma
    3. nyani
    4. yai
  3.  
    1. lala
    2. rula
    3. laana
    4. lawama
  4.  
    1. Nzige
    2. nzi
    3. nzito
    4. nia
  5.  
    1. Mzito
    2. mzuri
    3. msitu
    4. mzima
  6. Mkufu na Pete ni aina ya ________________________________
    1. mavazi
    2. mapambo
    3. sare
    4. chakula
  7. Ni vazi lipi kati ya haya huvaliwa na wavulana?
    1. rinda
    2. sketi
    3. blauzi
    4. kaptura
  8. Ni vazi lipi huvaliwa na wavulana na wasichana?
    1. suruali ndefu
    2. shati
    3. soksi
    4. sketi

Kamilisha nomino za makundi   

  1. Jeshi la __________________________
    1. sรญafu
    2. askari
    3. magari
    4. wazee
  2. Tita la ___________________________
    1. kuni
    2. gunia
    3. majani
    4. viti
  3. Darasa la ________________________
    1. ng'ombe
    2. wanasiasa
    3. wanafunzi
    4. wagonjwa
  4. Wingu la _________________________
    1. mvua
    2. upepo
    3. mawingu
    4. maji
  5. Umati wa _________________________
    1. wanyama
    2. kuni
    3. watu
    4. waganga
  6. Ni rangi gani hupatikana kwa bendera kati ya hizi?
    1. samawati
    2. nyekundu
    3. zambarau
    4. jivu
  7. Ni neno lipi kati ya haya huonyesha heshima?
    1. ana mimba
    2. anahara
    3. anakonjoa
    4. ni mja mzito
  8. Watoto wako na haki zao. Ni gani haki ya watoto kati ya hizi?
    1. mavazi
    2. masomo
    3. kuchapwa
    4.  kucheza
  9. Bendera ina rangi __________________________________
    1. tatu
    2. nne
    3. tano
    4. kumi
  10. Mtu ambaye analinda mlango huitwa ____________________________
    1. bawabu
    2. nesi
    3. daktari
    4. muuguzi
  11. Kati ya hizi ni gani ambayo si sehemu ya kompyuta?
    1. bodidota
    2. kipini
    3. kipanya
    4. kitufe
  12. Kipuli ni aina ya mapambo. je, pambo hili huvaliwa wapi?
    1. sikioni
    2. mguuni
    3. shingoni
    4. mkononi
  13. Jibu la Alamsiki ni _____________________________
    1. marahaba
    2. sijambo
    3. nzuri
    4. binuru
  14. Ni neno lipi lina sauti tofauti?
    1. dhamana
    2. thelathini
    3. dhiki
    4. dhoruba
  15. Ni neno lipi litakuwa la kwanza kwa kamusi?
    1. kalamu
    2. kabati
    3. kanga
    4. kampuni
  16. Ni nini kati ya hizi haipatikani kwa ambulensi?
    1. Bendeji
    2. Pamba
    3. Kipima joto
    4. Ratili

Soma hadithi ifuatayo kisha ujibu maswali

Mchezo wa kandanda hupendeza kutazama. Utawaona watu ishirini na wawili uwanjani. Ninajua utashangaa kwa kuwa huwa ni watu wengi sana. Kandanda hushirikisha timu mbili. Kila timu huwa na wachezaji kumi na mmoja. Vilevile kuna mwamuzi mmoja ambaye anaitwa refa. Refa akipuliza kipenga mchezo unaanza.

  1. Mchezo wa kandanda huwa na wachezaji wangapi?
    1. Ishirini na mmoja 
    2. Ishirini na wawili
    3. Ishirini
    4. Ishirini na watatu
  2. Kandanda huwa na timu ngapi?
    1. Mbili
    2. moja
    3. Tatu
    4.  Nne
  3. Je, timu moja ya kandanda huwa na wachezaji wangapi?
    1. Kumi
    2. Ishirini
    3. Kumi na mmoja
    4. Kumi na watatu
  4. Mtu ambaye hutoa uamuzi katika mchezo wa kandanda huitwa _______________________________
    1. mwalimu
    2. golikipa
    3. muamuzi
    4. refa
  5. Refa hupuliza ___________________________________________ ndio mpira uanze
    1. mpira
    2. kipenga
    3. mkono
    4. makofi
  6. Jina jingine la mpira wa kandanda ni ________________________________________
    1. mpira wa mikono
    2. mpira wa mabega
    3. mpira wa miguu
    4. mpira wa kichwa

Andika kitenzi kifaacho

  1. Mama alipika chakula (hali ya kutendewa)
    1. alipikika
    2. alipikwa
    3. alipikiwa
    4. alipikisha
  2. Mwalimu alisoma watoto (hali ya kutendesha)
    1. alisomeka
    2. alisomewa
    3. alisomwa
    4. alisomesha

INSHA

Andika insha ya kuvutia kuhusu:

NYUMBANI KWETU

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

MARKING SCHEME

  1. C
  2. B
  3. C
  4. D
  5. C
  6. A
  7. C
  8. B
  9. C
  10. D
  11. B
  12. D
  13. C
  14. B
  15. D
  16. C
  17. B
  18. A
  19. C
  20. A
  21. C
  22. B
  23. D
  24. B
  25. B
  26. A
  27. B
  28. C
  29. D
  30. B
  31. B
  32. D
  33. B
  34. A
  35. C
  36. D
  37. B
  38. C
  39. C
  40. D

MASWALI

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1 mpaka 5.

Mwanafunzi :   Shikamoo mwalimu?
Mwalimu :        Marahaba
Mwanafunzi :   Kuna mwanafunzi mmoja wa gredi ya sita anayeendeleza ulanguzi wa dawa za kulevya.Inaserhekana kuwa yeye hupitia uani                            kwenda kuzinunua. Wengi wa wateja wake ni wenzake katika gredi ya sita. Jina la mwanafunzi huyo ni Kamaliza.
Mwalimu :        Nashukuru sana kwa habari muhimu ambazo umenipa. Sijui kama una la ziada.
Mwanafunzi :   Mimi sina la ziada ila nakushukuru kwa kunialika ili tuzungumzie tatizo hili sugu. Niko tayari kushirikiana na utawala wa shule                             kuhakikisha kuwa mambo yote yako shwari. Hali hii imetokana na ung'amuzi kuwa jambo linaloshughulikiwa na wengi hufaulu.
Mwalimu :        Nakupa shukrani sufufu kwa kunifaa la jua. Bila shaka ningekuwa kwenye giza totoro kuhusiana na uuzaji huo wa dawa za                                kulevya. Naomba kuwepo ushirikiano wa dhati baina ya utawala wa shule na viranja kwa kuwa kofi hazilii ila kwa viganja viwili.                          Sisi kama utawala wa shule hii ya Twasonga, tutahakikisha kuwa tumekomesha utumizi wa dawa za kulevya. Kuwa na wakati                            mwema.
Mwanafunzi :   Asante sana. Pia nawe. (Anamsalimia.Kisha anainuka na kuondoka)

  1. Kwa nini mwanafunzi alimwendea mwalimu?
    1. Alitaka kumsalimia mwalimu wake
    2. Alitaka kujua kutoka kwa mwalimu wake shule zingefungwa lini
    3. Alitaka mwalimu ajue kuwa Kamaliza alikuwa akilangua dawa za kulevya.
    4. Alitaka kuripoti mateso aliyokuwa akipitia shuleni.
  2. Wateja wa dawa za kulevya zilizouzwa na Kamaliza:-
    1. walikuwa wanafunzi wa gredi ya nne
    2. walikuwa wanafunzi wa gredi ya sita
    3. walikuwa wanafunzi wa gredi ya tano
    4. walikuwa wanafunzi wa gredi ya tatu
  3. Ni methali gani mwafaka kuelezea kauli ifuatayo:- Jambo linaloshughulikiwa na wengi hufaulu?
    1. Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu 
    2. Aliye juu mngoje chini
    3. Bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi
    4. Polepole ndio mwendo
  4. Mwalimu ameonyesha wazi kuwa:-
    1. hata kama mwanafunzi hangemwambia alikuwa akijua kuhusu uuzaji wa dawa za kulevya
    2. kama si mwanafunzi huyo hangejua kuhusu uuzaji wa dawa za kulevya 
    3. hakutaka kujulishwa kuhusu uuzaji wa dawa za kulevya
    4. Kamaliza alikuwa mwanafunzi mwadilifu
  5. Kofi hazilii ila kwa viganja viwili ni mfano wa:-
    1. nahau C. tashbihi
    2. istiara
    3. tashbihi
    4. methali

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali nambari 6 mpaka 9.

Hapo zamani za kale Bweha, Ndovu, Simba na Tausi walikutana msituni karibu na kisima. Punde si punde, Ndovu alianza kutikisa masikio yake makubwa akawatazama wenzake na kujisifu.

"Bila shaka mtakubaliana nami kuwa mimi ndimi mnyama mwenye nguvu kuliko wanyama wote duniani. Ninaweza kupitia msitumi kwenye miti tele kwa kutumia mkonga wangu mrefu. Kwangu miti ni kama matawi," akajivuna.

"Huenda ukawa na nguvu" akalalama simba, "lakini hakuna kinachomithilishwa na ukali wangu. "Mimi ni mfalme wa msituni kwa sababu ya ukali wangu."

"Haiwezekani asilani.Maarifa na ujanja ni muhimu kuliko ukali na nguvu," akasema Mbweha. "Mimi huishi vyema kwa sababu ya akili zangu."

  1. Ni mnyama yupi ambaye hajatajwa kwenye kifungu?
    1. Mbweha
    2. Ndovu
    3. Simba
    4. Chui
  2. Chagua kauli isiyo ya kweli
    1. Ndovu alidai kuwa mnyama mwenye nguvu kuliko wote
    2. Simba alidai kuwa mnyama mkali kuliko wote
    3. Mbweha alidai kuwa mnyama mwenye akili kuliko wote
    4. Tausi alidai kuwa ndege mwenye urembo kuliko wanyama wote.
  3. Ni nini muhimu kuliko ukali na nguvu?
    1. Maarifa na ujanja
    2. Ujanja na ukali
    3. Nguvu na maarifa
    4. Wema na hekima
  4. Ni mnyama yupi alimpinga ndovu?
    1. Tausi
    2. Mbweha
    3. Simba
    4. Chui

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 10 mpaka 12.

Familia ya akina Bidii iliamua kutengeneza ratiba ya mapishi nyumbani kwao. Bidii, Zubedia, Hekima na Atieno walipendekeza aina ya vyakula ambavyo wangependelea kupika wikendi. Tazama jedwali lifuatalo

 Jamaa   Jumamosi   Jumapili  
 Bidii  Chapati  Pilau
 Zubedia   Ugali  Chapati
 Hekima  Sima  Chapati
 Atieno  makande  Pilau

 

  1. Ni chakula kipi kilipendekezwa mara nyingi?
    1. Chapati
    2. Pilau
    3. Makande
    4. Sima
  2. Taja jamaa wawili waliopika chakula sawa?
    1. Bidii na Hekima
    2. Atieno na Zubedia
    3. Zubedia na Hekima
    4. Bidii na Zubedia
  3. Ni chakula kipi hakikupendekezwa mara nyingi? 
    1. Chapati
    2. Pilau
    3. Sima
    4. Makande

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 13 mpaka 15.

Hapo zamani za kale, nyani na mamba walikuwa marafiki wa kufa kuzikana. Watoto wao walipendana na kufaana kama ndugu wa toka nitoke."Familia ya mamba iliishi mtoni nayo ya nyani iliishi katika msitu uliokuwa maili thelathini kutoka mtoni. Kila mara marafiki hawa walitembeleana na kusaidiana kwa hali na mali. Kwa vile mamba alikuwa mvuvi mashuhuri, aliweza kumsaidia nyani na familia yake kwa samaki wa aina mbalimbali. Nyani naye alimpelekea mamba matunda na nafaka kutoka shambani mwake.

  1. Chagua kauli ya kweli
    1. Nyani na mamba walikuwa maadui wakubwa
    2. Familia ya mamba iliishi msitumi
    3. Msitu ulikuwa mita thelathini kutoka mtoni
    4. Mamba alikuwa mvuvi mashuhuri
  2. Nyani naye alimpelekea mamba matunda pamoja na haya yote ila 
    1. Mahindi
    2. Maharagwe
    3. Mtama
    4. Mawele
  3. Hii ni tamathali gani ya lugha?
    Watoto wao walipendana na kufaana kama ndugu wa toka nitoke
    1. Tashbihi
    2. Istiara
    3. Chuku
    4. Tanakali za sauti

Soma kifungu kifuatacho. Kina nafasi 16 hadi 20. Umepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.

Katika enzi za mababu ___16___ wanyama ___17___ waliishi jinsi sisi binadamu ___18___ Waliweza kulima, kufuga, kuchota maji na hata kupika. Wanyama wote waliishi katika jamii tofauti tofauti kwenye vijiji. Vijiji kadhaa kwa pamoja___19___miliki iliyotawaliwa na mnyama
mmoja ___20___ na wanyama wengine kuwa mfalme wao.

   A   B   C   D 
 16.   yetu   wetu   zetu   letu 
 17.  sote  wote   zote   yote 
 18.  tunavyolishi   tunaishi   anaishi   aliishi 
 19.  ziliunda  iliunda   uliunda   viliunda 
 20.  aliyochaguliwa   aliyechaguliwa   aliochaguliwa   alivyochaguliwa 

 

Kuanzia swali nambari 21 mpaka 30, jibu kulingana na maagizo.

  1. Kivumishi ni kipi katika sentensi hii?
    Mwalimu mpole alienda shambani jana.
    1. mwalimu
    2. mpole
    3. alienda
    4. shambani
  2. Andika wingi wa sentensi ifuatayo:-
    Yai langu limepikwa na tarishi
    1. Mayai yangu yamepikwa na tarishi 
    2. Mayai yetu yamepikwa na tarishi
    3. Mayai yangu yamepikwa na matarishi
    4. Mayai yetu yamepikwa na matarishi
  3. Chagua sentensi iliyoakifishwa kwa usahihi
    1. Wanyama wafugwao ni pamoja na: ng'ombe, mbuzi na kondoo
    2. Ukienda ng'ambo uniletee yafuatayo: vikoi, saa na mkufu
    3. Ala, kumbe unajua kuendesha baiskeli
    4. Mwalimu alipoingia darasani! alikuwa na furaha
  4. Tunasema darasa la wanafunzi na _______________________ la nyuki
    1. bumba
    2. kundi
    3. fungu
    4. jamii
  5. Kitenzi 'panda' katika kauli ya kutendwa ni ____________________
    1. pandisha 
    2. pandika
    3. pandwa
    4. pandia 
  6. Chagua majina yaliyo katika ngeli ya U-U
    1. Ugonjwa, uyoga
    2. Ugali, uyoga
    3. Ute, uzi
    4. Ua, uji
  7. Kanusha sentensi ifuatayo:-
    Mwalimu ameelekea darasani
    1. Mwalimu hajaelekea darasani
    2. Mwalimu huwa hataelekea darasani
    3. Mwalimu huwa haelekei dukani
    4. Mwalimu hakuelekea dukani
  8. Ni sentensi gani yenye kielezi cha wakati?
    1. Mwalimu mpole ni huyu
    2. Magari ya safari Rally ni mengi
    3. Babu yangu atawasili kesho
    4. Ni wanafunzi wangapi wako huku?
  9. Ni sentensi gani yenye kivumishi cha pekee
    1. Mwanariadha mwingine ametuzwa 
    2. Vyote ulivyoleta vimeharibika 
    3. Uliza maswali mengi lakini yaliyo na umuhmu
    4. Wasanii wawili ndio wanaohitajika
  10. Kupiga miguu ni sawa na:
    1. Kukimbia kwa kasi
    2. Kutuliza miguu
    3. Kuteleza matopeni
    4. Kutembea

INSHA

Mwandikie rafiki yako barua ukimwelezea jinsi likizo yako ilivyokuwa.

MARKING SCHEME

  1. C
  2. B
  3. A
  4. B
  5. D
  6. D
  7. D
  8. A
  9. C
  10. A
  11. C
  12. D
  13. D
  14. B
  15. A
  16. C
  17. B
  18. A
  19. D
  20. B
  21. B
  22. D
  23. B
  24. A
  25. C
  26. B
  27. A
  28. C
  29. A
  30. D

INSHA    

Andika insha ya kusisimua ukimalizia kwa maneno yafuatayo:

.....................................................................................................Baada ya kisa hicho cha kuatua moyo, wanakijiji waligundua umuhimu wa kushirikiana.

 MASWALI

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.

Wanasiasa wa humu nchini sasa wametulia utadhani ___1___. Kila mwanajamii anasubiri kwa hamu na hamumu ___2___ kwa miradi mbalimbali waliyokuwa ___3___na ___4___ wao mwaka jana. Ni kweli kuwa kunao wale ambao wataziheshimu na ___5___ ahadi zao. ___6____, kunao wale ambao hata kuonekana kwao katika maeneo wanayoyawakilisha kutakuwa sawa na kuliona ___7___ hadi miaka mingine ___8___ ipite.

   A   B   C   D 
 1.   upepo wa tufani   maji ya mtungi   moto wa kifuu   maji ya bahari 
 2.  kuteketezwa  kutekelezwa   kutelekezwa   kutekelezewa 
 3.  wameahidiwa  wametendewa   wameahirishiwa   wameamuliwa 
 4.  washikadau  wapiga kura   wananchi   wawakilishi
 5.  kuzidunisha  kuziacha  kuzidhalilisha  kuzidumisha 
 6.  Kwa hivyo  Hivyo basi  Hata hivyo     Sasa basi
 7.  tone la maji    kaburi la baniani   vumbi la jangwani    ghubari la vumbi 
 8.  mitano  miwili  saba  tisa


Mchuano wa kombe la dunia mwaka uliopita ___9___ mataifa mengi ya humu barani na ya ___10___ Timu nyingi zilionyesha umahiri huku makocha wao wakizitolea maagizo. Hakuna kocha aliyetaka timu yake ___11___kwani___12___. Kipute hicho kilichoandaliwa nchini Qatar kilidhihirisha kuwa mchezo wa ___13___ huwa na mashabiki wengi zaidi. Hivi ni kutokana na ___14___ mkuu uliokuwa uwanjani. Mwisho wa kinyang'anyiro hicho, wanasoka wa Ajentina ___15___ washindi.

   A   B   C   D 
 9.   uliyavuta   uliyavutia   liliyavutia  liliyavuta 
 10.   ughaibuni   mbali   Kenya   Afrika 
 11.  ishinde   icheze   ishindwe   iongoze 
 12.  mcheza kwao hutuzwa   kazi mbi si mchezo mwema   angurumapo simba hucheza nani?  mwamba ngoma huvutia kwake 
 13.  kadanda  shoka  ngozi  kabumbu 
 14.  mlolongo  watu  timu  umayamaya
 15.  waliibuka  waliepuka  walilipuka  walikurupuka


Kutoka swali la 16 hadi 30. jibu kulingana na maagizo

  1. Mwanafunzi mkaidi alionywa ingawa hakusikia. Maneno yaliyopigiwa mistari ni 
    1. kiwakilishi, kiunganishi.
    2. kiunganishi, kiwakilishi.
    3. kivumishi, kiunganishi. 
    4. nomino, kiwakilishi.
  2. Chagua sentensi iliyo katika wakati uliopo.
    1. Mzazi alimnunulia mwanawe sare mpya.
    2. Bwana Ngao amelilima shamba lote.
    3. Wanafunzi hawaimbi darasani.
    4. Hatutasafiri hadi wiki ijayo.
  3. Bata amemdonoa duduvule katika hali ya wingi ni
    1. mabata wamewadonoa duduvule. 
    2. bata wamewadonoa duduvule. 
    3. mabata wamewadonoa maduduvule.
    4. bata wamewadonoa maduduvule.
  4. Mgomba huzaa ndizi, nao mbuni huzaa
    1. mikahawa.
    2. buni.
    3. mbuni
    4. karakara.
  5. Sehemu ya mwili inayosafirisha damu ni
    1. moyo.
    2. figo
    3. mifupa.
    4. mishipa.
  6. Chagua orodha ya vimilikishi pekee. 
    1. wa, cha, vya, la.
    2. huyu, hao, kile, huo. 
    3. yangu, kwangu, lake, lao.
    4. piga, cheza, lima, simama.
  7. Kamilisha tashbihi:
    Wanafunzi hawa ni wasiri kama
    1. kaburi.
    2. giza
    3. kondoo.
    4. mchana.
  8. Sungura ni kwa kitungule. Bata ni kwa
    1. kisuse.
    2. kisui.
    3. kiyoyo.
    4. kifaranga.
  9. Kanusha sentensi ifuatayo:
    Ungekuwa mgonjwa ungetibiwa.
    1. Hungekuwa mgonjwa hungetibiwa.
    2. Hangekuwa mgonjwa hangetibiwa.
    3. Usingekuwa mgonjwa usingetibiwa.
    4. Usingalikuwa mgonjwa usingalitibiwa.
  10. Watoto 12 222 kwa maneno ni watoto 
    1. kumi na wawili elfu, mia mbili ishirini na wawili.
    2. kumi na mbili elfu, mia mbili ishirini na mbili.
    3. kumi na wawili elfu, mia mbili ishirini na mbili.
    4. kumi na mbili elfu, mia mbili ishirini na wawili.
  11. Ni ipi hapa ni zana ya vita?
    1. Kayamba.
    2. Firimbi
    3. Nyambizi.
    4. Mkuki.
  12. Akina Pendo hupenda kujifunika 
    1. tiki.
    2. gubigubi.
    3. chekwachekwa
    4. mkikimkiki
  13. Tumia kiulizi pi kwa usahihi.
    Manukato ya mama ni
    1. ipi?
    2. yapi?
    3. zipi?
    4. upi?
  14. Tumia-ingine na -enyewe kwa usahihi.
    Ubao ________________ ulianguka sakafuni ________________.
    1. mwingine, wenyewe
    2. mwingine, yenyewe
    3. wengine, penyewe
    4. nyingine, wenyewe
  15. Je, ni neno gani lililo na silabi changamano?
    1. Mbwa
    2. Mbu
    3. Mtu
    4. Mbweha

Soma kifungu kisha ujibu maswali 31 hadi 40.   

Ilikuwa Jumamosi yenye baridi shadidi na umande uliotanda. Mashaka aliamua kuingia afisini. Aliingia bila woga wala wasiwasi, utoke wapi? Kilichomkaa akilini ni wingi wa maswali. Jambo usilolijua ni kama usiku wa giza. Moja alikuwa na hakika nalo: hakuna tamaa ya heri.

Alipoingia, alisimama mkabala na mwenye afisi, "Shikamoo bwana," akamwamkia. Aliyemwamkia hakutikisika wala kugeuka ila aliinamia jalada fulani akawa anatafakari au anasoma kitu fulani. Lo! Ishara mbaya kwa Mashaka ambaye alijikuta katikati ya chumba pasi na mwenzi wala mwenyeji. Akawa mgeni katika chumba ambacho zamani alizoea kukiingia. Alimtumbulia macho baba yake na kushangazwa na tabia yake ya kujitia hamnazo.

Hali katika afisi ilimkumbusha Mashaka siku zile alipokuwa shuleni. Kulikuwa na mwalimu mmoja mkorofi ambaye kila alipopelekewa hesabu kusahihisha, akiwa na kazi yake ya kusoma au kuandika mezani, ungesimama kwa muda mrefu kabla hajalipokea daftari lako kulisahihisha. Kisha alipolichukua kulisahihisha, ikatokea kuwa umekosea hata hesabu moja tu, basi huenda asingaligusa kabisa daftari lako. Hayo ya mwalimu yalikuwa afadhali. Bwana Juba hakumtambua hata mwanawe wa kumzaa.

Bwana Juba aliinama kwa muda jicho lake kali nyuma ya miwani-miwani iliyosimama juu ya uti wa pua-iliyoenda sawia na karatasi alizozifunua kwenye jalada. Naam, ukweli ni kuwa, Mashaka alizubaa zubezube na kuduwaa waa, asijue la kufanya. Alisimama mbele ya Bwana Juba kama mlingoti, hatikisiki, huku mikono yake kaifumbata na huku akimkagua Bwana Juba ambaye alikuwa kamvalia mwenziwe miwani ya mbao kama vile hakuwa mle afisini..

Mashaka alichukua nafasi hiyo kuukagua utukufu wa bwana yule, nao si haba! Isitoshe, jinsi afisi yenyewe ilivyopambwa, makochi ya kisasa yenye matakia manene ya kahawia, katikati meza ndogo iliyochutama na kubeba bakuli kubwa la maua, vitabu, majarida na magazeti machache yaliyopangwa hapo kwa madoido. Na matendegu je? Yalisimama tisti kwenye zulia jekundu lenye mapaku ya maua ya kutupiatupia ya manjano ambalo lilifunika sakafu nzima.

  1. Mashaka aliingia afisini akiwa
    1. ameaibika.
    2. na woga.
    3. jasiri.
    4. dhaifu.
  2. Kulingana na ufahamu, mwenye afisi alikuwa nani?
    1. Mashaka.
    2. Ndugu wa Mashaka.
    3. Baba wa Mashaka.
    4. Rafiki wa Mashaka.
  3. Jambo usilolijua ni kama usiku wa giza  ni
    1. nahau.
    2. methali.
    3. istiara.
    4. tashbihi.
  4. Ni jambo gani halikuwa la kawaida? Mashaka
    1. kupuuzwa na mwenye afisi.
    2. kutambuliwa na mwenye afisi.
    3. kuanza kuizoea afisi.
    4. kumpata asiyemjua afisini.
  5. Kulingana na Mashaka, mwalimu wao wa Hesabu alikuwa
    1. mvumilivu.
    2. mkorofi.
    3. nadhifu.
    4. makini.
  6. Mashaka alipojaribu kumwamkia mwenye afisi,
    1. Bwana Juba alikuwa akilala.
    2. kulikuwa na wageni afisini.
    3. Bwana Juba alikuwa ameinamia jalada fulani.
    4. kulikuwa na kazi nyingi zilizokuwa zikifanywa.
  7. Mashaka aliduwaa kwa sababu
    1. Bwana Juba alikuwa amehuzunika.
    2. hakuna aliyekuwa akiongea naye. 
    3. uchafu ulikuwa umetapakaa afisini. 
    4. alikuwa amepoteza matumaini.
  8. Yaelekea Mashaka alienda afisini kufanya nini?
    1. Kuonana na wafanyakazi wake.
    2. Kuongea na Bwana Juba.
    3. Kumaliza kazi yake.
    4. Kumjulia hali baba yake.
  9. Neno zulia kama lilivyotumika linaleta dhana ya
    1. kitambaa cha kupambia dirisha.
    2. aina ya kiti.
    3. kataza mtu kufanya jambo.
    4. tandiko la sakafuni.
  10. Afisi inayozungumziwa ilikuwa na
    1. viti vikuukuu.
    2. viti visivyo na thamani.
    3. pesa nyingi.
    4. viti vyenye thamani.

Soma kifungu kisha ujibu maswali 41 hadi 50.   

Utalii ni kati ya sekta muhimu sana zinazochangia ukuaji wa uchumi katika taifa la Kenya. Tunajivunia utalii, hali ya kusafiri kutoka kwako au kwenu ili kwenda kwingine kujifurahisha nafsi au hata kujifunza mambo mageni. Kuna aina mbili za utalii; utalii wa kitaifa na ule wa kimataifa. Wapo watalii wanaozuru nchi zao kujiburudisha na kujielimisha na wengine wanaovuka mipaka ya nchi zao.

Humu nchini, Mola ametutunukia mengi, mengi zaidi ya nchi nyingi duniani, hata ingawa kila nchi inacho angalau cha kujivunia. Kivutio kikuu humu nchini ni tamaduni zetu na wanyamapori. Wanyama hawa ni fahari ya nchi yetu. Wamechangia pakubwa katika ujenzi wa taifa kutokana na pesa za kigeni. Baadhi ya vivutio vingine ni maliasili mengi tuliyonayo.

Wanyama tunaojivunia nchini ni pamoja na twiga, simba, ndovu, kifaru, viboko na kadhalika. Wanyama hawa hususan huwa wanatengewa sehemu maalumu. Sehemu hizi aghalabu humilikiwa na serikali. Ili kuingia na kuwaona wanyama hawa, mtu hulazimika kulipa kiwango fulani cha pesa. Hakuna cha bwerere eti!

Licha ya kuwa wanyama hawa huletea nchi yetu sifa na faida chungu nzima, wao husababisha madhara pia. Mara kwa mara, simba wamekuwa wakitoroka mbugani. Madhara huwa wazi na huwa hayakadiriki. Simba na raia hupoteza maisha yao huku mifugo wakiwa hatarini kwani hufanywa kitoweo. Ndovu na viboko hawajaachwa nyuma. Wao huyavamia mashamba na kusababisha uharibifu mkubwa. Hali hii huleta njaa. Licha ya hali hii, tunalo jukumu la kuwalinda wanyama hawa. Tusiwe majangili tunaotafuta pembe za ndovu, na iwapo utakutana na mmoja, basi usikose kumripoti. Unahimizwa kupiga ripoti katika kituo cha polisi kilicho karibu au kupiga simu kwenda nambari 999. Moto unaowashwa misituni pia ukomeshwe. Vilevile, ukulima unaoendelezwa mbugani pia ukomeshwe. Sote tuungane pamoja tuwalinde wanyama wetu.

  1. Kulingana na aya ya kwanza,
    1. utalii ndiyo sekta ya pekee inayokuza uchumi.
    2. utalii haukuzi sana uchumi.
    3. wakenya wengi aghalabu hawajivunii utalii.
    4. utalii ni mojawapo ya sekta zinazokuza uchumi.
  2. Kulingana na kifungu,
    1. watalii ni wazungu wanaokuja nchini. 
    2. watalii hutoka nje na ndani ya nchi. 
    3. watalii daima huleta tabia mbaya nchini.
    4. hatuna mengi nchini ya kutalii.
  3. Taarifa yasema kuwa kivutio kikuu cha watalii ni
    1. maliasili na tamaduni.
    2. wanyamapori na tamaduni.
    3. wanyamapori na maliasili.
    4. tamaduni pekee.
  4. Mwandishi anaposema kuwa wanyama watengewe sehemu maalumu, bila shaka anarejelea
    1. mbuga.
    2. nyika.
    3. misitu.
    4. pori.
  5. Neno chungu kama lilivyotumika katika ufahamu lina maana ya
    1. chombo cha kupikia.
    2. inayouma.
    3. isiyo tamu.
    4. nyingi.
  6. Ni methali gani inayofaa kutoa mukhtasari wa mwanzo wa aya ya nne?
    1. Hakuna masika yasiyokuwa na mbu. 
    2. Zimwi likujualo halikuli likakuisha. 
    3. Uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mti.
    4. Mtaka unda haneni.
  7. Hasara zinazosababishwa na wanyama si pamoja na
    1. kuvamia mashamba.
    2. kuangamiza mifugo.
    3. kusababisha vifo.
    4. kubuni nafasi za ajira.
  8. ...pembe za ndovu ni sawa na
    1. vipusa. 
    2. tembo. 
    3. mikonga.
    4. mabori.
  9. Mwandishi asema kuwa
    1. wanyama wanaovamia mashamba wanaweza kuuawa.
    2. ili kuwaona wanyama, mtalii hulipa kiingilio.
    3. nchi nyingine hazina kivutio chochote cha watalii.
    4. mifugo huwala wanyama wanaowavamia.
  10. Mwisho kabisa, msemaji anamalizia kwa
    1. lawama.
    2. kero
    3. ombi.
    4. shime.

MARKING SCHEME

  1. B
  2. B
  3. A
  4. D
  5. D
  6. C
  7. B
  8. A
  9. B
  10. A
  11. C
  12. D
  13. D
  14. D
  15. A
  16. C
  17. C
  18. A
  19. B
  20. D
  21. C
  22. A
  23. C
  24. C
  25. D
  26. D
  27. B
  28. B
  29. A
  30. D
  31. C
  32. C
  33. B
  34. A
  35. B
  36. C
  37. B
  38. C
  39. D
  40. D
  41. D
  42. B
  43. B
  44. A
  45. D
  46. A
  47. D
  48. D
  49. B
  50. D

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1-5.

(Mwalimu na wanafunzi wamo katika mjadala kuhusu umuhimu wa kuyatunza mazingira
Bi Muli:          Salaam aleikum wanafunzi. M hali gani?
Wanafunzi:    (Wakiamka sawia) Njema Bi Muli, shikamoo.
Bi. Muli:         Marahaba (anawaashiria wakae) Naam, leo ningependa tuzungumze kuhusu namna n umuhimu wa kuyatunza mazingira kwa                         kuwa mazingira machafu huweza kutuletea magonjwa hatari.
Sofa:              Samahani mwalimu, mazingara ni nini? (Akionyesha uso wa kuchanganyikiwa
Bi Muli:          Sofia, si mazingara, ni mazingira. Haya ni yote ambayo...
Peru:              (Akiunyanyua mkono wake) Samahani mwalimu, naweza kulijibu swali hilo. Haya ni yote ambayo yanatuzunguka.
Bi Muli:          Makofi kwa Peru. (Wenzake wanampigia makofi kwa kujibu swali kwa usahihi). Safi. Ili kuyalinda mazingira, tunaweza kukata                        nyasi ndefu zinazowafuga mbu.
Maloba:         Vile vile, tunaweza kuhakikisha vyanzo vya maji vi safi. Hivi ni kama vile mito, maziwa na mabwawa.
Ali:                 Nadhani kuwa kuna hatari aidha katika kutumia mbolea za madukani kiholela. Zikitumiwa kupita kiasi huweza kuathiri udongo                         na hatimaye vyanzo vya maji. 
Bi Muli:           Vyanzo vya maji vinapoathirika, viumbe vya majini kama vile samaki, mamba, mimea na wanyama wengine huweza                                       kuathirika pakubwa. Kesho tutaandika insha kuhusu umuhimu wa kuyatunza mazingira. Kwaherini kwa sasa.
Wote:              Kwaheri ya kuonana mwalimu.

  1. Kulingana na maelezo ya mwalimu, mazingira machafu yana madhara gani? Huweza
    1. kuchafua vyanzo vya maji.
    2. kusababisha magonjwa. 
    3. kudumisha afya bora.
    4. kutukinga dhidi ya magonjwa.
  2. Peru alipigiwa makofi kwa sababu
    1. alilijibu swali la mwanafunzi mwenzake kwa usahihi.
    2. alikuwa mwanafunzi bora darasani mwao.
    3. alijaribu kulijibu swali la Sofia.
    4. alishindwa kulijibu swali la Sofia.
  3. Kulingana na mazungumzo haya, mbolea za madukani zikitumika kupita kiasi 
    1. huweza kusababisha hali mbaya ya anga.
    2. huweza kuchafua hewa.
    3. huathiri udongo na vyanzo vya maji. 
    4. huchafua pakubwa vyanzo vya maji
  4. Vyanzo vya maji vรญnapoathirika,
    1. wanyama wa porini huangamia. 
    2. nyuni wa angani hufa.
    3. wanadamu hupata taabu.
    4. wanyama wa majini huathirika.
  5. Chanzo gani cha maji hakijatajwa katika mazungumzo haya?
    1. Mito.
    2. Mvua.
    3. Mabwawa.
    4. Maziwa.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswall 6 hadi 8

Rununu yake ilikiriza mara kadhaa lakini akashindwa kuiwahi. Kichwa chake kilimwanga vilivyo. Usiku uliotangulia alikuwa amepiga maji na kulewa chakari. Hakuelewa alivyofika kitandani pake. Mlaraha alikuwa mwizi hatari. Hii ilikuwa shughuli haramu na hatari kweli kweli. Aliitazama simu yake ya mkononi ilivyokuwa imechakaa. Ghafla, mlango wake ukabishwa kwa kishindo. Alisita kidogo huku akijiuliza kama kweli alikuwa na ahadi ya kukutana na yeyote asubuhi hiyo.

Kufumba na kufumbua, pu! Mlango ulipigwa teke na kuanguka kando. Mlangoni walisimama maafisa wanne wa polisi na bastola huku wawili wakiwa na pingu mikononi. Mlaraha aliinua mikono juu ishara ya kusalimu amri. Moyoni alijua kuwa zake arubaini zilikuwa zimetimia. Naam, uhalifu haulipi chochote.

  1. Mlaraha hakuweza kuiwahi rununu yake kwa kuwa
    1. kichwa chake kilikuwa kizito.
    2. ilikuwa mbali.
    3. hakutaka kufanya hivyo.
    4. aliogopa kuzungumza na aliyekuwa akipiga.
  2. Chagua orodha ya sifa za Mlaraha kulingana na kifungu.
    1. Mwizi, mpole.
    2. Mlevi, mwizi.
    3. Mjeuri, mlevi.
    4. Mwizi, katili.
  3. Ni kweli kuwa waliobisha mlango walikuwa
    1. wenzake Mlaraha katika wizi.
    2. majirani waliotaka kumjulia hali Miaraha.
    3. maafisa wa polisi.
    4. waumini wa dhehebu aliloshiriki.
  4. Methali gani inayoweza kutumika kufupishia kisa hiki?
    1. Pwagu hupata pwaguzi.
    2. Mgaagaa na upwa hali wali mkavu. 
    3. Kawia ufike.
    4. Siku za mwizi ni arubaini.

Sema kifungu kifuatacho kisha ulibu maswoll 10 hadi 12   

Uhalifu ni hali ya kutenda kinyume na zinavyohitaji sheria za nchi ambazo siku zote huongozwa na katiba. Kunavyo viwango mbalimbali vya uhalifu katika jamii. Uhalifu hutendeka katika maeneo mbalimbali. Hata hivyo, kuna njia kadhaa za kukabiliana na uhalifu. Kwanza, wananchi wakiacha tabia za kuwaficha wahalifu miongoni mwao, uhalifu utapungua. Vile vile, wale ambao hupokea hongo wanastahili kufunguliwa mashtaka. Si hayo tu, uhalifu aidha huweza kupungua iwapo sehemu mbalimbali za umma kama vile afisini zitawekewa kamera za siri. Kwa jumla, kila mwanajamii akisimama kidete kupambana na uhalifu, tutaweza kujivunia kupungua kwa uhalifu.

  1. Mwandishi ametaja njia ngapi za kukabiliana na uhalifu?
    1. Tano.
    2. Nne
    3. Mbili.
    4. Tatu.
  2. Kulingana na habari hii, kamera za siri zinaweza kudhibiti uhalifu
    1. nyumbani.
    2. afisini.
    3. shuleni
    4. sokoni.
  3. Kwa jumla, jukumu la kudhibiti uhalifu ni jukumu la nani?
    1. Serikali.
    2. Watu wazima.
    3. Kila mmoja.
    4. Wazazi.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 13 hadi 15.

Shughuli kama vile kuogelea, kandanda, riadha na urukaji viunzi huitwa michezo. Shughuli hizi si muhimu tu katika kuijenga miili yetu bali pia huchangia kuwaleta watu pamoja. Michezo baina ya shule mbalimbali huwaleta wanafunzi pamoja ambapo wao huweza kubadilishana mawazo yanayoweza kuinua viwango vyao vya kimasomo. Shughuli za kimichezo aidha huchangia kutukinga dhidi ya magonjwa kama vile uzito wa mwili, ambayo hatimaye huweza kusababisha maradhi ya moyo. Baadhi ya wananchi hutumia michezo kama kitegauchumi cha kuwaletea pesa. Baadhi ya wanaspoti wamewahi kuiletea nchi yetu nishani na medali mbalimbali na hivyo kuiweka nchi yetu katika nafasi bora kimichezo.

  1. Chagua kauli isiyo sahihi kulingana na ufahamu.
    1. Shughuli za kimichezo si muhimu katika kuijenga miili yetu.
    2. Michezo haichangii katika kujenga miili yetu pekee.
    3. Wakati mwingine michezo huandaliwa baina ya shule mbalimbali.
    4. Baadhi ya watu hutumia michezo kama njia ya kujipatia riziki.
  2. Kulingana na habari hii, uzito wa mwili hatimaye huweza kusababisha
    1. mauti.
    2. uvivu.
    3. maradhi ya ngozi.
    4. maradhi ya moyo.
  3. Nchi yetu inapopata nishani na medali, 
    1. wananchi wengi hujiunga na spoti.
    2. hadhi yake kimichezo huinuka.
    3. hupoteza heshima yake kimichezo 
    4. huwa miongoni mwa mataifa yaliyotajirika.

Soma kifungu kifuatacho. Chagua jibu lifaalo zaidi kati va vale uliyopewa.

Mtoto ana haki ___16___. Yapo inahitaji ya kimsingi ambayo ni makazi, lishe na ___17___ haki ya mtoto kupata elimu___18___serikali ikaanzisha elimu ya bure katika shule za umma.___19___ anayemnyima intoto nafasi ya___20___shuleni lazima afikishwe mahakamani.

       A       B          C        D 
 16.   mingi   chache   zote   kadhaa 
 17.  elimu  makao  mavazi   maji 
 18.  sababu   maana   ili   ndipo 
 19.  Wowote   Yeyote  Yoyote   Wote 
 20.  kuenda  kufika  kusomesha   kuanguka 

 

Kutoka swali la 21-30. jibu swall kulingana na maagizo uliyopewa.

  1. Chagua kitenzi kilicholinganishwa visivyo na kinyume chake.
    1. Funga       fungua
    2. Shona       shonua
    3. Nuna         tabasamu
    4. Lia             cheka
  2. Kamilisha tashbihi hii: 
    Mariamu ana maneno mengi kama
    1. chiriku.
    2. tausi.
    3. kasuku.
    4. njiwa.
  3. Chagua ukubwa ws:
    Ndizi hizi ni ndogo.
    1. Dizi hili ni dogo.
    2. Kidizi hiki ni kidogo.
    3. Madizi haya ni madogo.
    4. Vidizi hivi ni vidogo.
  4. Chagua ukanusho wa sentensi ifuatayo:
    Wewe ulikuwa mgonjwa.
    1. Wewe haukuwa mgonjwa.
    2. Wewe hujawa mgonjwa.
    3. Wewe huwi mgonjwa.
    4. Wewe hukuwa mgonjwa.
  5. Chagua sentensi iliyo katika hali timifu.
    1. Mboso atauimba wimbo mpya.
    2. Kadogo amemaliza kuandika.
    3. Upepo haukuvuma kwa fujo.
    4. Walimu wanazungumza mkutanoni.
  6. Chagua wingi wa sentensi ifuatayo:
    Ufagio ulinunuliwa sokoni.
    1. Fagio zilinunuliwa masokoni.
    2. Ufagio zilinunuliwa sokoni.
    3. Fagio ulinunuliwa masokoni. 
    4. Ufagio ulinunuliwa masokoni.
  7. Chagua orodha ya nomino zilizo katika ngeli tofauti.
    1. Cheo, chupa.
    2. Magari, maua.
    3. Kiwavi, kipofu.
    4. Mitego, mikoba.
  8. Ni sentensi gani iliyo katika nafsi ya pili?
    1. Mlitutembelea jana kwa sherehe. 
    2. Alinunuliwa mwanasesere maridadi.
    3. Nimeamua kufanya bidii.
    4. Mwalimu aliyekuwa darasani ametoka.
  9. Chagua methali iliyo tofauti na nyingine kimatumizi.
    1. Kidole kimoja hakivunji chawa.
    2. Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.
    3. Mkono mmoja haumlei mwana.
    4. Mgaagaa na upwa hali wali mkavu.
  10. Chagua orodha ya majina ambayo ni visawe.
    1. Runinga, redio
    2. Ndovu, Pombe
    3. Mbung'o, ndorobo
    4. Ugonjwa, malaria

MARKING SCHEME

  1. B
  2. A
  3. C
  4. D
  5. B
  6. A
  7. B
  8. C
  9. D
  10. D
  11. B
  12. C
  13. A
  14. D
  15. B
  16. D
  17. C
  18. D
  19. B
  20. A
  21. B
  22. A
  23. C
  24. D
  25. B
  26. A
  27. A
  28. A
  29. D
  30. C

 INSHA

Anzisha insha yako kwa maneno haya:

Siku tuliyosubiri kwa hamu na ghamu iliwadia, hivyo basi sote .........

QUESTIONS

Soma kifungu kifuatacho. Kina nafasi hadi 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.

Kuoga ni ___1___ shartyi mtu ___2___kila wakati au kila siku. Hasa watoto ___3___kuoga ama kuogeshwa mara kwa mara. Watoto ___4___ jasho ___5___ wanapocheza. Jasho ___6___ huchanganyika na vumbi___7___ mahali ___8___. Nao wanapata ushafu. Baada
ya kupata uchafu ___9___ , ni lazima waoge. Tusipowasaidia watoto kutunza usafi ___10___ mili ___11___hawatakuwa na afya bora. ___12___magonjwa kama vile upele na harara ya ngozi. Usafi si muhimu kwa watoto tu ___13___ pia kwa watu ___14___. Hao ___15___
wasipooga ni hatari zaidi kuliko hata watoto wadogo

   A   B   C   D 
 1.   hiari   faradhi   kutaka   ngumu 
 2.   haogi   kuoga  aoge  anaoga 
 3.  hupasa   hupasua   hapaswa   hupaswa
 4.  hutoa  hutoka  hutia  hutokwa
 5.  mingi  nyingi  jingi  mengi
 6.  hilo  hiyo  huo  hizo
 7.  ya  za  la  vya
 8.  wanacheza   wanauchezea   wanapochezea   wanapocheza 
 9.  huo  hiyo  hilo  hizo 
 10.   ya  za  wa  la
 11.  zao  yao  lao  cha
 12.  watungua  wataugua  wataangua  watapungua
 13.  mbali  bali  wala  ili
 14.  wazima  wazimu  wasafi  yeyote
 15  ndipo  ndiye  ndio  ndivyo

 

Kutoka swali la 16 mpaka 30, chagua jibu lililo sahihi.

  1. "Sabalkheri wanafunzi," Mwalimu aliwasalimia wanafunzi wake. Huo ulikuwa wakati wa
    1. adhuhuri
    2. asubuhi
    3. jioni
    4. alasiri
  2. Chagua sentensi yenye kivumishi kiulizi
    1. Mashubaka haya yalitengenezwa lini?
    2. Leo wameapishwa wangapi?
    3. Wasusi, wanaelekea wapi?
    4. Huyu atavikwa pete gani?
  3. Andika sentensi hii kwa wingi
    Mtume huyo ana tunda hili
    1. watume hawa wana matunda haya
    2. Mitume hao wana matunda hizi
    3. Watume hao wana matunda haya
    4. Mitume hao wana matunda haya
  4. Miongoni mwa sehemu hizi za mwili ni sehemu ipi iliyo tofauti na zingine?
    1. Paja
    2. Kiganja
    3. Pafu
    4. Goti
  5. Methali inayofaa funzo kuwa;
    Mtu anaposababisha shida huishia kuwahusisha watu wake au jamaa yake ni 
    1. Kikulacho ki nguoni mwako.
    2. Mwiba wa kujichoma huambiwi pole.
    3. Mla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe. 
    4. Mchuma janga hula na wa kwao.
  6. Chagua sentensi iliyoakifishwa vizuri
    1. Lo? Amefika?
    2. Viti vyenu ni vipi?
    3. njoo nikutume!
    4. "mimi sisemi na mtu"
  7. Tumia kivumishi '-enye-'kwa njia sahihi
    Mbuzi____________madoadoa ni wangu.
    1. lenye
    2. chenye
    3. yenye
    4. mwenye
  8. Kamilisha methali hii
    Hakuna ____________________________________ yasiyo na mbu.
    1. masika
    2. vuli
    3. kiangazi
    4. kipupwe
  9. 'kazi ya kijungu jiko, 'ni kazi gani?
    1. kupika jikoni
    2. kukupatia riziki pekee
    3. kupika na kupakua
    4. kupika na jiko moja tu
  10. Nomino habari iko katika ngeli ya
    1. U-ZI
    2. I-I
    3. U-I
    4. I-ZI
  11. Chagua sentensi sahihi
    1. Viluwiluwi vile vilimezwa na samaki
    2. Mikebe hizo zimetupwa katika moto
    3. Ng'ombe hiyo ilikamuliwa maziwa
    4. mengi
    5. Wanajeshi wale walikuwa watiifu na wapole
  12. Wageni walikuja wakati ______________ tuliowangoja
    1. huu huu
    2. uo huo
    3. uu huu
    4. uo huu
  13. Ni saa ngapi sasa?
            C8MathT1BMQ28
    1. Saa kumi kasoro robo
    2. Saa nne kasoro robo
    3. Saa tisa kasoro robo
    4. Saa kumi na robo
  14. Andika kwa maneno tarakimu hii 8,000,001
    1. Milioni mia nane na elfu moja
    2. Milioni nane na moja
    3. Milioni mia nane na moja
    4. Milioni mi anane na mia moja
  15. Kipindi cha miaka mia huitwa
    1. muongo
    2. majira
    3. karne
    4. milenia

Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali kutoka 31-40.

Ni jambo la busara kwetu vijana kusikiliza mashauri tunayopewa na watu wazima kama vile wazazi na walimu kwani wametuzidi kwa maarifa. Ama kwa hakika,lolote lile wakuu wetu hutu.unbia yafaa tuzingatie tusije kufikwa na balaa iliyomfika kijana matatizo.

Matatizo alikuwa kijana mwenye sura nzuri na tabasamu ya kuvutia. Kwa nje aliweza kuwavutia wengi hasa wasiomjua. Hata hivyo, hakuna kizuri kisicho na dosari. Matatizo alikuwa na hulka mbaya isiyopendeza kwa watu wengi. Alikuwa mkali kama pilipili na mkaidi mfano wa mkia wa nguruwe. Tabia yake iliwashinda hata wazazi wake ingawa hawakusita kummwagia bahari ya maneno ya busara kwa tamaa ya kumwokoa.

Baadaye alipopelekwa shule angalau apate kisomo cha kumwekea nguzo maishani mwake, Matatizo alipatikana akishiriki visa vya ujeuri na kuwa mtundu. Visa hivi havikupungua, viliuma. Siku moja baba yake kijana huyu alishtuka alipojulishwa kuzidi kwa utundu wa mwanawe shuleni hasa alipoambiwa mtoto wake anapiga mtindi, hakosi sigara mdomoni na anashiriki wizi ili ajipatie pesa za kujitimizia haja zake. Matatizo alifukuzwa shule. Vitendo vya matatizo vilimtahadharisha mzee Toboasiri.

Wakati mmoja siku ya Jumapili alfajiri, mzee Toboasiri alijikuta ameshika mkongojo wake akienda kwake mzee Busara wakiwa na mzee Saidia.

Aliwaalika mkutano wa dharura nyumbani kwake siku iliyofuata. Wazee hawa wawili walipowasili, walimkuta Toboasiri na mtoto wake Matatizo wameketi kimya. "Wazee wenzangu," alianza huku sauti yake ikionyesha masikitiko, "Nimewaita hapa ili mnisaidie kumpa mawaidha kijana wangu. Nimejaribu niwezavyo kumkanya mwanangu dhidi ya matendo maovu lakini nimeshindwa. Nawaomba wazee wenzangu mnifanyie kazi hiyo."

Wazee hawa wawili walimshauri na kumshawishi Matatizo aache ile tabia yake mbaya. Kabla hawajamaliza, Matatizo alisimama huku akipandwa na hasira. Alifoka na kuwakodolea wale wazee macho huku amekunja uso wake na kuonekana kama jitu lililonyimwa chakula mwezi mzima.

Hapo alitoka nje, akawasha sigara kubwa na kupiga mikupuo miwili. Macho yakageuka na kuwa mekundu kami. pilipili. Akarudi na kumkabili mzee Busara. "Kwa vile unaitwa Busara, unadhani unahaki ya kunipa mawaidha, leo utanitambua. "Alimzaba mzee Busara kofi moja pa! Mzee huyu hakushimili kofi hilo na hapo akaanguka chini pu!

  1. Kulingana na aya ya kwanza, anayezungumza ni
    1. Toboasiri
    2. Matatizo
    3. Busara
    4. Mwandishi
  2. "Yafaa tuzingatie ya wakuu wetu tusije tukakumbwa na yaliyomkabili Matatizo" Ni methali gani isiyoambatana na maelezo haya?
    1. Usipoziba ufa utajenga ukuta
    2. Asiyesikia la mkuu hupatwa na makuu
    3. atangaye sana na jua hujua
    4. sikio la kufa halisikii dawa
  3. Kulingana na aya ya pili ni ipi si sifa ya matatizo?
    1. Alitemea mate nasaha za wazazi wake.
    2. Matatizo alikuwa mtanashati.
    3. Matatizo alikuwa mkaidi na mjanja.
    4. Tabia zake ziliambatana na sura yake.
  4. Lengo la Matatizo kupelekwa shuleni ni
    1. kupata masomo ili kuboresha maisha yake
    2. kuwafurahisha wazazi wake
    3. kuendelea kudumisha hulka yake
    4. kuelimika ili azidishe hulka yake
  5. Kulingana na kifungu hiki. Matatizo 
    1. Alibadilika alipoenda shuleni
    2. Alishiriki katika uvutaji sigara na kunywa pombe
    3. Alifanya bidii katika masomo yake
    4. Aliepukana na hulka ya wizi
  6. Baba yake matatizo ni
    1. mzee saidia
    2. mzee Busara
    3. Mzee Toboasiri
    4. Mwalimu mkuu
  7. Ni kweli kusema kuwa
    1. Baba yake matatizo alikuwa amefika mwisho
    2. Wazee walipoitwa hawakutoa nasaha
    3. Mkutano ulipangwa kwa siku nyingi
    4. Matatizo alitekeleza yote aliyoambiwa 
  8. 'kupiga mtindi' ni maneno yaliyotumiwa. Ni tamathali gani ya lugha?
    1. Istiari
    2. Nahau
    3. Methali
    4. Tashbihi
  9. Methali inayomlenga matatizo katika aya ya mwisho ni
    1. sikio la kufa halisikii dawa
    2. ushikwapo shikamana
    3. la leo litende leo
    4. aliyekalia kigoda mtii
  10. Neno 'foka' namna ilivyotumiwa katika kifungu hiki halima maana
    1. kughadhabika
    2. kuwa na mafutu
    3. kuwa na huzuni
    4. kupandwa na mori

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali ya 41-50.

Kulonga dhahiri shahiri Kiswahili ni mojawapo ya lugha za kimataifa zinazozungumzwa ulimwenguni. Hata hivyo inasikitisha sana sisi wenyeji wa eneo la Africa Mashariki ambao ni kitovu cha lugha hii, tumekuwa tukinyonga raslimali hii kwa ukatili mkubwa.

Ni aibu iliyoje kukitumia Kiswahili kiholela bila kuzingatia kanuni zake huku tukijidanganya kuwa sisi ni mahiri tunapokiporomosha Kimombo kwa usanifu mkubwa. Jinsi tunavyokitema kiingereza sawasawa. Kwa nini hali hii tusiizingatie katika lugha yetu tunu? Wageni kutoka nchi za ughaibuni waliopata fursa ya kuzuru eneo la Afrika Mashariki wametambua utamu wa Kiswahili wakajifunza wakajistawisha. Baadhi ya wageni hao wamekuwa walimu wa lugha hii.

Aidha tunazidi kukitia kitanzi Kiswahili kupitia uchapishaji wa magazeti yetu. Bei ya gazeti la kiswahili inaashiria uduni wake. Habari zinazochapishwa katika magazeti ya kiswahsili ni za kiwango cha chini na ni chache mno cha kuudhi zaidi ni kuwa baadhi ya kaifa za magazeti ya kiswahili hujikuta katika masuala ya kijamii kwa kiasi kikubwa na kuyapa kisogo au kugusia gusia tu mambo kuhusu uchumi,siasa na dini. Hakuna mazito kuhusu matangazo ya biashara. Hakuna habari ya vifo. Hakuna habari za ajira na kadhalika. Si ajabu wakati mmoja niliulizwa mtaani, "Hili gazeti ulilo nalo umemnunulia babu yako?" Swali hili lilinijulisha kuwa fikra za waja wengi imejengwa na mtindo wa wakati mrefu wa kuchapisha magazeti kwa njia hii; hivi kwamba magazeti ya kiswahili yanapaswa kusomwa na wazee na labda wale walioshindwa na masomo skulini.

Nawasihi wananchi wa eneo lote la Afrika Mashariki wazinduke na kukiendeleza kiswahili.

  1. Kulonga dhahiri shahiri ni sawa na;
    1. kunena ukweli
    2. kuamba bila hadaa
    3. kupiga vijembe
    4. kuongea waziwazi
  2. Maneno tunavyo kitema kiingereza yamepigiwa mstari. Maana yake ni
    1. Tunavyokikaia kiswahili
    2. Tunavyokikata kiingereza
    3. Tunavyokiongea kimombo barabara
    4. Tunavyokizungumza kiingereza ovyoovyo
  3. Neno lipi katika taarifa hii lina maana sawa na kaifa
    1. picha
    2. habari
    3. kurasa
    4. vichwa
  4. Kwa mujibu wa taarifa ni kauli gani sahihi?
    1. Magazeti ya kiswahili yana bei ghali
    2. Magazeti ya kiswaili huwavutia wengi kuyasoma
    3. Bei ya magazeti ya kiingereza ni rahisi
    4. Magazeti ya kiswahili yamedunishwa
  5. Watu mahiri ni watu
    1. woga
    2. wajuzi
    3. walaghai
    4. washindani
  6. Tunazidi kukitia kitanzi kiswahili ni
    1. kukfrunga kiswahili
    2. kukipa sifa kiswahili
    3. kukiharibu kiswahili
    4. kukienzi kiswahili
  7. Visawe vya neno waja si pamoja na
    1. Mahuluki
    2. Adinasi
    3. Nswi
    4. Wanadamu
  8. Kulingana na taarifa hii asili ya lugha ya kiswahili ni
    1. nchi ya ughaibuni
    2. nchi ya Kenya
    3. Afrika mashariki
    4. Hatujaambiwa
  9. Mwandishi anawashauri wakazi wa eneo la Africa mashariki
    1. wasiitumie kiswahili hadharani
    2. waache kutumia kimombo
    3. wakipe kiswahili kipaumbele
    4. wakididimize kiswahili
  10. Kichwa kifaacho taarifa hii ni
    1. Lugha za Afrika-
    2. Mbinu za kuboresha Kimombo
    3. Historia za kiswahili na kiingereza
    4. Kiswahili kitukuzwe

MARKING SCHEME

  1. B
  2. C
  3. D
  4. A
  5. B
  6. B
  7. A
  8. C
  9. A
  10. C
  11. B
  12. B
  13. B
  14. A
  15. C
  16. B
  17. D
  18. D
  19. C
  20. D
  21. B
  22. D
  23. A
  24. B
  25. D
  26. D
  27. B
  28. A
  29. B
  30. C
  31. D
  32. C
  33. D
  34. A
  35. B
  36. C
  37. A
  38. B
  39. A
  40. B
  41. D
  42. C
  43. B
  44. D
  45. B
  46. C
  47. C
  48. C
  49. C
  50. D

 MASWALI    

Soma vifungu vifuatavyo. Fina nafasi mpaka 15. kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya uliyopewa.

Katika baadhi ya ___1___ humu nchini, tatizo la uhaba wa maji ___2___ kuwaka kama ___3___. Wakazi wa maeneo hayo ___4___  changamoto kwani bei ya maji nayo imepanda maradufu. Wanaochuuza maji mitaani kwa ___5___ nao hawana ___6___  kwani ___7___ wakazi wa maeneo hayo na ___8___, wamepandisha bei ya bidhaa hiyo muhimu bila chembe ya hisia.

   A   B   C   D 
 1.   magatuzi   gatuzi   mataifa   mabara 
 2.  yanaendelea   inaanza   linaendelea   unazidi 
 3.  jua la mtikati  moto wa kifuu   hasira za mkizi   upepo wa tufani 
 4.  wamekumbwa   wamekumbana   wamekumba   wamekumbwa na  
 5.  mkokoteni  manowari   rukwama   helikopta 
 6.  amani  mioyo   shukrani   imani 
 7.  hawahurumii  hawawahurumii   hawawahurumi   hawahurumi 
 8.  badala yake  baada yake  kabla yake  mahali pake

 

Elimu ina ladha yake. Ingawa haihisiki kwa ulimi, utamu upo ___9___. Nasema hivi kwa sababu nimeyaona manufaa ya elimu. Nina uwezo wa kutambua maradhi kama ___10___ ambayo huambukizwa na ___11___ na mashairi ya aina nyingi kama vile ___12___ ambapo mshororo wa tano hukamilisha kila ___13___. Licha ya hayo, nimewafahamu wafanyakazi mbalimbali. ___14___ kuwa mfanyakazi anayeshughulikia mitambo ndiye
___15___

   A   B   C   D 
 9.   Ukiujua huu na huu huujui    Elimu ni taa, gizani huzagaa    Aisifuye mvua imemnyea   Msema pweke hakosi 
 10.   malaria  malale   Ukimwi   Korona 
 11.  chawa  kukohoa   ngono   mbung'o 
 12.  takhmisa  tarbia  tathlitha   tathmina 
 13.  mizani  ubeti   kina   ukwapi 
 14.  Ninamjua  Namjua   Ninafahamu   Ninamfahamu 
 15.  mwandishi  mhandisi   injini   sogora 

 

Kutoka swali la 16 hadi 30. jibu swali kulingana na maagizo.   

  1. Chagua sentensi yenye tanakali ya sauti.
    1. Lo! Kumbe alikuwa shangazi yake!
    2. Wanafunzi walisoma kutwa kucha.
    3. Sarafu ilianguka mchangani tifu! 
    4. Baba wa Juma ni mkali kama simba.
  2. Chagua kiwakilishi katika sentensi hii.
    Kijana huyu ni mzuri kushinda yule.
    1. yule
    2. mzuri
    3. huyu
    4. kushinda
  3. Tumia kirejeshi amba badala ya o-rejeshi.
    Wanafunzi waliofuzu vizuri walizawidiwa.
    1. Wanafunzi ambao waliofuzu vizuri walizawidiwa.
    2. Wanafunzi ambao walifuzu vizuri walizawidiwa.
    3. Wanafunzi ambaye walifuzu vizuri walizawidiwa.
    4. Wanafunzi ambayo walifuzu vizuri walizawidiwa.
  4. Kamilisha methali:
    Mwana wa kuku hafunzwi
    1. kuriaria
    2. kutembea
    3. kuchakura
    4. kupuruka
  5. Chagua majina yaliyo katika ngeli ya YA-YA pekee.
    1. Maumbo, maktaba, mate.
    2. Makawa, matatu, maji.
    3. Maradhi, maskanini, makavazi.
    4. Mafuta, mazingira, mauti.
  6. Ni neno gani halijaambatanishwa ipasavyo na jibu lake?
    1. Buriani  -  inshallah
    2. Makiwa  -   tunayo
    3. Alamsiki  -  binuru
    4. Sabalkheri  -  aheri
  7. Chagua sentensi iliyotumia o-rejeshi tamati kwa usahihi.
    1. Wageni wanaokuja ni wetu.
    2. Wanafunzi watakaotutumbuiza waje hapa mbele.
    3. Achanikaye kwenye mpini hafi njaa.
    4. Waliotuzwa wawape nafasi wengine watuzwe.
  8. Chagua sentensi sahihi kutokana na maneno haya:
    Kitabu, cha, nipe, vitate, hiki
    1. Nipe vitate cha hiki kitabu. 
    2. Kitabu hiki cha vitate nipe
    3. Nipe hiki kitabu cha vitate.
    4. Nipe kitabu hiki cha vitate.
  9. Makia ya mabuzi haya ni mafupi katika wastani ni
    1. mkia wa mbuzi huyu ni mfupi.
    2. mikia ya mbuzi hawa ni mifupi.
    3. mikia ya mbuzi hao ni wafupi.
    4. mkia wa mbuzi huyo ni mfupi.
  10. Ni ipi ala ya muziki kati ya maneno yafuatayo?
    1. Parapanda
    2. Manati
    3. Manowari
    4. Nyambizi
  11. Kanusha:
    Ningeenda ningempata akipepeta pojo kwenye ungo.
    1. Singeenda singempata akipepeta pojo kwenye ungo.
    2. Nisingeenda singempata akipepeta pojo kwenye ungo.
    3. Nisingeenda nisingempata akipepeta pojo kwenye ungo.
    4. Nisingeenda nisingepata akipepeta pojo kwenye ungo.
  12. Tegua kitendawili.
    Wanashindana wakifuatana.
    1. Kufuli
    2. Samaki
    3. Mtu na kivuli
    4. Magurudumu
  13. Chagua jibu linaloonyesha sifa iliyoundwa kutokana na nomino.
    1. Saka  -  msasi
    2. Ushujaa  -  shujaa
    3. Cheza  -  mchezo
    4. Lipa  -   malipo
  14. Chagua neno lenye sauti changamano.
    1. Mtoto
    2. Watoto
    3. Mwavuli 
    4. Wayo
  15. Upi ni usemi halisi wa sentensi ifuatayo?
    Maono alisema kuwa alikuwa akiwachukia waliowaajiri watoto.
    1. Maono alisema, "ninawachukia wanaowaajiri watoto.
    2. Maono alisema, "Ninawachukia wanaowaajiri watoto."
    3. Maono alisema, mimi siwapendi wanaowaajiri watoto.
    4. Maono alisema anawachukia wanaowaajiri watoto.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31 hadi 40.   

Ajali za barabarani nchini zimeongezeka maradufu. Swali ni je, nani aelekezewe kidole cha lawama? Ni serikali, ni madereva au ni sisi wasafiri? Hiki kimebaki kitendawili kisichoweza kuteguliwa. Kila siku utasikia kutoka kwenye vyombo vya habari watu walioaga dunia kutokana na ajali. Hili ni jambo la kuatua moyo hasa kwa wale wanaofiwa na wapenzi wao katika ajali.

Mojawapo ya kiini cha ajali barabarani kwetu ni barabara mbovu. Barabara zilizoharibika huchangia pakubwa katika kusababisha ajali. Mashimo yaliyojaa barabarani hufanya magari kuyumbayumba na kisha kupoteza mwelekeo. Mwishowe magari hugongana dafrau na hivyo kusababisha vifo vya watu wasiokuwa na hatia. Serikali yetu ina jukumu kubwa katika kukarabati barabara. Wawape kandarasi watu walio na ujuzi
katika ujenzi wa barabara.

Vilevile, magari yanayobeba abiria kupita kiasi husababisha ajali. Dereva na kondakta wake huwasomba abiria ukadhani ni mashehena ya mizigo. Lengo la haya yote ni ulafi wa pesa. Lawama hapa zinafaa kuelekezwa kwa madereva, makondakta na abiria. Ni sharti wenye magari wajali masilahi ya wasafiri, nao wasafiri ningewashauri kutoabiri magari yaliyojaa abiria.

Isitoshe, magari mabovu katika barabara zetu pia ni chanzo cha ajali. Si ajabu kuwaona madereva wakiyaendesha makatara barabarani. Magari hayo huharibikia mahali popote na wakati wowote. Waendeshaji hawa hujipa moyo na kujitetea kwa methali isemayo ukuukuu wa kamba si upya wa ukambaa. Hatua thabiti za kisheria zinafaa kuchukuliwa na serikali ili kuyaondoa magari ya aina hii. Tukumbuke kuwa kinga ni bora kuliko tiba. Aidha, tutahadhari kabla ya hatari.

Fauka ya hayo, madereva wasiohitimu huchangia katika kusababisha ajali. Wao huendesha magari bila kuhitimu. Labda waliwahonga wanaohusika na utoaji wa leseni. Hawajui ishara za barabarani. Kwa mfano, kivuko cha watoto na hata wanyama, barabara zenye matuta na pengine ishara ya kuonyesha kuruba. Wanaotoa leseni wanapaswa kuwajibika na kutoshiriki ufisadi.

Madereva waliotumia dawa za kulevya pia husababisha ajali. Uwezo wao wa kuona vyema huathirika kwa sababu ya vileo. Wao hawamakiniki wanapoendesha magari. Mihadarati pia huwafanya wengine kuendesha magari kwa kasi mithili ya duma. Wao husahau kuwa haraka haraka haina baraka.

Ni sharti sote tuungane mikono ili kukomesha ajali katika barabara zetu. Tukumbuke kuwa nia zikiwa moja, kilicho mbali huja. Sisi ndisi wenye nchi na kumaliza ajali kunatutegemea sisi.

  1. Katika aya ya kwanza, ni nani anastahili kulaumiwa kutokana na ajali?
    1. Madereva
    2. Abiria
    3. Hafahamiki
    4. Serikali
  2. Ni orodha ipi iliyo na vyombo vya habari pekee?
    1. Redio, televisheni, tishali. 
    2. Gazeti, redio, televisheni.
    3. Majarida, kiyoyozi, redio.
    4. Runinga, uyoka, magazeti.
  3. Barabara zilizoharibika husababishaje ajali?
    1. Magari huendeshwa kwa kasi na baadaye kuyumba.
    2. Magari huharibika, kuyumbayumba na kugongana.
    3. Magari hupoteza njia na kugongana. 
    4. Magari huyumbayumba na kuwagonga wapitanjia.
  4. Kwa nini madereva huwabeba abiria kupita kiasi?
    1. Mara nyingi wao huwa na haraka. 
    2. Abiria hupenda kubanana kama ndizi.
    3. Wao huwa na tamaa ya pesa.
    4. Viti huwa vichache mno magarini.
  5. Ni nini maana ya methali ukuukuu wa kamba si upya wa ukambaa?
    1. Tusidharau vitu vya zamani kwa kutamani vipya.
    2. Vitu vya zamani huwa tofauti na vipya.
    3. Tusividunishe vitu vipya kwani vina faida nyingi.
    4. Vitu vya zamani huwa si vizuri kama vipya.
  6. Madereva wasiohitimu huwezaje kupata leseni?
    1. Huzinunua kutoka madukani.
    2. Hupewa na maafisa wa trafiki barabarani.
    3. Hutoa hongo.
    4. Hupewa na serikali.
  7. Kulingana na ufahamu, mihadarati husababisha haya yote ila
    1. shida za kutazama barabarani.
    2. madereva kuugua magonjwa yatokanayo na dawa za kulevya.
    3. madereva kukosa uangalifu wanapoendesha magari.
    4. magari kuendeshwa kwa kasi.
  8. Unafikiri ni njia ipi mwafaka ya serikali kuhakikisha kuwa magari yameendeshwa kwa mwendo wa kadiri?
    1. Kuwa na maafisa wa trafiki katika kila mji nchini.
    2. Kuandaa semina kuwahamasisha abiria.
    3. Magari kutiwa vidhibitimwendo.
    4. Kutoa adhabu kali kwa abiria wanaoabiri magari yaliyojaa abiria.
  9. Ni ushauri upi uliotolewa kwa wale wote wasababishao ajali?
    1. Kuwafahamisha askari wa trafiki kasoro yoyote ya madereva.
    2. Kutowahonga wanaotoa leseni.
    3. Kutoabiri magari yaliyojaa wanaposafiri.
    4. Kuchukua tahadhari wanaposafiri.
  10. Kichwa kinachofaa zaidi ufahamu huu ni kipi?
    1. Athari za ajali barabarani.
    2. Chanzo cha ajali barabarani.
    3. Njia za kuzuia ajali barabarani.
    4. Ufisadi katika sekta ya uchukuzi.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41 hadi 50.   

Vumilia alikuwa mtoto wa kike. Alikuwa kifunguamimba katika familia ya mzee Juhudi. Baba wa Vumilia alikuwa maskini wa mali lakini tajiri wa moyo. Alifanya kazi za kijungujiko kuwakimu wanawe na mkewe ambaye walichukuana kama sahani na kawa. Wazee wa vumilia walikula yamini kufanya kila waliloweza ili kumrithisha mwana wao ufunguo wa maisha.

Vumilia alipohitimu darasa la nane, wazazi wake walichochea ari yake ya kufuzu maishani kwa kutumia mifano halisi ambayo Vumilia aliielewa. Wazee hao walimkumbusha binti yao kuwa bidii, utiifu, uvumilivu pamoja na heshima na uadilifu vilikuwa siri kubwa ya fanaka. Naam! Ilibainika kuwa samaki hukunjwa angali mbichi.

Binti wa watu alipopasuliwa mbarika, alikuwa kama mbwa aliyeonyeshwa ufuko, akakataa abadan katan kufa maji. Aliongeza bidii maradufu katika masomo yake na kuwa kama anayetegemea kisomo kuishi. Waliosema kuwa bidii hulipa hawakukosea. Mtihani ulipofanywa na matokeo kutolewa, Vumilia aliwaacha wengi vinywa wazi kwa kuwa alikuwa amewashinda watahiniwa wote nchini.

Halikuwa la mjadala tena. Anayechovya asali hachovyi mara moja. Vumilia hakulegeza kamba wala kuangalia nyuma. Makini yake yalikwama masomoni. Licha ya kuwa kijana, alikataa kuwa bendera ya kufuata upepo. Alimakinikia ndoto yake ya kuwa mhasibu ili kuwaauni wazee wake kama njia ya kushukuru kwa yote waliyoyatenda. Wafadhili wake waliridhishwa na hatua yao ya kumfadhili Vumilia tangu shule ya msingi hadi chuo kikuu.

Hewaa! Hayawi hayawi huwa. Tunapozungumza sasa, Vumilia ni mhasibu mkuu katika benki kuu ya Tulizeni. Amewajengea wazee wake kasri na kuhakikisha kuwa wanapata kila wanalohitaji. Daima huwasomesha wadogo wake na kuwahimiza kufanya bidii za duduvule wakifahamu mno kuwa jasho la leo ndilo faraja ya kesho.

  1. Ni kweli kusema kuwa katika familia ya mzee Juhudi
    1. Vumilia alikuwa mtoto wa pekee.
    2. Vumilia alikuwa yatima aliyefadhiliwa.
    3. kulikuwa na watoto kadhaa.
    4. Vumilia hakuwa na wanuna wowote.
  2. Kifunguamimba ni sawa na
    1. mwanambee.
    2. ndugu mdogo.
    3. mtoto wa pekee
    4. mtoto wa mwisho.
  3. Wazazi wa Vumilia waliichochea ari yake
    1. alipokuwa katika shule ya msingi.
    2. baada ya kumaliza masomo ya sekondari.
    3. alipokuwa katika chuo kikuu.
    4. alipomaliza masomo ya msingi.
  4. Ni sifa gani ambayo wazazi wa Vumilia hawakumfunza kama siri ya fanaka?
    1. Bidii.
    2. Utiifu.
    3. Ujanja.
    4. Uadilifu.
  5. Katika kidokezi samaki hukunjwa angali mbichi, anayelinganishwa na samaki hapa ni
    A. vumilia.
    B. wazazi.
    C. walimu.
    D. wanuna wa Vumilia.
  6. Kilichomwezesha Vumilia kupita vizuri katika mtihani wa darasa la nane ni
    1. utajiri wa wazazi wake. 
    2. hali ya umaskini wao.
    3. ushauri wa wazazi wake.
    4. mtihani kuwa rahisi.
  7. Vumilia alikuwa tofauti na vijana wenzake kwa kuwa
    1. hakushawishika kufuata mkondo mbovu.
    2. aliamua kuwa mhasibu.
    3. alisoma hadi chuo kikuu. 
    4. aliwafaa wazaziwe baadaye.
  8. Amewajengea wazee wake kasri ni 
    1. nahau.
    2. tanakali ya sauti.
    3. istiara.
    4. tashbihi.
  9. Wafadhili wa Vumilia
    1. walijutia uamuzi wao.
    2. walimwonea fahari Vumilia. 
    3. walimwonea wivu Vumilia.
    4. walisikitikia mafanikio ya Vumilia.
  10. Methali gani inayoweza kutumiwa kufupishia ujumbe wa ufahamu huu? 
    1. Heri nusu shari kuliko shari kamili.
    2. Mali bila daftari hupotea bila habari.
    3. Hasara humpata mwenye mabezo. 
    4. Mvumilivu hula mbivu.

MARKING SCHEME

  1. A
  2. C
  3. B
  4. D
  5. C
  6. D
  7. B
  8. A
  9. C
  10. B
  11. D
  12. A
  13. B
  14. C
  15. B
  16. C
  17. A
  18. B
  19. C
  20. D
  21. A
  22. C
  23. D
  24. B
  25. A
  26. C
  27. D
  28. B
  29. C
  30. B
  31. C
  32. B
  33. C
  34. C
  35. A
  36. C
  37. B
  38. C
  39. D
  40. B
  41. C
  42. A
  43. D
  44. C
  45. A
  46. C
  47. A
  48. C
  49. B
  50. D
Friday, 02 December 2022 07:56

Kiswahili Questions - KPSEA 2022 Exams

November 2022 - Muda Saa 1

MASWALI

Swali la 1 hadi la 5.
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali.

(Babu ameketi chini ya mti akisoma gazeti. Analiweka gazeti kando anapomwona Muli)
Muli: (akimsogelea Babu) Shikamoo Babu?
Babu: (kwa tabasamu) Marahaba mjukuu wangu! Habari za shule?
Muli: Njema babu! (kimya) Babu, nikwambie kitu?
Babu: Naam, niambie mjukuu wangu.
Muli: Wenzangu walinichagua kuwa kiranja wa darasa.
Babu: Hongera! Jambo zuri.
Muli: (akijikuna kichwa) Lakini Babu, sijui ninastahili kufanya nini ili niwe kiongozi bora.
Babu: Aha! Muli, sikiliza, ili kuwa kiongozi bora unastahili kuwa na maadili.
Muli: Ooh! Maadili...
Babu: Naam mjukuu wangu. Unaweza kuonyesha maadili kwa namna mbalimbali. Kwanza uwahudumie wenzako bila kuwabagua.
Muli: Kweli Babu, ninafikiria pia ninastahili kuwaonyesha upendo.
Babu: Ndiyo Muli. Unaweza kufanya hivyo kwa kuwajali na kuwasaidia wenzako.
Muli: Kweli Babu! Ninaona kwamba heshima, umoja na ushirikiano pia ni mambo muhimu.
Babu: Haswa! Heshima si utumwa. Je, unaweza kuonyesha heshima kwa njia gani?
Muli: (Kwa ujasiri) Kwa kuwaamkua wote na kusikiliza wanayoyasema.
Babu: Vyema! Unastahili pia kuwa mwaminifu. Tunaonyesha uaminifu kwa kusema ukweli na kufanya mambo inavyostahili.
Muli: Asante babu! Hakika umenifunza mengi.

  1. Muli alipoulizwa na babu kuhusu habari za shule, alimjibu
    1. Naam
    2. Njema
    3. Shikamoo
    4. Marahaba
  2. Maneno yafuatayo yametumiwa katika mazungumzo. Lipi halionyeshi adabu?
    1. Karibu
    2. Naam
    3. Asante
    4. Kweli
  3. Ni jibu lipi linaloonyesha maadili ambayo Babu alimfunza Muli?
    1. Kuhudumia, kuheshimu na kusikiliza. 
    2. Kuamkua, kusikiliza na kujali.
    3. Kujali, kusaidia na kuwa mwaminifu.
    4. Kuwa na heshima, kushirikiana na kusaidia.
  4. Unafikiri Muli atafanya nini baada ya kumuaga Babu?
    1. Atafurahia kuwa kiongozi shuleni.
    2. Atazingatia mawaidha ya babu.
    3. Atawaeleza wenzake kuhusu alivyokutana na babu.
    4. Atawapongeza wenzake kwa kumchagua kuwa kiranja
  5. Neno maadili limetumika katika mazungumzo maana yake ni
    1. Mienendo mizuri inayofaa kuzingatiwa na mtu.
    2. Maonyo ambayo hutolewa mtu anapokosea. 
    3. Matendo ambayo mtu huwafanyia wenzake.
    4. Mitindo mipya inayofuatwa na mtu.

Swali la 6 hadi la 9
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Sungura alirauka kabla ya jua kuchomoza. Alianza safari ya kwenda kumtembelea shangazi yake. Njiani alipanda milima na kuvuka mabonde. Jua lilipochomoza, aligundua kuwa alikuwa ametembea sana ila hakuwa amefika kwa shangazi yake. Alikuwa anaelekea kusini badala ya kaskazini. Kumbe alikuwa amepotea njia! "Nitafanya nini? Nimepotea njia," Sungura alijisemea kwa sauti.
"Nitakusaidia," alisema Kobe aliyekuwa kichakani, hapo karibu.
"Asante sana Kobe. Sikuwa nimekuona. Tafadhali nisaidie." Sungura alimwomba Kobe.
"Unakwenda upande gani?" Kobe alimuuliza Sungura.
"Naelekea kaskazini, anakoishi shangazi yangu," Sungura alimjibu Kobe.
"Jua huchomoza upande wa Mashariki wa dira kila asubuhi. Ukitaka kwenda Kaskazini, simama kisha unyooshe mikono yako juu. Mkono wa kulia uuelekeze kunakotoka jua. Huko ndiko Mashariki. Nao mkono wa kushoto uuelekeze upande huo mwingine. Huko ndiko Magharibi," Kobe alimweleza Sungura huku akimwonyesha kwa vitendo.
"Kwa hivyo uso wangu utakuwa unaangalia Kaskazini huku mgongo wangu ukiwa upande wa Kusini" Sungura alisema kwa furaha.
"Wewe ni mwanafunzi mzuri. Unaelewa haraka. Umelenga ndipo," Kobe alimwambia Sungura kwa bashasha.
"Undugu ni kufaana. Asante sana Kobe,"
Sungura aligeuka akarudi hadi kwake ili kuanza safari upya.

  1. Nyumbani kwa Shangazi kulikuwa upande gani kutoka kwa Sungura?
    1. Mashariki
    2. Magharibi
    3. Kaskazini
    4. Kusini
  2. Kwa nini Sungura aliamka mapema? Ili
    1. apande milima na kuvuka mabonde. 
    2. aone jua likichomoza.
    3. akutane na Kobe njiani.
    4. aende kumtembelea Shangazi.
  3. Kobe anawajali wengine. Chagua jibu lin- aloonyesha sifa hii ya Kobe.
    1. Alimwelekeza Sungura alikokuwa akienda. 
    2. Anamsikiliza Sungura akizungumza.
    3. Alikubali zawadi alizopewa na Shangazi.
    4. Alifikiria Sungura alikuwa mwanafunzi mwerevu.
  4. Chagua jibu lenye neno ambalo Shangazi angetumia kumwita Sungura.
    1. Binamu
    2. Mpwa
    3. Ndugu
    4. Ami

Swali la 10 hadi la 12
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Shule ya msingi ya Faulu huwa na siku tatu za michezo katika kila juma. Wanafunzi wa Gredi ya Sita wamegawanywa katika vikundi vinne kama ifuatavyo: Simba Kifaru Chui Ndovu
Kila kikundi hushiriki katika michezo tofauti kila juma. Tazama jedwali la juma hili kisha ujibu maswali.

VIKUNDI  JUMATATU   JUMATANO  IJUMAA 
 Simba  Kandanda   Netiboli  Riadha
 Kifaru  Riadha  Uogeleaji  Kandanda
 Chui  Netiboli  Riadha  Uogeleaji
 Ndovu  Uogeleaji  Kandanda  Netiboli
  1. Ni kikundi kipi hakikushiriki kandanda?
    1. Simba
    2. Chui
    3. Kifaru
    4. Ndovu
  2. Ni kikundi kipi hakikushiriki uogeleaji? 
    1. Ndovu
    2. Kifaru
    3. Chui
    4. Simba
  3. Ni kikundi kipi hakikushiriki riadha?
    1. Simba
    2. Chui
    3. Ndovu
    4. Kifaru

Swali la 13 hadi la 15
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali
Je, unajua kupika ugali? Kupika ugali ni rahisi. Kwanza, unahitaji unga wa mahindi, maji, sufuria, mwiko na jiko la kupikia lenye moto. Anza kwa kupima kiasi cha maji unayohitaji na kuyatia kwenye sufuria safi. Ibandike sufuria hiyo kwenye jiko. Funika sufuria ili uyapatie maji muda yachemke. Chukua unga kisha uutie kidogo kidogo ndani ya maji yanayochemka, huku ukikoroga kwa mwiko. Ongeza unga kulingana na unavyotaka ugali wako uwe. Kama unataka ugali mgumu, basi endelea kuongeza unga. Funika ugali wako, kisha upunguze moto jikoni ili ugali uive polepole.
Unaweza kuandaa ugali kwa vitoweo vya aina mbalimbali. Kuna wale wanaopenda kula ugali kwa maziwa yaliyoganda na mboga za kienyeji kama vile mchicha. Wengine hula ugali kwa samaki au nyama. Mimi napenda kula ugali kwa dagaa na kachumbari. Je, wewe unapenda kula ugali kwa kitoweo gani?

  1. Wewe unajiandaa kupika ugali.
    Chagua jibu linaloonyesha hatua ya kwanza utakayozingatia
    1. Kuwa na vitu utakavyohitaji kupika ugali.
    2. Kuinjika sufuria yenye maji jikoni. 
    3. Kuchukua mwiko na kuanza kukoroga.
    4. Kuwa na kitoweo ambacho unahitaji.
  2. Unampikia nyanya kitoweo cha kuliwa kwa ugali.
    Chagua jibu linaloonyesha kitoweo chenye lishe bora.
    1. Nyama na dagaa.
    2. Kabeji na sukumawiki.
    3. Samaki na mboga ya mchicha.
    4. Maziwa na maharagwe.
  3. Chagua jibu sahihi.
    Mchicha huupatia mwili vitamini, ugali huupatia mwili ..............................
    1. protini.
    2. madini.
    3. kinga.
    4. wanga.

Soma kifungu kifuatacho. Kina nafasi 16 hadi 20. Umepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.
Kanini 16                         katika michezo mbalimbali tukiwa shuleni. Mchezo 17                    alipenda zaidi ni netiboli. 18                    na timu ya mchezo wa netiboli 19                   alipoingia darasa la tano. Kanini alitia bidii kwenye mchezo huu na kuiletea timu yake ushindi. Alifahamu kuwa 20                     .

  1.                              
    1. alishirikia
    2. alishiriki
    3. alishirikisha
    4. alishirikiwa
  2.                
    1. ambao
    2. ambayo
    3. ambako
    4. ambamo
  3.                        
    1. Alikuunga 
    2. Aliwauunga
    3. Alijiunga
    4. Alituunga
  4.                      
    1. huku
    2. kama
    3. tena
    4. mara
  5.                  
    1. kila mwamba ngoma ngozi huivuta kwake
    2. mtaka cha mvunguni sharti ainame
    3. udongo upatilize uli maji
    4. jifya moja haliinyiki chungu

Kutoka swali la 21 hadi la 30, chagua jibu sahihi.

  1. Wanafunzi wana nidhamu, .............................. huheshimu walimu.
    1. wao
    2. wewe
    3. yeye
    4. nyinyi
  2. Tunasema, wingu ni kwa nzige. Tutasema, ......................................ni kwa matunda.
    1. kitia
    2. pakacha
    3. bunda
    4. robota
  3. Chagua wingi wa:
    Fundi yule hodari amejenga ukuta mrefu.
    1. Mafundi wale hodari wamejenga kuta ndefu.
    2. Fundi wale hodari wamejenga ukuta mrefu.
    3. Mafundi wale hodari wamejenga ukuta mrefu.
    4. Fundi wale hodari wamejenga ukuta mrefu.
  4. Kimeto alimsaidia Kamaa kuchora picha.
    Kamaa alikuwa ameumia mkono. Kwa hivyo, Kimeto
    1. alimchoresha Kamaa picha.
    2. alimchorea Kamaa picha.
    3. alichoreshwa picha na Kamaa..
    4. alichoreshea Kamaa picha.
  5. Ni sentensi ipi sahihi?
    1. Palipo na rutuba panafaa kwa kilimo.
    2. Palipo na rutuba kunafaa kwa kilimo.
    3. Mlimo na rutuba panafaa kwa kilimo.
    4. Mlimo na rutuba kunafaa kwa kilimo..
  6. Ni sentensi ipi iliyoafikishwa vyema?
    1. Neema amefika: kwetu leo asubuhi..
    2. Mwachia amenunua machungwa, maembe na papai.
    3. Je, umeandika barua ya kuomba msamaha.
    4. Salaale Kalama amefunga bao lingine.
  7. Chagua ukubwa wa sentensi ifuatayo: Mlango wa nyumba yake unapendeza.
    1. Lango la jumba lake linapendeza.
    2. Mlango wa jumba lake linapendeza.
    3. Lango la nyumba yake linapendeza.
    4. Mlango wa nyumba yake linapendeza.
  8. Chagua jibu lisilo sahihi.
    1. Tita la kuni.
    2. Thureya ya nyota.
    3. Kicha cha funguo.
    4. Kilinge cha wanariadha.
  9. Tunastahili kupiga chafya kwenye kiwiko cha mkono. Kupiga chafya ni
    1. kuchemua.
    2. kukohoa.
    3. kutema.
    4. kupenga.
  10. Simon ni wembe masomoni. Kauli hii ina maana kuwa Simon ni:
    1. mwenye subira.
    2. jasiri.
    3. mwenye bidii.
    4. mwerevu.

MASWALI

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1-5.
(Ni wakati wa mapumziko mafupi. Koi na Rao wameketi chini ya mti wakiwatazama wenzao wakicheza uwanjani.)

Koi: Sijui ni kwa nini siku hizi maradhi yanayohusiana na vyakula vichafu yamekuwa mengi hivi. Licha ya Roda, hata Hamisi anaendesha. (Akirusha jiwe dogo mbali kidogo)

Rao: (Akionyesha uso wa mshangao.) Ala! Hata Hamisi anaugua? Ndiyo maana hawakuja shuleni leo.(Muda unapita)Lakini kuna njia kadhaa za kupambana na magonjwa ya tumbo.

Koi: Ni kweli Rao. Kabla ya kula, ni sharti tuinawe mikono ili kuondoa uchafu. Mikono aidha hustahili kusafishwa kila baada ya kutoka msalani kujisaidia.

Rao: Naam, vyakula viliwavyo bila kupikwa kama vile matunda hustahili kuoshwa vizuri kabla ya kula. (Wamezama katika mawazo)

Koi: Nakumbuka pia mwalimu Kazamoyo akitushauri kupika vyakula kama vile nyama hadi viive vizuri.

Rao: Kwa nini Koi? (Akimsogelea)

Koi: Nyama ambayo haijapikwa ikapikika huweza kuwa na viini hatari vinavyoweza kusababisha maradhi mabaya ya tumbo.

Rao: Lo! Nitazingatia haya yote ili niwe salama. Sitaki kukaa nyumbani kwa ajili ya ugonjwa ilhali mtihani unakaribia. (Kengele inakirizwa. Wanaamka kuelekea
darasani mwao)

Koi: Leo jioni baada ya masomo, tupitie kwa kina Roda na Hamisi ili kuwajulia hali, sawa? (Rao anakubali kwa ishara ya kichwa)

  1. Moja kati ya magonjwa yanayozungumziwa hapa ni
    1. malaria. 
    2. UKIMWI. 
    3. kuendesha. 
    4. kifafa.
  2. Wanafunzi wanaougua ni 
    1. Koi na Hamisi.
    2. Rao na Koi. 
    3. Roda na Rao. 
    4. Hamisi na Roda.
  3. Inawezekana kuwa msalani ni 
    1. chooni. 
    2. shuleni. 
    3. darasani. 
    4. uwanjani.
  4. Kulingana na mazungumzo haya, nyama ambayo haijapikwa vizuri huweza kuwa na ยท 
    1. ladha ya kuvutia.
    2. viini hatari. 
    3. rangi ya kuvutia. 
    4. harufu nzuri mno.
  5. Baada ya kengele kukirizwa, Rao na Koi 
    1. waliwatembelea Roda na Hamisi. 
    2. walielekea uwanjani. 
    3. walikaa chini ya mti. 
    4. walielekea darasani. 

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 6 hadi 8.
Mimi na familia yangu tunaishi katika nyumba kubwa sana. Mimi ndimi mtoto wa pekee katika familia yangu, yaani, sina dada wala kaka. Baba yangu ni mwalimu katika shule ya msingi ya Nyotanjema naye mama yangu ni mwuguzi katika hospitali ya Ponaupesi. Baba yangu anayo magari mawili, moja jekundu na jingine jeusi. Hata hivyo, mara nyingi yeye hulitumia lile jeusi. Yeye hunipeleka shuleni kila asubuhi.
Ninaye mbwa nimpendaye. Mbwa huyo anaitwa Papi. Kila Jumamosi, mimi humwosha na kuyachana manyoya yake. Ingawa mimi ndimi mtoto wa pekee, sijihisi mpweke. Ninao wazazi na mbwa ambao huwa nami ninapowahitaji.

  1. Kulingana na taarifa, si kweli kusema kuwa 
    1. mwandishi hana dada. 
    2. katika nyumba hiyo, kunao watu watatu tu.
    3. mwandishi humsafisha mbwa wake kila siku. 
    4. mwandishi hajihisi mpweke.
  2. Baba wa mwandishi ana
    1. magari mawili na nyumba kubwa. 
    2. gari moja jeusi na mbwa mmoja.
    3. mbwa na gari jekundu. 
    4. nyumba kubwa na mbwa.
  3. Papi ni
    1. paka wa mwandishi. 
    2. mbwa. 
    3. rafiki wa mwandishi. 
    4. mama wa mwandishi.
  4. Ni nani huwa na mwandishi anapokuwa mpweke? 
    1. Marafiki zake. 
    2. Watu wa ukoo wake. 
    3. Mbwa wake na wazazi wake. 
    4. Mbwa wake.

Soma kifungu kafuatacho kisha ujibu maswali 10 hadi 12.
Jumamosi hiyo ni moja kati ya zile ambazo siwezi kuzisahau. Ilikuwa asubuhi angavu. ve joto kiasi na upepo uliovuma kwa maringo ya tausi jike. Huko juu, ndege waliimba na kuruka ovyo kutoka tawi hadi tawi. Hakika, ilikuwa ni siku ambayo wenyeji wa Kokotoa walikuwa wameisubiri kwa hamu.
Chaurembo na Ramadhani wangefunga ndoa. Harusi yenyewe ilikuwa katika kanisa la Hosana. Maarusi walipofika, watu walikusanyika wakiimba na kucheza kwa furaha. Baada ya harusi, wageni walikula na kunywa kwa furaha. Baadaye, kila mmoja alijiendea zake akiwa na furaha tele.

  1. Kulingana na kifungu, harusi hii ilikuwa lini? 
    1. Jumapili. 
    2. Jumamosi. 
    3. Jumatatu. 
    4. Ijumaa.
  2. Mwandishi wa taarifa hii ana maana gani anaposema huko juu
    1. Mtini. 
    2. Majini.
    3. Kanisani. 
    4. Nyumbani.
  3. Watu walikusanyika, kuimba na kucheza 
    1. baada ya kula na kunywa. 
    2. wakienda nyumbani. 
    3. maarusi walipoingia.
    4. nyumbani kwao. 

Soma kifungu kafuatacho kisha ujibu maswali 13 hadi 15.
Dukakuu la Tulizo liko katika kaunti ya Konambaya. Ingawa kunayo madukakuu mengine, Tulizo ndilo kubwa zaidi. Limejengwa kando ya barabara kuu ya Jogoo katikati ya kituo cha polisi cha Pingu na soko la Malimali. Mwenye duka hilo anaitwa bwana Sahara. Bwana Sahara amewaajiri wafanyakazi sita. Wengi wao ni wanaume. Hata hivyo, wanawake wachache waliomo hufanya kazi nyepesi nyepesi tu.
Bwana Sahara huhakikisha kuwa wateja wote wamehudumiwa vyema. Huwataka waende wakiwa wameridhika, Wakazi wengi hulipenda duka hili la bwana Sahara kwa sababu humo, wao hupata kila wanachohitaji kutoka unga hadi matunda

  1. Kulingana na habari, ni kweli kusema kuwa
    1. kunayo maduka mengine makubwa Konambaya. 
    2. barabara ya Jogoo iko kati ya soko na kituo cha polisi. 
    3. bwana Sahara hawezi kufanya kazi peke yake dukani mle. 
    4. kuna bidhaa chache dukani Tulizo.
  2. Dukakuu la Tulizo limejengwa 
    1. kando ya barabara kuu ya Jogoo. 
    2. nyuma ya soko la Malimali. 
    3. mbele ya kituo cha poliso cha Pingu. 
    4. juu ya kaunti ya Konambaya.
  3. Wakazi wanalipenda duka hili kwa kuwa 
    1. bidhaa huuzwa kwa bei rahisi. 
    2. wanunuzi hupata bidhaa wanazohitaji.
    3. bwana Sahara hupenda wateja wake wakifurahi. 
    4. kuna unga na matunda kwa wingi. 

Soma kifungu kifuatacho. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa tamu ilinukia.

Fisi _____16_____ na njaa, aliamua kuelekea sehemu ambayo harufu ya _____17_____ yake, Alipofika katika njiapanda, hakujua aelekee kushoto au_____18_____ .Kwa ajili ya _____19_____ aliamua kuzifuata njia zote mbili. Hapo ndipo alipasuka na_____20_____ papo hapo.

  1.                  
    1. alipozidi
    2. alizidisha
    3. alipozidishwa
    4. alipozidiwa
  2.            
    1. chakula
    2. mate
    3. nyama
    4. viazi
  3.                 
    1.  kulia
    2. kucheka
    3. katikati
    4. nyuma
  4.                  
    1. bidii 
    2. tamaa
    3. utamu
    4. kutamani
  5.            
    1. kula
    2. kushiba
    3. kufufuka
    4. kufa

Katika suala 21-30. jibu swali kulingana na maagizo uliyopewa.

  1. Kitenzi shinda katika kauli ya kutendwa huwa 
    1. shindana.
    2. shindwa.
    3. shindika.
    4. shindiwa.
  2. Chagua orodha ya wanyama wa porini pekee. 
    1. Ngiri, kifaru, twiga.
    2. Punda, ngiri, mbogo. 
    3. Paa, ndovu, ngamia.
    4. Nguruwe, paka, mbwa.
  3. Shida ni kwa tatizo kama vile televisheni ni kwa
    1. redio.
    2. rununu.
    3. runinga.
    4. barua
  4. Ni upi wingi wa: Kiazi kilipikwa kikaiva? 
    1. Viazi zilipikwa zikaiva. 
    2. Viazi vilipikwa vikaiva. 
    3. Kiazi zilipikwa zikaiva. 
    4. Viazi ilipikwa ikaiva.
  5. Chagua neno ambalo halipo katika ngeli ya LI-LI. 
    1. Jani.
    2. Joto!
    3. Jua
    4. Jasho.
  6. Mchungwa huzaa machungwa. Mnazi huzaa
    1. nanasi.
    2. minazi
    3. mnanasi.
    4. nazi
  7. Kamilisha methali ifuatayo: Mtoto umleavyo ndivyo
    1. akuavyo. 
    2. akuwapo
    3. achezavyo.
    4. aliavyo
  8. Bendera ya taifa letu inazo rangi ngapi? 
    1. Tano.
    2. Nne
    3. Tatu.
    4. Mbili
  9. Mstari mmoja katika ubeti wa shairi huitwa
    1. mshororo
    2. sentensi
    3. mizani
    4. kibwagizo
  10. Wazazi wachache tu ndio waliofika mkutanoni. Neno lililopigiwa mstari ni
    1. kielezi.
    2. kiunganishi.
    3. kiwakilishi
    4. kivumishi.

MARKING SCHEME

swa ms timer

Page 8 of 14