Displaying items by tag: kiswahili

SEHEMU YA KWANZA: KUSILIKIZA NA KUZUNGUMZA (Alama 10)

Mwalimu asome kifungu kifuatacho kisha amwulize mwanafunzi maswali kwa sauti.

Kandanda hupendwa na huchezwa kote duniani. Ni mchezo unaoleta watu pamoja kwa amani na furaha. Zamani mchezo huu ulichezwa na wanaume pekee. Siki hizi, wanawake pia hucheza. Mchezo wa kandanada pia huitwa soka, ngozi ama kabumbu. Huchezwa na watu kumi na mmoja kila upande.

Maswali

  1. Kandanda hupendwa na kuchezwa wapi? _____________________________
  2. Zamani mchezo huu ulichezwa na nani? __________________________
  3. Majina mengine yenye maana sawa na kandanda in ______________________
  4. Mchezo wa soka huchezwa na watu wangapi kila upande? ______________________________

SEHEMU YA PILI: KUSOMA KWA SAUTI (Alama 20)

Soma kifungu kifuatacho kwa sauti

Wanyama wanaofugwa huitwa mifugo. Wanyama hawa ni kama mbuzi, kondoo, ng'ombe, ngamia na punda. Wanyama hawa wana faida nyingi sana. Mfugaji huwakamua ng'ombe ambao humpa maziwa ambayo humpa pesa nyingi akiyauza.

Maziwa pia hutumiwa kutengeneza siagi. Jbini hizi ni tamu sana. Kondoo hutupa sufi ambazo hutumiwa kutengeneza fulana. Maziwa ya mbuzi ni mazuri sana. Ngamia hutumiwa kubebea mizigo.

Maziwa yake pia hunywewa na watu wengine huamini kuwa ni dawa. Wanyama wote wanahitaji kutunzwa. Sharti waishi mahali safi na wapewe chakula cha kutosha ili wawe na afya nzuri. 

SEHEMU YA TATU: UFAHAMU (ALAMA 5)

Soma kufungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

Hodari alikuwa kifunguamimba wa Bwana na Bi Omar. Kwa jumla walikuwa watoto wanne; wasichana wawili na wavulana wawili. Familia hii ilikuwa na maisha mazuri siku zote. Watoto hawa walilelewa na kusomeshwa vizuri.

Kwa bahati mbaya, baba yao alifutwa kazi kule alikoajiriwa. Alifutwa kwa sababu wenzake walimfitini. Hapo ndipo maisha yalipobadilika katika familia hii.

Maisha yakawa magumu. Ilibidi Hodari ambaye ni kifunguamimba kutafuta kibarua ili aweze kuwasaidia wazazi wake na wadogo wake. Kazi hizi za vibarua alikuwa anazifanya baada ya kutoka shuleni. Wakati mwingine chakula na mahitaji mengine yakakosekana. Ilibidi Hodari aache shule na kuamua kutafuta kazi ya uyaya. Kazi hizi zilikuwa nyingi kijijini.

Tajiri mmoja alimpa kazi ya nyumbani. Kazi ilikuwa ngumu sana kwa mtoto wa shule kama vile Hodari. Aliteseka sana kwa kukosa nafasi ya kucheza na watoto wenzake. Mizigo mizito aliyobebeshwa ilimwacha akiwa mchovu kwelikweli.

Kwa bahati nzuri msamaria mwema mmoja alimwonea huruma na kuamua kumsaidia. Pamoja na mambo aliyosaidiwa nayo ni ajira kwa wazazi wake.

Maswali

  1. Kisa hiki kinahusu mtoto aitwaye ___________________________
  2. Ni nani alifutwa kazi? ______________________________
  3. Ni vibaya kumnyima mtoto haki ya ________________________________
  4. Hapo mwanzoni maisha ya Hodari na wadogo wake yalikuwa  ___________________________
  5. Taja kazi moja aliyofanyishwa Hodari _______________________

SEHEMU YA NNE: SARUFI (ALAMA 25)

Kanusha sentensi hizi.

  1. Wewe unapenda chakula kitamu. 
    _______________________________________
  2. Alisoma hadithi.
    _______________________________________
  3. Yeye ataegesha gari karibu na soko.
    ________________________________________

Jibu kwa usahihi kwa kuchangua majibu kutoka kwa mabano.

Baada ya siku____4____ (mingi, nyingi) kuku alianza ___5___ (kutaga, kutoa) mayai. Alifurahi sana.

Alitaka mayai ____6____ (hiyo, hayo) yote yatoe vifaranga. Jioni ____27____ (monja, moja), aliporudi kibandani alianza kuatamia mayai ____8____ (zake, yake).

Ambatanisha nomino hizi ili kuunda nomino ambata

               A                           B

  1. Mwana                 hazina
  2. Askari                   sesere 
  3. Mweka                  kanzu
  4. Tegua kitendawili kifuatacho: Achora lakini hana kalamu _________________________ 
  5. Kisawe cha barabara ni ______________________
  6. Taja viungo viwili vya upishi.
    1. _______________________________
    2. _______________________________
  7. Tunga sentensi ukitumia nomino hizi.
    1. Upishi _________________________________
    2. Picha  _________________________________
  8. Jibu maagano haya. "Alamsiki" _____________________________________
  9.  
    Grade 5 End Term 2 Set 2 SWA Q17
    Kifaa hii hutumika _____________________________________
  10. Kikundi cha matunda huitwa__________________ (pakacha, mtumba, numbi)
  11.  
    Grade 5 End Term 2 Set 2 SWA Q19
    Kifaa hiki huitwa __________________________.
    Andika sentensi zifuatao kwa wingi.
  12. Ndoo hii imejaa maji ________________________________ 
  13. Ukuta huu umebomoka ____________________________________
  14. Sentensi moja katika ushairi huitwa________________________________
  15.  
    Grade 5 End Term 2 Set 2 swa Q23
    Hii ni namba gani? _____________________________________________

SEHEMU YA TANO: KUANDIKA (Alama 20)

Andika insha ya kusisimua ukizingatia maagizo uliyopewa

Andika insha ya kusisimua kuhusu: 

CHAKULA UKIPENDACHO

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

MARKING SCHEME

Sehemu ya kwanza

  1. Kote
  2. Na wanaume
  3. Kambumbu, soka
  4. Kumi na mmoja

Sehemu ya tatu

  1. Hodari
  2. Bwana Omar
  3. Kucheza/kula/kuomba
  4. Mazuri
  5. Kubeba mizigo mizito

Sehemu ya nne

  1. Wewe hupendi chakula kitamu
  2. Hakusoma hadithi
  3. Yeye hataegesha gari karibu na soko
  4. Nyingi
  5. Kutaga
  6. Haya
  7. Moja
  8. Yake
  9. Sesere
  10. Kanzu
  11. Hazina
  12. Konokono
  13. Njia/baraste
  14.  
    1. Pilipili
    2. Masala
  15.  
    1. Hakiki kwa usahihi
    2. hakiki kwa usahihi
  16. Binuru
  17. Kuonyesha saa
  18. Pakacha
  19. Kiwambo
  20. Ndoo hizi zimejaa maji
  21. Kuta hizi zimebomoka
  22. Mshororo
  23. Thelathini

KUSIKILIZA NA KUONGEA, KUSOMA KWA SAUTI

Sehemu ya A: Kusikiliza na kuongea

Ningependa tuzungumze kuhusu heshima na adabu. Wewe ni kiranja wa darasa lako una mazungumzo na mwalimu wako wa darasa.

  1. Anza mazungumzo kwa maamkizi yafuatayo.
    (Mwanafunzi ajibu)
  2. Taja maneno ya adabu ambayo kama kiranja unawasisitizia wanafunzi kuyatumia darasani.
    (Mwanafunzi ajibu)
  3. Eleza mwalimu umuhimu wa kuwa mwanafunzi mwenye heshima na adabu.
    (Mwanafunzi ajibu)
  4. Toa maelezo mafupi vile utakavyoonyesha heshima na adabu kwa mgeni aliyealikwa nyumbani kwenu.
    (Mwanafunzi ajibu)
  5. Taja maneno ya heshima na adabu badala ya maneno uliyopewa
    1. Mtoto anahara _________________________
    2. Fatuma ana mimba ___________________________
    3. Halima amezaa ________________________

Sehemu ya B: Kusoma Kwa Sauti

Mama alikumbuka kuwa baba alisahau kumeza dawa. Aliingia chumbani na kutoka na vidonge viwili vya dawa akampa baba aweze kumeza kwa maji. Baba alikuwa na ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu.

Alikuwa anatueleza kuwa ugonjwa wake ulitokana na hali ya maisha katika harakati zake za biashara ambayo ilikuwa mara inapanda mara inashuka. Alikuwa akizinunua bidhaa kutoka Uchina na kuziuza humu nchini. Ingawa aliipenda biashara hiyo, aliichukia hali ile ya ugonjwa na hivyo akaamua kupunguza shughuli zake na kuongeza muda wa kupumzika nasi nyumbani.

Baba alipokata kauli kupunguza shughuli aliendelea kuwa na afya nzuri. Tuliendelea kuzungumza naye mambo aliyofurahia kusikiliza kama vile umilisi tuliokuwa tumepata shuleni. Hasa, alifurahi tulipomwambia tulijifunza kuhusu jinsi ya kuzuia magonjwa. Tulimweleza pia kuhusu magonjwa yanayotokana na hali za maisha kama vile kisukari na shinikizo la damu.

SEHEMU YA A: Ufahamu

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata (alama 5)

Unapotembea mjini, chukua tahadhari kubwa sana. Kuna matapeli wanaohadaa watu mjini. Vile vile matapeli hao hujiweka katika makundi ili kungojea watembezi wanaoonekana wageni. Mara wanapowagundua, wao hunasa pesa, simu na vitu vingine na kukimbia navyo. Pia kuna wale hutumia maneno matamu. Wao hukuandama na ukifika kichorochoroni watakupora na kukimbia. Wengine watakupiga na kukuacha umeumia. Iwapo unataka msaada wowote, basi mtafute bawabu au askari akusaidie. Usijiingize kwenye shida tupu bure.

Maswali

  1. Kulingana na habari ni watu gani wanaoiba pesa? ___________________________
  2. Mwandishi anatushauri tufanye nini tunapotembea mjini? ____________________________
  3. Kamilisha: Maneno matamu humtoa __________________ pangoni.
    1. simba
    2. nyoka
    3. sungura
    4. mdudu
  4. Eleza maana ya neno wanaohadaa. _______________________
  5. Andika maana ya neno 'matapeli ________________________
  6. Unapofika vichochoroni huwa unafanyiwa nini? ________________________

SEHEMU YA B; SARUFI

  1. Chagua maneno yaliyopo kwenye mabano kujaza mapengo
    ____1____.anapenda sana kuogelea majini. Yeye hutaga mayai makubwa makubwa. ____2____ yake ni tamu sana. Kuku pia hutaga _____3_____ japo madogo kushinda va bata. Nyama va kuku pia ni _____4_____ Kuna kuku wa kienveji na kuku wa ______5_______ . Kuku wa gredi huwa na mapato ya juu zaidi. Wao hukua kwa haraka na kutaga mayai ______6______.
    ( mayai, tamu, nyama, bata, gredi, hukiwa, mengi)
  2. Jaza pengo kwa kutumia viunganishi vifaavyo.
    1. Juma alikula ______________________ hakushiba. (kwa sababu, lakini, pia)
    2. Tulipita mtihani _____________ tulifanya bidii. (lakini, na, kwa sababu)
    3. Halima ________________ Fatuma wanaosha vyombo. (na, lakini, kwa sababu)
    4. Waliadhibiwa ______________________ walivunja sheria za shule. (pia, kwa sababu, na) (5
  3.  Andika sentensi zifuatazo kwa umoja.
    1. Miti ya mapera imekatwa.
      _________________________________________________
    2. Nguo zao ni chafu sana.
      _________________________________________________
    3. Viti vizuri vitauzwa.
      _________________________________________________
    4. Wakulima wanalima kwa bidii.
      _________________________________________________
    5. Maembe hayo ni matamu.
      _________________________________________________
  4. Andika kinyume cha nomino hizi
    1. Mzee ____________________________________
    2. Mchana __________________________________
    3. Maskini __________________________________
    4. Rafiki ____________________________________
    5. Mfalme ___________________________________
  5. Pigia mstari nomino za makundi katika sentensi zifuatazo
    1. Barabarani kulikuwa na mlolongo wa magari.
    2. Safu ya milima hupendeza.
    3. kikosi cha askari kilikuwa kimesimama barabarani.
    4. Fatuma alinunuliwa jozi ya viatu.
    5. Mama alinunua pakacha la matunda kutoka sokoni.
  6. Kamilisha methali hizi
    1. Mgagaa na Upwa. ___________________________
    2. Achanikaye kwenye mpini ____________________________
    3. Mtumai cha nduguye ___________________________
  7. Tunga sentensi ukitumia maneno yafuatayo.
    1. Mlindalango
    2. Vinasasauti

INSHA

Andika insha kuhusu;

 JIRANI YANGU

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________________________________

MARKING SCHEME

KUSIKILIZA NA KUONGEA

  1. Anaendesha
  2. Ni mjamzito
  3. Anejufungua

LUGHA

Sehemu ya A 

  1. Matapeli
  2. Mtafute bawabu na askari
  3. Nyoka
  4. Wanaodanganya
  5. Wezi
  6. Kukupora

Sehemu ya B

  1.  
    1.  Bata
    2. Nyama
    3. Mayai
    4. Tamu
    5. Gredi
    6. Mengi
  2.  
    1. Lakini
    2. Kwa sababu
    3. Na
    4. Kwa sababu
  3.  
    1. Mti wa mapera umekatwa
    2. Nguo yake ni chafu sana
    3. Kiti kizuri kitauzwa
    4. Mkulima analima kwa bidii
    5. Embe hilo ni tamu.
  4.  
    1. Kijana
    2. Usiku
    3. Tajiri
    4. Adui
    5. Malkia
  5.  
    1. Mlolongo wa magari
    2. Safu ya milima
    3. Kikosi cha askari
    4. jozi la viatu.
    5. pakacha la matunda
  6.  
    1. Hali wali mkavu
    2. Halali njaa
    3. hafi maskini

INSHA

Andika Insha ya kusisimua itakayoanzia hivi

Asubuhi moja nilipokuwa nikielekea shuleni, nilimsikia mtoto akilia katika vichaka vilivyokuwa kando ya barabara ......................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................

LUGHA

Chagua jibu mwafaka kwa yale uliyopewa ujaze nafasi zilioachwa

Ni jambo la ____1____ kuona kuwa waja wengi____2____ usafi wa mazingira, Utembeapo kila mahali 3 mijini____4____ utaona watu wakiangushaangusha takataka bila___5___zozote zile. Mate na vikohozi ___6___ovyoovyo nusura wawachafue wenzao.____7____kuona wengine hata___8___kando ya barabara zetu.

Ajabu ni kuwa, watu____9____ watasikika wakilaumu___10___ ya jiji eti kwa kushindwa___11___ usafi. Ni kweli kuwa wanaohusika katika usafi wameshindwa kwa njia moja au nyingine. Lakini, mbona tuwaongezee mzigo? Kumbukeni ni sisi tutakaoteseka ___12____ni____13____ wa maradhi. Tutamlaumu___14___? Ikumbukwe ____15____.

  1.  
    1. kusikitisha
    2. kutatizika
    3. kuchosha
    4. kuumiza
  2.  
    1. hawajali
    2. hawaijali
    3. hawazijali
    4. hawakujali
  3.  
    1. katika
    2. kwa
    3. mnamo
    4. hususan
  4.  
    1. yetu
    2. mwetu
    3. zetu
    4. yote
  5.  
    1. hisia
    2. haraka
    3. nia
    4. ujasiri
  6.  
    1. vinatowa
    2. yanatemwa
    3. wanatemwa
    4. zinatemwa
  7.  
    1. Ni ajabu
    2. Si ajabu
    3. Si kawaida
    4. Ni nadra
  8.  
    1. wakitabawahi
    2. wakitanabahi
    3. wakitawahi
    4. wakiwahi
  9.  
    1. hawa wawa
    2. wawa hao
    3. wao hao
    4. wawa wale
  10.  
    1. kamati
    2. halmashauri
    3. ukumbi
    4. manispaa
  11.  
    1. kudunisha
    2. kudumisha
    3. kudhararisha
    4. kuidhinisha
  12.  
    1. kunapokuwa
    2. kutakapokuwa
    3. kukawa
    4. kunakuwa
    1. mkurupuko 
    2. mlipuko
    3. kuzika
    4. janga
  13.  
    1. nini
    2. gani
    3. nani
    4. kwa nini
  14.  
    1. msinacho hafaidi aliye nacho
    2. mwiba wa kujidunga hauambiwi pole
    3. yaliyopita si ndwele tugange yajayo
    4. kinga na kinga huwa moto

Kuanzia swala la 16-30 jibu swali kulingana na maagizo

  1. Kati ya mavazi yafuatayo, ni yapi ambayo huvaliwa na wanawake pekee? 
    1. Sidiria na suaruali. 
    2. Kaptura na surupwenye.
    3. Chepeo na bushati. 
    4. Gagro na kanchiri.
  2. Chagua sentensi ambayo ni sahihi kisarufi.
    1. Manyani waliharibu mimea yangu."
    2. Zulia ambayo imetandikwa sakafuni maridadi.
    3. Watu wengi huharibu masaa wakicheza.
    4. Gari ambazo zimenunuliwa zina rangi nzuri. 
  3. Kanusha
    Wachenje angekuja angetiwa mbaroni.
    1. Wachenje asingekuja angetiwa mbaroni.
    2. Wachenje hangekuja hangetiwa mbaroni. 
    3. Wachenje hangekuja asingetiwa mbaroni.
    4. Wachenje asingekuja asingetiwa mbaroni.
  4. Tumia kirejeshi -amba kwa usahihi
    Koja _______________  hupendeza ni ghali sana.
    1. ambacho
    2. ambalo
    3. ambayo
    4. ambao
  5. Nini ufupi ufupisho wa mwana wetu?
    1. Mwanetu.
    2. Mwanawetu. 
    3. Mwanaetu. 
    4. Mwanayetu. 
  6. Katika kujua usawa wa ukuta wa nyumba utatumia chombo kipi? 
    1. Pimamaji.
    2. Utepe. 
    3. Mizani.
    4. Timazi.
  7. Sentensi inayoonyesha hali ya kutendesha.
    1. Alisikia sauti ya mgeni. 
    2. Wimbo uliimbwa vizuri gwarideni. 
    3. Alipoteza kalamu ya jirani yake.
    4. Mshitakiwa alitozwa faini kubwa.
  8. Mke wa mwana ni
    1. mkazamwana.
    2. mka ahau.
    3. mwanyumba.
    4. mavyaa. 
  9. Jaza kwa kiunganishi kifaacho.
    _________________ mgeni akafika leo. 
    1. Labda
    2. Huenda
    3. Yakini
    4. Yamkini
  10. Baada ya Juma kusoma aliviweka vitabu katika
    1. dari.
    2. kigoda. 
    3. zulia.
    4. rafu.
  11. Nini udogo wa
    "Mwanamke ameenda" 
    1. kijanajike kimeenda.
    2. kijike kimeenda.
    3. kike kimeenda.
    4. kijimke kimeenda.
  12. Aina ya ngoma ndogo na nyembamba. Imewambwa upande mmoja na kutiwa vibati kwenye kingo zake, huchezwa kwa kutikiswa. Ala iliyoelezwa ni _______________
    1. zeze.
    2. mbiu.
    3. tarumbeta.
    4. dafu.
  13. Tambua sentensi iliyo na "kwa" ya umilikaji
    1. Yeye anaishi kwa nduguye. 
    2. Nyumbani kwao ni paradiso. 
    3. Mtalii huyo alitembea kwa madaha.
    4. Alipigwa kwa utovu wa adabu.
  14. Dada ni kwa kaka kama vile tembe ni kwa 
    1. kipora.
    2. dawa. 
    3. beberu.
    4. fahali.
  15. Malipo ya kuingilia ukumbini ni _________________
    1. mtaji.
    2. kiingilio.
    3. masurufu.
    4. koto.

Soma ufahamu huu taratibu kisha uyajibu maswali yote 31-40

Matatizo yalianza kumwandama binti Jamila alipojiunga na chuo kikuu na baadaye alipohitimu. Chaguo !a Jamila la kusomea siasa chuoni lilimwingiza kwenye uwanja wa wanaume wenye siasa kali kali. Ilikuwa vigumu kwake kupata kazi ya kudumu kwani wanaume walipinga sera na maoni yake hata yalipokuwa mazuri. Sehemu kadhaa alizozitembelea kuomba kazi, waajiri walimwangalia, wakamwuliza maswali na kumtakia asubiri majibu baadaye. Haikuwa vigumu kwake kujua kwamba kampuni ama mashirika hayo yalikuwa tayari kumwajiri mwanamume hata ingawa alikuwa amefaulu kuwazidi katika chuo kikuu

Jamila alianza kuhudhuria mikutano ya kuwahamasisha wanawake na kusoma katiba za vyama kadhaa vya kisiasa. Akiwa na imani kubwa kwamba wanawake wanaweza kuwa viongozi wazuri, alianza kuonyesha matumaini yake ya kugombea udiwani katika uchaguzi mkuu uliofuata. Pia alitembea vijijini na kuwashawishi wanakijiji kuhusu umuhimu wa kuwachagua wanawake zaidi ili wawe katika nafasi ya kutoa uamuzi wao. Alikuwa akiandika mfululizo wa makala kuhusiana na haki za wanawake yanayowaathiri. Waliowadharau wanawake na kudai kwamba kazi ni za nyumbani tu na wala sio kufanya uamuzi, iliwafaa kupata funzo kuwa hata mtoto wa kike anaweza kutoa maamuzi ya busara na anazo haki sawa na mtoto wa kiume.

  1. Nijinsia ngapi zimezungumziwa katika ufahamu huu? 
    1. Mbili. 
    2. Moja.
    3. Tatu.
    4. Nyingi.
  2. Shida za Jamila zilianza lini?
    1. Alipojiunga katika chuo kikuu.
    2. Kabla na baada ya kujiunga kwenye masomo chuoni.
    3. Baada ya kujiunga na kuhitimu chuo kikuu.
    4. Wakati wowote alipozungumza na wanaume kazini.
  3. Kutokana na kitenzi kuajiriwa tunapata nomino ipi?
    1. Mwajiri. 
    2. Mwajiriwa. 
    3. Majira.
    4. Ajira.
  4. Jamila alikuwa akisomea nini chuoni?
    1. Upigaji kura.
    2. Somo la sheria za wanawake.
    3. Haki za wanawake
    4. Siasa.
  5. Kwa nini kampuni na mashirika yalithamini wanaume kuliko wanawake?
    1. Wanawake hawakuwa na kisomo cha kutosha.
    2. Wanawake hawajui kufanya uamuzi kazini.
    3. Umuhimu wa wanawake haukuzingatiwa kwa sababu walidharauliwa na kuonekana kama waamuzi wa nyumbani.
    4. Wanazifahamu tu kazi za nyumbani na kazi za mashirika hawajazifahamu sana kama wanaume.
  6. Umoja wa wanawake ni mwanamke. Je, umoja wa wanaume ni
    1. mwanaume.
    2. mwanamume.
    3. mwanamme.
    4. kijana.
  7. Ni kweli kusema kuwa Jamila
    1. ana imani kuwa hata mke anaweza kuongoza vizuri.
    2. hana imani na wanaume wowote katika uongozi.
    3. anaamini kuwa hatapata kazi muradi wanaume wamo kazini.
    4. ni mwanamke mjane apiganiaye haki za wanawake.
  8. Maana ya kushawishi ni ____________
    1. kudanganya
    2. kufanya mtu avutike kutenda jambo fulani.
    3. kuchochea mtu kufanya jambo fulani.
    4. kuelimisha watu kuhusu jambo bila kushauriana.
  9. Sheria za vyama vya kisiasa zimo ____________
    1. vitabuni.
    2. bungeni.
    3. katibani
    4. shuleni.
  10. Unapata funzo gani kutokana na ufahamu uliousoma?
    1. Wanawake na wanaume sio sawa. 
    2. Ni vizuri kuwatia wanawake hamu ya kutenda mambo na kuwazingtia. 
    3. Sheria haijaruhusu mwanamke kuwa kiongozi na kufanya maamuzi yoyote.
    4. Elimu ya mtoto wa kiume ina manufaa kuliko ile ya mtoto wa kike.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41-50

Ukiyasoma majarida mbalimbali utazipata takwimu za kushangaza. Nyingi za takwimu hizi zinasababisha mtu hata akose matumaini. Takwimu zinaonyesha kuwa, watoto wanaokufa kabla ya kufikisha umri wa miaka mitano bado ni wengi. Wafao wakati wa kuzaliwa bado ni tele. Watu waambukizwao virusi vya ukimwi kila dakika ni wengi. Watu wanaokufa mikononi mwa majambazi wanazidi kuongezeka nao wafao katika ajali barabarani si haba. Watoto wetu wa kike wanaobakwa na wanyama katika ngozi za binadamu, idadi yao inazidi kuongezeka kila kukicha.

Utazidi kupoteza matumaini ukisoma na usikie kuwa, vijana wetu wanazidi kujiingiza katika utumiaji wa dawa za kulevya na pia vitendo vya ngono. Takwimu za watoto wafao kutokana na maradhi ya malaria nazo zinatisha.Sisemi wafao kwa maradhi mengine kama vile kifaduro. Ifahamike kuwa, wengine hufa kutokana na utapi wa mlo.

Upande wa uchumi, hakuna habari njema vilevile. Bila shaka kufikia sasa umezoea kusikia kuwa, zaidi ya sudusi ya raia nchini wamo katika kitovu cha umaskini. Hawawezi kupata hata angalau shilingi themanini kwa siku. Hebu fikiria kuhusu kiongozi wa jamii aliye na watoto sita ilhali hawezi kupata angaa shilingi themanini kwa siku. Nafasi za ajira nazo ni haba. Idadi ya wasio na kazi wala bazi inazidi kuongezeka

Kulingana na takwimu hizo, lile linaloonekana kukua kwa haraka ni mitaa ya mabanda katika miji yetu. Na je, unaelewa kuwa zaidi ya asilimia sabini ya wakazi wa mingi ya miji yetu huishi katika mitaa ya mabanda?
Tafadhali lifikirie hilo.

Nalo pengo kati ya matajiri na maskini linazidi kushamiri.Kila kukicha, matajiri wanazidi kunawiri huku maskini wakiendelea kudidimia na wengine hata kufifia kabisa.

Hali ya mazingira nayo haijaonyesha lolote la kuinua nyoyo zetu. Takwimu zinazidi kuonyesha misitu yetu inazidi kuangamizwa. Mito nayo inazidi kukauka. Maziwa yetu yanazidi kukauka na kuchafuka. Navyo viumbe vya majini kama vile samaki vinazidi kufariki dunia. Inasemekana pia kuwa kiwango cha joto duniani kinazidi kuongezeka. Si ajabu kujkosa theluji kileleni mwa mlima Kenya miaka michache ijayo. Nayo maradhi ya ngozi na ya saratani ya ngozi yazidi kuathiri na kufilisi ndugu na wazazi wetu.

Swali ni hili, je,tunaelekea wapi? Je, mambo haya yanatokea kwa kuwa hatuna uwezo wa kuyadhibiti au ni kwa sababu tunayavalia miwani? Katu, siamini kuwa hatuwezi kuyashinda. Uwezo tunao lakini nia haipo. Pasipo na nia njia haipo. Lakini tumaini lipo. Si tumaini pekee. Hata suluhisho. Nayo hayo ya mikononi mwenu enyi vijana. Kumbukeni mnao uwezo. Ni nyinyi viongozi wa kesho. Someni kwa bidii mwajibike ili muinusuru dunia.

  1. Katika aya ya kwanza, mwandishi ameyataja majanga mangapi?
    1. Sita.
    2. Matano.
    3. Saba.
    4. Manne.
  2. Kulingana na kifungu, mbali na maradhi, watoto wachanga aidha wanatishwa na :
    1. ukimwi.
    2. dawa za kulevya. 
    3. ukosefu wa chakula.
    4. wizi.
  3. Ni maelezo yapi sahihi?
    1. Ugonjwa wa malaria huwakumba watoto pekee. 
    2. Vijana wetu wametupilia mbali uovu wa ngono.
    3. Kifaduro ni uwele uwatishao watoto.
    4. Mengi ya maradhi yanadidimia.
  4. Kwa mujibu wa mwandishi, uhaba wa ajira unaweza kuzua matokeo yapi?
    1. Uhalifu.
    2. Kumarika kwa uchumi.
    3. Gharama ya maisha kupanda.
    4. Hatujaelezwa. 
  5. Kwa mujibu wa mwandishi, saratani ya ngozi inasababishwa na
    1. lishe bora.
    2. uchafuzi wa mazingira.
    3. mitaa ya mabanda.
    4. manukato yenye kemikali hatari.
  6. Je, unadhani hali ya mambo inayoelezwa hupatikana wapi? 
    1. Nchi zilizoendelea.
    2. Ni vigumu kujua.
    3. Katika mataifa yote duniani.
    4. Ulimwengu wa tatu.
  7. Kulingana na kifungu, ni takriban kiasi kipi cha wakazi wa mjini hakiishi katika mitaa ya mabanda? 
    1. Asilimia sabini.
    2. Ushuri tatu.
    3. Asilimia kubwa.
    4. Sudusi.
  8. Ni bayana kuwa uharibifu wa mazingira utasababisha?
    1. Kuzuka kwa maradhi kama vile ukimwi. 
    2. Kuangamia kwa viumbe mbalimbali.
    3. Kuongezeka kwa viwanda
    4. Kupunguka kwa kiwango kati ya wakwasi na walalahoi.
  9. Kulingana na taarifa, ni kipi kiini cha matatizo yote yaliyozungumziwa?
    1. Ugumu wa maisha. 
    2. Mazingira. 
    3. Matendo ya binadamu.
    4. Umaskini. 
  10. Ni sahihi kusema kuwa:
    1. Mwandishi ni mkwasi wa mali.
    2. Tamaa ya mwandishi ya kushuhudia. 
    3. Vijana wana fursa na satua ya kuboresha mambo.
    4. Binadamu hana uwezo wa kuyatatua matatizo yaliyozungumziwa.

MARKING SCHEME

  1. A
  2. A
  3. D
  4. B
  5. A
  6. A
  7. B
  8. A
  9. C
  10. B
  11. B
  12. B
  13. A
  14. C
  15. B
  16. D
  17. A
  18. D
  19. B
  20. A
  21. D
  22. C
  23. A
  24. B
  25. D
  26. A
  27. D
  28. B
  29. A
  30. B
  31. A
  32. C
  33. D
  34. D
  35. C
  36. B
  37. A
  38. C
  39. C
  40. B
  41. A
  42. C
  43. C
  44. D
  45. C
  46. D
  47. B
  48. B
  49. C
  50. C

KISWAHILI
DARASA LA SITA
MTIHANI WA MWISHO WA MUHULA WA 2 

Jaza nafasi zilizoachwa wazi kwa kuchagua kitenzi kifaacho zaidi.

Hapo    1      za kale aliishi mzee       2           3       Falsafa. Hilo     4     jina la       5     kwa sababu alikuwa na hekima. Baada ya kazi zake mchana   6    aliwakusanya vijana jioni na kuanza    7   .Alikuwa na    8    ya kuwakuza vijana wakiwa na   9      kwani alifahamu kuwa vijana    10  kizazi cha kesho.

Mzee Falsafa hakutaka kulipwa kwa sababu alikuwa akiifanya kazi hiyo kwa     11     ulikuwa ni mchango wake kwa     12    . Katika kuwaelekeza, aliwahimiza   13      bila kujali kabila au tabaka kwani umoja ni nguvu. Suala    14     lilikuwa ni     15      ya wavulana ilikuwa ni daraja la utoto utu uzima.

  1. A. zamani                B. samani             C.kale                 D.juzi
  2. A.moja                     B.mmocha            C.mmoja             D.mocha
  3. A anayeitwa             B.aliyeitwa            C.anaitwa           D.ataitwa
  4. A.lilikuwa                 B.likuwa                C.lilikua               D.litakuwa
  5. A.msiba                   B.mzaha               C.msimbo            D.mtaa
  6. A.kesho                   B.usiku                  C.kucha              D.kutwa
  7. A.kuwafunza            B.kuwasoma        C.kuwajali            D.kuwazomea
  8. A.lengo                    B.nia                     C.mpango           D.ujuzi
  9. A.maadili                 B.maisha               C.maadili mema  D.furaha
  10. A.ndicho                  B.ndiyo                  C.ndio                  D.ndizo
  11. A.sharti                    B.lazima                C.hiari                  D.shurti
  12. A.umati                    B.uma                    C.walimu             D.umma
  13. A.kutengana            B.kutangamana     C.kuchukiana      D.kulaumiana
  14. A.lingine                  B.zingine                C.nyingine           D.jingine
  15. A.kutahiri                 B. tohara                C.funzo               D.somo

Kuanzia swali la 16-30. jibu swali kulingana na maagizo.

  1. Kiongozi wa sala msikitini ni
    1. imamu
    2. kuhani
    3. katkisti
    4. mchungaji
  2. Wanaume walioa dada wawili huitanaje? 
    1. Mwamu
    2. Shemeji
    3. Mwanyumba
    4. Wifi 
  3. Andika wingi wa sentensi hii
    Nenda naye akuonyeshe mali yangu.
    1. Nenda nao wakuonyeshe mali yangu.
    2. Nendeni nao wamuonyeshe mali yetu.
    3. Nenda nao wawaonyesghe mali yetu.
    4. Nendeni nao wawaonyeshe mali yetu.
  4. Kikembe cha samaki ni;
    1. dagaa
    2. kichengo
    3. kimatu
    4. kiluwiluwi
  5. Tegua kitendawili kifuatacho
    Hakionekani wala hakishikiki
    1. kisogo
    2. mafiga
    3. uga
    4. hewa
  6. Andika katika hali ya ukubwa
    Mtoto mzuri anasoma
    1. Toto zuri linasoma
    2. Toto mzuri anasoma
    3. Kitoto kizuri kinasoma
    4. Kitoto zuri kinasoma
  7. Kamilisha methali
    Mwenda tezi na omo marejeo
    1. nyumbani
    2. kazini
    3. inshallah
    4. ngamani
  8. Zana hii ya ujenzi inaitwaje
    kisst6et2q23
    1. timazi
    2. msasa
    3. tupa
    4. parafujo
  9. Kitanda cha kubebea wagonjwa hospitalini huitwaje
    1. kigoda
    2. wadi
    3. machela
    4. mkungu
  10. Kanusha sentensi hii
    Mzee aliniita kuniadhibu
    1. Mzee hakuniita wala kuniadhibu
    2. Mzee hajaniita na hajaniadhibu
    3. Mzee hakukuita ili akuadhibu
    4. Mzee hajaniita ili akuadhibu
  11. Makazi ya mfalme huitwa
    1. ikulu
    2. kasri
    3. kizimba
    4. wamamu
  12. Anayetibu wagonjwa ni tabibu
    Anayeendesha gari la moshi ni
    1. Rubani
    2. Mzegazega 
    3. Kandawala
    4. Hamali 
  13. Kemboi alijifunika
    1. chepechepe!
    2. Rovurovu!
    3. Ndi!
    4. Gubigubi!
  14. Andika akisami subui
    1. 1/5
    2. 1/7
    3. 1/6
    4. 1/9
  15. Nyama ya mgongo huitwa
    1. shahanu
    2. ndewe
    3. sarara
    4. . kidari

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali ya 31 - 40.

Kiprop alikuwa na mkewe aliyeitwa Lilia. Walibarikiwa kupata watoto watatu. Walikuwa wakiishi katika shamba lao kwenye kitongoji kilichoitwa Mwendakwao. Kijiji hiki kilikuwa mbali na mji wowote.

Jamaa hii haikuishi peke yake. Hapo nyumbani pao palikuwa naye mwanamume mzee kidogo aliyekuwa ameishi nao kwa siku nyingi kidogo. Mtu huyu aliitwa Matakia. Alikuwa mtu mwema. Aliisaidi. sila ya Kiprop kwa mengi. Walikwenda kulima shambani pamoja. Aliwasaidia kupalilia akiwaangalia na kuwatunza watoto wa jamaa ya Kiprop Matakia alikuwa ni rafiki wa dhati hapo nyumbani. Lakini nguvu zilianza kumwishia alipoanza kuwa mzee.

Nyumbani hapo pa Bwana Kiprop alikuwapo pia mbwa aliyeitwa Jeki. Mbwa huyo ndiye aliyekuwa mlinzi wa nyumbani wakati watu walipokwenda shambani. Akawa ni rafiki wa nyumba ile kwa muda mrefu.

Jeki alianza kuchoka kwa ajili ya uzee. Nguvu zake zikaanza kumalizika. Akawa analala ovyo ovyo tu. Kubweka na ukali wake, vyote vilikuwa vimemwishia. Meno yake yakaanza kung'oka moja mojamifupa kwake ikawa shida kutafuna. Akawa anapikiwa vyakula laini laini, rojorojo hivi kama uji. Akawa hawezi kuirarua mifupa migumu kama alivyozoea hapo awali akiwa na meno.

Naye Matakia alianza kuuguagua. Hakuweza kutenda kazi zake sawa kama hapo mwanzo. Badala ya kuamka saa thenashara za asubuhi kama kawaida yake, alichelewa kitandani kufikia hata saa tatu hivi.

  1. Kiprop alikuwa na aila ya watu wangapi?
    1. Watatu.
    2. Watano.
    3. Sita.
    4. Saba.
  2. Matakia alikuwa
    1. Ajuza
    2. Bawabu
    3. Mlinzi
    4. Msaidizi
  3. Pamoja na shughuli zake pale nyumbani,
    Matakia hakushiriki
    1. kuwalea watoto
    2. kufyeka konde C
    3. kuwaogesha watoto
    4. kuwanyanyasa watoto
  4. "Matakia alikuwa ni rafiki wa dhati hapo nyumbani" kwani
    1. Alisaidia kwa mapana na marefu
    2. Alisaidia kwa hali na mali
    3. Alisaidia kufa na kupona
    4. Alisaidia daima dawamu 
  5. "Jeki alihesabiwa kama rafiki wa nyumba ile, "kwa sababu
    1. Alibweka sana
    2. Aliyalinda maskani yale
    3. Aliwalinda watoto wa mifugo
    4. Aliishi muda mrefu
  6. Jeki alipoanza kuzeeka alikuwa
    1. Akichoka ovyo
    2. Akijilaza ovyo ovyo
    3. Akibweka kwa ukali
    4. Akitaka uji tu
  7. Matakia alianza kuugua na kuchelewa kuamka
    1. Alipoanza kuwa mzembe
    2. Alipoanza kuzeeka
    3. Alipochoka kufanya kazi
    4. Alipogombezwa
  8. Neno muhali limetumiwa kuinaanisha
    1. vigumu
    2. rahisi
    3. hataki
    4. mahali 
  9. Saa thenashara ni
    1. Saa kumi
    2. Alfajiri
    3. Saa kumi na mbili
    4. Asubuhi
  10. Kichwa mwafaka cha habari hii ni
    1. Matakia na Jeki
    2. Jamii ya Kiprop
    3. Kiprop na rafiki zake
    4. Jamii ya Kiprop na rafiki zake

Soma shairi hili kwa makini kisha wjibu maswali kutoka 41 hadi 50.

Moyo wanambia penda, mtu mjinga sipende,
Mjinga ukimpenda, hajui nini atende,
Moyo wanambia tenda, lisilotendwa sitende,
Fanya wanavyotenda, wenzio wasikushinde.

Moyo wanambia imba, wimbo mbaya siimbe,
Imba wimbo wa kupamba uwapumbaze wakembe
Moyo wanambia omba, ombi ovu usiombe,
Omba Mungu Muumba, dhiki azifanye chembe.

Moyo wanambia meza, kinachokwama simeze,
Kinachokwama kumeza, kinywani sielekeze,
Moyo wanambia uza, roho yako usluze,
Fanya unavyoweza, neno hili jikataze.

Moyo wanambia cheza, michezo mbi sicheze,
Cheza walcupendeza, wenzio wakuigize,
Moyo wanambia kaza, bidii usipunguze,
Usipunguze kuwaza, mawazonijiingize.

Moyo wanambia kopa, deni kubwa usikope,
Usiloweza kulipa, siku zote usiepe,
Moyo wanambia apa, kwa batili usiape,
Wala usifanye pupa, kiapo ukiogope.

Moyo wanambia kana, neno la kweli usikane,
Kweli unapiona, fanya bidii unene,
Moyo wanambia chuna, ngozi yako usichune,
Japo nyeusi sana, bora kuliko nyingine.

  1. Katika ubeti wa kwanza:
    1. Moyo wamkanya mtunzi kumpenda mjinga
    2. Moyo wamkanya mtunzi aismpende mjinga
    3. Moyo wamwambia mtunzi asitende kama wenzake
    4. Mtunzi asema ukimpenda mjinga, hujui unachotenda.
  2. Mtunzi anasema
    1. Wimbo mbaya unaweza kukupamba 
    2. Umwimbie Mungu Muumba
    3. Meza kitu kinachoweza kukusakama
    4. Uendeleze uwezo wa kufikiri na kutafakari .
  3. Mshairi asema kwamba 
    1. Ikibidi ukope deni dogo la kulipa
    2. siku zote uyaepe madeni ya aina yoyote 
    3. unaweza kuapa kwa ubatili
    4. fanya bidii uwe mnene lakini usichune ngozi
  4. Shairi lenye muundo huu huitwa
    1. tathlitha
    2. taklimisa
    3. tarbia
    4. tathnia
  5. Kifungu kimoja cha shairi huitwa
    1. mshororo
    2. mizani
    3. kibwagizo
    4. ubeti
  6. Kibwagizo cha ubeti wa tatu kina mizani mingapi?
    1. 15
    2. 16
    3. 4
    4. 8
  7. Upini mpangilio sahihi wa vina vya kati na vya mwisho katika ubeti wa sita (mwisho)
    1. na-ne
    2. ne - na
    3. .za - ze
    4. .a-e
  8. Badala ya kutumia neno wakembe; mtunzi angetumia neno jingine sawa na hilo ambalo
    1. wazembe
    2. watu
    3. wapumbavu
    4. watoto
  9. Bingwa wa kutunga nyimbo huitwa manju, naye bingwa wa kutunga mashairi huitwa?
    1. Sogora
    2. Malenga
    3. Manju
    4. Hatibu
  10. Kichwa mwafaka kwa shairi hili ni
    1. Moyo
    2. Wakembe
    3. Shule yangu
    4. Ajali

MAAKIZO

  1. A
  2. C
  3. B
  4. A
  5. C
  6. D
  7. A
  8. B
  9. A
  10. C
  11. C
  12. D
  13. B
  14. D
  15. B
  16. A
  17. C
  18. D
  19. B
  20. D
  21. A
  22. D
  23. A
  24. C
  25. A
  26. B
  27. C
  28. D
  29. B
  30. C
  31. B
  32. D
  33. D
  34. A
  35. B
  36. C
  37. B
  38. A
  39. C
  40. D
  41. A
  42. A
  43. A
  44. C
  45. D
  46. B
  47. D
  48. C
  49. B
  50. A

MASWALI

Soma taarifa ifuatayo huku ukijaza pengo kwa neno lifaalo zaidi kati ya yale manne uliyopewa
Takriban _1_ imetupasa kufanya kazi. Tunafanya kazi ili tujimudu maishani. Kazi_2_uti wa_3_wa maisha_4_binadamu. Iwapo binadamu yeyote anataka kuishi maisha_5_ni sharti ajikaze_6_kazini. Ikiwa mitume watukufu walifanya kazi_7_ sisi ambao daraja_8_ni ndogo mbele ya Mwenyezi Mungu. Kazi humpa mtu_9_na vilevile kumwezesha kuikidhi_10_yake. Isitoshe, ataweza kuishi raha mustarehe.

  1.                
    1. zote 
    2. sote
    3. wote
    4. nyote
  2.                
    1. ndio
    2. ndilo
    3. ndicho
    4. ndiyo
  3.                        
    1. mgongo
    2. moyo
    3. roho
    4. mkono
  4.                   
    1. wa
    2. la 
    3. ya
    4. cha
  5.                       
    1. njema
    2. mema
    3. jema
    4. vyema
  6.                        
    1. sauni 
    2. kizabuni
    3. kisabuni
    4. kwa sabuni
  7.                      
    1. Ingawa
    2. Sembuze
    3. Licha ya
    4. Seuze
  8.                      
    1. letu
    2. chetu
    3. yetu
    4. wetu
  9.                      
    1. taadhimu
    2. taadhima
    3. tathmini
    4. thamini
  10.                        
    1. jamii
    2. jama
    3. jamani
    4. jamaa

Rehema alifurahi sana kukutana na nyanya yake. Pindi tu akamwamkua "_11__"Naye Nyanyake akaitikia" _12_ mjukuu wangu."Hapo wakaanza kupiga _13_ kuhusu mambo kadha wa_14_ Kulipokuchwa, wakaagana" _15_ ".

  1.                            
    1. Hujambo
    2. Sijambo
    3. Habari
    4. Shikamoo
  2.                              
    1. nzuri
    2. vyema 
    3. marahaba
    4.  salama
  3.                      
    1. gumzo
    2. kasia 
    3. mbinja
    4. stori
  4.                
    1. kadhaa 
    2. kadha 
    3. kadhia
    4. kadhalika
  5.                    
    1. sabalheri 
    2. masalheri 
    3. macheo
    4. alamsiki 

Kutoka swali la 16-30 chagua jibu lililo sahihi kulingana na maagizo 

  1. Kamilisha sentensi kwa tanakali zifaazo.
    Yusufu alitumbukia majini ............... na kuzama .................
    1. tumbwi, zii
    2. tumbwi, jii
    3. chubwi, zii
    4. chubwi, jii
  2. Tumia 'amba' kwa usahihi katika sentensi ifuatayo.
    "Tafadhali nionyeshe mfereji .............................. nyinyi huteka maji ya kunywa."
    1. ambapo
    2. ambao
    3. ambayo
    4. ambamo
  3. Kamilisha: Penye miti
    1. pana wajenzi. 
    2. kuna misitu.
    3. hapana wajenzi
    4. hakuna watu.
  4. Chagua jibu sahihi.
    1. mmoja mmoja.
    2. moja moja.
    3. mmoja kwa mmoja
    4. kimoja kimoja
  5. Kamau alisema angesafiri ndege.
    1. na 
    2. kwenye 
    3. penye
    4. kwa 
  6. Kifungu kimoja cha shairi huitwa
    1. mshororo. 
    2. ubeti. 
    3. kibwagizo.
    4. mizani.
  7. Msichana yule ana nywele...........................  na pua ............................
    1. mrefu, dogo 
    2. refu/dogo 
    3. ndefu/ndogo
    4. ndevu/ndogo 
  8. Kutokana na kitenzi KUFA, tunapata nomino
    1. mfu. 
    2. maiti.
    3. mkufa.
    4. mfua.
  9. . Kamilisha:
    Unataka nyumba yako ijengwe
    1. vipi
    2. yupi 
    3. ipi
    4. upi 
  10. Akisami inaitwaje?
    1. Thumuni tatu 
    2. Humusi tatu
    3. Tusui tatu. 
    4. Subui tatu.
  11. Kikembe cha simba ni sibli, je kikembe cha nguruwe ni 
    1. kisui. 
    2. kiyoyo.
    3. kinda.
    4. kivinimbi. 
  12. Neno unyasi liko katika ngeli gani?
    1. U-ZI
    2. U-U
    3. I-ZI
    4. A-WA 
  13. Soma, kula, tembea, cheza ni
    1. nomino. 
    2. vielezi.
    3. ngeli.
    4. vitenzi.
  14. Kanusha sentensi hii
    Johana ameandika kisha akalala. 
    1. Johana hakuandika na hakulala. 
    2. Johana hajaandika wala kulala. 
    3. Johana haandiki na halali.
    4. Johana hataandika wala hata lala.
  15.  Andika kwa wingi.
    Ulezi mwema umenisaidia. 
    1. Malezi mema yamemsaidia. 
    2. Ulezi mema yametusaidia. 
    3. Malezi mema yametusaidia. 
    4. Malezi mema yamenisaidia. 

Soma kifungu kifuatacho kisha uyajibu maswali 31-40
Fatuma aliachwa na mamake akiwa mchanga. Alipofikia umri wa miaka kumi naye babake mpendwa pia aliaga dunia. Kifo cha babake kilimtia sana simanzi.
Fatuma alibaki yatima na hakuwa na budi kuishi na ami yake Maina. Kwa kuwa lisilokuwa na budi hutendwa, Fatuma aliishi na Maina bila wasiwasi. Maisha ya Fatuma yalikuwa mazuri hadi Maina alipochukua jiko. Hapa acha ale mwata kwa huyo mkazaami wake!
Babake Fatuma alipoaga dunia aliacha mali ya kutosha lakini hayakumfaidi mwanawe wa kipekee. Kidosho aliyeolewa aliukatiza upendo baina ya mtu na mpwa wake. Mwanamke huyo alikuwa nduli mkubwa aliyemletea Fatuma madhila makubwa. Kwa hakika kidosho alileta mfarakano katika ukoo huo. Fauka ya hayo Fatuma alijikaza kisabuni na kuendelea kuishi hapo.
Bi. Kidosho alikazana kwa fitina bila kuchoka, kwani kinolewacho hupata."Naye Maina alisalimu amri kwa ua lake la moyo. Kwa ghafla, Maina alimgeuka mpwa wake mithili ya hewa inavyobadilika. Acha Fatuma aone cha mtema kuni. Jambo la kwanza alikatizwa masomo na kuwekwa nyumbani. Alitumwa kama kijakazi. Ungepata fursa ya kumwona ungemwonea huruma. Nguo alizokuwa akivaa zilikuwa nyeusi kama chungu, na uso wake ungedhani ni ule wa kipaka jiko.
Ni kweli kuwa mja akifunga wake wa Maulana u wazi. Haukupita muda mrefu kabla ya habari ya mateso ya Fatuma kusambaa kama moto wa nyasi. Bila ya tatizo lolote habari ilimfikia afisa msimamizi wa watoto katika sehemu hiyo. Fedheha kubwa ilimpata Maina kwani alishtakiwa kwa kumnyima Fatuma haki zake. Alionekana kuwa amevunja kufungu cha sheria ya watoto. Bila ya kusita hakimu alimhukumu Maina kifungu cha miaka sita au faini ya shilingi laki saba. Pia aliamrishwa arudishe urithi wa Fatuma. Fatuma aliambiwa arudi shuleni aendelee na masomo yake.

  1. Fatuma aliishi na
    1. mjomba wake.
    2. kakake baba.
    3. kakake mama.
    4.  dadake mama. 
  2. Ni kweli kusema kuwa
    1. mamake Fatuma alimwachia mali nyingi. 
    2. kidosho alileta mapenzi katika jamii hiyo.
    3. kifo cha babake Fatuma hakikumletea upweke. 
    4. Kidosho ndiye aliyekuwa chanzo cha masaibu ya Fatuma. 
  3. Kulingana na habari mama yake Fatuma alikuwa
    1. ameaga.
    2. ameenda safari.
    3. mzima.
    4. akifanya kazi mbali. 
  4. Mwanamke ni kwa kijakazi kama vile mwamume ni kwa
    1. topasi.
    2. mjakazi.
    3. kitwana.
    4. mzegazega.
  5. "ale mwata” katika habari ina maana ya
    1. kuona ujasiri. 
    2. kupata nafuu. 
    3. kupata ujasiri.
    4. kupata taabu.
  6. Nimethali gani inayowiana na habari hii?
    1. Mtaka cha mvunguni sharti ainame.
    2. Mola hamtupi mja wake.
    3. Usitupe mbachao kwa mswala upitao.
    4. Ukipanda pankwisha utavuna pantosha. 
  7. Kilichomwokoa Fatuma kilikuwa ni
    1. kufanya kazi kwa bidii.
    2. askari waliopiga nduru. 
    3. kuenea kwa habari zake za mateso.
    4. kuacha shule na kukaa nyumbani. 
  8. Maina aliaibika wakati
    1. aliposhtakiwa. 
    2. alipofungwa jela. 
    3. alipoamriwa kurudisha urithi.
    4. alimwoa kidosho. 
  9. Maina alitozwa faini ya shilingi?
    1. 7000
    2. 70,000
    3. 700,000
    4. 7.000.000 
  10. Kichwa mwafaka kwa hadithi hii ni
    1. Mnyonge hana haki.
    2. Meskia hachoki.
    3. Tupuuze haki za watoto.
    4. Ajira ya watoto.

Soma kifungu kifuatacho kisha uyajibu maswali 41-50
Rehema alikuwa mtoto wa tatu katika familia ya Mzee Kazamoyo. Alikuwa mziwanda kwa kuzaliwa na mama penda raha. Nduguze walikuwa Yusufu na Yohana
Hawa walikuwa wavulana watanashati sana. Rehema alikuwa banati mmoja tu miongoni mwa ghulamu wawili. Mzee aliwalea vizuri sana wanawe, kwa heshima na adabu, kwa utu na ubinadamu. Wavulana walikuwa wacheshi kama vinyago. Naye binti alikuwa malaika. Kwa upole na wema, Rehema alikuwa nambari moja. Watu wengi walimpenda na kumheshimu sana. Kweli heshima si utumwa. Lakini Mzee Kazamoyo alikuwa simba.
Mzee Kazamoyo alikuwa mwindaji haramu kwa jina jingine,jangili. Aliwaua wanyama pori kisha akauza nyama kwa wenye hoteli na vilabu vya starehe vya mjini. Kitendo hiki cha kuwaua wanyama, hakikumpendeza Rehema.
“Wanyama lazima walindwe badala ya kuwaua" alisema kimoyomoyo. “Mbona baba anaharibu maliasili? alizidi kuuliza. "Watalii wakija kwetu watawaona wanyama gani? Msichana alisikitika zaidi.
Kusema kweli wanyama wakiwindwa kiholela na kuuwawa ovyo ovyo, hatutakuwa na wanyama pori siku zijazo. Tunapohifadhi mazingira, tunawahifadhi wanyama pia. Siku moja Mzee Kazamoyo alimshika kasuku kwa mtego akaja naye nyumbani. Alitengeneza tundu akamtia kasuku huyo ndani. Tundu lenyewe akalitundika kwenye dari upenuni.
Rehema alikuwa akimwangalia babake kwa makini sana tangu alipokuwa na kasuku mpaka kumfungia kwenye tundu. Hakumwona baba akimpa ndege yule punje ya mchele au mtama.

  1. Katika aya ya pili Mzee Kazamoyo aliwalea wanawe kwa njia ifuatayo isipokuwa?
    1. Kwa taadhima. 
    2. Kwa ukatili.
    3. Kwa utu na ubinadamu.
    4. Kwa adabu. 
  2. Kulingana na habari uliyoisoma Mzee
    Kazamoyo alikuwa akifanya kazi gani? 
    1. Alikuwa akifanya kazi ofisini. 
    2. Alikuwa akiuza ndege aina ya kawaida. 
    3. Alikuwa mkulima hodari.
    4. Alikuwa mwindaji wa wanyama pori. 
  3. Ni kweli kusema kuwa
    1.  Mzee Kazamoyo alikuwa kitinda mimba kwa kuzaliwa. 
    2. Mzee Kazamoyo alikuwa mzalendo halisi ya nchi yake. 
    3. Rehema alikuwa mchapakazi shuleni. 
    4. Rehema ndiye aliyekuwa mtoto wa kwanza katika familia hiyo. 
  4. Neno wanyamapori kama ilivyotumika katika makala haya unaweza pia kuitwa ! 
    1. binadamu.
    2. vimelea.
    3. hayawani.
    4. nyuni. 
  5. Kinyume cha utumwa ni 
    1. uwazi.
    2. undugu. 
    3. ufungwa. .
    4. uhuru.
  6. Mwandishi ametaja Mzee Kazamoyo kuwa simba maanake?
    1. Alikuwa mfalme katika kijiji hicho.
    2. Alikuwa mkali kwa hivyo aliogopwa kwake. 
    3. Ni mzee aliyependa simba.
    4. Aliwinda simba sana. 
  7. Kati ya orodha ifuatayo ni gani ndege pekee?
    1. Chiriku, kasuku, mbayuwayu, njiwa. 
    2. Kasuku, korongo, mjomba, kuku. 
    3. Kasuku, nzige, tandu, mbuni.
    4. Sibli, njiwa, kaka, korongo. 
  8. Kulingana na taarifa ni nini hakikumfurahisha Rehema? 
    1. Maisha yake mwenyewe. 
    2. Hatujaambiwa. 
    3. Kitendo cha babake.
    4. Kitendo chake baadaye. 
  9. Baada ya Mzee Kazamoyo kumnasa ndege aliweka wapi? 
    1. Alihifadhi kwenye ghala. 
    2. Aliweka juu ya nyumba yake huku akaingiza kwenye paa. 
    3. Alimtengengezea nyumba mzuri nje ya nyumba.
    4. Alimwua na kuuza kwa wenye hoteli.
  10. Kichwa mwafaka cha taarifa hii ni
    1. Wanyamapori. 
    2. Kisa cha simba.
    3. Mwindaji hodari wa ndege. 
    4. Mzee Kaza moyo na familia yake.

Marking Scheme

swa ms

Insha

Andika insha ya kuvutia kuendeleza maneno uliyopewa.
Tulisikia kelele kwenye barabara iliyopo karibu na shule yetu. Sote tukatoka madarasani mwetu na ........................................

KISWAHILI
DARASA LA 8
MWISHO WA MUHULA WA 2

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo. Jaza kila pengo kwa kuchagua jawabu lifaalo zaidi.

Nchi     1       Kenya hujivunia umoja na      2       wa hali ya juu.     3      kuna makabila mengi, lugha ya Kiswahili    4        na wakenya wa makabila mbalimbali ili     5         Vilevile wimbo wa taifa, michezo na bendera ya taifa husaidia    6       magugu ya ukabila na chuki. Kila binadamu, bila      7       kabila wala lugha yake, ana umuhimu mkubwa. Tunapoishi       8       amani na umoja, bila shaka uchumi wetu utaimarika Ni vyema kukumbuka kuwa    9     

  1. A.la                         B.ya                         C.mwa                      D. kwa
  2. A. mgawanyiko       B. utengano             C. utangamano        D. vurugu
  3. A. Ingawa               B. Licha ya               C. Lakini                   D. Hata hivyo
  4. A. hutangazwa        B.husomwa             C. huandikwa            D. hutumiwa
  5. A. kuwastawisha na kuwalenga
    B. kuwadunisha na kuwajenga
    C. kuwaunganisha na kuwatambulisha
    D. kuwahamasisha na kuwalinganisha
  6. A. kupanda              B. kupalilia                C. kung'oa             D. kunyunyizia
  7. A. kujua                   B. kujali                     C. kuthamini          D. kutambua
  8. A. katikati                 B. kwa                      C. ndani ya            D. kwenye
  9. A. umoja ni nguvu utengoni ni udhaifu
    B. chururu si ndondondo
    C. akiba halozi
    D. haba na haba hujaza kibaba

Kijana   10    aliketi pale   11   baada ya hakimu kuamua kwamba afungwe kwa miaka kumi. Alifungwa kwa sababu ya utapeli   12    aliufanya akitumia simu. Pesa hizo za wizi zilimtajirisha hadi   13    katika jumba la kifahari.   14   siku yake ya arubaini ilikaribia, nayo ilipofika alikula    15    kwelikweli.

  1. A. yeyote           B. ambaye            C. mwenye            D. mwenyewe
  2. A. gerezani        B. rumande           C. kizimbani          D. chupani
  3. A. ambao           B. ambayo            C. ambalo              D. ambaye
  4. A. akahama       B. akaguria            C. akahamishwa   D. akagurisha
  5. A. Kumbe           B. Pengine            C. Kwa sababu     D. Labda
  6. A. njama            B. nyama ya ulimi  C gumzo               D. kalenda

Kuanzia nambari 16 mpaka 30. jibu kila  swali kulingana na maagizo uliyopewa.

  1. Chagua orodha yenye vielezi vya idadi pekee.
    1. mmoja, wengi, wachache
    2. polepole, vizuri, haraka.
    3. mapema, asubuhi, jana,
    4. sana, tena, aghalabu.
  2. Maneno yafuatayo yatakuwaje katika kamusi kuanzia la kwanza hadi la mwisho?
      1. Bahati
      2. Babaika 
      3. Bahari
      4. Baidika
    1. (iii), (i), (iv). (ii)
    2. (i), (iv) (iii) (i)
    3. (ii).(iii) .(i) (iv)
    4. (ii), (iii), (iv), (i)
  3. Ni orodha ipi yenye nomino za ngeli ya YA-YA pekee?
    1. maji, mate, mapishi.
    2. mazingira, mapishi, malezi.
    3. magonjwa, maumbo, maisha.
    4. manukato, mafuta, maradhi.
  4. Sentensi gani iliyo sahihi kati ya hizi?
    1. Mbuzi wowote watachinjwa kesho.
    2. Kitabu chenyewe kiliandikiwa ni chake.
    3. Nguo ile ingine itafuliwa
    4. Gari jeupe ni ya mwalimu. 
  5. Chagua sentensi iliyotumia ki kuonyesha wakati endelezi.
    1. Ukienda nyumbani uniambie.
    2. Mbuzi alikuwa akilala fisi alipompata
    3. Watoto walimwona alipotembea kijeshi
    4. kijibwa chake kimepotea.
  6. 'Mawazo, hasira, furaha' ni mifano ya nomino za aina gani?
    1. Nomino za pekee
    2. Nomino za dhahania .
    3. Nomino za kawaida
    4. Nomino za wingi. 
  7. Tambua sentensi ambayo inaonyesha istiara kati ya hizi.
    1. Wageni wote waliowasili ni malaika
    2. Mji ule ulimpokea kwa mikono miwi
    3. Wazazi wamekaa nyumbani wakisubiri watoto wao wachanga wawanunulie chakula
    4. Watu walijaa uwanjani hadi nafasi ya nzi kutua ikakosekana.
  8. Chagua ukanusho wa sentensi: Kitabu kilichopotea kimepatikana.
    1. Kitabu kilichopotea hakikupatikana.
    2. Kitabu kisichopotea hakijapatikana
    3. Kitabu kisichopotea hakikupatikana
    4. Kitabu kilichopotea hakijapatikana. 
  9. Neno gani lililo na silabi nne kati ya haya?
    1. Potelea
    2. Lala
    3. Mbuzi
    4. Mbaya
  10. Chagua sentensi inayomaanisha kuwa Musa hakuchelewa kazini kwa kuwa aliamka mapema
    1. Musa asingechelewa kazini angeamka mapema
    2. Musa asingeamka mapema angechelewa kazini
    3. Musa angeamka mapema angechelewa kazini.
    4. Musa angechelewa kazini angeamka mapema
  11. Maelezo gani ambayo si sahihi kuhusu neno shinda?
    1. Kuwa na ugumu wa kutendeka.
    2. Ni kuwa wa kwanza katika mashindano.
    3. Ni kukaa mahali mchana wote.
    4. Ni dhiki au matatizo
  12. Sentensi ipi iliyotumia kiunganishi kwa usahihi?
    1. Maadamu alimshauri vizuri hakufaulu.
    2. Ilhali mtoto ameanguka hajalia.
    3. Umeshindwa kununua baiskeli sembuse gari!
    4. Minghairi ya kununua gari alisafiri haraka
  13. Chagua orodha yenye aina za mashain pekee.
    1. Utenzi, mizani, kibwagizo
    2. Ngojera, tarbia, utenzi.
    3. Ukwapi, utao, mwandamizi.
    4. Mwanzo, mloto, mleo.
  14. Tambua sentensi iliyotumia kivumishi cha idadi ya nafasi katika orodha
    1. Mwanafunzi wa pili anajua kuogelea.
    2. Madawati mengi yamepakwa rangi
    3. Mama amenunua marinda mawili.
    4. Mipira michache imenunuliwa. 
  15. Wakati wa macheo, jua huwa upande gani wa dira?
    1. Mashariki
    2. Magharibi
    3. Kaskazini
    4. Kusini

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali kutoka 31 hadi 40.

Ni nani mwenye akili razini awezaye kupata hata lepe la usingizi usiku kama huo? Niligaagaa kitandani huku nimetawaliwa na kiwewe na wasiwasi uliopiku ule wa mwasi. Niliwaza na kuwazua jinsi siku iliyofuata ingekuwa keshoye, ilikuwa siku ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa gatuzi letu Uchaguzi huo mdogo ulifanyika baada ya aliyekuwa gavana wetu kufumwa na mvi wa manaya katika ajali ya barabarani. Bila shaka, hakuna aliyetarajia kwamba ningekuwa nambari ya pili, sembuse nambari ya kwanza? Ilikuwa wazi kama pengo kuwa ningeburura mgwisho. Tangu lini mja asiyekuwa na misuli ya kihela akaibuka mshindi katika kinyang'anyiro chochote cha uchaguzi? Licha ya kuwa mkata aliyekatwakatwa na ukata, nilitoka katika kabila lenye watu wachache mno.

Asubuhi ilipofika, nilichukua baiskeli yangu na kuiendesha polepole huku wafuasi wangu wakinishangilia nilipopita. Tuliwasili katika ukumbi wa kaunti ya Ingusi, ambapo matokeo ya uchaguzi huo yangetangaziwa. Ukumbi huo ulijaa sisisi ya watu wake kwa waume, wazee kwa vijana, waliosoma kwa wasiosoma. Mashangingi ya wapinzani wangu yalikuwa yameegeshwa pale nje. Maafisa wa polisi walizunguka hapa na pale ili kuhakikisha kuwa hakuna uhalifu uliotokea.

Afisa wa tume ya uchaguzi alipokichukua kinasasauti, kila mtu alitulia tuli kama maji mtungini. Kimya cha makaburini kilitanda kote, hata unywele ungedondoka chini ungesikika kama mlipuko wa bomu katika ukimya huo, afisa huyo alikoroma na kupasua ukimya uliokuwa umetawala. "Mshindi wa uchaguzi huu ni Amani Mlachake". Wote walionipinga waliduwaa kama mja aliyedungwa sindano ya ganzi. Wengine wote waliokuwa wakigombea kiti hicho walidhani kuwa walikuwa katika ndoto mbaya. Rafiki yangu Nyangweso na kundi lake la watumbuizaji walianza kupiga isukuti. Akina mama walisakata densi ya mabega yao. Vijana wenzangu waliniinua juu kwa furaha. Sherehe na shangwe hizo zilifanyika bila kujali mipaka ya ukabila.

Hewaa! Jua la mabadiliko lilikuwa limechomoza. Hiyo ilikuwa siku mpya. Tofauti na hapo awali, uchaguzi wa kiongozi ulikuwa umefanyika bila kuzingatia kuwa mkono mtupu haulambwi. Wale waliodhani kuwa wangechaguliwa madhali walikuwa wakiwarambisha wapigakura asali walinamisha vichwa vyao kwa tahayuri Walikuwa wamekula inwande. Aidha, waliokuwa wakijipiga kifua kuwa kiongozi alichaguliwa kwa kuegemea dhana ya ukubwa wa kabila lake waliinamisha vichwa na kujiendea zao.

Niliutuliza umati uliokuwa umepandwa na jazba. Hamrerehamrere na chereko zilipotulia, nilichukua kinasasauti ili niwashukuru raia walioniunga mkono. "Ninawapa shukrani za dhati kutoka sakafuni pa mtima wangu. Ninawakumbusha kwamba ahadi zote nilizowapa hazikuwa ahadi za Kiswahili. Vilevile, ninawapa shukrani kwa uzalendo wenu. Shughuli za uchaguzi zilifanyika bila fujo wala vurugu. Hata baada ya mshindi kutangazwa, sijaona visa vya uharibifu wa mali kama hapo awali. Nyinyi ni mashujaa na wazalendo kindakindaki."

  1. Kwa mujibu wa aya ya kwanza:
    1. msemaji alishindwa kulala kwa kuwa hakujua kama matokeo ya uchaguzi yangetangazwa
    2. msemaji hakutarajiwa kuwa nambari ya pili bali ya kwanza
    3. watu walitarajia kuwa msemaji angekuwa wa mwisho katika uchaguzi
    4. msemaji alikuwa tajiri aliyetoka katika kabila la watu wachache mno.
  2. Juhudi za msemaji kuwa kiongozi zilikumbwa na changamoto gani hasa?
    1. Umaskini na ukabila
    2. Ufisadi na utepetevu
    3. Utapeli na unyanyapaa
    4. Ukata na utapeli
  3. Nahau zifuatazo zina maana sawa na 'kufumwa na mvi wa manaya' ila 
    1. kukata kamba
    2. kuaga dunia
    3. kuacha mkono
    4. kuenda nguu 
  4. Maneno, hata unywele ungedondoka chini ungesikika kama mlipuko wa bomu ni mfano wa Tani yani ya lugha?
    1. tashbihi
    2. istiara
    3. chuku
    4. tanakali
  5. Matokeo ya uchaguzi yalipotangazwa
    1. kila mtu alifurahia matokeo
    2. kila mtu alienda nyumbani
    3. watu wengi walifurahi lakini wengine hawakuamini
    4. watu wote walimwinua msemaji kwa furaha.
  6. Maneno, hiyo ilikuwa siku mpya' yana maana kwamba ilikuwa siku ya
    1. uchaguzi
    2. mabadiliko
    3. sherehe
    4. matokeo
  7. Kulingana na aya ya nne, ni kweli kuwa
    1. jua lilipochomoza lilileta mabadiliko
    2. uchaguzi huo ulikuwa tofauti na wa siku za awali
    3. watu walishindwa kuulamba mkono mtupu
    4. ushindi wa msemaji ulifanya watu wajipige kifua
  8. Ufahamu huu unatufundisha kwamba:
    1. tusiogope kujaribu jambo hata kama hali ni ngumu
    2. tuheshimu watu wa makabila yetu kushinda wa makabila mengine
    3. tuchague viongozi ambao wana pesa pekee
    4. watu ambao hawana pesa hawawezi wakafaulu katika jambo lolote.
  9. Kwa nini msemaji anawashukuru wapigakura katika aya ya mwisho?
    1. Walimpigia kura vizuri.
    2. Waliungana kusherehekea ushindi wake
    3. Walipiga kura kwa amani bila fujo wala vurugu
    4. Walifanya kazi kwa bidii na umoja 
  10. Kulingana na mwandishi, alipanga kuzingatia methali gani katika aya ya mwisho?
    1. Jitihada haiondoi kudura.
    2. Dau la mnyonge haliendi joshi.
    3. Mkono mtupu haulambwi.
    4. Ahadi ni deni na dawa ya deni ni kulipa

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali 41 mpaka 50.

Ukeketaji ni dhuluma ambayo huendelezwa na baadhi ya jamii humu nchini. Licha ya serikali kujifunga kibwebwe ili kukabiliana na jinamizi hili, bado linatishia kuendelea kuharibu mustakabali wa vijulanga wa kike humu nchini. Kuna viongozi wa kidini hapa nchini ambao huegemea mila na desturi za jadi katika jamii na ambao kisiri huunga mkono ukeketaji, hivyo basi kuhujumu vita dhidi ya ukeketaji. Pia hali ni tofauti kabisa ambapo shughuli hiyo ambayo zamani iliendeshwa kisiri vichakani hasa huko mashinani, leo hii imekuwa ni biashara ya faida na ambapo kuna wauguz ambao hulipwa ili kukeketa katika usiri wa vyumba vya kifahari na pia katika hospitali

Aidha, kuna wakuu wa kiusalama ambao wamethibitisha kuwa wauguzi wengine wamejiunga na wale ambao wamekataa katakata kutupilia mbali tohara ya wanawake katika jamii. Wengi wac wanachochewa na tamaa ya kujipa pato. Hii ni ithibati ya kutosha kuwa umaskini ni mojawapo ya vizingiti vikubwa katika vita dhidi ya ukeketaji. Hata hivyo, si umaskini tu bali pia unyama. Unyama huu unatokana na ukweli kwamba ukeketaji huu una madhara si haba kwa yule anayekeketwa. Kwa hivyo, mtu anayethamini hela anazopewa kushinda maslahi ya mwenzake ni mwovu anayefaa kutiwa mbaroni na kuozea katika jel

Uchunguzi wa hivi karibuni umedhihirisha kuwa idadi kubwa ya wale waliokumbatia ukeketaji huu ama hawajui madhara yake au wanajitia tu hamnazo. Kuna wale ambao kwa kupofushwa na kauli kuwa mwacha mila ni mtumwa, wanajitolea mhanga kiasi cha kuwakeketa hata wasichana ambao wangali tumboni. Ni faradhi kila mkenya afahamu kuwa njia za kitamaduni za ukeketaji zina madhara si haba. Uvujaji wa damu kiasi cha kusababisha kifo ni mojawapo tu ya athari hizo Isitoshe, ngariba alikuwa na mazoea ya kutumia kijembe kimoja kuwapasha wasichana kadhaa tohara. Hali hii ilitokea kuwa rutuba ya kukuza maangamizi.

Ukeketaji wowote ule, uwe wa kale au wa kisasa, humwathiri mhusika kisaikolojia. Dhuluma hii huweza kumfanya mhusika huyo asijichukie tu bali pia jamii nzima iliyochangia kumletea madhila. Baadhi ya wale waliopitia ukatili kama huu, wasiposaidiwa kupona majeraha ya moyoni, huweza kulipiza kisasi kwa wenzao au hata kuishi maisha yaliyosheheni uchungu na maumivu ya ndani kwa ndani.

Ni jukumu la kila mkenya kutathmini faida tunazopata kutokana na mila na desturi zetu. Mila na desturi zisizokuwa na umuhimu wowote zitupiliwe mbali. Ukeketaji una faida gani? Wale waliokeketwa wanawashindia nini wale ambao hawajakeketwa? Tukilipiga suala hili darubini tutang'amua kuwa ukeketaji hauleti faida yoyote. Ni msisitizo utokao kwa wanajamii wanaodai kuwa mwacha mila ni mtumwa. Je, hawajui kuwa mwacha mila potovu ni mtume?

  1. Aya ya kwanza inadokeza kuwa ukeketaji
    1. huendelezwa na jamii zote humu nchini
    2. unatishia kuimeza serikali humu nchini
    3. unaendelea ingawa serikali imekuwa ikijaribu kukabiliana nao
    4. unaunga mkono kisiri viongozi wa kidini.
  2. Makala yanaeleza kuwa ukeketaji siku hizi;
    1. hauna tofauti kubwa na wa hapo awali.
    2. hauendeshwi kabisa huko mashinani na vijijini
    3. ni biashara ambayo inaleta faida kote nchini
    4. hufanywa kisiri hospitalini na katika majumba ya kifahari.
  3. Ni nini hasa kinachowafanya wauguzi wajiunge na shughuli ya ukeketaji? 
    1. Uzalendo
    2. Umaskini
    3. Utamaduni 
    4. Ukale 
  4. Kwa mujibu wa aya ya pili, imebainika kwamba;
    1. tunafaa kuwathamini wenzetu kushinda hela tunazoahidiwa
    2. umaskini ndiyo sababu pekee inayoendeleza ukeketaji
    3. idadi ya wauguzi ambao wanaendeleza ukeketaji inazidi kupungua.
    4. waliopatikana wakiendeleza ukeketaji walitiwa mbaroni na kuozea jela.
  5. Maneno, 'wanajitia tu hamnazo' yana maana gani jinsi yalivyotumika katika kifungu?
    1. Wanajipeleka jela
    2. Wanajifanya kuwa hawajui.
    3. Wanajiletea shida
    4. Wanashirikiana na wakeketaji.
  6. Aya ya tatu inadokeza kuwa madhara ya ukeketaji ni;
    1. kifo na athari za kisaikolojia
    2. ugonjwa wa UKIMWI na athari za kisaikolojia
    3. kifo na kusambaza ugonjwa wa UKIMWI
    4. uvujaji wa damu na madhara ya kisaikolojia 
  7. maumivu ya ndani kwa ndani' ni yale ambayo:
    1. hayana athari zozote
    2. yanaonekana na kila mmoja
    3. hayawezi yakatulizwa
    4. yanamtesa mtu ingawa hayaonekani 
  8. Makala haya yanaeleza kuwa ukeketaji wa kale au wa kisasa;
    1. haumwathiri mhusika kisaikolojia
    2. hufanya mhusika asijichukie
    3. hufanya mhusika ajichukie na pia kuichukia jamii iliyohusika
    4. hulipiza kisasi kwa wenzao.
  9. Ili kukabiliana na ukeketaji, tunafaa
    1. kufunza athari za UKIMWI na kuwatia mbaroni
    2. kuimarisha uchumi na kufunza jamii madhara yake.
    3. kuonyesha jamii madhara na kuondoa umaskini
    4. kufunza jamii madhara ya umaskini na kuimarisha ukeketaji.
  10. Aya ya mwisho inabaini wazi kuwa,
    1. mila zinaweza zikawa na faida na nyingine zina madhara
    2. mila zina madhara pekee
    3. mila hazina faida yoyote
    4. tufuate mila zote za kiafrika

MARKING SCHEME

  1. B
  2. C
  3. A
  4. D
  5. C
  6. C
  7. B
  8. B
  9. A
  10. D
  11. A
  12. A
  13. B
  14. A
  15. D
  16. D
  17. C
  18. D
  19. A
  20. B
  21. B
  22. A
  23. D
  24. A
  25. B
  26. D
  27. C
  28. B
  29. A
  30. A
  31. A
  32. A
  33. D
  34. C
  35. C
  36. B
  37. B
  38. A
  39. C
  40. D
  41. C
  42. D
  43. B
  44. A
  45. B
  46. C
  47. D
  48. C
  49. B
  50. A

 

SEHEMU YA KWANZA:LUGHA
SOMA MAAGIZO HAYA KWA MAKINI 

  1. Umepewa kijikaratasi hiki cha maswali na karatasi ya majibu. Kijikatatasi hiki kina naswali 50. 
  2. Katika karatasi ya majibu hakikisha umeandika:
    1. Jina lako
    2. Jina la shule yako

MASWALI

Kamilisha kifungu hiki kw akujaza nafasi kwa kuchagua kiteuzi kifaacho.
Hati nadhifu ni hati safi. Ni mwandiko _1__ na matatizo_2_. Herufi___3_ hutakiwa kuwa sawa, kuna herufi za kuweka vitone; ni__4_vitone hivyo viwepo. Kama ni herufi_5____kukunjwa chini au jau ya msitari_6__kukunjwa. Baadhi ya herufi huwa na vistari juu, kwa__7_ vistari hivyo hupaswa kuwekwa. Mwandiko unatakiwa uwe__8_wastani __9__ mkubwa sana _10_mdogo sana, usomeke vilivyo. Haifai kuka__11___ au kufutafuta kazi iliyoandikwa. Mwandiko12_unavutia na_13__machoni hata kabla ya mtu kukisoma
__14__kilichoandikwa. Jifunze kuandika_ 15_ 

  1.                    
    1. isiyo
    2. yasiyo 
    3. usio
    4. usiwo
  2.                      
    1. lolote
    2. zozote
    3. yoyote
    4. yeyote
  3.                            
    1. yote
    2. zote
    3. wote
    4. lote
  4.                          
    1. nzuri
    2. vizuri
    3. uzuri
    4. zuri 
  5.                          
    1. za
    2. ya
    3. kwa
    4. kunafaa
  6.                        
    1. linafaa
    2. zinafaa
    3. tunafaa
    4. hilo
  7.                            
    1. hapo 
    2. hiyo
    3. hivyo
    4. kwa
  8.                          
    1. ya
    2. wa
    3. na
    4. isiwe
  9.                        
    1. kusiwe
    2. zisiwe
    3. usiwe 
    4. tena
  10.                        
    1. pengine 
    2. zaidi
    3. au
    4. katakata
  11.                    
    1. takata
    2. kutakasa
    3. takataka
    4. nzuri
  12.                      
    1. zuri
    2. mizuri
    3. mzuri 
    4. kupendeza
  13.                            
    1. kupendwa
    2. kupendesa
    3. kupendea
    4. hiki
  14.                      
    1. hilo 
    2. kile
    3. hiyo
    4. mzuri
  15.                    
    1. bora
    2. viema
    3. vyema
    4. ta

Tegua kitendawili hii:.

  1. Ndege wengi baharini
    1. jua
    2. nyota
    3. gari
    4. meza 
  2. Umbo hili utaliitaje?
    17 ujggu
    1. tufe
    2. maraba
    3. mche
    4. mstatili
  3. Tunasema biwi la simanzi, pia tunasema .................... la moshi. 
    1. wingu
    2. mtungo 
    3. mvuke
    4.  mkuroro
  4. Katika kamusi, neno la tatu litakuwa lipi?
    1. landa
    2. lafudhi
    3. lahani
    4. laiki
  5. Mchele, mawele na wimbi ni nafaka ilhali ng'ombe, mbuzi, kondoo na nguruwe ni
    1. hombwe
    2. ombwe
    3. hongwe
    4. howa
  6. Shuka ni teremka. Shuka pia ni:
    1. kifaa cha kukatia hasa miti 
    2. kitambaa kinachotandikwa kitandani
    3. ndege mkubwa mwenye mbawa za kahawia
    4. mnazi mchanga unaochomoza
  7. Katika uwakifishaji, sauti (') huitwaje? 
    1. kituo
    2. kipumuo
    3. king'ongo 
    4. hisi 
  8. Majina haya ni ya ngeli gani? Maji, mafuta, maisha, manukato
    1. YA-YA
    2. U-ZI
    3. U-YA
    4. MA-MA
  9. Gari la majangili liliegeshwa....................njia.
    1. kando mwa 
    2. kando ya
    3. kando kwa
    4. kando na
  10. Nahau, piga mafarba haina maana ya
    1. kumzandiki mtu
    2. kumlaghai mtu
    3. kumghilibu mtu
    4. kumsema mtu
  11. Mshororo wa tatu katika shairi la tarbia huitwa
    1. mloto
    2. mleo
    3. tathlitha
    4. utao
  12. Wachezaji wanane kwa tisa ndio huitwa
    1. thumuni tisa
    2. tusui nane
    3. thumuni nane
    4. themanini na tisa .
  13. Kanusha sentensi hii
    Akinipiga nitalia
    1. kama hatanipiga sitalia
    2. asiponipiga nitalia
    3. akinipiga sitalia
    4. asiponipiga sitalia 
  14. Ni nomino ipi isiyostahiki katika orodha ifuatayo? 
    1. mtu
    2. mvulana 
    3. daktari
    4. juma 
  15. Kutokana na kitenzi "andika" hatupati nomino
    1. mwandishi
    2. kuandikika 
    3. uandishi
    4. mwandiko

Soma kifungu kifuqtacho kisha ujibu maswali kutoka 31 hadi 40.
Dalili za mvua ni mawingu. Baada ya kiangazi cha miezi tandatu, hatimaye mawingu yalitana angani. Wakulima walijawa na furaha kwa tumaini la kupata afueni ya mazao. Kila mtu alionekana shambani akiwa na jembe mkononi kwa kwamini kuwa achanikaye kwenye mpini hafi njaa.
Hatimaye jioni moja, kiza kiligubika nchi ikawa kama chumba kilichozimwa taa. Kwa ghafla mimweko na mingurumo ya radi ilisikika na kufuatwa na matone mazito yaliyosikika kwenye mapaa ya nyumba kijijini. Watu waliimba nyimbo za kumshukuru. Jalali kwa kuwajaalia mvua pamoja na kutoa dua za kushukuru.
Usiku ule mvua ilinyesha kwa makeke na upepo uliangusha miti na hata kubomoa nyumba zilizokuwa hafifu. Vifijo, hoi na nderemo viligeuka kuwa kwikwi za vilio kwa kupoteza mali na makao.
Mvua iliendelea kunyesha kidindia, siku zikaunda majuma ambayo hayakuchelewa kukomaa na a miezi. Kama kwamba Mungu alifungulia biluli akasahau, mvua ilinyesha kwa miezi takribani
la kupungua. Si wahenga walisema kuwa hakuna kapa isiyokuwa na usubi? Mito ilifurika, barabara zikaharibika, mashamba yakageuka kuwa vinamasoi huku watu wengi wakikosa makao.
Hewaa! Baada ya kisa mkasa. Ati hakuna msiba usiokuwa na mwenziwe. Katika hali ya sitaifahamu, mvua ilisababisha mlipuko wa maradhi mbalimbali. Wenye kipindupindu walitibiwa huku waliokuwa na homa ya matumbo wakipewa ushauri na walioumwa na mbu wakishughulikiwa kunako zahanati za muda. Hali hii haikukoma hata baada ya miezi minane mvua ilipopusa.
Si wenye ndimi za kihenga waliamba kuwa aisifuye mvua imemnyea?

  1. Kiangazi cha miezi tandatu ndicho kipi?
    1. Miezi ya kutanda kwa mawingu 
    2. Miezi sita 
    3. Miezi ya kutanda mvua
    4. Miezi saba 
  2. Mvua inayozungumziwa iliwapa nini wakulima?
    1. ukosefu wa sehemu za kujisetiri 
    2. wasiwasi wa kupoteza makao yao 
    3. wahaka kuhusu mafuriko
    4.  tumaini na afueni ya mazao
  3. Mbona mwandishi anamithilisha dunia na chumba kilichozimwa taa? 
    1. ilivyokuwa anga baada ya mawingu kutanda 
    2. ilivyokuwa hali baada ya umeme kupotea
    3. baada ya upepo mkali kuzizima taa vyumbani
    4.  baada ya vyumba kukosa mwangaza 
  4. Kwa mujibu wa aya ya pili, ni kipi kilichokuwa cha mwisho?
    1. Matone ya mvua 
    2. mingurumo ya radi
    3. mimweko ya umeme
    4. giza kufunika nchi 
  5. Iliponyesha mvua usiku wa kwanza, watu walifanya yote ila
    1. kushukuru 
    2. kukashifu
    3. kupiga dua 
    4. kushangilia
  6. Mvua inayonyesha kidindia ndiyo inayonyesha vipi?
    1. kwa wingi 
    2. bila kukoma 
    3. bila baridi
    4. na upepo mkali 
  7. Mvua inayosemwa ilinyesha kwa muda gani?
    1. Thuluthi mbili za mwaka 
    2. Thumni mbili za mwaka
    3. Robo tatu za maka
    4. Sudusi tatu za mwaka 
  8. Kwa mujibu wa aya ya nne, ni mambo mangapi ambayo yalitokea? 
    1. Matatu
    2. Manne 
    3. Matano
    4.  Mengi
  9.  Kulingana na kifungu maradhi yaliyozuka hayakuwa pamoja na? 
    1. Malaria . 
    2. Kichocho 
    3. Waba
    4. Homa ya matumbo 
  10. Kipe kifungu hiki kichwa mwafaka
    1. Maji ni uhai 
    2. Na ije baa iondoke baa 
    3. Hakuna kapa isiyokuwa na usubi
    4. Aisifuye mvua imemnyea

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali kutoka 41 hadi 50.
Kungutu aliugud maradhi mabaya kwa muda mrefu. Alikonda sana. Hakuwa na nguvu za kutafuta chakula. Njaa ilimuuma si haba. Hakujua jinsi ya kutafuta chakula kwani ubongo wake haungefikiria vizuri.
Nyumbani kwake kulikuwa na nyasi nyingi sana ndefu. Huko kulijaa panzi lakini kunguru nangeweza kuwadona kwa sababu walitoroka. Panzi walimcheka kunguru mnyonge kwalkwa!kwa! kunguru alipokuwa akitembea siku moja aliwaona panzi wawili wakipigana kufa na kupona. Baadaye waliaga dunia, baada ya kuumizana na kupata majeraha mabaya sana.
Kunguru alitoka pahali alikuwa na kuwadona. Aliwala, walikuwa watamu ajabu. Alijaribu kutafuta panzi wengine waliokuwa wamekufa kwa sababu hakushiba. Hakufanikiwa hata kidogo.
Aliamua kuwachochea panzi, alitumia panzi moja mlafi kwa kumdanganya ati alikulia nyasi mbovu ilk Ji wengine walikuwa nyasi nzuri. Panzi mlafi alienda na akaanza kutoa fujo kwa panzi wengine. Vita vilizuka baina ya panzi. Kunguru alikuwa mbali akicheka na kusema, "Wajinga ndio waliwao."
Panzi wengi walikufa sana kutokana na vita vile, karibu wamalizane. Kunguru alizidi kuchochea panzi kuuana aijifanya rafiki aliyekuwa na hofu zaidi. Baada ya panzi wengi kufa, waliamua kumaliza vita ili wasimalizane. Baada ya vita, kunguru alionekana akiwala mizogo wa panzi waliokufa kwa furaha sana. Panzi walipoona hivyo walijua kunguru ni mwongo.

  1. Kunguru alikonda kwa nini .
    1. aliugua muda mrefu 
    2. hakutaka kula 
    3. hakuwa na hamu ya kula
    4. hakukuwa na panzi 
  2. Kwa nini kunguru hakujua jinsi ya kupata chakula? 
    1. Aliatafuta panzi 
    2. Alikuwa peke yake
    3. Ubongo wake haungefikiria vizuri
    4.  Panzi hawakufa
  3. Kwa nini kunguru alitamani kuwala panzi wengine
    1. Panzi walikufa zaidi 
    2. Ni watamu sana
    3. Hakushiba
    4. Ili awe na nguvu 
  4. Kunguru alipowatafuta panzi wengine
    1. hakuwapata 
    2. aliwapata 
    3. alichoka
    4. walitoroka
  5. Kisawe cha neno maradhi ni 
    1. ugonjwa
    2. afya 
    3. njaa
    4. unyonge
  6. Kusema vita vilizuka ni kusema kwamba
    1. vita viliendelea 
    2. vita vilianza
    3. vita vilikoma
    4. vita vilimalizwa 
  7. Mnyama akiaga huitwa mzoga, je binadamu akiaga huitwa? 
    1. Mzoga
    2. Mtu 
    3. Maiti
    4. Jeneza 
  8. Kunguru alitumia mbinu gani kupata chakula? 
    1. Kutafuta panzi waliokufa
    2. Alichochea vita kwa panzi 
    3. Alienda hospitalini
    4. Aliwinda panzi na akala nyasi
  9. Panzi waliamua kumaliza vita wakati gani?
    1. Walipochoka kupiga 
    2. kunguru alipowacheka 
    3. walipouana sana .
    4. walipojua ulikuwa uwongo wa kunguru
  10. Kichwa kifaacho habari hii ni
    1. vita vya panzi furaha ya kunguru 
    2. Uongo wa kunguru 
    3. panzi watamu 
    4. kunguru mgonjwa

MEALEKEZO YA KUSAHISHA

swa ms

INSHA

Endeleza insha hii:
Asubuhi hiyo siku ya jumatatu tulipokuwa gwarideni, mwalimu mkuu.....................................................

INSHA MEALEKEZO YA KUSAHISHA

MARKING CRITERION
The composition will be assessed according to the following general guidelines.

  • The maximuin mark will be 40 and the minimum mark 01.
  • Does the script show that the candidate can communicate accurately, fluently and imaginatively in English?

Accurency (16 marks)

  1. Correct tenses and agreement of verbs (4 marks)
  2. Accurate use of vocabulary (4 marks) 
  3. Following a sequence (4 marks)
  4. Correct punctuation (4 marks)

Fluency (16 marks)

  1. Words in correct order (4 marks)
  2. Sentence connection and paragraphs (4 marks)
  3. Correct spellings (4 marks)
  4. Ideas developed in logic sequence (4 marks)

Imagination (8 marks)

  1. Unusual but appropriate use of words and phrases (4 marks) 
  2. Variety of structure (4 marks)
    NB: Please, teachers are requested to scrutinize this marking scheme before use, its worthy.

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi, umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.

Ili kuwa na jamii ___1___kila mmoja wetu anahitajika___2___, ___3___mstari wa mbele katika kuzungumza tu___4___ pia katika matendo yetu. Inaeleweka na kila mtu kuwa___5___ya mja hunena muungwana ni vitendo. Ni___6___letu kuhakikisha kuwa jamii yetu___7___. Hili linawezekana tu iwapo tutakuwa___8___katika kila tulitendalo. Kwa mfano, hatuwezi tukatarajia kuwa na jamii yenye bidii iwapo sisi ndisi___9___ Hilo haliwezekani.

  1.  
    1. thabiti
    2. dhabiti
    3. mathubuti
    4. dhaifu
  2.  
    1. kutolewa
    2. kujitoa
    3. kujitia
    4. kujitolea
  3.  
    1. Usiwe
    2. Tuwe
    3. Mwe
    4. Tusiwe
  4.  
    1. ingawa
    2. bali
    3. lakini
    4. mbali
  5.  
    1. afua
    2. desturi
    3. ada
    4. kawaida
  6.  
    1.  toleo
    2.  wajib
    3.  dhima
    4. jukumu
  7.  
    1.  imeidilika
    2. imeadilika
    3.  imebaidilika
    4. imebainika
  8.  
    1. vielelezo
    2. tegemeo
    3. vielezo
    4. vigezo
  9.  
    1. tunaolaza damu
    2.  tunaokufa kikondoo
    3. tunaopiga moyo konde
    4. tunaojitolea mhanga

Baada ya___10___ na darasa la nane, niliamua kudurusu zaidi ili nifaulu. Sikutaka kuvuta mkia ___11___, ___12___kuhusu aina___13___maneno kama vile nomino, vitenzi na vielezi ambavyo pia huitwa ___14___ . Kuna vielezi vingi___15___ polepole, upesi, nyumbani na sokoni.

  1.  
    1. kuungana
    2. kuunganishwa
    3. kujiunga
    4. kuunga
  2.  
    1. tena
    2. asilani
    3. yamkini
    4. angalau
  3.  
    1. Nimesoma
    2. Ninasoma
    3. Nilisoma
    4. Ningesoma
  4.  
    1. ya
    2. wa
    3. na
    4. za
  5.  
    1. viigizi 
    2. viarifa
    3. visifa
    4. viingizi
  6.  
    1. :
    2. ;
    3. -
    4. ,

Kutoka swali la 16 - 30, chagua jibu sahihi kulingana na maagizo.

  1. Chagua ukanusho wa: Mgeni aliyewasili ana kofia.
    1. Mgeni asiyewasili ana kofia.
    2. Mgeni asiyewasili hana kofia. 
    3. Mgeni aliyewasili huna kofia. 
    4. Mgeni aliyewasili hana kofia.
  2. Tambua sentensi iliyo na kivumishi cha idadi katika orodha.
    1. Barabara zote zimejaa magari.
    2. Miti mingi imepandwa na wanafunzi.
    3. Mwalimu amesahihisha insha mbili.
    4. Kitabu hiki ni cha mwanafunzi wa pili.
  3. Tambua matumizi ya 'ki' katika sentensi.
    Mpishi yule alipika akiimba.
    1. Kuonyesha vitenzi sambamba.
    2. Kuonyesha hali endelezi.
    3. Kuonyesha kufuatana kwa vitendo. 
    4. Kuonyesha hali ya masharti.
  4. Sentensi ipi iliyo katika hali ya mazoea kati ya hizi?
    1. Wewe hukufika mapema tulivyoelewana.
    2. Mtoto atikaye shuleni mapema ndiye huyu.
    3. Alitembea huku ameangalia.
    4. Hungesoma kwa bidii hungefaulu.
  5. maji, chai, uji' ni mfano ya nomino za aina gani?
    1. Nomino za hali
    2. Nomino za wingi 
    3. Nominoambata
    4. nomino za jamii.
  6. Tambua nomino ambayo haijalinganishwa kwa usahihi na ngeli.
    1. moyo - U - ZI, U-I 
    2. kipepeo - KI-VI, A - WA
    3. ua - LI-YA, U - ZI
    4. moto - U-T; U-U
  7. Chagua maelezo ambayo ni sahihi.
    1. Kitengele ni kiungo cha mkono kati ya kiwiko na bega. 
    2. Kwapa ni kiungo cha mwili kilicho juu ya bega. 
    3. Nyongo ni kiungo cha mwili kinachopatikana juu ya kiuno.
    4. Goko ni mfupa wa mbele unaotoka kwenye kifundo cha mguu mpaka kwenye goti.
  8. Orodha ipi ambayo ni ya vihusishi pekee?
    1. langu, vyao, zake
    2. kabla ya, juu ya, baada ya
    3. licha ya, fauka ya, minghairi ya 
    4. ala, ebo, afanalek
  9. .'a, e, i, o, u' ni mifano ya
    1. konsonanti
    2. silabi funge 
    3. vokali
    4. sautighuna.
  10. Teua umoja wa: Vita huharibu maendeleo ya mataifa.
    1. Vita huharibu maendeleo ya taifa 
    2. Kita huharibu maendeleo ya taifa 
    3. Vita huharibu endeleo la taifa 
    4. Kita huharibu maendeleo la taifa.
  11. Jibu lipi ambalo halijalinganishwa kwa usahihi? 
    1. fuma - fumua 
    2. chimba - chimbua
    3. pakia - pakua
    4. funga - fungua
  12. Maamkizi gani yatumikayo wakati uliotofauti na mengine?
    1. Sabalheri
    2. Chewa
    3. Umeamkaje 
    4. Umeshindaje
  13. Tambua sentensi iliyotumia kiunganishi kwa usahihi.
    1. Nipe aghalabu shilingi hamsini ninunulie kitabu.
    2. Umeshindwa kuandika aya moja sembuse insha nzima. 
    3. Mathalani umewasili, tutaanza safari.
    4. Bighairi ya kumnunulia nguo, pia alimnunulia kalamu.
  14. Jibu lipi lenye kitenzi kilichoundwa kutokana na sifa? 
    1. cheka - mcheshi 
    2. mwalimu - funza
    3. vumilivu - vumilia
    4. mjuzi - ujuzi.
  15. Mtoto ni kwa binadamu kama vile __________ ni kwa ndege.
    1. kinda 
    2. kifaranga 
    3. kiota 
    4. kizimba

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali 31-40.

Siku moja, mume na mke wakiwa wamekaa pamoja, mume alimwambia mke wake, "Mke wangu nimewakumbuka sana ndugu zangu (kaka zangu, dada zangu na hata baba na mama) tujumuike pamoja na kula pamoja. Kesho nitawaalika ili tufurahie nao katika chakula cha mchana, itabidi uandae chakula kwa ajili yao."

Mke alijibu kwa unyonge, “Sawa, Mungu akipenda."

Asubuhi ya siku iliyofuata, mume alitoka kwenda katika shughuli yake lakini baada ya saa kadhaa alirejea nyumbani. Alimsaili mke wake, “Mke wangu, umeandaa chakula cha mchna kwa ajili ya wageni? Baada ya saa moja watakuwa wameshafika." Mke alijibu, "La. Sijapika madhali ndugu zako sio wageni hapa. Watakula chochote wakipatacho." Mumewe alimwambia kuwa Mungu amsamehe. Alitaka kujua kwa nini mkewe aliyasema hayo ilhali alikuwa amemweleza kuhusu wageni tangu siku iliyotangulia. Aliuliza kwa nini mke wake hakumwambia kuwa asingepika ilihali wazazi wake wangewasili baada ya muda mfupi.

Basi mume ilimbidi aondoke pale nyumbani ili aibu isimfunike na kumzamisha. Baada ya dakika kadhaa, mlano ulibishwa. Mke alienda kuufubgua mlango. Alipigwa na butwaa alipokuta kuwa wageni waliokuja ni wazazi wake: baba yale, mama yake, dada zake pamoja na kaka zake. Alishtuka nusura azimie. Hata hivyo, aliwakaribisha ndani.

Baba yake alimwuliza alikokuwa mume wake. Mke alimjibu kwamba alikuwa ametoka dakika chache zilizopita. Baba alimwambia "Mumeo jana alitupa taarifa kuwa leo anatualika hapa tuje kula pamoja chakula cha mchana. Sasa vipi yeye ameondoka? Tendo hili si la busara." Mwanamke yule alishangaa kwa taarifa hiyo. Alianza kufikicha mikono yake huku akipigapiga mguu chini kwa kuchanganyikiwa. Ilimbidi aingie ndani na kumpigia mume wake simu. Alimwambia, "Kwa nini hukuniambia kuwa wazazi wangu ndio wanaokuja?"

Mume alimjibu, "Wazazi wangu na wazazi wako wote ni kitu kimoja, hawana tofauti."

Mke alimwambia mumewe, “Leta chakula huku. Chakula kilichokuwepo ni kichache. Hakitawatosheleza."

Mume alimjibu, "Mimi nipo mbali na hao si wageni. Watakula chochote kilichopo namna wewe ulivyokuwa ukitaka kuwalisha wazazi wangu." Mke alibabaika sana. Mikono yake ilitetemeka huku akimwomba mumewe msamaha. Aliwaelezea wazazi wake yote yaliyojiri. Nao waliamuru kuwa wazazi wa mume watafutiwe siku ya kuwatembelea wana wao ili waandaliwe mlo.

  1. Kulingana na aya ya kwanza, mume
    1. alikumbushwa kuhusu ndugu zake na mkewe. 
    2. alijua kuwa mke angekataa kuwahudumia wageni. 
    3. alinuia kuwatendea wema wakwe wake. 
    4. alimwekea mkewe mtego ili amnase.
  2. Maneno yaliyosemwa na mke, “Sawa,Mungu akipenda", yanaonyesha
    1. udhaifu wa mke
    2. kutojali kwa mke 
    3. jinsi mke alivyomtegemea Mungu 
    4. uaminifu wa mke.
  3. Makala haya yamendhihirisha mke kuwa
    1. mwenye tamaa, katili 
    2. mkakamavu, goigoi 
    3. mwenda nguu, mchoyo 
    4. mbinafsi, kaidi
  4. Methali gani isiyoweza kumrejelea mke katika makala haya?
    1. Ndugu ni kufaana si kufanana.
    2. Mkuki mtamu kwa nguruwe kwa binadamu uchungu:
    3. Mchimba kisima huingia mwenyewe.
    4. Kila mwamba ngoma, ngozi huivuta kwake.
  5. Maneno 'itabidi uandae chakula' yanatoa maana zifuatazo isipokuwa
    1. una hiari ya kuandaa chakula 
    2. ni lazima uandae chakula 
    3. huna budi kuandaa chakula 
    4. ni faradhi uandae chakula.
  6. .... aibu isimfunike na kumzamisha' yametumia fani gani ya lugha?
    1. Chuku
    2. Istiara 
    3. Tashhisi 
    4. Kinaya
  7. Hali ya mke kupata kwamba wageni waliokuja walikuwa ni wazazi wake badala ya wazazi wa mume inaweza ikaelezewa kwa nahau ipi? Mke
    1. alikula mwande
    2. alikula mwata 
    3. alikula muku 
    4. alikula mori
  8. Makala haya yameonyesha kuwa mume
    1. aliwahusudu wazazi wa mkewe
    2. aliwastahi wazazi wa mkewe
    3. aliwahadaa wazazi wa mkewe
    4. aliwadhalilisha wazazi wa mkewe.
  9. Neno 'alimsaili' lina maana gani jinsi lilivyotumika katika kifungu?
    1. Alishangazwa
    2. Alimwuliza 
    3. Alimtuliza 
    4. Alimwagiza
  10. Kwa mujibu wa aya ya mwisho, si kweli kuwa
    1. huenda mume hakuwa mbali ila alikasirishwa na tabia ya mkewe. 
    2. mume alikuwa amegundua kuwa wazazi wa mkewe hawakuwa wageni pale nyumbani.
    3. mke alitetemeka kuonyesha kujutia yale aliyoyatenda. 
    4. mume alimwelewa mkewe na kumpa nafasi nyingine.

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali 41 - 50.

Wakenya zaidi ya elfu kumi na tano walihusika katika ajali za barabarani mwaka jana. Kati yao elfu tatu na mia nne walifariki huku wengine zaidi ya elfu sita mia sita wakipata majeraha mabaya. Jambo la kuhuzunisha mno. Hata hivyo, imebainika kuwa huenda magari yaliua watu wengi zaidi mwaka jana kuliko idadi hiyo iliyotolewa na Mamlaka ya Usalama wa Barabarani. Utafiti umekuwa ukifanywa kila uchao. Wanasayansi sasa wanasema kuwa moshi unaotolewa na magari yanayotumia mafuta ya dizeli huenda unachangia katika ongezeko la vifo vinavyosababishwa na hora ya mapofu (nimonia).

Watafiti kutoka chuo kikuu kimoja walibaini kwamba hewa iliyochafuliwa na moshi wa mafuta ya dizeli inaweka watu katika hatari ya kupatwa na maradhi ambayo ni hatari ya nimonia. Aidha, utafiti huo unasema kuwa watu wanaopumua hewa iliyo na moshi wa mafuta ya dizeli wanakuwa na uwezekano mkubwa wa kupatwa na nimonia ambayo husababishwa na bakhteria wanaojulikana kama 'Streptococcus pneumonia.

Bakhteria hao ndio husababisha maradhi ya nimonia na homa ya uti wa mgongo. Magonjwa haya huchangia kwa kiasi kikubwa vifo vya watoto wachanga walio chini ya miaka mitano. Kadhalika, husababisha vifo vya maelfu ya watu wazima kote duniani. Takwimu zilizotolewa zinaonyesha kuwa tangu mwaka wa elfu mbili kumi na tano, maradhi ya nimonia yamekuwa yakiongoza kwa kusababisha idadi kubwa ya vifo humu nchini. Licha ya hayo, kulingana na ripoti kuhusu hali ya kiuchumi ya mwaka wa elfu mbili, kumi na nane iliyotolewa na Shirika la Takwimu Nchini, waliouawa na maradhi ya nimonia ni karibu mara nne kuliko waliofariki kutokana na ukimwi.

Ugonjwa wa nimonia uliua watu elfu ishirini na moja, mia mbili tisini na watano na elfu ishirini na mbili, mia nne sabini na watatu katika mwaka wa elfu mbili kumi na sita na elfu mbili kumi na tano mtawalio. Ni wazi kama mchana kuwa magonjwa mengine yaliyoangamiza idadi kubwa mwaka wa elfu mbili kumi na saba ni malaria ulioua watu elfu kumi na saba, mia tano hamsini na watu elfu kumi na sita, mia tisa hamsini na watatu.

Mnamo mwaka wa elfu mbili na kumi na nane, watu milioni moja na elfu mia nne walienda hospitalini kutibiwa nimonia na mwaka uliotangulia wa elfu mbili, kumi na saba, watu milioni moja na elfu kumi na saba. Watu milioni moja na elfu mia mbili waliitafuta matibabu ya nimonia katika hospitali kote nchini. Takwimu za wizara ya afya zinaoonyeha kuwa watoto elfu mia saba hutibiwa maradhi ya nimonia kila mwaka. Licha ya takwimu hizo zilizotelewa, jambo la kusikitisha ni kwamba karibu asilimia ishirini na tano hufariki kwa sababu huchelewa kupelekwa hospitalini wanapougua maradhi hayo.

Ripoti iliyotolewa na shirika moja lisilo la serikali mnamo mwaka wa elfu mbili kumi na saba, ilionyesha kuwa vipimo visivyotoa matokeo sahihi na uhaba wa dawa za kukabiliana na bakhteria ni miongoni mwa sabab zinazochangia katika ongezeko la vifo vinavyotokana na nimonia. Wanasayansi waliohojiwa walisema kuwa ugonjwa huo ukigunduliwa mapema unatibika kwa dawa inayouzwa kwa shilingi mia mbili. Isitoshe chanjo ya kukabiliana na maradhi ya nimonia ilianza kutumika humu nchini mnamo mwaka wa elfu mbili, kumi na moja kwa watoto wa kati ya umri wa wiki sita na kumi na nne.

Lakini takwimu zilionyesha kuwa zaidi ya watoto elfu mia nne na kumi na nane wa umri wa miczi kumi na miwili na ishirini na mitatu hawakupewa chanjo hiyo mnamo mwaka wa elfu mbilli kumi na saba. Vifo vilivyotokana na nimonia huenda vikaendelea kushuhudiwa humu nchini kwani takwimu zinaonyesha kuwa kiwango cha mafuta ya dizeli yanayotumiwa humu nchini kinaongezeka kila mwaka.

  1. Kulingana na aya ya kwanza, imebainika kuwa
    1. wakenya takriban elfu kumi na tano walihusika katika ajali za barabarani mwaka jana.
    2. wakenya zaidi ya elfu kumi na tano walihusika katika ajali mwaka jana. 
    3. wakenya zaidi ya elfu sita na mia sita walijeruhiwa katika ajali za barabarani mwaka jana.
    4. utafiti umekuwa ukifanyika kila uchao ili kutambua idadi ya walioumia katika ajali ya barabarani.
  2. Ni kweli kuwa moshi unaotolewa na magari yanatumia mafuta ya dizeli.
    1. umechangia katika ongezeko la ajali barabarani.
    2. umeongeza maambukizi ya nimonia.
    3. yanawezekana kuwa umechangia katika ongezeko la vifo visababishwaVyo na nimonia. 
    4. umechangiwa na kukithiri kwa vifo vya homa ya mapafu.
  3. Neno 'walifariki' halimaanishi kuwa
    1. waliaga dunia 
    2. walienda na ulele ngoma
    3. walifumwa na mvi wa manaya 
    4. walienda nguu.
  4. Kifungu kimedhihirisha kuwa vifo vya watoto
    1. wachanga kwa kiasi kikubwa husababishwa na homa ya mapafu na homa ya uti wa mgongo. 
    2. wachanga walio chini ya miaka mitano husababisha maambukizi ya nimonia.
    3. wachanga walio juu ya miaka mitano husababishwa na nimonia na homa ya uti wa mgongo.
    4. wachanga na watu wazima walio chini ya miaka mitano husababishwa na nimonia na homa ya uti wa mgongo.
  5. Maneno ni wazi kama mchana' yametumia fani gani ya lugha?
    1. Nahau 
    2. Chuku
    3. Tashbihi
    4. Tasfida
  6. Makala yameeleza kuwa watu waliouawa mwaka wa elfu mbili kumi na tano kutokana na nimonia ni 
    1. 21295 
    2. 22473 
    3. 17553 
    4. 16953
  7. . ... asilimia ishirini na tano hufariki kwa sababu huchelewa kupelekwa hospitalii...' kauli hii inaweza ikaelezwa kwa methali ipi? 
    1. Simba mwenda pole ndiye mla nyama. 
    2. Fisi akimla muwele mzima funga mlango. 
    3. Kifo cha wengi harusi.
    4. Akutanguliaye chanoni hukuzidi tonge.
  8. Kulingana na aya ya sita, ni kweli kuwa
    1. ongezeko la vifo vinavyotokana na nimonia husababishwa na ukosefu wa damu za kukabiliana na bakhteria. 
    2. ukosefu wa dawa na vipimo visivyotoa matokeo ni sababu zinazochangia ongezeko la vifo vya nimonia.
    3. upungufu wa dawa na vipimo visivyotoa matokeo sahihi na sababu zingine huchangia ongezeko la vifo vitokanavyo na nimonia.
    4. vifo vinavyotokana na nimonia huchangia uhaba wa dawa na vipimo duni.
  9. Ongezeko la matumizi ya mafuta ya dizeli
    1. litaongeza matumizi ya magari 
    2. linaweza likaongeza vifo vinavyotokana na nimonia 
    3. limesababishwa na maambukizi mengi ya ugonjwa wa nimonia.
    4. limechangia kutokea kwa ajali nyingi za barabarani.
  10. Ili kupunguza vifo vinavyotokana na maambukizi ya nimonia 
    1. tunafaa kubuni vifaa vinavyotoa matokeo sahihi.
    2. tunafaa kutafuta mikakati kabambe ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa nimonia. 
    3. tunafaa kutafuta dawa za kutosha ili kutibu ugonjwa wa nimonia.
    4. tunafaa kuimarisha usafiri ili wagonjwa wafikishwe hospitalini mapema.

MARKING SCHEME

  1. A
  2. D
  3. D
  4. B
  5. C
  6. D
  7. B
  8. A
  9. A
  10. C
  11. B
  12. C
  13. D
  14. D
  15. A
  16. D
  17. D
  18. A
  19. B
  20. B
  21. D
  22. D
  23. B
  24. C
  25. D
  26. B
  27. D
  28. B
  29. C
  30. A
  31. C
  32. B
  33. D
  34. A
  35. A
  36. A
  37. A
  38. B
  39. B
  40. B
  41. C
  42. C
  43. D
  44. A
  45. C
  46. B
  47. D
  48. C
  49. B
  50. B
Thursday, 16 September 2021 06:44

Insha - Class 7 Kiswahili Revision Notes

Insha ya Masimulizi

Insha hii huwa na hisi mbili: furaha na huzuni

Vinaweza visa vya kubuni au halisi

Mtahiniwa aweza kutahiniwa mara tatu

Mwanzo wa handithi – dokezo
Huhitajika aendeleze
Kimalizio/tamati

Mtahiniwa lazima aane insha na atamatishe kwa kutumia kimalizio hicho

Huzuni au Tanzia

Visawe vya huzuni ni masikitiko, majonzi, jitimai, buka, chonda na msiba

Hivi ni visa vinanyoleta majonzi, huzuni, simanzi, sikitiko au jitimai

  • Mikondo
  • Ujambazi/unyang’anyi/uporaji/wizi
  • Utekajinyara
  • Ujangili
  • Wizi wa mifugo
  • Ulaghai
  • Magendo
  • Ugomvi wa kijamii
  • Uvamizi na watu katili
  • Migomo

Misamiati na mapambo

  • Mayowe – ukemi, usiahi, mayowe
  • Wasiwasi- jekejeke, jakamoyo, kiherehere
  • Kufa – kata kamba, enda ahera, jongomeo
  • Hasira – pandwa na mori, kuwa na tumbo joto, kama zaibaki kwenye kipimajoto
  • Nilinyapianyapia/nilinyatianyatia nyatunyatu
  • Joho la kiwewe lilinivaa
  • Nilichana mbuga/nilitifua vumbi ili kuyaokoa maish -
  • Moyo ulinidwikadwika/ulinipapa kama ngoma za mahepe
  • Malaika yalinisimama wima
  • Tulisikia sauti zilizotweta kama
  • Sikuyaamini macho nilipoona
  • Nilipiga usiahi ambao ungewafufua wafu
  • Ulimi uliniganda kinywani
  • Nililia kwa kite na imani lakini kilio si dawa
  • Nilitoka shoti kama
  • Ngeu ilimtiririka kama
  • Milio ya risasi ilitamalaki kwenye anga
  • Parafujo za miguu ziliregea
  • Macho yalinitoka pima kama
  • Nilitetemeka kama unyasi nyikanu
  • Kijasho chembamba kikaanza kunitoka

Methali

  • Mbwa hafi maji akiona ukoko
  • Damu ni nzito kuliko maji
  • Tama mbele mauti nyuma
  • Unjanja wa nyani huishia jagwani
  • Siku za mwizi ni arubaini
  • Pwagu hupata pwaguzi

Ragba

  • Juhudi ziligonga mwaba
  • Maisha yalianza kuingia ufa
  • Jaribu kwa udi na uvumba
  • Sijui alipandwa na pepo gani
  • Mambo yalimwendea tege/upogo upogo
  • Alitoka na michirizi ya damu
  • Alipigwa kitutu/kipopo

Dekeza

  • Alifunzwa na ulimwengu usiokuwa na huruma
  • Huruma zake ziligeuka kama umande
  • Alilia kilio cha kite na shake bila kufahamu kilio si dawa
  • Alivamiwa vaa bin vu

Takriri

  • Haambiliki hasemezeki
  • Hana hanani
  • Hazindishi hapunguzi
  • Hapiki hapakui
  • Jando wala togo

Insha ya Mikasa

Mikasa ni matukio yaletayo maafa, masaibu na matatizo kwa watu
Visawe

  • Msiba
  • Balaa
  • Zani
  • Baa
  • Maafa
  • Janga
  • Belua

Mifano ya mikasa

  • Moto
  • Wizi
  • Ajali barabarani
  • Ugaidi
  • Ubakaji
  • Utekaji nyara
  • Zilizala
  • Kuza maji
  • Maporomoko ya ardhi
  • Mlipuko wa bomu
  • Ukame
  • Kabobo

Jinsi yakujadili

  • Eleza mahali pa mkasa
  • Jinsi tukio lilivyotukia
  • Wakati
  • Msaada uliotoa
  • Maafa/hasara
  • Utafiti
  • Changamoto
  • Mkasa wa moto

Mada

  • KIFO KICHUNGU
  • JEHANAMU DUNIANI
  • NDIMI ZA JEHANAMU
  • MOTO WA KUTISHA
  • NDIMI ZA MANAYA/MAUTI
  • NARI YA KUTISHA

Msamiati

  • Ndimi za moto
  • Jiko lililolipuka laweza kuwa gesi, umeme , mbomba la mafuta.tangi la mafuta
  • Mavundo ya moshi yalifuka
  • Mashungi ya moto
  • Cheche za moto
  • Moto ulitatarika an kurindima
  • Upepo ulivuma kwa ghamidha na ghadhabu
  • Matagaa na mapogoo mabichi
  • Kujitoma ndani ya nyumba kama mwehu
  • Nahodha hodari haogopi mawimbi
  • Moto ulifakamia majengo kama nzige wavamiavyo shamaba la mihogo
  • Wengine walichomeka kiwango cha kutotambulikavilio vilinywewa na kuwapwetea
  • Nilifadhaika kwa fadhaa na wahaka
  • Kichwa kilinizunguka kama tiara
  • Vilio vya ving’ora vya makarandinga na ambulensi vilitanda na kuhinikiza hewa
  • Uma uliuputa moto na kuwaokoa manusura
  • Tulitoa huduma za kwanza
  • Wengi walisali/kufanya dua zisizoeleweka

Msamiati mwingine

  • Nilibaki kinywa wazi
  • Machozi ya majonzi yalinilengalenga
  • Machozi yalinienda njia mbilimbili
  • Lia kwikwikwi
  • Nilifikiri macho yangu yalikuwa yakinchezea shere
  • Choka hoi bin tiki
  • Fafanua kinaga ubaga
  • Pigwa na butwaa
  • Nilibung’aa na kuduwaa waa
  • Ponea chupuchupu

Ragba

  • Alipovunja ungo alianza kuwa na mienendo benibeni
  • Mambo yalimwendea upogo/tenge/msobemsobe
  • Alitokwa ma michirizi ya damu ______________ baada ya kupigwa kipopo/kitutu
  • Kijasho chembamba kilianza kumtoka
  • Aliondoka kichwa kifuani kama kondoo /shikwa na zabaiki ya uso, tayarini/haya/soni
  • Uzuri wake ulimteka bakunja akawa haoni hasikii
  • Akasahau penye urembo ndipo penye ulimbo
  • Aliyatemea mawaidha/nasaha mate
  • Alikuwa hayawani kwenye ngozi ya binadamu
  • Ama kweli _____________
  • Dekeza/engaenga kama yai
  • Alifunzwa na ulimwengu usiokuwa na huruma
  • Huruma zake ziligeuka kama umande
  • Alilia kilio cha kite na shaka bila kufahamu kuwa kilio si dawa
  • Alikuwa ndumakuwili kikulacho ki nguono mwako
  • Husuda/wivu zilimzidi hadi akakosa utulivu
  • Alivamiwa ghafla bin vuu

Methali

  • Maji hufuata mkondo
  • Bendera ikipepea sana huraruka
  • Mpiga ngumi ukuta huumia mwenyewe
  • Mpiga mbizi kwenye nchi kavuhuchunue usoni
  • Pwagu hupata pwaguzi
  • Mchimba kisima huingia mwenyewe
  • Vyote ving’aavyo si dhahabu
  • Vyote viowevu si maji
  • Njia ya mhini na mhiniwa ni moja

Takriri

  • Haambiliki hasemezeki
  • Hana hanani
  • Hazidishi hapunguzi
  • Hapiki hapakui
  • Jando wala togo
  • Vihusishi
  • Lahaula!
  • Yarabi!
  • masalaale!
  • Lo!
  • Lakwata!
  • Usaindizi
  • Walitupiga njeki
  • Niliwatupia upondo
  • Niliwapa mkono
  • Tulisaidiana kama kiko na dagali, maiti na jeneza

Tamati

  • Hakika, hakuna msiba usiokuwa na mwenziwe
  • Daima dawamu sitalisahau tukio hilo
  • Matukio hayo hayatafutika kutoka tafakirini mwangu
  • Ninapokumbuka kisa hicho, machozi hunitiririka njia mbilimbili

Hisia za Furaha

Furaha hutokana na

  • Sherehe – harusi
  • Mwakampya
  • Kuzaliwa kwa motto
  • Sikukuu ya krismasi
  • Sikukuu ya pasaka
  • Mahafali – sherehe za kufuzu
  • Siku ya tuzo/harambee
  • Kutembelewa na wageni
  • Sherehe za kitaifa
  • Sherehe za asili

Msamiati na mapambo

  • Maua ya kila ainati – si asmini, mawaridi
  • Ukumbi ulijaa na kuwatapika adinasi
  • Vipaza sauti vilihinikiza sauti
  • Vyakula vya kila aina/jamii vilitishia kuangusha meza
  • Msichana /kidosho/kipusa alitembea kwa madaha
  • Mkalimani na mfawidhi walishirikiana kama
  • Tulilakiwa kwa kupigwa pambaja
  • Waja walijaa si si si si
  • Waja waliwasili makundimakundi/mmoja mmoja/pacha pacha
  • Nikitembea aste aste hadi jukwaani
  • Kula/kushtaki njaa/fanyia mlo haki
  • Nilikumbuka nilivyojifunga kibwebwe/masombo
  • Kaka angeasi ukapera
  • Waja walisakata ruma/dansi
  • Msafara/mlolongo wa magari
  • Mrembo/spoti/sawa na hurulaini kutoka peponi
  • Wapambe walivalia sare za kupendeza
  • Kusakata rumba/dansi/kunengua viungo
  • Msafara/mlolongo wa magari
  • Mtibwiriko wa kukata na shoka
  • Sheheneza pongezi sufufu
  • Mkono wa tahania
  • Pofushwa na vimulimuli vya wapiga picha
  • Walijaa sisisi/pomoni
  • Hojiwa na sailiwa na wanahabari

Vipokezi vya methali

  • Yakini, ___________
  • Waama, _____________
  • Ama kweli ________________
  • Wahenga hawakukosea walipokili _______________

Methali

  • Chanda chema huvishwa pete
  • Baada ya dhiki faraja
  • Hauchi hauchi unakucha
  • Siku njema huonekana asubuhi
  • Mvumilivu hula mbivu
  • Safari ys kesho hupangwa leo
  • Msafiri ni aliye bandarini

Insha za Ndoto/Njozi/Ruya/Ruiya

Ni maono anayoyapata mtu akiwa usingiziniBarua/Waraka

Huketa hisia za furaha au huzuni

Mtu anaweza kupiga mayowe au kuweweseka kulinga na ndoto

Ndoto za huzuni zinaweza kuhusu

  • Kifo
  • Wizi
  • Moto
  • Mafuriko
  • Kutishwa na viumbe hatari

Wakati mwingine mhusika hutokwa na jasho, kutabawali au kujikuta mvunguni mwa kitanda

Ndoto ya furaha humfanya mhusika kujilaumu kuwa ilikuwa ni ndoto tu. Inaweza kuhusu

  • Mahafali
  • Kuwa tajiri
  • Kapasi mtihani
  • Kuzaliwa mahali kama ikulu

Mwandishi asianze kwa kusema kuwa alianza kuota

Mapambo

  • Baada ya kula chajio _____________
  • Nilikuwa nimechoka hoi bin tiki _______________
  • Niliubwaga mgogole wangu kwenye kitanda ____________
  • Nilijifunika gubigubi na kulala fo fo fo
    Hisia za furaha
  • Nilifurahi ghaya ya kufurahi
  • Furaha upeo wa furaha
  • Nilidamka wanguwangu na kushika hamsini zangu
  • Niliamka alfajiri ya Mungu/ya musa
  • Ukumbi ulijaa shangwe, nderemo na hoi hoi
  • Nilipaa na kuelea angani
  • Vicheko vilishika hatamu jari moja
    Hisia za huzunu – jinamizi
  • Maji yalikuwa yamenifika shingoni
  • Ulimi uliniganda kinywani
  • Moyo ulinipapa kama kwamba ulitaka ufunguliwe utoke
  • Nilishindwa kuongea ni kawa kama mja aluyepokonywa ulimi
  • Malaika alinisimamia tisti/wima/kititi
  • Mambo yaliniendea mpera mpera
  • Nilipiga usiahi/mayowe ambayo yangewafufua wafu
  • Zogo na zahama lilizuga
  • Nililia kwa kite na imani lakini hakuna aliyenihurumia
  • Niliduwaa na kubung’aa kama mzungu wa reli
  • Kilio cha kikweukweu kilihitimu kikawa cha mayowe

Barua/Waraka

Kuna aina mbili

  1. Barua ya kirafiki
  2. Barua rasmi

Barua ya Kirafiki/Kidugu

Huandikwa ili kupeana mwaliko, kujuliana hali, kufahamisha au kuarifu kuhusu jambo

BIDII FAULU,
S.L.P 93,
NAIVASHA.
18-11-2015

Kwa sahibu yangu, fundi msanifu ,
Utangulizi _______________
Mwili

Hatima
Ni mimi wako,
Jina lamwandishi

Sehemu muhimu za barua hii ni anwani ya mwandishi

  • Huandikwa pembeni kabisa wa kulia sehemu ya juu
  • Hujumuisha jina la mwandishi au anakosomea au kufanya kazi
  • Huwa pia na mahali anakoishi na sanduku la posta

Kianzio

  • Hudhihirisha anayeandikiwa
  • Hubainisha uhusiano wake na mwandishi
  • Kwa mpendwa
  • Kwa laazizi
  • Rafiki yangu
  • Kwa mwanangu mpendwa

Utangulizi

Haya ni maamkizi na kujuliana hali
Mfano

  • Pokea salamu sufufu/furifuri
  • Mimi ni buheri w afya/mzima kama

Mwili

  • Hubeba ujumbe au kusudio la barua
  • Lengo/nia/azma ya kukuandikia barua hii ni __________
  • Jina la
  • Ninaomba unitendee hisani/fadhila
  • Kwa kuwa wema hauozi
  • Ninakuhakikishia kuwa nitatia bidii
  • Ningependa kukujuvya kuwa
  • Tumia viunganishi ili kuunganisha mawazo
    • Isitoshe, zaidi ya hayo, aidha

Tamati

  • Ningependa kutia nanga kwa kukueleza
  • Ningependa kukunja jamvi
  • Kwa kuwa muda umenip kisogo
  • Ni mimi wako mpenzi,
  • Ni wako mpendwa,
  • Jina la mwandishi

Barua Rasmi

  • Huandikwa ili kuwasilisha ujumbe maalum
  • Huandikwa ili kuomba msamaha
  • Kuomba nafasi kwa kazi
  • Kuwasilisha malalamishi
  • Kuagizia/kuthibitisha mapokezi ya kampuni, shirika , idara

Sehemu

Anwani ya mwandishi

  • Huandikwa pembeni kabisa upande wa kulia sehemu ya juu ya karatasi
  • Hujumuisha jina la mwandishi, sanduku la posta, mahali anakoishi na tarehe baada ya anwani vuka mstari mmoja

Anwani ya mwandikiwa

  • Hutaja cheo cha anayeandikiwa
  • Taja jina la kampuni/shirika/dara
  • Taja S.L.P

Kianzio

  • Huanzia chini ya anwani ya mwandikiwa
    • Bwana/BW
    • Bibi/BI
    • Mabibi
    • Mabwana

Mtajo

  • Huelezea lengo la barua
  • Hutangulizwa kwa MINT: (mintirafu), KUH: (kuhusu), OMBI: , kumb: (kumbuka)
  • Pigia mstari ujumbe wenyewe

Mwili

Hubeba ujumbe wa barua

Maudhui hutegemea nia au lengo la barua

Lugha iwe rasmi

Msamiati

  • Nina furaha riboribo/kuu/firifuri
  • Nina bashasha belele
  • Ninasikitika ninapokuandika waraka huu ____________________
  • Ningependa kuchukua fursa/wasaa/nafasi
  • Kurejelea habari Fulani
  • Kwa mujibu w habari niliyoisoma/kutokana na taarifa/ kulingana na ______________
  • Shule.kampuni/shirika _____________ imesifika
  • Imetajwa na kutajika
  • Sifa zake zimeenea kote _______________ kamamoto nyikani kama wakati wa hari/kiangazi
  • Katika Nyanja za michezo ____________________ idara/shirika/shule yako
  • Wasifu/tawasifu _____________ mimi ni mwananchi kindakindaki/halisi
  • Nina nidhamu na taadhima ya hali ya ___________________
  • Nina talanta katika fani ya riadha uimbaji
  • Nina sauti ya ninga
  • Nitakuwa kielelzo dhabiti kwa
  • Nitatia bidii za mchwa ajengaye kichunguu
  • Nitavumilia/nitajikaza kisabuni ili kuafikia ndoto yangu
  • Vyeti vyangu vimeambatanishwa pamoja na waraka huu

Tamati

Ni mwisho wa barua
Huandikwa pembeni upande wa kulia sehemu ya chini
Herufi ya kwanza iwe kubwa

Insha ya Methali

Methali ni usemi wa kisanii wa kimapokeo unaofikiliwa na jamii na hutumiwa kufumbia jambo fulani

Methali hutahiniwa kwa namna tatu

Ikiwa kama mada

Mwanafunzi anafaa aeleze maana ya juu na ya ndani yake na matumizi yake iwapo anaifahamu vyema

Methali za Majuto, Maonyo na Tahadhari

  • Hutumiwa kuonyesha athari au madhara yanayotokea baada ya mtu kugaidi maagizo, nasaha au maonyo
  • Methali hutahiniwa kwa njia tatu
    Ikiwa mada
    Mwanzo – mwanafunzi huhitajika kuendeleza bila kufafanua maana ya methali
    Kimalizio – lazima kisa kishahibiane na methali ile.

    Tanbihi
    Ikiwa methali itakuwa mada, mtahiniwa atahitajika kueleza maana ya nje, ya ndani na matumizi endapo anafahamu

  • Hutumiwa kutoa funzo kwa wenginekutokana na dhiki na majuto yaliyomfika mhusika
    • Asiyefunzwa na mamaya hufunzwa na ulimwengu
    • Asiyeskia la mkuu huvunjika guu
    • Mchelea mwana kulia hulia mwenyewe
    • Mbio za sakafuni huishia ukingoni
    • Mchuma janga hula na wa kwao
    • Ujanja wa nyani huishia jangwani
    • Majuto ni mjukuu huja kinyume
    • Mchimba kisima huingia mwenyewe
    • Msiba wa kujitakia hauna kilio
    • Kilio si dawa
    • Asiyeangalia huishi laiti ningalijua
    • Mkata pema pabaya panamwita
    • Sikio la kufa halisikii dawa
    • Haraka haraka haina baraka
  • Vipokezi vya methali
    Yawe yasiwe ____________
    Aisee! __________
    Labeka! _________________
    Lahaula! Lakwata ____________
    Chambilecho wenye ndimi walihenga ______________
    Hapo ndipo nilipoamini na kusadiki kuwa ______________
    Waledi wa lugha waligonga ndipo walipoganga kuwa _______________
    Wakale hawakupanda upepo wakavuna tufani _____________
  • Visa husika
    • Wizi
    • Utumizi wa dawa za kulevya
    • Kujiingiza katika anasa

Mapambo na msamiati

  • Kutofuata ushauri
    • Alikuwa hakanywi hakanyiki
    • Hasikii la mwadhini wala la mteka maji msikitini
    • Alikuwa haliki hatafunuki
    • Haambiliki hasenezeki
    • Alikuwa hajijui hajitambui
  • Kujuta
    • Aliishia na laiti kinywani
    • Alijiuma kidole/alilia chanda kili kinywani
    • Nilikabiliana ana kwa ana na ulimwengu usiokuwa na huruma
    • Niliyaona ya firauni
    • Nilikiona kilichomtoa kanga manyoya
  • Kupuuza
    • Alivalia miwani mashauri
    • Niliyatemea mate mawaidha
    • Alijitia hamnazo
    • Aliyatia kapuni yota aliyoambiwa
  • Mambo kuharibika
    • Mambo yalimwendea pete/tenge/mrisi/shoto/shambiro
    • Kutowezekana kwa
    • Ilikuwa sawa na kukama tetere
    • Kufunuka jua kwa ungo au chekeche
    • Kuchota maji kwa pakacha
  • Tashbihi
    • Pukutikwa na machozi kama ngamia
    • Tiririkwa na machozi kama maji mlimani
    • Mchafu kama kilihafu/fungo
    • Nuka kama mzoga/beberu/kindonda
  • Unafiki na kujitakia shida
    • Chui aliyevalia ngozi ya kondoo
    • Panya aliyeumia na kuvuvia
    • Kujipali makaa kama chachandu
    • Kuogelea katika bahari ya moto
    • Methali ni usemi wa kisanii wa kimapokeo unaofikiliwa na jamii kuwa wa kweli na unaotumia kufumbia
  • Ragba
    • Aliona cha mtema kuni
    • Kilichompata peku na lungo kilimpata
    • Mambo yalimwendea visivyo
    • Alitamani mauti yaje yamwokoe
    • Maji yalizidi ynga
    • Alitamani dunia ipasuke immeze mzima mzima
    • Kumwashia kipofu taa
    • Alitia masikio pamba
    • Machozi ya majonzi
    • Lia kilio cha kite na shaka
    • Machozi yalimtoka kapakapa
    • Pyorea mdomo
    • Huzunika ghaya ya kuhuzunika
    • Machozi yalinienda mbilimbili
    • Kuwa na kamusi ya matusi
  • Tashbihi
    • Pukutikwa na machozi ka,a ngamia
    • Tiririkwa na machozi kama maji mlimani
    • Bubunjikwa na machozi kama mfereji
    • Nuka kama mzoga
    • Mchafu kama fugo
  • Takriri
    • Hakiri hakubali
    • Hajali jando wala togo
    • Si wa uji si wa maji
    • Kutomjulia heri wala shari
    • Akiulizwa haungani

Methali za Kutohadaika na Uzuri wa Nje wa Kitu na Tamaa

Hutumiwa kuwaonya adinasi dhidi ya kudanganyika au kuhadaika na uzuri wa kitu bila kudadisi matokeo na athari zake.

Methali ikiwa kama kichwa huhitajika kuelezea maana ya nje, ya ndani na matumizi
Mfano wa visa

  • Kumkaribisha mtu nyumbani
  • Kupatiwa lifti
  • Biashara gushi
  • Urembo
  • Fisadi

Methali

  • Uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mti
  • Hakuna kizuri kisichokuwa na dosari
  • Penye urembo ndipo penye ulimbo
  • Uzuri wa mkakasi, ukipata maji basi
  • Vyote ving’aavyo sio dhahabu
  • Tama ilimwua fisi
  • Uzuri si hoja hoja ni tabia
  • Mpanda farasi wawili hupasuka msamba
  • Mtaka yote hukosa yote
  • Mbio za sakafuni huishia ukingoni
  • Mla kwa wawili hana mwisho mwema
  • Penye uhondo pana uvundo
  • Uzuri wa biyu ndani mabuu
  • Usiache mbachao kwa msala upitao

Vipokezi vya methali

  • Kwa yakini ______________
  • Taib ___________
  • Ama kweli ______________
  • Kuntu _____________
  • Ni jahara kama pengo kuwa _____________
  • Ni wazi kama ju ala mtikati kuwa _____________
  • Chambilecho wahenga au wazee wenye tabasuri tepetepe _______________

Nahau

  • Maji kuzidi unga
  • Kitumbua kiliingia mchanga
  • Valia miwani
  • Meza mrututu
  • Meza mate machungu
  • Tulia huku ukitolea kule
  • Vimba kichwa
  • Kuwa na mkono mrefu
  • Bwaga zani

Takriri

  • Dhahiri shahiri
  • Haambiliki hasemezeki
  • Hakanywi hakanyiki
  • Kuwa kiguu na njia
  • Hana harusi hana matanga

Ragba

  • Walimdekeza mwana wao
  • Alikuwa ndumakuwili aliyeuma ndani yakini kikulacho ki nguoni
  • Alijaribu bahati kwani asiyekuwa na bahati habahatishi
  • Pigwa kipopo
  • Temea mate
  • Kumwonea gere
  • Mambo yalimwendea sambejambe
  • Alilia kilio cha kite

Tashbihi

  • Huzunika kama mfiwa
  • Kuwa na wasiwasi kama mwasi
  • Aminika kama njiwa
  • Jambo wazi kama mchana
  • Kuwa mzembe kama kupe

Insha ya Maelezo

Huitwa wasifu

Hutoa ufafanuzi kuhusu jambo, mtu, mahali au kitu fulani

Maelezo haya huwa ni sifa au hoja maalum

Insha hizi hutahadharisha, huelezea, huarifu na huburudisha

Mtahiniwa atangulize kwa ufafanuzi wa mada yake

Ahitimishe kwa kutoa changamotokwa waliohusika

Mtahiniwa asijadili chini ya hoja sita. Atoe hoja za ukweli

Mfano

  • Athari za ukimwi
  • Athari za dawa za kulevya
  • Faida na Athari za teknolojia
  • Mchezo niupendao
  • Haki za watoto
  • Faida ya elimu, miti na wanyamapori
  • Ukosefu wa usalama
  • Dawa za Kulevya

Haki na Ajira za Watoto

  • Haki ni mstahiki au ni jambo ambalo ni halali ya mtu
  • Mstahiki pia ni mtu mwenye haki ya kupata kitu
  • Ajira ni kazi zinazofanywa katika mashamba, viwanda, nyumbani na migodini
  • Watoto wanapopewa ajira ni kinyume cha sheria
  • Baadhi ya haki hizi ni
    • Lishe bora
      • Watoto wanafaa wapewe mlo ulio na viinilishe muhimu kwa protini, kabohaidrati, madini na maji safi.
      • Wasipolishwa huenda wakaathiriwa na magonjwa kama kwashakoo, utapiamlo.
    • Mavazi
      • Humkinga dhidi ya mabadiliko ya hali ya anga
      • Huzuia maradhi kama mafua, nimonia na pumu
        Methali
        Kinga ni bora kuliko tiba
    • Makao salama
      • Humsitiri dhidi ya wanyama hatari, maadui na mabadiliko katika hali ya anga
    • Kupata elimu
      • Asibaguliwe kwa misingi ya jinsia, kidini, kikabila au rangi ya ngozi
      • Wasichana wasiozwe mapema
      • Wasijiingize katika vitendo vya ukosefu na maadili kama ukahaba
      • Wafundishwe maadili na nidhamu
        Methali
        Elimu haitekeki
        Elimu ni bahari
        Elimu haina mwisho
    • Afya njema
      • Watoto wanafaa kukulia katika mazingira safi
      • Wapewe matibabu wanapougua
      • Wapewe lishe bora
        Methali
        Afya ni bora kuliko mali
        Kinga ni bora kuliko tiba
    • Wakingwe dhidi ya dhuluma
      • Hii ni kama kuchomwa na kukatakatwa mwilini
      • Waadhibiwe kwa kadiri na wastani
      • Wakuzwe vyema kwa maadili na mapenzi
        Methali
        Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo
        Masukuzi ya leo ndio msitu wa kesho
    • Wasiajiriwe
      • Hii ni kinyume na sheria katika katiba ya nchi
      • Waajiri huwatesa na kuwanyanyasa watoto
      • Wengine huwarapua kwa mijeledi
      • Wengine huajiri kama vijakazi, watwana

Michezo

Ni jambo lifanywalo kwa ajili ya kujifurahisha kujichangamsha au kupoteza wakati

Baadhi ya michezo

  • Jugwe
  • Gugwi
  • Bembea
  • Kibe
  • Msabaka
  • Kandanda
  • Riadha
  • Sarakasi
  • Netiboli
  • Naga
  • Voliboli
  • Gololi
  • Hoki
  • Langalanga
  • Kriketi
  • Mpira wa wavu

Kandanda

Pia huitwa kambumbu, soka , gozi au mpira wa miguu

Hushirikisha timu mbili pinzani
Wachezaji huvalia

  • jezi
  • Daluga
  • Soksi
  • Bukta

Katikati  ya uwanja huitwa kitovu/senta
Otea – kujificha kwa makusudi ya kushambulia kwa ghafla
Penalty – adhabu kwa mlindalango
Mlindalango, mdakaji, golikipa
Kimia
Refa/refarii
Mshika bendera/kibendera
Mhimili/goli
Ngware – cheza visivyo
Kipindi cha lala salama ni kipindi cha nwishi
Kadi nyekundu huonyesha kutimuliwa kwa mchezaji
Kadi ya jano – onyo

Huwa na wachezaji kumi na mmoja katika kila upande

  • Walinzi au difensi
  • Wachezaji wa kati
  • Safu ya mashambulizi
  • Wachezaji wa akiba
  • Piga mkwanju
  • Kocha/mkufunzi

Mapambo

  • Uwanja ulijaa hadi pomoni
  • Wachezaji walishonona
  • Mdakaji aliudaka mpira ungedhani ni tumbili aliyedadia tawi la mti
  • Pasi fupifupi na za uhakika ungedhani walikuwa na mashine miguuni
  • Mpira haukulenga goli _______ kweli kulenga si kufuma
  • Kuutia mpira vifuani kana kwamba una spaki za kuunasa
  • Walinda ngome walikuwa imara kama chuma cha pua
  • Kwenda kubwaga moyo baada ya kipindi cha kwanza
  • Safu ya ilinzi ulikuwa imara kama ukuta uliotengenezwa kwa zege
  • Enda nyatunyatu na kufyatua zinga la kombora
  • Visha kanzu
  • Nyota ya jaha
  • Bao la kuta machozi
  • Piga kombora kimo cha mbuzi , kuku au ngamia
  • Mashabikiwalijawa na bashasha
  • Kipindi cha pili tukihisi kuwa na nishati mpya
  • Bao la bua liliweza kuzitubua nyoyo za wapinzani wetu
  • Mrisi bin kappa

Dawa za Kulevya

Hatua

Kufafanua maana

Ni kitu chochote kinachoathiri fahamu au mwili wa binadamu
Dawa hizi ni kama vile

  • Bangi
  • Sigara
  • Heroini
  • Miraa/mirungi
  • Pombe haramu

Anayeuza dawa hizi huitwa mlaguzi
Njia ya kutumia dawa hizi ni

  • Hunuswa
  • Hunywewa
  • Hudungwa
  • Hulambwa
  • Hutafunwa

Madhara ya dawa za kulevya

  • Kuvurugika kwa akili
  • Mja hugeuka kuwa zuzu, mkia wa mbuzi
  • Hupata ujasiri bandia
  • Hujiingiza katika visanga
  • Hudhuru afya
  • Hukonda na kukondeana kama ng’onda
  • Sura huambuliwa na kusawijika kama sokwe
  • Utovu wa nidhamu
  • Husheheni cheche za matusi
  • Kutabawali kadamnasi
  • Vaa mavazi vichungi na vioo
  • Kuzorota kwa uchumi
  • Kukosa elimu
  • Jamaa hukosa mavazi, makao na mlo
  • Humtilisha mtumiaja
  • Husababisha uraibu
  • Hushinda kutwa kucha wakitumia dawa hizo
  • Huwa kupe
  • Huwa maajenti wa mawakala
  • Chanzo cha maafa
  • Madereva hukosa kuwa waangalifu
  • Huleta shinikizo la damu mwilini
  • Ajali barasteni
  • Wizi wa mabavu
  • Kufanya mapenzi bila kinga

Tamati

  • Changamoto/nasaha
  • Wasiwe pweza kujipalia makaa
  • Kizazi cha baadaye kitaangamia
  • Kushirikiana kama kiko na digali kuangamiza janga hili
  • Wito kwa serikali – kuwasaka
  • Kufungua mashtaka

Mada

  • KIDIMBWI CHA MANAYA
  • NAULI YA AHERA
  • BARABARA YA KUZIMU
  • TARIKI YA MAUKO

Misemo

  • Kujipalia makaa
  • Bwaga zani
  • Meza mrututu
  • Tumbulia macho
  • Gofu la mtu

Takriri

  • Kufa kupona
  • Kwa hali na mali
  • Liwalo liwe
  • Balaa belua
  • Methali
  • Tahadhari kabla ya hatari
  • Mwiba wa kujidunga hauambiwi pole
  • Ajali haina kinga
  • Mchezea mavi humnukia
  • Nzi kufia juu ya kindonda si haramu
  • Masukuzi ya leo ndiyo msitu wa kesho
  • Wazee hukumbuka vijana hukumbushwa

Tashbihi

  • Konda kama ng’onda
  • Nyong’onyea kama muwele wa malaria
  • Dhaifu kama mkufu
  • Epuka ambao kama mgonjwa wa ukoma/ebola

Umuhimu wa Maji

Mwongozo ambao ni mwanzo wa insha kisha aendeleze
Mfano
“maji yana manufaa anuwai ___________ ”

  • Atoe hoja zisizopungua sita
  • Iwe na mtiririko mmoja
  • Sehemu ya hitimisho;atoe change moto kwa jamii au serikali

Mfano

UMUHIMU WA MAJi

Utangulizi

Maana ya maji
Maji ni kiowevu kisicho na rangi kinapatikana mtoni, ziwani, baharini na hata kutokana
na mvua
Maji ni uhai

Umuhimu wa maji

  • Kukonga roho au kukata kiu
    Adinasi hukonga roho
    Huweza kuishi bila shabuka au shida yoyote
    Husaidia usagaji wa chakula
    Mapishi ya vyakula
    Chakula hulainika na kuwa na ladha
    Huimarisha siha/udole wa binadamu
    Humweupusha mlimwengu na magonjwa
  • Usafi na unadhifu
    Kutakata mili ili kuepukana na magonjwa
    Kupiga deki
    Kusafisha mashine viwandani
    Kuwa mchafu kama fungo
    Kusafiri jongomeo baada ya kugua maradhi
  • Usafiri baharini, maziwani na mitoni
    Kusafirisha shehena za mizigo
    Mizigo mizito kama nanga
    Vyombo hivi vya usafiri ni meli, motaboti, ngalawa, merikebu, mashua, manahodha na maserahangi
  • Kuzungusha mitambo au mashine
    Hupata nguvu za umeme au nishati
    Nishati hizi huweza kutengeneza bidhaa za madini, vyakula na mavazi
  • Makao ya wanyama
    Kama samaki, kiboko, mamba, kamba na kasa
    Samaki ni chakula murua kwa mja na humzuia mja kuoata ndwele
  • Burudani na michezo
    Hamamu na mandibwi ya maji hutumika na wanamichezo kwa mashindano ya kuogelea
  • Huwa sehemu ya ajira
  • Huletea nchi pesa za kigeni
  • Kuondoa uchafu baada ya kazi
  • Maji ni asili ya uhai
  • Kuuzima moto
  • Kivutio cha watalii
  • Kunyunyizia mimea maji

Viunganishi

  • Mbali na _____________
  • Fauka ya ______________
  • Isitoshe _______________
  • Zaidi ya ______________
  • Hali kadhalika _______________

Hitimisho

  • Nikilikunja jamvi ninawashauri ________________
  • Hatuna la msalie mtume wala nabii ili kuyatumia maji ipasavyo __________________
  • Ama kweli maji ni kito cha dhamani ambacho kinafaa kulindwa kwa hali na mali

Methali

  • Maji yakimwagika hayazoleki
  • Maji ya kifuu ni bahari ya uchungu
  • Maji mapwa hayaogwi
  • Maji ni uhai
  • Maji hufuata mkondo
  • Maji ukiyavulie nguo yaoge

Hotuba

Hotuba ni maneno au malezo maalum yanayotokana na mtu mmoja mbele ya hadhira

Anayetoa hotuba huitwa hatibu

Hadhira ni watu wanaohutubiwa

Hotuba inaweza kuwa ya

  • Mwalimu mkuu juu ya wazazi
  • Mwanasiasa nyakati za kampeni
  • Maafisa wa serikali katika sherehe tofauti
  • Rais akihutubia taifa

Mambo ya kuzingatia

  • Kufuata itifaki
  • Kutambua waliohidhuria kufuata cheo/mamlaka na umri
    Mfano “mwalimu mkuu, naibu wa mwalimu mkuu, viranja na wanafunzi wenzangu hamjambo? ______
  • Wakati uliopo hutumika yaani usemi halisi
  • Nafsi ya kwanza na ya pili hutumika
    Mfano
    Nimesimama kadamnasi nikiwa mzima kama kigongo ________
  • Hutumia alama za kunukuuu ikiwa unahutubia kwa niaba ya mtu mwengine
    Mfano
    rais, naibu wa rais ______
  • Kila hoja husimuliwa katika aya yake
  • Hitimisho huhusu kuwashukuru wasikilizaji na pia kuwapa funzo au changa moto au nasaha

Umuhimu wa Elimu

Elimu ni mafunzo yanayopatikana shuleni na maishani
Hupevusha fikira
Mja hujielewa, huelewa wengine na ulimwengu
Huheshimiana
Huweza kutumia raslimali vilivyo
Elimu huondoa ujinga/ujuha
Mwanafunzi humakinika katika maisha ya baadaye
Msamiati

  • Leo si jana, jana si leo
  • Enda na ucheo, siende na uchwao

Elimu ya vitabu humsaidia mtu kuhifadhi siri ujumbe na kumbukumbu za kutumia na kizazi cha baadaye

Msamiati

  • Elimu huboresha maisha
  • Kujenga makao mazuri
  • Kuwasaidia jamaa na jamii
  • Elimu ni daraja la kuvusha mtu kwenye gange/kazi yenyefulusi nono
  • Mtu hupata hela za kujimudu pasi kuwategemea wengine
    Methali
  • Mtegemea cha nduguye hufa maskini
  • Mtegemea nundu haachi kunona
  • Mja hupewa heshima
    Ragba
  • Nimesimama imara kama chuma cha pua
  • Tisti kama ngarange za mvule
  • Kidete kama kitawi cha mkarakala
    Pongezi za dhati
  • Ninawapa mkono wa tahania kwa kufanya bidii za mchwa na duduvule
  • Nawamiminia shukrani sufufu
  • Ninawashukuru kwa kujitolea mhanga na kujifunga kibwebwe/masombo/kujikaza kisabuni

Methali

  • Elimu ni bahari
  • Elimu maisha si vitabu
  • Elimu ni taa gizani hung’aa
  • Elimu ni mali ambayo adui hawezi kuteka
  • Elimu bila mali ni kama nta bila asali

Tashbihi

  • Bidii za mchwa /duduvule
  • Ng’aa kama mbalamwezi
  • Pesa kama njugu
  • Julikana kama pesa

Misemo

  • Kujitolea mhanga
  • Shika usukani
  • Kuna kichwa
  • Ambua kitu
  • Tia pamba/nta

Mjadala

Insha sampuli hii huwa na sehemu mbili: Kuunga na kupinga
Mwanafunzi ana uhuru wa kuunga ama kupinga

Katika sehemu ya hitimisho mtahiniwa anatarajiwa kutoa mawazo yake

Tamati
Ningependa kuwajuza kuwa ______________
Ningeomba sote tupinge kwa jino na ukucha _____________
tusiwe kama chachandu wa kujipalia makaa kwa ______________

Teknolojia

Ni maarifa ya sayansi na matumizi yake katika mitambo, vyombo na zana katika viwanda, kilimo, ufundi na njia za mawasiliano
Mifano

  • Kilimo 
    Trekta   
    Beleshi   
    Pilau   
    Mbolea   
    Toroli   
  • Zana za vita   
    Manowari   
    Bazooka   
    Vifaru
    Darubini   
    Grunedi   
    Bunduki   
    Bastola
    Gomborora
    Nyambizi
    Mzinga
    Kombati
    Dirizi/dereya
  • Mawasiliano
    Simu – tamba/rununu/mkono
    Tarakilishi
    Tovuti
    Kitenzambali
    Barua meme
    Kikotoo
    Kimemeshi
  • Mitambo
    Kiyoyozi/feni/pauka/pangaboi
    Lifti/eleveta
    Kreni/winchi/kambarau
    Meli
    Ndege
    Mashua

Faida za Teknolojia

  • Mawasiliano – kupasha habari
  • Elimisha na kutumbuiza
    Methali
    Kipya kinyemi ngawa kindonda
  • Utafiti
    Kuvumbua dawa za ndwele/mitambo kurahihisha kazi
    Mitambo ya kuchunguza hali ya anga
  • Elimu
    Matumizi ya mitambo
    Kanda za video
    Methali
    Elimu ni bahari
    Elimu haitekeki
    Mali bila daftari hupotea bila habari
    Elimu bila mali ni kama sega bila asali
  • Usalama
    Zana za vita
    Donge nono hupatikana baada yakuuza vifaa
    Methali
    Tahadhari kabla ya hatari
    Kilimo na ufugaji
    Pembenjeo – mbegu, mbolea, dawa
    Ghala la kuhifadhi mazao
    Mashine za kukama ng’ombe
    Methali
    Tembe na tembe huwa mkate
  • Usafiri
    Vyombo vya majini, nchi kavu au barabara
    Kuokoa wakati na maisha
    Methali
    Ngoja ngoja huumiza matumbo
  • Mavazi
    Rahisisha kazi
    Kuimarisha uchumi wa nchi

Madhara

  • Mmomonyoko wa maadili
  • Huleta maradhi kama saratani
  • Huleta maafa
  • Punguza nafasi za kazi
  • Kuiga tabia za kigeni
  • Vita
  • Kuwafanya waja kulaza damu
  • Mambo mengine muhimu

Viunganishi vya insha ya maelezo

  • Licha ya
  • Fauka ya
  • Aidha
  • Zaidi ya
  • Pia isitishe
  • Mbali na
  • Hali kadhalika

Insha ya Mazungumzo

Mazungumzo ni maongezi, mahojiano ama malimbano baina ya mtu na mwengine au kundi moja na jengine
Yanaweza kuwa Porojo/soga/domo
Ni mazungumzo ya kupitisha wakati
Kutafuta ujumbe maalum
Hufanywa kwa njia ya mahojiano
Kudadisi au kumwelekeza mtu
Baina ya mtu na tajriba na Yule anayetakamsaada

  • Mhusika mmoja asichukue nafasi kubwa
  • Tumia alama za uakifishaji kama vile koloni, kitone na kipumuo
  • Sharti pawe na mahali pa kumchachawiza
  • Vitendo viweze kuandikwa katika alama za mabano
  • Fani za lugha zitumike ili kuleta uhondo
  • Pawe na maagano

Hatua

  • Mada/kichwa
    Huandikwa kwa herufi kubwa kupigiwa mstari
  • Maudhui
    Ni lengo au kusudi la mazungumzo
    Msamiati kutegemea lengo la mazungumzo
  • Vitendo na ishara
    Haya yataandikwa katika mabano (akitari, akilia, akicheka)
  • Alama za uakifishaji
    • Koloni( : ) Huandikwa baada ya jina au cheo cha watu
    • Alama za dukuduku ( _ _ _ ) Mazungumzo yanaendelea
    • Parandesi au mabano ( ) Kubana maneno ambayo hayatasemwa
    • Alama ya hisi ( ! ) Hutumiwa pamoja na viigizi kuonyesha hisia

Insha za Hadithi

Hadithi hutambiwa kwa njia ya kusimuliwa
Hurejelea matukio au visa vyenye nasaha kwa jamii
Visa hivi hutumiwa

  • Kuelimisha
  • Kushauri
  • Kuonya
  • Bidii
  • Kuonyesha umoja

Enzi za kale watoto walisimuliwa visa hivi na babu au nyanya wakati wa jiono
Mifano

  • Abunuwasi
  • Shamba la wanyama
  • Sungura mwenye pembe
  • Shujaa fumo liyongo

Ikiwa kisa kilisimuliwa na mwingine mwanafunzi atahitajika kunukuu kazi yake
Mfano
“ babu alizoea kutuambia ngano.alianza hivi ____________”

Baada ya kuhitimisha kisa mtahiniwa anahitajika kufunga
Ahitimishe kwa ushauri au nasaha

Insha hii yaweza kuchukua mikondo tofauti

  • Furaha
  • Majuto
  • Huzuni
  • Bidii

Tanbihi
Sanasana wahusika huwa wanyama ambao huwa na hisia za binadamu

Jinsi ya kuanzisha

  • Paukwa?pakawa!
  • Aliondokea chanjagaa kujenga nyumba kaka mwanangu mwana siti kijino kama chikichi cha kujengea vikuta na vilango vya kupitia
  • Hapo zama za zama _____________
  • Hapo kale ___________
  • Hapo jado aliondokea _____________
  • Enzi za konga mawe ______________
  • Miaka na dahari iliyopita ___________________
  • Katika karne za mababu na bibi zetu _____________________
  • Miaka na mikaka iliyopita _____________
  • Hadithi!hadithi! hapo zama za kale katika kaya/kijiji ______________

Fani za lugha

Takriri

  • Miaka na mikaka
  • Dhahiri shahiri
  • Hana hanani
  • Maskini hohehahe
  • Daima dawamu
  • Afriti kijiti

Misemo

  • Salimu amri
  • Shika sikio
  • Temea nasaha mate
  • Valia miwani
  • Tia kapuni
  • Mambo kuenda shoro
  • Kutojulia heri wala shari
  • Kuwa fremu ya mtu

Tashbihi

  • Roho ngumu kama paka
  • Zurura kama mbwa msokwao/mbwakoko
  • Tabia kunuka kama kindonda/beberu
  • Macho mekundu kama ngeu/damu
  • Kuchukua wekundu wa moto

Methali

  • Bendera hufuata upepo
  • Sikio la kufa halisikii dawa
  • Kutosikia la mwadhini wala la mteka maji msikitini
  • Nzi kufia juu ya kindonda si haramu
  • Maji hufuata mkondo
  • Aambiwaye akakataa hujionea

Ragba

  • Kabla ya mwadhini kuadhana adhna zake
  • Maji kwa pakacha
  • Julikana kwa ufedhuli
  • Kuwa sawa na kutumbutia maji
  • Andamana na makundi yenye mienendo benibeni
  • Heshima likawa neno geni kwake
  • Lala kitandani hoi akiwangoja pumzi yake ya mwisho
  • Lia kilio cha mbwa

Hitimisho

  • Nyanya/babu alitueleza bayana umuhumu wa
  • Hapo ndipo niliposandiki kuwa
  • Ulumbi wa ulidhihirika waziwazi kuwa

Mnyambuliko wa Vitenzi

Huku ni kuvibadili vitenzi kwa kurefusha viambishi tamati ili kuleta kauli mbalimbali Kauli hizi ni.

  • Tendana: uma - umana
  • Tendesha: lala – laza
  • Tendeka: Lima – limika

Huu ni upachikaji wa viambishi kwenye mzizi wa kitenzi ili kuunda vitenzi vipya

Kauli ya Kutendeshwa/Fanyisha

Huonyesha kuwa kitendo kimesababishwa na kitu Fulani

Vitenzi hivi hutambulishwa na vitenzi vya, za, sha, fya, na ,sa

Kauli ya Kutendata

Kauli hii huonyesha dhana ya kurudia rudia tendo
Mfano
Kata – katakata
Imba – imbaimba
Tia – tiatia
Ruka – rukaruka

Sifa Kutokana na Vitenzi

Ni kuunda maneno yenye kivumishi au kusifu nomino kutoka kwenye viarafa

Sifa hizi huwa ni herufi kama f, v, mw
Mfano
Amini – mwaminifu
Sikia- sikivu
Tii – tiifu
Dhulumu – dhalimu

Tanakali za Sauti

Ni maneno yanayoonyesha au kuiga milio ya sauti, hali Fulani, sura au vitendo mbalimbali. Hutumia kusisitiza namna vitendo vilivyo, vinavyotendeka au kitakavyotendeka

Mfano:

  • Funika gubigubi!
  • Papatika papatupapatu!
  • Kula fyu!
  • Kuregea regerege!

Matumizi ya Vihusishi ‘katika’ na Kiambishi Tamati –ni’

Katika na –ni ni vihusishi vinavyotumiwa kumaanisha ndani ya au kwenye

Vihusishi hivi havitumiwi pamoja katika sentensi

Mfano

  • Ingia katika darasani ni kosa
  • Ingia darasani au ingia katika darasa ni sahihi

-ni huambishwa kwenye nomino za kawaida kisha nomino hiyo huorodheshwa katika ngeli ya PAKUMU
Pia hutumika kuonyesha ndani ya au mahali ndani
Mfano
Vijiko vimo jikoni
Walimu wamo majilisini

Katika

  1. hutumiwa kuleta maana ya Miongoni mwa
    mtu mmoja katika wale ni mgonjwa
  2. Wakati
    Tutakuwa na likizo katika mwezi wa Aprili
  3. Ujumla wa vitu
    Wote walishiriki katika michezo hiyo

Alama za Uakifishaji

Ni alama zinazotumiwa ili kuwasilisha nia halisi na maana kamili ya kwenye maandishi

Alama hizi pia hufanya kusomeka kwa sentensi kuwa rahisi
Mfano

Nusukoloni /Semikoloni/Nukta kipumuo(;)

Hutumiwa kuunganisha mawazo mawili
Mfano
Ninataka kuondoka mapemasipendi kuchelewa

Koloni/Nuktambili/Nukta pacha (:)

Hutumiwa kuonyesha orodha ndefu
Mfano
Nenda ununue vutu vifuatavyo:maziwa, mkate, sukari, mafuta na chumvi

Ukubwa, Udogo na Wastani wa Nomino

Ukubwa ni hali ya kukuza nomino na udogo ni hali ya kudunisha nomino
Wastani ni hali ya kawaida ya nomino

Nomino katika ukubwa huwekwa katika ngeli ya LI – YA na nomino katika hali ya udogo huwekwa
katika ngeli ya KI – VI

Zipo kanuni ambazo hutumiwa

  • Nomino zenye silabi mbili- dodosha moja
    Mtu- jitu
  • Nomino zinazoanza kwa ki dondosha ki pachika ji
    Kiatu-jiatu

Kukanusha

Kukanusha Amri

Wakati wa amri hukanushwa kwa kutumia si
Mifano
Aende – asiende
Nimpe – nisimpe
Ule – usile

Swali lije baadaye
Wewe kunywa dawa
Wewe usikunywe dawa

Wingi na Kukanusha

Wakati wa sasa hukanushwa kwa ha
Mifano 

unasoma – mnasoma – hamsomi
unakula – mnakula – hamli

Vivumishi

Vivumishi vya Pekee Ingine na -O-ote

Vivumishi hivi ni ote, o-ote, enye, enyewe na ingine

Vitawe

Ni maneno yaliyo na maana zaidi ya moja
Mfano

  • Vua-toa samaki majini
            Toa nguo mwilini
  • Ala-aina ya mfuko ambamo kisu hufichwa
          Tamko la kushangaa
          Aina yoyote ya chombo cha kufanyia kazi 

Viwakilishi

Ni neno linalosimama badala ya nomino kama yeye, sisi, wewe

Ngeli na Viambishi Ngeli

Mifano ya ngeli:

  • A – WA
  • U – YA
  • I – ZI
  • U – U
  • YA – YA
  • I – I

Ngeli ya A- WA

Ngeli hii inahusisha majina yenye sifa na hali ya wanyama, nyuni, malaika, samaki na wanadamu

Kutoa mifano katika umoja na wingi
Mfano
Mnyoo – minyoo
Kiwete – viwete
Nzi – nzi
Mkunga – mikunga

Ngeli ya U – I

Nomino za ngeli hii huchukua upatanisho wa U katika umoja na I katika wingi
Mifano
Mkono – mikono
Muundi – miundi
Mzigo – mizigo
Mtaa – mitaa
Muhula – mihula
Mwaka – miaka
Mlingoti – milingoti

Ngeli ya KI – VI

Nomino za ngeli hii ni vitu vya kawaida

Majina huanza kwa ‘ki’ katika umoja na ‘vi’ katika wingi

Mengine huanza kwa ‘ch’ kwa umoja na ‘vy kwa wingi
Mifano
Kiazi – viazi
Kiatu – viatu
Kioo – vioo
Kina – vina
Kikuba – vikuba
Cheti – vyeti
Chakula – vyakula
Chanda – vyanda
Chungu – vyungu

Wastani            udogo
Mlango             kilango
Mguu                 kiguu

Ngeli ya LI – YA

Maneno katika ngeli hii huanza na ma, me

Maneno yote katika hali ya ukubwa huingizwa katika ngeli hii
Mifano 
Dirisha – madirisha
Embe – maembe
Zulia – mazulia

Ukubwa

Guu – maguu
Jibwa – majibwa

Ngeli ya U – YA

Maneno katika ngeli hii huanza kwa U katika umoja na Ya katika wingi
Mifano
Ugonjwa – magonjwa
Uuaji – mauaji
Ujazi - majazi
Upana - mapana

Ngeli ya YA – YA

Nomino zote huanzia kwa ma
Mifano
Masihara - masihara
Matatu-  matatu
Makazi - makazi
Mahakama - mahakama
Maakuli - maakuli
Mawasiliano - mawasiliano

Ngeli ya I – ZI

Nomino hazibadiliki katika umoja na wingi
Mifano
Mashine - mashine
Sinia - sinia
Sahani - sahani
Ngozi - ngozi
Taa - taa
Pete - pete
Sakafu - sakafu
Shingo - shingo

Ngeli ya U – ZI

Maneno katika ngeli hii huwa na upatanisho wa U na ZI katka wingi
Mifano
Ubeti – beti
Uchane – chane
Uchega – chega
Ubavu – mbavu
Ubao – mbao
Ulimi – ndimi
Udevu – ndevu
Ujari – njari
Ujiti – njiti
Ugoe – ngoe
Uzi – nyuzi
Ufa – nyufa
Waadhi – nyaadhi
Walio – nyalio
Waraka – nyaraka

Ngeli ya U – U

Huchukua U katika umoja na U katika wingi
Kuelezea maneno hayabadiliki katika umoja na wingi
Mifano
Moto - moto
Ugali - ugali
Wema - wema
Ufisadi - ufisadi
Wizi - wizi
Ubaya - ubaya
Uzembe - uzembe

Ngeli ya KU

Maneno katika ngeli hii huchukua upatanisho wa kisarufi KU

Ngeli ya I – I

Majina ya nomino hii huchukua upatanisho wa sarufi kuwa I katika umoja na I katika wingi

Ngeli ya PA KU MU

Ni ngeli ya mahali

Huelezea hali tatu

  • Hapa/hapo/pale- mahali dhahiri
  • Huku/huko/kule – kusiko dhahiri
  • Humo/humu/humo – mahali ndani

Kuelezea viambishi tofauti

Page 13 of 14