Barua ya Kirafiki - Kiswahili Insha Notes

Share via Whatsapp


Utangulizi

  • Inayoandikwa kwa ndugu, jamaa na marafiki.
  • Pia huitwa barua ya kidugu


Muundo

  • Anwani ya mwandishi (wima au mshazari. Jina lisiwekwe!)
    • Anwani huandikwa katika sehemu ya juu ya karatasi upande wa kulia.
    • Katika kuandika anwani, yafuatayo hujumulishwa:
      - Makao ya mwandishi k.m. Shule yake, kijiji chake, mtaa wake n.k;
      - S.L.P. (Sanduku la posta); Nambari ya sanduku la posta apokeapo barua;
      - Mji ambapo posta apokeleapo barua zake ipo;
      - Tarehe aandikapo barua hiyo; Tarehe, mwezi na mwaka. (22 Februari, 2011)
  • Mwanzo wa barua
    • Sehemu hii huonyesha ni nani anayeandikiwa barua k.m. Kwa mpendwa mama/ kaka/ shangazi/mwanangu n.k
  • Utangulizi/Aya ya kwanza
    • Katika utangulizi yafuatayo huorodheshwa:
      - Maamkizi - Kujuliana hali.
      - Pongezi, labda kwa barua ya hapo awali.
      - Msamaha labda kwa kuchelewa kujibu barua n.k.
  • Kiwiliwili/Mwili/yaliyomo (ujumbe)
    • Sehemu hii huchukua nafasi kubwa katika barua ya kirafiki.
    • Katika sehemu hi, mtahiniwa au mwandishi wa barua, hueleza mambo kadhaa kulingana na swali.
  • Aya ya Mwisho/Tamati/Hitimisho (Kwa leo sina mengi. Wasalimie jamaa wote. Ni mimi wako/wenu,
    • Katika aya hii, mwandishi hutoa salamu kwa watu kadhaa; yaani, hutaka watu hao kufikishiwa salamu zake/humwomba aliyemwandikia kumjibu/huwasilisha jambo lolote.
    • Ni vizuri ujumbe kama huo kuongezewa uzito kwa methali murwa k.m. - Ndugu soma kwa bidii kwani elimu ni nguzo aushini; au, jiepushe na anasa kwani mchezea tope huchafuka. n.k.
  • Wasalaam/Jina (wima au mshazari)
    • Sehemu hii huwa inaonyesha aliyeiandika barua hiyo.
    • Sehemu hii hufuata tu pindi baada ya aya ya tamati.
    • Huandikwa kulingana na uhusiano wa mwandishi na mwandikiwa wa barua k.m. dada/kaka yako wa toka nitoke, msena wako wa kufa kuzikana, mwanao wa pekee, mama yako mpendwa n.k.

 

 

 

 



Mfano wa Barua ya Kirafiki

Shule ya Wamahiga, 
S.L.P 17, 
SABASABA.
20-02-2006.

Kwa baba mpendwa,

Zipokee salamu tele kutoka kwangu. Mimi ni mzima na mwenye buheri wa afya.

Lengo la kukutumia barua hii ni kukujulisha kuwa, wanafunzi wote wa kidato cha kwanza watafanya ziara katika kiwanda cha kutengenezea maziwa. Kwa hivyo baba ninakuomba iwapo hali itakuruhusu, unitumie shilingi mia tano. Kiasi hicho kitanitosha kulipia nauli na hata kununulia pamba.

Mbali na hayo, mimi hapa ninazidi kujifunga nira masomoni. Aidha ninazingatia nidhamu. Daima hujaribu juu chini kuzingatia mashauri yako kwani jungu kuu halikosi ukoko. Kamwe sitaki kusafiria mtumbwi wa mfinyanzi.

Tafadhali baba, wasalimie wote nyumbani. Waeleze sina neno na ninawapenda wote. Kwaheri baba mpendwa.

Mwana wako akupendaye,
Tumaini Njeri Kipande.

Join our whatsapp group for latest updates

Download Barua ya Kirafiki - Kiswahili Insha Notes.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest