Muhtasari wa Sura / Mtiririko wa Maonyesho - Mwongozo wa Bembea ya Maisha

Share via Whatsapp

Menyu ya Urambazaji:



MUKHTASARI / Ploti ya Bembea ya Maisha

  • Hadithi hii inafuatilia haswa maisha ya familia ya Yona na Sara. Yona na Sara wana watoto wawili, Neema na Asna. Inapoanza, tunawaona Yona na Sara wakiwa kwa nyumba yao. Mazungumzo yao yanaongelea mila na majukumu yao na ya watoto wao kwao. Sara tunafahamishwa ni mgonjwa. Anaugua ugonjwa wa moyo. Ugonjwa huu umemfanya asiweze kufanya hatakazi za nyumbani kama kupika na kwa hivyo nanasaidiwa na jirani yao kwa jina Dina. Dina huwa huwa na urafiki na Sara. Dina ana mtoto kwa jina KIwa ambaye amekaribiana kiumri na Neema. Kupitia kwa maungumzo ya Dina na Kiwa, tunapata kuyaelewa zaidi yale Sara na Yona wameweza kuyapitia kwa jamii.
  • Sara anapelekwa mjini ili akapate matibabu ya ugonjwa wake na mwanawe Neema. Neema anamsafirisha mjini kwa gari lake, jambo ambalo ni linaonekana la kifarahi kwa jamii yao. Mjini Sara na Neema wanatulia nyumbani kwao ambapo matayarisho ya chakula yanafanywa na yaya, Bela. Bela kwa mara nyingi ndiye anayeshugulikia mtoto wa Sara , Lemi. Kwa sababu ya kazi za Sara na bwanake Bunju hawawezi kushugulikia yote yanayohusu mtoto wao.
  • Ingawa anamshughulikia matibabu, Sara hawezi lala kwa nyumba yao kwa sababu inakiuka mila na desturi zao. Ni jambo ambalo pia mumewe Neema, Bunju, anagusia. Inambidi Sara akae kwa mwanawe mdogo wa Neema , Asna. Asna pia ni msomi kama Neema lakini hajaweza kufanikiwa kupata kazi nzuri. Asna anaishi kwa upweke Fulani. Ameng’ang’ana kujiweka aonekane wa tabaka tofauti ili kuonyesha watu wan je ila hali anayoishi si nzuri sana. Pia, Asna anaogopa ndoa kulingana nay ale anayoyaona kwa ndoa ya dadake na ya mamake. Ingawa Bunju amejitolea kushughulikia famiia ya Neema jinsi anavyoweza n ahata kumwahia uhuru wa kufanya jinsi atakavyo na mshahara wake, Asna anaona bado kamgeuza dadake mtumwa.
  • Kabla ya kumpeleka mama yake hospitalini, Neema anaitisha usaidizi wa kifedha kutoka kwa Bunju. Bunu hafurahishwi na jambo hili kwa sababu amejitolea jinsi anavyoweza na kwa hali ilivyo, hana uwezo wa kuendelea kujitolea kifedha. Majukuu yake yamekuwa mengi mno. Anamjatia Neem ahata kwamba hajamwitisha usaidizi ila amemwachia fedha zake na mshahara wake afanye jinsi atakavyo. Neema anamwelewa Bunju na anampeleka mamake hospitalini kupata matibabu. Sara anashinda akiwapa mawaidha binti zake jinsi ya kuishi. Anamwelewa Bunju na hali yake kwa yote aliyowafanyia na anawaambia Neema na Asna wamwelewe pia. Baadae, Sara anatoka hospitalini na anarudi kwa Asna akingoja safari ya kurudi nyumbani.
  • Siku kabla ya kurudi kwa Sara nyumbani, kunatoa utata kwa nyumba ya Neema. Utata huu unatokea pale Lemi anapotaka kupelekwa kujivinjari naye Neema anamwuliza babake aweze kufanya hivyo kwa sababu yeye atakuwa akimsafirisha mamake kurudi nyumbani. Jambo hili linamkasirisha Bunju kwa sababu hajashughulishwa kwa mipango hii ila yeye anaambiwa tu. Neema anamwomba msamaha na kusema kwamba atakuwa akimshugulisha kwa mipango mengine ya mbele.
  • Nyumbani , naye Yona ameenda kumtembelea rafikizake Beni na Luka. Wanazungumza kuhusu hali ya mabadiliko kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Vizazi kwa sasa havizingatii mila na detsuri zao kama wapasavyo. Yona anaonekana kuwa yeye anaelewa mabadiliko haya na ameyakubali kwa vile anavyonena kuhusu kuelewa hali ya bibi yake na hata kuwathamini watoto wake. Luka anamuunga mkono Yona ila Beni amekwama kwa tamaduni. Yona anawaambia marafiki zake kwamba ikiwa si Sara kuweza kusimamia familia yake alipokuwa ulevini, familia yake haingesimama.
  • Sara na Neema wanaporudi nyumbani, wanampata Yona bad hajafika. Sara anampa mawaidha Neea kuhusu kuishi na bwana yake. Anamwambia jinsi anavyopaswa kutumia elimu na hekima yake ili kubdili maisha yao na maisha ya jamii kwa pole pole. Asubuhi inayofuata, Neema na Sara wanapoamka, wanampata Yona ameshughulikia staftahi. Yona anawaambia kwamba anaelewa hali ya Sara nay a kwamba amejitolea kushughulika zaidi kumsaidia bibi yake na wanakumbatiana.


MTIRIRIKO WA MAONYESHO

Hadithi hii imegawanywa katika sehemu nne. Kila sehemu kimegawanyishwa tena kwa maonyesho.

Sehemu I

Onyesho I

  • Nyumbani kwa Sara, Sara ameketi kwenye kochi baada ya kumeza vidonge vya dawa kwa sababu ya maradhi yanayomsumbua. Yona anayeonekana mchovu na mwenye kukinai anaingia kwa nyumba.
  • Onyesho linaanza kwa kuonyeshwa namna Yona asivyofurahia hali katika nyumba yake. Analalamikia Sara kuwa hajamwandalia chakula. Yona hababaishwi na hali ya Sara ya ugonjwa, haja yake ni chumba kivuke moshi. Sara anamweleza namna mwili wake ulivyo, hapo mazungumzo kuhusu mwana wao, Neema, yanaanza. Yona anatoa wazo lake kwa Sara amwite bintiye aje ampeleke hospitalini. Sara anakataa wazo hilo kwa kukiri kuwa bintiye ana familia yake ambayo anafaa kuishughulikia.
  • Maoni ya Sara yanazua mgogoro baina yake na Yona kuhusiana na mtoto wao Neema. Yona anashikilia kuwa ni jukumu la bintiye kuwajibikia matibabu ya mamake, naye Sara anashikilia kuwa bintiye ana majukumu ya kwake na tayari amewafanyia mengi, kwa hivyo, awachwe apumzike.
  • Mgogoro huu unasawazishwa onyesho linapoelekea kuisha. Sara na Yona wanakubaliana kuwa wanafaa kumpa binti yao baraka zao.
  • Onyesho linamalizika kwa kuonyeshwa Yona akirejelea suala la chakula. Sara anamweleza asubiri kwa kuwa amempelekea Dina salamu aje awafanyie chochote.
Masuala makuu
  • Onyesho hili linakunjua jamvi la mjadala kuhusiana na majukumu ya watoto kwa wazazi wao. Inabainika kuwa katika jamii nyingi watoto wa kiume ndio wanaotarajiwa kuwatunza wazazi wanapozeeka.
  • Inachukuliwa kuwa watoto wa kike walioolewa wanapaswa kupewa fursa ya kushugulikia jamii za kule walikoolewa. Ingawa Neema ni mtoto wa kike, anaonekana kuyamudu majukumu yake kama ambavyo mtoto wa kiume angaliweza kuyamudu. Msemo wa 'kutoa ni moyo usambe ni utajiri' unadhihirishwa na matendo ya Neema. Mazungumzo baina ya Sara na Yona yanadhihirisha kuwa hata ajira za kiwango cha chini kama zile za kufanya kazi shambani na nyumbani pia huwa na changamoto zake. Baadhi ya waajiriwa huwaibia waajiri wao huku wengine wakidhihirisha hali za uvivu na kushindwa kutekeleza wajibu wao kama inavyotarajiwa.

Onyesho Il

  • Onyesho hili linafanyika katika nyumba na Dina. Kima amepitia kumjulia hali na inaanza Dina akitoa vyombo mezani. Kiwa anaonekana kuwa hana hamu ya kula na Dina anamchokoza kwa ajili ya kukosa kula  kwake na pia kwa kukonda. Kiwa anaiwekelea hali hii yake kwa janga la chakula lakini Dina anamwambia kwamba ingali chakula kipo anapaswa ale.

  • Kiwa anajitetea kwamba wakati wa sahi sio misuli inayoongea wala ni akili za mtu n ahata anaingiza binti wa Sara kwa mazungumzo yao, jinsi walivyojikakamua, haswa Neema. Kwa mazungumzo yao, Dina anamweleza  Kiwa kwamba ingawa binti wake Sara wako wazuri na wameimarika, Sara ameteseka sana kwa ajili yao. Kwanza, Sara alijulikana kama tasa kwa sbabu hakuweza kuwapata watoto. Ilifika mahali Yona alianza kuambiwa na watu wengine wa kijiji amtafute bibi mwingine. Kwa bahati, Sara aliweza kuwapata watoto lakini kwa sababu wote walikuwa mabinti, Yona alianza kuingiliwa tena na wana jamii, wakimshwishi amtafute mtoto mvulana hata ikibidi amtafute nje ya ndoa. Maswala haya yalimsikitisha Yona na aliigia ulevini n ahata kuanza kumpiga bibiye Sara kwa yale yaliyowafnyikia.

  • Kwa mazungumzo yao, Kiwa anamwambia mamake Dina kwamba wako na bahati kwa sbabu Kiwa hangejua la kufanya kama mamaye angekumbwa na ugonjwa ule uliomtatiza Sara. Wanazungumza kwa ufupi kuhusu jinsi bado baada ya yote Sara aliyopitia amemtunza bwanake Yona ata kwa ulevi wake. Dina anakatiza mazungumzo na kumwarifu kwamba ameenda kusaida Sara na anamwaga mwanake.

Masuala makuu

  • Onyesho hili linamulika masuala matatu muhimu. Taasubi ya kiume na mila potovu, ukosefu wa ufahamu kuhusu chanzo cha jinsia ya watoto na umuhimu wa bidii maishani. Kulingana na somo la Biolojia, chembechembe za kromosomu zinazofanya uamuzi wa jinsia ya mtoto hutokana na wazazi wa kiume ambao wamebeba kromosomu aina ya Y isababishayo kuzaliwa kwa mtoto wa kiume. Mwanamke hana uamuzi kuhusiana na jambo hili. Hali ya kuwafedhehesha na kuwanyanyasa wanawake kutokana na kuzaliwa kwa watoto wa kiume halina msingi wowote. Tatizo hili linatokana na ubabe dume na taasubi ya kiume. Hali hii inatiliwa mbolea na utamaduni potovu wa jamii kutaka kumrithisha mtoto wa kiume na kumkandamiza mtoto wa kike. Suala la bidii maishani linajitokeza kama kiungo muhimu cha ujenzi wa maisha.
  • Dina anajitolea kuwasaidia Sara na Yona katika kazi za nyumbani kutokana na hali mbaya ya afya ya rafikiye Sara. Tendo hili linadhihirisha udugu na ujirani mwema.

Onyesho III

Onyesho hili linafanyika katika nyumba ya Sara na Yona. Dina anang’angana jikoni kutayarisha mlo. Yona tunafahamishwa kwa mazungumzo ya hawa wanawake wawili kwamba ametoka. Sara anamshukuru Dina kwa kujitokeza kumsaidia kwa hali yake naye Dina anamwabia kwamba kila kinachomfanyikia mtu ni mpango wa Mungu. Dina anamwona Sara kama aliye na Faraja kwa sababu ya jinsi nyumba yake iliyovyo, watoto wasomi na mengie mazuri lakini Sara haoni hayo kwa sababu ya ugonjwa wake.

Wanazungumza kuhusu hali ya Sara na jinsi katika hali yake, Yona huwa si wa usaidizi mkubwa nab ado anategemea Sara aweze kuwajibika kama mke kwa mfano kwa vitu kama vyakula. Licha ya kuwa Yona si msaidizi sana Sara anamtetea kwamba maneno yatakapo toka nje kwamba Yona hushugulika jikoni au nyumbani, itamshusha hadhi yake katika jamii zaidi.

  • Dina anamuuliza kwanini Sara hakuweza kukata tikiti ingawa alipaswa kuenda mjini naye Sara anamwarifu kwamba Neema alikuwa aje kumchukua kwa gari lake waende naye mjini kwa shughuli za matibabu.
  • Onyesho hili linatokea nyumbani kwa Sara, jikoni. Dina yupo katika harakati ya mapishi naye Sara amejikunyata kwenye kibao. Mchuzi u tayari. Sara anamshukuru Dina kwa kufika kumsaidia. Dina anapokea shukrani na kumpa Sara maneno ya kumtia nguvu. Dina anamweleza Sara kuwa kila kitu hufanyika kwa mpango wa Manani. Anamweleza atazame faraja ilivyovuka kwake kwa vile watoto wake wamefaulu maishani. Anampa matumaini kwamba atapona kwa kuwa hospitali ambayo Neema anampeleka ina watalaamu.
  • Mazungumzo ya matumaini yanaendelea kunoga huku Dina akiendelea na mapishi. Dina anauliza Sara alikokwenda Yona na hapo mazungumzo kuhusu mwanamume na utamaduni yanazuka.
  • Tunaelezwa namna utamadumi ulivyowajenga wanaume kama watu wasiofaa kuingia jikoni.
  • Onyesho hili linatimia Sara akimweleza Dina kuhusu mipango iliyopangwa na Neema kuhusu namna atakavyorudi kliniki kupata matibabu.

Masuala makuu

  • Katika onyesho hili inadhihirika wazi kwamba taasubi ya kiume imemtawala Yona na kumfanya kutoona hali ya unyonge wa mkewe.
  • Inamlazimu Sara kuomba usaidizi kwa jirani ndipo waandaliwe chakula ilhali ni kazi ambayo Yona angeifanya bila malalamishi na kuficha siri ya familia yake.
  • Suala la wanaume kutosaidia katika shughuli za nyumbani hutokana na mila na desturi ambazo zinamdhalilisha mwanamke. Mwanamume anapomsaidia mkewe jikoni huona ni kama kwamba hadhi yake imeshushwa.
  • La kutia moyo ni kwamba, ingawa jamii inamdhalilisha mwanamke, ni dhahiri kuwa mwanamke wa sasa amejizatiti na kujiinua na kufikia kiwango cha kutajika. Neema anakuwa mfano mzuri katika jamii kwa kuyabeba majukumu yake binafsi na yale ya nyumbani alikotoka.
  • Anahakikisha mama yake anatibiwa na kumfanya Yona amuonee fahari si tu kama msaidizi bali nguzo muhimu ya kutegemewa hata ingawa ni mtoto wa kike, tena aliyeolewa.
  • Umuhimu wa ujirani mwema pia unazungumziwa. Dina anajitokeza kuwa jirani na rafiki wa kutegemewa wa Sara. Ni wazi kuwa Sara na Yona wanaishi vizuri na majirani wao.

SEHEMU II

Onyesho I

Onyesho hili linafanyika nyumbani mwa Neema , mjini. Neema na mamake, Sara, wameketi ukumbini. Wote wana vipepeo mkononi na wanajipepea kwa mara kwa mara. Wanazungumza kuhusu joto na kuhusu hali ya maisha, Neema akisema kwamba yale yote mtu anayotaka mazuri lazima ajikakamue aje mjini. Sara anaonesha hisia za kuchoka , jambo linalomfanya Neema kumwita Bela, mfanyi kazi wake kujua kama chakula kiko tayari. Pia anamuuliza kuhusu mwanawe, ambaye hajafika nyumbani hadi kwa wakati huo na anafahamishwa kwamba walikuwa na shughuli za michezo na kujiandaa walizokuwa nazo shuleni. Neema anamaka kwamba mamb ni mengi na Sara anamshauri kwamba yamekuwa mengi na kwamba anapaswa kufurahi kwa kuweza kumpata mtoto mapema, jambo lililo mletea shida sana.

  • Wanazungumza kuhusu yale Yona alimpitisha Sara. Sara anamweleza Neema jinsi ilivyobidi aweze kupambana na hali ilivyokuwa, na hata kukubali hali ya maisha ilivyo. Licha ya yote aliyopitia, anaendlea kumtetea Yona akisema kwamba haikuwa rahisi kwake kutoka kuwa mwalimu hadi kuwa mlevi. Katika mazungumzo yao tunapata kujua hali ya kudhoofika kwa afya ya Sara ilisababishwa na yale Yona alimpitisha. Sara anaendela kumpa mawaidha Neema kuhusu kuishi maisha yalivyo kuwa akieleza kwa mfano wa kutumia bembea kwamba iwe Kamba au chuma ameweza kukubali hali yake ilivyokuwa. Baadae Bela anawaletea chakula.

Tathmini

  • Kupitia kwa mazungumzo haya, masuala kadhaa yanajitokeza yakiwemo maeneo ya mashambani yaliyopuuzwa kimaendeleo, bidii maishani, taasubi ya kiume pamoja na athari za uraibu wa pombe. Usemi 'mrina haogopi nyuki,'(uk. 18) unaotumiwa na Sara unaelezea bidii inayohitajika ili mtu afaulu maishani. Kwamba, sharti mtu akabiliane na magumu anayokumbana nayo. Sara anayasema haya anapogundua kuwa Lemi ana kazi nyingi za kufanya huko shuleni. Kwa sababu ya kazi hizo, inakuwa vigumu kwa Sara kuonana na mjukuu wake.
  • Suala la uwajibikaji miongoni mwa wanasiasa linajitokeza pia. Suala hili linaangaziwa kupitia usafiri unavyotatizwa na miundo misingi duni katika sehemu za vijijini.
  • Inabainikakwambayonaanajitokomezaulevinikutokananamsukumo wa wanajamii kwa kukosa kuzaa mtoto wa kiume. Huu ni utamaduni uliopitwa na wakati. Pombe inakuwa kimbilio la kumsahaulisha malengo aliyoshindwa kuyafikia. Sara anasisitiza kwamba wazazi wana wajibu wa kumlea mtoto wa jinsia yoyote ile bila ubaguzi.

Onyesho Il

Onyesho hili linafanyika siku ya mbili baada ya onyesho I katika nyumba ya Neema bado. Neema amewasili nyumbani na kumpata Bela akiwa kazini. Anavyowasili anamjulia hali na Bela pia anamfahaisha kwamba mwanawe amelala. Aidha, anamfahamisha kuhusu yale yanayoendelea shuleni. Kwa mazungumzo yao, tunapata kujua hii ndiyo hali yao kwa wakati mwingine. Neema anapoenda kazini asubuhi , ni mapema sana na anaporudi, hupata mwanawe amelala , kwa hivo huwa hawaonani sana, jambo linalomsikitisha Neema. Bela anamwarifu kwamba hilo si jambo mbaya sana kwa sababu kulinagana na kazi yake, hajaweza kuwaona watoto wake wakiwa wakubwa na hata sasa wamefikia mahali pa kuhama.

Kwa mazungumzo yao pia, tunapata kujua kumenyesha, jambo lililosababisha msongamano mdogo wa magari na kwamba pia Sara amepelekwa kwa dadake Neema, Asna kwa sababu hawezi kubali kulala kwa sababu jadi hazikubali. Wanaongea kuhusu jinsi mila hizi zimepitwa na wakati na baada ya kuzungmza ya kujitayarisha ya siku itakayofuata, wanaagana na kuenda kulala.

  • Onyesho hili linafanyika nyumbani kwa Neema akiwa na Bela, mfanyakazi wake.
    Kupitia mazungumzo yao inabainika kwamba maisha ya leo yana changamoto nyingi kiasi kwamba wazazi hawatangamani na watoto wao jinsi inavyotakikana. Hali hii inaonekana kuwakera wazazi.
  • Suala la shughuli nyingi kazini linaonekana kuhitilafiana na shughuli ya malezi.
    Katika sehemu hii inabainika kuwa Neema haonani na Lemi kwa sababu kila afikapo nyumbani mtoto huwa amelala.
  • Suala la mila pia linaibuka. Wazazi wa Sara hawawezi kulala kwa mtoto wao aliyeolewa. Neema analizungumzia jambo hili kwa mshangao. Hili ni jambo la kutatiza kwa sababu mara kwa mara mamake Neema huenda mjini kwa shughuli za matibabu na huwa anahitaji mahali pa kulala.
  • Isingekuwa kwamba Asna anaishi mjini na kwamba anaweza kumuauni mamake, basi ingempasa Neema kumkodishia chumba mamake, jambo ambalo Kiafrika ni makosa. Suala la utandawazi linajitokeza na ni dhahiri kwamba baadhi ya mila zimepitwa na wakati na zinapaswa kutupiliwa mbali kama Bela anavyoeleza:
  • Hayo ni ya kale...na ya kale hayanuki. Wengi hawafuati tena mila hizo.
    Walimwengu sasa wanavaa sare moja (uk. 24). Kauli hii inaonyesha namna mabadiliko ya kijamii yamefanya baadhi ya mielekeo ya kitamaduni kupuuziliwa mbali.

Masuala makuu

Sehemu hii inadhihirisha jinsi hali za maisha ya kisasa zinavyowatatiza wanajamii. Wanalazimika kufanya kazi mchana kutwa ili kujikimu na kuzifaa familia zao. Matokeo ni kwamba hawapati nafasi ya kutangamana na familia zao ipasavyo. Ni bayana kwamba bado wanajamii wamefungwa na mila ambazo kwa hakika ni vigumu kuzitii kwa sababu ya maisha ya kisasa. Mfano mzuri ni miko inayowazuia wakwe kutolala katika makaazi ya wana wakwe zao.

Onyesho Ill

Onyesho hili linafanyika siku mbili baada ya onyesho la pili. Inafanyika masaa ya asubuhi sebuleni mwa nyumba ya Bunju na Neema ambapo Bunju anajitayarisha kuenda kazini. Bunju anaanza na kumuuliza Neema kama Lemi ameamka na anaarifiwa kwamba bado hajaamka. Bunju anaona ya kwamba Neema anamdekeza mtoto wao sana. Wanaongea kuhusu matokeo yake ambapo Bunju hafurahishwi na nambari Lemi alikuwa kwa mtihani licha ya alama zake kuongezeka.

Neema anajaribu kuongea na Bunji kuhus matibabu ya mama yake pia. Bunju hafurahishwi nakuwekelewa jukumu hili. Anasema kwamba amewekelewa majukumu mengi na ameweza kuyafanya yote kama mumewe Neema. Anamkumbusha Neema kuhusu kuwajengea wazazi wake, kumnunulia gari, kulipa karo ya Lemi na Mina na pia ya dadake Asna na kusema kwamba hana uwezo ya kuongezewa majukumu mengine. Neema amamwelewa na anakubaki yale anayoambiwa. Anajaribu kuongea na Bunju kuhusu mamake kukaa nao naye Bunju anakataa kwa kutajia mila ambazo hazikubali jambo kama hilo kufanyika. Bunju anaondoka na kumwacha Neema akiwa mawazoni.

Lemi anaamka na kumwita mamake na Neema anagutuka kutoka kwa fikira zake. Lemi anamjulia mama yake hali na anamuuliza maswali kuhusu kazi na Neema anamjibu kisha anamwambia ajitayarishe ile aende shuleni.

  • Katika onyesho hili Bunju yuko tayari kuondoka kwenda kazini asubuhi.
    Mazungumzo na mkewe Neema yanahusu matokeo ya mitihani ya Lemi, mtoto wao. Huku Neema akionekana kuridhishwa na matokeo hayo Bunju anamtaka Lemi kujitahidi zaidi ili apate matokeo ya kuridhisha zaidi. Mgogoro baina ya wazazi kuhusu masomo ya watoto wao unajitokeza. Hali ya Neema na Bunju kutokubaliana kuhusu bidii ya mtoto wao inaweza kuzua msukosuko.
  • Neema anapomwelezea Bunju kuwa mamake tayari ameshafika mjini kwa matibabu, anakataa kutoa pesa za kusaidia matibabu hayo. Bunju anadai kuwa ana majukumu mengi. Kwamba anagharamia mahitaji yote ya nyumbani, yakiwemo karo ya shule, kodi ya nyumba na amemnunulia Neema gari.
    Anamtaka Neema awajibike kwa sababu amemruhusu kutumia mshahara wake kwa mahitaji ya familia yake.
  • Bunju anasisitizia ile dhana ya kutomruhusu mama mkwe kulala nyumbani kwao. Mila na desturi hizo zinamkera Neema sana. Kwa Neema, hizo ni mila na desturi zilizopitwa na wakati.

Tathmini

  • Onyesho hili linazungumzia mambo muhimu ya kifamilia, hasa malezi na elimu. Neema anaridhishwa na matokeo ya mwanawe, ila Bunju anamtaka Lemi aongeze bidii masomoni. Hayo yakijiri, inaonekana kana kwamba ni Neema pekee anayejitahidi kushughulikia matakwa ya Lemi shuleni. Bunju analipa karo na kutekeleza majukumu mengine ila kazi yake imembana hadi hana muda wa kutangamana na familia yake ipasavyo. Mfumo wa uchumi umewagandamiza raia na kuwalazimisha kufanya kazi masaa mengi kupindukia.
  • Mfumo wa elimu unawapa watoto shinikizo la kujibidiisha zaidi masomoni, jambo ambalo linaweza kusababisha msukumo wa kiakili miongoni mwa watoto. Ni bora wazazi wakiwa na msimamo mmoja kuhusu masuala yanayohusu elimu ya watoto wao.
  • Mchango wa mwanamke katika ndoa unamulikwa. Bunju analipa kodi ya nyumba, karo na hata kamnunulia mkewe gari. Je, mchango wa mkewe katika majukumu ya kifamilia ni upi? Ni muhimu mwanamke anayefanya kazi kuwekeza kiwango fulani cha pato lake katika mali ya familia ili kupata heshima na pia kama njia mojawapo ya kujifunza kuimudu familia ikiwa ataondokewa na mumewe mapema.

Onyesho IV

Onyesho hili linafanyika nyumbani mwa Asna. Mwandishi anatupa maelezo ya nyumba ya Asna inavyokaa. Ni nyumba ndogo yenye chumba kimoja. Asna hana mali nyingi ila vitu vidogo vidogo. Kulingana na Sara, maisha ya mjini kama haya yana mashida mengi. Sara na Asna wanazungumza kuhusu maisha ya mjini. Sara anapoangalia maisha ya Asna, anaona afadhali ya kijijini ila Asna anaona afadhali yake ya mjini anayoisha ingawa si mazuri kwa sababu yanatamaniwa na watu wengi. Nyumba yake ingawa ni ndogo nalipiwa kodi ya nyumba mbili za mitaa zingine. Kukonda kwake ndio urembo, jambo linalomshanganza Sara sana. Sara anamtajia kwamba pia angetaka leso, ishara ya kwamba angemtaka Asna aolewe.

Neema anawasili nyumbani mwa Asna. Wanajuliana hali na Sara anamuuliza jinsi Bunju alivyo. Asna anasema kwamba Bunju anajaliwa sana na mamake, Sara. Kwa mazungumzo yao Asna anataja sbabu moja yake ya kutotaka kuolewa ni kwamba nyumba ingegeuka kambi ya jeshi, na masharti yake. Neema anamwambia mamake Sara kwamba Asna anangoja mwanaume aliye safi kama pamba, aliye kamili. Sara anaongezea kwa kusema kwamba kwa yale Bunju amefanya yeye ni malaika. Asna anaingilia na anasema kama Bunju ni malaika basi hiyo ni utumwa. Neema anasema kwamba hiyo si utumwa kwa sababu amewachiwa mshahara wake afanye jinsi atakavyo nayo. Bado Asna na Neema lakini wanaona shida na mila ya kwamba Sara hawezi lala nyumbani kwa Neema. Neema anamwambia mamake Sara kwamba wanapswa kuondoka kuenda hospitalini.

  • Mjini, nyumbani kwa Asna. Asna anamwandalia mamake kiamshakinywa. Mama mtu anashangaa mbona bintiye anaishi katika chumba kidogo. Bintiye anajitetea kuwa chumba hicho kiko katika mtaa wa kifahari na anakifurahia. Sara analinganisha maisha ya mjini na ya kijijini na kuona kuwa yale ya mjini yanaudhi, afadhali ya kijijini.
  • Anasema kwamba, watu wa mjini wako mbioni kila wakati na mapato yao ni haba.
    Asna hakubaliani na mamake; kwake, kiwango chake cha elimu hakimruhusu kwenda kukaa kijijini.
  • Sara anamsihi Asna aolewe amletee mjukuu. Asna hakubaliani na jambo hilo.
    Kulingana na Asna, ndoa ina matatizo mengi kama yale anayopitia Neema, dada yake, ambaye ingawa amesoma na kupata shahada mbili, hazimsaidii kupigana na msimamo wa kitamaduni alionao Bunju, mumewe. Badala ya kupigania mabadiliko ya msimamo wa Bunju, Neema anaonekana kuukubali kwa sababu ya uhuru wa matumizi ya mshahara wake aliopewa na Bunju.
  • Utepetevu kazini unazungumziwa kupitia madaktari na utendakazi wao. Baadhi ya madaktari daima wako mbioni kutoka hospitali moja hadi nyingine ili kuchuma hela za ziada bila kuwazingatia wagonjwa wao kikamilifu.

Masuala makuu

  • Kuna mambo muhimu yanayojadiliwa katika onyesho hili. Jambo la kwanza ni hadhi. Ile hali ya kutaka kuishi sehemu za kifahari hata ingawa pato ni dogo. Asna anaishi maeneo ya juu ingawa mazingira ya nyumba yake ni duni.
    Anajikakamua kulipa kodi ya juu ya nyumba bila kujali mazingira anamoishi.
  • Jambo la pili linaakisi athari za elimu ya juu dhidi ya mila na desturi za Kiafrika.
    Inasahaulika kwamba,elimu pekee bila uelewa haiwezi kubadilisha dhana na fikra za kitamaduni. Bunju ana elimu lakini elimu yake haijamtoa katika mila na desturi za jamii yake. Neema ana elimu lakini haimsaidii kuelewa chanzo cha mila na desturi za Bunju. Jambo la tatu ni kutosheka kwa mwanamke. Neema anaonekana kutosheka na hali ya mumewe ya kumruhusu kutumia pesa zake atakavyo. Hafikirii kuwa huenda ikawa ni mtego. Mara nyingi mwanamke anapopata uhuru wa aina hii, huweza kubugikwa na akili asiweze kufikiria kuwekeza kwa ajili ya maisha ya baadaye. Kisha mambo yanapoharibika hujikuta hana lolote la kutegemea.

Sehemu III

Onyesho I

Onyesho hili linafanyika nyumbani mwa Neema. Neema amejishughulisha na usafi wa nyumba lakini pia ako mawazoni kuhusu malipo ya hospitalini ya mamake Sara. Bunju anapoisngia , Neema anashtuka. Wanajuliana hali na Bunju anampongeza Neema kwa sababu ya nyumba ilivyo. Mazungumzo yao yanaingia kwa ya fedga, jambo lisilomfurahisha Bunju kwa sababu amejitolea yote anavyoweza ila anaona Neema hana shukrani. Wakat huu, Neema aanataka mkopo ili kuwesza kushughulikia malipo ya hospitalini alikolazwa mamaye. Bunju anamweleza kwamba hawezi kumkopesha kwa sababu hana pesa na pia yeye mwenyewe ana madeni mengi ambayo anang’ang’ana nazo kuzilipa. Bunju anaamka ilia toke na kumwambia kwamba ameenda kuonana na rafikiye waliyesoma naye shuel ya upili ili amsaidie kwa jambo Fulani na huenda hata anaweza lipwa. Jambo hili linamfanya Neema kuona kweli kwamba Sara alivyosema kwamba Bunju ni kama ndugu yao hakukosea kwa sababu amejitolea jinsi awezavyo kuwasaidia kwa hali yao. Onyesho hili linafungwa kwa maneno ya Neema anapozingatia walivyokutana na Bunju, aliye mwokoa kutoka kwa ajali.

  • Nyumbani kwa Neema na Bunju. Neema yuko nyumbani anafanya usafi.
    Anafikiria jinsi ugonjwa wa mamake ulivyomfanya fukara. Bunju anapoingia chumbani, Neema hamsikii, anashtuka. Kwa mara nyingine, anakataa kumsaidia Neema kugharamia ugonjwa wa mamake.
  • Anasema kwamba anafanya majukumu yote ya pale nyumbani na haoni ni kwa nini Neema hawezi kuupangia mshahara wake ili uweze
  • kuyakidhi mahitaji yake. Neema anahuzunishwa na msimano wa Bunju lakini pia anakumbuka maneno ya mamake kuwa Bunju ni zawadi kwake, jambo ambalo linampa heri kidogo.

Masula makuu

  • Onyesho hili linampa msomaji au mtazamaji nafasi ya kuelewa mahusiano katika taasisi ya ndoa. Wanandoa hao wawili wanashikana mkono kuendeleza maslahi ya jamii yao. Mume anaheshimu rai ya mkewe ya kutumia hela zake kushughulikia wazazi wake ambao ni wahitaji.
  • Mama ni mgonjwa na baba yake amepoteza ajira. Tofauti ya matumizi ya pesa kati ya mwanamke na mwanamume yanajitokeza. Mwanamume anajenga na mwanamke anapamba. Mambo yanapoharibika, mwanamke huachwa bila makao kwa sababu ya dhana kuwa hakuwekeza katika
  • ujenzi wa nyumba. Hili ni jambo linalohitaji mjadala zaidi. Bunju anajitokeza kama mwanamume anayefanya majukumu yote ya kifamilia, hali ambayo haimtayarishi mkewe kwa maisha ya baadaye iwapo mambo Kuna pia suala la matumizi ya pesa ili kutibu magonjwa. Familia nyingi yataharibika. hazina bima ya matibabu. Magonjwa yanapobisha hodi basi huziacha baadhi ya familia hizo katika hali ya umaskini. Wengi huitisha michango kama Neema anavyoitisha msaada kutoka kwa Bunju.
  • Katika mazungumzo yao, pia inadhihirika wazi kwamba mapato ya kazi moja hayatoshi kamwe. Umuhimu wa kujishughulisha zaidi ili kuweza kuyamudu mahitaji unajitokeza.

Onyesho II

Onyesho hili linafanyika baadae hospitalini ambako Sara amelazwa. Ametembelewa na Neema na Asna. Sara anasifu hospitali hiyo kwa kuwa na huduma nzuri. Anaisif an akusema kwamba hata kitanda na mlo ni mzuri kuliko za hoteli. Wanalinganisha hospitali za nyumbani kwao na seli kwa huduma. Sara anamuuliza Neema kuhusu hali ya mwanawe Lemi. Sara anamsifia Lemi kwa vile amekuwa mkubwa na kwa kumanika kwake kiakili. Sara anazungumzia hisia zake za kurudi nyumbani. Kwanza, anasema kwamba malipo ya hospitali si ya oesa kidogo. Pili,anataka kwenda kushugulika nyumbani kwa kazi zake na kumshugulikia bwanake, Yona. Kulingana naye, si taswira nzuri kwa wazee wengine wa kijiji kumwacha Yona ajifanyie kazi za nyumbani ila yeye ametulia na hata kulisha huku aliko. Sara anamwulizia kule Bunju ako na anaarifiwa kwamba amekimbia kuenda shugli. Kwa Asna, huu ni ukosefu wa adabu. Anamwona Bunju kama aliytemkosea Sara heshima na kama anamgeuza Neema mtumwa. Anaona kwamba Bunju hataki huwasaidia kwa hali yao ila yeye ana pesa lakini Neema na Sara wanamkosoa. Neema anamtetea bwanake, Bunju, kwa kusema kwamba sio kupenda kwake kuwa vile alivyo bali ni jinsi alivyolelewa. Anaeleza kwamba Bunju ni kitindamimba na kwa hivyo wazazi wake walishughulikiwa na ndugu zake wakubwa ila hajaelewa kwamba Neema ndiye mtoto wa kwanza na shugli za kuwashugulikia wazazi zinamwangukia yeye. Neema anamwambia Asna kwamba hataki wakosane bure na anamwambia pia mamake hataki amweke hatarini kwa sababu ni mvutano hizi za kifamilia ambazo zimemfanya kuwa mgonjwa. Onyesho hili linaisha na Sara na Neema wakiondoka kwenda kulipa bili ya hospitali.

  • Sara yuko hospitalini ambako amelazwa. Neema na Asna wamefika kumwona. Sara anataka kuruhusiwa kwenda nyumbani kwa sababu gharama ya hospitali inaendelea kupanda. Sara analinganisha huduma za matibabu za kule kijijini na za mjini. Hospitali za mjini ni kama hoteli ilhali za kijijini ni kama seli ambako mtu akilazwa hata matumaini ya kupona hudidimia.
  • Sara anataka atoke hospitalini arudi kijijini kwenda kumsaidia Yona ambaye alimwachia kazi zote za nyumbani. Bunju anafanya shughuli zake bila kupita hospitalini kumjulia hali Sara. Jambo hili linamkera Asna ambaye anamwona Bunju kama mchoyo na asiyewajibika kuhusu mkwe wake. Neema anamtetea Bunju.
  • Anasema kwamba tabia yake inatokana na jinsi alivyolelewa, kwa hivyo wasimlaumu.

Masuala makuu

  • Mazungumzo haya yanaibua mambo matatu muhimu kuhusu hospitali aliyope´lekwa Sara. Mosi, malazi na chakula ni vya hali ya juu. Pili, gharama ya huduma ni ya juu mno. Tatu, hospitali hiyo ina aina nyingi za wataalamu. Hali hii inakinzana na hali ilivyo katika baadhi ya hospitali nchini ambazo ni duni na hutoa huduma mbovu zinazomfanya mgonjwa kutamauka na kukata tamaa.
  • Hospitali za kibinafsi hutoa mazingira mema zaidi ya kimatibabu na ni mwafaka zaidi kwa wale wanaoweza kulipia gharama zake, Mazingira ya hospitali za umma ni duni, nyingi zikiwa hazina huduma bora, hazina madaktari na hata dawa za kutosha.
  • Pia, mwanamume angali anapewa hadhi ya juu kuliko mwanamke. Jamii haimruhusu mwanamume kufanya kazi za jikoni kwa sababu kazi hizo huchukuliwa kuwa ni za kike. Ndiposa, ingawa Sara angali mgonjwa, bado ana ari ya kurudi nyumbani kumshughulikia Yona, mumewe.
  • Bunju amechorwa kama mtu asiyemjali mama mkwe. Ingawa Neema haridhishwi na hali hiyo, anashindwa kumkabili na kusingizia malezi.
  • Heshima anayopewa mwanamume na mwanamke katika onyesho hili, inawekwa kwenye mizani.

Onyesho III

Onyesho hili linafanyika katika nyumba ya Neema na Bunju. Neema anamsaidia Lemi katika masomo kisha Lemi anaanza kumwuliza mamke maswali kama wataenda kujivinjari. Neema anamwambia kwamba hataweza kwa sababu atakuwa akimpeleka bibi yake, Sara, nyumbani. Lemi anamwuliza kwanini ingawa ametoka hospitalini hakuja kumsalimia na inabidi Neema amdanganye kwamba alikuwa amechoka. Neema anamkumbusha Lemi kwamba hakuwa ameosha hanchifu yake ili kumfanya aondoke pale. Neema anamwuliza Buju kama ataweza kumpeleka mtoto kujivinjari na Bunju anamgeuka Neema tena. Bunju anaonekana kuwa amekasirishwa. Neema anamwomba Bunju amweleze nini kinachomkula akili na Bunju anasema kwamba licha ya kujitolea kumpa Neema uhuru wake, Neema amezidi kumwongezea majukumu kufikia mahali ni kama yeye si mwanaume. Hashugulishwi hata kwa mipango ya Neema ila yeye huambiwa tu kile walichopanga. Neema anajieleza kwake Bunju kwamba hilo halikuwa nia yake na anamwambia kwamba ataanza kumshugulisha kwa maamuzi yao ya kifamilia. Bunju anamkumbusha Neema jinsi alivyompata akiwa mahututi. Jambo hili linamhuzunisha Neema anapoanza kumbukumbu za jisi hali yake ilivyokuwa. ONyesho hili linaisha na Neema akilia na Bunju anaamkana kumkumbatia akimbembeleza.

  • Neema anamsaidia Lemi katika masomo yake. Lemi analalamika kwamba kwa muda mrefu wazazi wake hawajampeleka ziara. Neema anamweleza kuwa hataweza kumpeleka ziara kwa sababu anamrudisha bibi kijijini. Lemi haelewi ni kwa nini bibi yake hakuja kumsalimia.
  • Neema anamwomba Bunju ampeleke Lemi kwenda kuogelea kwa kuwa yeye anapanga kumrejesha mama yake nyumbani. Bunju anakataa kwa sababu ya gharama na pia anasema anaenda kutafuta riziki. Analalamika kuwa Neema mara nyingi yuko nje kikazi na anamwachia majukumu yote ya nyumbani.
  • Bunju analalamika kwamba hakujulishwa kuwa mama mkwe ametoka hospitalini na kwamba atasafirishwa kijijini. Neema anamwambia Bunju kuwa mkewe hakutaka kumsumbua na mambo ya kwao nyumbani.
  • Kulingana na Bunju, Neema ameanza kumdharau. Bunju anamkumbusha Neema alivyokuwa mahututi wakati alipompata. Suala hili linamhuzunisha Neema hata anaanza kulia. Bunju anamhurumia na kumwambia atulie asilie mbele yake.

Tathmini

Katika onyesho hili, suala la mivutano baina ya wanandoa kuhusu majukumu ya familia yao linajitokeza. Ni bayana kwamba suala hili linahitaji tahadhari ili lisiwe chanzo cha mafarakano katika ndoa. Pia, kuna suala la gharama za kulea watoto. Ni lazima wazazi wawape muda wana wao kama Neema anavyomsaidia Lemi na kazi za shule. Lakini pia kuna gharama nyingine za kuwafurahisha watoto ambazo zinahitaji pesa na mara nyingi pesa hizo hazipo. Kwa hivyo, ni lazima kuwe na maelewano baina ya wazazi na watoto kuhusu mambo hayo ili kusiwe na mikurumbano. Ni vyema pia wazazi kuwaeleza watoto kuhusu gharama hizo ili wazielewe mapema. Onyesho hili linatukia nyumbani kwa Asna. Sara na Asna

Onyesho IV

Onyesho hili linafanyika jioni ya siku hiyo ya onyesho III. LInafanyika nyumbani mwa Asna. Asna na Sara wamo katika mlo na Sara anamsifu Asna kwa upishi wake. Asna anamweleza mamake kwamba akiwa pkee yake hapendi kupika na anajitetea kuwa ni hai ya kuwa tomboy, kwa maelezo yake: kuishi kama mvulana. Sara anamwambia kwamba ujana ni moshi na kwamba bado angetaka kumwona Asna ameoa. Asna anamweleza mama yake kwamba kwa kuna ndoa yake na ya Neema, amekuja kuogopa ndoa. Sara anamkosoa kwamba licha ya ndoa zao kuwa na doa, Asna anapaswa kujifundisha kutokana na yale anayoyaona. Kwa mazungumzo yao, Asna anamtaja tena Bunju na kusema yeye hajui maana ya familia na Sara anamwingilia tena kuteta ndoa ya Bunju na Neema. Asna anamwambia mamake kwamba angetaka angekuwa wakili naye mamake anamwambia kuwa akili walizo nazo wamepata kutoka kwake. Asna anasema kwamba akili zao sio kama za watoto wa Dina na Sara anawatetea kwamba wanazo hekima ingawa masomo iliwalemea. Asna anapojaribu kutaja jinsi walivyokuwa maskini kitambo, Sara anamweleza kwamba pia wao walikuwa maskini. Sara anataja umaskini wa aina tatu. Kwanza ni umaskini wa watoto, kisha umaskini wa mrithi na umaskini wa kifedha. Anamwambia kwamba licha ya umaskini wao, waliweza kufarijika na ndio maisha yalivyo. Mlano mja ukifungika, mwingine unafunguka.

  • wanazungumza. Mazungumzo ya mama na bintiye yanagusia masuala mengi. Inabainika kuwa Asna hana imani na ndoa. Anaridhika na maisha ya kuishi bila mume ingawa amefikia umri wa kuolewa. Kulingana na Asna, ndoa ya Neema ina doa. Hii ni kwa sababu Bunju ni bahili na hapendi wazazi wa Neema walale nyumbani kwake. Pili, anaonelea kuwa, Sara pia aliteseka sana katika ndoa yake. Hata ugonjwa alionao ulitokana na kero za Yona, baba yao. Asna anaamua kuishi nje ya ndoa kwa sababu ya mifano ya ndoa hizo mbili zisizoridhisha. Katika onyesho hili, Sara anapata muda wa kumzungumzia Asna masaibu ya ndoa yake na babake na jinsi yalivyoanza.
  • Sara na Asna wanazungumzia juhudi za Dina na wanawe ambazo zimewasaidia kujitoa katika lindi la umaskini. 

Masuala makuu

  • Kulingana na Asna, taasisi ya ndoa ina uwezo mkubwa wa kumletea binadamu shida nyingi. Anamweleza mama yake kwamba msongo wa moyo alionao unatokana na matatizo yaliyo katika ndoa yake. Pia, anaona kuwa ndoa ya Neema ina matatizo.
    Kwamba Bunju ni mchoyo na hajali ugonjwa wa mama yao, hali inayomfanya Neema kutokuwa na raha katika ndoa yao. Mifano hiyo miwili inamfanya Asna kutoridhishwa na asasi ya ndoa na hivyo, kuikinai. Lakini Sara anamweleza kuwa ingawa ndoa huwa na changamoto nyingi, uvumulivu huwasaidia wanandoa kukabiliana na changamoto hizo.
  • Kulingana na Sara, bidii ni silaha inayoweza kumkomboa mwanadamu kutoka umaskini. Familia ya Dina inatumika kama mfano wa familia ambayo awali ilikuwa maskini lakini ikafaulu kujinyanyua kutoka hali hiyo ya umaskini na kujikimu ipasavyo.
  • Sara anamweleza Asna kuwa hata yeye (Sara) na mumewe Yona walikuwa maskini lakini hawakusita kufanya bidii. Waliungana katika juhudi zao ili kujimudu katika kuwatunza na kuwasomesha watoto wao hasa wakati Yona alipopoteza kazi yake ya ualimu. Hatimaye, watoto wao waliweza kuhitimu hadi Chuo kikuu. Inamsikitisha kuwa wanajamii bado waliwachukulia kuwa maskini wa kutojaliwa kupata mtoto wa kiume hata baada ya kufanya juhudi hizo zote. Suala la unyanyapaa dhidi ya familia za walevi linajitokeza pale ambapo familia ya akina Asna inadharauliwa na kunyimwa hadhi katika jamii kwa sababu ya ulevi wa Yona.

Sehemu IV

Onyesho I

Onyesho hili linafanyika nyumbani kwa Luka. Luka ni rafikiye Yona. Wanashiriki chakula cha mchana pamoja na rafiki yao Beni. Walikutana kwa nia ya kusherehekea mazao ya kwanza. Mazungumzo yao yanaanza yakizingatia mila na desturi zao na jinsi ambavo vizazi vya sasa havizingatii mila na desturi zao. Wanawaona kama wamewacha mila zao. Wanatoa mifno kama vile kulazzimika kuongea Kiswahili na kiingereza na wajukuu wao wakiwa nyumbani na ia watoto hao kukosa kujua tofauti ya wanyama kama mbuzi na kondoo. Wanatilia shaka malezi ya mjini ambao wanataja pia kwamba wazazi hawapati kuwalea watoto wao wenyewe ila ni yaya wanatawala nyumba. Yona anaonyesha kuelewa mabadiliko amabayo kwake hayana budi ila kufanyika na inapswa wazikubali. Kwake, afadhali maisha hayo ya mjini ya kutafuta kuliko umaskini wao.

Yona anawaambia kwamba kwa mabadiliko watoto wa kike wanaweza kusomeshwa n ahata kurithi mali, jambo lisilo la kawaida kwa mila zao. Nafasi ya mtoto wa kike kimepanuka na hata thamani yake kupanda. Beni anamwuliza kama ni hao watoto wake wa kike na Luka anamkatika kwa kumwambia kuwa watoto wao wa kiume hata hawawafikii hao wa Yona wa kike. Luka anampongeza Yon akwa kujitolea kuwasomesha watoto wake wa kike. Watoto wa Yona wamewaeka raha kwa yale wanayofanya kama kujiimarisha maisha kufikia kwa kuendesha gari. Beni anajaribu kumkosoa kwa kumwambia kuwa si wao tena na anajaribu kuwaambia kwamba Yona amewachwa pekee yake kujilisha ilhali wamemchukua bibi yake na kumweka mjini aishi na wao. Yona anaonyesha kuwa anaelewa mambo yalivyo kwa kumwambia kuwa Sara yuko mjini kwa sababu ya matibabu ambayo watoto wake ndio wanashugulikia. Kulingana na Beni, mwanaume hapasi kujipikia lakini kwa maoni ya Yona na Luka, ya muhimu ni nafuu.

Wanazungumza kuhusu ujana wao ambapo Yona anato kumbukumbu yake akiwa mwalimu alivyokuwa mkali hadi wakati alipopoteza kazi kwa ulevi. Na alipoppoteza kazi, Yona anakiri kwamba ikiwa si kwa Sara kuangalia familia, hangekuwa na familia. Anaringa kwamba hata sasa Sara ako kwa watoto wake, jambo analosema ndio uzuri wa kusomesha. Beni anamwingilia kwamba anajigamba kama wake pkee ndio waliosoma naye Luka anamtania kwamba wake anafanya kazi kiwandani ila Beni anakwamilia kuwa yeye ni injinia. Beni anaonekana kukasirikwa kwa utania nayofanyiwa na Luka anamwuliza mbona ila yeye ndiye aliyekuwa wa kwanza kumwingilia Yona. Onyesho hili linaisha wakinywa huku wakibariki mashamba, mimea na vizazi vyao.

  • Kijijini nyumbani kwa Luka. Luka anawakaribisha Beni na Yona kwa sherehe ya kufurahia mazao yake. Beni anazungumzia jinsi watu walivyozitupa mila zao kabisa. Anasema kwamba vizazi vijavyo havitakuwa na mila na desturi. Katika mazungumzo yao, wazee hao watatu wanakubaliana kuwa vizazi vya siku hizi vinafikiria kuwa uzungu ndio ustaarabu. Jambo hilo linatokana na malezi ya mjini ambayo mara nyingi yameachiwa wafanyakazi wa nyumbani. Wazazi wanaraukia vibaruani asubuhi na kurudi usiku watoto wakiwa wameshalala.
  • Luka anawakumbusha wenzake kuwa mila za zamani hazikuwaruhusu watoto wa kike kwenda shuleni wala kurithi mali ila walitegemea usaidizi wa waume zao. Lakini anakubali kuwa thamani ya mtoto wa kike imepanda na nafasi yake kupanuka. Watoto wa kike wa Yona wanamulikwa katika mazungumzo haya. Japo walidharauliwa hapo awali, sasa wamekuwa nyota ya jaha. Ni wazi kwamba wao sasa ndio wanaogharamia matibabu ya mama yao katika hospitali za hali ya juu huko mjini.
  • Hata hivyo, fikra za kitamaduni bado zinatawala. Beni anamlaumu Sara kwa kumwacha Yona peke yake akifanya kazi zote za nyumbani. Luka anapinga kauli ya Beni ya kuwadunisha watoto wa kike na mwanamke kwa jumla.
  • Katika onyesho hili, masuala ya ulevi na athari zake, taasubi ya kiume, usawa wa kijinsia na mabadiliko yanaangaziwa.

Masuala makuu

  • Suala la utamaduni linajitokeza wakati wazee wanapotoa rai kwamba dini za kisasa zimewafanya watu kudharau utamaduni wao.
  • Yona na Beni wanalalamikia kukengeushwa kwa wanajamii. Wanaeleza kuwa watoto wa siku hizi hawazifahamu lugha zao za kiasili, kwamba wamezama katika Kiswahili na Kiingereza. Wanashindwa kutofautisha hata wanyama wa kufuga kama vile mbwa, mbuzi na kondoo. Suala la usawa wa kijinsia linazungumziwa kupitia maelezo kuwa wanawake wa zamani waliwategemea waume zao lakini sasa jinsia zote zinachuma na kushirikiana katika malezi ya watoto. Neema, anakuwa mfano mwema wa mwanamke aliyefaulu maishani na ambaye anachuma na kuwatunza wazazi wake kama vile mtoto wa kiume angalivyoweza kufanya. Nafasi ya mtoto wa kike katika maendeleo ya familia inajitokeza. Ni wazi kwamba tofauti na zama za kale, watoto wa kike wa sasa wamesoma na kuajiriwa, na kuwa tegemeo muhimu katika familia zao na jamii nzima kwa jumla.
  • Aidha, suala la chanzo cha ulevi wa kupindukia linamulikwa. Ni wazi kuwa vijana wengi huingizwa kwenye mitego ya ulevi wanapotangamana na wenzao chuoni. Kwa wengine, mbegu hiyo ya ulevi huota na kuwa chanzo cha vurugu na maangamizi maishani. Kutangamana kwa vijana katika taasisi za elimu kumeleta athari nzuri na mbaya kutegemea jinsi wanavyotumia uhuru wao.

Onyesho Il

Onyesho hili linafanyika jioni nyumbani mwa Sara. Sara na Neema wamesafiri kurudi nyumbani. Wanaonekana wenye furaha na jinsi kulivyokaa. Wanaanza mazungumo yao kwa kutaja jinsi teknolojia ilivyorahisisha usafiri. Teknolojia imeendelea na kwa maoni ya Neema, teknolojai si yao. Ingawa wanaitumia na vile inavyoendelea, hawako kwa kipaumbele kwa kuiendeleza ila wanangoja isonge nao wasonge nayo. Wanaoinendeleza ndio wanapata faida zaidi. Kulingana na Neema, wasiochukua nafasi zao mapema wanakwisha kujipoteza kwa ulevi na utumwa.

Neema anajaribu kutaja jinsi baba yao bado hajaingia nyumbani ila saa kumi zimefika lakini Sara anamwambia kuwa kulingana na alivyoona alifanya kazi za kushughulikia mifugo na mengineo mapema halafu akatoka akaenda zake. Sara anamtetea Yona kwamba anamsaidia jinsi anavyoweza, kulingana na tamaduni na jadi zao. Yona akapita hapo, wenye kijiji watamwongelea vibaya , kwamba kageuzwa mtumwa na bibi yake. Sara anamshauri Neema kwamba anapaswa kumwelewa mume wake pia, aelewe ukingo wa uwez wake wa kusaidia. Anamwambia ingawa wanaume na wanawake wanagombea nafasi sawa kwa kazi na kijamii, ikifika nyumbani wanapaswa kuwa timu moja, kushirikiana kwa yale wanayotaka kufanya. Isingekuwa kushirikiana kwa Sara na Yona, hawangeweza kuwasomesha Neema na Asna na hatimaye hawangekuwa kwa nafasi waliyo wakati huo. Neema anajaribu kumwonyesha mama yake kwamba hatima ya kujitolea kwa imekuwa ungonjwa na Sara anamwambia kuwa hakuna mema yasiyokuja na mabaya yake. Anamweleza umuhimu wa kupanda mbegu za ambayo lazima iote. Anamwambia Neema kwamba ingawa anataka kuleta mabadiliko kwa njia zao za kitamaduni anapaswa kutumia elimu aliyo nayo na hekima pia. Ingawa mambo huchukua muda, Neema anapaswa kuanza pole pole.

Onyesho hili linaisha wakiwa wanaenda kupumzika kwa sababu ya safari yao.

  • Onyesho hili linatokea nyumbani kwa Sara, kijijini. Sara na Neema wanajadiliana kuhusu suala la utamaduni na mabadiliko ya kijamii.
  • Neema anasema ulimwengu unakwenda mbio ilhali watu wengine wamebaki nyuma katika mielekeo ya kijadi ya kubugia pombe bila kikomo.
  • Sara anamtetea Yona kwa kutowajibika ipasavyo na majukumu ya nyumbani hasa yale ya mifugo. Kulingana na Sara, mwanamume hawezi kuwekwa katika kiwango kimoja na mwanamke. Anasema
  • Yona anatekeleza majukumu yake ipasavyo. Hizo ni fikra za kitamaduni. Kwa Sara, mwanamume ana nafasi yake katika jamii na hapaswi kumsaidia mwanamke kazi za nyumbani. Kufanya hivyo ni kualika minong'ono ya wanajamii na kuwakosesha wanawe waume wa kuwaoa.
  • Sara anatunza heshima ya ndoa yake ili watoto wake wapate fanaka maishani licha ya mateso anayopata kutoka kwa mumewe. Sara anampa Neema ushauri unaoweza kuifanikisha ndoa yake. Anamshauri Neema azungumze na baba yake kwa hekima ili amsaidie kubadilisha msimamo wake, hasa kuhusiana na ulevi.

Masuala makuu

  • Kwa mara nyingine, taasisi ya ndoa inazungumziwa. Ingawa wanandoa wanapaswa kusaidiana, ni wazi kuwa jamii za Kiafrika bado zinatilia mkazo mgawo wa kazi katika jamii. Kuna majukumu mengine ambayo jamii haitarajii yafanywe na mwanamume mwenye mke, na iwapo ataamua kuyachangamkia, basi inakuwa ni kama yanampunguzia hadhi katika jamii. Ingawa fikra hizo zimepitwa na wakati na jamii imebadilika, bado jamii inatumia vigezo vya tamaduni hizo kumwekea mipaka mwanamke. Hata hivyo, Sara anamuasa Neema kuzitilia maanani tamaduni hizo ili kudumisha ndoa yake.
  • Onyesho hili pia linazua suala la ukoloni mamboleo. Kutokana na mazungumzo ya Sara na Neema, ni wazi kwamba matatizo ya kiuchumi ya mataifa machanga yanasabishwa na hali ya mataifa hayo kuendelea kuwa masoko ya bidhaa za nchi za nje. Yamebakia tu kuwa masoko ya bidhaa zitokazo ng'ambo badala ya kujibidiisha kuzalisha bidhaa zao.

Onyesho III

Onyesho hili linafanyika siku ya pili asubuhi , nyumbani mwa Sara na Yona. Yona ako sebuleni na anajizungumzia kwa huzuni. Anajilaumu kwa yale yaliyompata Sara na anasema kwamba angalijua asingaliingia katika ulevi. Yona pia anaonekana kujitolea kushugulikia bibi yake kwa ile hali aliyokuwa na kujitolea kumsaidia.

Neema anaamka na wanaamkuana na baba yake. Yona anamjulia hali yake na ya familia yake. Yona namwambia Neema kwamba anaona amekonda sana na Neema anamwambia si haba kwa sababu si ugonjwa lakini anamfahamisha kuwa mam yake itabidi aishi kwa madawa maisha yake yote. Yona anaonekana kusikitishwa na jambo hili lakini anaongea na kusema kuwa amejitolea kumwangalia Sara jinsi awezavyo.

Neema anamwuliza baba yake jinsi kazi zilivyo nyumbani na anaambiwa kuwa kazi zilizo lazima mtu ajitume kuzifanya kwa sababu ni mingi. Anamweleza kwamba kazi hizi ata ukimpa tu kibarua azifanye bado lazima umwangalie kwa makini. Wanaongea kuhusu jinsi Yona alivyohitimu shule baada ya Yona kutoa msemo kwa kimombo. Kwa mazungumzo yao tunapata kujua kwamba Yona ndiye bado aliye na rekodi chuoni alikosomea. Pia, Yona anamtaja baba yake, kalasinga, aliyepata jina yake kwa kuwa Mwafrika wa kwanza kufanyia Mhindi kazi. Kila mhindi alikoenda babake Yona akifuata na ndio ilisababisha apewe jina Kalasinga.

Sara anaamka na anaingilia mazungumzo yao kwa kusema kwmaba Yona hashindiki. Anamwambia Neema atengeneze kiamsha kinywa na anapata kwamba Yona alishatengeneza. Yona namwambia Neema kuwa jiko la gesi alilowanunulia limewasaidia sana kwa kurahisisha upishi. Neema ameshtuka kwa sababu hajai sikia babake akipika na Sara anamwambia ni sababu walikuwa shuleni kwa muda mrefu.

Onyesho hili linaisha Yona akinena. Anmwambia neema mambo haya amejua kuchelewa na anamwambia Sara pole kwa maumivu yake kisha wote wanakumbatiana.

  • Onyesho linafanyika asubuhi pale kijijini. Yona yuko peke yake sebuleni. Ugonjwa wa mkewe unamhuzunisha na anajutia maisha yake ya awali yaliyomletea mkewe ndwele. Neema anampata babake akiwa katika hali ya mawazo mengi. Yona anashangaa kumwona bintiye amekonda.
  • Yona anamwelezea Neema jinsi maradhi ya Sara yalivyoathiri mji wake. Anamshukuru kwa kumshughulikia mamake.Yona anakumbuka maisha yake ya chuoni na jinsi alivyokuwa mwerevu. Neema anapata mshangao anapogundua kuwa babake ameandaa kiamshakinywa mapema, yeye na mama yake wakiwa bado wamelala. Neema anafurahi na kumshukuru babake kwa wema wake.
  • Onyesho linaisha kwa kuonyeshwa Yona akiomba msamaha kwa Neema kwa makosa aliyowafanyia wakiwa wangali wachanga. Yona anatumai kuwa mabinti wake wengine watamsamehe siku moja. Yona pia anaomba msamaha kwa mke wake na kumwahidi kuwa asitie shaka atakuwa naye katika kila hali. Taa zinazima na wote watatu wanakumbatiana kuonyesha hali ya kusameheana na kuja pamoja kwa familia hiyo.

Masuala makuu

Katika onyesho hili, Yona anapata fursa ya kujirudia na kufikiria maisha yake ya siku za usoni. Anatambua kuwa mke wake ni mgonjwa kwani sasa maisha yake yanaendeshwa na madawa. Anaamua kuacha kunywa pombe kabisa. Uamuzi wa Yona una umuhimu mkubwa kwa sababu anakubali kuwa alimkosea mkewe na kwamba umefika wakati wa kujutia makosa hayo na kuanza upya. Kupitia kwa Sara na Neema, anaonekana kuomba msamaha familia yake kwa yote aliyowatendea na kuwaomba wampe nafasi ya kuanza maisha yake upya. Hii ni hatua kubwa na mwafaka katika maisha ya Yona na familia yake. Anaahidi kumtunza mkewe kikamilifu.

MSUKO

Kazi ya fasihi huwa imepangwa kwa muundo maalumu. Muundo huu huitwa msuko. Msuko ni mtiririko wa matukio katika kazi ya fasihi, Ni namna kazi ya fasihi huwa imepangwa kutoka mwanzo hadi mwisho.
Msuko huwa na sehemu tatu kuu ambazo ni:

  1. utangulizi/ mwanzo/ ufunguo
  2. kati/ sehemu ya pili- kilele na mpomoko
  3. hitimisho/ mwisho

..........

  1. Utangulizi/mwanzo
    • Mwanzo katika tamthilia hii unaanza kwa kueleza uhusiano uliopo bainaya wahusika. Hivyo basi, utangulizi huu unatusaidia kujua uhusiano wa wahusika. Kwa mfano, mwandishi wa tamthilia ya Bembeaya Maisha ameonyesha uhusiano wa wahusika kama vile: Sara na Yona ambao ni mke na mume na waliobarikiwa na watoto watatu wa kike ambao ni
    • Neema, Asna na Salome. Mhusika Dina ameelezwa kama mama yake Kiwa na rafikiye Sara. Bunju ni mumewe Neema; wamejaliwa na watoto wawili ambao ni Mina na Lemi. Beni na Luka wanatajwa kama wazee wa kijiji.
    • Utangulizi au mwanzo wa tamthilia ya Bembea ya Maisha unamsaidia msomaji kujua uhusiano uliopo bainaya wahusika najinsi wanavyoshiriki katika kitabu.
    • Sehemu ya utangulizi pia humsaidia msomaji kujua mahali na wakati mchezo unafanyika. Tamthilia ya Bembea ya Maisha ni mchezo/kazi ya fasihi inayofanyika katika eneo la Afrika wakati wa jana na leo.
    • Utangulizi katika tamthilia hii pia unamwezesha msomaji kupata kiini cha mchezo. Kiini katika tamthilia ya Bembea ya Maisha kinajitokeza katika onyesho la kwanza na la pili. Kulingana na tamthilia hii, kiini chake ni pamoja na namna utamaduni, mila na desturi za jamii husika zinavyoweza kuidunisha familia.
  2. Kati/sehemu ya pili
    • Sehemu hii huwa imegawika katika sehemu mbili ambazo ni kilele/ upeo na mpomoko. Msomaji hupata mivutano au migogoro baina ya wahusika. Sehemu hii inasaidia kuibua maudhui katika kazi ya fasihi.
    • Katika tamthilia ya Bembea ya Maisha, sehemu ya kati inajidhihirisha katoka sehemu ya Il kuendelea.
    • Mivutano baina ya wahusika inajidhihirisha kupitia wahusika kama vile Sara na Asna kuhusu suala la ndoa. Wawili hawa wana mitazamo tofauti kuhusiana na suala la ndoa. Asna ana mtazamo hasi ilhali Sara ana mtazamo chanya. Sara anamtaka Asna aolewe ili amletee mjukuu ampakate kwa mikono yake kabla hajaaga dunia. Hata hivyo, Asna anaona ndoa kama suala la kuleta matata katika familia. Mtazamo huu unachochewa na jinsi ndoa ya wazazi wake na ile ya dadake zinavyojidhihirisha. Asna anaona kuwa ndoa imemuweka mama yake katika hali ya ugonjwa atakaoishi nao milele (uk. 54). Vilevile, kulingana na Asna, ndoa imemfanya Neema kutokwa na hali ya ukakamavu na kujiamini kwa dhati (uk. 54).
    • Maudhui yanayojitokeza katika sehemu hii ni ndoa, utamaduni, taasubi ya kiume, nafasi ya mwanamke na mengineyo.

Kilele/ Upeo

  • Kilele katika tamthilia ni sehemu ambayo matukio yanafanyika katika hali ya taharuki. Msomaji akifika katika sehemu hii, hupatwa na mshawasha wa kutaka kusoma ili apate ujumbe kamili.
  • Katika tamthilia hii ya Bembeaya Maisha, sehemu ya kilele inajitokeza katika mazungumzo ya Dina na Sara. Ni baada ya mazungumzo hayo, ndipo msomaji atapata hamu ya: kutaka kujua namna walivyofanikiwa, kujua kama ugonjwa wa Sara utapona, kujua kama ulevi wa Yona ulipungua au ulifikia kikomo. Msomaji anapata hamu ya kujua kama mtazamo wa jamii kuhusu familia ya Yona na Sara ulibadilika au uko vilevile.

Mpomoko

  • Hii ni sehemu ambayo mhusika mkinzani anashindwa. Katika sehemu hii, tensoni/msuko wa tamthilia unashuka.
  • Mpomoko katika tamthilia hii ya Bembea ya Maisha unajidhihirisha wakati Yona anapokuwa akijizungumzia na kujilaumu kwa kukosa kumshughulikia mkewe Sara (uk. 70). Yona anakata shauri ya kutoshiriki katika unywaji wa pombe. Anasema kuwa atatumia siku zake kumwangalia mke wake mgonjwa. Hapa ndipo msuko wa tamthilia unashuka kwa kuwa msomaji ameshapata suluhu ya tensoni au taharuki aliyotaka kujua itaishia wapi.

c). Mwisho/Hitimisho

Hii ni sehemu ya mwisho katika msuko wa tamthilia. Sehemu hii inamwezesha msomaji kujenga au kupata suluhu ya suala kuu linalojitokeza katika tamthilia. Mwisho wa mchezo wa Bembea ya Maisha unajitokeza Yona anapoomba msamaha kwa mwanawe Neema na kutumainia kuwa wanawe wengine watakuja kumwelewa. Aidha, anaomba msamaha kwa mkewe kwa kutomjali siku za awali. Anamwahidi kuwa atasimama naye katika kila hali (uk. 74).

Join our whatsapp group for latest updates

Download Muhtasari wa Sura / Mtiririko wa Maonyesho - Mwongozo wa Bembea ya Maisha.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?