Bembea ya Maisha Maswali na Majibu ya Dondoo

Share via Whatsapp

Swali 1

Basi usijipandishe presha mama! (al.10)

  1. Eleza muktadha wa dondoo. (al.4)
  2. Bainisha vipengele viwili vya kimtindo vinavyojitokeza katika dondoo. (al.2)
  3. Eleza sifa za msemewa. (al.4)
  4. Jadili jinsi maudhui ya utamaduni yanavyojitokeza katika tamthilia. (al.10)

Majibu

  1. Msemaji - Neema
    Msemewa-Sara
    Mahali- Hospitali
    Neema alikuwa akimtuliza Sara baada ya kukasirishwa na Asna aliyesema babake anaweza kuteka maji kisimani.
  2.  
    • Utohozi- presha kutokana na neno la kiingereza pressure
    • Nidaa- mama!
  3.  
    • Mwenye bidi
    • Anayewajibika
    • Mvumilivu
    • Mwenye mapenzi wa dhati kwa wanawe
    • Mtamaduni
    • Mshauri mwema
    • Mwenye busara
    • Mwenye mlahaka mwema
  4.  
    • Mtoto wa kiume anatukuzwa kama mrithi
    • Mtoto wa kwanza ana jukumu la kuwasaidia wazazi wake
    • Sara hawezi kulala kwa Bunju
    • Wazazi hawawezi lala chumba kimoja na wanao
    • Leso hutolewa wakati wa posa
    • Enzi za kitambo elimu ya wasichana haikutiliwa maanani
    • Jamii inashikila utamaduni wa wazee kukutana baada ya mavuno ya kwanza na kutoa baraka
    • Kizazi  cha sasa kimetupa mila zao
    • Mume hafai kufanya kazi za nyumbani (hasa jikoni)
    • Mwanamke hafai kushindana na mwanwmume

Swali 2

Katika tamthilia hii Maisha yamesawiriwa kama Bembea. Kwa kutolea mifano mwafaka oanisha kauli hii na wahusika mbalimbali. (alama 20)

Majibu

Maisha ya familia ya Sara na Yona yanaleta taswira ya bembea. Mwanzoni, ndoa ya Sara na Yona inaonekana yenye furaha. Hii ina maana kuwa, kama bembea inavyokuwa juu, maisha yao yalikuwa yenye mafanikio na furaha. Maisha yao yanaingiwa na dosari wakati wawili hao wanakosa mtoto baada ya kipindi kirefu katika ndoa. Zaidi ya hayo, wanajaliwa na watoto wa kike watatu. Hawajaliwi na mtoto wa kiume, kinyume na matarajio ya jamii. Wanachekwa, wanasutwa na kukejeliwa.

  • Bembea ya maisha yao inarudi chini. Sara anaanza kuchapwa kichapo cha mbwa na bwana yake Yona. Yona anaidharau familia yake na kuingilia ulevi, ulevi uliomfanya kupigwa kalamu kazini. Sara anasema, japo kuna wakati maisha yanabwagwa na bembea ya maisha, lazima maisha hayo yaendelee. Hata kama kamba, chuma au minyororo ya maisha inakatika, hawana budi kujiinua na kuendelea na maisha (uk. 20-21). Hivyo basi Sara anasimama na familia yake kidete akifahamu kuna siku atafanikiwa na maisha yao yatakuwa mema tena.
  • Maisha ya familia ya Yona yanabadilika kutoka kuwa maisha ya kukosa mahitaji ya kiuchumi. Bembea yao ya maisha ilionekana kuwachini. Baada ya Neema kufanikiwa na kupata kazi, bembea ya maisha yao inakuwa juu. Wanafanikiwa kujengewa nyumba, wanapata wafanyakazi wa kuwasaidia nyumbani na hata kuwa na jiko la gesi la kupikia.
  • Bembea ya maisha ya Neema inaonekana kusukumwa na Bunju mumewe. Kwanza Bunju alimsaidia Neema alipokuwa amepata ajali. Bunju alimtumia flying doctors ili aweze kupata matibabu zaidi (uk.41).
  • Bunju anasaidia kuisukuma bembea ya maisha ya Neema kwa kumsaidia kuwasomesha dada zake. Vilevile, anamsaidia kuwajengea wazazi wa Neema nyumba.
  • Maradhi ya Sara yanaifanya bembea ya maisha ya Sara kuwa kama iliyokatika na kuwa chini. Sara anakosa matumaini ya kuishi na kutamani kufa.
  • Bembea ya maisha ya mjini huwa juu kutokana na maendeleo. Kuna maendeleo ya barabara, magari mengi, majengo mengi na hata sekta ya matibabu imeimarishwa.
  • Watu mjini wanapokea matibabu ya hali ya juu ilhali, bembea ya maisha ya kijijini huwa chini kwa sababu ya kukosa maendeleo hasa katika sekta ya matibabu na barabara nzuri. Sekta ya matibabu ya kijijini inamfanya Neema kumtafutia mamake hospitali ya mjini sababu zile za kijijini hazimpi mtu matumaini ya kutoka akiwa mzima ilhali za mjini zinampa mgonjwa matumaini ya kutoka akiwa buheri wa afya.

Swali 3

Hiyo ndio ajabu! Kizazi hili hakitaki kufanya kazi. Kinataka kuja kazini kwa sababu ya mshahara tu. Wachapa kazi hodari ni njozi iliyopotea.

  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (ala 4)
  2. Eleza sifa za msemaji wa dondoo hili. (ala 4)
  3. Fafanua imuhimu wa msemewa katika kazi ya Bembea ya Maisha. (ala 4)
  4. Taja na uonyeshe mbinu za uandishi zilizotumika katika dondoo. (ala 4)
  5. Eleza maudhui yanayokuzwa katika muktadha wa dondoo. (ala 4)

Majibu

  1. Eleza muktadha wa dondoo. (al 4)
    • Haya ni maneno ya Sara akimwambia Yona kuhusu majukumuwakiwa nyumbani mwao. Ni baada ya kuvutanna kuhusu majukumu ya pale nyumbani na namna Neema aliwasaidia.
  2. Eleza sifa za msemaji. (al 4)
    • Mwenye huruma
      • Anamhurumia Neema kwa majukumu yake na kwa wazazi wake.
    • Mwajibikaji
      • Anamwalika Dina ili aje kumpikia mumewe Yona.
    • Mvumilivu
      • Anavumilia kusutwa, kudharauliwa na hata kuchapwa na mumewe.
    • Mchangamfu
      • Uso wake umejaa tabasamu
    • Mshawishi
      • Anamshawishi Asna aolewe.
    • Mshauri mwema
      • Anawashauri mabinti zake kuhusu maisha. (1x4)
        Mwanafunzi afafanue sifa ili pate alama.
  3. Fafanua umunhimu wa msemewa
    • Ni kielelezo cha watu wenye bidii katika jamii.
    • Anaendeleza maudhui ya athari za ulevi.
    • Ni klielelezo cha watu wanaowajibika.
    • Anawakilisha watu wasiowazia matendo yao na kuishia kujuta.
    • Anakuza ploti. (1x 4)|
      Mwanafunzi athibitishe kila umuhimu.
  4. Taja na uonyeshe mbinu za uandishi katika dondoo. (ala 4)
    1. Nidaa – Hiyo ndiyo ajabu!
    2. Isitiara – wachapa kazi hodari ni njozi iliyopotea.
  5. Eleza maudhui yanayokuzwa katika muktadha. (ala 4)
    1. KAZI
      • Vijana siku hizi hawapendi kufanya kazi.
      • Vijana hawafurahii kazi bali mishahara tu.
    2. MABADILIKO
      • Zamani vijana walikuwa wenye bidii na walipenda kazi lakini siku hizi wao huthamini mshahara tu.
      • Yona alipokuwa mwalimu alifika shuleni alfajiri.

Swali 4

Kila binadamu hukabiliana na mabadiliko katika maisha yake. Jadili kauli hii ukirejelea tamthilia ya Bembea ya Maisha. (ala 20)

Majibu

  1. Kutoka ujana hadi uzee – Yona
  2. Sheria kubadilika – katika Elimu. Huwezi kumnyoosha mtoto kwa Kiboko.
  3. kubadilika kwa mtazamo. Yona anabadilisha mtazamo wake kwa sara na kumwelewa kuwa alikuwa mgonjwa.
  4. Kubadilika kwa hisia.- Yona analalamikia Sara kwa kutopika lakini baadaye Anamhurumia.
  5. Yona anabadilisha hali yake ya zamani na kuamua kufuata mkondo mpya wa maisha.
  6. Yona anasawiriwa kama mtu mzuri mwanzoni, lakini baada ya kusutwa na kudharauliwa.
  7. Yona anabadilika na kujutia ulevi wake kuwa pombe ilimchezesha kama mwanasesere.
  8. Kuna mabadiliko kuhusiana na mila na desturi – kuhusiana na mtoto wa kike na wakiume.
  9. Katika kizazi cha leo mtoto wa kike anaweza kurithi na kushughulikia wazazi wao.
  10. Ndoa inakumbwa na mabadiliko – mtu hujichagulia wakati wa kuoa/ kuoelewa kinyume na hapo awali msichana alipolazimishwa.
  11. Majukumu vilevile yanabadilika Yona anaingia jikoni kumpikia Sara.
  12. Mbeleni wazee walifunzwa na dunia lakini kizazi cha leo kinategemea vitabu tu ili kufahamu lolote.
  13. Hali ya uchumi inabadilika – wanaotegemea mifuko yao watakabiliana na kipindi kigumu.
  14. Mitindo ya nyimbo-
  15. Burudani – watoto wa kisasa hupenda kupelekwa out.
  16. Elimu ya sasa haina mafundisho kwa vijana kuhusu ndoa.
  17. Mbeleni watoto walifunzwa na kuzishikilia mila na desturi ila sasa wamwezitupa mila na desturi zao.
  18. Watoto walitumia lugha asilia, leo hawajui hata neno moja.
  19. Zamani wasichana hawakuendelea na masomo.
  20. Safari za kwenda kijijini hazibughudhi kama zamani kutokana na mabadiliko ya kiteknolojia.
    (zozote 20 x 1)

Swali 5

Ukirejelea Anwani ya Tamthilia ya Bembea ya Maisha, onyesha namna wahusika wanavyobembea maishani mwao. (alama 20)

Majibu

Bemba - Ukirejelea Anwani ya Tamthilia hii onyesha namna wahusika wanavyobembea maishani mwao. (alama 20)

  • Familia ya Yora na Sara inabembea katika shutuma mbalimbali kutoka kwa watu baada ya kukaa muda mrefu bila kupata mtoto. Baadaye Mungu aliwajalia watoto wa kike.
  • Watu walianza kumsonga Yona kula kuwa amepata watoto wa kike tu na kuwa amekosa mrithi. Yona akaanza kuishi kwa hofu na simanzi na akaanza kubembea maisha ya ulevi.
  • Neema anabembea katika maisha ya ndoa ambayo yana mchanganyiko wa mivutano na upendo ndani yake. Kuna mivutano ya kiutamaduni inayosababisha Neema na Bunju wasirlewane. Buju anadai tamaduni haziruhusu yeye kukaa nyumba moja na wazazi wa Neema, jambo ambalo Neema anadai zimepitwa na wakati lakini Bunju anashikilia papo hapo.
  • Bembea ya maisha ya Neema inaonekana kusukumwa na Bunju mumewe. Bunju alimsaidia alipopata ajali kwa kutumia 'flying doctors' ili aweze kupats matibabu. Bunju pia anasaidia kuisukuma bembea ya maisha ya Neema kwa kumsaidia Neema kuwasomesha dada zake na anamsaidia kuwajengea wazazi wa Neema nyumba.
  • Asha anaishi katika bembea ya maisha mjini akihangaika hapa na pale kufanya shughuli za kujikimu ingawa amehitimu masomo ya chuo kikuu.
  • Neema anabembea katika swala la malezi ya mwanawe Lemi. Hana muda kutokana na shughuli nyingi za kazini na kutoa huduma kwa mama yake.
  • Maisha ya familia ya Yona yanabadilika kutoka kuwa ya kukosa mahitaji ya kiuchumi kwani badala ya Neema kifanikiwa kupata kazi, bembea ya maisha yao inakuwa juu. Kujengewa nyumba.
  • Bembea ya maisha ya mjini huwa juu kutokana na maendeleo k.m barabara, magari, majengo n.k.
  • Maradhi ya Sara yanaifanya bembea ya maisha ya Sara kuwa kama iliyokatika na kuwa chini na anakosa matumaini ya kuishi.
  • Watu mjini wanapokea matibabu ya hali ya juu ilhali bembea ya maisha ya kijijini huwa chini kwa sababu ya matibabu ya hali ya chini, hali inayomfanya Neema kumtafutia mamake hospitali ya mjini.
  • Beni anabembea katika swala la kuelimisha watoto wa kike. Aidha anayumbayumba kuhusu thamani ya watoto wa jinsia ya kike au kiume.
    (zozote 10 x 2 = 20)

Swali 6

Maskini mke wangu! Kumbe ugonjwa haukumsaza mwaka baada ya mwaka. Umemla bila huruma. Awali niliona kuwa mchezo kumbe ilikuwa kweli yake ninaona imesimama. Ni mwele hakika. Laiti ningejua, jana ningeishi tofauti. Silezi zetu za maisha tungezila zilivyokuja kwa furaha. Siku hazigandi wala jana hairudi. Sasa jana imebaki kumbukizi baada ya kusombwa na wakati mfano wa mafuriko msimu wa masika."

  1. Yaweke maneno haya katika muktadha wake (alama 4)
  2. Eleza kwa mfano mbinu nne za kimtindo zilizotumika (alama 4)
  3. Barusha toni katika dondoo hili. (alama 2)
  4. Ni maudhui gani yanayojitokeza katika dondoo hili? (alama 4)
  5. Onyesha sifa za mzungumzaji zinazodhihirisha kuwa silezi zao hawakuzila kwa furaha. (alama 6)

Majibu

  1. Ni maneno ya Yona akijisemea akiwa sebuleni kwake nyumbani anapoamua kuacha unywaji pombe na kuanza maisha mapya. (alama 4)
  2. Nidaa - wangu?
    Tashihisi - ugonjwa kumla
    Tashbihi - mfano wa mafuriko.
    Takriri - mwaka baada ya mwaka (4 x 1 = 4)
  3. Majuto - laiti ningejua. (1 x 2 = alama 2)
  4. Madhara ya ulevi
    Athari za maradhi. (2 x 2 = alama 4)
  5. Sifa za Yona
    Ni hodari - Ni mwalimu wa shule ya msingi aliyefaulisha wanafunzi na kupewa zawadi.
    • Huenda shuleni alfajiri.
    • Ni katili - alimpa Sara kichapo cha mbwa akiwa mlevi.
    • Mwenye majuto - Anajutia uraibu wa pombe na kujiletea hasara.
    • Ni mtamaduni - Anaamuru kuwa watoto wa kike hawapaswi kuwa warithi.
    • Mwenye msimamo thabiti - Hakushawishika na watu aoe mke mwingine.
      (zozote 3 x 2 =6)

Swali 7

“Mwanangu binadamu mchoyo kwa lake lakini mkarimu ajabu kwa la mwenziwe. Atakukarimu kwa la mwenziwe na atakupa nyongeza usiohitaji lakini lake atalizika katika giza la kina cha moyo wake. Ndiyo hulka yake mwana wa Adamu.”

  1. Eleza muktadha wa maneno haya. (alama 4)
  2. Jadili namna chanya msemaji na wenzake wa jinsia ya kike walivyosawiriwa katika tamthilia ya Bembea ya maisha. (alama 6)
  3. Fafanua umuhimu wa mazungumzo kati ya msemaji na msemewa katika tamthilia ya Bembea ya Maisha (alama 10)

Majibu

“Mwanangu binadamu mchoyo kwa lake lakini mkarimu ajabu kwa la mwenziwe. Atakukarimu kwa la mwenziwe na atakupa nyongeza usiohitaji lakini lake atalizika katika giza la kina cha moyo wake. Ndiyo hulka yake mwana wa Adamu.”

  1. Eleza muktadha wa maneno haya.
    • Maneno ya Dina.
    • Anamwambia Kiwa.
    • Yuko nyumbani kwa Dina.
    • Dina alikuwa akimwambia Kiwa kuhusu yale magumu ambayo Sara ameyapitia katika maisha . 4x1=4
  2. Jadili namna chanya msemaji na wenzake wa jinsia ya kike walivyosawiriwa katika tamthilia ya Bembea ya Maisha.
    • Mwanamke ni karimu k.m Neema anatumia mshahara wake kulipia karo Asna na Salome.
    • Mwanamke ni mwenye bidii k.m Salome amesoma na kuhitimu first class.
    • Mwanamke ni mwajibikaji k.m Neema anamwendea mamake kijijini ili kumpeleka hospitali.
    • Ni mwenye utu k.m Dina anaenda kumsaidia Sara kwa upishi.
    • Mwanamke ni mtiifu k.m Bela anaitika anapoitwa na Sara na kuagizwa kuamka mapema.
    • Mwanamke ni mwenye busara k.m Sara anamshauri Neema kuwa maisha ya ndoa ni bembea. 6x1=6
  3. Fafanua umuhimu wa mazungumzo kati ya msemaji na msemewa katika tamthilia ya Bembea ya maisha
    • Yanachimuza maudhui ya uwajibikaji k.m Kiwa amekuja kumjulia hali mamake.
    • Yanadhihirisha sifa za Sara k.v uvumilivu k.m anapoitwa tasa anavumilia.
    • Yanaonyesha maudhui ya changamoto ya ndoa k.m Dina anasema Sara alikaa kwa muda kabla ya kujaliwa motto.
    • Yanaonyesha sifa za Neema wakati Kiwa anasema ana akili kama za simaku.
    • Yanachimuza maudhui ya umbea k.m wanajamii walimsema sana Sara.
    • Yanaendeleza ploti ya hadithi.
    • Yanaonyehsa Yona kama mwenye msimamo dhabiti.
    • Yanaonyehsa maudhui ya nafasi ya mwanamke. Ni mnyonge.
    • Yanaonyesha sifa za Dina kama mdadisi k.m anamuuliza mwanawe kwa nini amekonda.
    • Yanakuza maudhui ya mila na utamaduni k.m jamii inashinikiza Sara apate mtoto wa kiume wa kumrithi.
    • Yanachimuza falsafa ya mwandishi ya kupinga tamaduni zinazothamini mtoto wa kiume na kumdunisha wa kike.
    • Yanaonyesha mgogoro kati ya Yona na jamii huku ikimtaka azae mtoto wa kiume na kumrithi.

Swali 8

Jadili maudhui yafuatayo kwa kutolea mifano maridhawa kama yanavyoshughulikiwa katika tamthilia ya Bembea ya maisha.

  1. Mabadiliko
  2. Migogoro

Majibu

Jadili maudhui yafuatayo kwa kutolea mifano maridhawa kama yanavyoshughulikiwa katika tamthilia ya Bembea ya maisha.

  1. Maudhui ya mabadiliko
    Ni hali ya kutoka katika hali moja hadi nyingine.
    • Yona alikuwa akiwanyoosha viboko wanafunzi lakini sheria ikabadilika kwamba siku huwezi kumnyoosha mtoto kwa kiboko.
    • Tofauti na hapo awali Yona ataka kuzitumia siku zake za uzee kumshughulikia mkewe.
    • Yona alikuwa mzuri lakini akageuka na kuwa mlevi.
    • Mtazamo kuhusu mtoto wa kike kutazamwa kama asiye na haki ya kurithi unabadilishwa na kizazi cha leo.
    • Zamani wasichana wakiozwa punde wanapobuleghe lakini ziku hizi wanaolewa wakitaka.
    • Zamani Yona hangepika lakini tunamwona akiandalia familia yake kiamsha kinywa – utamaduni kubadilika.
    • Uk. 72 Neema anabadilisha mtazamo wake kuhusu babake.
    • Bunju anabadilisha mtazamo wake wa kutomsaidia Neema katika matibabu ya Sara – sasa anasema atampiga Jeki.
    • Afya nzuri ya Sara kubadilika na kuwa duni.
    • Jamii inabadilika na kuiheshimu familia ya Yona – ambayo ilikuwa ikidharauliwa hapo mbeleni. Alama 10
  2. Maudhui ya migogoro
    • Kati ya kizazi cha jana na kizazi cha leo k.m katika ndoa.
    • Migogoro ya kitamaduni kati ya Asna na mamake – kuhusu babake kuchota maji kisimani.
    • Kitamaduni kati ya Asna na Sara. Sara anaamini kuwa msichana aolewe tu anapobaleghe.
    • Tamaduni- Bunju dhidi ya Neema, Asna na Bela. Bunju haamini wazazi kulala nyumbani kwa mkwe.
    • Migogoro kati ya Sara na Yona ambapo Yona anampiga Sara kwa kukosa mtoto wa kiume.
    • Kati ya Neema na Bunju kuhusu majukumu ya kifamilia-matibabu ya Sara.
    • Neema na Bunju wanavutana nani ampeleke Lemi Ziara.
    • Bunju anasema Neema anapenda kukana na kubishana, jambo ambalo litamfanya kuonekana mbwa kasoro.
    • Mgogoro kati ya jamii ya Yona na ile ya Sara baada ya Sara kutojaliwa na mtoto.
    • Mgogoro wa familia ya Yona na Sara unakuzwa na kuwa wa kijamii-inayomlaumu Yona kwa kukosa mtoto wa kiume.

Swali 9

"... wakati mwingine mwindaji huwa mwindwa. Hata kijijini wanaishi watu . Watu hao hawakumbwi na dhiki kiasi hiki. Ya nini kung'ang'ana kuyatafuta maisha kama kwamba hayapiti? Maisha ni mshumaa uso mkesha! Ukijiachia sana peupe hata upepo unaweza kuuzima kabla ya kulika hadi nchani.”
Maswali

  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama. 4)
  2. Bainisha toni katika kauli hili (alama. 2)
  3. Eleza vipengele vinne vya kimtindo alivyotumia msemaji kufanikisha uwasilishaji wa ujumbe. (alama. 4)
  4. Eleza umuhimu wa msemaji katika kuendeleza ploti ya tamthilia hii. (alama 10)

Majibu

  1.                          
    • Msemaji ni Sara
    • Msemewa ni Asna
    • Walikuwa nyumbani kwa Asna/servant’s quarter.
    • Sara ana maoni kuwa Asna angehamia kijijini kumsaidia. (4x1=4)
  2. Toni ya kushauri (1x2=2)
  3. Vipengele vya kimtindo:
    • Methali-mwindaji huwa mwindwa
    • Swali ya balagha- ya nini kung’ang’ana kuyatafuta maisha kama kwamba hayapiti?
    • Nidaa- Maisha ni mshumaa uso mkesha!
    • Jazanda/ sitiari- Maisha ni mshumaa uso mkesha( maisha ni mafupi na hayapo daima)
    • Mdokezo - …wakati mwingine
    • Tashihisi / uhuishi - upepo unaweza kuuzima kabla kulika hadi nchani.
    • kweli kinzani – mwindaji – mwindwa
    • msemo/nahau - Maisha ni mshumaa uso mkesha! (za kwanza 4x1 = 4)
  4. Umuhimu wa Sara katika kujenga ploti
    • Sara ametumiwa kuonyesha athari ya migogoro katika ndoa. Maradhi ya moyo anayogangua ni tokeo la mzozano baina yake na mumewe Yona.
    • Kupitia kwake tunaona alivumilia ndoa yake na kufanya juu chini ili wanawe wapate elimu ili kuboresha mustakabali wao.
    • Aidha, anahakikisha kuwa binti zake Neema na Asna wanapata elimu.
    • Ni mfano wa wanawake wenye bidii. Hata akiwa hospitalini, akili yake inafikiria mazao yake aliyoyaacha shambani.
    • Kupitia mazungumzo baina yake na Asna, yanamsawiri Asna kama kijana aliyekengeuka kiasi cha kutotaka kuingia katika ndoa.
    • Kupitia kwake tunaelezwa kuhusu usuli wa kutopika. Sara anaeleza kuwa kwa sababu ya ugonjwa wake hangeweza kupika.
    • Sara alisemwa na kutukanwa na wanajamii kwa sababu ya kuwapata watoto wa kike pekee. Hii ilipelekea Yona kuingilia ulevi.
    • Baadhi ya matukio katika maisha ya wahusika fulani yanaangaziwa katika nyumba yake. k.m Dina anaangaziwa kama mwenye utu kwani anaenda kumpikia kwa kuwa alikuwa mgonjwa.
    • Kupitia mazungumzo baina yake na Yona, tunapata kujua kuwa Neema ndiye aliyewasomesha wanuna wake hadi chuo kikuu.
    • Pia, Sara anatujuza kuwa Neema ndiye aliyewaajiri wafanyakazi nyumbani kwake.
    • Ametumiwa kuonyesha uwajibikaji wa Neema. Neema anagharamia matibabu ya Sara na pia anampa babake/Yona pesa za kwenda kwa wazee wenzake.
    • Kupitia kwake tunafahamu kuwa Bunju ndiye aliyemsaidia Neema baada ya kupata ajali na kulipia gharama za hospitali ilhali Bunju hakuwa amemjua Neema.
    • Kupitia mazungumzo baina yake na Neema na Asna tunapata kujua kuhusu tofauti baina ya hospitali za mjini na kijijini. Huduma za hospitali mjini ni mzuri lakini za kijijini zinalinganishwa na seli na wahudumu hawana mlahaka mwema.
    • Hatima ya mgogoro baina ya Sara na Yona. Yona anaachana na mila na tamaduni za kutopika kwa Mwanaume.
    • Anaonyesha jinsi utamaduni ulivyowakandamiza wasichana –Sara anamwambia Asna kuwa siku zao elimu ya wasichana ilifanyiwa bezo na kuwa Sara aliachia darasa la saba.
    • Kuonyesha mustakabali wa Sara wa kumsamehe,Yona-Yona anamwomba Sara msamaha kwa kuwa hakujua upeo wa ugonjwa wa moyo. (zozote 10x1=10)

Swali 10

  1. Fafanua umuhimu wa mazungumzo kati ya Luka, Beni na Yona katika kujenga tamthilia ya “Bembea ya Maisha” (alama 10)
  2. "Bembea inapolika na kukatika haiwi mwisho wa michezo.Huungwa na mchezo kuanza tena." Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa kutolea mifano mwafaka tamthiliani. (alama. 10)

Majibu

  1.                        
    • Yanaonyesha sifa ya Luka kuwa ni mkarimu -anawakaribisha wenzake kwake nyumbani kwa chakula cha mchana na kinywaji..
    • Kuonyesha mila na utamaduni - Luka anadokeza kuwa kitendo cha kula pamoja kwa wazee kilikuwa kinafanywa na wazee wao kwani mavuno ya kwanza huonjwa na wazee na kutoa baraka. (uk. 58)
    • Yanachimuza ukengeushi - Beni anasema kuwa tatizo la watu siku hizi ni kuzitupa mila zao kabisa. (uk.58) Wajukuu wa Yona hawafahamu lugha yao ya asili. (uk-59)
    • Yanadhihirisha mchango wa dini - Yona anaeleza dini,imechangia watu kuona mila kuwa chafu. (uk.58)
    • Yanaonyesha mabadiliko katika malezi - Yona anaambia wazee wenzake kwa malezi kule mjini yameachiwa kina yaya. (uk.59)
    • Yanaonyesha jinsi mila na tamaduni zilikuwa kandamizi kwani hazikuruhusu mtoto wa kike kuenda shule au kuridhi kitu – kulingana na Luka.(u.k 60)
    • Yanadhihirisha jinsi hao kina Luka walivyomshinikiza Yona kuoa mke mwingine apate mtoto wa kiume.(u.k 60)
    • Yonadhihirisha sifa za Beni jinsi ana wivu kwa watoto wa Yona kwani hataki Luka awataje katika mazungumzo yake.
    • Yanachimuza ufanisi wa watoto wa Yona – Luka anasema walikuwa nyota ya jaha. Neema anarudi kijijini akiwa na gari.
    • Yonaonyesha thamani ya mtoto wa kike ilivyopanda na nafasi yake kupanuka kwani zamani walikuwa wakiwategemea waume zao laikini sasa hali ni tofauti(u.k.60)
    • Yonaonyesha maudhui ya uhafidhina – Luka anamuona Neema kama si wao tena baada ya kuolewa.
    • Yanachimuza hekima ya Luka – Luka anamuuliza Beni kuwa lipi muhimu kati ya tiba au mtu kuja kumpikia mwenzake? (uk.61)
    • Yanaonyesha sifa za Yona hapo awali kuwa alikuwa mualimu mwenye bidii - Yona anasema angefika kazini majira ya alfajiri, kiboko mkononi, siku nzima kazi tu, aliweza kufunga vitabu kwenye baskeli kwenda kuvisahihisha wikendi. (uk. 62)
    • Yanadhihirisha mabadiliko katika nyanja ya elimu - Yona anasema siku hizi huwezi tena kumnyoosha mtoto kwa kiboko. (uk.62)
    • Yanachimuza athari za pombe - jinsi pombe ilivyomfanyaYona kuwa mtumwa akashindwa kuishi bila kulewa (uk62)
    • Yanaonyesha uvumilivu au stahamala za Sara wakati Yona alipokuwa mlevi. Yona anasema Sara alimsaidia kulea na kusomesha watoto na kwamba bila yeye chombo kingezama. (uk-62)
    • Yanaonyesha jinsi Yona alivyoanza kutumia tembo alipokuwa chuoni. Wenzake walimpa mvinyo kumrai kuonja. (uk. 62)
    • Yanadhihirisha uongo wa Beni- kuwa mtoto wake ni fundi wa mitambo na wala si injinia. (uk. 63)
    • Yanaendeleza ploti- tunatambulishwa kuwa Luka,Beni na Yona ni marafiki na walishiriki vileo pamoja. (zozote 10x1=10)
  2.                  
    • Neema nusura apoteze uhai wake katika ajali Lakini Bunju akamnusuru kwa kumpeleka hospitalini.
    • Neema na Bunju baada ya kugombana kuhusu mchango wake Bunju katika matibabu ya Sara, Neema anaamua kumuelewa Bunju hivyo ndoa yao kuendelea vyema.
    • Baada ya changamoto ya kutopata watoto iliyoyumbisha ndoa baina ya Sara na Yona, hatimaye walijaliwa watoto watatu.
    • Maradhi ya moyo yalipomlemea Sara kiasi cha kukata tamaa na maisha, Neema anajitolea kuhakikisha mamaye amepata matibabu murua hivyo kumrejeshea matumaini.
    • Japo Yona na Sara walikosa mwana wa kiume na kusimangwa na wanajamii, mabinti zao wanakuwa wembe masomoni hivyo kuwapa furaha katika ndoa yao.
    • Neema alipoonekana kukata tamaa kutokana na kile alichokiona kuwa ni ubahili wa Bunju, Sara alimpa wasia uliompa nguvu zaidi katika ndoa yake.
    • Yona baada ya kugundua kuwa ulevi wake unaangamiza familia yake, anaapa kutolewa tena na kumhudumia mkewe Sara.
    • Yona na Beni walipotofautiana kuhusu watoto wao,Luka anafaulu kutuliza hali na wazee hawa kuendelea na sherehe zao.
    • Baada ya kumsababishia mkewe maradhi ya moyo,Yona anamwomba Sara msamaha kwa kuwa hakujua upeo wa ugonjwa wa moyo.
    • Mgogoro baina ya Sara na Neema kuhusu Yona unaisha Neema anapogundua upendo wa Yona Kwao anapoacha utamaduni wa kutopika chakula.
    • Mgogoro baina ya Sara na Yona unaisha. Yona anapoachana na mila na tamaduni za kutopika kwa mwanaume.
    • Tatizo la Sara la kushindwa kumpikia mkewe linasuluhishwa na jiraniye Dina anapokuja kumsaidia.
      (zozote 10 x 1=10)

Swali 11

Ni mshtuko wa namna Fulani unaotokana na mtu kukabiliwa na hali ya maisha ya watu wengine ambayo inapingana na ile yake.

  1. Eleza muktadha wa dondoo hili? (alama 4)
  2. Eleza namna ambavyo msemewa wa dondoo hili anavyojenga maudhui ya nafasi ya mwanamke.    (alama 6)
  3. Onyesha namna maudhui ya ubabe dume yanavyodhihirika katika tamthilia hii.     (alama 10)

 Majibu

  1. Msemaji: Asna
    Msemewa : Sarah
    Mahali : Hospitalini
    kiini: Alijerelea alivyoshangaa namna ambayo Bunju alizingatia kushughulikia familia yake, yeye mke ma watoto bila kujali mwengine/ Alikuwa akitafsiri ujumbe wa 'culture shock' kwa mamaye 
    1x4=4
  2. Msemewa ni Sarah
    • Anajenga maudhui ya uvumilivu
    • Anaendeleza mila na tamaduni
    • Mwanamke amewajibika kuilinda jamii k.v. kuwafunza wanawe
    • Anashauri vyema k. vile kwa wanawe
    • Mwanamke anaonekana ndiye wa kudhulumiwa katika ndoa
    • Nafasi ya mwanamke ni jikoni na kumhudumia mmewe
      zozote 6, 1x1
      Tanbihi
      1. Kadiria majibu mengine ya mwanafunzi
      2. Akikosea msemewa kwenye swali la (4b) asituzwe hapa.
  3. Maudhui ya ubabedume
    • Kazi za nyumbani ni za mama
    • Mtoto wa kike kutothaminiwa k.v Wanawe Sara kuonekana si muhimu
    • Panapotokea tatizo la uzazi mama ndiye kulaumiwa k.v Sarah
    • Mwanamke kumjuza mmewe kila kitu akifanyacho
    • Masomo ya mtoto wa kiume kuthaminiwa

Swali 12

  1. Changanua mtindo katika kifungu kifuatacho (alama 10)
    ‘‘Mwanangu usitake sana kuhoji alacho kuku. Utachafukwa roho umchukie kuku bure. Wala usitake kujua nyuki ameitengenezea nini asali. Hutaila. Maadamu yameshakuja,yapokee. Mtoto akinyea kiganja hakikatwi wala hatuulizi kwa nini. Ni maumbile. Maumbile hayo,sawa na vidole, hayafanani. Sawa na watoto wachezeao bembea, tumeicheza na tungali tunaicheza sehemu yetu kwa zamu. Haidhuru iwe ya kamba au chuma. Muhimu ni kwamba tumeshirikiana kusukumana kwenye bembea ya maisha. Upo wakati inakuwa raha tele na upo wakati inakatika na kutubwaga. Hiyo ndiyo raha hasa ya maisha. Ni sawa na chombo kinachomenyana na mawimbi katika bahari. Hutufanya kuwa macho katika safari…”
  2. Fafanua namna mandhari ya dondoo hili yalivyochangia usukaji wa tamthilia. (alama 10)

Majibu

  1. Mtindo
    1. Usemi halisi “mwanangu….
    2. Msemo- Kuchafukwa roho
    3. Jazanda- kuku, nyuki, Kamba, chuma, bembea
    4. Sentensi fupifupi-Hutaila.
    5. Mdokezo wa methali- yameshakuja, yapokee
    6. Taswira- mtoto akinyea kiganja.
    7. Takriri- Maumbile, maumbile.
    8. Usambamba- sawa na vidole hayafanani, sawa na watoto
    9. Kinaya- raha unapobwagwa na bembea.
    10. Tashihisi- chombo kumenyana na mawimbi.
    11. Mdokezo- safari…
  2. Umuhimu wa mandhari haya
    1. kuchimuza maudhui
    2. kuchimuza dhamira
    3. kujenga ploti
    4. kuchimuza wahusika.
    5. kuchimuza sifa zao (wahusika)
    6. kuchimuza mahali na wakati wa tukio
    7. kuchimuza njia ya kusuluhisha mgogoro ulego.

Swali 13

‘‘Walishasema baada ya dhiki ni faraja, Faraja ni zao la dhiki. Leo hii kikapu cha mama kimejaa ndago.”

  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
  2. Eleza vipengele viwili vya kimtindo kwenye dondoo. (alama 4)
  3. Eleza maudhui mawili yanayodokezwa kwenye dondoo. (alama 2)
  4. Eleza sifa za msemaji. (alama 5)
  5. Kwa kutolea mifano mwafaka eleza dhiki alizopitia mama ambaye sasa kikapu chake kimejaa ndago.

Majibu

  1. Msemaji ni Dina kwa Kiwa nyumbani kwa Dina. Dina anataka kumuonyesha kuwa Sara alikuwa amepitia shida nyingi.
  2. Vipengele vya kimitindo
    1. Methali-baada ya dhiki ni faraja
    2. Jazanda- leo kikapu cha mama kimejaa ndago 
  3. Maudhui mawili
    1. Mabadiliko- kitambo Sara na familia yake walipitia dhiki na sasa hivi wana faraja.
    2. Uvumilivu- Sara ni mtu ambaye alivumilia dhiki nyingi na baadaye zikampa faraja.
  4. sifa-Dina
    1. Mwenye huruma
    2. Ujirani mwema
    3. Mwenye roho safi
    4. Mwenye mapenzi ya dhati
    5. Mcha Mungu
    6. Mfariji
    7. Mwenye utani 
  5. Mama (Sara)
    1. Kukosa watoto na kusemwa na wanajamii
    2. Kukosa mtoto wa kiume na kusemwa na majirani
    3. Mumewe (Yona) kuingilia ulevi na kumdhulumu.
    4. Anaachiwa jukumu la malezi
    5. Anapata maradhi ya moyo kutokana na mateso ya mumewe.

Swali 14

Ukilazwa tayari unakuwa umeonja seli. Hata wahudumu wenyewe hawana mlahakamwema. Amri na vitisho kama askari. Unashindwa kama uuguze moyo ama ugonjwa. Katika wodi hewa iliyojaa harufu ya dawa imezagaa, vitanda vimesalimu amri mpaka shiti zikagura. Yaani hali nzima haikupi matumaini ya kutoka ukiwa bora. Matumaini yanadidimia. Tumaini lako unaliweka sala.

  1. Fafanua muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
  2. Tambua toni mbili katika kifungu hiki. (alama 2)
  3. Chambua mbinu za kimtindo katika kifungu hiki. (alama 5)
  4. Eleza namna mandhari ya dondoo hili yalivyochangia kujenga hadithi Bembea Ya Maisha.

Majibu

  1. Fafanua muktadha wa dondoo hili.
    1. Msemaji ni Asna
    2. Wasemewa ni Sara na Neema
    3. Pahali ni hospitalini mjini..
    4. Tukio ni kuhusu hali duni za hospitali za vijijini (4x1=4)
  2. Tambua toni mbili katika kifungu hiki.
    1. Toni ya kutamauka - hali nzima hospitalini haikupi matumaini ya kutoka ukiwa bora.
    2. Toni ya huzuni - matumaini yanadidimia. Tumaiani lako unaliweka katika sala. (2x1= 2)
  3. Chambua mbinu za kimtindo katika kifungu hiki.
    1. Taswira mnuso - hewa iliyojaa harufu ya dawa imezagaa.
    2. Utohozi - seli, shiti wodi.
    3. Tashbihi - amri na vitisho kama askari.
    4. Nahau/msemo - vitanda vimesalimu amri.
    5. Tashihisi - vitanda vimesalimu amri; shiti zikagura. (5x1= 5)
  4. Eleza namna mandhari ya dondoo hili yalivyochangia kujenga hadithi Bembea Ya Maisha.
    1. Yanalinganisha huduma duni za afya kijijini na huduma bora za afya mjini.
    2. Yanatusaidia kuelewa maudhui ya uwajibikaji kupitia kwa wahudumu wa hospitalini za mjini.
    3. Yanachimuza pia maudhui ya uongozi mbaya hospitalini kijijini.
    4. Yanachangia katika kuonyesha sifa za wahudumu wa hospitalini mjini ni wenye bidii na watiifu.
    5. Yanasaidia kuonyesha sifa za wahudumu wa hospitalini kijijini kama wezembe na dhalimu.
    6. Yanachimuza matatizo yanayokumba hospitali za mashambani kama vile uchafu, uhaba wa vitanda vizuri, shiti n.k.
    7. Yanachangia mtiririko wa vitusi, vile Sara anapofika hospitalini kupata matibabu.
    8. Yanakuza sifa za Asna kama mdaku.
    9. Yanajenga sifa za Neema na kumsawiri kama mtu mwadilifu.
    10. Yanachimuza mbinu za kimtindo kama vile utohozi,tashbihi, taswira n.k.

Swali 15

  1. ‘Hizo juu-chini chini-juu ndizo utamu wake. Ni kama maisha kwa jumla. Yana pandashuka ndiyo lakini pandashuka hizo ndizo hutupa kuridhika hatimaye tunapozishinda.’
    Thibitisha kuwa maisha yamejaa pandashuka ukirejelea tamthilia: Bembea ya Maisha (alama 10)
  2. ‘Umenirudisha nyuma kweli katika siku zile za ujana wangu. Asubuhi niko skuli majira ya alfajiri…’’ 
    1. Eleza mbinu ya kimtindo inayojitokeza katika dondoo hili. (alama 2)
    2. Fafanua mifano mingine minane (8) ya matumizi ya mbinu hii katika tamthilia (alama 8)

Majibu

  1.  
    1. Sara alikuwa buheri wa afya alipoolewa na Yona. Baadaye anapata ugonjwa wa moyo kutokana kupigwa na Yona.
    2. Sara na Yona wanakaa muda mrefu bila mtoto. Wanasimangwa na kudharauliwa na wanajamii. Hata hivyo, wanajaliwa Neema, Asna na Salome
    3. Yona aliyekuwa mwalimu hohari baadaye anafutwa kazi kutokana na ulevi.
    4. Elimu ya mtoto wa kike haikuthaminiwa katika enzi za kina Sara. Sasa inathaminiwa kwa kuwa binti zake Yona wamesoma na kuhitimu.
    5. Sara anapougua na kushindwa kupika, Dina anakuja kumsaidia kupika
    6. Wazazi wa kijijini walijilelea watoto wao na kuwaadilisha kwa mfano, Sara.Wazazi wa sasa kama Neema wanakosa muda wa kutosha na watoto wao kutokana na kazi nyingi.
    7. Yona anatelekeza majukumu yake ya nyumbani baadaye anaepa kumsaidia mkewe katika kazi za nyumbani kama kupika.
    8. Sara anasema kuwa barabara za mjini zilikuwa mbovu. Siku hizi zimesakafiwa na usafiri umekuwa wa haraka.
    9. Watoto wa Dina zamani walikuwa maskini sasa wana afadhali
    10. Sara na Yona wanatengwa kwa kukosa mrithi. Neema anajaza pengo hilo kwa kuusimamia mji wa Yona vizuri.
    11. Sara anapougua Neema anampeleka hospitalini. Anatibiwa na mwishowe akapona.
    12. Nduguze Neema (Salome na Asna) wanapokosa karo, Neema anawalipia hivyo kuendeleza masomo yao.
    13. Neema anamtumia baba yake (Yona) pesa za kununua dawa. Hata hivyo, Yona anatumia pesa hizo kwenda kwa wazee wenzake ili asionekane shabiki.
    14. Yona anapofutwa kazi watu wanawatenga na kuwaita maskini wa fedha lakini mwishowe Neema anamsaidia.
    15. Mwanzoni Yona hakuweza kuelewa athari ya ugonjwa wa Sara lakini baadaye anaelewa na kuwa tayari kumsaidia.
    16. Yona alikuwa wa kwanza kuingia chuoni kijijini mwao lakini anamalizia kuwa mlevi hodari jambo linalomfanya kushindwa kufanya kazi.
    17. Asna anaona kuwa ndoa ina mitihani chungu nzima ambayo haina silabasi mahususi, hata hivyo, Sara anampa ushauri kuwa si ndoa zote zina changamoto na kumtia moyo aolewe.
    18. Zamani Neema alikuwa anaona kuwa baba yake hakuwathamini yeye na wanuna wake lakini baadaye anagundua kuwa baba yao (Yona) anawapenda na kuwathamini.
  2. ‘Umenirudisha nyuma kweli katika siku zile za ujana wangu. Asubuhi niko skuli majira ya alfajiri…’’
    1. Eleza mbinu ya kimtindo inayojitokeza katika dondoo hili. (alama 2)
      • Mbinu rejeshi / Kisengerenyuma – umenirudisha nyuma kweli
        kutaja -1
      • kueleza -1
    2. Fafanua mifano mingine minane (8) ya matumizi ya mbinu hii katika tamthilia    (alama 8)
      Mifano zaidio ya mbinu rejeshi:
      1. Dina aneleza kuhusu maisha ya awali ya familia ya Yona na Sara ambapo walipata masimango kwa kukosa mtoto.
      2. Yona anakumbuka wakati alipokuwa mwalimu alivyokuwa akibeba vitabu vya wanafunzi kwa baiskeli ili kuvisahihisha wikendi.
      3. Neema anakumbuka namna usafiri wa zamani ulivyokuwa mgumu kabla ya maendeleo ya teknolojia. Safari iliyochukua siku tatu sasa inachukua saa chache tu.
      4. Bunju anasema kuwa zamani Neema alikuwa anamheshimu lakini sasa heshima hiyo imepungua.
      5. Dina anamkumbusha Kiwa namna Yona alikuwa akimtesa na kumpiga Sara hadi anapoteza fahamu.
      6. Bunju alimwachia Neema mshahara wake ili awasaidie wazazi wake na kumwelimisha Asna.
      7. Kupitia kwa mbinu hii, tunapata kujua kwa Salome aliwahi kuishi na familia ya Neema na kwamba alipata ufadhili wa kwenda ng’ambo.
      8. Asna anasema kuwa zamani watoto wa Dina walidharauliwa kwa kuwa maskini, tofauti na alivyo sasa.
      9. Zamani Yona alipenda dini. Baadaye aliacha dini na kuwa mlevi baada ya kushinikizwa na wenzake chuoni.
      10. Sara anakumbuka zamani akiwa angali mzima na afya yake.
      11. Sara anamkumbusha Yona kuwa alipokuwa na afya yake walishirikiana kutafuta riziki ya kuwalea watoto wao.
      12. Sara anakumbuka namna ambavyo Bunju aliokoa maisha ya Neema.
      13. Neema anakumbuka namna Bunju alivyompata barabarani katika ajali mbaya.

Swali 16

“Mwenyewe ona ulivyokonda kama ng’onda!”

  1. Yaweke maneno haya katika muktadha wake. (alama 4)
  2. Tambua mbinu mbili za lugha katika dondoo hili. (alama 4)
  3. Eleza umuhimu wa msemaji wa maneno haya. (alama 6)
  4. Fafanua umuhimu wa mandhari ya dondoo hili. (alama 6)

Majibu

  1. Yaweke maneno haya katika muktadha wake. (alama 4)
    1. Haya ni maneno ya Sara. (al. 1)
    2. Anamwambia Asna (al 1)
    3. Walikuwa chumbani mwa Asna kule mjini (al.1)
    4. Baada ya Sara kuona jinsi ambavyo Asna alivyokuwa akikumbwa na changamoto nyingi mjini na kumtaka arudi kijijini naye Asna akakataa kwa kuwa alikuwa ameelimika na kutaka kujitegemea binafsi. (alama 1)
  2. Tambua mbinu mbili za lugha katika dondoo hili. (alama 4)
    • Tashbihi – konda kama ng’onda!
    • Nidaa -Ng’onda! (kutaja 1, mfano 1= 2x2 = 4)
  3. Eleza umuhimu wa msemaji wa maneno haya. (alama 6)
    Umuhimu wa Sara:
    1. kielelezo cha mlezi bora- anatoa ushauri kwa watoto wake
    2. Anaonyesha uvumilivu. Maradhi yamemfanya akonde sana lakini anavumilia
      • alivumilia mateso ya mumewe Yona
      • alivumilia masimango ya watu alipokuwa hana watoto na alipopata wasichana tu.
    3. Anadumisha utamaduni wa jamii ambapo mwanamke anafaa kumtumikia mumewe
      • Kila wakati- nafasi ya wanawake katika jamii.
    4. Anaendeleza maudhui ya ugonjwa
    5. Anaendeleza maudhui ya ndoa
    6. Anaendeleza maudhui ya utiifu- alikuwa mtiifu kwa mumewe Yona
  4. Fafanua umuhimu wa mandhari ya dondoo hili. (alama 6)
    1. Kuonyesha mkengeuko- Asna amekengeuka
    2. Kuonyesha changamoto za ndoa
      • kati ya Neema na Bunju
      • Kati ya Sara na Yona
    3. Kuonyesha ushauri nasaha unaotolewa na Sara kwa Asna
    4. Nafasi ya mwanamke katika jamii – wapishi bor
    5. Malezi- Sara alivyowalea watoto wake
    6. Elimu na changamoto zake- Asna kutopata kazi, anaishi kwenye SQ
    7. Kazi- Asna anafanya kazi ya vibarua
    8. Mandhari ya mjini mabadiliko/ mkengeuko- watu wa mjini wanastahabu kukonda ili Wapendeze.

Swali 17

“…anachukua vidonge vyake na kuvimeza kabla ya kuketi kwenye kochi mpya.”

  1. Weka dondoo hili katika muktadha wake. (alama 4)
  2. Tambua aina za taswira katika dondoo hili. (alama 2)
  3. Eleza umuhimu wa mandhari ya dondoo hili. (alama 4)
  4. Eleza nafasi ya mwanamke ukijikita katika utamaduni wa jamii ya “Bembea ya Maisha”. (alama 10)

Majibu

  1. Weka dondoo hili katika muktadha wake. (al 4)
    • Msemaji-mwandishi
    • Mrejelewa-Sara
    • Mahali- nyumbani kwa Sara
    • Wakati- sara ana maradhi kwa hivyo anameza vidonge
  2. Tambua aina ya taswira katika dondoo hili. (al 2)
    • Taswira oni- jinsi abachukua vidonge
  3. Eleza umuhimu wa mandhari ya dondoo hili. (al 4)
    Haya ni mandhari ya nyumbani kwa Sara ambayo yanadhihirisha yafuatayo:
    • Malezi-sara anawalea wanawe vyema
    • Mapenzi- sara anampenda Yona
    • Migogoro- kuna mtafaruku kati ya Yona na Sara.
    • Sifa za Yona kama mlevi, mvivu na mbabedume zinakuzwa.
    • Tunatanguliziwa mhusika Dina kama rafiki wa dhati wa Sara.
    • Utamaduni- Sara anaamini kuwa fimbo ya mzee hurithishwa mtoto wa kwanza.
  4. Eleza nafasi ya mwanamke ukijikita katika utamaduni wa jamii ya “Bembea ya Maisha”. (al 10)
    1. Mshichana lazima aolewe. Msichana anafaa kuolewa baada ya kutimiza umri wa kubaleghe.
    2. Msichana apewi nafasi ya kupata elimu. Kizazi cha jana hakikudhamini elimu ya mwanamke. Sara anasema elimu kwa mtoto wa kike ilikuwa bezo.
    3. Mwanamke anafaa kutii mumewe. Ni utamaduni kwa mke kutunza mumewe. Sara anapoenda mjini, Yona anakosa wa kumtunza.
    4. Mke anafaa kuwa mvumilivu kwenye ndoa. Sara anasalia kwenye ndoa yake licha ya madhila aliyopitia.
    5. Mwanamke anafaa kuongozwa na mume. Bunju anasema kuwa yeye ni kichwa naye Neema awe shingo.
    6. Zamani mabinti walienda unyagoni na kufunzwa jinsi ya kutunza familiazao na waume zao. Sara alieleza haya.
    7. Utamaduni ulikandamiza msichana. Utamaduni wa jadi haukumruhusu mtoto wa kike kwenda shule. Sara anaeleza kuwa hakupata nafasi ya kusoma.
    8. Mwanamke anawekewa laana sisizo na misingi yeyote. Sara anaenda kulala kwa Asna licha ya chumba chake kuwa kidogo.

Swali 18

. “ Wakati mwingine maisha haya hukufanya kijisikia kama abiria kwenye gari liendalo kwa kasi. Unatamani dereva apunguze mwendo lakini unakumbuka kuwa safari bado ni ndefu na hutaki kufika ukiwa umechelewa. Basi unatulia japo ndani una wasiwasi, hutulii. Lakini huwezi kushuka maana safari itaganda. Kwa hivyo, unajitahidi tena, japo wakati mwingine unajikuta umetambaliwa na uchovu, shaka na tuhuma.”

  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
  2. Changanua mtindo katika dondoo hili. (alama4)
  3. Dhihirisha umuhimu wa mzungumziwa wa maneno haya katika kuijenga tamthilia ya “Bembea ya Maisha”. (alama 6)
  4. Eleza namna maisha yanamfanya mzungumzaji “kujisikia kama abiria kwenye gari liendalo kwa kasi”.(alama 6)

Majibu

  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (al 4)
    • Msemaji- Neema
    • Msemewa-Bunju
    • Mahali- sebuleni mwao
    • Wakati- hii ni baada ya Buju kumdokezea kuwa hawezi kumsaidia na hela za kumtibu mamake na jinsi ni laana kukaa na wakwe kwa nyumba moja.
  2. Changanua mtindo katika dondoo hili. (al 4)
    • Tashbihi- kijisikia kama abiria kwenye gari liendalo kwa kasi.
    • Jazanda/ istiara- safari bado ndefu-maisha bado ni marefu na yana mengi
    • Tashihisi-umetambaliwa na uchovu, shaka na tuhuma
  3. Dhihirisha umuhimu wa mzungumziwa wa maneno haya katika kuijenga tamthilia ya “Bembea ya Maisha”. (al 6)
    Huyu ni Bunju
    • Anaendeleza migogoro katika ndoa. Anatofautiana na mkewe kuhusiana na malezi ya mwana wao Lemi. Anasema mume hafai kutumwa na mkewe.
    • Anadhihirisha sifa za mkewe Neema kama mkarimu kwa kuwa alitumia mshahara wake kumlipia dadake Asna karo chuoni na kuishi pamoja na Salome kwao nyumbani.
    • Anaendeleza ploti-kupitia mbinu rejeshi, anadokeza alivyompata Neema akiwa mahututi.
    • Anakuza maudhui ya elimu. Anawalipia wanawe karo. Anamlipia shemeji yake Salome karo pia.
    • Anawakilisha wanaume ambao ni wawajibikaji kwani anamjengea babake nyumba, kuwapa chakula, mavazi, kulipia wanawe karo na kumnunulia mkewe gari.
    • Ni kielelezo cha watu watamaduni kwani anadai kuwa mama mkwe hafai kulala kwake kwani ati ni laana.
    • Anatumiwa kuonyesha uhuru ulioko katika ndo za kisasa. Anamruhusu mkewe kutumia mshahara wake apendavyo.
    • Anawakilisha wanaume wababedume. Anaona yeye ni mwanaume na ndiye kichwa cha familia, anastahili heshima, hastahili kupewa majukumu na mkewe kama kumtembeza mtoto wao Lemi.
  4. Eleza namna maisha yanamfanya mzungumzaji “kujisikia kama abiria kwenye gari liendalo kwa kasi”.
    • Mamake Sara ana amaradhi ya moyo.
    • Hana hela za kutosha kumtibu mamake Sara, anamuomba mumewe usaidizi.
    • Ana kazi nyingi kule kazini-anasema kazi hizo ni kama safari ya ahera.
    • Anakosa muda wa kumlea mwanawe Lemi. Malezi amemuachia yaya Bela.
    • Anakosa muda wa kumpeleka mwanawe matembezini.
    • Wana mivutano katika ndoa na mumewe kuhusu malezi, mila na majukumu.
    • Ana wajibu wa kushughulikia wazazi wake –kuwaajiria wafanyakazi.

Swali 18

Ulevi. Ulevi mwanangu! Gongo liliyamega maadili yake kimyakimya na taratibu uwajibikaji ukawa umemponyoka na kuteleza kama sabuni ya povu jingi na kumwacha na kisomo chake tu.

  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
  2. Fafanua mbinu nne za kimtindo zilizotumiwa katika dondoo hili. (alama4)
  3. Eleza sifa nne za anayerejelewa . (alama 4)
  4. Jadili umuhimu wa mandhari ya mazungumzo haya.

Majibu

  1.  
    1. Msemaji-Sara
    2. Msemewa- Asna
    3. Mahali- chumba cha Asna mjini
    4. Sababu-Sara anamweleza Asna jinsi Yona alivyoishia kujipata ulevini.
  2.  
    1. Takriri/ urudiaji/uradidi -Ulevi.ulevi, kimya kimya
    2. Nidaa-Ulevi mwanangu!
    3. Uhuishi/ uhaishaji/tashihisi - Gongo liliyamega maadili,uwajibikaji umemponyoka
    4. Istiari/ jazanda - gongo –ulevi
    5. Tashbihi- kuteleza kama sabuni ya povu jingi
    6. Taswira mguso- kuteleza ( za kwanza 4 x 1 =4)
  3. sifa za Yona
    1. Katili-anampiga Sara hadi anapoteza fahamu
    2. Mwenye taasubi ya kiume- hakuwathamini wanawe kwa kuwa wasichana
    3. Mwenye majigambi/majivuno- anajipiga kifua kuwa aliacha rekodi kubwa ya idara chuoni.
    4. Mwenye majuto – anajuta kupuuza ugonjwa wa Sara
    5. Mwenye bidii- alipokuwa mwalimu alifanya kazi yake kwa bidii
    6. Mgomvi- Neema anasema kuwa alipenda kugombana na kulalamika.
    7. Mlevi- anakuwa mraibu wa pombe hadi anafutwa kazi. ( za kwanza 4x1=4)
  4. Umuhimu wa mandhari-chumba cha Asna.
    1. kuchimza maudhui ya umaskini- Asna anaishi katika chumba kidogo.Anaketi kitandani huku sara ameketi kwenye stuli .
    2. Sifa za wahusika  zinakuzwa katika mandhari hayakama vile Asna –ni mdaku, Bunju kama mkarimu/Sifa za Sara kama vile- kuwa mshauri zinakuzwa –anamshauri kuhusu ndoa.
    3. Athari za ulevi zinaonyeshwa hapa- Yona anafutwa kazi kutokana na ulevi.
    4. Tunafahamishwa sababu za Sara kuwa mgonjwa-vipigo vya mara kwa mara.
    5. Mbinu za kimtindo kama vile Mbinu rejeshi zimekuzwa.
    6. Katika mandhari haya tunafahamishwa kuwa Neema alikuwa hodari masomoni.
    7. kutambulisha wahusika kama vile Bunju – kuwa mkarimu.
    8. Kujenga dhamira ya mwandishi - kwa mfano, maisha ya mjini/ usasa
    9. kukuza ploti-katika mandhari haya tunafahamishwa kuwa Neema alipopata ajali aliokolewa na kutunzwa na Bunju aliyelipa hata ada yake ya hospitali.
    10. kukuza mgogoro – Bunju na Asna/ usasa na ukale/ Asna na Sara
    11. kuonyesha hali za kitabaka – jinsi Asna alivyoishi katika SQ na chumba chake kilivyokuwa kidogo

Swali 19

“Maji yangekuwa yamewafika Shingo basi wangeshindwa kuishi pamoja. Ndoa ni bembea. Kuna wakati itakuwa juu na wakati itakuwa chini. Hizo juu-chini chini-juu ndizo utamu wake. Ni kama maisha kwa jumla. Yana pandashuka ndiyo lakini pandashuka hizo ndizo
hutupa kuridhika hatimaye tunapozishinda. Maisha yangekuwaje bila hali kubadilika?”

  1. Eleza vipengele sita vya kimtindo vinavyojitokeza katika dondoo hili. (alama 6)
  2. Fafanua umuhimu wa mazungumzo kati ya Luka, Beni na Yona katika kujenga tamthilia Bembea ya Maisha.

Majibu

  1. Eleza vipengele sita vya kimtindo alivyotumia msemaji kufanikisha uwasilishaji wa ujumbe. (alama 6)
    • Sitiari - Ndoa ni bembea. Swali ya balagha - maisha yamekuja bila hali kubadilika
    • Msemo - Maji yangekuwa yamewafika Shingo
    • Tashhisi - Maji yangekuwa yamewafika Shingo
    • Jazanda - Ndoa ni bembea.
    • Tanakuzi - Kuna wakati itakuwa juu na wakati itakuwa chini,juu chini
    • Takriri - Hizo juu-chini chini-juu ndizo utamu wake.
    • Taswira - Hizo juu-chini chini-juu ndizo utamu wake./
    • Ukweli kinzani - Ni kama maisha kwa jumla. Yana pandashuka ndiyo lakini pandashuka hizo ndizo hutupa kuridhika hatimaye tunapozishinda.
    • Balagha - Maisha yangekuwaje bila hali kubadilika?.
  2. Fafanua umuhimu wa mazungumzo kati ya Luka, Beni na Yona katika kujenga tamthilia ya "Bembea ya Maisha"
    • Yanaonyesha sifa ya Luka kuwa ni mkarimu -anawakaribisha wenzake kwake nyumbani kwa chakula cha mchana na kinywaji..
    • Kuonyesha mila na utamadum-Luka anadokeza kuwa kitendo cha kula pamoja kwa wazee kilikuwa kinafanywa na wazee wao kwani mavuno ya kwanza huonjwa na wazee na kutoa baraka. (uk. 58)
    • Yanachimuza ukengeushi -Beni anasema kuwa tatizo la watu siku hizi ni kuzitupa mila zao kabisa. (uk.58) Wajukuu wa Yona hawafahamu lugha yao ya asili. (uk-59)
    • Yanadhihirisha mchango wa dini - Yona unaeleza dini,imechangia watu kuona mila kuwa chafu. (uk.58)
    • Yanaonyesha mabadiliko katika malezi - Yona anaambia wazee wenzake kwa malezi sule mjini yameachiwa kina yaya. (uk.59)
    • Yanaonyesha jinsi mila na tamaduni zilikuwa kandamizi kwani hazikuruhusu mtoto wa kike kuenda shule au kuridhi kitu - kulingana na Luka.(u.k 60) nba
    • Yanadhihirisha jinsi hao kina Luka walivyomshinikiza Yona kuoa mke mwingine apate mtoto wa kiume.(u.k 60)
    • Yanadhihirisha sifa za Beni jinsi ana wivu kwa watoto wa Yona kwani hataki Luka awataje katika mazungumzo yake.
    • Yanachimuza ufanisi wa watoto wa Yona - Luka anasema walikuwa nyota ya jaha. Neema anarudi kijijini akiwa na gari.
    • Yanaonyesha thamani ya mtoto wa kike ilivyopanda na nafasi yake kupanuka kwani zamani walikuwa wakiwategemea waume zao laikini sasa hali ni tofauti(u.k.60) Yanaonyesha maudhui ya uhafidhina Luka anamuona Neema kama si wao tena baada ya kuolewa.
    • Yanachimuza hekima ya Luka - Luka anamuuliza Beni kuwa lipi muhimu kati ya tiba au mtu kuja kumpikia mwenzake? (uk.61)
    • Yanaonyesha sifa za Yona hapo awali kuwa alikuwa mualimu mwenye bidii - Yona anasema angefika kazini majira ya alfajiri, kiboko mkononi, siku nzima kazi tu, aliweza kufunga vitabu kwenye baskeli kwenda kuvisahihisha wikendi (uk. 62) 
    • Yanadhihirisha mabadiliko katika nyanja ya elimu - Yona anasema siku hizi huwezi tena kumnyoosha mtoto kwa kiboko. (uk.62)
    • Yanachimuza athari pombe-jifs pombe ilivyomfanya Yona kuwa mtumwa akashindwa kuishi bila kulewa (uk62)
    • Yanaonyesha uvumilivu au stahamala za Sara wakati Yona alipokuwa mlevi. Yona anasema Sara alimsaidia kulea na kusomesha watoto na kwamba bila yeye chombo kingezama. (uk-62)
    • Yanaonyesha jinsi Yona alivyoanza kutumia tembo alipokuwa chuoni! Wenzake walimpa mvinyo kumrai kuonja. (uk. 62)
    • Yanadhihirisha uongo wa Beni-kuwa mtoto wake ni fundi wa mitambo na wala si injinia. (uk. 63)
    • Yanaendeleza ploti- tunatambulishwa kuwa Luka, Beni na Yona ni marafiki na walishiriki vileo pamoja.

Swali 20

"Bembea inapolika na kukatika haiwi mwisho wa michezo. Huungwa na mchezo kuanza    tena." 

  1. Eleza muktadha wa dondoo hili.                       (alama 4)
  2. Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa kutolea mifano mwafaka katika tamthilia Bembea ya Maisha.   (alama 10)
  3. Tathmini  mchango wa msemaji wa maneno haya katika kufanikisha ploti ya tamthilia Bembea ya Maisha.   

Majibu

  1. Eleza muktadha wa dondoo hili.    (alama 4)
    • Msemaji ni Sará
    • Msemewa ni Neema
    • Walikuwa nyumbani kwa Neema
    • Sara anamshauri Neema kuhusu maisha.
  2. Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa kutolea mifano mwafaka katika tamthilia  "Bembea ya Maisha"   (alama 10)
    • Neema nusura apoteze uhai wake katika ajali Lakini Bunju akamnusuru kwa kumpeleka hospitalini.
    • Neema na Bunju baada ya kugombana kuhusu mchango wake Bunju katika matibabu ya Sara, Neema anaamua kumuelewa Bunju hivyo ndoa yao kuendelea vyema.
    • Baada ya changamoto ya kutopata watoto iliyoyumbisha ndoa baina ya Sara na Yona, hatimaye walijaliwa watoto watatu.
    • Maradhi ya moyo yalipomlemea Sara kiasi cha kukata tamaa na maisha, Neema anajitolea kuhakikisha mamaye amepata matibabu murua hivyo kumrejeshea matumaini.
    • Japo Yona na Sara walikosa mwana wa kiume na kusimangwa na wanajamii, mabinti zao wanakuwa wembe masomoni hivyo kuwapa furaha katika ndoa yao.
    • Neema alipoonekana kukata tamaa Kutokana na kile alichokiona kuwa ni ubahili wa Bunju, Sara alimpa wosia uliompa nguvu zaidi katika ndoa yake.
    • Yona baada ya kugundua kuwa ulevi wake unaangamiza familia yake, anaapa kutolewa tena na kumhudumia mkewe Sara.
    • Yona na Beni walipotofautiana kuhusu watoto wao, Luka anafaulu kutuliza hali na wazee hawa kuendelea na sherehe zao.
    • Baada ya kumsababishia mkewe maradhi ya moyo, Yona anamwomba Sara msamaha kwa kuwa hakujua upeo wa ugonjwa wa moyo.
    • Mgogoro baina ya Sara na Neema kuhusu Yona unaisha Neema anapogundua upendo wa Yona Kwao anapoacha utamaduni wa kutopika chakula:
    • Mgogoro baina ya Sara na Yona unaisha. Yona anapoachana na mila na tamaduni za kutopika kwa mwanaume.
    • Tatizo la Sara la kushindwa kumpikia mkewe linasuluhishwa na jiraniye Dina anapokuja kumsaidia.
  3. Eleza umuhimu wa msemaji katika kuendeleza ploti ya tamthilia hii. (alama 6)
    • Sara ametumiwa kuonyesha athari ya migogoro katika ndoa. Maradhi ya moyo anayogangua ni tokeo la mzozano baina yake na mumewe Yona
    • Kupitia mazungumzo baina yake na Asna, yanamsawiri Asna kama kijana aliyekengeuka kiasi cha kutotaka kuingia katika ndoa.
    • Kupitia kwake tunaelezwa kuhusu usuli wa matukio. Sara alisemwa na kutukanwa na wanajamii kwa sababu ya kuwapata watoto wa kike pekee. Hii ilipelekea Yona kuingilia ulevi.
    • Baadhi ya matukio katika maisha ya wahusika fulani yanaangaziwa katika nyumba yake. k.m Dina anaangaziwa kama mwenye utu kwani anaenda kumpikia kwa kuwa alikuwa mgonjwa.
    • Kuchimuza matukio fulani. Kupitia mazungumzo baina yake na Yona, tunapata kujua kuwa Neema ndiye aliyewasomesha wanuna wake hadi chuo kikuu. elmor
    • Kupitia mazungumzo baina yake na Neema na Asna tunapata kujua kuhusu tofauti baina ya hospitali za mjini na kijijini. Huduma za hospitali mjini ni mzuri lakini za kijijini zinalinganishwa na seli na wahudumu hawana mlahaka mwema. Jay Hatima ya mgogoro baina ya Sara na Yona. Yona anaachana na mila na tamaduni za kutopika kwa Mwanaume.
    • Anaonyesha jinsi utamaduni ulivyowakandamiza wasichana - Sara anamwambia Asna kuwa siku zao elimu ya wasichana ilifanyiwa bezo na kuwa Sara aliachia darasa la saba.
    • Kuonyesha mustakabali wa Sara wa kusamehe, Yona - Yona anamwomba Sara msamaha kwa kuwa hakujua upeo wa ugonjwa wa moyo.

Swali 21

“Siwezi kuendelea kuishi hivi. Sasa nimekata shauri. Pombe! Umenichezesha kama mwanasesere kwa muda mrefu. Umeninyima fursa ya kuielewa familia yangu. Hapana! … Lazima nimshukuru kwa vitendo kwa jinsi alivyojitolea kuijenga familia yetu…kwa heri pombe. Buriani.”

  1. Weka dondoo hili katika muktadha wake. (alama 4)
  2. Eleza vipengele vinne vya kimtindo alivyotumia msemaji kufanikisha uwasilishaji wa ujumbe.    (alama. 4)
  3. Fafanua changamoto ya asasi ya ndoa kwa kuangazia ndoa zilizo katika tamthilia ya Bembea ya Maisha.
  4. "...Wakati mwingine mwindaji huwa mwindwa. Hata kijijini wanaishi watu. Watu hao hawakumbwi na dhiki kiasi hiki. Ya nini kung'ang'ana kuyatafuta maisha kama kwamba hayapiti? Maisha ni mshumaa uso mkesha! Ukijiachia sana peupe hata upepo unaweza kuuzima kabla ya kulika hadi nchani.”
    Eleza umuhimu wa msemaji katika kuendeleza ploti ya tamthilia hii. 

Majibu

  1.  
    1.  
      1. Ni maneno ya Yona
      2. Anajiambia 
      3. Yuko kwake nyumbani
      4. Yona anajutia matendo yake. Hii ni baada ya yeye kuelewa kuwa mkewe alikuwa muwele kwa kweli na alihitaji usaidizi wake   
    2.  
      1. Ritifaa- Yona kuisemesha pombe kana kwamba anasema na mtu. Kwa heri pombe.
      2. Uhaishaji- pombe imepewa sifa za kibidamu, umenichezesha kama mwanaserere.. 
      3. Uzungumzi nafsia- siwezi kuendelea …
      4. Msemo / nahau- nimekata shauri
      5. Uashiriaji – hivi
      6. Tashbiha – Kama mwanasesere
      7. Nidaa - pombe !
    3. Changamoto za  ndoa
      1. Kuelimisha watoto. - Bunju alimsaidia Neema katika kuwaelimisha ndugu zake na kuwajengea wazazi wa Neema nyumba.
      2. Kuwapa ushauri. Sara anamshauri Neema kuhussu namna ya kukabiliana na hali mbalimbali maishani./ bembea inalika
      3. Kukosa watoto. Jamii inawasema Sara na Yona kwa kukosa kizazi katika kipindi cha awali cha ndoa yao.
      4. Malezi ya watoto. Neema na Bunju wanabishana kuhusu majukumu yao kumwelekea Lemi na jinsi ya kumlea. Neema anaonyesha kuridhika na juhudi za Lemi katika elimu ilhali kulingana na Bunju Neema analea unyonge.
      5. Kuendeleza mila na tamaduni za jamii. Yona anamtaka Sara kumwita Neema ampeleke Sara hospitali kwa kuwa fimbo ya mzee hurithi mtoto wa kwanza. Sara anamwambia Neema kuwa utamaduni haumruhusu kulala kwao na Bunju kukosa mtoto wa kiume- Yona na Sara kusutwa na jamii kwa kukosa mrithi.
      6. Kuoa mke mwingine- jamii inamshinikiza Yona aoe mke mwingine
      7. Kichapo cha mbwa- Yona kumpiga Sara na kunsababishia dhiki ya kisaikolojia
      8. Ulevi – ulevi wa Yona kumfanya ampige Sara na kumsababishia uwele.
      9. Majukumu ya wanaume na wanawake- Bunju na Neema
      10. Asna kuonyesha hofu katika ndoa- itamnyima uhuru/ ubahili wa Bunju
    4. Umuhimu wa Sara katika kujenga ploti
      1. Sara ametumiwa kuonyesha athari ya migogoro katika ndoa. Maradhi ya moyo anayogangua ni tokeo la mzozano baina yake na mumewe Yona.
      2. Kupitia kwake tunaona alivumilia ndoa yake na kufanya juu chini ili wanawe wapate elimu ili kuboresha mustakabali wao.
      3. Aidha, anahakikisha kuwa binti zake Neema na Asna wanapata elimu.
      4. Ni mfano wa wanawake wenye bidii. Hata akiwa hospitalini, akili yake inafikiria mazao yake aliyoyaacha shambani.
      5. Kupitia mazungumzo baina yake na Asna, yanamsawiri Asna kama kijana aliyekengeuka kiasi cha kutotaka kuingia katika ndoa.
      6. Kupitia kwake tunaelezwa kuhusu usuli wa kutopika. Sara anaeleza kuwa kwa sababu ya ugonjwa wake hangeweza kupika.
      7. Sara alisemwa na kutukanwa na wanajamii kwa sababu ya kuwapata watoto wa kike pekee. Hii ilipelekea Yona kuingilia ulevi.
      8. Baadhi ya matukio katika maisha ya wahusika fulani yanaangaziwa katika nyumba yake.  k.m Dina anaangaziwa kama mwenye utu kwani anaenda kumpikia kwa kuwa alikuwa mgonjwa.
      9. Kupitia mazungumzo baina yake na Yona, tunapata kujua kuwa Neema ndiye aliyewasomesha wanuna wake hadi chuo kikuu.
      10. Pia, Sara anatujuza kuwa Neema ndiye aliyewaajiri wafanyakazi nyumbani kwake.
      11. Ametumiwa kuonyesha uwajibikaji wa Neema. Neema anagharamia matibabu ya Sara na pia anampa babake/Yona pesa za kwenda kwa wazee wenzake.
      12. Kupitia kwake tunafahamu kuwa Bunju ndiye aliyemsaidia Neema baada ya kupata ajali na kulipia gharama za hospitali ilhali Bunju hakuwa amemjua Neema.
      13. Kupitia mazungumzo baina yake na Neema na Asna tunapata kujua kuhusu tofauti baina ya hospitali za mjini na kijijini. Huduma za hospitali mjini ni mzuri lakini za kijijini zinalinganishwa na seli na wahudumu hawana mlahaka mwema.
      14. Hatima ya mgogoro baina ya Sara na Yona. Yona anaachana na mila na tamaduni za kutopika kwa Mwanaume.
      15. Anaonyesha jinsi utamaduni ulivyowakandamiza wasichana –Sara anamwambia Asna kuwa siku zao elimu ya wasichana ilifanyiwa bezo na kuwa Sara aliachia darasa la saba.
      16. Kuonyesha mustakabali wa Sara wa kumsamehe,Yona-Yona anamwomba Sara msamaha kwa kuwa hakujua upeo wa ugonjwa wa moyo.

Swali 22

"Ndivyo...ndivyo... hayakuishia hapo. Baada ya ile mvua ya baraka iliyowanyea, watu walianza tena kuwasema kuwa hawana mtoto wa kiume."

  1. Eleza muktadha wa dondoo hili.
  2. Tambua mbinu mbili za kimtindo katika dondoo hili.
  3. Fafanua umuhimu wa msemaji katika kuijenga tamthilia hii.
  4. Eleza sifa mbili za msemaji wa kauli hii.
  5. Kwa kutolea mifano, onyesha jinsi mwandishi alivyoshughulikia maudhui ya utamaduni wa kale katika tamthilia hii.

Majibu.

  1.  
    • Msemaji-Dina
    • Msemewa-Kiwa
    • Mahali-nyumbani mwa Dina
    • Ni baada ya Kiwa kumtembelea mamake. Mamake anasimulia hali ya ndoa ya Sara mwanzoni
  2.  
    • Takriri-Ndivyo...ndivyo
    • Mdokezo-ndivyo...
    • Kisengere nyuma-baada ya ile mvua ya baraka iliyowanyea, watu walianza tena kuwasema
  3. Dina
    1. Anajenga maudhui mbalimbali. Malezi, ushirikiano
    2. Anachimuza sifa za wahusika wengine kama vile Dina kuwa mlezi mwema
    3. Kielelezo cha watu wenye utu katika jamii. Anamsaidia dina kuandaa chakula wakati alikuwa mgonjwa
    4. Anaendeleza ploti. Anaturudisha kwa matukio ya awali kuhusu maisha ya Sara (4×1=4)
  4.  
    1. Mwenye huruma-Sara anapougua, Dina anamsaidia kupika chakula
    2. Mwenye uhusiano mwema-anapoitwa na Sara amsaidie kupika bwana yake anaitikia wito
    3. Mwenye mapenzi ya dhati-anamsaidia rafiki yake kazi ya nyumbani
  5.  
    1. Wanajamii wanasisitiza kuwa familia sharti iwe na mtoto wa kiume. Familia ya Yona inadharauliwa kwa kukosa mtoto wa kiume. (uk 10)
    2. Luka anawaalika wazee wenzake; Yona na Beni ili kuonja mavuno ya kwanza na kuibariki (uk 58)
    3. Bunju anashikilia utamaduni wa kutowakubali wazazi wake au wa Neema kulala nyumbani kwake (uk 24, 29)
    4. Sara anamweleza Asna kuwa siku zao msichana akisha baleghe ilikuwa hana amani. Lazima aozwe. (uk.52)
    5. Mila na desturi za zamani zimewaumba wanaume kama watu wasioweza kusaidia katika kazi za jikoni. (uk. 66)
    6. Sara anaambia Yona kuwa fimbo wanarithi watoto wa kiume, si wa kike. (uk.2)
    7. Yona anaambia Sara kuwa fimbo ya mzee hurithiwa na mtoto wa kwanza (uk.20)
    8. Luka anaambia Yona na Beni kuwa zamani mila zao hazikuruhusu watoto wa kike kwenda skuli kurithi kitu (uk.60)
Join our whatsapp group for latest updates

Download Bembea ya Maisha Maswali na Majibu ya Dondoo.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?